Tuesday, April 10, 2012

Serikali ya mpito ya Libya yapingana na mahakama ya Kimataifa.

Zintan, Libya - 10/04/2012. Serikali ya Libya imeitaka mahama ya kimataifa inayo shughurikia makosa ya jinai na kutetea haki za binadamu kutoa muda ili kuweza kuaanda kesi ya mtoto aliyekuwa mtoto wa rais wa Libya Muammar Gaddafi.
Serikali ya mpito ya Libya iliomba kwa kusema " Libya haitampeleka Saif al Islam Gaddafi nchi Uhollanzi kwani serikali ya Libya inauwezo wa kuendesha kesi zidi yake."
Seif al Islam Gaddafi ambaye alikamatwa baada ya baba yake Muammar Gaddafi kuangushwa kutoka katika kiti cha urais na kuwawa, anashutumiwa kwa kuhusika katika kukiua haki za binadamu wakati wa utawala wa baba yake.

Mozambique na Ureno zazungumzia utata wa bwawa la Cahora Bassa.


Maputo, Mozambique - 10/04/2012. Serikali ya Mozambique na Ureno zimekubaliana kudumisha ushirikiano wa karibu zaidi ili kweza kushirikiana kwa kila nyanja za kiuchumi na biashara.
Makubaliano hayo serikali ya Mozambique na Ureno yamekuja baada ya ziara ya waziri mkuu wa Ureno  Pedro Passos kufanya ziara nchini  Mozambique  na kubaliana kuangalia upya ni kwa jinsi gani mzozo wa bwawa la Cahora Bassa ambao ulikuwa haujatafutiwa ufumbuzi.
Mozambique ilikuwa koloni la Ureno kabla ya kupata uhuru mwaka 1975 chini ya chama cha FRELIMO.
na uhusiano kati ya nchi hizombili kupungua kwa muda mrefu.

Mtuhumiwa wa mauaji ya Norway adaiwa ni mzima wa akili.


Oslo, Norway - 10/04/2012. Wachunguzi wa afya ya akili  walio mfanyia  mtu aliye husika katika  mauaji ya kutisha yaliyo tokea nchini Norway mwaka 2011/ Julai/22 wametoa majibu kuhusu hali ya akili ya mshutumiwa huyo .
Anders Behring Breivik 33 ambaye aliwauwaa watu 77 na kutega mabomu ambayo yalileta maafa makubwa ameripotiwa na wachunguzi wa afya ya akili yakuwa akili yake haipo katika hali ya kufanya unyama na ni mzima.
Majibu kuhusu ali ya kiafya ya kiakili juu ya Breivek yamekuja baada ya uchunguzi zaidi kufanywa kuhusu afya yake.
Awali mtuhumiwa Anders Behring Breivik alidhaniwa ya kuwa anamatatizo ya akili, jambo ambalo lilifany wakili kufikilia ni kwa jinsi gani watashughurikia kesi ya muaaji huyo.

Iran yadai kuwakamata majasusi waliotaka kufanya mashambulizi hivi karibuni.


Tehran, Iran - 10/04/2012. Wizara ya usalama ya Iran imetangaza yakuwa imewakamata watu kadhaa na kufanikiwa kuvunja nguvu za majasusi ambao walikuwa wamepanga kufanya mashambulizi nchini humo hivo karibuni.
Kwa kujibu wa habari zinasema " baada ya kukamatwa kwa watu hao, ushahidi umeonekana ya kuwa kuna nchi za Ulaya Magharibi  Marekani na washiriki wake wanahuzika katika ujasusi huo.
Idadi ya siraha na mabomu na mitambo mingine ya kijeshi ilikamatwa wakati baada ya wapelelezi wa Iran kupata uhakika kamili."
Kufuatia kukamatwa kwa watu hao, serikali ya Iran imedai ya kuwa habari nyingine zitafuatia hivi karibuni ili kuthibitisha mpango huo wa majasusi.ulikuwa ni wa kweli.
Iran imekuwa inavutana na nchi za Magharibi, hasa katika swala  la utengenezaji nguvu za kinyuklia, ambapo Iran inadai ni haki yake kuwa na uwezo wa kutengeneza nguvu za nyuklia.

Sunday, April 8, 2012

Joyce Banda aapishwa kuwa rais wa Malawi.

Mamia waudhuria misa ya Pasaka Vatican City.

Vatican City, Vatican - 08/04/2012. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameongoza misa ya sikukuu ya Pasaka na kwa kuomba amani na utulivu kutawa nyoyo za binadamu.
Papa Benedikt XVI akiongoza misa alisema" tukiwa tunasherekea kufufuka kwa Yesu Kristu aliyeshinda mauti, tunaomba ufufuo wake ulete amani  kwenye maeneo yote duniani yanayo kabaliwa na vita na ukame.
Kuanzia nchi za Mashariki ya Kati, Syria, Izrael Palestina Irak na kwa wale wote walio kumbwa na matatizo ya vurugu katika bara la Afrika."
Papa Benedikt pia aliwatakiwa waumini wote duniani Pasaka njema yenye furaha na amani.
Siku ya leo Wakristu duniani kote wansherekea siku ambayo Yesu Kristu alifufuka baada ya kuhukumiwa na Pilato na baadaye kutundikwa msalabani ili maandiko yatimie.

