Sunday, December 22, 2013

Mahakama ya Uingereza yatupilia mbali kesi ya mwanasiasa wa Libya.

Mahakama ya Uingereza yatupilia mbali kesi ya mwanasiasa wa Libya.


Tripol, Libya -22/12/2013.  Mahakama  jijini London imetupilia mbali kesi ya mmoja wa kiongozi waliosaidia kuung'oa utawala wa Muammar Gaddafi 2011.

Akitoa hukumu kabla ya kutupilia mbali kesi ya Belhaj imedai Jaji  Simon alisema, " kwa kuangalia mwenendo mzima wa kesi hii, matendo mengi yalitendeka Malasyia, Thailand and  Libya na ambapo ni  nje ya nchi na hivyo hayahusiki na Uingereza."

Akiongeaa baada ya  hukumu kutolewa Belhaj  alisema " Maelezo ninavyo fahamu ni kuwa ikiwa kesi hii itaendelea, wanadai kuwa itawaaibisha Marekani, navilevile itahatarisha usalama wa taifa la Uingereza."

" Lakini hata hivyo kwa kupitia mwanasheria wangu tutapambana hadi tupate ushindi na kwani haki itatendeka mwisho wa siku."

Abdul - Hakim Belhaj,ambaye kwa sasa amekuwa mmoja wa viongozi wa siasa nchi Libya, ambaye amemeushitaki uongozi wa juu wa ofisi ya mambo ya nje wa Uingereza na mkuu wa MI6, Sir Mark Allen  kwa kosa la kumkamata kwa nguvu na kumpeleka  Libya wakati wa utawala wa Gaddafi na kuteswa.

Kesi ya kuwakamata watu kwa nguvu na kuwapekeka katika maeneo ya mateso, zimekuwa zikiiandama serikali ya Uingereza, na hata baadhi ya majaji kudai kuwa sheria ilivujwa na wakuu wa usalama wa Uingereza katika kufanya vitendo hivyo.

Mkwe wa Bin Osama Bin Laden aongezewa mashitaka.

New York,Marekani - 22/12/2013. Mahakama jijini New  York katika kitongoji cha Manhattan, imemuongezea mashitaka mawili zaidi aliyekuwa mkwe wa mkuu wa kundi la Al Qaeda Osama Bin Laden.

Suleiman Abu Ghaith, ameongezewa mashitaka ya  kusaidia kimali na kutoa habari katika kundi la Al Qaeda kuweza kufanya mashambulizi yake nchini  Marekani ya Sept 11 2001.

Suleiman Abu Gaith ambaye ni mzaliwa wa Kuwait alikutwa hapo awali na kosa baada ya kuongea maneno yakuunga mkono mashambulizi ya Sept 11. kwa kusema " tunafuraha kuona wapiganaji wa Mijaidini wameweza kushambulia nchi Marekani kwa uwezo wa Mungu na mapema dunia itashuhudia kushambuliwa kwa miradi ya Marekani na Waizrael."

Mashambuzi ya Sept, 11-2001 nchini Marekani yalisababisha vifo vya watu 3000, na watu kadhaa kuumia na mali nyingi kuharibiwa baada ndege zilizo kuwa zimetekwa na magaidi wa kundi la Al Qaeda kufanya mashambulizi Trade Centre New York, Pentagon na Pennsylvania.

Suleiman Abu Gaith anatarajiwa kufikishwa mahakamani kusikiza kesi zake Februri 3, 2014.

Friday, December 20, 2013

Rais Vladmir Putin aonyesha huruma yake. 
 

Moscow, Urusi -20/12/2013. Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa msamaha kwa aliyekuwa bilionea ambaye alikuwa amefungwa kwa makosa ya rushwa na kukiuka matumizi ya usambazaji wa pesa wa nchi ya Urusi.
 
Mikhail Khodorkovsky, ambaye amekaa jela miaka 10, baada ya kuhukumiwa kwenda jela mwaka 2003 aliachiwa huru leo kutoka katika gereza lililopo katika mji wa Karelia km 1,000 toka jiji la Moscow, baada ya rais Putin kutoa msamaha kutokana na sababu za kibinadamu na kiutu.
 
Akithibitisha kuachiwa na kuwasili Ujerumani, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Hans-Dietrich Genscher amesema " Mikhail Khodorkovsky amewasili katika jiji la Berlin kwakutumia ndege binafsi na mimi ndo nimemchukua toka kiwanja cha ndege."
 
Kuachiwa kwa Khodorkovsky kumekuja baada ya jitihada za Kansela  Waujerumani Angela Markel kukubalika na rais Putini ambapo kila walipo kutana aliomba serikali ya Urusi kumwachia Mikhail Khodorkosky.
 
