Thursday, April 3, 2008

Waziri mkuu wa zamani wa Kosovo,hanahatia, mahakama ya mwachia huru.

Bi, Naomi awa matatani na polisi uwanja wa ndege mjini London.

London,Uingereza - Mwana dada, Naomi Campbell amekamatwa na polisi kwenye kiwanja cha ndege Heathrow.
Bi, Naomi, amekamatwa na polisi,baada ya kukorofishishana na polisi wakiwanja cha ndege.
Bi, Naomi aligombana na polisi, baada ya kupishana lugha na na polisi hawa kuhusu mizigo yake kwenye termimal 5.
Pichani za hapo juu anaonekana bi Naomi, akiwa amepozi wakati wa moja ya maonyesho ya sanii.
Umoja wa mataifa upo kwa ajili yakuleta amani na utuilivu duniani kote"asema katibu mkuu"
Bucharest, Romania - Katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana, Ban Ki moo, amesema ya kuwa umoja huu haupingi Uislam.
Bwana Ki moo, aliyaongea haya kwenye kikao cha NATO kinacho fanyika mjini Bucharest, na kupinga maneno ambayo ya meongewa na kiongozi na mbili wa Alqaida, bwana Ayman Al- Zawahir, ambaye amedai yakuwa umoja huu wa mataifa unashiriki katika kupiga vita Uislamu.
Aliongezea yakuwa umoja huu upo kwa ajili ya kuleta amani na utulivu duniani kote.
Bwana Ki moo, amealikwa katika kikao hiki kuongea na viongozi wa NATO, kuhusu maswala ya amani duniani,kwanai NATO , ni shirikisho lenye nguvu duniani.
Picha hapo juu anaonekana bwana, Ban Ki moo, akongea na waziri mkuuwa Uingereza kuhusu maswala fulani, huku akonyesha kwa vitendo kutumia mkono wake.
Chini ni picha ya kiongozi namba mbili wa kundi la Aqaida, bwana Ayman Al Zawahiri, akiongea kupitia mtandao.
Waziri mkuu wa zamani wa Kosovo, hanahatia, mahakama ya mwachia huru.
The Hague, Holland - Mmoja ya watuhumiwa wa vita vya Kosovo,bwana Ramush Haradinaj,ameachiliwa huru baada ya kesi dhidi yake kukusa ushaidi kamili.
Bwana, Ramush Haradinaj, ambaye alishawahi kuwa waziri mkuu wa Kosovo, aliachiwa huru , baada ya baadhi ya mashahidi kushindwa kutoa ushahidi dhidi yake kwa kuhusika katika viata vya wenyewekwa wenyewe ambavyo vilifanyika nchin Kosovo 1998.
Akiongea mbele ya koti , jaji Alphonss Orie, alisema ya kuwa imekuwa ni vigumu kumtia hatiani mtuhumiwa kwani ushahidi haukuwa wakutosha.
Kabla ya hapo wakili wa mahakama hiyo waliomba mahakama imuhukumu bwana Ramush Haradinaj kifungo cha miaka 25 jela, laki hata hivyo kutokana na ukosefu wa ushahidi imekuwa ni vigumu , alimalizia mmoja ya wanasheria wa mahakama hiyo.
Picha hapo juu kulia ni picha ya bwana Ramush Haradinaj, akitabasamu baada ya jaji kusema yakuwa hakuna ushahidi na hivyo hayupo hataiani.
