Maandamano yafanya rais wa Misri kuvunja serikali.
Saturday, January 29, 2011
Maandamano yafanya rais wa Misri kuvunja serikali.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 29, 2011
1 comments
Friday, January 28, 2011
Serikali ya Misri ipo njia panda.
Nelson Mandela aruhusiwa kutoka hospital.
Johannesburg, Afrika ya Kusin - 28/01/2011. Aliyekuwa rais wa kwanza baada ya kuanguka kwa utawala wa kibaguzi wa makaburu ameruhusi kutoka hospital Mill Park ambako alikuwa amekwenda kwa matibabu.
Nelson Mandela mwenye umri wa miaka 92 alikuwa hospitalini kwa matibabu baada ya kutojisikia vizuri kiafya.
Makamu wa rais Kgalema Motlanthe aisema " Mandela ana nafuu na alikuwa anataniana nasi na tuzidi kumwombea afya yake iwe nzuri."
Picha hapo juu anaonekana Winnie Mandela akitokea hospital kumwangalia mumewe Nelson Mandela ambaye alikuwa amelazwa hospital.
Serikali ya Misri ipo njia panda.
Kairo, Misri 28/01/2011.Maelfu ya wananchi nchini Misri wameandamana kupinga serikali iliyopo madarakani na huku polisi wakipambana na waandamaji kwa kutumia gasi na maji.
Posted by
Kibatala
at
Friday, January 28, 2011
0
comments
Wednesday, January 26, 2011
Uchumi wa dunia kujadiliwa tena Davos.
Uchumi wa dunia kujadiliwa tena Davos.
Davos,Swiss - 26/01/2011. Viongozi wa serikali, wafanya biashara,,wanasiasa na wanauchumi, wanakutana nchi Uswisi ili kujadili mpangilio mzima wa uchumi dunia. Mkutano huo ambao utachukua siku tano, unatarajiwa kujadili mbinu za kuinua uchumi baada ya mtikiso mkubwa wa uchumi ulio ikumba dunia miaka miwili iliyo pita.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kiuchumi wanasema " inabidi katika mkutano huu viongozi, wanasiasa,wafanya biashara na wanauchumi watafute ufumbuzi wa kuinua uchumi na siyo kuweka ahadi ambazo zimekuwa ziki tawaliwa na mzunguko wa siasa na hai halisi ya kiuchumi.
Picha hapo juu ni mji wa Davos, ambao viongozi wa nchi tofauti, wafanya biashara, wanasiasa na wanauchumi wanakutana kujadili hai halisi ya uchumi duniani.
Tunis,Tunisia - 26/01/2011. Polisi wa kimataifa wameombwa kukamata aliye kuwa rais wa Tunisia, mkewe na washiriki wa karibu wa familia yake ili wajibu mashitaka mbele ya mahaakama.
New York, Amerika - 26/01/2011. Umoja a Mataaifa umeombwa kuchangia mbinu mbadala za kupambana na maharamia waliopo katika pwani ya Somalia hadi kufikia pwani za Afrika ya Mashariki na kuanzisha koti maarumu itakayo husika na kesi za kiaaramia.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, January 26, 2011
0
comments
Tuesday, January 25, 2011
Serikali ya Palestina yakanusha kuridhia Waizrael.
Ukanda wa Magharibi, Palestina - 25/01/2011. Serikali ya Wapalestina imekanusha vikali habari zilizo patikana ya kuwa uongozi huo umeridhia swala Wakimbizi wa Kipalestina.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, January 25, 2011
0
comments
Saturday, January 22, 2011
Tony Blair awelwa kiti moto tena.
Tony Blair awekwa kiti moto tena
London, Uingereza - 22/01/2011. Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza wakati wa vita vya Irak na kumtoa madarakani hayati Saadam Hussein ameojiwa kwa mara nyingine tena na tume ya uchunguzi wa mwenendo mzima wa vita vya Irak.
Tony Blair ambaye alikuwa waziri mkuu wa Uingereza, chini ya serikali yake alishirikiana na serikali ya Amerika iliyo kuwa ikiongozwa na rais George Bush na kumn'goa madarakani rais Saadam Hussein wa Irak.
Akiongea mbele ya tume hiyo Tony Blair alisema " nasikitika kwa kwa wale wote waliopoteza maisha au kuathirika kutokana na vita hivi." Na nilimwahidi rais wa Amerika ya kuwa kutakuwa bega kwa bega katika vita hivi kwani niliamini Saadam Hussein alikuwa kiongozi hatri kwa jumuia ya kimataifa."
