Tuesday, August 4, 2009

Nashukuru kuondoka kwa Eto'o,alikuwa ananipa ndoto zisizo za kawaida.

Nashukuru kuondoka kwa Eto'o, alikuwa ananipa ndoto zisozo za kawaida.

Madrid, Uispania - 04/08/09. Golikipa au mlinzi namba moja wa timu ya taifa ya Uispania Iker Casillas, amesema amefurahi kuondoka kwa mshambuliaji hatari wa timu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Kameroon, Samwel Eto'o.
Akiongea leo hii, Casillas, alisema ya kuwa Eto'o, alikuwa akimfanya aote ndoto zisizo eleweka kila anapo fikilia mechi na timu ya Barcelona.
Akiulizwa na waandishi wa habari, Iker Casillas, kuhusu mshabuliaji ,Zlatan Ibrahimovic, mlinda mlango huyo, alisema Ibrahimovic ni mchezaji mzuri, lakini Eto'o ni hana mfano.
Hapo juu, ni picha tofauti, zinaonyesha ni kwa kiasi gani,mlinzi wa timu ya Madrid, Iker Casillas, alivyokuwa akiteswa na kuteseka kila anapo kutana na mshambualiji wa Barcelona, Samwel Eto'o.
Kwani, Eto'o amekuwa akimpa wakati mgunga mlizi huyo, Iker Casillas na kuona nyavu zilizo chini ya ulinzi wa kipa huyo.

Monday, August 3, 2009

Katibu mkuu wa NATO aanza kazi rasmi.

Mfereji wa Suezi wa kumbwa na upepo wa kiuchumi. Suez Kanal, Misri - 03/08/09. Serikali ya Misri imesema ya kuwa kutokana na hali ya uchumi kuyumba na vitendo vya ugaidi kuzidi katika bahari za Hindi ,kumefanya mapato ya kodi kushuka kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia 7.2 (7.2%). Mfereji wa Suez, unatumika kwa kupitishia meli zote, zinazo ingia na kutoka bara la Ulaya na Amerika kuelekea bara la Asia, Afrika na nchi za Mashariki ya kati. Akiongea haya, mkuu wa mfereji huo wa Suez, Ahmed Ali Fadel,alisema yakuwa matatizo ambayo yanaikumba dunia kiuchumi yanachangia kwa kiasi kikibwa, anaamini hali ya mapato ya kodi yataanza kupanda hapo hali ya uchumi itakapo kuwa nzuri. Picha hapo juu, nimoja ya boti ya polisi, ikiwa katika ulinzi wa mfereji wa Suez, ambapo kwa kipindi hiki, meli zimekuwa hazipiti kwa wingi kwa sababu tofauti, moja wapo swala la usalama katika pwani karibu na Somalia.

Katibu mkuu mpya wa NATO, aanza kazi rasmi.
Brussel, Ubeligiji 03/08/09. Katibu mkuu mpya wa NATO, Fogh Rasmussen,ambaye pia alishawahi kuwa waziri mkuu wa Denmark,ameanza kazi rasmi leo.

Kabla ya kuanza rasmi kazi ya ukatibu mkuu wa NATO leo, amesema wakati wa uongozi wake , atahakikisha ya kuwa Afghanistan, wanakuwa na ulinzi wao wenyewe na kulinda usalama wa nchi yao, na hivyo kuzitaka nchi wanchama wa NATO, kushirikiana zaidi ili kufanikisha lengo hilo.

Aliongezea ya kuwa NATO, itazidisha ushirikiano na nchi wanachama wa jumuiya zanchi za Kiislaam.

Jumuiya hizo ni Mediteranian Dialogue (MD) na Istambul Co- operation Initiative (ISCI).

Fogh Rasmusessen, amechukua kazi iliyo achwa na katibu mkuu wa zamani wa NATO, Jaap de Hoop Sheffer.