Picha ya pili naonekana bwana Ramush Haradinaj,akiingia mahakamani wakati wa mwazo wa kuanza kesi dhidi yake.
Mtetezi wa haki za binadamu awekwa ndani na Pilato kwa kuongea.
Beijing, China - Mmoja wa watetezi wa haki za binadamu nchini China bwana Hu Jia, amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miaka mitatatu na nusu, kwa kosa la kuongea mambo amabyo serikali ya China haikufurahishwa nayo.
Bwana Hu Jia, amekutwa na hatia baada ya habari alizo ongea na waandishi wa habari, kuonekana kwenye (internet) au mtandao.
Bwana Hu Jia ,amekuwa mtetezi wa haki za binadamu nchini China ,na amekuwa akiongelea hasa swala la wagojwa wa ukimwi na matatizo yanayo wakuta wagonjwa hao nchini China.
Hata hivyo shirika la kuteteta haki za binadamu na mataifa ya magharibi yameiomba serikali ya Chnia kumwachia huru, bwana Hi Jia, kwani wanakiuka haki zabinadamu na haki za kila mtu kueleza au kutoa maoni yake.
Pichani hapo juu ni picha ya bwana Hu Jia kabala yakukamatwa kwake. Na picha nyingine anaonekana bwana Hu Jia alipo kuwa amewekwa kifungo cha ndani siku za nyuma
Imani za dini inapogongana na sheria alizo weka binadamu nani mkweli?
New-York, Umoja wa mataifa - Katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ba Ki- moo, siku ya ijumaa ya 28/3/ 2008, ameonya na kulani kitendo cha mmoja wa wabunge na kiongozi wa chama cha siasa bwana Geert Wilders kwa kitendo chake chakutaka kuonyesha picha za sinema ambazo zinahusisha Uislam.
Bwana, Ban Kim-moo, alisema yakuwa hali hii inahatarisha na inaleta mgongano wa kiimani katika jamiii. Na alieleza ya kuwa anafahamu ni kwa jinsi gani, serikali ya Holland ,inavyo jitahidi kuzuia sinema hii isionyeshwe.
Katibu mkuu huyu alisema hakuna sheria ambayo inayo ruhusu mtu kueleza maoni yake ambayo yanaweza leta maafa katika jamii, na hivyo lazima tuwe wangalifu na sheria hizi.
Bwana Geert Wilders, ametengeneza picha ya sinema ijulikanayo kama FITNA, ambayo imeleta mzozo mkubwa katika jamii ya wananchi wa Holland na Jamii ya waumini wa dini ya Kiislaam duniani.
Pichani hapo juu wanaonekana baadhi ya wananchi wakianadamana kupinga kuonyeshwa picha ya sinema ijulikanayo kama FITNA.
Picha ya pili anaonakana katibu mkuu wa umoja wa mataifa bwana Ban Ki moo, akiongea na wandishi wa habari hivi karibuni.
Picha ya tatu , ni picha ya bwana Geert Wilders, ambaye picha yake ya sinema ijulikanayo kama FITNA inagonganisha vichwa vaya watu.