Uingereza na Amerika kwa kushirikiana na washiriki wengine ziliongoza vita vilivyo vikia kungólewa madarakani kwa rais wa Irak, Saadam Hussein.
Picha hpo juu ni ya aliye kuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ambaye aalikuwa akijibu maswali kutoka katika tume ya kuchunguza mwenendo mzima wa vita vya Irak.
Paris,Ufaransa - 22/01/2011. Kiongozi wa kundi la Al Qaeda ametishia na kuitaka serikali ya Ufaransa kutoa wanajeshi wake aliopo katika nchi za Kiislaam.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 22, 2011
0
comments
Wednesday, January 19, 2011
Ombi la kukamatwa kwa Tzipi Livni lakataliwa.
Odinga, Ouwattara na Gbagbo hakuna maelewano.
Abidjan, Ivory Coast-19/01/2011. Msuruhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast ambaye pia ni waziri mkuu wa Kenya ameondoka nchi humo bila kupata suruhisho la mgogoro huo.
Tunis, Tunisa- 19/01/2011. Rais wa kipindi cha mpito nchini Tunisia ametangaza yakuwa atahakikisha maswala yaliyo leta kutokuelewana na kunyanyasa wanachi hayatarudiwa tena na kutaka wanchi wa Tunisia kufungua ukurasa mpya.
Fouad Mebazaa, akitangaza kupitia TV na vyombo vingine vya taifa na kimataifa alisema, sisi sote kwa pamoja tunaweza kuiongoza na kuijenga nchi yetu na hivyo tufungue ukurasa mpya ili kuijenga nchi yetu ambayo imeyumba kisiasa na kiuchumi."
Hata hivyo bado kunahali ya mvutano wa kisiasa nchini Tunisia huku wanchi wakudai ya kuwa bado serikali hiyo inaviongozi waliokuwa wakati wa utawala wa rais Zine Ben Ali ambaye ameikimbia nchi baada ya wanachi kutaka atoke madarakani.
Nayo serikali ya Swissi imezizuia mali zote za aliyekuwa rais wa Tunisia Zine Ben Ali.
Picha hapo juu anaonekana rais wa mpito wa Tunisia Fouad Mebazaa akishuka kutoka kwenye gari, huku akiwa analindwa vikali na walinzi wake tayari kuelekea ofisini kuanza kazi rasmi ya kuongoza nchi.
Ombi la kukamatwa kwa Tzipi Livni lakataliwa.
Pretoria, Afrika ya Kusini- 19/01/2011. Serikali ya Afrika ya Kusini imekataa ombi la kutaka akamatwe aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini humo.
Ombi hilo lilitolewa na Shirika la Uhusiano la Wapalestina, kwa adai ya kuwa aliyekuwa waziri wa mamboya nje wa Izrael Tzipi Livni alihusika katika wakati jeshi la Izrael lilipo shambulia eneo la Gaza mwidho wa mwaka 2008 hadi mwanzoni mwa mwaka 2009.
Mclntosh Polela ambaye ni msemaji wa ofisi ya usalama na makosa ya jinai alisema "tumepata ombi la kutaka kukamatwa kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya njee wa Izrael na hatutachukua hatua hiyo na Tzipi Livni hatakamatwa kwani hakuna ushahidi wa kutosha zidi yake."
Picha hapo juu ni ya Bi Tzipi Livni, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya njee kati ya miaka ya 2009-9.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, January 19, 2011
0
comments
Saturday, January 15, 2011
Rais wa Tunisia akimbia nchi.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 15, 2011
0
comments
Thursday, January 13, 2011
Wahaiti wakumbuka siku ya tetemeko la ardhi.
Wahaiti wakumbuka siku ya tetemeko la ardhi.
Port au Prince, Haiti - 13/01/2011. Maelfu ya wananchi wa Haiti wamekutana katika jiji la Port au Price kukumbuka siku ambayo tetemeko la ardhi lilitkea na kupoteza maisha ya watu na kuleta maafa makumbwa kwa kila jamii kiuchumi na kiafya.
Tetemeko hilo ambalo lilipoteza maisha ya watu wapatao 316,000 kupoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa mashirika tofauti yanayotoa misaada nchini Haiti yamesema " hadi kufikia sasa hali nchini humo bado siyo ya kulizisha na juhudu zinatakiwa kuongezeka ili kuijenga nchi hiyo na kuinua hali ya misha ya watu wake."
