Thursday, April 9, 2009

Swala la nguvu za nyuklia ni kitendawili kwa Iran, Amerika na washiriki wake.

Kim Jong Il, achaguliwa kuwa rais wa Korea Kaskazini tena.

Pyongyang,Korea ya Kusini - 09/04/09.Kiongozi wa Korea ya Kaskazini,Kim Jong Il, amechaguliwa tena kuwa kiongozi na rais na bunge la nchi hiyo.
Kim Jong Il, alikuwa anashikilia madaraka yaliyo achwa na baba yake Kim Il Sung alifaliki dunia 1994, alikuwa ka rais wa mpito.
Kwa kuchaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, atakuwa ni kiongozi wa jeshi la Korea ya kaskazini.
Picha hapo juu, anaonekana akikagua jeshi, ambalo kwa sasa litakuwa chini yake.
Picha ya pili, wanaonekana, baadi ya wanchi wakiwa katika moja ya sherehe za kitaifa nchini Korea ya Kusini.
Swala la mguvu za nyuklia ni kitendawili kwa Iran, Amerika na washiriki wake.
Isfahan,Iran 09/04/09 - Rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad, amefungua rasmi mtambo kutengenezea nguvu za kinyuklia, katika mji wa Isfahan.
Katika sherehe ya ufunguzi wa mtambo huo, rais wa Iran, alisema mazungumzo ni lazima yawe ya faida kwa pande zote mbili na siyo kwa faida ya upande mmoja tu
.
Rais, Mahmoud Ahamadinajad, alisema hayo,kuonyesha ya kuwa, maelezo yaliyo tolewa na rais wa Amerika , Baraka Obama hivi karibuni,hayakuwa kizuizi cha Iran kuendelea kiteknolojia katika nyanja za matumizi ya nguvu za nyuklia.
Huku akisisitiza, rais ,wa Iran , alisema, mazungumzo kati ya Amerika na Iran katika swala la nyuklia, yanatakiwa yawe ya kisheria za kimsingi, na siyo Amerika nchi ye nye nguvu kutumia,chombo cha kutathmini nguvu kusimamisha maendeleo ya Iran kiteknolojia.
Hata hivyo , rais wa Amerika, alionya ikiwa Iran, inatakakuwa na uhusiano mzuri na Amerika na jumuia ya kimataifa ni lazima isimamishe mpango wake wa kuendeleza kuzalisha nguvu za kinyuklia.
Picha ya hapo juu, anaonekna rais, wa Amerika , Baraka Obama, akiongea katika moja ya mkutano na wandishi wa habari, wakati wa ziara yake ya kwanza katika bara la Ulaya tangu kuwa rais wa Amerika.
Picha ya pili , ni ya rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, akiongea mara baada ya kufungua mtambo mpya wa kuendeshea nguvu za kinyuklia katika mjin wa Isfahan.
Utata wa kisiasa nchini Georgia, waleta mshaka kwa rais.
Tiblisi, Geogria -09/04/09 - Hali ya kisiaasa nchini Georgia imeendela kuwa ya utata , baada ya mamia ya fuasi wa vyama vya upinzani na viongozi wao wameaaandamana hadi kwenya maeneo ya bunge kwa madai razima rais Mikheil Saakashvili, ajiudhulu kutaka madarakani kwa kushindwa kutekeleza ahadi alizo zihaidi kabla ya uchaguzi nakuwa na ukilitimba wa madaraka.
Akiongea hayo wakati wa maandamano hayo,Levan Gachechiladze, ambaye alikuwa mgombea mpizani wa kiti cha urais wa Georgia, alisema watakaa mbele ya bunge mpaka hapo, rais atakapo sikiliza hoja za wananchi.
Hata hivyo wakati viongozi wa vyama vya upinzani wanafanya maandamano , rais Mikheil Saakashvili alikuwa akiwahutubia wanchi wa Georgia kwa kusisitiza umoja kwa wanchi wa Geogria,katika kumbukumbu za kuazimisha tangu, Georgia ilipo kwa moja ya nchi za umoja wa shirikisho za nchi za Kirashia.
Picha hapo juu , ni ya rais wa Georgia, Mikheili Saakshvili, anaye daiwa ajiudhulu toka madarakani na vyama vya upinzani.
Picha pili, wanaonekana wanchi wa vyama vya upinzani wakiandamana kuelekea kwenya ukumbi wa bunge kwa madai ya kuwa ni razima rais ajiudhulu.
Picha ya tatu , wanaonekana mamia ya waandamanaji wakiwa mbele ya bunge la Georgia, wakidai rais ajiudhulu,ndipo watatoka katika eneo hilo.
Wafuasi wa Al Sadr,wataka majeshi ya kigeni yaondoke.
Baghdad,Irak - 09/04/09 - Maelfu ya watu wameaandamana ,kwa madai ya kuwa jeshi la Amerika na washirika wake waondoke nchini humo.
Wafuasi na mwadau wa kiongozi wa Shia Murtada al Sadr, ambaye anajulikana kupinga kuwepo kwa majeshi ya kigeni, walionekana wakiwa wameshikilia mabango ya picha ya kiongozi huyo na huku wakidai ni lazima majeshi hayo ya kigeni yaondoke.
Waandamanaji hao wakikusanyika katika mnara wa aliyekuwa rais wa Irak , hayati Saddam Hussein, ambapo mnara huo, uling'olewa na jeshi la Amerika,mara baada ya kufanikiwa kuianguha serikali ya rais Saddam Hussein.
Irak,imekuwa chini ya majeshi ya kigeni kwa kipindi cha miaaka sita, tangu kuuangushwa kwa aliyekuwa rais wa Irak, Saddam Hussein na jeshi la Amerika na washirika wake.
Picha hapo juu wanaonekana waandamanaji wakiwa wameshikilia mabango na bendera katika moja ya mtaa mjini Baghadad.