Ufaransa yaanza mikakati ya kutaka kuachiwa kwa bi, Ingrid Betencourt's

WTA, Miami yaonyesha ya kuwa Serena bado kiboko kwa kila anaye kuja.

Miami, Amerika - Mwana dada Serena Williams, ameweza kuendelea kwenya mashindano ya tenis kwa upande wa wanawake (WTA) baada ya kufika nusu fainali.
Bi, Serena Williams, ambaye kufika kwake nusu fainali kumekuja baada ya kumnyanyasa bi Justine Henin.
Bi Serena, alishinda kwa pointi 6-2, 6-0, kwenye mpambano wa kukata na choka uliofanyika mjini Miami.
Bi, Justine Henin na bi Serena Williams wamekuwa wapinzani wa jadi tangu walipo anza kukutana kiprofecheni miaka isiyo pungua mitano iliyo pita.
Waziri mkuu ajiuzuru kwa kufuatwa na kashfa za mafaranga.
Dublin, Irland(Irish) - Waziri mkuu wa Irland ( Irish) bwana Bertie Ahern , amaetangaza ya kuwa atajiuzuru wadhifa wake ifikapo mwezi wa mei tarehe 6, baadha ya kudhuka kwa kashfa juu yake.
Bwana, Bertie Ahern mwenye umri wa miaka 56, anashutumiwa kwa kuchukua pesa kutoka kwa baadhi ya wafanyabishara kwa vipindi tofauti kati ta miaka ya 1989 na 1992.
Lakini bwana Bertie Ahern, amekanusha kashfa hii na kudai yakuwa hana hatia wa wasiwasi wa swala hili.
Hata hivyo, waziri Bertie Ahern, anasifika kwa kuinua uchumi wa kisiwa hiki cha Irish.
Pichani hapo juu anaonekana bwana Bertie Ahern akitangaza tarehe ya kujiudhuru kwake.
Picha ya chini anaonekana waziri, Bertie Ahern akwaaga baadhi ya watu aliokuja kusikiliza yale aliyo yasema.
Mambo si shwali tena nchini Somalia, wapinzani wateka baadhi ya maeneo.
Mogadishu, Somalia - Mapigano mapya yamezuka tena nchini Somalia, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 19, mapigano hayo ambayo yamesababisha hali ya wasiwasi kurudi tena jiji Mogadishu.
Mapambano haya yaliongozwa na kundi la Islamic Courts Union, amablo pia limedai ya kuwa limeteka mji wa Baidoa na kuteka vifaa vingi vya kijeshi kutoka kwenye kundi la wanajeshi wa serikali.
Pichani wanaonekana baadhi ya wananchi wakiwa hawajui la kufanya , mmoja wa wapiganaji akiwa ameshikilia bunduki tayari kwa lolote litakalo tokea.
Wazimbabwe tuwepamoja kujenga nchi yetu, tuachane na siasa," Mfanya biashara aomba".
Harare, Zimbabwe - Baadhi wa wakazi wa jamii ya ulaya au wazungu ambao ni wazaliwa wa nchi ya Zimbabwe wamekuwa na maoni tofauti kuhusu hali halisi ya uchaguzi nchini humo.
Mmoja wa wakazi hawa bwana Mercer, ambaye ni mfanyabiashara, alisema ya kuwa inabidi sisi kama Wazimbabwe tuungana kujenga nchi yetu, na maswala ya siasa yasituvuluge vichwa vyetu, kwani siasa ndio chombo pekee ambacho siku zote kinaleta migogoro kataika jamii, na matatokeo yake hivi leo ni vikwazo kila kukicha , na juu ya vikwazo hivi ni vigumu kwetu kufanya biashara na ndio maana hatuagizi, wala hakuna wateja, kutokana na migogoro ya siasa.
