KKKKK
Saturday, March 27, 2021
Sunday, November 27, 2016
Rais Fidel Castro hatupo naye tena
Rais wa kwanza wa Kuba aaga dunia.
Akitangaza kupitia luninga ya nchi hiyo, rais was sasa wa Kuba Raul Castro, alisema kuwa "rais wetu wa kwanza na kiongozi na mwanamapinduzi Komrade Fidel Castro amefariki leo 25/11/2016."
Kufuatia kifo cha rais Castro, Kuba itakuwa katika maombelezo ya siku tisa. Mazishi ya rais huyo wa Kuba yanatarajiwa kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wa dunia.
Fidel Castro alikuwa mpinzani wa siasa za kibepari na alikuwa akipenda kusema "Uwanamapinduzi ni ni mapambano mpaka kufa ya wakati uliyo pita na wakati ujao."
"Wanaongea kushindwa kwa ujamaaa, lakini yapo wapi mafanikio ya siasa za kibepari katika bara la Afrika Asia na Latin Amerika?
" Sikubaliani na ubepari, ni mbaya auvutii na unatenganisha unaleta vita vitna na mashindano yasiyo na tija katika jamii."
Marehemu rais mstaafu wa Kuba Fidel Castro alizaliwa mwaka 31/08/1926 mjini Biran Kuba.
Posted by Kibatala at Sunday, November 27, 2016 0 comments
Wednesday, November 9, 2016
Donald John Trump ashangaza ulimwengu wa Siasa, Achaguliwa kuwa rais wa Marekani
Donaldo John Trump achaguliwa kuwa rais wa 45 wa Marekani
Donald Trump akiongea mbele ya wapenzi na washabiki wake walikuwa katika hotel yake inayo julikana kama The Trump alisema. " Hillary Clinton amenipigia simu na kutupongeza na ninampongeza kwa jitihada zake wakati wa harakati wa uchaguzi huu."
"Ushindi wa leo, ni harakati na hazikuwa kampeni za uchaguzi, hivyo hizi harakati ndio sasa zimeanza kazi."
Vilevile rais mteule Donald Trup, aliwaomba watu wote kuwa wamoja na kwa kusema kuwa wale waliomchagua na wasionipigia kura wote wawe kitu kimoja na kuwa atakuwa rais wa Wamarekani wote. "Nawaomba wote walio umia kutokana na uchaguzi tuwe wamoja ili kujenga Marekani mpya."
Rais mteule, Donald Trump, alikumbana na vikwazo vya kila namna katika kampeni za kuwania urais wa Marekani, kwa kudaiwa kuwa mbaguzi, msemaji wa vitu na mambo ambayo si yakiutu an pia kudaiwa kuwa alikuwa anadhalilisha wanawake.
Ushindi wa Donald Trup unatafsiliwa kuwa ni jibu kwa wanasiasa kwamba wabadirike kwa kuwa wa watu wamechoka na siasa zisizo eleweka na haadi wazizotimiza.
Posted by Kibatala at Wednesday, November 09, 2016 0 comments
Friday, October 28, 2016
Tony Blair ateta lake juu ya Brexit
Akiongea na BBC 4 radio, Blair alisema "Ikiwa tutatoka katika jumuiya ya Ulaya, basi madhara yake yatakuwa makubwa kijamii na kiuchumi."
Blair aliyasema hayo kwa kusisitiza kuwa watu 48% ya wakipiga kura walipiga kura ya kubaki ndani ya Umoja wa Ulaya na kwani walijua umuhimu wake.
"Wananchi wanatakiwa wapewe nafasi ya kuliangalia hili suala kwa undani, ikibidi kuwepo na kura ya nyingine kuhusu Uingereza kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya."
Hata hivyo Maria Caulfield, mbunge wa chama tawala cha Conservative na mmoja wa viongozi wanao shughulikia Uingereza kujitoa katika muungano wa umoja wa Ulaya amesema " Blair anatakiwa kutoa mawazo ya kuijenga Uingereza iliyo amua kuwa nje ya jumuiya ya nchi za Ulaya na siyo vinginevyo"
"Blair anapinga demaokrasi, wanachi walishaamua na matakwa yao lazima sisi kama viongozi tuyatekeleze." Alisisitiza Caulfield.