 
Edward Snowden azidi kuziumbua Marekani na Uingereza.
 
 
London Uingereza - 20/12/2013. Sakata la shirila la kijasusi la Uingereza  na mshirikiwa wake Marekani kugundulika kuwa walikuwa wanachunguza na kusikiliza mazungumzo na mawasiliano ya simu na mtandao yamefichuliwa kwa mara nyingine tena.
 
Magazeti ya The Guardian Uingereza, The New York Time Marekani  na Der Spiegal la Ujerumani yameandika zaidi ya  majina 1000 ya watu wambao walikuwa wakuchunguzwa, kufuatiliwa nyendo zao kimtandao na kusikilizwa simu zao na  mashirika ya kijasusi ya NSA ya Marekani na GCHQ ya Uingereza  kinyume cha sharia za kimataifa.
 
Magazeti hayo yameandika kuwa "NSA na GCHQ wamechunguza nyendo za viongozi umoja wa Ulaya, mashirika ya haki za binadamu, waziri mkuu wa Izrael na pia zaidi ya nchi 60  hasa viongozi wa Afrika na familia zao, na pia  shughuli zinazo endeshwa na Umoja wa Mataifa na viongozi wake."
 
Kutolewa kwa ripoti hizi mpya ambazo chanzo chake ni raia wa Marekani Edward Snowden ambaye alikuwa mfanyakazi wa NSA na  kwa sasa yupo ukimbizini nchini Urusi, kumekuja baada ya ile kashfa ya kuwa mashirika hayo kwa pamoja yalikuwa yanashirikiana kusiliza mazungumzo ya  Kansela wa Ujerumani Angela Markel na kuleta mtafaruku wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.
 
 
 Chama tawala Afrika ya Kusini njia panda na washirika wake.
 
Pretoria, Afrika ya Kusini - 20/12/2013. Moja ya chama kikuu  cha wafanyakazi nchini Afrika ya Kusni kimetangaza kutounga mkono chama tawaza cha ANC - (African National Congress) wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 2014. 
 
NUMSA ambacho ni chama cha wafanyakazi wa viwanda vya vyuma,  ambacho kinawanachama zaidi ya 3,00,000, kimetoa azimio hilo wakati wa mkutano wa wanchama hao uliyofanyika hvi karibuni jijini Johannesburg.
 
Kiongozi wa chama hicho Irvin Jim  alisema  "NUMSA inajitoa katika kuunga mkono ANC, kwani chama cha ANC kimekuwa hakifanyi jitihada ya kupambana na rushwa na kupunguza umasikini na ufukara kwa wanachi wake na pia kukiuka ilani ya chama."
 
NUMSA imekuwa bega kwa bega na ANC tangu mwaka 1994, na hivi miaka ya karibuni imekuwa ikivutana na ANC kwa kudai ya kuwa chama cha ANC hakitekelezi kazi zake vizuri na kuwa kinatizama sana upande wa uchumi huria ambao haunufaishi watu walio wengi nchi Afrika ya Kusni.
 
ANC imekuwa na wakati mgumu katika sera zake kukuza uchumi chini Afrika ya Kusini, kutoka na na msukumo nguvu uchumi wa kuleta mabadiliko kuruhusu kuwepo na uchumi huria, jambo ambalo vyama vingi vya wafanyakazi vimekuwa vikiupinga mfumo huo.
 
 
Jela maisha ukiwa shoga nchini Uganda.
 
 
Kampala, Uganda - 20/12/2013. Bunge la Uganda limepitisha musuada ambao utakuwa wa kifungo cha maisha kwa mashoga wa kiume na wakike katika kura zilizo pigwa bungeni humo leo.
 
Uamuzi wa bunge la Uganda kupigia kura ya ndiyo ya kupitisha adhabu ya kukaa jela maisha, imekuja maada ya adhabu ya awali ya kunyongwa ambayo ilipingwa vikali na wana harakati wa kimataifa wa kutete haki za mashoga.
 
Msemaji wa bunge la Uganda amesema "Ushoga  ulikuwa ni haramu tangu enzi za serikali ya kikoloni nchini Uganda na kama tukiachia tabia hii itatualibia jamii nzima ya Waganda."
 
Sheria ya kuukataza  ushoga nchini Uganda  ilipitishwa kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 2009 ambapo spika wa bunge Rebeka Kadaga alisema "kupitishwa kwa sheria ya kupinga ushoga ni zawadi nzuri ya Krismasi kwa Waganda."
 
Wabunge wa Uganda wamekuwa wakidai yakuwa kanisa la Kievanjilisti la asili ya kuutoka Marekani limekuwa likiunga mkono ushoga na linakampeni ya kuusambaza ushaoga barani Afrika, madai ambayo wakuu wa kanisa hilo kutoka Marekani walikanusha.
 