Hivyo Wazimbabwe tujenge nchi yetu na kuwa pamoja.
Ufaransa yaanza mikakati ya kutaka kuachiwa kwa bi, Ingrid Betancourt's.
Bogota, Kolombia - Serikali ya Ufaransa na washiriki wake Spain na Uswisi wanafanaya mkakati wa kutaka kuachiwa kwa mwana siasa na mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, bi Ingrid Batancourt's, ambaye ameshikiliwa na wanajeshi wa kundi la FARC.
Kundi hili la FARC, linapingana na serikali ya Kolombia kwa kipindi kisicho pungua miongo miwili.
Bi Ingrid Betancourt's ambaye ana uraia wa Ufaransa na Kolombia, na alisha wahi kuwa mgombea wa Urais kipindi cha nyuma kabla ya kukamatwa kwake na waaasi wa FARC.
Kutokana na habari kutoka kwa ndugu na familia , zinasema yakuwa bi, Betancourt's anamatatizo ya kiafya na huenda yakahatarisha maisha yake.
Picha hapo juu anaonekana mama wa bi Ingrid Betancourt's , akiongea kwa uchungu na majonzi kuhusu hali ya afya ya mwanae bi Ingrid.
Picha nyingine anaonekana, bi Ingrid Betancourt's akiwa kwenye kambi ya wapinzani wa FARC , ambao wanamchikilia hadi sasa.
Picha ya chini anaonekana na mtoto wa bi, Ingrid Betancourt's, Lorenzo akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya kiafya ya mama yake, ambaye amashikiliwa na waasi wa FARC.
Waumini wa dini ya Bodee, watafikishwa mbele ya Pilato kujibu mashitaka.
Beijing, China - Zaidi ya watu wasiopungua 1000, watafikishwa mahakamani katika jimbo la Tibeti, mapema mwezi wa mei mwaka huu. .
Mmsemaji mmoja wa serikali ya Beijing, amesema ya kuwa , watuhumiwa hawa wana husika na machafuku ya kisiasa na kijamii katika jimbo la Tibeti.
Mmsemaji huyo alisema ya kuwa machafuko haya yalikuwa yamepangwa na waumini wa dini ya Mabodee ambao wanaongozwa na Dalai Lama.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya waumini wa dini ya Bodee, wakiwa wanasoma vitabu vya dini yao.
Mvutano kati ya NATO na Urusi bado kitendawili, wapewa matumaini hapo baadaeye.
Bucharest, Romania - Shirikisho la Umoja wa Kijeshi la nchi za Ulaya (NATO) limekubaliana kwa pamoja ya kuwa nchi za Georgia na Ukreini kusubiri kuwa mwanachama wa shirikisho la NATO.
Hali ya uamuzi huu inakuja baada ya kuwekewa ngumu na nchi ya Rusia ( Urusi), kwani nchi hii ina ona ya kuwa nchi hizi kuwa mwanachama wa shirikisho hili litahatarisha usalama wa nchi ya Urusi, kwa kuzingatia nchi hizi zipo karibu na Urusi.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa NATO wamesema nchi hizi zisiwe na wasiwasi ipo siku zitajiunga na shirikisho hili.
Vile vile Rusia ( Urusi) ina pinga mpango wa Amerika kuweka mizinga ya ke karibu na mipaka ya Urusi, ama nchi ambayo ipo karibu na nchi hii ya Urusi.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi vinara wa NATO, waziri mkuu wa Uingereza bwa Gordon Brawn na rais wa Amerika bwana George Bush.