Pichani hapo juu wanaonekana, Jaap Hoop Sheffer,ambaye anatoka madarakani kama katibu mkuu wa NATO na kulia ni katibu mkuu mpya wa NATO, Fogh Rasmussen,akiongea ni kwa jinsi gani wakati wa uongozi wake atakavyo fanya.

Picha ya pili, ni ya Katibu mkuu mpya wa NATO, Fogh Rasmussen, akiongea mbele ya wajumbe NATO.

Sunday, August 2, 2009

Google ya pata wapinzani wa kitandao.

Google ya pata wapinzani wa kimtandao.

Redmond,Amerika - 02/08/09. Makampuni makubwa duniani yanayo ambayo ndiyo yanayo shughulikia nugu za mitaandao, Microsoft na Yahoo, zimeamua kuungana ili kushindana kibiashara na kamuni nyingine kubwa ya Google.
Makampuni ya Microsoft na Yahoo yalitiliana saai mkataba wa makubaliano ya ushirikiano siku ya Jumatano,29/07/09, na kukamilisha mipango yote hivi karibuni.
Akiongea mbele ya vyombo vya habari, mkurugenzi mkuu wa Microsoft,Steven A Ballmer, alisema ya kuwa ushirikiano huu ni mzuri kwani utainua kampuni zote mbili, na kuweza kushindana na Google.
Picha hapo juu ni ya alama ya kampuni ya Googe ikiwa mbele ya ofisi zake, ambapo kwa sasa itakuwa na washindani wawili wakubwa Microsoft na Yahoo katika biashara ya kimtandao..
Picha mbili zinazo fuatana za Microsoft na Yahoo,zimeungana kibiashara, ili kuleta ushindani wa kibiashara na Google.
Mtandao kutumika katika kutibu wanajeshi.
Hawaii, Amerika - 02/08/09. Kituo cha afya TriWest, kilichopo Hawaii nchini Amerika, kimeseama kitaanza kuwatibu na kutoa ushauri kwa wanajeshi na familia zao kiakili kwa kutumia mtandao picha ( Webcam).
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana , zinasema ya kuwa wataalamu wa hali za utimamu wa binadamu na waganga, wataanza matibabu hayo kakuangali ni kwa kiasi gani wanajeshi ambao wameumia vitani wataweza pata kurudi katika hali ya kawaida.
Mpango huu, umeweza kufanikiwa katika majaribio kwa kushirikiana na wataalamu wa maswala ya kijeshi ya Amerika alisema, David J. McInntyre.
Picha hapo juu, wanaonekana, wanajeshi wakiwa wanambeba mmoja ya mwanajeshi mwenzao , baada ya kuumia wakati wa mapambano.
Picha hapo
Rwanda kuupa utalii kipao mbele.
Kigali, Rwanda - 20/08/09. Serikali ya Rwanda pamoja na kampuni ya Dubai , ( Dubai World),
zimeanza kushirikiana kwa pamoja ili kukuza utalii nchini humo.
Kwa mujibu wa , mkurugenzi mkuu wa wa maendeleo ya Rwanda,Clare Akamanzi, alisema ushirikiano huu, ni muhimu kwani serikali ya Rwanda, moja ya nchi ambayo ina vivutio vingi vya utalii na utalii utachangia katika kuinua hali ya uchumi wa nchi.
Pichani hapo juu, wanaonekana, ujenzi wa moja ya hotela ya kitalii, ukiendelea kwa ushirikiano wa serikali ya Rwanda na Dubai World.
Magorila hatarini na virusi vya ugonjwa wa ukimwi
Alabama, Amerika - 02/08/09. Wachunguzi wa maswala ya utibabu wa magorila, wamesema wamegundua ya kuwa ugonjwa wa ukimwi unaweza kuwazuru wanyama hawa kama unavyo waathiri wanadamu.
Kwa mujibu wa Dr, Beatrice Hahn wa chuo cha Alabama,amesema uchunguzi ulifanywa unaonyesha wazi ya kuwa virusi ukimwi vinateta hali ya hatari kwa magorila hao.
Hapo juu, anaonekana, mmoja ya magorila, akiwa ameshikilia mtoto wake.