Joyce Banda aapishwa kuwa rais wa Malawi.
Lilongwe, Malawi - 08/04/2012. Makamu wa rais wa Malawi ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo kufuatia kifo cha rais Bingu wa Mutharika  kilichotokea siku ya 05/04/2012.
Joyce Banda 61, atakuwa rais wa kwanza mwanamke kuchukua madaraka hayo ya juu ya kuongoza nchi  Malawi na katika ukanda wa Kusini na Mashariki ya Afriaka.
Rais Joyce Banda alisema haya baada ya kuapishwa "nitafanya kazi yangu kama inavyo sema katiba ya nchi na kuitumikia Malawi kwa moyo wangu wote, na napenda tuwe na matumaini mema na umoja, kwa imani naamini hakutakuwa na mwanya wa kulipizana visasi, na kwakuwa sisi ni taifa linalo muamini Mungu basi hatutashindwa kutimiza aliyo agiza."
Rais Banda alisisitiza utulivu hasa katika kipindi hiki cha malombelezi ya kuondokewa na aliye kuwa rais wa Malawi Bingu wa Mutharika.

Uingereza yapiga marufuku kuweka wazi sigara madukani.

London, Uingereza - 08/04/2012. Serikali ya Uingereza imepiga marufuku na kuagiza maduka yote nchini humo kuziba na kufunika sigara zilizopo madukani.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikalini zinasema "kwa kuziba na kufunika sigara zilizopo madukani kutasaidia kupunguza kishawishi cha kuvuta sigara na vilevile huenda tabia ya kuona sigara na kutaka kuvuta ikapungua."
hata hivyo baadi ya wafanyabiashara na raia wamesema "kitendo hicho hakita saidia kwani kila mvuta sigara anajua nini sigara gani anavuta."
Uamuzi huo wa serikali ya Uingereza kupiga marufuku kuweka sigara wazi madukani umekuja baada ya kampeni kubwa ya kupambana na magonjwa yanayo husiana na uvutaji wa sigara kuongezeka.

Friday, April 6, 2012

Jeshi la China latakiwa kupuuzia uvumi wa kisiasa.

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika afariki dunia.


Blantyre, Malawi - 06/04/2012. Rais wa Malawi amefariki dunia baada ya kuupata matatizo ya moyo siku ya Alhamisi 05 April wakati akiwa katika shughuri zake za kiofisi.
Bungu wa Mutharika 78 ambaye alichaguliwa kuiongoza Malawi mwaka 2004 na kuchaguliwa tena kwa mara ya pili mwaka 2009 kuwa rais wa  Malawi na mwaka 2011 kukumbwa na mvutano wa kisiasa na Uingereza hivi karibuni jambo ambalo lilisababisha uhusiano kati ya Malawi na Uingereza kudorola.

Watuareg wajitangazia uhuru ndani ya Mali.

Timbuktu, Mali - 06/04/2012. Kikundi la upinzani lililopo nchini Mali la Tuareg limetangaza kujitawala badaa ya kuchua eneo kubwa nchini Mali.
Kundi hili linalo julikana kama (MNLA)-The National Movement for the Liberation of Azawad ambalo lilifanikiwa kuchukua eneo kubwa nchini Mali, lili tangaza ya kuwa linataka lijulikane kama "Azawad."
Hata hivyo Umoja wa Afrika umepinga swala hilo na kuagiza kuwa jumjuiya ya kimataifa kutokubaliana na kundi hilo.
Nayo serikali ya Ufaransa imeunga mkono ombi la Umoja wa Afrika na kusema "Ufaransa haitaitambua ombi hilo la MNLA na Mali ni nchi moja na tunataka Mali kuwa nchi moja.

Mahakama ya Hague ya Uhollanzi yamtaka Saif al-Islaama Gaddafi. 

Hague, Uhollanzi - 06/04/2012.  Mahakama inayo shughulikia makosa ya jinai na kutetea haki za binadamu iliyopo Uhollanzi imetaia serikali ya Libya kumpeleka mtoto wa Muammar Gaddafi nchini Hollanzi.
Mahakama hiyo ya Hague ambayo ilitoa hati ya kukamatwa Saif al-Islaam Gaddafi ambaye yupo chini ya mikono ya serikali ya mpito ya Libya tangu alipo kamatwa  mwaka 2011 Novemba wakati akiwa katika harakati za kutoroka.
Naye mwanasheria anaye mtetea Saif al-Islaam Gaddafi alisema " tangu Saif kakamatwa amekuwa ananyanyaswa, kunyimwa haki zake na kufungiwa kwenye vyumba vya giza."
Serikali  ya Libya imekuwa ikivutana na mahakama ya Hague, kwa madai wanataka kesi dizi ya Saif al-Islaam Gaddafi  ifanyike nchi Libya.

Wakuba washerekea kwa mara ya kwanza sikukuu ya Ijumaa Kuu tangu mwaka 1959.

Havana, Kuba - 06/04/2012. Wanchi wa Kuba wamesherekea kwa mara ya kwanza siku ya kumbukumbu ya kuteswa kwa Yesu Kristu msalabani.
Siku ya Ijumaa Kuu siku ambayo haikuwa katika sikukuku za serikali ya Kuba kwa muda wa miaka mingi, ilisherekewa na waumini wa dini ya Kikristu wa Kuba, baada ya Papa Benedikt XVI kuiomba serikali ya kuitambua rasmi siku hiyo.
Ombi hilo la Papa limefuatia ombi la kwanza lililo fanywa na marehemu Papa John Paul II aliye iomba serikali ya Kuba kufanya siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu - Krismas kuwa siku ya mapumziko na kusherehekewa kitaifa.
Serikali ya Kuba ilipiga marufuku sikukuu za kidini mwaka 1959 baada ya kufanyika mapinduzi.


Jeshi la China latakiwa kupuuzia uvumi wa kisiasa.


