Monday, August 24, 2009

Wakuu wa majeshi wataka nguvu zaidi ili kupambana na Taliban.

Makundi ya kivita ya Somalia ya ungana kuipinga serikali.

Gedo,Somalia - 24/08/09. Kundi la Hizbu lililopo kusini mwa Somalia,limesema ya kuwa limeungana na kundi la Al-Shabaab. Kujiunga kwa kundi la Hizbu, kulitangazwa na , Sheikh Ahmed Mohamud, ambaye ni makamu wa wa kundi hilo alitangaza hayo wakati alipo kutana na waandishi wa habari hivi karibuni. Kiongozi huyo wa Hizbu, alisema wanaungana na wenzao ili kupambana na wapinga Wasomalia na tutawashinda alimalizia kwa kusema kiongozi huyo wa kundi la Hizbu lililopo mjini Gedo kusini mwa nchi ya Somalia.Picha hapo juu, ni wapiganaji wa kundi la Hizbu,kundi ambali limeungana na kundi la Al- Shabaab kupambana na serikali. Shirika la ujasusi la Amerika na mkuu wake wasimama njia panda.

Washingiton, Amerika - 24/08/09.Shirika la kijasusi la Amerika, huenda lakawa na wakati mgumu kufuatia habari ya kuwa huenda kesi zinazo husiana na mateso ya watu walio daiwa ni magaidi, zikafunguliwa na kuanza kuchunguzwa tena. Kesi hizo zilifutwa wakati wa uongozi wa rais wa zamani wa Amerika, George Bush, lakini tandu uongozi mpya wa rais , Baraka Obama, chini ya mwanasheria mkuu ,Erik H. Holder umekuwa na mtazamo upya katika swala zima la ugaidi. Picha hapo juu, ni alama ya shirika la kijasusi la Amerika, ambalo ndicho kiini cha ulinzi wa serikali ya Amerika. Picha ya pili, ni ya mwanasheria mkuu, wa Amerika, Erik H.Holder, ambaye tangu achukue ofisi, amekuwa na wakati mgumu kujaribu kuweza kurudisha hadhi ya shirika la kijasusi la Amerika.
Wakuu wa majeshi wataka nguvu zaidi ili kupambana na Taliban.
Bargam, Afghanistan - 24/08/09.Wakuu wa majeshi ya Amerika na NATO wamesema ya kuwa hawana majeshi ya kutosha kuweza kupambana na kundi la Taliban hadi kuliangamiza.
Kwa mujibu wa habari zilizo tolewa, zinasema yakuwa mashambulizi ya nayo fanywa na kundi la Taliban yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na kufanya jeshi la Amerika na NATO,kupanga mikakati mipya ya kupambana na kundi la Taliban.
Kufuatia hali hiyo, wakuu wa NATO na Amerika wamesema kuna haja kubwa ya kuogeza wanajeshi kutoka katika nchi wanacham wa NATO.
Picha hapo juu, anaonekana,mmoja wa mwanajshi akiwa mstari wa mbele kupambana na kundi la Taliban.

Friday, August 21, 2009

Usain Bolt, hana mpinzani katika mbio za mita 100 na 200.

Usain Bolt, hana mpinzani katika mbio za mita 100 na 200.