Maoni hayo ya Tony Blair yamekuja kufuatatia maswali mengi yanayo ulizwa kuhusu nafasi ya Uingereza baada ya kujitoa rasmi katika muungano wa jumuiya ya nchi za Ulaya na kushuka kwa thamani ya fedha ya Uingereza tangu Waingereza kupiga kura ya kukataa kuwa jumuiya ya Ulaya.
Posted by Kibatala at Friday, October 28, 2016 0 comments
Sunday, March 20, 2016
Rais Jakaya Kikwete
Posted by Kibatala at Sunday, March 20, 2016 0 comments
Wednesday, March 9, 2016
Iran yarusha makombora.
Tehran, Iran 09/03/2016. Jeshi la Iran limefanikiwa kurusha makombora mawili (Ballist missiles) Urushaji wa makombora hayo yaliyo pewa majina ya Qadr -H na Qadr F ulifanyika kaskazini mwa nchi hiyo katika eneo lijulikanao Alborz Mashariki. Makombora hayo yanauwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 1500 hadi 2000.
Kamanda wa kitengo cha usalama wa anga wa Iran, Brigedia, Amirali Hajizadeh amesema kuwa. "Kombora aina ya Qadr H linuwezo wa kushambulia umbali wa kilomita 1700 na jingine Qadr F linaweza haribu na kuchakaza kabisa kitu chochote kilichopo umbali wa kilomita 2000."
Tamko la Iran kuhusu kurusha makombora yake, limekuja baada ya msemaji wa serikala ya Marekani Mark Toner kukosoa kitendo hicho nakusema " Kufuatia kitendo hicho cha Iran, Marekani italifikisha suala hilo katika balaza la usalama la umoja wa mataifa."
Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, amesema kuwa " Iran haitaji ruhusa yoyote katika masuala yake ya kiulinzi wa nchi, na tulisha sema kuwa hatuta ulizia wala omba ruhusa katika kushughulikia masuala yetu ya kiulinzi."
Iran nchi ambayo ilikuwa imewekewa vikwazo vya kiuchumi kwa muda mrefu na Marekani na washiriki wake, imekuwa kwa miaka mingi ikijitengenezea mitambo ya kiulinzi ya kijeshi na pia kuhakikishia jumuia ya kimataifa kuwa utengenezaji wa zana za kiulinzi ni harakati za kujiimarisha katika suala la ulinzi wa nchi.
Posted by Kibatala at Wednesday, March 09, 2016 0 comments
Wednesday, March 2, 2016
Osama bin Laden alitaka mirathi yake itumike kundeleza mapambano.
Aliyekuwa kiongozi wa kundi la Al Qaeda, Osama bin Laden, alikuwa ameandika kuwa mirathi yake ya kifedha zipatazo $29 millioni, kwa kiasi kikubwa zitumike takika kusaidia kuendeleza "Jihad" mapambano, na kiasi kidogo kigawiwe kwa ndugu wa familia, ijapokuwa mpaka hazijulikani hizo fedha zipo wapi.
Zikiwa zimeandikwa kwa mkono wa Osama bin Laden, habari hizi, zimetolewa na serikali ya Marekani wiki hii, baada ya kuruhusu mafaili yaliyo kamatwa na kikosi maalumu cha kijeshi cha Marekani wakati walipo kuvamia makazi na maficho ya Osama bin Laden yaliyo kuwepo kwenye mji wa Abbottabad Pakistan siku ya 1. Mai 2011 na kufanikiwa kumua.
"Nivyema kwa jamii kufahamu nini kiongozi wa Al Qaeda alipanga" Alisema Brian Hale Mkurugenzi wa mambo ya jamii kutoka idara ya upelelezi ya taifa ya Marekani huku akiwa anaonyesha makaratasi yaliyo chukuliwa kutoka katika makazi wa Osama bin Laden
Karatasi hiyo ambayo inaonyesha nini kiongozi wa Al Qaeda alitaka kifanyike katika mirathi yake, ni moja ya makatasi 100 ambayo yameruhusiwa kuwekwa hadharani, baada ya kamati ya ulinzi na usalama kuyapitia kwa uangalifu.