Hata hivyo musuada huo utakuwa sheria baada ya rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museni kusaini kuwa sheria.
 
 
Baraka Obama aonya kuhusu mapigano nchini Sudani Kusini.
 
Juba, Sudani ya Kusini - 20/12/1213. Rais wa Marekani amezitaka pande zote zinazo pigana nchini Sudani Kusini kusimamisha mapigano haraka iwezekenavyo.
 
Baraka Obama alionya kwa kusema kuwa " Inabidi pande zote zinazo pigana nchi Sudani ya Kusini kucha mara moja vita, kwani vinaweza kuleta maafa makubwa kwa jamii na hatimayake kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe."
 
" Kitendo cha kutumia siraha ili kuweza kupata nguvu za kisiasa ndani ya nchi ni kitendo kibaya, na kila upande lazima wasikilize busara za kimataifa." Alimalizia rais Obama.
 
Wakati amani nchini Sudani ya Kusini imevurugika, mwanajehi wa umoja wa Mataifa kutoka nchi Indi amefariki dunia na mmoja kujeruhiwa, baada ya kushambuliwa ya wapiganaji wanao muunga mkono mpinzani wa serikali ya  ambaye alikuwa makamu wa rais Riek Machar kwa  kushambulia ngome ya makazi ya wafanyakazi wa umoja wa mataifa katika mji wa Bor.
 
Hadi kufikia sasa, zaidi ya watu 500 wamesha potea maisha yao wakiwemo wanajeshi 100, tangu mapambano yalipo anza, baada ya serikali ya rais Salva Kiir kudai ya kuwa imegundua mbinu za kutaka kuipindua serikali, zilizo kuwa zimepangwa na makamu wa rais Riek Machar, ambaye mmpaka sasa ajulikaani mahaali alipo.
 
 
Rwanda kupeleka majeshi yake Afrika ya Kati.
 

Kigali, Rwanda - 20/12/2013.Serikali ya Rwanda imekubali ombi la umoja wa Afrika kupeleka wanajeshi wake katika nchi ya Afrika ya Kati ili kusaidia kurudisha amani.

Akithibitisha hayo, kwa kutukia mtandao wa twiter, waziri wa mambo ya nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo aliandika " Rwanda iliombwa kuchangia wanajeshi nchini Afrika ya Kati, na wanajeshi wa Rwanda wapo katika matayarisho kuwasili jiji Bangui mapema iwezekanavyo"

Uamuzi wa Umoja wa Afrika kuomba msaada kwa jeshi la Rwanda umekuja baada ya ya hali ya amani katika nchi ya Afrika ya Kati kuwa mbaya zaidi, ambapo imefikia kuwa ugomvi wa kidini, kati ya  kundi linalo julikana kama Anti-Balaka la Wakristu kuanza kushabuliana na kundi la  Kiislaam la Seleka.

Kuchafuka kwa amani katika nchi ya Afrika ya Kati, kumesababisha zaidi ya watu 6,00,000 kukimbia makazi yao na huku kati yao 2,00,000 wakiokea jiji Bangui.

Wednesday, December 18, 2013

Angela Markel kuonngoza Ujerumani kwa mara ya tatu.
 
 
Berin, Ujerumani - 18/12/2013. Angela Markel 59, ameapishwa tena kwa mara ya tatu kuwa Kasela wa Ujerumani na kupewa madaraka ya kuiongoza nchi hiyo ambayo ni uti wa mgongo katika jumuiya wa nchi wanachama wa muungano wa Ulaya.
Kuapishwa kwa Angela Markel kumekuja baada  ya kufikia makubaliano ya chama chake cha CDU  na chama chenye mrengo wa kati kushoto cha SPD ambapo kwa pamoja wataunda serikali ya muungano itakayo iongoza Ujerumani.
 
Angel Markel amekuwa kiongozi wa kwanza kushinda uchakuzi nakuwa kansela tangu vita vya pili vya dunia chini ya chama chake cha CDU ( Christian Democratic Union).
 
Kufuatia kuapishwa kwa Angela Markel kuwa  Kansela wa Ujerumani, wanchi wa Ujerumani wanatongezewa kima cha chini cha mshahara  kama ahaadi ambazo zili aidiwa wakati wa kampeni.
 
  
Baada ya mapinduzi kushindwa hali ya hatari yatangazwa chini Sudani Kusini.
 