Tuesday, July 28, 2009

China na Amerika zakutana kujadili ushirikiano wa kiuchumi.

Unene wa mwili ni hali ya hatari kwa mtu na matumizi ya serikali.

Chicago, Amerika - 28/07/09. Swala la kunenepa kwa watu kupita kiasi hasa katika nchi za Magharibi, zimekuwa zinaleta vichwa kuuma kwa watu na jamii nzima ya maeneo haya.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa wa mambo ya afya ya watu, zinasema ya kuwa unene wa mwili ni hali ya hatari kwa binadamu mwenyewe na serikali za nchi hizo kwa kutumia pesa nyingi katika matibabu yanayo sababishwa na unene wa mwili.
Akiongea haya, Dr Thomas Frieden, alisema hipo haja ya watu kwa kusaidiana na serikali kupambana na hali hii.
Picha hapo juu, anaonekana mmoja ya watu, ambao unene umekuwa ukiwa tatizo kwa jamii.
Picha ya pili, wanaonekana, baadhi ya watu wa nchi za Magharibi, ambao wanakabiliwa na hali ya kuongezeka kwa watu kuwa wanene kupita kiasi, na kutetetlesha hali ya afya zao.
Utumiaji wa simu ya mikono huku ukiendesha gari, ni hatari kwa watumiaji wa barabara.
Virginia, Amerika - 28/07/09. Wataalamu wa mambo ya usalama barabarani, wamesema yakuwa kuna ya asilimia kubwa kwa dereva anaye endesha gari wakati anaandika teksti kwa kutumia simu ya mkono kupata ajali, au kusababisha ajali kwa madereva wengine wanaotumia barabara wakati huo.
Kwa mujibu wa wataalamu kutoka chuo cha usafiri cha Virginia, zimesema kugonga ao kugongana na gari jingine kuanaweza kutokea wakati wowote wakati dereva anaandika teksti kwa kutumua simu ya mkono huku akiwa anaendesha gari.
Wachunguzi hao walisema, hata upokeaji wa simu kwa kutumia mkono kuhu uanendesha gari, kunaleta hatari pia.
Picha hapo juu, ni moja ya picha za video zinaonyesha kwa kiasi gani dereva, anapo endesha gari, huku huku akituma teksti anaweza sababisha ajali barabarani.
China na Amerika zakutana kujadili ushirikiano wa kiuchumi.
Washington,Amerika - 28/07/09. Rais wa Amerika, Baraka Obama, ameukaribisha uhusiano wa Amerika na China na kutaka uwe wa faida kwa nchini zote mbili na wanachi wake.
Rais , Obama aliyaongea hayo wakati alipo kuwa anawakaribisha viongozi wa China wakiongozwa na makamu wa waziri mkuu wa China, Wang Quishan.
Ujumbe huo kutoka China, upo nchini Amerika, kujadili ni jinsi gani nchi hizi mbili zitashirikiana kiuchumi.
Picha hapo juu, anaonekana rais, Obama, akiongea mbele ya wajumbe wa China na Amerika kabla ya kuanza mjadiliano ya kiuchumi.
Picha ya pili,rais , Baraka Obama, akimkaribisha, makamu wa waziri mkuu wa China, Wang Qishan, na kulia ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton.
Picha ya tatu, wanaonekana wajumbe na viongozi kutoka China,wakimsikiliza rais wa Amerika, Baraka Obama wakati wa ufunguzi wa mazungumzo ya kiuchumi wa nchi hizo mbili, (Amerika na China)
Sijawahi kula nyama ya mtu, adai rais wa zamani wa Liberia.
Hague,Nederland - 28/07/09. Rais wa zamani wa Liberia , Charles Taylor, amekanu sha shutuma zakuwa alikuwa anatafuta na kula nyama za watu, na kuesam nu upuuzi mtupu.
Akiongea kwa msisitizo , rais huyo wa zamani wa Liberia, Charles Talor, aliambia koti ya kuwa watakuwa ni wagonjwa kama wakiamini ushaidi unaotolewa juu yake yakuwa alikuwa ana kula nyama za watu, inafanya mtu aweze kutapika.
Rais huyo wa zamani wa Liberia, anakabiliwa na makosa ya kukiuka haki za binandamu,na ya kivita zidi ya nchi ya Sierra Leone.
Picha hpo juu anaonekana, rais wa zamani wa Liberia , Charles Taylor, akiwa mahakani, huku akiandika pointi na huku akisikiliza shutuma zidi yake.
Machafuko yaleta hali ya wasiwasi nchini Nigeria.
Kano , Nigeria - 28/07/09. Hali ya usalama nchini Nigeria imeingia katika hali ya utata, hasa katika eneo la jimbo la Kano, lililopo kaskazini mwa Nigeria.
Kufuatia machafuko hayo amboyo bado yanaendelea chini humo katika jimbo la Kano,yamesababisha baadhi ya watu kupoteza maisha yao.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema watu wapatao 100, wamesha poteza maisha mpaka sasa.
Ghasia hizo ambazo zinakuja baada ya wakazi wa eneo hilo la Kano, hawakubaliani na mpango wa elimu ya kisasa, kwa madai yakuwa haiendani na matakwa ya jamii hii, na wanataka elimu iwe inaendana na dini yao ya Uislaam.
Kufuatia mvutano huo, watu walikwenda kuvamia kituo cha polisi,kwa madai ya kuwa kuna mmoja ya mwenzao amekamatwa, na hivyo polisi kujibu mashambulizi na kuteta maafa makubwa.
Picha hapo juu, wanaonekana baadhi ya watu wakiwa chini ya ulinzi, mara baada ya kutiwa chini ya ulinzi.

