Tuesday, July 14, 2009

Rais wa zamani wa Liberia akanusha mashitaka zidi yake.

Muungano wa Ulaya wapata rais mpya. Brussels, Ubeligiji - 14/07/09.Mbuge wa Poland, Jerzy Buzek, amechaguliwa kuwa rais wa bunge la muungano wa Ulaya, baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi zaid ya 555 kati ya kura 644 zilizo pigwa katika uchaguzi wa rais wa bunge la muungano wa Ulaya. Mbunge, Jerzy Buzek, ambaye ni mbuge wa mlango wa kati kimsimamo, amechaguliwa, ikiwa nchi yake ina miaka minne tangu kujiunga na muungano wa Ulaya. Picha hapo juu, anaonekana, rais wa sasa wa muungano wa Ulaya, akiongea mara baada ya kuchaguliwa kwake.

Rais wa Liberia atuhumiwa na kwa kuhusika kusaidia vita.
Monrovia ,Liberia - 14/07/09. Rais wa sasa wa Liberia,Ellen - Sirleaf, amekumbwa na wakati mgumu, baada ya kamati inayo simamia hali halisi ya uharibifu wa vita nchini Liberia, umeomba rais wa Liberia asimamishwe uongozi wake kwa kuhusika na kundi moja ambalo, lilikuwa likipigana miaka 20 iliyo pita nchini Liberia.
Kamati,inayo shughulika mapatana, mariziano na kusameheana,inasema yakuwa katika watu ambao wametajwa ni rais wa sasa wa Liberia, Ellen - Sirleaf, kwa kuhusika kwa karibu na uongozi wa rais wa zamani Charles Tayrol, ambaye yupo Hague, kujibu mashitaka yana yo mkabili zidi yake.
Hata hivyo, msemaji wa rais , Ellen Serleaf, Cyrus Badio, amesema yakuwa rais ,bado anatafakali ripoti hiyo na ataongea hapo baadaye.
Rais wa zamani wa Liberia, akanusha mashitaka zidi yake.

Hague, Holland - 14/07/09. Rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor ametoa ushahidi wake leo zidi ya makosa 11, ambayo yanamkabili.

Akiongea, mbele ya jaji, rais huyo wa zamani wa Liberia,Charles Taylor,alisema ya kuwa makosa zidi yake ni ya , uzushi,uongo ulio jaa fununu za ajabu,uvumi, na hayana ukweli ndani yake na wale wanao zania ya kuwa yeye alihusika,katika mauaji na machafuko ya liyotokea nchini Sierra Leone.

Machafuko na mauaji hayo yaliyo tokea mwaka 1991 - 2001, yalipoteza maisha ya watu wapatao 200,000. Hata hivyo kesi hii bado inaendelea. Picha hapo juu, anaonekana, rais wa zamani wa Liberia Charles Tayrol kushoto, akiwa mahakamani kutoa ushahidi wake.

Sunday, July 12, 2009

Rais wa Amerika , Baraka Obama, Barani Afrika.

Rais , Baraka Obama, awasili barani Afrika kwa mara ya kwanza akiwa rais wa Amerika.