Juba, Sudani ya Kusini - 18/12/2013. Milio ya risasi imekuwa ikisika katika jiji la Juba na wanajeshi wanao muunga mkono rais wa sasa Sudani ya Kusini Salva Kiir kuvamia makazi ya makamu wa rais wa nchi hiyo ambaye anasadikiwa kuwa kiongozi wa kutaka kupindua serikali ya Kiir.
 
 Hadi kufikia sasa  watu  zaidi ya 500 waliopoteza maisha kutokana na mashabulizi ya kukusudiwa ya kuaangusha serikali ya rais Kiir na watu  wengine zaidi ya 20,000 kukimbilia katika eneo lenye makazi ya  ofisi za Umoja wa matafa nchi Sudani ya Kusini.
 
Kufuatia jaribio la kuipindua serikali, makamu wa rais Riek Machar ameshutumiwa kuwa muhusika mkuu baada ya kufukuzwa kazi na rais Kiir na baadhi ya watu kukamatwa na kupigwa marufuku matembezi ya usiku hadi hapo hali itakapo kuwa shwari.
 
Riek Machar alitangaza kuwa anataka kugombea urais wa wakati wa uchaguzi wa urais wa mwaka 2015, na alitoa kauli ya " nchi aiwezi kutawaliwa na udikteta wa utawala wa mtu mmoja."na bado hajakamtwa wala alipo hapajulikani.
 
Sudani ya Kusini imekuwa na msuguano wa kisiasa wa ndani tangu kupata uhuru wake toka  Sudan 2011.
 
Jela miaka minne na bakora juu.
 
Riyadh, Saudi Arabia - 18/13/2013. Mwanaharakati nchi Saudi Arabia amehukumiwa kupigwa viboko 300 na kifungo cha miaka 4 kwa baada ya kukutwa na hatia ya kupinga sharia zilizo wekwa na serikali ya  ufalme wa nchi hiyo.
 
Omar al Saed 24, ambaye kesi yake ilisikilizwa katika mahakama ya ndani na kukataliwa kuwa na mwanasheria wa kumtete  nabaadaye  kukutwa na kosa la kuikosoa serikali ya  kifalme ya Saudi Arabia kwa kukiuka  haki za binadamu na
 
Saudi Arabi ni moja ya nchi tano ambazo zimekuwa zikishutumiwa na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnest International kwa kukiuka haki za binadamu. 
 
 
Urusi yazidi kutanua nguvu za mabawa yake
 
 
Moscow, Urusi - 18/12/2013. Serikali ya Urusi na serikali ya Ukraini  zimekubaliana kibiashara na kiuchumi, baada ya viongozi wa nchi hizo mbili kukutana jiji Moscow.

Rais wa Urusi Vladmir Putin na rais wa UkrainiVictor Yanukovich walikubaliana kushirikiana kwa ukaribu kati ya nchi hizo katika masuala ya kibiashara, kiuchumi na kisiasa, ambapo Urusi ilikubali kushusha bei ya gesi na mafuta kwa nchi ya Ukraini na kutoa kiasi cha $ dola za Kimarekani 15 billion kwa Ukraini ili iliweze kujenga uchumi wa nchi yake.

Akiongezea baada ya makubaliano hayo rais Putini alisema "makubaliano ya leo ni ya hiyari kati ya nchi hizi mbili na Urusi itachangia pia kwa kiasi kikubwa katika masuala ya kiulinzi nchi Ukraini"

Makubaliano hayo yamekuja wakati wanachi wa Ukraini wakiwa wamegawanyika,  baaadhi yao kutaka nchi yao ijihusishe zaidi na nchi za jumuiya ya muunganao wa Ulaya (EU), na wa wengingene wakitaka nchi hiyo kuwa karibu na Urusi, jambo ambalo limesababisha maandamano makubwa katika jiji la Kiev na kwenye baadhi ya mikoa nchini humo.

Kufuatia makubaliano hayo kati ya Urusi na Ukraini, viongozi wa vyama vya upinzani nchi Ukraini wamedai yakuwa kitendo cha rais Yanukovich kukubaliana na Urusi ni kuvunja nia ya nchi hiyo kuwa mwanachama wa nchi za muungano wa umoja wa Ulaya,  ambao baadhi ya Waukraini wanahisi kutawarahisishia kuwa karibu na nchi hizo za umoja wa Ulaya.

Sunday, December 15, 2013

Nelson Rolihlahla Mandela apumzishwa kwenya makao yake ya milele.

Nelson Rolihlahla Mandela apumzishwa kwenya makao yake ya milele.




Qunu, Umthatha,  15/12/2013. Nelson Rolilhalha Mandela - Madiba kiongozi na rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini huru amepumzishwa kwa amani katika makao yake ya milele kwenye kijiji alicho kulia na kucheza wakati wa udogo na ujana wake.