Berlinn Ujerumani - 21/08/09. Usain Bolt, mwana riadha wa Jamaika, amevunja rekodi za dunia za mbio za mita 100 na 200 kwa upande wa wanaume.
Usain Bolt,ambaye amekuwa hana mpinzani, aliwashangaza wapenzi wa riadha, na kuwaacha macho yakiwa hawaamini ya kuwa rekodi ya mbio za mita 200 ya sek 19:32, iliyo wekwa na Michael Johnson, baada ya kukumbia mbio hizo za mita 200 kwa sek 19:19.
Picha hapo juu,anaonekana, Usain Bolt, akiwa mbele pekee yake mara baada ya kuvuka mstari wa mwisho, na kuvunja rekodi.
Picha ya pili, anaonekana, Usain Bolt, akiwa mbele ya wakimbiaji wenzake wakati wa fainali za mita 200.
Picha ya tatu, anaonekana, Usain Bolt, akiwa mbele ya tangazo, linalo onyesha ya kuwa ameweka rakodi mpya ya dunia ya mbio za mita 200.
Mtuhumiwa wa Lockerbie awasili nyumbani.
Tripol, Libya -21/08/09. Abdel Basset al Megrahi,ambaye anatuhuniwa kwa kuhusika na mlipuko wa bomu nadni ya ndege ya Pan Am 103, amewasili nyumbani, baada ya kuachiwa huru jana na serikali ya Uingereza, kwa kuzingatia hali ya afya yake.
Bwana, Abdel Basset al Megrahi, alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha, mara baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika na ulipuaji wa ndege iliyo kuwa imebeba watu 270, watu wote kupoteza maisha kutokana na mlipuko huo.
Kufuatiwa kuachiwa kwake, baadhi ya viongozi wa kimataifa wamekuwa wakitoa maoni tofauti,kuhusu kuachiwa kwake.
Lakini hata hivyo, Abdel Basset al Megrahi, alipokelewa kwa shwange alipo wasili jijini Tripol.
Picha hapo juu, anaonekana, akiwa ameshikiliwa na baadhi ya watu waliokuja kumpokea.
Picha ya pili, anaonekana A.B. al Megrahi,akipanda ngazi kuingia ndani ya ndege, tayari kuanza safari ya kurudi nyumbani Libya.
Picha ya tatu, A.B.al Megrahi, akishuka kutoka kwenye uwanja wa ndege nchini Libya na wanaonekana mamia wakija kumpokea kwa shangwe.

Thursday, August 20, 2009

Uchaguzi wa Afghanistan, wakamilika jumuia ya kimataifa yangoja matokeo yake
Kabul, Afghanistan - 20/08/09. Wanachi wa Afghanistan, wamemaliza kupiga kura kuwachagua viongozi watakao ongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano mingine.
Kufuatia kumalizika kwa kupigwa kwa kura leo 1700( saa kumi na moja) kwa masaa ya Afghanistan, kura zimeanza kuhesabiwa rasmi. Kumalizika kupiga kura nchini Afghanistan, kumesifiwa na mwakilishi wa serikali ya Amerika, Richard C Holbrooke.
Bwana, Holrbooke, alisema ya kuwa wanchi wa Afghanistan, wameweza kupiga kura bila kuogopa vitisho vya Taliban, na huu ndiyo mwanzo wa kuijenga nchi yao Waafghanistan.
Picha hapo juu ni za wagombea wa kiti cha urais wa Aghanistani, kutoka kushoto,Abdullah Abdullah,Ramadhani Bashardost, Ashraf Ghani na Hamid Karzai.
Picha ya pili, wanaonekana wanchi wa Afghanistan, wakiwa katika mstari tayari kupiga kura kuchagua viongozi wao.
Uingereza yatakiwa kudhibiti biashara ya siraha.
London, Uingereza 20/08/09.Shirika linalo shughulikia usimamizi wa uuzaji wa siraha duniani, limeitaka serikali ya Uingereza, kuchukua hatua upya ya kusimamia reseni na uuzaji wa siraha wa makampuni yanayo uza siraha hizo ambazo zinatikea nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika hilo,limesema yakuwa, katika uchunguzi wake, limegundua ya kuwa siraha nyingi zinazo tumika katika mapigano sehemu tofauti zinaalama ya matengenezo kutoka Uingereza.
Shirika hilo pia limeitaka serikali ya Uingereza kujaribu kushirikiana na mashirika ya siyo ya kiserikali ili kudhibiti uuzaji haramu wa siraha hizo.
Hata hivyo serikali ya Uingerza imesema yakuwa inafuata sheria za kimataifa na itazidi kuimarisha udhibiti huo.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Uingereza nchi ambayo imetakiwa kuongeza bidii kudhibiti uuzaji wa siraha zinazo tokea nchini humo.