Akkra Ghana - 11/07/09 . Rais wa Amerika, Baraka Obama, amefanya ziara ya siku moja ya kiserikali nchini Ghana, ikiwa ni kuonyesha ya kuwa serikali yale inatilia mkazo uhusiano Amerika na Afrika.
Katika ziara hiyo, rais Obama, alisema viongozi wa Afrika, wana jukumu kubwa la kujenga na kuendeleza nchi zao kwa misingi uongozi bora kwani wa Afrika ndiyo watakao jenga Afrika.
Picha hapo juu, anaonekana, rais Baraka Obama, akipokea heshima kutoka kwa jeshi la Ghana, kabla ya kuanza rasmi mazungumzo na viongozi wa serikali ya Ghana.
Picha ya pili,anaonekana, rais Baraka Obama, akiongoea mara baada ya kuwasili nchini Ghana.
Picha ya tatu, rais Baraka Obama, mtoto wake Sasha na mtunza jumba la Cape Coast Castle, akiwapa maelezo kwa undani jinsi gani watumwa walivyo kuwa wakitolewa katika jumba la Cape Coast Castle, na kupitia kwenye mlango ambao wanatokea, mlango ambao watumwa alikuwa wakitolewa tayari kwa kusafirishwa kwenda Amerika na kwingine duniani, kuwa watumwa.
Picha ya nne, anaonekana , rais Baraka Obama, akiwa na mwenyeji wake, rais wa Ghana, John Atta Mills, wakielekea kwenye ofisi za Ikulu ya Ghana, tayari kwa mazungumzo.
Picha ya pili, anaonekana, rais Baraka Obama, akiongea na viongozi na wananchi wa Ghana.
Picha ya tano wanaonekana, rais Baraka Omba na mke wake, Michelle Obama, wakiwa waslimia wauguzi na wagonjwa wa hospitali kuu ya jijini Akkra.

Thursday, July 9, 2009

Majina ya walioanzisha vurugu nchini Kenya yakabidhiwa kwa ICC.

Mgomo waleta kichwa kuuma kwa wapenzi wa soka duniani.

Cape Town, Afrika ya Kusini - 09/07/09. Maelfu ya wafanyakazi wanaofanya kazi katika ujenzi wa viwanja vya mpira wa miguu, ambavyo vitatumika katika kuchezea fainali za mpira wa miguu za kombe la dunia 2010 nchini Afrika ya Kusini, wameanza mgomo wao leo, kwa kudai waongezwe malipo ya kipato chao (mshahara) kufikia (asilimia) 13%.
Akiongea na waandishi wa habari, mmoja ya wafanyakazi wa viwanja hivyo 10 vya mpira wa miguu,Martin Baloyi, alisema hayo huku akiwa amelala katika vyuma vya kujengea,yakuwa wanataka wapate pesa ambazo ni haki kwao.
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa vyama vya wafanyakazi viwili na South Africa Federation of Civil Engineering Contractors, vimekuwa katika majadiliano bila kufukia muafaka. Vyama hivyo vinavyo wakilisha wafanyakzi wapatao 70,000,, vimedai yakuwa wafanyakazi wamekuwa wakipata malipo ya $ 1.75, kwa saa na vyama hivyo vinataka kipato hichao lazima kiongezwe.
Kufuatia mgomo huu, hali ya ukamilishwaji wa viwanja hivyo kwa ajiliya mshindao hayo, huenda ukaleta kichwa kuuma kwa serikali ya Afrika ya Kusini.
Picha ya kwanza, wanaonekana wafanyakazi wa ujenziwa moja ya kiwanja jijini Cape Town, wakiandamana kudai kipato kiongezeke.