Kijiji cha  Qunu, kijiji ambacho Nelson Mandela amelazwa na  huku  misa ya kumuaga ilifanyika kwa muda wa masaa mawili,wakati ndugu wa karibu, jamaa, machifu wa ukoo wa Nelson Mandela, viongozi tofauti kutoka sehemu mbalimbali dunia, na marafiki zake wakaribu walishuhudia kupumzishwa kwa Madiba.

Nelson Rolihlahla Mandela 95, kabla ya kushushwa kwenye makao yake ya  milele, aliaagwa kwa kupigiwa mizinga 21 ikiwa ni ishara ya kumuaga kama kiongozi na rais wa nchi.


Na kwa sasa Nelson Rolihlalha Mandela - Madiba hatupo naye kimwili, ila kiroho tupo naye na mishumaa 95 iliyo washwa ikiwa ni ishara ya kuwa miaka 95 aliyo ishi bado tupo naye daima, Amin.

Amba Kahle Utata, Umkhulu, Nelson Rolihlahla Mandela - Madiba.


Friday, December 13, 2013

Mazungumzo ya Irani na nyuklia yaingia dosari.

Tehran, Iran 13/12/201. Iran imesimamisha mazungumzo ya kinyuklia na nchi  sita kubwa duniani baada ya  Marekani kuiwekea vikwazo Iran.

"Umuzi wa Marekani kuyaongeza makampuni 19 ya kutoka Iran katika vikwazo vya kibiashara,kumeelezwa na Tehran kama ni ujumbe unao onyesha kuwa  juhudi za mazingumzo ya Iran na mpango wake wa kujadili maendeleo yake ya kinyuklia ni bure." Alisema Abbas Araghchi ambaye ni  makamu wa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran.
 
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Marekani Jay Carney  amesema kuwa "kitendo cha kuwekewa vikwazo makampuni 19 ya  Iran hakikuvunja mkataba wa Novemba 24"

Mazungumo kati ya nchi sita, China, Uingereza, Fransa, Germani, Urusi na Marekani kuitaka Iran kuachana na mpango wake wa kuendelea kuzalisha  nguvu za kinyuklia ulikuwa umesha fikia katika kipindi cha kukubaliana, baada ya mazungumzo ya Novemba 24, ambapo Iran na nchi sita ziliafikiana kimsingi kufikia makubaliano.

Rufaa ya Victoire Ngabire yakataliwa.

Kigali, Rwanda - 13/12/2013. Maakama ya rufaa jiji Kigali, imetupilia mbali rufaa ya maombi ya aliyekuwa kiongozi wa chama cha upinzani nchini humo Victorie Ngabire.

Kufuatia kukataliwa kwa rufaa hiyo, Victoire Ngabire ataendelea kutumika kifungo cha miaka 15 jela, baada ya kukutwa na hatia na makama jiji Kigali kwa kosa la kuchonganisha makabila, na vilevile kueneza chiki za mauaji ya kimbari yaliyo fanyika  Rwanda 1994.

VictoireNgabire mama mwenye watoto watatu na mume, alikamatwa mwaka mwezi Oktoba 2010, kwa kosa la kudai ya kuwa pia wale "Watutsi walio husika katika kuua wa Hutu nao washitakiwe."

1994, dunia nzima ilishikwa na mstuko, baada ya mauaji ya watu zaidi ya 800,000 kuuwawa, kutokana na visa vya kikabila kati ya  Watutsi na Wahutu, na Wahutu walio wengi waliuwawa.

Victoire Ngabire 45 ambaye alirudi nchi Rwanda kama kiongozi wa chama cha  Nguvu za Muungano wa Demokrasia Unified Democratic Force (UDF) baada ya kukaa nje ya nchi kwa muda wa miaka 16.

Kim Jong Un ammgeuka mjomba wake.

Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 13/12/2013. Mjomba wa kiongozi na aliyekuwa mkuu wa pili katika uongozi wa jeshi na madaraka yote wa Korea ya Kaskazini amenyongwa kwa mujibu wa shirika la habari KCNA la nchi hiyo.

"Jang Song Thaek, ambaye anadaiwa kwa kukutwa na hatia ya kutaka kupindua serikali, kula rushwa na kuvunja miiko ya serikali." Liliripoti shirika hilo la habari la Korea ya Kaskazini KCNA.

Kunyongwa kwa Jang Song Thaek, kumetamfsiliwa kuwa ni moja ya myumbo wa kiungozi, kwani inaaminika kuwa " Jang Sing Thaek ndiye aliye simamia na kumsaidia  kiongozi wa sasa Kim Jong Un hadi kuweza kuwa imara katika uongozi aliyo nao sasa.