Wednesday, April 8, 2009

Rais wa zamani wa Peru aongezewa miaka 25 zaidi kukaa jela.

Tetemeko la ardhi la leta maafa nchini Itali.

Rome Itali - 08/04/09.Idadi ya watu waliokufa kutokana na maafa ya tetemoko la ardhi lililo tokea katika mji wa L'Aquila mji uliopo karibu na Rome wamefikia 260.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa shirika la msalaba mwekundu, kunaidadi ya watu 30,000, ambao wamepoteza makazi yao kutokana ma tetemeko hilo lililo kuwa na nguvu ya 5.6 magnitude.
Meya wa L'Aquila, alisema tetemeko hilo lilitokea usiku wa manane wakati watu wakiwa wa melala.
Picha hapo juu, yanaonekana matenti ambayo yanatoa huduma ya kwanza kwa watu walio kutwa na maafa.
Picha ya pili anaonekana, mmoja ya wahudumi wa huduma ya kwanza akijaribu kumtuliza mmoja mkazi aliyekumbwa na maafa.
Rais wa zamani wa Peru, aongezewa miaka 25 zaidi kukaa jela.
Lima,Peru - 08/04/09.Mahakama nchini Peru, imetoa adhabu ya kifungo cha miaaka 25, kwa rais wa zamani wa nchi hiyo Alberto Fujimori ambaye kwa sasa anamiaka 70.
Rais huyo wa zamani, ambaye kwa sasa,alikuwa anatumika kifungo cha miaka sita baada ya kukutwa na hatia katika kesi ya awali.
Hukumu hiyo ,ilitolewa baada ya mahakama kumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji, utekaji nyara, na kukiuka haki za binadamu wakati alipo kuwa madarakani wakati wa miaka ya 1990s.
Hata hivyo , rais huyo wazamani amekuwa akikana mashitaka yake hayo. Picha ya hapo juu anaonekana, rais wa zamani wa Peru, akiongea enzi za utawala wake alipokuwa rais wa Peru.
Picha ya pili, anaonekana mmoja ya wapenzi na mdau wa uongozi wa rais wa zamani wa Peru,akilalamika kwa uchungu mara baada kuhukumiwa na mahakama nchini Peru.
Hali ya kisiasa nchini Thailand yaanza kuyumba tena.
Bang Kok,Thailand - 16/04/09. Waandamaji wanazidi kuandamana nchini Thailand, kudai waziri mkuu Abhisit Vejjajiva, ajiudhulu kutoka madarakani.
Waandamaji hao wapatao 300,000, waliovalia shati za rangi nyekundu, walionekana wakiwa na mabango, huku wakidai wanataka waziri wao wa zamani, Thaksi Shinawatra aliyepo ukimbizini, arudishwe madarakani.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja wa waandamanaji anaonekana akipiga kerere kudai serikali ijiudhulu.
Picha ya pili, wanaonekana waandamaji wakielekea mjini kuandamana.

Sunday, April 5, 2009

Baraka .H.Obama atangaza kupunguzwa kwa siraha za nyuklia duniani.

Korea ya Kaskazini yarusha chombo chake angani.

Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 04/04/09.Serikali ya Korea ya Kaskazini, imetangaz rasmi yakuwa imefanikiwa kurushwa chombo chake angani saa 0029GMT na kwa sasa kinazunguka dunia.
Chombo hicho kilichorushwa katika kituo cha sayansi cha Musudan- ri, kinasemekana kilipita katika maeneo ya Japan kuelekea maeneo ya Bahari ya Pasifiki.
Kwa mujibu wa serikali ya Korea ya Kaskazini, chombo hicho nikwa ajili ya mawasiliano, na hakipo anga kwa matumizi ya kivita.
Hata hivyo, kurushwa kwa chombo hicho angani na Korea ya Kaskazini, kumeleta wasiwasi, kwa jumuiya ya kimataifa, kwani Korea ya Kaskazini, imekiuka moja ya sheria za kimataifa,kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa.
Picha hapo juu wanaonekana , baadhi ya wana nchi wa Korea ya Kaskazini, wakiangali kwa makini, chombo cha anga kilicho rushwa na walaataamu wa nchi yao.
Picha ya pili, ni ya chombo, cha kurushia mitambo angani, kikiwa tayari kurusha chombo angani, ambacho kipo angani kwa sasa, kwa mujibu wana sayansi wa anga.
Baraka .H.Obama, atangaza kupunguzwa kwa siraha za nyuklia dunia.
Prague,Chech -04/04/09. Rais wa Amerika Baraka .H. Obama, amesema serikali yake itafanya kila jitihada ili kupunguza matumizi ya nguvu za kinyuklia kwa ajili ya kutengeneza siraha, ambazo zitakuja kuleta maangamizi hapo baadaye pindipo zikipitia kwenye mikono potofu.
Rais, Baraka .H. Obama,akiwahutubia maelfu, alisema ni muhimu kwa Amerika kuanza kuongoza katika swala hili la kupunguza siraha za nyuklia, kwa ilisha wahi kutumia siraha hizo, na nilazima nchi nyingine zifuate mfano huo wa Amerika wa kupunguza siraha za nyuklia.
Rais , Obama, alisema ingawaje maangamizi hayo hayatokea wakati wa uhai wake , lakini ni lazima yaanze mara moja, na atahhakikisha serikali yake, itakuwa mstari wa mbele, kwani kwa kufanya hivyo ni kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Picha hapo juu anaonekana, rais wa Maerika , Baraka .H.Obama, akihutubia maelfu waliokuja kumlaki na kumsikiliza, akiongea kuhusu hali halisi ya mabadiliko ambayo walimwengu wanatakiwa kuyafanya ili kuokoa dunia mna mzingira yake yasiharibike, na yatunzwe kwa kizazi kijacho.
Picha ya pili wanaonekana, maelfu waliokuja kumsikiliza rais wa Amerika, Baraka Obama, badaa ya hutuba yake anaonekana rais Baraka .H.Obama, akiwasalimia wananchi kwa kuwapungia mikono.
NATO yatimiza miaka 60 tangu kuanzishwa"Afghanistan bado kitendawili".
Strasbourg,Ufaransa - 03/04/09.Viongozi wa NATO wakiwa wanaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwa NATO, wamekutana nchini Ufaransa, ili kujadili hali halisi ya Afghanistan na kutathmini, mafanikio ya demokrasi yanavyo endelea nchini humo.
Katika kikao hicho viongozi hao wote kwa pamoja walikubalina ni muhimu kujenga Afghanistan, na kuahakikisha hatakuwa tena kwenye mikono ya utawala wa Taliban,na mafanikio hayo yataletwa ikiwa nchi wanachama zitashirikiana kwa zati.
Vilie vile viongozi wa NATO walijadili ni jinsi gani watashirikiana na nchi nyingine ambazo siyo wanachama wa NATO, ili kuweza kuushinda ugaidi unaosumbua dunia.
Picha hapo juu, wanaonekana mawaziri wanchi za nje wakisaini kwa mara kwanza kukubali k,uanzishwa kwa NATO 4/04/1949.
Picha ya pili, anaonekana katibu wa sasa wa NATO, Jaap de Hoop Scheffer, akihutubia viongozi wa nchi wanchama wa NATO, kabla ya kuanza kikao rasmi.
Picha ya pili wanaonekana viongozi wa nchi wanchama wa NATO, wakiwa wamepiga picha kwa pamoja kabla ya kuanza mazungumzo na mjadara wa kuimarisha NATO, tangu miaka 60 ilipo anzishwa.
NATO yapata katibu mpya"Baada ya Uturuki kuridhika".
Brussel, Ubeligiji,03/04/09 - Waziri mkuu wa Denmark Anders Fogh Rasmussen, amechaguliwa kuwa katibu mkuu wa shirikisho la jumuia za nchi zinazo shirikiana kiulinzi na usalama wa nchi wanachama wa Amerika na Ulaya - NATO.
Anders Rasmussen, atachukua ofisi abayo hapo mwanzo ilikuwa ikiongozwa na Jaap Scheffer, ambaye muda wake wakuongoza unakwisha mwezi wa julai (Saba).
Hata hivyo kuchaguliwa kwake, kumekuja baada ya Uturuki, kukubaliana na nchi wanachama,kwani Uturuki ilikuwa ikitaka maelezo zaidi na uhakika kutoka kwa nchi wanchama yakuwa Anders Rasmussen, hatakuwa na msimamo aliyo weka wakati mmoja ya magazeti nchini mwake 2005 yalichapisha picha ta kumkashifu Mtume Muhammed,na hakuchukua hatua kali dhidi ya wahusika.
Nabaada ya nmaelezo ya kutosha ndipo Anders Fogh Rasmussen, alichaguliwa , na anatarajiwa kuanza kazi rami mwezi wa saba 2009.
Picha hapo juu , anaonekana waziri mkuu wa Den Mark, Anders Fogh Rasmussen, akiongea katika moja ya mikutano ya kimataifa ,kujadili hali ya dunia na maendeleo yake.

Thursday, April 2, 2009

Viongozi wa dunia wakubaliana kuikomboa dunia kiuchumi.

Viongozi wa dunia wakubaliana kuikomboa dunia kiuchumi.