Posted by Kibatala at Wednesday, March 02, 2016 0 comments
Sunday, February 28, 2016
Urusi yazidi kujiimarisha kijeshi.
Urusi yazidi kujiimarisha kijeshi.
Urusi imeonyesha rasmi gari mpya aina ya Batmobile ambayo itatumika katika mapambano ya kivita na vurugu za aina yoyote. Gari hiyo ambayo hapo awali ilijulikana kama Punisher, inasemekana ni jibu kwa gari la kijeshi la Kimarekani Humvee.
Akiongea wakati wa kukagua gari hii mpya ya kijeshi, rais wa Urusi, Vladmir Putin alisema "nawashukuru kwa jitihada na hii inahakikishia kuwa Urusi ipo tiyari kujibu mashambulizi ya aina yoyote pindipo tutakapo shambuliwa."
Kwa mujibu wa shirikala la habari la Urusi RT, gari hii mpya ya Kirusi, inauwezo wa kuchua watu kumi na ndani gari hii ina muundo wa V ambao inatoa kinga kubwa kwa watumiaji wa gari hii pindipo wakishambuliwa au gari kushambuliwa na bomu na vilevile hili gari lina mitambo ya kurushia mizinga.
Uzinduzi wa gari hili, unatarajiwa kuleta vichwa kuuma kwa Marekani na washiriki wake, kwani Urusi tangu iingilie vita vya Syria, nguvu zake za kijeshi zimefanya kuwepo na mabadiriko makubwa ya kivita kati ya serikali ya Syria inayo ungwa mkono na Urusi na wapinzani wa serikali wanao ungwa mkono na nchi za magharibi.
Posted by Kibatala at Sunday, February 28, 2016 0 comments
Thursday, February 4, 2016
Shirika la utangazaji la RT la Urusi lawa tishio.
Shirika la utafiti wa masuala ya kiusalama la Marekani CEPA, limemlaumu George Galloway mtangazaji na mwanasiasa mkongwe wa Uingereza ya kuwa kipindi chake Sputnik kinacho tangazwa katika luninga ya Kirusi - RT kuwa kinahatarisha na kuzidharaulisha serikali za nchi za Magaharibi na NATO.
CEPA Center for European Policy Analysis yenye makao ya ke makuu jijini Washington, limesema kutokana na kuwepo na RT inayo tangaza kiingereza, kipindi cha Sputnik, kimekuwa kikitumika kama sehemu ya kukuza na kundesha juhudi za Urusi dunia kwa kuponda mipango na mikakati ya Marekani na washirika wake.
Ripoti ya hiyo ambayo ilitolewa January 2016, iliandaliwa ili kufanya utafiti ni kwa jinsi gani amshirika ya habari yanavyo fanya kazi na shirika la utangazaji wa luninga RT likanonekana kuwa linazidi kukua na kuwa tishio kwa mashirika ta utangazaji ya nchi za Ulaya Mgharibi na Marekani.
Posted by Kibatala at Thursday, February 04, 2016 0 comments
Tuesday, November 10, 2015
Rais Putin asema njama za Marekani zipo wazi.
Akiongea na katika mkutano wa Sochi, rais Putin alisema " Iran na Korea ya Kaskazini zinatumiwa na Marekani kama kigezo cha kuwekwa mitambo ya kijeshi barani Ulaya. Lakini nia yake ni kujaribu kupunguza dhamira ya Urusi ya kuwekeza nguvu zake za kijeshi.
" Hivyo napenda kuwahakikishia kuwa Urusi haitakubaliana na kitendo hicho, na kwa sasa tunatengeneza siraha ambazo zitaweza kukabiriana na siraha hizo za Kimarekani." Alisisitiza raia Putin.
Mvutano wa kijeshi kati ya Urusi na Marekani, umekuwa wa muda sasa, tangu Marekani ilipo pendekeza kuweka mitambo yake ta Kijeshi barani Ulaya kwa madai kuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa NATO jambo ambalo Urusi inalipinga.
Posted by Kibatala at Tuesday, November 10, 2015 0 comments
Tuesday, June 16, 2015
Urusi kuandaa kuwekeza siraha za kinyukia kiulinzi.