Wednesday, August 19, 2009

Mmea wa bangi majaribioni kutibu kansa.

Rais wa za zamani wa Zambia, ashukuru Mungu, "Kesi imefutwa" Lusaka, Zambia - 19/08/09. Rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, ameachiwa huru, baada ya kukutwa hana hatia ya kula rushwa wakati wa uongozi wake akiwa rais wa Zambia. Kesi hiyo, ambayo aliyo kuwa inamkabiri rais huyo wa zamani wa Zambia, Fredrick Chiluba ni kuhusika na upotevu wa $500,000 za Amerika Kwa mujibu wa mahakama, wanasheria wa serikali walio fungua kesi hiyo walikosa ushahidi kamili. Rais huyo wa zamani wa Zambia, Fredrick Chiluba, amekuwa akikabiliwa na kesi iliyo chukuwa miaka minane tangu ashitakiwe. Mungu ni mkubwa, ameonyesha ukweli upo wapi na alisikika akisema hayo rais huyo wa zamani wa Zambia. Picha hapo juu, anaonkekana, rais wa zamani wa Zambia, Fredrick Chiluba, akinyanyua mikono juu kumshukuru Mungu, mara ya kusikia kesi iliyo kuwa ikimkabili imetupiliwa mbali na mahakama. Wanaume wabakwa kwa wingi nchini DRC. Goma, DRC - 19/08/09. Hali imezidi kuwa mbaya katika eneo la Goma, baada ya wanaume kuanza kubakwa. Kwa mujibu wa mmoja ya watu waliokumbwa na mkasa huo,Kazungu Ziwa,alisema alivamiwa na kukamatwa na watu wenye mapanga na virungu. Baada ya kuvamiwa alijaribu kupigana nao, lakini alishindwa , na matokeo ya ke wakamtawiti kwa nguvu, na baadaye walimwacha akiwa taabaani. Kwa mujibu wa bwana Ziwa, alisema ya kuwa watu hao, walikuwa ni moja ya makundi wanaopigana katika maeneo hayo. Picha hapo juu, ni moja ya picha za watu ambao walikumbwa na mikasa ya kulawitiwa.

Mmea wa bangi majaribioni kutibu kansa.
London,Uingereza -19/08/09.Mmoja wa wataalamu wanaofatilia tiba ya kansa,Ine Diaz-Laviada, amesema ya kuwa mmea wa bangi unaweza kusaidia kuponyasha ugonjwa wa kansa.
Ine Diaz Laviada, alisisitiza ya kuwa chunguzi wa muda mrefu umeonyesha mmea huu unaweza kutumika kama dawa ya kusaidia kutibu kansa.
Hata hivyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.
Picha hapo juu, ni ya mmea wa bangi, mmea ambao huenda hapo baadaye ukasaidia kutibu kansa.
Mwanafunzi mzee kuliko wote, afariki dunia.
Nairobi, Kenya - 19/08/09. Raia wa Kenya, Mzee, Kimani Nganga Maruge aliyekuwa na miaka 90, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kansa ya tumbo.
Mzee Kimani Nganga Muruge, ambaye aliweka historia,na kuandikwa katika kitabu cha historia, kwa kujiandikisha shule ya msingi huku akiwa na miaka 84,na mzee wa kwanza kuanza shure akiwa na umri mkubwa.
Mzee, Kimani Nganga Magure, aliamua kujiandikisha shule,baada ya kuhisi ya kuwa muhubiri alikuwa anatafsili vibaya na kupoteza maana ya ujumbe kamili.
Mzee, Kimani Nganga Maruge, alikuwa mmoja ya wapigania uhuru wa Kenya miaka ya 1950, chini ya Uongozi wa Mau Mau.
Picha hapo juu, anaonekana katikati mzee Kimani Nganga Maruge,akiwa darasani na yupo tayari kuuliza swali.Mungu ailaza mahari pema peponi roho yake mzee Kimani Nganga Maruge.
Wajenzi wa viwanja kupata tiketi za bure, " Mchezo wa soka Afrika ya Kusini.
Johannesburg, Afrika ya Kusini -19/08/09. Chama cha mpira nchini Afrika ya Kusini, kwa kushirikiana na shirikisho la kandana ulimwenguni FIFA, zimepanga kutoa tiketi zaidi ya 120,000 za bure, ili waler wapenzi wa sika nchini humo, wasio na uwezo wa kulipa waweze kuhudhulia mashindano hayo ya soka yatakayo fanyika nchini humo - ( Afrika ya Kusini).
KWa mujibu wa FIFA, tiketi hizo za bure, zitadhaminiwa na mashirika na makampuni ya Adidas,Coca Cola, kampuni ya Magari ya KIA, Emarates, Hyundai, Sony na Visa.
Kufuatia kutolewa kwa tiketi hizo, wajenzi wote waliohusika katika kujenga viwanja hivyo, watakuwa wa kwanza kupata tiketi hizo.
Picha hapo juu ni ya mmoja ya washibiki wa soka nchini Afrika ya Kusini, ambaye huenda akabahatika kupata tiketi ya bure kuona mpambano wa soka wa kunyanyia kombe la Dunia.

