Baraka Hussein Obama, aapishwa rasmi kuwa rais wa 44 wa Amerika. "Amerika ya pata rais wa kwanza Mwafrika (Mweusi) na ukurasa mpya umefunguliwa, na ndoto imetimia.


Baraka Hussein Obama, aapishwa rasmi kuwa rais wa 44 wa Amerika. "Amerika ya pata rais wa kwanza Mwafrika (Mweusi) na ukurasa mpya umefunguliwa, na ndoto imetimia.


Posted by
Kibatala
at
Tuesday, January 20, 2009
0
comments
Ethiopia ya ondoa majeshi yake nchini Somalia,"Wasiwasi wazidi".
Addis Ababa,Ethiopia-13/01/09. Serikali ya Ethiopia, imetangaza rasmi, jeshi lake lililo kuwa linasaidia kulinda usalama nchini Somalia, limeanza rasmi kuondoka nchini Somalia kuelekea nyumbani.
Kufuatia kuondoka kwa jeshi la Ethiopia,hali ya usalama nchini Somalia imekuwa katika hali ya wasiwasi kwa mujibu wa mmoja wa makzi wa mji wa Mogadishu
Hata hivyo, kuna habari ya kuwa umoja wa Mataifa, upombioni kupitisha mswada wa kupeleka jeshi la kimataifa ili kulinda amani,kwani kuondoka kwa jeshi la Ethiopia, kumeacha majeshi ya Burundi na Uganda kuwa majeshi pekee ambayo yanasaidia kulinda amani kwa serikali ya Somalia.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza awa na kazi ngumu na mgogoro wa Mashariki ya Kati.
London,Uingereza-13/01/09.Vita vinavyo endelea katia ya Izrael na Palestina,vimeleta utata na kazi kuwa ngumu kwa aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Brair, ambaye anashughulikia swala la kuleta amani katia ya Waizrael na Wapalestina.
Washington, Amerika-13/01/09.Rais mchaguliwa wa Amerika, Baraka Obama,atatia sahii kufungwa mara moja kwa gereza la Guantanamo Bay, mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Amerika, Gantanamo Bay, imekuwa jela ya kuwafungia watuhumiwa wanao shukiwa kuhusika na ugaidi.
Jerusalem,Israel-13/01/09. Waziri Mkuu wa Izrael, Ehud Olmert, amesema yakuwa alimpigia simu rais George Bush, kuomba Amerika isipige kura kupitisha kura ya kutaka kusimamisha mapigano kati ya Izrael na Palestina.
Doha, Katar-13/01/09. Serikali ya Misri,imekataa kukubaliana na jumuia ya nchi za Kiaarabu kutumia mkutano unao tarajiwa kufanyika mjini Doha,tarehe 18/01/09,kujadiri swala la vita vinavyoendelea katia ya Israel na Palestina.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, January 13, 2009
0
comments
Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi zachafua jina la letu"China ya dai"
Beijing,China-08/01/09.Waziri wa mambo ya nje ya China Quin Gang, ameziliaumu nchi za Magharibi kwa kutumia vyombo vya habari kuharibu jina la nchi yake China.
Dakar, Senegal-08/01/09- Watu tisa wamehukumiwa kwenda jela miaka minane, baadada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na maswala ya ushoga.Kwa mujibu wa mwanasheria wa watuhumiwa hao,Diadji Diouf.
Brussel,Belgium-08/01/09.Jumuiya ya Ulaya imekuwa na mazungumzo na kampuni ya mafuta ya Urusi Gazprom, ambayo imefunga usambazaji wa gasi katika nchi za jumia ya Ulaya.
Gaza, Ukanda wa Gaza-08/01/09.Shirika la kutoa misaada la Umoja wa Mataifa, limesimamisha misaada yake yote kuelekea eneo la Gaza.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, January 08, 2009
0
comments
Accra Ghana -7/01/09. John Atta Mills, mwenye miaka 64, ameapishwa kuwa rais wa Ghana, baada ya kushinda uchaguzi wa urais zidi ya mpinzani wake Nana Akufo Addo.
Gaza,Ukanda wa Gaza - 4/01/09.Vita vinavyo endelea kati ya Israel na Kundi la Hamas, zimefikia hatua ya kugonisha vichwa jumuiya za kimataifa.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, January 07, 2009
0
comments
Nchi za Kiarabu zatakiwa kuongeza juhudi kutatua mgogoro wa Palestina na Israel "Katibu waUmoja wa mataifa ".
Umoja wa Mataifa,Amerika-29/12/08. Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon,amezitaka Palestina na Israel kusimamisha mapigano mara moja , na kurudi katika meza ya majadiliano.
Katibu huyo, Ban Ki-moon, akisitiza hayo,alizitaka nchi za Kiaarabu kufanya kila juhudi ili kuleta amani katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza kwani juhudi wanazo zifanya hazisaidi, hivyo inabidi waongeze juhudi zaidi.
Katibu Ban Ki-moon, alisema vita vilivyopo kwenye Ukanda wa Gaza, haukubaliki na jumuia ya kimataifa, hivyo lazima visimamishwe mara moja kwani vita hivyo vinaleta mazara makubwa kwa jamii na watu wa pande zotembili, Israel na Palastina kupoteza maisha yao.
Picha hapo juu anaonekana, Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kikao na kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali alisi na nini kifanyike ili kuwepo na amani katika eneo la Ukanda wa Gaza.
Umoja wa nchi za Afrika waonyesha makali yake"Guinea yasimamishwa uanachama".
Conakry,Guinea-29/12/08.Umoja wa nchi za Afrika (AU- African Union), umesimamisha uanachama wa nchi ya Guinea, baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi.
Baidoa, Somalia-29/12/08.Rais wa Somalia, Abdullahi Yusufu Ahmed amejiuzuru nafasi yake ya urais wa kuingoza nchi hiyo ambayo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi.
Gaza,Ukanda wa Gaza-29/12/08.Mgogora wa Mashariki ya Kati yameingia hatua nyingine, baada ya serikali ya Israel kushambulia katika maeneo ya Gaza, kwa kutumia ndege zake, ili kuvunja kabisa nguvu la kundi la Hamas, ambalo linaongoza katika mapambano na serikali ya Israel.
Posted by
Kibatala
at
Monday, December 29, 2008
2
comments