London,Uingereza - 02/03/09.Viongozi wa nchi G20 (nchi tajiri na zili zilizoendelea kiuuchumi) zilizo udhulia mkutano ili kujadili kuokoa dunia kuanguka kiuchumi, kwa kuamua kwa pamoja kuwekeza fadha kiasi cha $ 1trillion kwa ajili ya IMF (Internationl Monetary Fund),na benk ya dunia, ili ziweze kuzisaidia nchi ambazo zimeasilika vibaya na mporomoko wa uchumi ambao umeikumba dunia.
Kikao hicho ambacho kimewafanya viongozi wa dunia, wakutane baada ya dunia kukumbwa na mporomoko wa kiuchumi tangu miaka 1930s.
Akifunga kikao,hicho cha G20, waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, ambaye ndiye aliyekuwamwenyeji na mwandalizi wa kutano huu, alisema, zimekubaliana kwa pamoja yakuwa zitachapisha majina ya maeneo ambayo kodi huwa hazilipwi na wawekezaji, na kuhakikisha ya kuwa , hali hii haitarudia tena, kutakuwa na vikwazo kwa wale wote watakao kiuka makubaliano haya.
Vilevile, usili na uficho wa mabenki umefikia mwisho,na lazima uachwe kabisa na wale wote wanaofikilia kuendelea basi wajue jumuia ya kimataifa hatawaachia.
Picha hapo juu , wanaonekana viongozi wa G20,walioudhulia mkutano London 02/04/09, wa kuikwamua dunia kiuchumi wakiwa pamoja kabla ya kuagana baada ya kumaliza mkutano.
Picha ya pili, anaonekna waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, akielekea kwenye jukwa ili kufunga mkutano wa G20.

Wednesday, April 1, 2009

Baraka Obama,ziarani,Ulaya kujadili hali ya uchumi na viongozi wa dunia.

Mkuu wa Taliban, atangaza hali ya hatari kwa Amerika. Washington,Amerika - 01/04/09 - Serikali ya Amerika imetangaz itatoa zawadi ya dola za Kiamerika $ 5 million, kwa mtu atakaye toa habari wapi alipo kiongozi wa Taliban, Baitullah Mehsud, ambaye ametangaza kuwa kundi lake litashambulia Amerika na kuishangaza dunia. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana, zinasema yakuwa kiongozi huyo wa Taliban, alisema ya kuwa kundi lake ndili lililo husika na ulipuaji wa kituo cha polisi mjini Rahore, siku ya jumatatu. Baitatullah Mehsud, anashukiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistani Bi Benazir Bhutto, na mashambulizi yaliyo tokea katika hotela ya Marriot iliyopo Islamabad. Na inaaminika anauhusiano wa karibu na kundi la Al Qaeda. Picha hapo juu ni ya, Baitullah Mehsud, ambaye anatafutwa akiwa hai au amefariki na serikali ya Amerika kwa kuwekewa zawadi ya US dola $ million 5 kwa mtu atakaye toa habari zake ili akamatwe. Hatimaye Israel yapata waziri mkuu mpya.

Jerusalem, Israel - 01/04/09.Benyamin Netanyahu, ameapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Israel, baada ya kupata baraka kutoka kwa bunge la nchi hiyo.
Kuchaguliwa kwa Benyamin Netanyahu, kumekuja baada ya muda mrefu wa mvutano wa kisiasa baada ya uchaguzi uliofanyika mapema mwanzo mwa mwaka huu.
Serikali ya waziri mkuu Benyamin Netanyahu, itakuwa na baraza kubwa la mawaziri katika historia ya Israel.
Baada ya kuapishwa kuwa waziri mkuu wa Israel, Benyamin Netanyahu, alisema yakuwa swala la amani na kuundwa kwa taifa la Wapalestina atalipa kipao mbele katika maswala ya kisiasa, uchumi na ulinzi, huvyo kuwataka viongozi wa Palestina wawe tayari kwa ajiri ya kuleta amani kati ya Waisrael na Wapelestina wenyewe.
Picha hapo juu, anaonekana, Benyamini Netanyahu, akiwa anasubiri matokea ya kura ya yeye kuchaguliwa kuwa waziri mkuu wa Israel.
Picha ya pili, wanaonekana,waziri mkuu wa anayetoka madaraka, Ehud Olmert, akimpongeza waziri mkuu mpya wa Israel Benyamin Netanyahu mara baada ya kuchaguliwa kuwa waziri mkuu.
Baraka Obama, ziarani, Ulaya kujadili hali ya uchumi na viongozi wa dunia.
London,Uingereza - 01/04/09.Rais wa Amrika Baraka Obama, ameanza ziara katika nchi za Ulaya na ataudhulia mkutano wa kiuchuni ambao umeandaliwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Wakati walipo kutana na baadaye kuongea na waandishi wa habari, rais wa Amerika Barka Obama, alisema ni muhimu kwa kila nchi kujitahidi kujikwamua kiuchumi, ingawaje itachukua muda na maumivu makubwa katika jamii.
Picha hapo, juu wanaonekana, polisi ambao wapo katika doria ,ili kuhakikisha ulinzi na usalama wa nchi nzima ya Uingereza wakati wa mkutano huu unaotarajiwa kuanza kesho 02/04/09.
Picha ya pili wanaonekna rais wa Amerika, Baraka Obama na mkewe Michel Obama, wakiwasili katika makazi ya waziri mkuu wa Uingereza kabla ya kuanza mazungumzo na kuudhulia mkutano wa kiuchumi.
Latin Amerika na nchi za Kiaarabu, kuongeza ushirikiano wa karibu.
Doha,Katar - 31/03/09.Viongozi Latini Amerika na viongozi wa jumuia nchi wanachama wa nchi za Kiaarabu,wamekutana ili kujadili maendeleo na ushirikiano wakaribu.
Akiongea katika mkutano huo, Mfalme wa Qatar , alisema yakuwa ingawa Latin Amerika na nchi za Kiaarabu zipo mbali ki jiografia lakini zinauhusiano wa karibu, na ipo haja yakuwashirikisha wanchi wa nchi hizi kwa karibu zaidi.
Katika mkutano huo, utaudhuliwa pia na rais wa Brazil, Lula da Silva, ambaye ndiye mwanzilishi wa ushirikiano wa karibu kati ya mabara haya.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Venezuela, Hugo Chavez , mmoja ya viongozi ambaye anaudhulia mkutano huo.