Wednesday, August 12, 2009

Kura ya maoni ya Niger yaleta maswali kwa EU.

Kura ya maoni ya Niger yaleta maswali kwa EU.

Brussels, Ubeligiji - 12/08/09. Muungano wa nchi za Ulaya EU, umesema uhenda ikapunguza kuendela kuisaidia nchi ya Niger, baada ya rais Mamodou Tandja, kubadilisha katiba na kumwezesha kutawala tena kwa kipindi kingine.
Kubadilishwa kwa katiba hiyo ya nchi ya Niger, kumekuwa kukilaumuwa na nchi wanchama wa EU.
Mabadiliko hayo ya katiba, yatamwezesha rais Mamodou, kutawala kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.
Picha hapo juu ni ya bendera ya nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya, ambao umekuwa ikisaidia nchi ya Niger kwa muda mrefu.
Picha ya pili ni ya rais, Mamodou Tandja,ambaye kura za maoni zilikubali pendekezo lake.
Urusi kuimarisha jeshi lake karibu na mipaka na Georgia.
Sukhumi,Abhakazia - 12/08/09. Waziri kuu wa Urusi, Vladimir Putin, amesema ya kuwa nchi nyingi za Ulaya zinailaumu Georgia kwa kuanzisha vita,na viongozi Georgia hawataki kukubali ya kuwa wao ndiyo waliotoa mri ya kuanza vita.
Waziri mkuu yuho, Vladimir Putin,alisisi tiza kwa kusema yakuwa viongozi wa Georgia hawawezi kukubari kutokana na mkandamizo wanao upata kutoka Amerika.
Ziara hiyo katika jimbo la Abhakazia, ni katika kuangalia na kuwapa pole wale wote walio athirika na vita.
Waziri mkuu, Putin, alisema Urusi itawekeza $ 470, ili kuimarisha ulinzi katika eneo la Abhakazia na kipaka na Georgia.
Picha hpo juu, anaonekana mama , mmoja alimsalimia waziri mkuu, wa Urusi, Vladimir Putin, alipo tembelea Abhakazia.
Rais atoa amri kutafutwa kwa meli iliyo potea.
Moscow, Urusi -12/08/09. Rasi wa Urusi, Dmitry Medvedev, ametoa amri ya kutafutwa kwa moja ya meli ya mizigo iliyo potelea karibu na pwani ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa msemaji wa idara ya ulinzi wa bahari wa Urusi,Vladimir Vysotsky,alisema amri hiyo,imekuja mara baada ya juuudi za kutafuta meli hiyo kuleta utata.
Meli hiyo iliyo kuwa na raia wa Urusi, ilipotelea njiani tangu tarehe 4/8/09, njiani kuelekea Algeria.
hata hivyo kuna wasiwasi yakuwa meli hiyo,huenda ikawa imetekwa na na maharamia.
Picha hapo juu ni rais wa Urusi, Dmitry Medvedev , ambaye ameagiza kutafutwa kwa meli iliyopotelea baharini.