Pyong Yang - China - 06/04/2012. Jeshi la China limewataka wanajeshi nchini humu kutilia maanani swala la ulinzi wa nchi na kuachana na uvumi ya kuwa kulikuwa kuna mpango wa kufanywa mapinduzi.
Habari hizi zimetolewa na gazeti la jeshi la China, kwa kuripoti " wanajeshi wa China wanatakiwa kuzuia na kulinda propaganda za aina yoyote, kwani zinaleta kelele zisizo na maana na hazitasaidia lolote kwa ni uvumi wa kisiasa."
Wanchi wa China wana tarajia kuona mabadiliko ya uongozi wa kisasa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Thursday, April 5, 2012

Rais wa Malawi alazwa hospitali.

Raia wa Urussi haukumiwa miaka 25 jela nchini Marekani.

New York, Marekani - 05/04/2012. Jaji wa mahakama katika jiji la New York amemuhukumu kwenda jela miaka 25 raia wa Urussi ambaye alikuwa mfanya biashara wa kuuza siraha.
Voktor Bout 44 ambaye alipiga ukelele kwa kusema " huu ni uongo" alikutwa na hatia ya kuhusika na njama za kuhatarisha maisha ya Wamarekani na kwa kutaka kuuza siraha kwa magaidi.
Pia inaaminika mtuhumiwa Viktor Bout, alihusika katika kuuza siraha nchi za Rwanda, Angola na Congo.
Hata hivyo upande wa utetezi wa Viktor Bout ulidai yakuwa mteja wao alikuwa akiuza ndege mbili za mizigo zanye thamani ya $5million.

Pakistani yataka ushahidi kamili kutoka na madai ya  Marekani.

Islamabad, Pakistan - 05/04/2012. Serikali ya Pakistani imeitaka serikali ya Marekani kutoa ushahidi kamili wa madai yakuwa raia wa Pakistan alihusika katika milipuko iliyotiokea nchini India 2008.
Habari kutoka ofisi ya mambo ya nje ya Pakistani zinasema "tungependa tupate ushahidi wa kutosha ili tuanze kufuata sheria badala ya kuongelea kwenye mitandao na njia tofauti.
Mohammad Saeed alisema " nipo naishi maisha yangu ya kila siku bila shida na kama kuna mtu ananihitaji basi tuwasiliane nipo sina shaka."
Madai hayo yamekuja baada ya serikali ya Marekani kutangaza kitita cha dola $10 million kwa mtu atakaye toa habari zitakazo fanya kukamatwa kwa Mohammad Saeed ambaye Marekani inasema alihusika katika milipuko ya ugaidi ya mwaka 2008 na kuu watu 166.

Rais wa Malawi alazwa hospitali.


Blantyre, Malawi - 05/04/2012. Rais wa Malawi amelazwa hopsitali baada ya kukutwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo.
Rais Bingu wa Mutarika 78 alianguka wakati akiwa katika shughuli zake za kiserikali.
Kwa mujibu wa habari kutoka ofodi ya rais zimasema " kumekuwa na mshituko mkubwa kwani nchini nzima kutokana na tukio hilo."
Malawi ni nchi ambayo imekumbwa na misukosuko ya kiuchumi kwa muda sasa na hasa pale mauaji ya watu 19 yalipo tokea mwaka 2011 na kusababisha nchi za Ulaya Magharibi kulaani kitendo hicho  na nyingine kupunguza misaada kwa kudai serikali ya Malawi ifanye mabadiriko haraka  iwezekanavyo.




Monday, April 2, 2012

Senegal yapata rais wa nne tangu kupata uhuru.

Miaka 30 yatimia tangu vita vya Falkland.

London, Uingereza - 02/04/2012. Miaka 30 imefikia leo tangu Uingereza kuvamia visiwa vya Falklands, ilikuling'o jeshi la Argentina lililo chukua kisiwa hicho.
Katika kuadhimisha kumbukumbu hiyo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alisema "leo ni siku ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha katika vita hivyo, na Uingereza itaendelea kuwalinda Wanafalkland hadi hapo watakapo amua wao wenyewe.
Naye rais wa Argentina Christina Fernandez alisema "kitendo cha Uingereza kuendelea kukishikilia kisiwa hicho ni kinyume cha sheria na lazima wakiachie kisiwa hicho ni cha Argentina."
Mvutano wa Argentina na Uingereza zimekuwa zikivutana nani anamiliki kisiwa hicha kwa muda sasa jambo ambalo halijapatiwa jibu.


Chama cha Aung San Kyi chashinda viti vya bunge. 


Myanmar. Naypyitaw - 02/04/2012. Chama cha mwana harakati wa mapinduzi ya kisiasa nchini Myanmar kimetapa ushindi mkubwa katika uchaguzi uliyo fanyika hivi karibuni.
Chama cha Aung San Kyi NLD-National League for Democrcy kilipata viti 44 katika uchaguzi huo.
Aung San Kyi alisema " huu ni mwanzo wa mageuzi nchini mwetu, vita bado vinaendelea ili kuleta haki na usawa, na tunamatumaini ya kuwa ushindi huu utaliwezesha bunge kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi."
Katika harakati za uchaguzi huo serikali ya Mynmar imedai ya kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na wasimamizi wa kimataifa waliruhusiwa kuangalia uchaguzi huo unakwenda kihalari.


Senegal yapata rais wa nne tangu kupata uhuru.


Dakar, Senegal - 02/04/2012. Wananch wa Senegal wameoata rais mpya, ambaye amepishwa wiki moja baada ya matikeo ya uchaguzi kutolewa.
Macky Sall 50, aliapishwa kuwa rais wa Senegal baada ya kumshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdullaye Wade katika uchaguzi uliofanyika mara ya pili baada ya uchaguzi wa kwanza kutotoa mshindi.
Macky Sall alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura asilimia 66% na Wade alipata asilimia 34%.