Tuesday, July 21, 2009

Taliban watumia mbinu mpya katika kutengeneza nyenzo zao za kivita.

Swala la Rio Tinto, serikali mbili kukutana kuliongea.

Sydney, Australia - 22/07/09. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Australia Stephen Smith, amesema atakutana na waziri wa mambo ya nchi za nje wa China Yang Jienchi,ili kuzungumzia mgogoro uliopo kati ya serikali hizi mbili, kufuatia China kumkamata mkubwa anayesimamia kampuni ya Rio Tinto, Stern Hu, ambaye ni rai wa Australia.
Stern Hu, alikamatwa July 5/2009 na serikali ya China, kwa madai ya upelelezi na kutaka kutoa rushwa kwa baadhi ya wafanyakazi ili aweze kuapata siri ya mikataba inavyotolewa .
China imekuwa ikifanya biashara na Australia,na hasa katika usambazaji wa vyuma, ambapo kampuni ya Rio Tinto, ndiyo kampuni mama katika uchimbaji na usambazaji.
Picha hapo, juu ni moja ya mitambo ya Rio Tinto, kampuni ambayo ni maarufu kwa uchimbaji wa madini kutoka ardhini.
Picha ya pili ni ya Stern Hu, ambaye kwa sasa yupo kizuizini nchini China kwa kudaiwa kuhusika na makosa ya jinai.
Nchini wanachama wa EU wapewa ruhusa kuweka akiba ya gas asilia.
Brussel, Ubeligiji - 22/07/09. Muungano wa Ulaya, umeziagizia nchi wanachama kuanza kuweka akiba ya gas ya asili, endapo kutatokea kutokuelewa tena na Urussi.
Kwa mujibu wa kamati inayo shughulikia maswala hayo imesema yakuwa kila nchi mwanachama, inatakiwa kuwa na gas ya asili ya kutosha ifikapo mwaka 2014, na gasi hiyo iwe na uwezo wa kutumika kwa muda wa miezi hadi miwili (Siku 60).
Mgogoro wa gas kutoka Urussi, umekuwa ukizisumbua nchi nyingi za Muungano wa Ulaya,kwa muda mrefu na kusababisha baadhi ya nchi kutiliana mkataba na Uturuki, ili kujengwa mabomba mapya yatakayo wezesha gas kutoka Caspian na Mashariki ya Kati,ili kupunguza kuitegemea Urussi katika upatikanaji wa gas.
Picha hapo juu,ni ya nembo ya nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya, ambapo nchi wana chama wamekuwa wakipata msukosuko wa kupata gasi, pindipo panapotokea mtafaruki.
Picha ya pili ni moja ya mitambo ianayo tumika kuhifadhi gas, ambapo kuanzia sasa mitambo hiyo itabidi iongezewe uwezo wa kuhifadhi gasi hiyo.
Taliban, watumia mbinu mpya katika kutengeneza nyenzo zao za kivita.
Gardez ,Afghanistan - 22/07/09. Wapinaji wa kundi la taliban, wameshambulia maeneo ya yaliyopo majengo na ofisi za serikali kwenye miji tofatuini ncini Afghanistan.
Maeneo hayo ambayo yameshambuliwa yapo katika miji ya, Gardez na Jalalabad,wakati nchi hiyo inajiandaa mna uchaguzi wa rais utakao fanyika mwisho wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, watu watun sita waliova nguo za kike, huku wakiwa na siraha na mabomu, walishambulia maeneo hayo tofauti ya serikali.