Tuesday, August 11, 2009

Daw Aung San Suu Kyi, aongezewa kifungo zaidi.

Yangon Myanmar - 11/08/09. Serikali ya Myanmar,imemuhukumu kifungo cha miezi 18 au mwaka mmoja na nusu, Daw Aung San Suu Kyi, ambaye kiongozi wa National League for Democracy - NLD.
Uamuzi wa kumgunga kifungo cha ndani ulikuja baada ya mahakama kudai ya kuwa , Suu Kyi, alivunja sheri ya ndani na hivyo atatumikia kifungo cha mieizi 18 baada ya kukutana John Yettaw Ambaye ni raia wa Amerika nyumbani kwake.
Picha hapo juu, ni picha ya, Daw Aung San Suu Kyi,akichungulia dirishani, na hivi sasa amehukumiwa kifungo cha ndani cha miezi 18 zaidi.
Picha ya chini, ni moja ya gari la polisi la Myanmar, likiwa na walinzi na baadhi ya watu ndani ya gari hilo tayari kuelekea mahabusu.

Monday, August 10, 2009

Uingereza haitaruhusu watu kuteswa na makachero.

Wepesi wa mawasiliano ya kimtandao kuwepo Afrika. Mombasa, Kenya - 10/08/09.Kampuni ya SEACOM, imewekeza kiasi cha $ 2.6billion katika eneo la Afrika ya Mashariki katika kuinua mawasiliano ya kimtandao. Kwa mujibu wa mtasmini wa mambo ya mawasiliano, David Lerche, alisema ya kuwa Afrika itafaidika kwa kiasi kikubwa zaidi ya mara 10, na kuweza kuwasiliana na mabara mengine kiuraisi zaidi kwa kutumia mtandao, kwani mitambo hiyo itaunganisha bara la Asia na Ulaya na itakuwa na nguvu zaidi. Picha hapo juu wanaonekana, wafanyakazi wa kiwa kazini kuvuta moja ya waya za kupitishia mawasiliano katika mji wa Mombasa nchini Kenya kuelekea ndani ya bahari ya Indi kuelekea katika bara la Asia. Uingereza haitaruhusu watu kuteswa na makachero. London,Uingereza, 10/08/09.Serikali ya Uingereza, imesema yakuwa itakuwa ni vigumu, kwa makachero au majasusi wa nchi kukubali au kukataa ya kuwa habari zilizo patikana, lizipatikana kutoka kwa watu washukiwa wa makundi ya uhaini, baada ya kuteswa kwa kinyume cha sheria za haki za binadamu. Akiongea hayo, waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Miliband, alisema hayo alipo kuwa akiongea na vyombo habari, na kusema ya kuwa serikali ya Uingereza, hairuhusu wa kutesa watu kwa aajili ya kupata habari na hii ni kinyume na haki za binadamu. Picha hapo juu ni ya waziri wa mambo ya nje wa Uingereza, David Miliband,alipo kuwa akiongea na vyombo vya habari siku ya jumapili wiki hii. Uhusiano wa Venezuela na Kolombia wawa wa wasiwasi. Caracas, Venezuela - 10/08/09. Rais wa Venezuela, Hugo Chavez, amekaripia nchi ya Kolombia kwa kudai yakuwa imetuma wanajeshi kuingia Venezuela. Akisisitiza ,rais Hugo Chavez, alisema ya kuwa hawakuwa askari wa kulinda mpaka, bali walikuwa ni wanajeshi na walivuka Mto wa Orinoco na kuingia hadi ndani ya Venezuela. Na wakati wanjeshi wa Venezuela walipokwenda kwenye eneo hili, walikuta wanajeshi wa Kolombia wamesha ondoka. Venezuela, imekua ikipinga kitendo cha Kolombia kuruhusu, Amerika kuweka kambi zake za kijeshi nchini Kolombia. Na wakti huo huo , Kolombia imekuwa ikiilaumu Venezuela, kwa kuwasaidia waasi wa kundi la FARC, ambalo linapingana na serikali ya Kolombia. Hata hivyo, serikali ya Kolombia imekanusha madai hayo. Picha hapo juu, wnaonekana, rais wa Venzuela, Hugo Chavez, akiongea na vyombo vya habari.