Picha ya pili juu, wanaonekana baadhi ya wafanyakazi wa kujenga moja ya kiwanja cha mpira wakiwa wamekaa chini baada ya kuanza mgomo,huku nyuma yao ni kiwanja cha mpira wa miguu kikiwa hakijakamilika ujenzi wake.
Majina ya lioanzisha vurugu nchini Kenya, yakabidhiwa kwa ICC.
Hague, Uhollanzi - 09/07/09. Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, amekabidhi majina ya watu waliohusika katika vurugu wakati na baada ya uchaguzi wa Kenya, uliofanyika mwaka 2007.
Kwa mujibu wa habari, zinasema Kofi Annan, alimkabidhi mwanasheria wa mahakama inayo shughulikia makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu, bwana, Moreno Ocampo.
Hata hivyo, swala hilo halikuwafurahisha baadhi ya viongozi wa Kenya, kwani walikuwa wanadai yakuwa kesi za watu hao ingebidi zisikilizwe nchini Kenya, lakini baadhi ya viongozi wengine walisema,ikiwa kesi hizo sitasikilizwa nchi Kenya, huenda kukakiukwa baadhi ya sheria na kutakuwa hakuna njia bora ya kuwalinda mashahidi.
Hapo juu,anaonekna Kofi Annan, akiwa amefunga mkono, huku akiangali juu.
G8, zahaidi kushirikiana kupunguza uzalishaji wa hewa chafu duniani.
Laquila, Itali - 09/07/09. Viongozi wa nchi tajiri duniani, G8 wanaendelea kukutana nchini Itali, kujadili ni jinsi gani, zitashirikiana kupunguza uzalishaji wa hewa chafu inayozalishwa na viwanda vikubwa, mitambo mikubwa na teknoloji zinazo atarisha mazingira na viumbe vyake kwa ujumla.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, wakiongozwa na rais, Baraka Obama, walihaidi kupunguza hewa chafu kwa kiasi cha (digree) nyuzi 2 celsius mpaka itakapo fika 2050.
Akiongea kusisitiza hayo rais Amerika , Baraka Obama, alisema ya kuwa viongozi wa sasa wana deni kubwa ambalo itawabidi washirikiane ili kulinda hali ya hewa isichafuliwe zaidi na hewa chafu inayo tokana kukua kwa maendeleo ya nchi tajiri, na akashauri ni lazima nchi tajiri ziangalie na kubuni mbinu mpya za kuleta maendeleo bila kuharibu mazingira kwani hakuna wa kulaumiwa, hili ni jukumu la kila nchi na watu wake.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa G8, wakiwa pamoja baada ya mkutano wao kwanza kuisha.
Hali ya usalama wa Irak,bado mthiani kwa serikali ya Irak.
Tal Afar,Iraq - 09/07/09.Watu wapatao 33wamefariki dunia kwa mlipuko wa mabomu, baada ya mauaji ya kujitolea muhanga kulipuka sehemu tofauti, na kuacha zaidi ya watu 70, wamejeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu , wa msemaji wa polisi,Kanali, Khaled Omar, mashambulizi hayo, yametoke karibu na ofisi za mahakama.
Wakati huo huo, kwa mujibu wa habari zilizotolewa na serikali, zina sema zaidi ya watu 437, wamepoteza maisha tangu kutangazwa kwa jeshi la Amerika, kulipa madaraka jeshi la Iraq.
Picha hapo juu, anaonekana kijana, mmoja ambaye ameumia vibaya baada ya kuwa katika eneo bomu lililolipuka.