Monday, March 24, 2008

Pope John Poul II aonekana katika umbile la moto"Adai aliye piga picha"

Nyota ya the Green Eagles yataka weka daruga za soka muda si mrefu.

London, Uingereza - Mchezaji na nyota ya timu ya taifa ya Nigeria Jay Jay Okacha, amesema ya kuwa msimu wa soka wa 2007-2008, huenda ukawa mwisho wake wa kucheza soka la kulipwa.
Ja Jay Okacha, ambaye kwa sasa anachezea timu ya Hull, amekuwa kivutio kikubwa kila awapo uwanjani kulisakata gozi la ngombe,hasa alipo kuwa amevalia jezi ya timu yake ya taifa ya Nigeria na kufunga magori 59 mpka hapo malipo jiudhuru kuchezea timu hii ya taifa.
Jay Jay Okacha, ambaye ameanzia kucheza timu ya Ujerumani Franfrut, Uturuki Fenebasche,PSG Ufaransa na Bolton ya Uingerea, amekuwa chachandu kwa kila timu aliyo chezea.
Pichani hapo juu anaonekana Jay Jay akiwa nanafanya vitu vyake ndani ya jezi ya the Green Eagles.
Picha ya pili anaonekana,Jay Jay Okacha akiuliza ya kuwa vipi, kwani kila aje kwangu ajue nipo kazini, lazima wawe fiti.
Picha ya tatu anaonekana Jay Jay Okacha, anaonekana akitoa kitu ambacho makipa huwa ni vigumu kutabiri ni jinsi gani wanaweza kuzuia kitu hiki.
Pope John II aonekana katika umbile la moto" adai mpiga picha hii".
Rome, Itali - Picha ambayo ipo katika umbile la moto, imeoneka hivi karibuni wakati wa kuazimisha miaka miwili toka kiongozi wa kanisa Katoriki Duniani hayati Pope John Poul II aiage dunia
Picha hii ilipigwa na polisi mmoja ambaye alipiga picha hii aliseama alikuja kuitambua picha hii baada ya ya muda fulani.
Maadhimisho haya yalifanyika karibu na eneo alilozaliwa Pope John II, kwenye mji wa Beskid Zywiecki.
Pichani hapo juu ni picha ya hayati Pope John II, akitoa salamu na baraka kila alipo kuwa akiwa ziarani, na upande wa pili ni picha ya umbile la moto ambayo ilipigwa siku ya kuadhimisha miaka miwili toka aage dunia.
Miaka mitano ya vita vya Irak, bado utata, " nani zidi".
Baghdad, Iraq - Dunia nzima hivi karibuni imeazimisha miaka mitano tangu vita vya Iraq vianze vikiongozwa na Amerika.
Haki hii imekuwa ya maoni tofauti na mabadiliko makubwa kijamii na kisiasa, aliongea haya , mmoja ya wafanyakazi wa zamani wa shirika la msaraba mwekundu bwana Roland H Benjanin ambaye alikuwa nchini Iraq, wakati wa vita vinaanza.
Shirika la msaraba mwekundu lilitoa wafanayakazi wake wote baada ya jengo lao kulipuliwa na na kusababisha vifo vya wafanayakazi wake. Hata hivyo vita hivi vmeleta maafa ya kupoteza maisha ya watu kutoka jamii tofauti,kuanzia wanajeshi na raia pia
Vita hivi mpaka sasa inasemekana idadi ya wanajeshi 4000, wa Amerika wamepoteza maisha yao, hii ni kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa mambo ya kivita nchi Amerika.
Picha hapo juu anaonekana mmoja wa raia wa Iraq akiwa ameshikiliwa na wenzake huku akiwa na uchungu na majonzi baada ya mmoja wa familia yake kuuwawa na bomu hivi karibuni.
Picha pili chini anaonekana mwanajeshi wa jeshi la Amerika akiwa kazini huku raia wa Iraq,wakimwangalia kwa walakini.
Hatuelewi wanamuomba nani msamaha," kwani wanatakiwa kutimiza walicho haidi, mmoja wa wanajeshi waliopigana vita vya Iraq".
New York, Amerika - Harakati za kupata walichokuwa wakipigani imefika hali ya kuwa usumbufu kwa wanajeshi waliopigania nakutetea nchi ambayo walikuwa wanajua ya kuwa wakimaliza kutimiza kazi waliyo tumwa na hawatakuwa na wasiwasi wakuwa raia wa nchi amabyo walipigania na nchi ambayo ilikuwa ndoto yao, haya yalisemwa na mmoja wa wapiganaji ambao walikuwa mstari wa mbele kataika vita vya kumng'oa madarakani rais wa Iraq hayati Saadam Hussein.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wapiganaji hawa, bwana Abdool Habibullah mwenye miaka 27, ambaye ni mzaliwa wa Guyana, alisema yakuwa aliomba urai wa amerika semptemba 2005, baada ya kurudi kwenye mambano ya Iraq,na mpaka sasa 2008, bado anangojea majibu, nas inaelekea alicho ongea rais Bush ya kuwa hali itakuwa nzuri na kila kitu kitakuwa sawa tutakapo rudi kutoka vitani. Sasa hatuelewi nani wanaomba msamaha,kwani wanatakiwa kutimiza hahadi waliohaidi.
