Wabrazil wamchagua rais mwanamama kuiongoza nchi yao
Wabrazil wamchagua rais mwanamama kuiongoza nchi yao
Posted by
Kibatala
at
Monday, November 01, 2010
0
comments
Mizigo inayo sadikiwa kuwa na bomu yapatikana.
Dubai, UAE - 30/10/2010. Makachero wa UAE na makachero wa kimataifa wa nchi za Uingereza na Amerika wamefanikiwa kuukamata mizigo ambao inasadikiwa ilikuwa ndani ya ndege tayari kuelekea Amerika.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "mizigo hiyo ilikuwa imetokea nchini Yamen. Mizigo hiyo likutwa na aina fulani ya unga PETN ambao unasadikiwa ungetumika kuleta madhara."
Picha hao juu inaonekana moja ya ndege ya kubebea mzigo ikiwa inafanyiwa ukaguzi mara ya habari kupatikana ya kuwa kuna moja ya ndege za kubebea mizigo imebeba mzigo wenye bomu.
Kabul,Afghanistan - 30/10/2010. Serikali ya Afghanistani imekubali kuongeza muda wa kuwepo kwa makampuni ya ulinzi ya kibinafsi.
Santa Cruz,Argentina - 30/10/2010. Aliyekuwa rais wa Argentina Nestor Kirchner azikwa nyumbani kwao alikozaliwa Rio Gallegos.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, October 30, 2010
0
comments
Tarik Aziz ahukumiwa kifo na mahakama kuu nchini Irak.
Baghdad, Irak 26/10/2010. Mahakama kuu nchini Irak imemuhukumu adhabu ya kifo aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na naibu waziri mkuu wakati wa utawala wa rais Saddam Hussein.
Posted by
Kibatala
at
Tuesday, October 26, 2010
0
comments
China huenda ikatumia kura yake ya veto.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, October 24, 2010
0
comments
Michezo ya 19 ya jumuia ya Madola yamalizika nchini India.
New Delhi, India 15/10/2010. Mashindano ya 19 ya nchi za jumuia ya Madola yamemalizika rasmi leo nchini India.
Moscow, Urussi - 15/10/2010.Serikali ya Venezuela imetiliana sahii mkataba na serikali ya Urussi kujenga mtambo wa nguvu za kinyuklia nchini Venezuela.
Milima ya Alps , Uswis 15/10/2010. Uchimbaji wa barabara chini ya milima ya Alps ambayo itakuwa barabara ndefu duniani kupita ndani ya mlima imemalizika.
Posted by
Kibatala
at
Friday, October 15, 2010
0
comments
Kazi ya uokoaji yamalizika salama nchini Chile.
Atacama, Chile 14/10/2010. Waokoaji wamefanikisha kazi ya kuwaokoa wafanyakzi 33 waliokuwa wamekwama kutoka katika migodi iliyopo kwenye jangwa la Atacama baada ya kukwama ndani ya machimbo ya migodi kwa zaidi ya miezi miwili .
Beiruti, Lebanon-14/10/2010. Rais wa Iran amewahutubia maelfu ya Walebanoni kwa nyakati tofauti tangu kuanza kwa ziara yake ya kiseikali nchini humo.
Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad katika hotuba zake aliwasifu wananchi wa Lebanon kwa kusema "ujasiri wane wa kutokukubali kuonewa na ndiyo imekuwa changamoto katika eneo zima la Mashariki ya Kati."
Seoul, Korea ya Kusini - 14/01/2010. Mamia ya watu wameandamana katika jiji la Seoul kupinga kitendo cha kiongozi wa serikali ya Korea ya Kaskazini kumteua mtoto wake kushika madaraka yake.
London Uingereza - 14/10/2010. Waziri Mkuu wa Uingereza amekutana na Mkuu wa Majeshi wa Amerika anayesimamia vita vya Afghanistan ili kupata muafaka kuhusu kifo cha raia mmoja wa Uingereza.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, October 14, 2010
0
comments
Swala la amani kati ya Waizrael na Wapalestina la chukua sura mpya.
Jerusalem, Israel - 11/10/2010. Waziri mkuu wa Izrael amewataka viongozi wa Kipalestina kukubali na kutambua ya kuwa Izrael in taifa la Mayahudi.
Budapest Hunguri - 11/10/2010. Polisi nchini Hungari wamemkamata na kuweka kizuizini mkuu wa kampuni ya kuzalisha vyuma kwa kosa la kupasuka kwa bwawa lenya maji yaliyo changanyika na sumu hivi karibuni.
Posted by
Kibatala
at
Monday, October 11, 2010
0
comments
Askofu Desmond Tutu astaafu kazi zote za kiofisi.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, October 07, 2010
0
comments
Mashindano ya Jumuia ya Madola ya funguliwa.
