Thursday, July 3, 2014

Kundi la Al Qaeda lawa na mbinu mpya za kupitisha mabomu viwanja vya ndege.

Polisi wa watawanya waandamanaji nchini Afrika ya Kusini.



Pretoria, Afrika ya Kusini - 03/07/2014. Polisi wamepambana na wafanyakazi na wanachama chama cha wafanyakazi wa viwanda vya chuma NUMSA ambao walikuwa wanadai ongezeko la posho.

 NUMSA chama ambacho kinawafanyakazi wanachama  waapatao 220,000 kiliitisha mgomo kwa wafanyakazi wake ilikiwa ni njia ya kushirikiza ombi lao lakutaka kuongezewa posho toka asilimia 12 hadi 15.

Msemaji wa polisi, Ronel Otto alisema "maandamano hayo yanafuata mgomo ambao umechukuliwa na wanachama wa NUMSA, na pia  ilibidi polisi kutumia mbinu za kiulinzi ili kutuliza ghasia baada ya baadhi ya wafanyakazi kuzuia mlango mkuu wa kuingia katika kampuni ya kufua umeme ya Eskom iliyopo Midupi Kaskazini mwa jimbo la Limpompo."

Maandamano na mgomo wa wafanyakazi wa NUMSA  umelalamikiwa na viongozi wa mashirika yanayo husika na zualishaji wa chuma kwa kudai kuwa lika siku Rand 300 millioni zinapotea na hivyo kuwataka wafanyakazi warudi kazini.

Jonh McCain aja na sera mpya ya Irak na Syria.



Arizona, Marekani - 03/07/2014. Mbunge wa Seneti la Marekani, ameshinikiza na kusisitiza kuwa inatakiwa kuwapa siraha wapiganaji wa wanaopingana na serikali ya Syria ambapo pia watatumia siraha hizo kupambana  na na kundi la ISIL lililopo nchini Irak.

Seneta John McCain aliyasema hayo wakati alipo kutana kiongozi wa mambo ya kigeni wa kundi linalo pingana na serikali ya Syria wakati alipo kuwa  ziarani nchini Uturuki.

Akiongea Seneta McCain alisema " kutokuwepo na niya ya kuwasaidia kisiraha wapinzani wa serikali ya Syria, kunahatarisha maslahi ya Marekani."

" Napia hili kundi la ISIL lililopo Irak lisipo kabiriwa haraka litakuwa ni hatari kwa katika eneo zima la Mashariki ya Kati jambo ambalo litasababisha hali ya usalama na ulinzi kwa Marekani na mafao yake kuwa katika hali tete."

Akiongezea Seneto John McCain alisema kuwa "Iraq na Syria zimekuwa nchi ambazo ni hatari na zitakuwa hatari zaidi hapo baadaye katika manufaa ya Wamarekani kama hazitazibitiwa mapema."

Hata hivyo habari kutoka ndani ya kundi hilo la ISIL zimesema kuwa
"wapiganaji wake wengi walikuwa wakipata mafunzo kwa kipindi cha miaka miwili nchi Jordan, ili kuwan
tayari kupambana na serikali ya Syria, lakini waliamua kubadirika toka kwenye mwelekeo huo."

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyo endelea nchini Syria na Irak, vimekuwa vikiwapa vicha kuuma viongozi na wataalamu wa maswala ya ulinzi na usalama, kwani kuna baadhi ya raia kutoka nchi za Magharibi  wapo katika makundi hayo ya kivita na inahofiwa huenda raia hao wakaja kuwa tishio pindipo watakapo rudi makwao.

Kundi la Al Qaeda lawa na mbinu mpya za kupitisha mabomu viwanja vya ndege.

London, Uingereza - 03/07/2014. Serikali ya Uingereza imeweka hali ya tahadhari katika viwanja vyake vya ndege, baada ya kutahadharishwa kuwa kuna uwezekano wa mabomu kupita.

Habari kutoka ofisi ya waziri wa usafiri zinasema kuwa "ulinzi umeimarishwa baaada ya serikali ya Marekani kuitaadharisha Uingereza kuwa mabomu ambayo si chuma cha kuonekana kwa mitambo yameaandaliwa kupita katika viwanja vya Uingereza kuelekea Marekani kwa ajili ya mashambulizi."

Hali ya tahadhari katika viwanja vya ndege nchini Uingereza imekuja, baada ya kuaminika kuwa "raia wa Ulaya ndiyo watakao beba mabomu hayo, kwani hawaitaji visa kuingia nchin Marekani."

Kuthibitisha ukweli huo wa kuwepo kwa aina hiyo ya mabomu, maafisa usalama wa Marekani wamesema kuwa "kundi la Al-Qaeda ambalo linamakao nchini Yemen na Syria ndilo linalo husika katika kutengeneza mabomu hayo."

Akizungumzia kutokana na habari hizi, makamu wa waziri mkuu wa Uingereza Nick Clegg ameonya kuwa Uingereza imejiaandaa kikamilifu katika swala la ulinzi, na hasa katika viwanja vyake vyote.