Akiongezea yakuwa hali hii ni kuto kuwajibika kwa baadhi ya watu waliopo maofisini, mmoja ya wapiganaji walio rudi kutoka vitani Krzsztof Matejqowasqi mwenya miaka 22, ambaye amekaa Iraq kwa kipindi cha miezi 15 alipo rudi alikuta yakuwa karatasi za maombi yake ya kuwa raia wa Amerika zimepotea.
Picha hapo juu ni moja ya wanajeshi ambao wamepigana vita vya Iraq, na mpaka sasa wanasubiri uraia wao kupitishwa.
Kamati ya Usalama na Ulinzi ya Umoja wa mataifa, inakiuka miiko yake,na Darfur wanateketea.
New York - Amerika -Aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa bwana Kofi Annan, amesema ya kuwa kamati ya ulinzi na usala ya Umoja wa Mataifa ina kiuka( miiko)wajibu wake kwa kufungia macho matatizo yanayao tokea Darfur.
Akiongea haya wakati alipo kuwa amealikwa kwenye chakula, bwana Kofi alisema ya kuwa dunia nzima imekuwa ikitegemea kamati hii ya ulinzi na usalama kufanya maamuzi ambayo yana manufaa kwa wanadamu wote, lakini sivyo kamati hii inavyo fanya.
Aliongozea ya kuwa kupelekwa kwa jeshi la Umoja wa Afrika Darfur, imekuwa ni kitendawili kwa kamati hii, na wakati huo huo watu wanazidi teketea kwa kipindi kirefu sasa.
Bwana Annan, ingawa hakutaja nchi, lakini inaeleweka ni nchi zipi zipo kwenye kamati hii, aliongea haya mmoja ya wageni walioalikwa kwenye chakula hiki kula pamoja na bwana Annan
Wa Cyprus wataka kuwa kitu kimoja, viongozi wao wasisitiza.
Nicosia, Cyprus - Viongozi wapinzani wa kisiwa cha Cyprus, bwana Mehmet Ali Tarat na Demetris Christofias, walikutana na kuongea chini ya usimamizi wa umoja wa Mataifa.
Mkutano huu ulifanyaiaka kwenye eneo ambalo lipo chini ya Umoja wa mataifa.
hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa viongozi hawa kukutana baada ya bwana kuwa rais wa Cyprus ambayo ipo upanda wa Greeki.
Viongozi hawa walisema ya kuwa wanataka kufungua kitabu kipya, na kuleta mabadiriko ya kisiasa kisiwani hapo.
Kisiwa cha Cyprus, kimegawanyika sehemu mbili, moja ipo chini ya serikali ya Uturuki na nyingine ipo chnini ya serikali ya Greesi.
Talibani, wasema bado wapo ngangali, waja na mbinu mpya za mapigano.
Kabul, Afghanistani - Kiongozi wa kundi la Talinani bwana Jalaluddini Haqqani, ametangata ya kuwa kundi lake litaanz mashambulizi umpya ya kupigana na wanajeshi wa NATO amabao wapo nchini Afghanistani.
Akiongea katika runinga ambayo ememuonyesha bwana, Jalaluddini Haqqani akiwa amepauka kwa kiasi,aliendelea kusema ya kuwa. kupotea kwao ilikuwa ni moja ya mbinu za kujijenga upya, na hivyo vita hivi hawakuwa wameshindwa, na sasa wamekuja na mbinu mpya ya kushambulia kwa kutumia mbinu za kuvuizia na kushusha.
Picha hapo juu anaonekana kiongozi wa Talibani, bwana Jalaluddini Haqqani akiwa ndani ya gani moja nchini Aghanistani.
Picha nyingine ni picha ambayo inaonyesha jinsi gani Talibani wanavyosumbua vichwa ya jumuia ya kimataifa,kwani hapo katika picha ni moja uaribifu uliotokea baada ya bomu kulipuka na kuuwa baadhi ya wanajeshi wa NATO na wakazi wa eneo hili.
Jeshi la Umoja wa Afrika kuanza kuonyesha misuri yake katika kutatua matatizo ya bara la Afrika?
Njuani, Komoro - Kikosi cha jeshi la Umoja wa Afrika, kimewasili kwenye kisiwa cha Njuani, tayari kupamabana kurudisha kisiwa hicho mikononi mwa serikari.
Inaaminika zaidi ya wanajeshi wasiopungua 1000, kutoka Tanzania, Sudani, na Senegali wapo tayari kukiweka kisiwa hicho mikononi mwa serikali, aliongea haya msemaji wa jeshi hilo la umoja wa Afrika, kamanda Yahaya Abdalhah.
Serikali ya Libya ndiyo itakayo toa kila aina ya misaada ya kiufundi na kitaaluma.
Kisiwa cha Komoro kimekuwa na mgogoro wa kisiasa tangu ulipo fanyika uchaguzi 2002.
Pichani hapo juu wanaonekana wanajeshi wa jeshi la jeshi la Umoja wa Afrika wakiwasili kwenya kisiwa cha Juani nchini Moroko.