Mkuu namba 2 wa Al-Qaeda auawa.
Kuuawa huko kwa Nasir al- Wahishi, kunasadikiwa ni pigo la pili kubwa kwa kundi la Al-Qaeda, kufuatia pigo la kwanza la kuuawa kwa kiongozi mkuu wa Al-Qaeda Osama bin Laden mwaka 2011.
Kutokana na kuuawa kwa kiongozi huyo namba mbili wa Al-Qaeda, Qassim al Raim, huenda akachukua kiti cha uongozi wa kundi hilo katika maeneo ya Peninsula.
Rais aliyepinduliwa nchini Misri ahukumiwa kifo.
Kairo, Misri - 16/06/2015. Mahakama kuu nchini Misri, imemuhukumu adhabu ya kifo rais aliye pinduliwa Mohamed Mosri.
Mahakama imemkuta na hatia bwana Musri kwa kuhusika katika makosa ya mauaji na makosa mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Pia hukumu kama hiyo ilitolewa kwa wanachama 80 wa chama cha Undugu wa Kislaam (Muslim Brotherhood), japokuwa hawakuwepo mahakamani.
Rais Mohamed Mosri,alipinduliwa kijeshi kutoka madarakani mnamo mwaka 2013 July, na toka hapo amekuwa chini ya ulinzi, nahuku mlolongo wa kesi zikimfuta, kutokana naaliyoyafanya wakati alipo kuwa madarakani.
Urusi kuandaa kuwekeza siraha za kinyukia kiulinzi.
Akiongea katika sherehe za kuazimisha maonyesho ya kijeshi, rais Putin alisema "Mizinga 40 yenye uwezo wa kubeba siraha za nyuklia zitakuwa zimekwisha wekezwa ifikapo mwisho wa mwaka wa 2015."
Matamshi hayo ya rais Putin, yamekuja baada ya Marekani kutamka hivi karibuni, itaongeza ulinzi wa kisiraha katika bara la Ulaya ikiwa nji ya kujihami kutokana na vitisho vinavyo wekwa na Urusi.
Posted by Kibatala at Tuesday, June 16, 2015 0 comments
Sunday, February 1, 2015
Mmoja wa waandishi wa habari wa Aljazeera aachiwa.
Rais Robert Mugabe mwenyekiti wa AU.
Adis Ababa, Ethiopia - 01/02/2015. Rais Robert Mugabe , amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya muungano wa nchi za Afrika AU, baada ya mwenyekiti wa sasa rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kumaliza muda wake.
Akiongea mara baada ya kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti, rais Mugabe alisema " kazi yangu ni kuhakikisha yote yaliyo azimiwa yanatimizwa, hivyo kama nchi za Ulaya na washiriki wake watasema kuhusu kuchaguliwa kwangu, hilo haliniusu."
"Lengo ni kuhakikisha tunatumikia wananchi wa Afrika, na hasa kuinua hali ya wanawake, japo tupo tofauti kimaumbile, wanawake wanaweza fanya kazi fulani na kuna kazi nyingine wanaume hawawezi kufanya kama kubeba motto tumboni, hivyo tunaangalia ni njinsi gani wanawake wasaidiwe katika jamii ili kuchangia ujenzi wa bara hili kiuchumi."
"Zimbawe leo tuna majaji na marubani wanawake, hivyo tunajua umuhimu wa wanawake katika jamii nzima ya kiaafrika."
Rais Robert Mugabe, ndiye rais mkubwa kiumri, na ambaye amekuwa akisifiwa na kupendwa sana katika bara la Afrika kama mginaji halisi wa Wafrika, na hasa kwa kupinga na kufokea hadharani tabia za baadhi ya nchi zinazo taka kuleta muvurugo na kuiba mali zilizopo katika bara la Afrika kiujanja ujanja.
Mmoja wa waandishi wa habari wa Aljazeera aachiwa.
Greste Muaustralia na wenzake Baher na Fanny, wamekaa jela siku 400, tangu mahakama jijini Kairo kuwahukumu vifungo, baada ya kushatakiwa kukisaidia kihabari chama kilicho tolewa madarakani cha Muslim Brotherhood kwa nguvu na rais wake Mohammed Mosri kukamatwa.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema kuwa " Greste alipakizwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Misri leo hasubuhi, akiwa na kaka yake.
