Edward "Ted" Kennedy, Simba wa utetezi wa haki kwa watu wote, hatuko naye tena.
Massachusetts, Amerika - 26/08/09. Kiongozi wa muda mrefu chama cha Demokratiki cha Amerika, Edward "Ted"Kennedy na ambaye amekuwa Seneta kwa kipindi kirefu amefariki leo kutokana na ugonjwa wa tarasani ya ubongo kwa muda mrefu.
London, Uingereza - 26/08/09. Waziri mkuu wa Izrael, Nenyamin Netanyahu, ameanza ziara ya bara la Ulaya , ili kuzungumza na viongozi wa bara Ulaya kuhusu swala zima hali ya Mashariki ya Kati.
Waziristan ya Kusini,Pakistan - 26/08/09. Kundi la Taliban, limekubali ya kuwa kiongozi wao Baitullah Mehsud, amefariki dunia jana siku ya jumapili, kutokana na majeraha aliyo yapata baada ya mashambilizi yaliyo fanywa na ndege mtandao ya Amerika.
Beijing, China - 26/08/09. Serikali ya China, imetoa ruhusa kwa watu ambao kwa matakwa wapo tayari kutoa baadhi ya viongo vyao kwa ajili ya kusaidia watu wengine.
Kwa mujibu wa serikali, shirika la msalaba mwekundu la China,kwa kusaidiana na wizara ya afya zitasimamia kwa uangalifu swala zima la hali hiyo.
Washington, Amerika - 26/08/09. Shirika linalo shughulikia kuangalia afya za watu duniani, limesema yakuwa kiasi cha watu wapatao millioni 6, watapoteza maisha yao kutokana magonjwa yanayo sababishwa na uvutaji wa sigara, ifikapo mwisho wa mwaka ujao.











