Wednesday, March 5, 2008

Polisi atoa siri ya serikali"Serikali ya kanusha" Ushwari kuanza kurejea.

Nyota ya timu ya Barcelona yapata majeraha kwa mara nyingine.

Barcelona, Uispania - Mchezaji nyota wa timu ya Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi, hataweza kucheza kwenye mechi au mazoezi kwa kipindi kisicho pungua wiki sita, baada ya kuchanika misuri ya mguu wake wa kushoto.
Messi,amekuwa akisumbuliwa na majeraha tofauti ambayo yamekuwa yakimkuta kila mara.
Akisema haya mganga wa timu ,aongezea yakuwa itambidi apumzike kwa kipindi na siyo vyema kumharakisha kuanza mazoezi.
Akiongezea haya kaptaini wa timu ya Barcelona, Chales Puyol alisema ya kuwa wapenzi wa timu yao wamakuwa wanadai Messi achezeshwe, pindipo akionekana ana nafuu kidogo, na akashauri wawe wavumilivu na kuacha kazi hii iwe ya waganga wa timu.
Pichani hapo juu anaonekana Lionel Messi akiwa na nyota ya soka Diego Armando Maradona.
Picha ya pili anaonekana Messi akiwa anafanya mavitus kabla ya kupata majeraha ya misuri wakati wa pambano la marudiano na timu ya Celtic ya Schotland.
Picha nyingine naonekana Mesi akiwa anagaaga chini, baada ya kupata maumivu,na picha ya chini anaoneka Lionel Messi akiwa anatolewa nje ya uwanja na mmoja wa viongozi wa timu ya Barcelona.
Bi, Madona atoa album mpya, wapenzi wake kukonga roho.
London, Uingereza - Malkia wa muziki wa pop, bi Madonna amezindua rasmi album mpya ijulikanayo kama Hard Candy.
Album hiyo ambayo imekuwa ikingojewa kwa hamu saana, imeanza rasmi kupataikana tangu tarehe, 29/april/2008.
Madonna ambaye kila anapotoa album yake huwa ana kujas na kitu kipya, hivyo kwenye album hii, amesema ya kuwa hii albumu ni kwa ajili ya wale wanaopenda lawalawa.
Picha hapo juu anaonekana bi Madonna , akiwa ame mwaga tabasamu ya hali ya juu, kuashiria ya kuwa wapenzi msiwe na shaka album hii ita konga roho zenu.
Picha ya pili na ya tatu anaonekana bi Madonna anapo kuwa kazini hataki mchezo, huwa anafanya kweli kwa kila zana za muziki.
Picha ya bhapo chini anonekana bi Madonna akiwatumbwiza wapenzi wake huku akiwa amavalia vazi lenye rangi ya mapenzi.
Mafuriko yaleta madhara makubwa kwa wakazi wa Kusini mwa Afrika.
Windhoek, Namibia - Mvua kubwa ambayo inaendelea kunyesha maeneo ya Kusini mwa Afrika, inasababisha uharibifu mkubwa na kuleta madhala makubwa kwa wakazi wamaeneo haya,haya ni kwa mujibu wa msemaji wa msemaji wa kamati ya uokoji na kusaidia kwenye maeneo yaliyo dhurika na mvua hizi bwana Gabriel Kangowa.
Kwa mijibu wa msemaji wa UN, kwa upande wa kusaidia watoto alisema kunazaidi ya watoto wapatao 15000, ambao wanahitaji msaada wa haraka zaidi kwenye maeneo haya..
Mafuriko haya yameleta madhara maeneo tofauti ya nchi za Namibia, Zambia,Zimbabwe, Mozambiki na Malawi.
Picha hapo juu zinaonekana sehemu tofauti amabazo zimekumbwa na mafuriko na kuleta madhara makubwa kwa wakazi wa maeneo ya kusini mwa Afrika.
Polisi atoa siri ya serikali "Serikali yakanusha" ushwari kuanza kurejea.
Nairobi, Kenya - Serikali ya Kenya imekanusha ya kuwa haijawahi kuwa na mkutano wa siri na kundi la Mungiki, kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Akiongea, msemaji wa serikali alikanusha ya kuwa hakukuwepo na mkutano waina yoyote kati ya serikali na kundi hilo.
Inasadikiwa mkutano huo ulifanyika kwa siri, ili kuweza kupanga ni jinsigani kundi hili linaweza kulinda watu wa kabila la Wakikuyu na mali zao hasa maeneo ya Lift Valley.
Siri hii imefichuka baada ya moja wa askari wa polisi kuongea na shirika moja la habari,na kueleza ni kwanini kwenye baadhi ya maeneo, watu wenye siraha waliruhusiwa kuvivuka vizuizi vya polisi bila kuzuiliwa kuelekea maeneo yaliyo tokea fujo.
Picha hapo juu, wanaonekana polisi wa Kenya wakipambana na moja ya watu amabo wanashutumiwa kuleta vurugu na machafuko.
Picha nyingine wanaonekana wananchi wenye huruma wakimsaidia mmoja wa majeruhi, aliye pata majeraha kutokana na vurugu hizi.
Picha ya chini anaonekana, aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Matifa bwana Kofi Annan, akiongea na waandishi wa habari baada ya viongozi wa pinzani wa Kenya, bwana Mwai Kibaki na Laila Odinga kukubaliana kuongoza nchi kwa pamoja.