Kufuatia tahadhari hiyo, abiria wameonekana wakisubiri kwa muda zaidi ili kuweza kukaguliwa  katika viwanja vyote vya ndege nchini humo.



Monday, June 30, 2014

Waasi wa Irak wajitangazia utawala.

Wataalamu wasema Oscar Pistorius ni mzima wa akili.

Pretoria, Afrika ya Kusini - 30/06/2014. Ripoti ya upimaji wa akili ya mwanariadha  maafuru wa Afrika ya Kusini  imetolewa na kukabidhiwa jaji anaye sikiliza kesi hiyo tayari kwa kesi kuendelea.


Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na wataalamu wa kupima akili na utashi, wamesema kuwa " Pitorius ni mzima wa akili."

Akiongea kuhusu ripoti hiyo, jaji anaye sikiliza kesi hiyo, Jaji  Thokozile Masipa amesema, " nimepata ripoti hii leo Jumatatu hasubuhi na bado sijaisoma."

Jaji Masipa, alitoa ruksa kupimwa akili kwa Pistorius, baada ya mwanasheria wake, kudai kuwa mteja wake anamatatizo ya akili kutokana na historia ya maisha yake.

Ripoti hiyo ambayo ina muhusu mwanariadha Osca Pistorius 27,  ambaye alipelekwa kwenye nyumba ya kuangalia mwenendo wa tabia na akili yake ili ilikuweza kufahamu kuwa wakati alipo kuwa akifanya kitendo cha mauaji alikuwa hali ya uzima wa akili au la.
 
Oscar Pistorius akikutwa na hatia ya kuua, huenda hakaukumiwa kwende jela si chini ya miaka 15 au kifungo cha maiasha.

Waasi wa Irak wajitangazia utawala.


Diyala , Irak - 30/06/2014. Kundi linalo julikana kama ISIS lilipo nchini Irak, limetangaza kuwa maeneo ambayo imefanikiwa kuyatwaa yatabadilishwa majina na kuitwa kwa ujumla  kama  majimbo ya nchi za Kiislaam.

Likitoa uthibitisho wa kubadilishwa kwa majina haya, kundi hili lilisema " kuanzia sasa, maeneo ya Diyala  na  jombo la Aleppo yataitwa  kwa pamoja nchi ya Kiislaam na yataongozwa Kiislaam."

Pia kundi hilo liliongeza kuwa " Abu Bakar al Baghdad, ndiye kiongozi wa kundi hilo kwenye eneo hilo zima."
Kundi la ISIS limetangaza hivyo, baada ya miaka kumi kupita tangu jeshi la Marekani na washiriki wake kuiangusha  serikali ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Saadam Hussein.

Kundi hilo limeshutumiwa hivi karibuni kwa kufanya mauaji ya kinyama ambayo yamelaaniwa na mashirika ya haki za binadamu na ya kutetea haki za binadamu, kwa kusema kuwa lazima hatua za kisheria zichukuliwe mapema ili kuhakikisha kuwa mauaji kama hayo yasitokee tena.

Kufuatia kuwa na nguvu kwa kundi hilo ISIS na kufanikiwa kutwaa maeneo inayo yashikilia, waziri mkuu wa Irak Nour al Marik kuomba msaada katika kupambana na kundi hilo, ambalo kwa sasa jeshi la serikali ya Irak linapambana na kundi hilo katika jimbo la Tikrit, ambapo ndiko aliko zaliwa Saadam Hussein.  

Friday, June 13, 2014

Mashindano ya kombe la dunia yaanza kwa vishindo.

Mashindano ya kombe la dunia yaanza kwa vishindo.

Sao Paulo, Brazil - 13/06/2014. Mashindano ya kugombea kombe la dunia kwa mchezo wa soka  yameeanza rasmi huku timu wenyeji kiondoka na ushindi.

Wenyeji Brazili ilibidi wafanye kazi ya ziaada na huku bahati kuwaangukia kwa kushinda magoli matutu kwa moja zidi ya timu ya Croatia katika mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo. Magoli ya Brazili yalifungwa na Neymar aliye pachika mabao mawili, moja la penati na Oscar alifunga bao la tatu na Croatia walipata goli baada ya beki wa Brazil Marcelo kujifunga katika harakati za kuokoa mpira usiingie golini

Mashindano ya kombe la dunia yanazishirikisha timu 32 kutoka mabara yote yaliyopo duniani na yanafanyika kwa mara ya ishirini tangu kuanzishwa mwaka 1930.

Mashindano ya kombe la dunia kwa mchezo wa kandanda yanatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa na huku baadhi ya washabiki wakitoa matumanini kwa timu mwenyeji Brazil kuibuka na ushindi kwa kubeba kombe hilo tena kwa mara ya sita.


Sunday, June 8, 2014

Viongozi wa Wapalestina na Izrael wakutana Vatican.

 Viongozi wa Wapalestina na Izrael wakutana Vatican.

Vatican City, Vatican - 08/06/2014. Papa Fransis ameongoza ibada ya misa ya amani ambayo iliudhuriwa na viongozi wa juu wa Izrael na Palestina.