Monday, March 30, 2009

Mkutano wa nchi za wanachama wa jumuiya za nchi za Kiaarabu waanza kwa vishindo"Rais wa Sudan audhuria mkutano".

Wapenzi wa soka wapotezamaisha"Fifa yataka maelezo".

Abdjan, Ivory Coast - 30/03/09. Zaidi ya watu 22 wamepoteza maisha baada ya kukanyagana wakati walipotaka kuingia uwanjani kuangalia mpira kati ya timu yao ya taifa na timu ya taifa ya Malawi katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya kuingia katika fainali ya kombe la dunia litakalo fanyika nchini Afrika ya Kusini mwakani.
Kufuatia mkasa huo,shirikisho la mpira wa miguu duniani,FIFA, limeitaka chama cha mpira cha Ivory Coast, kutoa maelezo kuhusu mkasa huo ambao umesababisha mauaji na majeruhuhi ya watu.
Picha hapo juu ni alama ya shirikisho la mpira wa miguu duniani,ambalo linasimamia michezo yote ya mpira wa miguu duniani na kupanga sheria za mchezo huo.
Picha ya pili wanaonekna polisi wakiwa wamembeba mmoja ya watu alijeruhiwabaada ya kukanyagwa wakati akijaribu kuingia uwanjani kuangaria mechi kati ya timu ya taifa lake na timu ya taifa ya Malawi.
Waziri wa mambo ya ndani aponea chupuchupu.
Mogadishu, Somalia - 30/09/09. Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Abdirahman Ali, amenusurika kupoteza maisha baada ya gari alilo kuwa akisafiria kukanyaga bomu na kulipuka na kupoteaz maisha ya walinzi wake katika kitongoji kimoja katika mji wa Mogadishu.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, jina limehifadhiwa ,alisema inaelekea hili shambulizi lilikuwa limemlenga waziri huyu.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja ya wapiganajiwa moja ya kundi linalo pingana na serikali ya Somalia.
Mkutano wa nchi za nchi wanachama wa jumuiya za nchi za Kiaarabu waanza kwa vishindo"Rais wa Sudan audhuria mkutano".
Doha, Katar - 30/03/09. Mkutano mkuu wa kuwakutanisha viongozi na marais wa nchi wanachama wa nchi za Kiaarabu, umeanza rasmi nchini Katar, ili kutafuta ni jinsi gani nchi hizi zita weza kutatua matatizo yanayo zikabili nchi zao.
Katika mkutano huo, ambao umekuwa una malumbano mengi ya kisiasa, hasa baada ya mahakama ya kimataifa inayo shughulikia kesi za uarifu na mauaji iliyipo nchini Uhollanzi kutoa hati ya kukamatwa kwa rais wa Sudan Omar Al bashir, ili ashitakiwe kwa makosa ya jinai.
Wakihutubia mkutano huo kwa nyakati tofauti, viongozi wa Syria na Libya, walisema imekuwa jambo la aibu kwa nchi za Kiaarabu kushindwa kushirikia na baadhi ya nchi wanchama wa nchi hizo kuwa vibaraka wa nchi za Ulaya na Amerika.
Katika mkutano huo, rais wa Misri, hakuudhulia mkutano huo, na kwa mujibu wa chunguzi wa maswala ya kisiasa wanasema hii ni kutokana na hali halisi iliyopo eneo la Mashariki ya Kati.
Picha hapo juu ni ukumbi wa mkutano ambamo viongozi wa nchi za jumuia wanachama wa nchi za Kiaarabu wanakutana.
Picha ya pili anaonekana rais wa Libya, Muammar Ghadaffi, akuongea na viongozi wenzake wakati wa mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya ya nchi Wakiarabu mji Doha.
Picha ya tatu ni rais wa Syria, Bashar al Assad, aliongea na kukumbusha makubaliano ya amani katika eneo la Mashariki ya Kati bado kutimizwa hivyo ni lazima nchi za kiaarabu ziungane kuhakikisha mkataba huo unafikiwa na kukamilishwa.
Picha ya nne, anaonekana rais wa Sudan, Omar al Bashir, akiwasili katika mkutano wa viongozi wa nchi za Kiaarabu unaofanyika nchini Katar Doha.
Chuo cha polisi cha shambuliwa nchini Pakistan.
Rahore,Pakistan - 30/03/09 - Mashambulizi yametokea katika kituo cha kufunzia polisi kilichopo Rahore na kusababisha mauaji na majeruhi ya polisi walio kuwa katika majengo hayo.
Chuo hicho kilikuwa na watu wapatao 800, ambao walikuwa katika chuo hicho kwa ajili ya mfunzo ya polisi.
Hata hivyo kwa msemaji wa serikali na mkuu wa operasheni hiyo Majr General Athar Abbas,alisema makamanda waliweza kuwashinda watu walioteka nyara majengo hayo na baadhi yao walikamatwa na wapo chini ya mikono ya serikali.
Picha hapo juu, wanaonekana na baadhi ya polisi na maafisa usalama wakiwa wamemshikilia mmoja ya mtuhumiwa ambaye anasadikiwa kuwa mmoja ya watu walio leta maafa katika chuo cha mafunzo ya polisi cha Rahore.
Picha ya pili wanaonekana wafanyakazi, zima moto na huduma ya kwanza wakiwa wamembeba mmoja wa watuwalio jeruhiwa wakati wa mashambulizi yaliyo tokea katika chuo cha polisi.
Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari kizimbani nchini Kambodia.
Phnom Penh, Kambodia - 30/03/09.Mahakama ya ualifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa iliyopo nchini Kambodia, imeanza kusikiliza kesi ya mauaji ya kimbari yaliyo fanyika mapema miaka ya 1970s, ambapo zaidi ya watu wapatao million 1.7 waliuwawa na baadhi ya viongozi wa kundi la Khmer Rouge.
Majaji watano, wataanza kusikiliza kesi zidi ya aliyekuwa mmoja wa kiongozi, wa kundi la Khmer Rouge, Kaing Guek Eav au kwa jina jingine Duch anashitakiwa kwa kuhusuka na mauaji hayo ya kimbari wakati alipo kuwa mkuu wa jela moja nchini Kambodia.
Kaing Guek Eav au Duch,mwenye miaka 66,anashitakiwa kwa makosa ya kubaka, kuua kwa makusudi,na kutesa watu bila hatia kati ya miaka 1975-1979.
Picha hapo juu, anaonekana, Kaing Guek Eav au Duch, akiwa mahakamani kusikiliza kesi zidi yake zikisomwa.
Picha ya pili anaonekana, Kaing Guek Eavau Duch,akiwa amezungukwa na wanasherika ambao wapo kusikiliza kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari zidi ya mteja wao.