Ukanda wa Gaza, bado waleta kichwa kuuma kwa serikali ya Amerika.
Gaza, Palestina - Rais wa Palestina bwana Mahmoud Abbas, ameseama ya kuwa hataendelea na mazungumzo ya kuleta amani kati ya Israeli na Palestina.
Rais Mahamoud Abbas aliyasema haya wakati alipo kuatana na waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Amerika bi, Condoleeze Rice, wakati alipo kwenda kumuona kujadili ni jinsigani utulivu unaweza kurudi, baada ya machafuko yaliyo tokea siku za karibu, kati ya kundi la Hamas na na Jeshi la Israel.
Waziri wa mambo ya nje wa Amerika, yupo ziarani kwenye maeneo haya, kuendeleza mazungumzo ya amani katai ya Israeli na Palestina.
Machafuko haya ambayo yameanza tena kwenye ukanda wa Gaza yamekuwa ya kuwa, yakivuruga upatikanaji wa amani katika eneo hili kwa muda mrefu.
Picha hapo juu anaoneka arais Mahamoud Abbas, akimkaribisha bi, Condoleeze Ricealipo kwenda kumtembelea hivi karibuni.
Picha chini anaonekana bi,akikaribishwa na mmoja wa viongozi wa Israeli, alipokwenda kuongea na viongozi wa Israeli
Viongozi wa dini zote kukutana mjini Rome, kuunga dalaja la imani kwa waumini wao.
Rome Itali - Kiongozi wa Kanisa Katoliki diniani Pop Benedict,ataongoza mkutano kati ya Waumini wa Kikristu na Waumuni wa Kiislamu utakao fanyika mwezi wa November mwaka huu.
Akiongea haya msemaji wa wa Vatican alisema ya kuwa mkutano wa kwanza utafanyika november 4 mpaka 6 mjini Rome.
Mkutano huu utaudhuliwa na viongozi wa dini wa wapatao 24 na walimu wa dini zote.
Moja ya mazungumzo yatakayo watakayo zingatia na kujadili kwa undani ni Upendo wa Mungu,n upendo kwa jirani , utu na kuheshimiana kwa watu na imani zao.
Picha hapo juu ni alama inaonekana alama ya mwezi na nyota kama alama ya Uislamu, kati ni alama ya Msalaba ikiwa ni ishara ya kuamini Ukristu
Chini ni picha ya Pop Benedict, akiwa ameshikilia na kukinyanyua kitabu kitakatifu juu.
Rais,Hugo Chavez aionya, serikali ya Kolombia kaeni chonjo, kazi mbaya si mchezo mwema.
Cucuta,Vanezuela - Serikali ya Venezuela, imeaanza kupeleka majeshi yake pamoja na vifaru kwenye mpaka na nchi ya Kolombia,haya ni kwa mujibu wa msemaji wiraza ya ulinzi.
Kupelekwa kwa wanajeshi hawa mpakani, kuna kuja baada ya jeshi la Kolombia, kuingia kinyume cha sheria nchini Ekuado na kumua kiongozi wa kundi la FARC,bwana Raul reyes.
Kuwepo kwa majeshi haya mpakani mwa Kolombia na Venezuela, ni kuwa seriakli ya Venezuela inajiandaa kuzuia uwezekano wa majeshi ya Kolombia kuvuka mpaka na kuingia nchini Venezuela, ambapo inadaiwa ya kuwa, mipakani humo ndipo wapinzani wa serikali ya Kolombia FARC, wanaishi.
Picha ya juu, anaonekana rais Hugo Chavez, akiongea na waandishi wa habari kuhusu maswala ya ulinzi nchini Venezuela.
Picha nyingine anaonekana, rais Hugo Chavez, akijaribu siraha amabyo ni moja ya siraha zitakazo tumika, pindipo vita vikianza kati ya Venezuela na Kolombia.
Picha ya chini wanaonekana wanajeshi wa Venezuela wakiealeka mpakani mwa Venezuela na Kolombia.