Serikali ya Syria yakubaliana na Koffi Annan.


Damascus. Syria - 02/04/2012. Serikali ya Syria imekubaliana na mpango wa amani uliopendekezwa na mwakilishi wa umoja wa mataifa Koffi Annan.
Rais wa Bashar al Assad, amekubaliana ya kuwa tarehe 10/April itakuwa siku ya kuanza mpango mzima wa kusimika muhimiri  amani uliyo pendekezwa.
Koffi Annan ambaye ni msimamizi wa kuleta amani nchini Syria alisema " lazima kamati ya ulinzi ya umoja wa Matifa ifikirie mpango wa kuandaa wajumbe ambao watakuwa na majukumu ya kusimamia na kuangalia hali ya usalama.
Mpango huo ambao  wa 10/April unatarajiwa kutoa ruhusa kuwepo kwa amani na jeshi la Syria litaanza kutoka katika miji ambayo ipo chini ya jeshi hili.

Tuesday, March 27, 2012

Papa Benedikt XVI awasili nchini Kuba.

Kenya yatangaza kuwa na mafuta katika ardhi yake.

Nairobi, Kenya - 27/03/2012. Serikali ya Kenya imetangaza kugunduliwa kwa mafuta nchini humo katika maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Turkana.
Rais Mwai Kibaki alisema" hii ni habari  jema kwani ni kwa mara ya kwanza Kenya inagundulika ya kuwa ina mafuta"
Ugunduzi wa mafuta hayo umefanywa na kampuni inayo julikana kama Tullo Oil ambayo pia imedai yakuwa mafuta yenye uboara kama haya ya Kenya  yamegunduliwa nchini Uganda.
Uchimbuzi wa mafuta hayo nchini Kenya unatarajiwa kwenda kina cha umbali wa mita 2,700 ifikapo mwezi wa Mei.


Papa Benedikt  XVI awasili nchini Kuba.


Havana, Kuba- 27/03/2012.  Kiongozi wa madhehebu ya Kikatoliki duniani amewasili nchini Kuba kwa ziara ya siku tatu nchini humo.
Papa Benedikt wa Kumi na Sita - XVI, aliwasili nchini Kuba baada ya kumaliza ziara yake nchini Mexico.
Rais wa Kuba Raul Castro katika kumkaribisha  Papa Benedikt alisema " Kuba inatambua umuhimu wa Kanisa Katiliki  nchini Kuba na Wakuba wapo pamoja na Kanisa katika kulinda haki za Wakuba na kwa kushirikiana na Kanisa Wakuba watailinda Kuba."
Papa Benedikt allsema " nawaomba wa Kristu wenzangu kumwamini Mungu na kupingana nakila aina ya njia za shetani kwani ndiyo njia pekee ya kushinda umasikini na ubaya wa ubinadamu."
Katika ziara hiyo Papa Benedikt anatarajiwa kukutana viongozi wa serikali ya Kuba ili kujadili hali halisi ya kiimani nchini humo.

Korea ya Kaskazini bado kitendawili kwa Marekani.


Seoul, Korea ya Kusini - 27/03.2012. Serikali ya Marekani imeitaka serikali ya Korea ya Kaskazini kuachana na mpango wake wa kuendeleza mradi wa kinyuklia.
Onyo ilo lilitolewa  baada ya rais wa Marekani,  Baraka Obama yupo   ziarani nchini Korea ya Kusini na ameuhduria kikao cha viongozi wa dunia ili kujadili udhibiti wa matumizi ya sirha za kinyuklia.
Rais Obama alisema "Korea ya kaskazini  lazima iachane na mradi wa kinyuklia kwani kitendo cha serikali ya Korea ya Kaskazini kuendelea na mpango wake wa kuendeleza  vitisho vya kinyuklia  kwa kujaribu mabomu havita saidia ila vina ifanya Korea ya Kaskazini kutengwa zaidi."
Serikali ya Korea ya Kaskazini imekuwa ikivutana na jumuiya ya kimataifa katika harakati zake za  kinyuklia kwa muda sasa baada ya mazungumzo kukwama miaka michache iliyo pita.

Iran bado yasisitiza yakuwa itajibu mashambulizi.

Tehran, Iran - 27/03/2012. Mmoja wa viongozi wa  ya Iran amedai ya kuwa kitendo chochote  cha kuishabulia Iran kitakuwa cha kujutiwa.
Ayatollah Seyyed Ahmad Khatami alisema " ikiwa Izrael au nchi yoyote kuishambulia Iran, basi wajuwe yakuwa majibu yetu Iran yatakuwa ya kuiwezesha dunia  kutambua ya kuwa tunachosema huwa tunatekeleza.2
"Kwani kumekuwa na vitisho vingi vya kuishambulia Iran, Izrael imekuwa  ikiishawishi jumuiya ya kimataifa kuamini ya kuwa Iran ni adui wa jamii, jambo ambalo si la kweli.
"Iran hajawahi kuishambulia nchi  yoyote na kitendo cha kuishamblia Iran kitakumbwa na majibu ambayo yatafanya jamii isituke na uenda ikawa fundisho kwa wale wote wanao taka kutumia nguvu kwa ajili ya manufaa yao."
Iran imekuwa ikishutumiwa na Mareakani na washiriki wake yakuwa inampango wa kutengeneza siraha za kinyuklia kinyume na sheria, jambo ambalo  Iran imekanusha vikali kwa kudai yakuwa mradi wake wa  nyuklia ni kwa ajili ya maendeleo ya kisayansi.