Mostefa Soug, mkuurugenzi mkuu wa Aljazeera akiongea kuachiwa kwa Peter Grste alisema "tunafurahi kuwachiwa kwa Peter Greste, lakini hata hivyo bado tunasisitiza Baher na Fanny lazima waachiwe huru, na hatuta pumzika mpaka waachiwe."
Kuachiwa huko kwa Greste kumekuja kutokana na msukomo wa kimataifa unao isukuma serikali ya Misri ya kutaka kuachiwa kwa waandishi wa habari wa Aljazeera waliopo ambo mmoja wao Peter Greste kuachiwa huru na wenzake Beher Mohammed na Mohamed Fanny bado wapo jela.
Wakwepa kodi nchini Ugiriki walikuwa kitisho kwa serikali.
Athens, Ugiriki - 01/02/2015. Mkuu wa umiliki na ukusanyaji wa kodi nchini Ugiriki Nikos Karavitis Theoharis, alilazimika kujiudhuru, baada ya kupokea vitisho kutoka kwa wakwepa kodi.
Akiongea, mara baada ya kuchaguliwa kwa serikali mpya ya Siryiza, Theoharis alisema " Nilikuwa napokea simu za vitisho ofisini kwangu na ujumbe kupitia mitandao yakuwa ni Euro 5,000 zitatumika kuvunja miguu yangu."
"Vitisho nilivyo kuwa nikipokea, vinaonyesha ni kwa kiasi gani wakwepa kodi walivyo kuwa wanaibia nchi bila uwoga, na hivyo baada ya kuona nipo imara ndipo walipo nitisha na kwa usalama ikabidi nijiudhuru."
"
"Lakini naamini serikali iliyo ingingia madarakani, itakuwa shubiri kwa wakwepa kodi. kwani vitisho walivyo kuwa wakivitumia havita saidia"
Theohari,s aliyaongea haya baada ya kushinda kuwa kama mbuge, na ambaye anaunga mkono serikali mpya iliyo chaguliwa nchini Ugiriki, inayo pinga mbinyo na makato ya serikali kwa wananchi ili kulipa madeni ya nchi. Hatua ambayo inadhaniwa huenda ikaleta mtafaruku katika jumuiya ya umoja wa Ulaya.
Posted by Kibatala at Sunday, February 01, 2015 0 comments
Thursday, January 1, 2015
Mamilioni washerekea kuanza kwa mwaka mpya.
Mamilioni washerekea kuanza kwa mwaka mpya.
Mungu Baba tunakushukuru, utubariki, utulinde, utuzidishie kwa kila jambo tulifanyalo na utufanye tuzidi kukuomba na kukutegemea wewe Muumba kwa kila jambo. Amina.
Wapalestina wajiunga na Mahamakama ya Kimataifa.
Ramalhah, Palestina - 01/01/2015. Rais wa Palestina Mahamoud Abbas, ametia siani mkataba wa makubaliano wa kujiunga rasmi kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa inayo shughulikia makosa ya jina na ukiukwaji wa haki za binadamu ICC, masaa machache baada ya kamati ya usalama ya umoja wa mataifa kushindwa kupitisha ombi la uhuru wa Wapalestina.
Akiongea baada ya kumaliza kusaini kujiunga na ICC, rais Mahmoud Abbas alisema " wanatushambulia kila siku, angani, majini na kila sehemu, wapi tutapeleka malalamiko yatu? Ikiwa kakati ya usalama ya umoja wa mataifa imetukataa."
Akiunga mkoni kitendo cha rais Abbas kusaini kujiunga na ICC, Hanan Ashrawi, ambaye ni mwanadiplomasia alisema " tumekuwa watu wapole katika majadiliano tangu 1991, wakati mpango wa kuwa na mataifa mawili ya Kipalestina na la Kizrael kuzikwa, hivyo hiki kitendo cha leo ni muhimu kwa Wapalestina."
Kufuatia kujiunga kwa Wapalestina na ICC, kumetoa uwezo kwa mahakama ya kimataifa kuweza kuchunguza mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yamefanyika katika maeneo ya Wapalestina.