Kundi la Talibani limekuwa likitumia mbinu za kisasa kutengeneza mabobu yake, kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya kijeshi.
Hata hivyo , walinzi wa serikali waliweza kuwaua watu watatu, na wengine watatu waliweza kukumbia.
Picha hapo juu, wanaonekana, baadhi ya wanajeshi wakiimgia katika helkopta tayari kwenda mstari wa mbele kupambana na kundi la Talibani.
Picha ya pili, ni anaonekana mmoja ya mwanajeshi akikimbia, kukwepa bomu, ambalo lililipuka karibu yake.
Vijana wamiminika katika hospitali na zahanati kufanyiwa operesheni(Kutailiwa).
Bloemfontein, Afrika ya Kusini - 22/07/09.Kutokana na kuthibitishwa ya kuwa wanaume waliotailiwa wana nafasi kubwa ya kutoambukizwa ugonjwa wa ukimwi,vijana walio wengi nchini Afrika ya Kusini, wanamiminika katika zahanati tofauti ili kufanyikwa operesheni hiyo ndogo( Kutailiwa)
Kwa mujibu wa mmoja wa madokta ambao wanashughulikia operesheni hizo Dr, Diono Rech, alisema amekuwa anafanya operasheni hizo hadi kufikia 50 kwa wiki.
Picha hapo juu, wanaonekana, baadhi ya vijana wakiwa katika zahanati moja, tayari kufanyiwa opereshieni au ( Kutailiwa).
Kansa ya mapafu yajadiliwa kiundani na wataalamu jijini New York.
New York, Amerika - 22/07.09. Wanasayanchi nchini Amerika, wamesema ni hivi karibuni, walipo kutana jijini, New Yor, kwatafanikiwa vipi kutibu kansa ya mapafu,kwa kutumia vyombo ya kitaalamu zaidi.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana kutoka katika mahaabara inayo shughulikia uchunguzi na matibabu ya kansa, iliyopo jijini New York,zilisema muda si mrefu wataalamu wataamua ni njia ipi iliyo bora zaidi katika kutibu ugonjwa huo.
Picha hapo juu, ni ya mapafu, ambapo wataalamu wana sema muda si mrefu waataanza kutumia vidonge kuanza kutibu mapafu yaliyo kuwa na kansa.
Mamiliona washuhudia kupatwa kwa jua barani Asia.
Bangkok , Thailand - 22/07/07. watu wapatap millioni katika bara la Asia, wamekusanyika katika sehu maalumu zilizo tayarishwa kwaajili ya kuangalia kupatwa kwa jua katika karne hii.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya kijiografia, wamesema ya kuwa, maeneo tofauti katika bara la Asia, Japan, India ,na China,wataweza kuona kitend hicho ambacho hutokea kwa mara moja katika kila bara
Picha hapo juu, ni ya jua linaonekana kuzibwa kabisa , na kuleta giza kwa muda katika eneo ambalo lilitakiwa jua liwe linawaka.
Picha pili hapo juu wanaonekana, baadhi ya wanafunzi, wa wanaosomea maswala ya sayansi, wakiangali kupatwa kwa jua katika jimbo la Bihar nchini India.