Sunday, August 9, 2009

Viongozi wa siasa nchini Madagaska wakibaliana

Viongozi wa siasa nchini Madagaska wakubaliana kimsingi

Maputo, Mozambiki - 09/08/09. Vyama vya upinzani nchini Madagaska, vimekubaliana kushirikiana kuunda serikali ya mpito kwa kipindi cha miezi 15 chini ya usimamizi wa rais wa zamani wa Mozambiki, Joakim Chissano.
Kwa mujibu, wa msemaji wa UN (Umoja wa Mataifa) Tiebile Drame, pande zote mbili zimekubaliana kimsingi yakua kipindi hicho cha mpito cha miezi 15, kikifikia wanachi wa Madagaska, watajiandaa kupiga kura kwa uchaguzi mkuu.
Picha hapo juu, ni ya rais wa sasa wa Madagasca, Andry Rajoeli,ambaye aliingia madarakani, baada ya kung'olewa madarakani rais, Marc Ravalomanana.
Picha ya pili, ni ya rais wa zamani wa Madagaska, Marc Ravalomanana,ambaye kutolewa kwakwe madarakani watu wapato 100, walifariki dunia.
Picha ya tatu ni ya bendera ya Madagaska, nchi ambayo imekuwa na myumbo wa kisiasa tangu kufanyika mapinduzi yaliyo mng'oa madarakani rais, Marc Ravalomanana.

Wednesday, August 5, 2009

Mahmoud Ahmadinajed, aapishwa tena kuwa rais wa Iran.

Billy Clinton, azuru Korea ya Kaskazini, waandishi wa habari wa achiwa huru.

Los Angeles,Amerika - 05/08/09. Waandishi wa habari wawili raia wa Amerika, Laura Ling na Euna Lee,wameachiwa huru na kuwasili nyumbani kuungana na familia zao, baada ya kukaa jela kwa muda wa miezi minne na siku kadhaa kwa msamahaa wa rais wa Korea ya Kaskazini.
Kuchiwa kwao kumekuja mara baada ya rais wazamani wa Amerika,Billy Clinton kufanya ziara ya ghafla nchini Korea ya Kaskazini, na kuongea na rais Kim Jong Il.
Hata hivyo hakuna habari zozote zilizo elezwa kuwa viongozi hawa waliongea nini.
Picha hapo juu, wanaonekana, rais wa zamani wa Amerika, Billy Clinton kushoto,na rais wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong Il, wakati alipo kuwa nchini Korea ya Kaskazini.
Picha ya pili, wanaonekana, Laura na Euna, wakishuka kutoka kwenye ndege, kukanyaga ardhi ya Amerika, baada ya kuachiwa huru kwa msamahaa wa rais wa Korea ya Kaskazini.
Picha ya tatu, wanaonekana, Laura na Euna wakikaribishwa kuingia kwenye ndege na rais wa zamani wa Amerika Billy Clinton.
Mahmoud Ahmadinajed, aapishwa tena kuwa rais wa Iran.
Tehran,Iran - 05/08/09. Mahmoud Ahmadinejad ameapishwa kwa mara ya pili kuwa rais wa Iran.
Akiongea baada ya kuapishwa, rais, Mohmoud Ahmadinejad,alisema ya kuwa atafanya mabadiliko katika serikali yake, kitaifa na kimataifa.
Katika, sherehe ya kuapishwa kwake, kuliudhuliwa na viongozi na mabalozi wa nchi tofauti, lakini baadhi ya viongozi wa vyama pinzani walisusia sherehe hiyo.
Picha hapo juu, anaonekana,rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad kulia,akikabidhiwa hati za serikali na kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei aliyepo kushoto.
Picha ya chini, anaonekana, rais wa Iran,Mahmoud Ahmadinejad,akiongea mara ya baada kuapishwa kwake.