Tuesday, July 7, 2009

Dunia nzima yamuaga Michael Jackson kwa huzuni. Mungu ailaze roho yake peponi.Amina

Dunia nzima, yamuaga,Michael Jackson kwa huzuni. Mungu ailaze roho yake peponi. Amina.

Los Angeles, Amerika - 0 7/07/09.Maelfu waliuzuria misa na maombi ya mwisho ya kumuaga mfalme wa musiki wa Pop Michael Jackson,ambaye alifariki siku 25/05/09.
Katika maombi hayo yaliuzuriwa, ndugu, marafiki,viongozi wa dini zote,waumini na wapenzi wa hayati mfalme wa musiki wa POP, Michael Jackson.
Picha hapo juu picha, zilizo pigwa wakati wa misa ya mwisho kukumuaga Michael Jackson, zinajieleza zenyewe, ni kwa jinsi gani tulivyo mpenda, Michael Jackson, wa kubwa kwa watoto.
Mfalme wa musiki, Michael Jackson, dunia nzima tutakukosa,umetwachia kumbukumbu ya milele kwa musiki wako na staili ya uchezajiwa wako, ulikuwa Michael Jackson,utabaki Michael Jackson, milele..
Michael Jackoson, Mungu ailaze roho yako peponi. Amina.

Monday, July 6, 2009

Urussi na Amerika zakubaliana kushirikiana katika swala la nyuklia. Moscow, Urussi - 06/07/09. Urussi na Amerika zimekubaliana kupunguza siraha za nyuklia, wakati marais wa nchi hizo walipo kutana leo siku ya jumatatu jijini Moscow. Makubaliano hayo,yamefanyika wakat Rais wa Amerika , baraka Obama, akiwa ziarani Urussi, kuongea na viongozi wa Urussi,ili kudumisha uhusiano, ambao ulikuwa umeingia utata, baada ya Amerika kutaka kuweka makombo yake katikati mwa Ulaya, kwa kudai ni kaajili ya kulinda mashambulizi ambayo yanaweza kutokea Iran au Korea ya Kaskazini, lakini Urussi ilililikataa jambo hilo na likazusha mgogoro. Picha hapo juu, wanaonekana rais wa Amerika, Baraka.H.OBama, akiongea na rais wa Urussi Dmitri . A. Medvedev wakati walipo kutana kwa mazunguzo ya kikazi jijini Moscow.

Sunday, July 5, 2009

Serena na Venus Williams Malkia wa tenis wa Wimbledon 2009.

Serena na Venus Williams, Malkia wa tenis wa Wimbledon 2009.