Thursday, March 22, 2012

Mswada wa Kofi Annan juu ya Syria wakubaliwa na Umoja wa Mataifa.

Mswada wa Kofi Annan juu ya Syria wakubaliwa na Umoja wa Mataifa.

New York, Marekani - 21/03/2012. Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imepitisha mswada ulio pendekezwa ili kuleta amani nchini Syria.
Mswaada huo ambao ulipendekezwa na aliye kuwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Kofi Annan
ambaye alipewa jukumu la kusuruhisha mgogoro wa kisiasa uliyopo nchini Syria, ambao umesababisha vurugu na vifo vingi nchini huko.
Mswaada huo ambao unazitaka pande zote mbili, serikali ya Syria na wapinzani kuweka siraha chini ili kutoa njia kwa misaada inayotakiwa kutolewa kwa watu walioathirika na vita na kila pande ikubali kumaliza mgogoro huu kwa kukaa chini ya meza na kuongea."
Mswaada huo pia ulikubaliwa na China na Urussi nchi ambazo hapo mwanzo zilipinga mswaaada uliopendekezwa kabla ya huu mpya uliotolewa na Kofi Annan.

Mwingereza aliyetekwa nyara nchini Somalia ahachiwa huru.

Mogadishu, Somalia - 21/03/2012. Raia wa Uingereza aliyekuwa ameshikiliwa na kundi la maharamia ameachiwa huru.
Judith Tebbut 57 alisema " nafurahi kuwa huru japo ninamajonzi kutokana na kifo cha mume wangu na nashukuru kupata fursa ya kuwa na familia yangu tena.
Nawakati wote nilipo kuwa chini ya maharamia hawakuni nyanyasa, na walikuwa wananiangalia kwa makini, na hasa nilipo umwa walitoa matibabu haraka."
Kundi lililo mteka nyara limedai yakuwa "kunamalipo ya pesa zilitolewa na ndipo wakaamua kumwachia huru Judith."
Judith Tebbutt ambaye alitekwa nyara katika mji wa Lamu ulipo kwenye pwani ya bahari Indi nchi Kenya mapema mwezi Semptemba 2011 wakati wakiwa  katika mapumzikoni nchini Kenya na mume wake kuuwawa wakati wa tukio la kutaka kuwateka nyara wote.
Ofisi ya mabo ya nje ya nchi Uingereza imethibitisha kuachiwa huru kwa Judith Tebbutt na kuhusu swala la kutolewa kiasi cha pesa, msemaji wa serikali alikanusha madai hayo na kusema "cha umuhimu kwa sasa ni kuhakikisha Judith anaelekea nyumbani kwani amechoka na anahitaji kuwa na mapumziko na kujiunga na familia yake.



Tuesday, March 20, 2012

Malkia wa Uingereza atimiza miaka 60 tangu kutawazwa rasmi kuwa Malkia.

Malkia wa Uingereza atimiza miaka 60 tangu kutawazwa rasmi kuwa Malkia. 


London,Uingereza - 20/03/2012. Malkia wa Uingereza amesherekea miaka 60 tangu kutawazwa rasmi kuchukua wadhifa huo.
Malkia Elizabeth II alisema " huu ni ukumbusho wa maisha yetu yanayo ambatana na historia ya nchi yetu ambayo kila mtu anahaki sawa na kuheshimina ni msingi wake mkuu.
Nipata bahati ya kushuhudia mambo memgi ya kihistori yakitokea, na nashukuru familia yangu kwa kuwa na mimi wakati wote kwa hali na mali, na najitolea kuitumikia nchi yangu na watu wake kwa sasa na miaka mingi ijayo."
Malkia Elizabeth wa Uingereza ni Malkia wa pili katika historia ya kifalme ya Uingereza kutimiza miaka 60 ya kuwa mtawala Malki kwa kufuata nyayo za Malkia Viktoria 1897. 

Mauaji yaliyofanywa na mwanajeshi wa Marekani yaundiwa kamati kuchunguzwa 
Washington, Marekani - 20/03/2013. Jeshi la serikali ya Marekani imepanga kuchunguza kiundani ili kutaka kufahamu kiini cha mauaji yaliyo fanywa na mmoja ya wanajeshi wa Kimarekani hivi karibuni nchini Afghanistani.
Gen Ajonh Allen alisema " kamati maalumu itaundwa ili kuchunguza kwa makini mauaji hayo na kutaka kujua kiundani ilikuwaje mshukiwa Staff Sgt. Robet Bale  alifanya mauaji hayo."
Mauaji hayo yaliyo fanywa na mwanajeshi huyo wa Marekani  nchini Afghanistan yameleta vichwa kuuma kwa serikali ya Marekani na kusababisha maamdamano nchini Afghanistan ya kutaka mwanajeshi huo ashitakiwe. 

Kiongozi wa Iran aonya nia ya kuishambulia Iran.

Tehran, Iran - 20/03/2012. Kiongozi mkuu wa serikali ya Iran, ametoa onyo ya kuwa ikiwa nchi yake itashambuliwa nayo serikali ya Iran bila kusita.
ayatollah Ali Khamenei aliseme " tutajibu shambuio lolote lile kwa kiasi tutakavyo shambuliwa na tutafanya hivi kwa kujilinda.
Hatutengenezi mabomu ya nyklia na hatuna mpango huo, na tusingependa kuona Marekani inafanya makosa hayo, kwa kuitishia Iran hakuta vunja Iran."
Kiongozi huyo wa Iran, aliyaongea hayo baada ya rais wa Marekani Baraka Obama, kutoa hotuba ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya wanachi wa Iran.
Katika hotuba hiyo rais Obama alisema "Iran imewawekea wananchi wake ukuta wa umeme ili wasiweze kusikika, kuona, kuongea kwa kutofuata haki za binadamu."