Tuesday, August 4, 2009

Nashukuru kuondoka kwa Eto'o,alikuwa ananipa ndoto zisizo za kawaida.

Nashukuru kuondoka kwa Eto'o, alikuwa ananipa ndoto zisozo za kawaida.

Madrid, Uispania - 04/08/09. Golikipa au mlinzi namba moja wa timu ya taifa ya Uispania Iker Casillas, amesema amefurahi kuondoka kwa mshambuliaji hatari wa timu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Kameroon, Samwel Eto'o.
Akiongea leo hii, Casillas, alisema ya kuwa Eto'o, alikuwa akimfanya aote ndoto zisizo eleweka kila anapo fikilia mechi na timu ya Barcelona.
Akiulizwa na waandishi wa habari, Iker Casillas, kuhusu mshabuliaji ,Zlatan Ibrahimovic, mlinda mlango huyo, alisema Ibrahimovic ni mchezaji mzuri, lakini Eto'o ni hana mfano.
Hapo juu, ni picha tofauti, zinaonyesha ni kwa kiasi gani,mlinzi wa timu ya Madrid, Iker Casillas, alivyokuwa akiteswa na kuteseka kila anapo kutana na mshambualiji wa Barcelona, Samwel Eto'o.
Kwani, Eto'o amekuwa akimpa wakati mgunga mlizi huyo, Iker Casillas na kuona nyavu zilizo chini ya ulinzi wa kipa huyo.

Monday, August 3, 2009

Katibu mkuu wa NATO aanza kazi rasmi.

Mfereji wa Suezi wa kumbwa na upepo wa kiuchumi. Suez Kanal, Misri - 03/08/09. Serikali ya Misri imesema ya kuwa kutokana na hali ya uchumi kuyumba na vitendo vya ugaidi kuzidi katika bahari za Hindi ,kumefanya mapato ya kodi kushuka kwa kiasi kikubwa na kufikia asilimia 7.2 (7.2%). Mfereji wa Suez, unatumika kwa kupitishia meli zote, zinazo ingia na kutoka bara la Ulaya na Amerika kuelekea bara la Asia, Afrika na nchi za Mashariki ya kati. Akiongea haya, mkuu wa mfereji huo wa Suez, Ahmed Ali Fadel,alisema yakuwa matatizo ambayo yanaikumba dunia kiuchumi yanachangia kwa kiasi kikibwa, anaamini hali ya mapato ya kodi yataanza kupanda hapo hali ya uchumi itakapo kuwa nzuri. Picha hapo juu, nimoja ya boti ya polisi, ikiwa katika ulinzi wa mfereji wa Suez, ambapo kwa kipindi hiki, meli zimekuwa hazipiti kwa wingi kwa sababu tofauti, moja wapo swala la usalama katika pwani karibu na Somalia.

Katibu mkuu mpya wa NATO, aanza kazi rasmi.
Brussel, Ubeligiji 03/08/09. Katibu mkuu mpya wa NATO, Fogh Rasmussen,ambaye pia alishawahi kuwa waziri mkuu wa Denmark,ameanza kazi rasmi leo.

Kabla ya kuanza rasmi kazi ya ukatibu mkuu wa NATO leo, amesema wakati wa uongozi wake , atahakikisha ya kuwa Afghanistan, wanakuwa na ulinzi wao wenyewe na kulinda usalama wa nchi yao, na hivyo kuzitaka nchi wanchama wa NATO, kushirikiana zaidi ili kufanikisha lengo hilo.

Aliongezea ya kuwa NATO, itazidisha ushirikiano na nchi wanachama wa jumuiya zanchi za Kiislaam.

Jumuiya hizo ni Mediteranian Dialogue (MD) na Istambul Co- operation Initiative (ISCI).

Fogh Rasmusessen, amechukua kazi iliyo achwa na katibu mkuu wa zamani wa NATO, Jaap de Hoop Sheffer.