Wimbledon, Uingereza 05/07/09. Kwa mara nyingine tena, Serena na dada yake Venus, wameweza kushinda mchezo wa tenis kwa wanawake na kuchukua kikombe cha Wimbledon kwa ushindi wa seti 7-6, 6-4 zidi ya Samantha Stosur na Rennae Stubbs.
Huku wakiwa na furuha, Venus alisema ya kuwa ushindi huu umekuja kutokana na jitihada yao, na kwa kuzingatia tumecheza zaidi ya masaa matatu jana na leo,hivyo inabidi tuwe na furaha kwa kutokubali kuruhusi uchovyo ututalawale.
Senena, ambaye alishinda siku ya jumamosi kwa upande wa wanawake, alisema huwa anajisikia furaha saana anaposhinda huku akiwa na dada yake pamoja katika mchezo wa wawili wawili.
Picha hapo juu wanaonekana , Serena na Venus Williams, wakiwa wamechikia vikombe vya ushindi baada ya kushinda tenis fainali wanawake katika mchezo wa wawili wawili.
Picha ya pili, wanaoneka Venus kulia akienda kumkumbatia mdogo wake Serena, mara ya kushinda seti ya mwisho iliyo wapa ubingwa.
Picha ya tatu, anaonekana , Serena akiangalia kwa tabasamu sahani ya ubingwa wa tenis wa Wimbledon,mara baada ya kukabidhiwa.
Picha ya nne, anaonekanam Serena , akilionyesha sahani la ubingwa wa tenis, kwa upande wa wanawake, baada ya kushinda dada yake Venus.
Picha ya tano, anaonekana, Venus hali siyo nzuri, wakati alipo kuwa akishindana na mdogo wake kugombania ubingwa wa kombe la teni wanawake la Wimbledon.
Picha ya sita, wanaonekana, Serena akimkubatia dada yake, Venus , mara baada ya mpambano kati yao, ambao Serena aliweza kumshinda dada yake.
Picha ya saba, anaonekana, Serena , akiwa amepiga magoto kushangilia, ushindi zidi ya dada yake.
Roger Federer,aweka rekodi ya mchezo wa tenis duniani.
Wimbledon Uingereza - 05/06/07.Roger Federer, ameshinda kombe la Wimbledon katika mchezo wa tenis , na kuweka rekodi ya kuwa ushindi wa mashindano makubwa ya tenis kwa mara ya 15.
Katika pambano hili ambalo lilimpa Roger Ushindi zidi ya Andy Rodick, kwa kumshinda kwa seti 5-7 (6) ,7-6,(5), 3-6 na 16-14.
Roger Federer, ambaye ameshinda fainali za Wimbledon mara 6,katika mchezo uliowachukua muda wa masaa 4 : 18dk.
Picha hapo juu anaonekna Roger Federer, akiuchonga mpira ambao ulimshinda, Andy Rodick, na kumpa ushindi, Roger Federer kwa seti 16-14.
Picha ya pili, anaonekna Roger Fedrer, akiwasalimia kwa furuaha wapenzi wa mchezo wa tenis waliokuja kushuhudia pambano kali kati yake na Andy Rodick.
Picha ya tatu, anaonekana, Roger Fedrer, akibusu kikombe cha ubingwa cha mchezo wa tenis, mara baada ya kukabiziwa kikombe hicho.
Amerika na Urussi kuziba ufa uliopo?
Moscow Urussi -05/07/09. Rais wa Urussi, Dimirti Medvedev, atakuwa mwemyeji wa rais wa Amerika, Baraka Obama hivi karibuni, ili kuzidi kuimarisha uhusiano wa karibu.
Ziara ya rais Baraka Obama nchini Urussi, itakuwa ni pili katika bara la Ulaya, baada ya mkutano wa kiuchumi ulifanyika mjini London Uingereza.
Mambo mengine yatakyo zungumziwa ni maswala ya makombora ya kivita ambayo Amerika inampango wa kuyakeka katika moja ya nchi moja ya Ulaya, jambo ambalo Urussi inalipinga vikali.
Picha ya hapo juu wanaonekana, raia wa Urussi, Dimitri Medvedev, akiwa anamnongoneza waziri mkuu wa Urussi, Vladamir Putin.
AU haihukubaliana na mahakama ya kimataifa. rais, Al - Bashir yupo huru kusafiri.
Tripol Libya - 04/07/09. Kikao cha viongozi wa Afrika kimamua kwa pamoja ya kuwa nchi za Afrika hazita husika katika kumkamata au kumkamata rais wa Sudan, Omar Al - Bashir.
Uamuzi huo ulichukuliwa na wakati viongozi wa muungano wa nchi za Afrika walipo kutana chini ya uwenyekiti wa rais wa Libya Muhamar Ghadafffi.
Rasi wa Sudan, anakabiliwa na kesi ambayo imefunguliwa zidi yake na mahakama inayo shughulikia kesi za ukiukaji wa haki za binadamu iliyopo nchi Nederland (The Hague).
Kufuatia uamuzi huo, rais wa Sudan anaweza safiri katika nchi yoyote ya Afrika bila kuwa na wasiwasi, kwa kuzingatia nchi 33 za Afrika zilikubaliana na kutia sahii makubaliano ya mjini Rome Itali,ya kufungua mahakama itakayo shughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu iliyopo nchi Nederland.
Picha hapo juu, anaonekna rais , wa Sudan, Omar Al bashir , akiwa katika kikao cha viongozi wa Afrika kilicho fanyika hivi karibuni.

Thursday, July 2, 2009

Binti aliyepona katika ajali ya ndege akutana na baba yake.