Sunday, March 29, 2009

Rasi wa Brazil,azilaumu nchi tajiri kwa mporomoko wa uchumi.

Rais wa Brazil, azilaumu nchi tajiri kwa mporomoko wa uchumi.

Sao Paulo,Brazil -28/03/09. Rais wa Brazil, Lula da Silva, amezilaumu nchi za tajiri duniani kwa kuleta hali mbaya ya kiuchumi, wakati alipo kutana na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, ambaye yupo nchi Brazili kwa ziara ya kiserikali.
Rais Lula da Silva, alisema yakuwa wazungu wenye macho ya bluu, ndiyo wakulaumiwa, kwa kusababisha mporomoko wa uchumi, kwani hakuna, watu weusi wala waindi ambao wameleta maafa haya ya kiuchumi duniani, na hivyo nchi masikini zisilazimishwe kulipa hasara iliyo sababishwa na watu hawa wenye machoi ya bluu.
Rais, Lula, aliongezea kwa kusema ya kuwa, mporomoko wa uchumi duniani, umeweka wazi ni jinsi gani baadhi ya watu wanavyo fikiria wao ni bora na kumbe sivyo.
Hata hivyo waziri wa Uingereza, Gordo Brown, alisema hivi sasa ni wakati wa kushirikiana kutafuta njia ya kutatua matatizo haya ya kiuchumi.
Picha hapo juu, anaonekana, rais wa Brazil, Lula da Silva, akiongea na wandishi wa habari, mara baada ya mkutano na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Picha ya pili, anaonekna waziri mkuu wa Uingereza, akimwangalia kwa makini, rais wa Brazili, wakati akiongea kuhusu hali halisi, kwa nini uchumi umeporomoka.
Urussi kushirikiana na NATO kuijenga Afghanistan.
Moscow, Urussi-28/03/09.Serikali ya Urussi, imesema ipo ytayari kushirikiana na NATO,ili kuijenga Afghanistan.
Akisema hayo , waziri wa mambo ya nje wa Urussi,Sergei Lavrov,alisema haya wakati wa mkutano unaozungumzia hali halisi ya Afghanistan, uliofanyikia Mocsow, na kusema ya kuwa serikali ya Urussi inatizama kiundani ni jinsi gani itashirikiana na NATO, ili kuijenga upya Afghanistan.
Picha hapo juu ni baadhi ya wanchi wa Afghanistan, wakiwa katika moja ya shamba lao wakiangalia matunda, ambayo huwa wanauza na kupata kipato cha kila siku, lakini kutokana na zao hili, ndimo madawa ya kulevya hutengenezwa, na jumuia ya kimataifa imekuwa inatafuta njia mpya ya kuijenga kiuchumi Afghanistan, ili wananchi wasitegemee zao hili.
Jacob Zuma,azilaumu nchi za Magharibi.
Johannesburg,Afrika ya Kusini-28/03/09.Mwenyekiti wa chama tawala cha Afrika ya Kusini Jacob Zuma, amezilaumu nchi za Magharibi, kwa kushindwa kuisaidia Zimbabwe., kwa kudai ya kuwa ni njia moja wapo ya kushinikiza rais wa Zimbabwe ili akubaliane na mabadiliko.
Jacob Zuma, alisema hii si sawa , kwani rais Robert Mugabe amekuwa madarakani, kwa kipindi kirefu kama rais wa Zimbabwe, na hivyo sivyo kama wanaovyo ona nchi za Magharibi, bali hali ya wanchi wa Zimbabwe ndito ya muhimu, kwani katika kupiga kura kila mwananchi alipiga kura, na siyo kila mwananchi alipiga kura kwa rais Mugabe au waziri mkuu ,Tsvangirai.
Hata hivyo , Jacob Zuma, alisema kuukubali kushirikiana kwa rais Mugabe na Tsvangirai,ni mwanzo wa mageuzi yatakayo waletea wa Zimbabwe manufaa na Maendeleo.