Pichani hapo juu wanaonekana, Jaap Hoop Sheffer,ambaye anatoka madarakani kama katibu mkuu wa NATO na kulia ni katibu mkuu mpya wa NATO, Fogh Rasmussen,akiongea ni kwa jinsi gani wakati wa uongozi wake atakavyo fanya.

Picha ya pili, ni ya Katibu mkuu mpya wa NATO, Fogh Rasmussen, akiongea mbele ya wajumbe NATO.

Sunday, August 2, 2009

Google ya pata wapinzani wa kitandao.

Google ya pata wapinzani wa kimtandao.

Redmond,Amerika - 02/08/09. Makampuni makubwa duniani yanayo ambayo ndiyo yanayo shughulikia nugu za mitaandao, Microsoft na Yahoo, zimeamua kuungana ili kushindana kibiashara na kamuni nyingine kubwa ya Google.
Makampuni ya Microsoft na Yahoo yalitiliana saai mkataba wa makubaliano ya ushirikiano siku ya Jumatano,29/07/09, na kukamilisha mipango yote hivi karibuni.
Akiongea mbele ya vyombo vya habari, mkurugenzi mkuu wa Microsoft,Steven A Ballmer, alisema ya kuwa ushirikiano huu ni mzuri kwani utainua kampuni zote mbili, na kuweza kushindana na Google.
Picha hapo juu ni ya alama ya kampuni ya Googe ikiwa mbele ya ofisi zake, ambapo kwa sasa itakuwa na washindani wawili wakubwa Microsoft na Yahoo katika biashara ya kimtandao..
Picha mbili zinazo fuatana za Microsoft na Yahoo,zimeungana kibiashara, ili kuleta ushindani wa kibiashara na Google.
Mtandao kutumika katika kutibu wanajeshi.
Hawaii, Amerika - 02/08/09. Kituo cha afya TriWest, kilichopo Hawaii nchini Amerika, kimeseama kitaanza kuwatibu na kutoa ushauri kwa wanajeshi na familia zao kiakili kwa kutumia mtandao picha ( Webcam).
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana , zinasema ya kuwa wataalamu wa hali za utimamu wa binadamu na waganga, wataanza matibabu hayo kakuangali ni kwa kiasi gani wanajeshi ambao wameumia vitani wataweza pata kurudi katika hali ya kawaida.
Mpango huu, umeweza kufanikiwa katika majaribio kwa kushirikiana na wataalamu wa maswala ya kijeshi ya Amerika alisema, David J. McInntyre.
Picha hapo juu, wanaonekana, wanajeshi wakiwa wanambeba mmoja ya mwanajeshi mwenzao , baada ya kuumia wakati wa mapambano.
Picha hapo
Rwanda kuupa utalii kipao mbele.
Kigali, Rwanda - 20/08/09. Serikali ya Rwanda pamoja na kampuni ya Dubai , ( Dubai World),
zimeanza kushirikiana kwa pamoja ili kukuza utalii nchini humo.
Kwa mujibu wa , mkurugenzi mkuu wa wa maendeleo ya Rwanda,Clare Akamanzi, alisema ushirikiano huu, ni muhimu kwani serikali ya Rwanda, moja ya nchi ambayo ina vivutio vingi vya utalii na utalii utachangia katika kuinua hali ya uchumi wa nchi.
Pichani hapo juu, wanaonekana, ujenzi wa moja ya hotela ya kitalii, ukiendelea kwa ushirikiano wa serikali ya Rwanda na Dubai World.
Magorila hatarini na virusi vya ugonjwa wa ukimwi
Alabama, Amerika - 02/08/09. Wachunguzi wa maswala ya utibabu wa magorila, wamesema wamegundua ya kuwa ugonjwa wa ukimwi unaweza kuwazuru wanyama hawa kama unavyo waathiri wanadamu.
Kwa mujibu wa Dr, Beatrice Hahn wa chuo cha Alabama,amesema uchunguzi ulifanywa unaonyesha wazi ya kuwa virusi ukimwi vinateta hali ya hatari kwa magorila hao.
Hapo juu, anaonekana, mmoja ya magorila, akiwa ameshikilia mtoto wake.