Sunday, July 19, 2009

Ndugu,jamaa, marafiki na viongozi washerekea siku ya kuzaliwa Nelson Mandela.

Ndugu, jamaa, marafiki, na viongozi washerekea siku ya kuzaliwa Nelson Mandela.

Johannesburg, Afrika ya Kusini - 18/07/09. Maelfu ya watu wamesherekea siku ys kuzaliwa kwa aliye kuwa rais wa kwanza mwafika, mpigani uhuru, haki na usawa kwa wanchi wa Afrika ya kusini, Nelson Mandela,ambapo ametimiza miaka 91 tangu kuzaliwa.
Moja kati ya watu walioudhulia sherehe hizo ni rais wa sasa wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma.
Nelson Mandela, ameweza kuleta mabadiliko na kuwa changa moto kwa watu wengi, bila kujali rangi zao na wapi wanatokea.
Picha hapo juuwanaonekana, rais wa sasa wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma, akiwana rais wa kwanza mwafrika wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, kabla ya kupata maakuli kushangilia siku ya kuzaliwa kwa Nelson Mandela.
Picha ya pili, anaonekana, rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, akitabasamu mbele ya watu walio kuja kusherekea siku ya kuzaliwa kwake.
Picha za mwanajeshi aliyetekwa nyara zasambazwa kwenye mitandao.
Paktika, Afghanistan - 16/07/09. Mwanajeshi wa Amerika aliye potea waktai akiwa mstari wa mbele siku ya tarehe 30/juni/2009, ameonekana kwen picha za video na kwenye mitaandao huku akiongea ni kwajinsi hali anayotarajia, na kwa kiasi gani ana wakumbuka watu wote wa famial yake.
Video ya mwanajeshi huyo, mwenye umri wa miaka 23, ilionyeshwa kwa dakika 28 siku ya jumamosi, huku akiwa amekatwa nywele zake za kichwani.
Pentagon, imesema ya kuwa mwanajeshi huyo, Bowe Bergdahl, wa Kentchum Idaho,juhudi za kumtafuta mahali alipo fishwa kama mateka bado zinaendelea, na jeshi la limesambaza vikaratasi katika eneo ambalo alikamatwa mwanajeshi huyo na kutaka mtu yoyote atakaye saidia kupatikana kwa mwnajeshi huyo, atapewa zawadi.
Na wakati huo huo , makao makuu ya jeshi la Amerika , limesema kitendo cha kundi ambalo limemkamata mwanajeshi huyo, kusambaza video zake ,ni kinyume na sheria za kimataifa.
Picha hapo juu ni ya mwanajeshi aliye tekwa nyara, Bowe Bergdahl, amnaonekana akila chakula alicho pewa na kundi ambalo lime mteka nyara.

Thursday, July 16, 2009

Kifo cha rais wa Palestina chaleta kitendawili kati ya viongozi wa Wapalestina.

Iran na Amerika bado kupeana majibu.