Jang Song Thaek, alikuwa ni mtu wa karibu wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini marehemu Kim Jong Il ambaye ni baba wa kiongozi wa sasa Kim Jong Un.

M23 na serikali ya DRC Kinshasa wasaini mkataba wa amani.



Kinshasa, DRC - 13/12/2013. Serikali ya DRC imetiliana sahii makubaliano ya kusimamisha mapigano na kundi la waasi M23 linalo pingana na serikali ya Kinshasa.

Mkataba huo wa makubaliano ambao umewekwa sahii jijini Nairobi Kenya, na kukubaliana  yakuwa wale wapiganaji wa M23 wataaungana na  wanajeshi wa jeshi la serikali na vilevile kusalimisha siraha na vifaa vyote vya kivita ambavyo vilikuwa vinatumika na kundi la M23.

Akisisitiza baada ya kutiliana sahii ya amani, msemaji wa serikali ya DRC, Lambert Mende amesema "katika mkataba huu ni kwamba wale wote walio husika katika uvunjaji wa hali za binadamu, na kutakiwa kujibu mashitaka kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kulinda haki za binandamu hawata husishwa na wala kupewa msamahaa kama tulivyo kubaliana."

M23, ni kundi la wapiganaji wa kijeshi, ambao wanaaminika wengi wao wanaasili ya Kitutsi,  na wamekuwa napigana na serikali ya Kinshasa, kwa madai ya kuwa  serikali ya DRC haiwatendei haki.

Wednesday, December 11, 2013

Wezi wavunja nyumba ya Askofu wakati yupo kwenye misa ya Nelson Mandela.

Papa Fransis achaguliwa kuwa mtu muhimu wa mwaka 2013.

Vacan City, Vatican - 11/12/2013. Papa Fransis amechaguliwa kuwa mtu muhimu duniani na  gazeti la Time na kuwashinda Edward Snowden na rais wa  Syria Bashar Al Assad.

Akieleza uamuzi wa kumchagua Papa Fransis kuwa mtu muhimu katika msimu wa mwaka 2013, mhariri mkuu Nancy Gibbs amesema "Katika kipindi cha miaka 1200 Papa Fransis ni kiongozi wa kwanza kutoka Amerika kuongoza kanisa kubwa duniani na ameonyesha uwezo wake na hasa katika kubadirisha mwenendo  wa kanisa Katoliki."

Papa Fransis  amekuwa kiongozi wa tatu wa kanisa Katoliki kuteuliwa kwa kufuata nyayo za Papa John XXII mwaka 1962 na Papa John Paul II 1994.


Wezi wavunja nyumba ya Askofu wakati yupo kwenye misa ya Nelson Mandela.
 
Cape Town, Afrika ya Kusini - 11/12/2013. Wezi wamevunja na kuingia kwenye nyumba ya Askofu Mkuu Mstaafu  wa Kanisa la Anglikani  jiji Cape Town.

Tukio hilo limetokea wakati Askofu Desmond Tutu 82 na mkewe walipokuwa wamekwenda jijini Johannesburg kuhuria misa ya kumkumbuka ya marehemu  rais Nelson Mandel ambaye alikuwa rais wa kwanza  mweusi wa Afrika ya Kusini tangu kuangushwa kwa utawala wa ubaguzi wa rang


Mwangalizi na msimamizi wa Askofu Tutu Roger Friedman alisema" nyumba ya Askofu imevunjwa na mpaka sasa hatuwezi kusema ni vitu kiasi gani vimeibiwa "

Hii itakuwa ni mara pili kuvunjwa kwa  nyumba kwani mara ya kwanza ilivunjwa Agosti 7/2013, ambapo wezi waliingia nakuchukua baadhi ya vitu huku Askofu Desmond Tutu akiwa amelala na mkewe ndani.

Askofu Desmond Tutu 82 ni mshindi wa Nobel ya Amani ya mwaka 1984.

Matumizi ya Bangi yahalishwa nchini Uruguay.

Mwili wa Nelson Rolihlahla Mandela kuonyeshwa kwa mara ya mwisho.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 11/12/2013.Familia, ndugu na jamaa pia  maelfu ya watu wamajipanga mstari ili kumuaga na kumona kwa mara ya mwisho aliyekuwa rais wa kwanza mweusi waAfrika ya Kusini Nelson Mandela katika jengo  serikali - Union Building lililopo jijini Pretoria.

Mwili wa marehemu Nelson Mandela ulikuwa umewekwa wazi kwa wanchi, wazalendo na watu kutoka mataifa tofauti ili kutoa heshima zao za mwisho. Mwili wa Nelson Mandela utaonyeshwa kwa watu kwa muda wa siku tatu.