Picha hapo juu, anaonekna , Jzcob Zuma ,akiwa kavalia vazi la kiasili la Kizulu, wakati wa sherehe za kuazimiasha kumbukumbu ya Mfalme Shaka Zulu.
Picha ya pili ni viongozi wa Zimbabwe, rais Robert Mugabe na waziri mkuu, Morgen Tsvangirai wakipeana mkono mara baada ya kukubaliana kushirikiana kuongoza serikali na wananchi wa Zimbabwe kwa pamoja.
Sudan ya shuku Israel kwa mashambulizi nchini mwake.
Kartoum,Sudan-28/03/09. Serikali ya Sudan,imesema huenda mashambulizi yaliyo fanywa katika eneo moja lililopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, lilifanywa na Israel na kupoteza maisha ya watu 40.
Mashambulizi hayo yalioyo tokea mapema mwezi wa kwanza na wapili mwaka huu 2009.
Hata hivy msemaji wa serikali ya Sudan, alisema yakuwa mashamulizi hayo mwanzo yalizaniwa yamefanywa na Amerika, lakini , baadaye serikali ya Amerika ilikanusha madai hayo.
Aliendelea kwa kusema, msemaji huyo wa serikali ya Sudan, yakuwa bado wanachunguza kwa makini, lakini huenda mashambuliz haya yalifanywa na Israel,kwani hapo awali Israel ilidai yakuwa kua siraha, zina pitia Sudan kupelekwa Ukanda wa Gaza.
Picha hapo juu, inaonyesha ramani,ni jinsi gani mashambulizi yalivyo vyanywa ikiwa ni Israel iliyafanya.
Picha ya pili ni ya moja ya gari, ambalo lilishamuliwa na makombora ya liyoshambulia eneo lililopo Kaskazini Mashariki mwa Sudan, bilia serikali ya Sudan kufahamishwa.
Japan yawa tayari kuzuia chombo cha anga cha Korea ya Kaskazini.
Tokyo, Japan-28/03/09.Serikali ya Japan, imepitisha amri ya kulitaka jeshi la ulinzi wa anga kujiandaa kuzuia chombo cha anga kitakacho rushwa na Korea ya Kaskazini.
Uamuzi huo umekuja mara baada ya Korea ya Kaskazini kutangaza ina mpango wa kurusha chombo chake angaani kati ya Aprili 4 na 8 mwaka huu 2009.
Uamuzi huu unakuja baaada ya serikali ya Japan, kuona ya kuwa kitendo cha Korea ya Kusini, kutaka kurusha roketi hiyo ni hatari kwa Japan.
Picha hapo juu, inaonekana meli ya kijeshi ya Japan, iliyo na mitambo tayari kuzuia chombo cha anga cha Korea ya Kaskazini.
IAEA-Shirika linalo shughulikia nguvu za nyuklia duniani la vutana kupata kiongozi mpya.
Vienna, Austria - 28/03/09.Shirika la umoja wa Mataifa linalo shughulikia maswala ya nguvu za nyuklia limeshindwa kumpata mkurugenzi wake mkuu, katika uchaguzi uliochukua mzunguko mara tano kwa kipindi cha siku mbili.
Uchaguzi huo unafanyika,ili kumpzta mkurugenzi mpya, atakaye ongoza shirika hilo , baada ya mkurugenzi wa sasa Mohamed El Baredei ambaye anatarajiwa kujiuzuru.
Wagomea waliogombea kuwa wakurugenzi wa shirika hilo,Abdul Samad Minty wa Afrika ya Kusini na Yukiya Amano, hawakuweza kushinda baada ya kushindwa kupata kura zinazo hitajika ili kuwa mkurugenzi wa shirika hilo.
Picha hapo juu, ni ya mkurugenzi wa sasa wa shirika linalo shughulikia nguvu za nyuklia, Mohamed El Baredei,ambaye anatajariwa kujiuzuru kutoka madarakani.