Washingtone, Amerika - 16/07/09. Serikali ya Amerika imesema ya kuwa utafika wakati mpango wa mazungumzo na Iran hautakuwa na maana tena, kwa kuzingati Iran imesha pewa hadi kufikia mwezi wa Septemba, iwe imesha toa jibu kama itakuwa tayari kuongea na Amerika, kupitia Umoja wa Mataifa.
Hayo yaliongewa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Hilary Clinton, jana wakati akiongelea mipango ya serikali ya Amerika katika maswala mambo ya nje, na kudai ya kuwa Iran haitakiwa kuwa na nguvu za kijeshi za kinyuklia, bali wanaweza kuwa na nyuklia kwa ajili ya uzalishaji na maendeleo ya jamii.
Wakati huo huo, mkuu wa idara ya nyuklia wa Iran Gholama Reza Aghazadeh, amejihuzuru nyazifa yake wiki tatu zilizo pita.
Kwa mujibu wa shirka la habari ISNA, limesema ya kuwa hakuna habari kamili zilizo sababisha kujihuzuru kwake.
Picha hapo juu ni ya waziri wa mambo ya nje wa Amerika, ambaye amesema yakuwa serikali ya Amerika, itafika wakati hatua za mazungumzo hazitafaa tena.
Picha ya pili ni mkuu wa nyklia wa Iran, ambaye aneng'atuka madarakani.
Kifo cha rais wa Palestina chaleta kitendawili kati ya viongozi wa Wapalestina.
Tunis, Tunisia - 16/07/09. Kiongozi wa mkuu wa kundi la Wapigania Ukombozi wa Wapalestina (PLO) Palestina Liberation Organasation Farouk Kaddoumi, ameongea na vyombo
vya habari na kudai ya kuwa ripoti aliyotoa anaisimamia na yoyote aneye ona siyo kweli, basi aje na ushahidi mwingine wa kutosha.
Farouk Kaddoumi,alikuwa anasisitiza hivyo, kuhusu yeye kuandika ripoti ya kuwa kuna baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Wapalestina walishiki katika mauaji ya aliyekuwa rais wa Wapalestina, hayati, Yasir Arafat.
Hata hivyo, baada ya habari hizi kupatikana, baadhi ya vyama vilivyo tajwa vimekanusha habari hizo.
Farouk Kaddoumi, ambaye no mmoja wa viongozi waanzilishi wa PLO, aishie Tunisia.
Picha hapo juu, ni ya hayati rais, wa Palestina, Yasir Arafat, ambaye aliga dunia miaka mitano iliyo pita nchini Ufaransa, wakati alipo pelekwa matibabu.
Picha ya pili ni ya, Farouk Kaddoumi, ambaye ametoa ripoti ambazo zinateta kitendawili kwa Wapalestina.

Wednesday, July 15, 2009

Rais, Muammar Gaddafi,NAM, ipataiwe kiti cha kudumu cha Usalama UN.

Wairan na Walmania wakumbwa na msiba.