Historia na ndoto za Williams za jirudia nchini Uingereza. Wimbledon, Uingereza - 02/07/09. Historia ya mchezo wa tenisi, imejirudia tena, baada ya ndugu wawili mkubwa na mdogo,kukutana tena katika fainali ya kugombea kikombe cha Wimbledon. Ndugu hao , mabao pia ni Dada mdogo Serena Williams na dada mkubwa Venus Williams, watakutana mara ya kibarua kigumu cha kupambana na kushinda michezo yote ya tenisi kwa upande wa wanawake, kutoka hatua ya mwanzo hadi kufikia kukutana fainali. Katika, mchezo wa nusu fainali, Serena aliweza kumshinda, Elena Demetieva kwa seti 7-5,8-6, japo kayika seti ya kwanza Serena alishindwa kwa seti 6-7. Naye dada Venus, alishinda , bila huruma Dinara Safina kwa seti 6-1,6-0. Kufuatia ushindi wa madada hawa, Venus na Serena , ambao wanazaliwa na mama na baba mmoja, kumewafanya wakutane tena katika fainali ya Wimbledon kwa mara ya nne. Kukutana kwa madada hao,kunazidi dhihirisha ya kuwa ndoto zao walizo kuwa wakiziota miaka 20 iliyo pita kwenye mji walio kulia, Compton Califonia za kukutana kwenye fainali ya mashindano makubwa inakuja kila wanapo amua kufanya kazi ya ziada, alisema Venus. Picha hapo juu wanaonekana, madada mgogo Serena Williams kulia na mkubwa Venus Williams, wakiwa wameshikilia vikombe vya ubingwa wa tenisi kwa upande wa wanawake, baada ya kushinda (DOUBLES) wawili kwa wawili hapo miaka ya nyuma nchi Uingereza. Korea ya Kaskazini, yazidi kutunisha misuri kwa jumuia ya Kimataifa. Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 02/07/09.Kora ya Kusini, imerusha makomora ya masafa mafupi hivi karibuni. Kwa mijibu wa Yanhap, shirika la utangazaji, limesema, makombora hayo yalirushwa kuelekea upande wa mashariki ya pwani. Makombora ambayo yallirushwa nia nchi kavu , hewani kuelekea kwenye melikebu. Makombora hayo yanajulikana kama, Silkwom. Kurushwa kwa makombora hayo, kumeweka hali ya wasiwasi katika eneo zima, hasa kati ya Korea ya Kusini na Korea ya Kaskazini. Picha hapo juu, nia moja ya michongo ya makombora yakiwa yamewekwa kama minara kwenye sehemu moja ya mji, nchini Korea ya Kaskazini. Binti aliyepona katika ajali ya ndege, akutana na baba yake.

Paris, Ufaransa - 02/07/09. Baba ya msichana aliyepona katiaka ajaili ya ndege ya shirka la Yemen,amempokea binti yake, Bahia Bakari, wakati alipo wasili nchini Ufaransa baada ya kupata matibabu ya kwanza nchini Komoro.
Binti huyu, Bahia Bakari, ndiye abiria pekee, aliye jaliwa kuwa hai katika jali hiyo.
Ndege aina ya Airbus, ilianguka siku ya jumanne alfhajiri katika bahari ya Indi wakati ikitokea, Sanaa Yemen kuelekea visiwa vya Komoro.
Picha, hapo juu wanaoneka,Kassim Bakari, babaya Bahia Bakari, akiwa ameshikilia, binti yake, huku wakiwa njiani kuelekea hospital, mapema alipo wasili Paris.
Picha ya pili ni ya shrika la ndege la Yemen,ambapo moja ya ndege yake, ilianguka siku ya jumanne alfhajiri.
Umoja wa mataifa wapata mkurugenzi mkuu mpya wa kusimamia atomi na nyuklia.
Viena , Austria - 02/07/09. Shirika la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia ukaguzi wa nguvu za atomi na nyuklia ( International Atomic Enegy Agency), limemchagua Yukiya Amano kuwa mkurugenzi wake mkuu, ili kushika nafasi itakayo achwa wazi na mkurugenzi wa sasa, Mohamed El Baradei kuanzia mwezi November 2009.
Katika uchaguzi, huo,Yukiya Amano, alimshinda mpinzani wake mkuu, Abdul Samad Minty, kutokea Afrika ya Kusini kwa kupata kura 35,kutoka kwa nchi wanchama.
Picha hapo juu, anaoneka Yukiya Amano,ambaye atashikia kiti cha ukurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalo shughulikia ukaguzi wa nguvu za atomi na nyuklia,kuanzia mwezi wa November 2009.
Picha ya pili, wanaonekana, kushoto mkurugenzi mkuu wa sasa,Mohamed El baradei, akiwa na mkurugenzi mchaguliwa Yukiya Amano, wakati walipo pokea zawadi ya nishani ya Nobel nchini Norway mwaka 2005.