Urussi kuafikia mapendekezo ya Kofi Annan juu ya Syria.

Moscow, Urussi - 20/03/2012. Serikali ya Urussi imekubaliana na mpango wa amani uliopendekezwa na aliyekuwa katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa Kofi Annan.
Waziri wa mambo ya nje wa Urussi Sergie Lavrov alisema " mpango wa mapendekezo ya Kofi Annan, ili kuleta amani nchini Syria in mzuri na nimuhimu kutekelezwa kama alivyo alivyo pendekeza."
Matamko haya ya Urussi yamekuja wakati Kofi Annan amesha fanya mazungumzo mara mbili na rasi wa Syria Bashar al Assad ili kujadili mbinu za kuleta amani nchini Syria.



Saturday, March 17, 2012

Aliyehusika na mauaji ya Sobibor aaga dunia.

Hugo Chavez arudi nyumbani baada ya matibabu nchini Kuba

Karakas, Venezuela - 17/03/2012. Rais wa Venezuela amewasili nyumbani baada ya kumaliza matibabu ya kansa ambayo ilikuwa ina muathiri afya yake.
Rasi Hugo Chavez akiongea kutoa shukurani kwa wale wote walio mwombea na kuwa naye katika wakati mgumu wa ki afya   alisema "nimerudi nyumbani na nguvu mpya na nipo tayari kuongoza jahazi" 
Hugo Chavez alitolewa uvimbe wakati wamatibabu yake nchini Kuba.
Venezuela nchi ambayo inakalibia kufanya uchaguzi wa rais, Hugo Chavez anatarajiwa kugombea tena kiti cha urais wa Venezuela kwa mara nyingine tena.

Aliyehusika na mauaji ya Sobibor aaga dunia.

Berlin, Ujerumani - 17/03/2012. Askari wa mwisho aliyehusika katika mauji katika kambi ya Sobibor nchini Paland amefariki dunia.
John Demjanjuk 91 ambaye alikutwa na makosa ya kuhusika katika mauaji zaidi ya watu 167,000 wakati akiwa kama mlinzi kati ya mwaka 1942-43.
Habari za kuhusika kwa Demjanjuk kuhusika katika vifo hivyo zilipatikana katika kumbukumbu za mauaji ya Holokost ambayo yalifanya afunguliwe kesi na kukutwa na hatia baadaye alihukumiwa kwenda jela miaka mitano.
Hata hivyo Demjanjuk alikata rufaa na kuruhusiwa kuishi katika nyumba za wazee ambapo ndipo umauti ulimkuta.

Iran ya dai yakuwa Izrael haina uwezo wa kupigana vita zaidi ya wiki.

Tehran, Iran - 17/03/2012. Waziri wa mambo ya nje wa Iran ametahadharisha ya kuwa kitendo cha Izrael kushambulia maeneo yaliyo na mitambo ya kinyuklia ya Iran kitaleta matokeo ambayo hayatasemeka.
Ali Akbar Salehi alisema " kitendo cha Izrael kushabikia vita zidi ya haikisaidii kwani kama vita vikiianza basi Izrael haina uwezo wa kupigana zaid ya wiki moja, hivyo  kila kitisho kinachotolewa tunakichukulia kwa makini na hatuzani kama Izrael ni kitisho kwa Iran."
Iran imekuwa ikisukumwa kusimamisha mradi wake wa kinyuklia na  nchi za Magharibi, jambo ambalo Iran imekuwa ikidai ya kuwa ni haki kwa nchi hiyo kuendelea na mradi huo wa nguvu za kinyuklia kwani ni kwa ajili ya maendeleo ya kisayansi.

Serikali ya Syria yadai Saudi Arabia inawauzia siraha wapinzani.

Damascus, Syria - 17/03/2012. Serikali ya Syria imetangaza ya kuwa siraha zinazo tumiwa na wapinzani wa serikali zinatoka katika nchi za Kiarabu.
Waziri wa habari wa Syria Adnan Mahmoud alisema " Saudi Arabis na Katar ni nchi ambazo zipo mbele katika kuwasaidia wapinzani wa serikali ambo wengi ni maharamia wanatumia siraha hizo kinyume na sheria na hata kuwadhuru raia."
Maelezo hayo yamekuja baada ya bomu kulipuka katika jiji la Damascus na kuuwauwa zaidi ya watu 20 na kuwajeruhi watu wapatao 27.
Serikali ya Syria imekuwa ikidai ya kuwa tangu mwezi wa Machi 2011, Saudi Arabia na washiriki wake wamekuwa wakishiriki katika kuwapa siraha wapinzani wa serikali na kusababisha machafuko nchini Syria.

Wednesday, March 14, 2012

Mahakama ya Hague yamtia hatiani Thomas Lubanga.

Mahakama ya Hague yamtia hatiani Thomas Lubanga.

Hague, Netherlands - 14/03/2012. Mahakama inayo shughurikia  makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu iliyopo jijini Hague imemkuta na hataia aliyekuwa kiongozi wa Union of Congolese Patriots UPC Thomas Lubanga kwa kuwatumia vijana wadogo chini ya miaka 15 kama wanajeshi katika kundi lake.
Lubanga anatarajiwa kuhukumiwa siku za karibuni, kwa mujibu wa wanasheria waliofatilia kesi hii wanasema " huenda akahukumiwa kifungo cha maisha"
Thomas Lubanga, amekuwa kiongozi wa kwanza kukutwa na hatia tangu koti hiyo iliyopo Netherlands Hague kuanzishwa miaka 10 iliyo pita.

Ikulu ya rais wa Somalia yashambuliwa.