Kufuatia kitendo cha watu kuruhusiwa kuona mwili wa  Nelson Mandela kwa mara ya mwisho, watu kadhaa waliishiwa nguvu huku wakilia na wakati huohuo wengine kuzimia.

Mwili wa hayati rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela utapelekwa kupumzishwa Qunu katika mji wa Umtatha.

Matumizi ya Bangi yahalishwa nchini Uruguay.


Montevideo, Uruguay, - 11/12/2013. Bunge la Senete la Uruguay limepitisha kwa kura nyingi uamuzi wa zao la bangi kuwa halali. Kura ambazo 16 kati ya 29 ziliunga mkono uhalali wa  kulima bangi na kuwa inatumika bila kuwa kosa la jinai nchini humo.

Kufuatia kukubali kwa wabunge wa senete, rais wa Uruguay Jose Mujic atasahini muswaaada huo kuwa sheria.

Mmoja  kati ya wabunge waliopiga kura ya kukubali uhalali za zao la bangi Seneta Roberto Conde amesema " uamuzi wa bunge kupitisha  muswaada huu, ni kwa sababu ambazo hazikuweza kuzuilika.

Bangi ni moja ya zao amblo linatumika na watu wakila lika, na inaeleweka kuwa inamadhara madogo sana katika jamii."

Hata hivyo shirika la kupambana na madawa ya kulevya limepinga vikali kitendo cha bunge kukubali kuruhusu matumizi ya bangi kwa kusema "nikinyume na makubaliano ya mwaka 1961 ambapo Uruguay ni mwanachama."

Uruguay imingia katika  kundi la nchi kama  Netherlands na Spain ambazo sheria za matumizi ya bangi zinruhusu matumizi ya zao hilo kwa matumizi ya mtu binafsi.




Tuesday, December 10, 2013

Maelfu wasema Amba Kalhe Utata Nelson Rolihlahla Mandela.

Nelson Rolihlahla Mandela aombewa  na maelfu.



Johannesburg, Afrika ya Kusini - 10/12/2013. Viongozi kutoka nchi 91, marais, wakuu wa nchi,  na maelfu ya watu, wameudhuria ibada ya maombolezi ya kumwaaga aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela ambaye alifariki  ya tarehe 05/12/2013 huku akiwa na umri wa miaka 95.


Viongozi mbali mbali walitoa hotuba zao za mwisho kwa  Nelson  Mandela ikiwa ni ishara ya kukubali kwao kuwa yote aliyo simamia Nelson Mandela yalikuwa ni ya haki na kukubalika katika harakati zake za kupigania kuung'oa utawala wa kibaguzi wa Makaburu.

Akiongea  rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma alisema "Nelson  Mandela - Madiba alikuwa mtu wa aina yake na hakuna mwingine atakaye kuwa kama Madiba."



Naye rais wa Marekani Baraka Obama akihutubia katika siku ya kumuuga Nelson Mandela alisema" Hatuta mwona tena Nelson Mandela.
Mandela ulikuwa mtu wa watu na tunakushukuru kwa kila jambo ulilofanya, ulikuwa unampenda kila mtu, na wala ukujali rangi yake au wapi alitokea na umetuachia kumbukumbu kubwa na tumejifunza mengi toka kwako."

Ili kuthibitisha aliyo simamia Nelson Mandela ya kumpendana na maadui zetu na ndiyo njia pekee ya kufikia kuwepo na amani  kwa maasimu wa kubwa wa kisiasa wa kihistoria ni pale rais wa Baraka Obama alipo peana mkono na rais wa Kuba Raul Castro wakati alipo wasili kwenye jukwaa la tayari kwa kuanza misa rasmi ya maombelezi ya rais wa kwanza Mwafrika mweusi Nelson Mandela.

Wajane, Winnie Mandela na Graca Machel wakiwa wamekaa kwa huzuni katika misa ya maombelezi ya mume wao Nelson Mandela na picha ya chini wakipusiana kabla ya kukaa tayari kwa misa.

Nelson Mandela hata wakati wa hatupo naye kimwili, lakini  anauwezo wa kuwakutanisha viongozi wenye mitazam tofauti katika jamii.

Mwili wa Neslon Mandela utawekwa katika jengo kuu la serikali - Union Bulding kwa siku tatu, kwa ajili ya watu kumwaga kwa mara  mwisho kabla ya kuhifadhiwa katika kijiji alichokulia Qunu siku ya tarehe 15/12/2013.

Saturday, December 7, 2013

Nelson Rolihlahla Mandela atutoka na hatupo naye kimwili.

Afrika yampoteza shujaa mwingine.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 07/12/2013. Ulimwengu mzima upo katika  maombelezi ya kifo cha  Nelson Mandela 95, kiongozi mashuhuri aliyeingia katika madaftari ya historia ya karne ya 20.