Qazvin, Iran - 15/07/09. Ndege ya shirika la ndege la Caspian imedondoka na kuuwa watu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo.
Kwa muibu wa msemaji wa serikali wa Iran,Mohammed Reza Montezer Khorasan, alisema ndege hiyo ambayo ilikuwa imebeba watu wapatao 168 kutoka Iran Tehran na kuelekea jijini Yerevan Almenia, ilianguka karibu na mji wa Qazvin siku ya leo jumajatano, na kuwaauwa watu wote waliokuwemo kwenye ndege hiyo, wafanyakazi 15 na abiria 153.
Chanzo cha ajali bado kinachunguzwa, alimaliza msemaji huyo wa serikali.
Picha hapo juu, anaonekana, mmoja wa mama aliyepoteza ndugu zake katika ajali hii, akiwa analia kwa uchungu uku akisaidiwa na ndugu wengine.
Picha ya pili ni shirika la ndege la Caspiana Airline, ambapo moja ya ndege yake imeanguka na kupoteza maisha ya watu wapatao 168.
Picha ya tatu, wanaonekana wafanyakazi wa shirika la kutoa huduma ya kwanza wa Iran, wakiwa wamebeba baadhi ya mabaki ya miili ya watu waliopata ajali na ndege.
Picha ya mwisho, inaonekana,moja ya enjini ya ndege, ikiwa imeharibika vibaya ,ka kutupwa mbala na eneo ambalo ndege iliangukia.
Vita vya Gaza, habari tata za aanza kusikika hazarani?" Izrael".
Jerusalem,Izrael, - 15/07/09. Baada ya miezi sita kupita tangu, kusimama kwa vita kati ya kundi la Hamas na Izrael, baadhi ya wanajeshi wa Izrael, wamekuwa wakieleza matukio tofauti yaliyotokea wakati wa vita hivyo, ambavyo vilialibu vibaya eneo zima la Ukanda wa Gaza.
Wanajeshi hao, walisema ya kuwa matimizi ya siraha zenye gasi ya kunguza, zilitumika kwa nyakati fulani, na kudai kuna wakati mwingine waliamuliwa kuchukua hatua ambazo haziendani na maadili ya kijeshi.
Hata, hivyo , msemaji wa jeshi la Israel,Leutenant Colonel, Avital Leibovich, alikanusha madai hayo. na kusema madai hayo siya ukweli na hayana ushahidi wala tarehe ya matukio.
Picha hapo juu, ni ya moja ya tanki la kijeshi la Izrael likiwa mstari wa mbele katka maeneo ya Ukanda wa Gaza.
Rais,Muammar Gaddifi,NAM ipatiwe kiti cha kudumu cha usalama wa UN.
Sharm el Sheikh, Misri - 15/07/09. Rasi wa Libya, Muammar Gaddadfi, ameshutumu, Balaza la Usalama la Umoja wa mataifa ni kama chombo cha kutishia, ambacho kinatumika kwa baadhi ya nchi zenye viti vya kudumu katika kamati hiyo,na kunyima usawa katika maamuzi muhimu ya dunia, hasa kwa nchi masikini. aliyasema haya katika mkutano wa viongozi wa nchi zisizofungamana na upande wowote unaofanyika nchini Misri (Non Aligned Movement)
Akiongezea , rais Muammar Gaddafi, alisema wakati umefika wa NAM, kuwa na kiti katika kamati hiyo ya usalama ya umoja wa Mataifa , kwani tumekuwa tunajaziwa siraha na sasa zina kuwa mzigo kwa nchi wanachama wa NAM.
NAM, ambayo ni jumuia ya nchi zitokazo, Afrika, Asia na Latin Amerika.
Picha hapo, ni ya rais wa Libya, Moammar Gaddafi, ambaye amateaka NAM, ipatiwe kiti, katika balaza la Usalama la Umoja wa mataifa.
Kiongozi wa Al Qaeda namba mbili achomoza tena katika mitandao.
Islamabad/Pakistan - 15/07/09. Kiongozi namba mbili wa kundi la Al Qaeda's Ayman al Zawahiri, amewataka wafuasi wa kundi lake na wa Pakistani kupigana na Amerika na washirika wake waliopo nchini Pakistani, kwa kudai wamekuja kuwatawala na kuchukua nchi ya Pakistani.
Ujumbe huo wa Ayman al Zawahiri, uliwekwa kwenye mitandano siku ya jumanne wiki hii.
Hamasa hiyo kutoka kwa kiongozi wa Al Qaeda namba mbili, zimekuja wakati majeshi ya Pakistani, Amerika na washiriki wake, wakizidisha mashambulizi zidi ya kundi la Taliban na washiriki wake hivi karibuni katika eneo la maporomoko na mabonde ya Swat. Picha hapo juu ,ni ya Al Qaeda, Ayman al Zawahiri, akiongea kwa ujumbe wake katika moja ya mitandao ya kisasa.
Picha ya pili, wanaonekana, wanajeshi wa Pakistani, wakiwa katika doria, kulinda maeneo yao ili yasishambuliwe na Taliban na washiriki wake.