New Dheli, India - 03/10/2010. Wananchi wa India wamewakaribisha wanamichezo mbalimbali ili kushiriki mashindano ya nchi wanachama wa jumuia ya nchi zilizo kuwa koloni la Uingereza ambayo yanajulikana kama mashindano ya nchi za jumuia ya madola.
Mashindano hayo ya 19th yameanza rasmi baada ya habari za wasiwasi kuenea ya kuwa itakuwa vigumu kwa mashindano hayo kufanyika kutoakana na maandalizi yaliyo tiliwa mashaka.
Picha hapo juu wanaoneka wanamichezo wakishiriki wakati wa ufunguzi huku wakiongozwa na maonyesho yalioandaliwa kwa ajili ya ufunguzi.
Berlin, Ujeruman - 03/10/2010.Wananchi wa Ujerumani wameshangilia siku ya kuungana Ujerumani ya Mashariki na Ujerumani ya Magharibi ambapo ziliungana 1990.
Athens, Greece - 03/10/2010. Serikali ya China imesema itaisaidia kikamilifu serikali ya Greek katika kujenga uchumi wake uliyo yumba.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, October 03, 2010
0
comments
Denzel Washington kutangaza siku yamshindi wa Nobel nchini Oslo.
Oslo, Norway - 01/10/2010. Mcheza simema maarufu duniani atakuwa mtangazaji wakati wa kutoa zawadi ya Nobel Price itakayo fanyika mwaka huo Oslo.
Denzel Washington ambaye amekuwa maarufu kwa kucheza sinema zenya kusisimua hisia katika jamii alisema "niheshima iliyoje kuwa mmoja wapo ya watu watakao kuwepo na kushiriki kwenye sherehe hiyo."
Picha hapo juu anaonekana Denzel Washington akiwa ameshikilia zawadi aliyo shinda kuwa mshindi bora katika kucheza sinema nzuri na kusisimua.
Rwanda na Uganda zakanusha madai ya repoti ya Umoja wa Mataifa.
Posted by
Kibatala
at
Friday, October 01, 2010
0
comments
Kiongozi wa Korea ya Kaskazini ampa madaraka ya chama mtoto wake.
Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 29/09/2010. Kiongozi wa serikali ya Korea ya Kaskazini amemteua mtoto wake wa kiume kushika nyazifa zake za uongozi wa chama nchi humo.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, September 29, 2010
0
comments
Rais Robert Mugabe ataka Afrika ipewe kiti cha kudumu.
UN, New York 27/09/2010. Rais wa Zimbabwe ametaka bara la Afrika lipewe kiti katika baraza la usalama la umoja wa Mataifa.cha kudumu
Rais Robert Mugabe alisema "ni kitu kisichokubalika na wala kueleweka kwa bara la Afrika kuwa nara pekee lisilokuwa na kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja wa matifa na ihii inaleta kutokuwa na usawa kihistoria"
Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa ina wakilishwa na Uingereza, Marekani, China, Urussi,France na wawakilishi kumi ambao uchaguliwa kila baada ya miaka miwili na watano kubadilishwa kila mwaka.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe akihutubia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa katika kikao cha 65 cha umoja huo wa mataifa 2010.
Serikali ya Ufaransa ya haidi kuwaokoa raia wake waliotekwa nyara.
Bamako, Mali - 27/09/2010. Serikali ya Ufaransa iko mbioni iki kuwaokoa raia wa Ufaransa ambao wametekwa nyara na kundi la Maghreb ambao linashirikiana na kundi la Alqaeda.
Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya rais alisema" tunaamimini ya kuwa raia waliotekwa na kundi hilo bado wazima na niwajibu wa serikali kuokoa maisha ya raia wake"
Pichani anaonekana rais wa Ufaransa ambaye serikali yake inafanya kila mbinu kuwaokoa raia wake waliotekwa nyara na kundi la Maghreb.
Paris, Ufaransa - 27/09/2010. Rais wa taifa la Wapalestina amesema ya kuwa hatasimamisha mazungumzo na serikali ya Izrael kwa sasa ili kutoa muda wa kusimamishwa ujenzi wa makao mapya ya Waizrael.
Posted by
Kibatala
at
Monday, September 27, 2010
0
comments
Baraka Obama asisitiza ushirikiano kutatua mgogoro wa Mashariki ya Kati.
New York, Amerika- 23/09/2010. Rais wa Amerika amezitaka jumuia za kimataifa kushirikiana ili kuleta amani kati ya Waisrael na Wapalestina.
UN,New-York - 23/09/2010. Rais wa Iran imeitaka dunia kutangaza mwaka 2011 kuwa mwaka wa kuhangamiza na kuharibu siraha zote za mabomu ya kinyuklia kote duniani.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, September 23, 2010
0
comments