Enzi za ujana wa Nelson Rolihlahla Mandela.

 Serikali duniani kote  zimeshushwa bendere za nchi zao nusu milingoti ikiwa ni ishara ya  maombolezi  baada ya rais  wa kwanza Mwanaafrika Nelson Rolihlahla  Mandela - Madiba kutangazwa kuwa ameaaga dunia.  

Kufuatia kifo chake, viongozi wa kimataifa wameelezea masikitiko yao na kusifu mchango wake wakati wa uhai wake na jinsi alivyo weza kupambana na ubaguzi wa rangi na mtu aliyekuwa akipigania haki, uhuru na usawa.
Nelson Mandela baada ya kuachiwa huru akiwa na mkewe Winnie Madikizela Mandela.


Ahaahaaa "Rolihlahla, usiwaambie kitu, tuonyeshe vitendo"Hapa anaoekana hayati Nelson Mandela akiwa na mkewe Winnie Mandela  siku kadhaa baada ya Nelson Mandela kutoka gelezani ambapo alikaa jela miaka 27 na Winnie Mandela alikuwa imara katika hali na mali kuendeleza harakati za kumuunga mumewe huku akitunza watoto wao.

Wakiongea kwa nyakati tofati.

Rais Barack Obama wa Marekani amesema kwa kufariki dunia Nelson Mandela " ulimwengu umempoteza mmojawapo wa binaadam mwenye ushawishi mkubwa kabisa, mwenye moyo wa kijasiri kupita kiasi na mwenye imani kupita kiasi. 

Akinukuu  aliyosema wakati  Mandela anahukumiwa  kwende jela maisha, rais Obama 
"Madiba alipofikishwa mahakamani mwaka 1964  alisema nimepigana dhidi ya utawala wa kimabavu wa waupe na nimepigana dhidi ya utawala wa kimabavu wa watu weusi. napiganiamaadili ya kuwepo jamii huru na ya kidemokrasia ambapo watu wote wataishi pamoja kwa furaha na kuwa na fursa sawa  na pia ni  maadili ninayotaraji kuyaendeleza maishani mwangu na ikihitajika, basi pi niko tayari kufa kwa ajili ya maadili hayo."

Naye rais wa Brazil Dilma Roussel amemtaja Nelson Mandela kuwa  "mtu mashuhuri mwenye ushawishi mkubwa kabisa wa karne ya 20 na  ameongoza utaratibu wa maendeleo katika historia ya binaadam kwa busara na mapenzi ,  utaratibu uliopelekea kumalizika kwa ubaguzi wa rangi na mtengano nchini Afrika ya Kusini"
Nelson Mandela akiwa jela katika kisiwa cha Roben kilichopo katika bahari ya Atlantiki karibu na jiji la Cape Town - Afrika ya Kusini.


Malkia Eliabeth wa pili wa Uingereza pia ameelezea masikito yake kutokana na kifo cha Nelson Mandela akisifu juhudi za Nelson Mandela nakusema  "Juhudi zake ndizo zilizopelekea kuwepo Afrika kusini yenye amani hii leo."
Baadi ya viongozi ambao walikuwa na urafiki wa karibu na Nelson Mandela.


Enzi za uhai wao, Nelson Mandela akiwa na rais wa kwanza wa Tanzania Julius Nyerere ambaye serikali yake ilichangia kwa kiasi kikubwa  katika  vita ya kuuong'oa utawala wa  serikali ya Kikaburu ya  Afrika ya Kusini.


"Comredi karibu" haya ndo maeneo aliyosema Hayati Nelson Mandela wakati akimkaribisha rais wa Kuba Fidel Castro.

Nelson Mandela alikuwa mtu wa shukurani, hapa anaonekana akiwa na kiongozi wa Libya hayati Muammar Gaddafi wakati alipo kwenda kumwona japo dunia ilimtenga Gaddafi.


Hadi kukutwa na umauti, Nelson Mandela na Robert Mugabe urafiki wao ulikuwa waukaribu, hapa wanaonekana wakibadirishana mawazo wakati viongozi hawa walipo kutana, enzi za uhai wa Nelson Mandela.
Kila mpigania  haki za binadamu mabdela alikuwa rafiki ya Mandela. Hapa Hayati Yasir Arafat na Hayati Nelson Mandela enzi za uhahi wao walipokutana.

Hayati Nelson Mandela  alizaliwa July 18/ 1918 na kufariki Desemba 05/ 2013 anatarajiwa kupunzishwa 15/12/2013, hii ni kwamujibu wa serikali ya Afrika ya Kusini.