Mogadishu, Somalia - 14/03/2012. Watu watatu watano wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya ya bomu kulipuka kwenye Ikuru ya rais yaliyopo  mjini Mogadishu.
Kundi la Al-Shabab limekili kuhusika na "mlipuko huo na kuonya yakuwa milipuko  na mashambulizi mengine yatafuata."
Al Shabab walifukuzwa katika maeneo ya jiji la Mogadishu baadaya ya majeshi ya umoja wa Afrika kwa kusaidiana na majeshi ya Somalia kuzidi nguvu kundi la hilo.

Tuesday, March 13, 2012

Muamar Gaddafi alikuwa mtu wa karibu wa Nicolas Sarkoozy.

Ndizi zilizo iva ni muhimu kwa nguvu za kiume.

Kampala - Uganda - 13/03/2012.  Ndizi zilizo iva au kwa jina jingine "banana" zimetambulika kwa kuongeza nguvu zaa kiume mwilini.
Kama inavyo julikana ndizi zilizo iva zinakusaanya vitamini na vilishe  vya potassium, chuma zinc, cabohydrates,B6,A,C,B1,B2 na E ambavyo uhongeza nguvu.
Mataalaamu wa mambo ya  lishe Geoffrey Babaghirana alisema " ndizi zinasaidia kukuza nguvu za mwili hasa kwa wanaume na kuongeza uwezo wa kimapenzi kutokana na vilishe vinavyo patikana katika zao hilo na vile vile zinajenga ngozi ya mwili kutokana na kuwa na Vitamini C."
Zao la ndizi ni chakula kikuu katika jamii kubwa ya Waganda na sehemu za Tanzania zilizo pakana na Uganda.

Muamar Gaddafi alikuwa mtu wa karibu wa Nicolas Sarkoozy.

Paris, Ufaransa - 13/03/2012. Shirika moja linaloshughurikia uchunguzi wa maswala ya siasa na siri zake limetoa habari kuwa rais wa Libya Muaamar Gaddafi alichangia pesa ili kumsaidia rais wa Ufaransa.
Kwa mijibu wa shirika hilo zinasema "kiasi cha Euro 50 million zilitolewa kwa rais wa sasa wa Ufaransa Nicolas Sarkozy  na rais wa Libya Muammar Gaddafi kabla ya kuangushwa kutoka madarakani."
Hata hivyo rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy alikanusha madai hayo kwa kusema " nafikri mnajua ya kuwa Gaddafi alikuwa akiongea atakalo na hizi habari si za ukweli."
Uhusiano wa rais Sarkozy wa Ufaransa na rais Gaddafi wa Libya ulikuwa wa karibu saana na hasa pale iliposhuhudiwa rais Sarkozy kumwalika Muammar Gaddafi nchini Ufaransa baada ya uchaguzi mkuu wa Ufaransa.

Mashambulizi ya mabomu yatokea Nairobi.

Nairobi, Kenya - 13/03/2012. Mabomu yamelipuka hivi karibuni katika jiji la Nairobi na kusababisha vifo na watu wengine kujeruhiwa.
Msemaji wa polisi Charles Owinom alisema " kulikuwepo na milipuko tofauti ambayo imesababisha vifo vya watu wanne na watu wapatao 40 wamejeruhiwa."
Jeshi la Polisi nchini Kenya limeilaumu kundi la Al-Shabab kwa kuhusika na mashambulizi na kuhaidi ya kuwa mashambulizi hayo hayata tikisa taifa la Kenya.
Mashambuulizi hayo yaliyofanyika hivi karibuni ni mrorongo wa mashambulizi ambayo yamefuatia yale yaliyo tokea mwishoni mwa mwaka  jana na kusababisha maafa kwa jamii.

Wednesday, March 7, 2012

Machifu watanagaza serikali yao nchini Libya.

Iran yakubalia kuendelea mazungumzo juu ya haja na mipangoo ya kinyulia.

Viena, Austria - 07/03/2012. Shirika linalo shughulikia maswala ya  kinyuklia limetangaza ya kuwa mazungumzo yanayo husu swala la Iran na nguvu za kinyuklia huenda yakaanza karibuni.
Marekani, Fransi, Britain, China, Urussi na Ujerumani zimekubali kuanza mazungumzo ambayo yalikuwa yamesimamishwa kutokana na kutokuelewana kati ya nchini hizo na Iran.
Rais wa Marekani Baraka Obama alisema " hii ni faida kwa kila mtu, kwani kutatua swali hili kiamani ni jambo la maana."
Wakati huo huo, serikali ya Iran imetoa ruhusa kwa wakaguzi wa maswala ya kinyuklia wa kimataifa kutembelea eno la kambi ya jeshi ambao linazaniwa kuwa na mitambo ya kinyuklia.
Marekani na waashiriki wake wamekuwa wakishuku ya kuwa Iran inampango wa kutengeneza sirha za kunyukia, jambo ambalo Iran imekataa ya kuwa inampango huo.


Machifu watanagaza serikali yao nchini Libya.
Benghazi, Libya - 07/03/2012. Serikali ya mpito ya Libya imetangaza kupinga kitendo cha viongozi wa Mashiriki ya Benghazi kutangaza kujitawala na kuunda serikali yao.
Kiongozi wa serikali ya mpito Mustafa Abdel Jalil alisema " tutalinda muungano na Libya ni moja, hatupo tayari kuigawa nchi.
"Ningependa kuwatahadharisha ya kuwa wawe waangalifu na wafuasi wa Muamar Gaddafi na serikali itatumia kila nguvu zilizopo kulinda Libya na inashangaza ya kuwa baadhi ya nchi za Kiarabu zimeounga mkono uamuzi huo na nisingependa kuzitaja."
Libya ilizaliwa mwaka 1959 -63 baada ya kuungana kwa majimbo ya kichifu ya Cyrenaica, Tripolitania na Fezzan.