Sunday, March 22, 2009

China kujiandaa kushindana na nguvu za kiaanga.

Mchezaji wa mpira wa miguu apigwa risasi kiwanjani.

Baghdad,Irak-22/03/09.Polisi nchini Irak wamesema mmoja ya mchezaji wa mpira wa miguu, alipigwa risasi ya kichwa na kufa hapo hapo wakati alipo kuwa anaijiandaa kupiga mpira wa adhabu ndogo.
Msemaji wa polisi, Mej,Muthanna Kharid, alisema mchezaji huyo wa timu ya Buhairat, alipigwa risasi na moja ya mshabiki wa timu pinzani ya Sinjar wakati zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya mpira kumalizika.
Katika mechi hiyo timu ya Sinjar, ilikuwa inaongoza kwa goli moja.
Hata hivyo, shabiki huyo alikamatwa na polisi mara moja, alimalizia kusema haya masemaji wa Polisi.
Picha hapo juu, wanaonekana baadhi ya wapenzi wa mpira wa miguu wakishangilia mara baada ya timu yao kushinda kombe la matifa ya Asia wakati walipo rudishwa kushiriki mashindano ya kimataifa.
China kujiandaa kushindana na nguvu za kiaanga.
Beijing, China, 22/03/09.Makubaliano kati ya China na Muungano wa Ulaya, kuhusu ujenzi wa pamoja wa chombo cha kuruka angani Galileo, kutoleta zao mafanikio, yameifanya China kuamua kujenga chombo chakuruka angani peke yake .
Kuamua kwa Chini kuendelea na ujenzi huo, kutaifanya China kuwa na uwezo sawa wakianga na nchi kama Amerika na Urussi.
Kutoleta mafanikio ya kushirikiana kujenga chombo hicho, kumekuja hasa kwa kuzingztia swala la usalama ambalo lililtwa na moja ya nchi mwanachama wa Muungano wa Ulaya.
Picha hapo juu, inaonekana moja ya chombo kinaruka kuelekea ngani , kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano.
Vita vya Gaza vyaleta mjadala katika jamii nchini Israel.
Jerusalem. Israel 22/03/09.Habari zinazo endele kutolewa na baadhi ya askari wa jeshi la Israel, kuhusu hali halisi ya vita kati ya Israel na Palestina, mapema mwisho wa mwaka 2008 hadi mwazo wa mwaka 2009, zinazidi kuleta hali ya wasiwasi na mvutano hivyo na kuleta mjadala mkubwa katika jamimii nzima ya Israel na kuhusu imani na ulinzi wa nchi.
Hii ina kuja baada ya ya baadhi ya watu kujadili kuwepo kwa vita hivi kwani vinakwenda kinyume na matakwa ya kidini,na wengine wana sema hii ni lazima kulinda taifa la Israel,kwani ni taifa teule na ni lazima walilinde kwa hali na mali.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya askari wa Israel wakiwa wamesima kwa pamoja kabla ya kuendelea na mapambano na kundi la Hamas kwenye eneo la ukanda wa Gaza.
Rais wa Sudan ashauriwa kuto kuhudhuria mkutano.
Khartoum,Sudan 22/03/09. Shule moja ya kidini nchini Sudan imemshauri rais wa Sudan,Omar Al bashir , kuto safiri nchini Katar, kuhudhuria mkutano wa nchi wanachama wa jumuia ya nchi za nchi za Kislam unaotarajiwa kuanza 30,03/09.
Shule hiyo Ulema, imesema hatuapendele rai Omar Al Bashir, kwenda huko kwenye mkutano, badala yake aende mwakilishi wake atakaye chaguliwa na serikali..
Hii onyo limetolewa, baada ya mahakama ya ianayo shughulika makosa ya jina na iliyopo nchini Uhollandi, kutowa kibali cha kukamatwa kwa rais huyo wa Sudan, ili ashitakiwe.
Picha hapo juu, anaonekana rais wa Sudan Omar Al Bashir, akishangalia kwa kucheza moja ya ngoma za kiasili za Sudan, wakati alipo tembelea katika jimbo moja nchini Sudan.
Picha ya pili wanaonekana, baaadhi ya wananchi maelfu wamekuja kumlaki, rais Omar Al bashir,alipo kwenda kuwatembele kwenye maeneo yao.