Kufuatia kujiunga kwa Wapalestina kwenye koti ya ICC, waziri mkuu wa Izrael, Benjamin Netanyahu amesema " Kitendo cha Abbas, kutawafanya Wapalestina kushitakiwa, kutokana na vitendo vyao vya kigaidi na hasa kwa kuunga mkono kundi la Hamas.
"Sisi kwa upande wa Izrael hatukubaliani na uamuzi wa Wapalestina, na tutalinda haki za Waizrael."
Uamuzi huu wa Wapalestina kujiunga na ICC, kumekuja baada ya kamati ya Usalama ya umoja wa mataifa kushindwa kupitisha muswaada ulioletwa na Wapalestina, baada ya Marekani na Australia kupinga muswaada huo, ambao ulikuwa unadai Izrael kusimamisha kitendo cha kuchukua ardhi ya Wapalestina kwa nguvu na kurudisha wanazo kalia kwa kufuata mipaka ya makubaliano ya mwaka 1967.
Posted by Kibatala at Thursday, January 01, 2015 0 comments
Tuesday, December 30, 2014
Marekani yataka nguvu za kijeshi kutumika nchini JD Kongo.
Russ Feingold, ambaye ni mwakilishi wa Marekani katika ukanda wa Maziwa makuu amesema "
"Ikiwa kutatokea ucheleweshaji wa kukabidhisha siraha, kundi la DFLR ndilo litakalo faidika, huenda wakazitumia siraha hizo katika ukiukaji wa haki za binadamu.
"Hivyo jeshi la umonja wa mataifa - MUNUSCO, lipo tayari pindipo hili nilisemalo litatokea ili kukabiliana na kundi hilo, na napenda hili lieleweke kuwa nguvu za kijeshi zitatumika."
Kundi la DFLR ambalo ni la Wahutu wenye mlengo mkali na wanaopingana na serikali ya Kigali, wamekuwa wakishutumiwa kwa kuhusika na ukiukwaji wa haki za binadamu na inaaminika bado kuna wapiganaji 1400 ambo bado wanashirikiria siraha zao.
Iran yadai haita buruzwa katika mazungumzo ya kinyulia.
Tehran, Iran - 30/12/2014. Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Mohammad Javad Zalif, amesemakuwa Iran itasimama imara katika majadiliano yake kinyuklia yatakayo anza 15/01/2015.
Akiongea Javad Zalif alisema " bado kuna upana ambao unatakiwa kipunguzwa katika mazungumzo hayo. Hatupo tayari kusukumwa sukumwa.
"Tutakuwa Imara kama mwanzo na la muhimu ni kuhakikisha vikwazo vyote vinaondolewa kama tulivyo sema hapo awali. Nakama hakutakuwa na makubaliano, Iran ipo tayari kwa hali na mali kukabiliana na lolote litakalotokeo."
Mazungumzo hayo ya Iran na mpango wake wa kuendelea na muzalisha nyuklia yanangojewa, kwani matokeo ya katika mkutano huo yanaweza badirisha sura ya dunia katika ulimwengu wa kinyuklia.
Mazungumzo ya kinyuklia ya Iran yanajulikana kamaya nchi 5+1 ambayo yanajumuisha Urusi, Marekani, China, Unigereza na Ufaransa.
Uingereza kupingwa muswaada wa Wapelestina UN.
New York, Marekani - 30/12.2014. Uingereza imetamka kuwa itapinga muswaada wa Wapalestina walio uwakilisha umoja wa mataifa, ambao unaitaka Izrael kusimamisha chukuaji wake wa ardhi ya Wapelestina kinguu, na kurudisha maeneo yote wanayo miliki Waizrael.
Mark Lyall, ambaye ni balozi wa Uingereza wa Umoja wa mataifa ameseama kuwa " jibu la Uingereza ni hapana kwa muswaada huo.
"Kwani lugha ambayo imetumika inaleta walakini, hasa kuongezeka kwa lugha ya wakimbizi, na hivyo kunaugumu katika sualazima la hali hiyo."