Picha hapo juu ni misaraba ikiwa inawakilisha watu waliopoteza maisha wakati wa tetemeko la ardhi lililo tokea mapema mwaka 2010.
Waamerika waombwa kuungana na kushirikiana.
Tucson, Amerika - 13/01/2011. Rais wa Amerika amewataka Waamerika wote kuungana na kuishi kwa ushirikiano ijapokuwa kunatofauti za kisiasa.
Rais, Baraka Obama aliyasemahayo wakati alipo udhulia siku maalumu ya kuwakumbuka watu walioshambuliwa kwa risasi na kupoteza maisha ya kwenye jimbo la Arizona.
Baraka Obama alisema " mambo mabaya hutokea na nilazima tujitahidi kuwa wavumilivi hasa tukizingatia tumepoteza watu sita kutokana na ukatili uliofanyaka."
Mtu anayehusika na mauaji hayo Jared Lougher 22 anashikiliwa kutokana na kufanya kitendo hicho cha kikatili.
Picha hapo juu wanaonekana rais Baraka Obama akiwa na mke wake Micheel wakishika kwenye ndege kuelekea kuhudhulia siku maalumu ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mashambulizi ya kikatili.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, January 13, 2011
1 comments
Wednesday, January 12, 2011
Kesi ya Julian Assange yaanza kusikilizwa.
Kesi ya Julian Assange yaanza kusikilizwa.
Brisbane, Australian - 12/01/2011. Maelfu ya wakazi wa mji wa Brisbane wamehama mji mara baada ya mji mzima kukumbwa na mafuriko ya kihistoria.
Beiruti, Lebannon - 12/01/2011. Serikali ya Lebanon imevunjika baada ya washiriki katika serikali ya muungano Hezbollah kujitoa.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, January 12, 2011
0
comments
Sunday, January 9, 2011
Wasudan wapiga kura kuamua muungano wa nchi yao
Wasudan wapiga kura kuamua muungano wa nchi yao.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, January 09, 2011
0
comments
Friday, January 7, 2011
Al Shabab walaumiwa kwa kuzuia misaada ya utu.
Al shabab walaumiwa kwa kuzuia misaada ya utu.
Mogadishu, Somalia - 07/01/2010. Serikali ya Somalia inalimaumu kundi la Al Shabab kwa kuzuia misaada ya kiutu ambayo inatolewa ja jumuiya ya kimataifa.
Habari kutoka wizara ya mambo ya ndani ya nchi zinasema ' inakuwa vigumu kusambaza misaada ya kiutu kutokana na hali ya kutokuwepo kwa usalama kwa wafanyakazi wanaohusika katika kutoa misaada."
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Somalia ni moja ya nchi ambayo ilikubwa na hali ya ukame, kiasi cha kuhatarisha hata mifugo.
Picha hapo juu inaonyesha ni kwa kiasi gani hali ya ukame ilivyo hasili maisha ya watu na na wanyama.
Posted by
Kibatala
at
Friday, January 07, 2011
0
comments
Tuesday, January 4, 2011
Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wakubali kukutana.
Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wakubali kukutana.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, January 04, 2011
0
comments
Sunday, January 2, 2011
Brazil wapata rais wa kwanza mwana mke.
Brazil wapata rais wa kwanza mwanamke.
Brasilia, Brasil - 02/01/2011. Wananchi wa Brazil wameshuudia kuapishwa kwa rais mpya wa nchi yao, baada ya muda wa rais wa sasa Luiz Lula da Silva kumalizika.
Dilma Rousseff aliapishwa mbele ya watu wapatao 70,000 wakiwemo wageni waalikwa kutoka nchi tofauti duniani.
Rais Dilma aisema " nitajitahidi kulinda na kuendeleza yale yote ambayo rais Luiz Inacio Lula Da Silva aliyo fanya katika kuinua uchumi wa wanchi wa Brazil na kuinua kiwango cha kila mwanchi kiuchumi."
Picha hapo juu anonekana rais wasasa wa Brazil Dilma Rousseff kushoto akiwa na rais aliye mwachia ofisi Luiz Inaci Lula da Silva kwa pamoja wakiwa wamenyanyua mikono mara baada ya kuapishwa kwa Dilma Rousseffe kuwa rais wa kwanza mwanamke.
Urussi yaaanza kuiuzia China mafuta.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, January 02, 2011
0
comments
Saturday, January 1, 2011
Dunia nzima yashangilia kuanza mwaka 2011
Dunia nzima yashangilia kuanza mwaka 2011.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, January 01, 2011
0
comments