Aliyefanya mauaji nchini Norway afunguliwa kesi ya uhaini namauaji. 
Olso, Norway - 07/03/2012.  Serikali ya Norway imemfungulia mashitaka ya kesi ya uhaini na mauaji kwa raia wanchi hiyo ambaye aliyafanya na kuisitua dunia nzima.
 Anders Behring Breivik 33 amefunguliwa kesi hiyo, baada ya mauaji aliyo yafanya kwa kuua watu 77 kwa kuwapiga risasi katika kituo Utoeya na kuhuusika na kutega mabumu katika jiji la Olso.
Mwanasheria wa serikali Svein Holden  alisema " Anders amefanya makosa ya kihaini ambayo ni ya kihistoria katika nchi yetu."
Kwa mujibu wa habari zilizopo zinasema huenda Anders Behring Breivik akahukumiwa kwenda jela miaka 30 ingawa hapo awali alionekana na ubovu wa akili.


Mwakilishi wa umoja wa Maataifa awasili nchini Syria.
Bab Amr, Syria - 07/03/2012. Mwakillishi wa Umoja wa Mataifa katika kushughulikia haki za binadamu amewasili nchini Syria na kutembelea maeneo yaliyo athirika na mapambano.
Valerie Amos alitembelea Bar Amr baada ya serikali ya  Syria kuhakikisha yakuwa hali ya usalama wake ulikuwa umekamilika.
Waziri wa mambo ya nje wa Syia Walid Muallem alimweleza ya kuwa serikali ya Syria inatoa huduma za chakula n madawa kwa wale wote walio athirika na mashambulizi hayo.
Valerie Amos aliwasili nchini Syria baada ya kukubaliwa kutembelea maeneo yaliyoathirika na vita kati ya majeshi ya serikali na yale yanayo pinga serikali ya Syria.

Sunday, March 4, 2012

Vladmir Putin ashinda uchaguzi wa urais.

Vladmir Putin ashinda uchaguzi wa urais.

Mosccow, Urusi - 04/03/2012. Matokeo ya uchaguzi nchini Urusi yamempa ushindi mkubwa waziri mkuu wa Urusi kwa asilimia kubwa kuliko wapinzani wake.
Vladmir Putin ameshinda uchaguzi huuo kwa zaidi ya asilimia 60% na anayemfuata kwa ushindi amepata 17%.
Huku machozi yakimtoka mbele ya wanachama na watu wapatao 100,000 walio kuwepo kwenye makao makuu ya chama United Russia Vladmir Putin alisema "tumeshinda kama tulivyo haidi na ni ushindi kwa wale wote waitakiayo Urusi mema."
Vladmir Putin alihutubia mkutano huo baada ya mtokeo ya uchaguzi kuonyesha ya kuwa ameshinda uchaguzzi huo kwa asilimia kubwa.


Baraka Obama ataoa onyo kwa serikali ya Iran. 
Washington, Marekani - 04/02/2012. Rais wa Marekani ameoinya Iran kuachana na mpango wake kinyuklia au hatasita kutumia nguvu za kijeshi.
Rais Baraka Obama alisema "viongozi wa Iran lazima watambue hili, itabidi kutumia nguvu za kijeshi ikiwa mbinu zote za kisiasa kuisimamisha Iran kuendelea na mpango wake wa kinyuklia.
Ningeomba Izrael wawe na subira ili jitihada za kidilpomasia kufanya kazi yake, ikiwemo vikwazo vya kiuchumi ambavyo nafikiria vitafanikiwa na swaala la mazungumzo ya kivita tusiliongelee kwa sasa."
Hata hivyo serikali ya Iran imekuwa ikipinga ya kuwa haina nia ya kutengeneza siraha za kinyuklia na kuonya ya kuwa ikiwa kuna shambulizi lolote litafanyika nchini humo , basi Iran itajibu mashambulizi hayo kwa nguvu zote.


Izrael ianuwezo wake wa kujiamualia kuhusu Iran.
Tel Aviv, Izrael - 04/03/2012. Waziri wa mambo ya nje wa Izrael amehaidi yakuwa Izrael itamua niwakati gani kufanya mashambulizi nchi Iran bila kujali washiriki wake.
 Avigdor Lieberman akiongea alisema "kweli Marekani ni nchi yenye nguvu kijeshi na mshiriki wetu mkuu wa karibu lakini Izrael ni nchi iliyo huru na inauamuzi wake yenyewe.
"Na uamuzi juu ya mpango wa kuisimamisha Iran isiendele na nguvu za kinyuklia ni uamuzi utakao faywa na Izrael."
Waziri Lieberman aliyasema hayo wakati wakati waziri mkuu wa Izrael Benyamin Netanyahu akiwa njiani kwenda kuonana na rais wa Marekani Baraka Obama, na swala la nyuklia Iran litakuwa na kipao mbele.


China kuongeza matumizi ya kijeshi.
Beijing, China - 04/03/2012. Serikali ya China imetangaza kuongeza matumizi ya kijeshi ili kuweza kupata uwezo sawa katika kujenga uchumi na ulinzi.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema " serikali ya China imesha panga kuongeza matumizi ya kijeshi kufikia asilimia 11.2%."
China imehaidi kuweka swala la ulinzi mbele na halitaharibu mipango mingine ya kiuchumi kwani fedha
 hizo zitatumika kati mafunzo hya kijeshi kwa ajili ya wanajeshi wa China.