Matamshi hayo ya Uingereza, yamekuja baada ya hapo awali Marekani kutamka kuwa inapinga muswaada huo wa Wapalestina kwa kuwa haukuelezakuhusu usalama wa Izrael
Muswaada wa Wapalestina umekuwa ukipigiwa chepuo na Jordan, ambapo inataka kura ya kupitisha muswaada huo ipigwe siku ya Alhamis, jambo ambalo kwa sasa linaelekea kuwa na ugumu. Kwani Uingereza na Marekani zaweza tumia kura zao za vito kupinga muswaada huu.
Posted by Kibatala at Tuesday, December 30, 2014 0 comments
Talibani waikejeli NATO.
Wapalestina wawakilisha muswaada wao uhuru umoja wa Mataifa
"Ni suala la kuwaunga mkono Wapalestina ni muhimu, na ndio maana nchi za muungano wa nchi za Kiarabu zimeunga mkono muswaadahuo.
Alisema balozi wa Dina Kawar, ambaye ni balozi wa Jordani wa Umoja wa Mataifa.
"Kutakuwa na mazungumzo na wajumbe wa Palestina, nini kifanyike na lini kura zipigwe, ili kupitisha muswaada huo." aliongezea Kawar
Muswaada huo wa Wapalestina, ulipingwa na Marekani na Izrael, kwa madai kuwa hauelezei kuhusu hali ya Amani ya Izrael.
Hata hivyo wajumbe wa Palestina wamesema kuwa katika muswaada huo, lipo suala la majadiliano ya miji ya West Bank, Mashariki ya Jerusalem na Ukanda wa Gaza, miji ambayo michoro yake ya kiramani ilibadirika baada ya vita vya Mashariki ya Kati vya 1967.
Hatung'oi buti nchini Sudani ya Kusini, asema raia Museven.
Kampala, Uganda - 29/12.2014. Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Mseven, amesema kuwa jeshi la Uganda litaondoka nchini Sudani ya Kusini pindipo Amani ya kudumu itakapo patikana.
Akiongea kuhusu hali ya Amani ya Sudani ya Kusini, rais Museven alimeam, "tatizo si la Uganda, tatizo ni Amani ya kudumu inayo takiwa nchini Sudani ya Kusini.
Kunatakiwa hali ya utulivu na Amani iwepo, kwani jeshi la Uganda haliwezi ondoka na kuachia mwanya wa vurugu kurudia.
Serikali ya Uganda iliamua kupeleka jeshi lake nchini Sudan ya Kusini, baada ya kutokea mvutano wa madaraka kati ya rais Salva Kiir na makamu wake Riek Machar, jambo ambalo lilileta kuvurugika kwa Amani.
Hata hivyo Riek Machar, amekuwa akidai kuwa jeshi la Uganda linatakiwa kuondoka nchini Sudani ya Kusini,kwa kuhisi kuwa lina unga mkono utawala wa SPLM uliopo chini ya raia Salva Kiir.
Talibani waikejeli NATO.
"NATO na washiriki wake wamekunja bendera katika mazingira ya kushindwa, na kukabidhi madaraka ya kiulinzi kwa serikali ya Afghanistan, ni jibu kuwa Taliban wameshinda, kwani mpaka leo sisi bado tupo. Alisema msemaji wa Taliban Zabihulla Mujahid.
"Na Kuanzia sasa Taliban itashika usukani, na wale waliofikiliwa kuachiwa madaraka watashughulikiwa kama tulivyo lishughulikia jeshi la NATO na washirikia wake na sasa wanakimbia." Aliongezea Mujahid.
Vita zidi ya kundi la Taliban vilianza mwaka 2001, vikiwa na madhumuni ya kuungamiza utawala wa Taliban, na kusababisha vifo wanajeshi karibu 3,500, na pia kuleta hasara kijamii nchini Afghanistan na watu wengi kupoteza maisha yao.
Posted by Kibatala at Tuesday, December 30, 2014 0 comments
Monday, December 22, 2014
Muhammad Ali alazwa hospitalin.
Obama alaani mauaji ya Polisi.
New York, Marekani - 21/12/2014. Rais wa Marekani Barack Obama amelaani mauaji ya polisi wawili katika jiji la New York, ambao walikuwa wakishika doria ndani ya gari lao.
Rais wa Misri amfuta kazi Mkuu wa ujasusi
Kairo Misri - 21/12/2014. Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi leo amemfukuza kazi mkuu wa upelelezi Jenerali Mohamed Farid el- Tohamy aliyeteuliwa siku chache tu baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani Mohamed Mursi mwezi Julai mwaka jana.Jenerali Khaled Mahmoud Fuad Fawzy ambaye alikuwa msaidizi wa Farid el Tohany ndiye aliyeteuliwa kuchukua nafasi yake.
Hata hivyo hakuna sababu zozote zilizo elezwa za kufukuzwa kazi kwa Jenera Farid el
Tohan.
Wakati huo huo, Misri leo imekifungua mpaka wa Rafah, ambao utawawezesha wakazi wa Ukanda wa Gaza, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miwezi miwili kuweza kuingia na kutoka Misri.
Misri ilifunga mpaka wa kuingia Gaza, Oktoba 25 baada ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu katika eneo la Sinai kuwauwa wanajeshi wake 33.
"Kwani hatufanyi maamuzi kwa kupitia vyombo vya habari, bali ukweli utakapo patikana basi sheria zitafuata."
Mazungumzo hayo ya rais Obama yamekuja baada ya Korea ya Kaskazini kukanusha kuhusika na mashambulizi ya kimtandao kwa kampuni ya Sony, na kuitaka Marekani kuonyesha ushirikino ili kulitafutia ukweli suala la uvamiaji wa mtandao wa kampuni ya Sony.
Muhammad Ali alazwa hospitalini.
Kentaki, Marekani - 21/12/2014. Aliyekuwa bingwa ndondi kwa uzito wa juu duniani Muhammad Ali mwenye miaka 72, amelazwa katika hospitali ya mji wa Loiseville ili kutibiwa homa ya mapafu.
Bob Gunnell, ambaye ni msemaji wa Ali, alisema " Ali anatibiwa na kundi la madaktari wake na yuko anaendelea vyema.
Mohammed Ali, ameshakuwa hospitali kwa siku moja na anatarajiwa kuruhusuhusiwa kutoka hopitalini baada ya Madaktari kulidhika na mwenendo wa afya yake .
Posted by Kibatala at Monday, December 22, 2014 0 comments
Saturday, December 20, 2014
Liberia yasifiwa na Ban Ki-moon zidi vita vya Ebola.
Nchi za
Africa zatakiwa kushirikiana na mahakama ya ICC.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema kuwa Mogherini atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri mkuu Haider Al-Abadi, na baadaye siku ya Jumanne atakuwa na mazungumzo na rais wa jimbo la Kurdi, Masoud Barzani katika mji wa Irbil.
Ziara hiyo za Mogherini itakuwa na madhumuni ya kuona ni kwa jinsi gani Umoja wa Ulaya, utasaidia katika kupambana na kundi na dola la Kiislaam , ambapo hadi sasa Umoja wa Ulaya umeshatoa euro milioni 20 kusaidia kutatua matatizo ya kiutu ambayo yamesababishwa na kundi hilo wapiganaji wa IS wanaoshikiria maeneo kadhaa nchini Iraq.
Waziri Frank Walter Steinmeier aonya kuhusu Urusi.
Waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier,ameleezea wasiwasi wake kuhusu msukumo uliyopo wa vikwazo kutoka kwa nchi wanachama wa nchi za umoja wa Ulaya kuwa hutahatarisha na kuiyumbisha Urusi, ambapo wimbi lake litaleta mtikiso katika bara la Ulaya.
Walter Steinmeier alisema kuwa, kushuka kwa tahamni ya Lubo, fedha inayo tumika Urusi, hakutakuwa na faida kwa nchi za Ulaya, hivyo ni bora kuwepo na uangalizi katika sheria za kuweka vikwazo kwa Urusi.
Mazungumzo hayo ya Steinmeier, yamekuja baada kikao cha wakuu wanchi za jumuiya ya Ulaya, kuionya Urusi kuwa kama haitabadiri msimamo wake dhidi ya Ukraine, nchi za Umoja wa Ulaya hazita sita kuongeza vikwazo zidi ya Urusi.
Posted by Kibatala at Saturday, December 20, 2014 0 comments