Ibada hiyo ambayo ilikuwa na nia ya kuombea amani kati ya Waizrael na Wapalestina, ilidhuriwa na rais wa Izrael Shimon Peres na kiongozi wa Wapalestina Mahamoud Abbas.

Kukutana huko kwa viongozi wa juuu wa jijini Vatican  kumekuja baada ya mwaliko uliofanywa na Papa Fransis baadanya kufanya ziara katika  eneo la nchi za Mashariki ya Kati za Izreal na maeneo ya Wapalestina ilikutafuta njiaa ya kuleta amani katika eneo hilo.

Akiongea baada ya ibada ya misa na kukutana kwa viongozi hao wa kuu wa Wapalestina na Waizrael, Padri Pierbattista Pizzaballa ambaye ni mkuu wa kitengo kinacho simamia masuala ya amani ya Mashariki ya Kati alisema "hatuwezi jidanganya kuwa amani ya Mashariki ya Kati italetwa bila mazungumzo, na ndoyo maaana Papa Fransis ameweka mkakati katika suala hili, na kwa sara na maombi basi mafanikiyo yataonekana."

Viongozi hao wa Palesestina, Izrael na ongozi wa Vatican kwa pamoja walikaa na kuongea ili kutafuta suruhu ya amani katika eneo zima la Mashariki ya kati na kuwa na ujumbe kuwa eneo la Ardhi takatifu lazima liwe na amani.

Hatimaye  Wamisri wapata rais.

Kairo, Misri - 08/06/2014.  Aliyekuwa  wa majeshi ya Misri, Abdel Fattah al Sisi ameapishwa rasmi kuwa rais wa nchi ya M,isri mwaka mmoja baada ya kuongoza mapinduzi ya kuipindua serikali ya kiongozi wa Muslim Brotherhoods Mohammed Mosri

Akiongea mara baada ya kuapishwa kuwa rias Abdel Fattah Sisi alisema" mafanikio ya Wamisri ya po wazi, hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunajenga Misri bora ambayo inaweza zalisha makate, yenye kufuata sheria na haki za binadamu ambazo  zinafuata haki"

Hata hivyo wapinzani wa Sisi, wameeleza wasiwasi wao kuwa "huenda rais  huyu mpya wa Misri akafuata nyayo Hosni Mubaraka"

Rais Abdel  Fattah al Sisi aliapishwa kwenye jengo ambalo aliapishiwa rais  aliyempindua Mohammed Mosri na kuudhuliwa na badhi ya viongozi wa serikali na huku watu wanao mmuunga mkono wakishangilia kwa kupeperusha bendera ya Misri.

Abdel Fattah al Sisi amekuwa rais wa nne kutoka kuwa mkuu wa jeshi hadi kushika nafasi ya uongozi wa juu wa  kiti cha urais.

Uongozi wa Kifalme nchi Uhispania wakubwa na mthiani.

Madrid, Uhispania - 08/06/2014. Mamia ya watu wameaandamana katika jiji la Madrid kwa madai ya kuupinga utawala wa kifalme siku chache baada ya mfalme wa sasa wa Uhispania Juan Carlos 74 kutangaza kuwa anamwachia  kiti cha ufalme mwanae wa kiume Prince Filipe
.
 Maandamano hayo ambayo yalikuwa na nia ya kutaka Uhispania kuwa na serikali ya Jamuhuri, badala ya sasa ambayo inatawaliwa na mfalme.

Mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo ana amabaye pia ni mkuu wa chama cha Pademos Pablo Igresias amesema " tunataka suala hili likabidhiwe kwa wananchi, tunaka kura ya maoni ipigwe, na siyo tatizo kama Waispania wakipewa nafasi ya kuamua kwa aajili ya maisha ya baadae ya kila Mspania."

Maandamano hayo yamefanyika ikiwa zimebakia siku 11 kabla ya  mwana wa mfalme Prince Filipe kuapishwa rasmi ili kukabidhiwa kiti cha ufalme wa Uispania.

Uongozi wa kifalme unaungwa na chama kilichopo madarakani  na baadhi ya vyama vikuu vya upinzani,  na Prince Filipe anatarajiwa kukukabidhiwa kiti cha Ufalme Juni 19- 2014 ambapo sherehe hiyo itakuwa ikiendena na shughuli za kibunge katika siku hiyo ya kuapishwa kwa mwana huyo wa mfalme.




Thursday, June 5, 2014

Wakuu wa G7 vichwa kuuma juu ya Urusi.

Rais Bashar al Assad ashinda tena uchaguzi mkuu nchini Syria.

Damascus, Syria - 05/06/2014. Matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais  uliyofanyika 03/06/2014 nchi  Syria umempa ushindi mkuu rais wa sasa wa Syria kwa asilimia kubwa.

Bashar al Assad ambaye ndiye rais wa sasa wa Syria na ambaye alikuwa akigombea kiti hicho kwa mara nyingine ameshida uchaguzi huo kwa mara ya tatu kwa asilimia zaidi ya 90 kutoka kwa wapiga kura milioni 10.

 Hata hivyo matokeo ya ushindi  wa kura wa rais Bashar al Assad, umepingwa vikali na serikali za Marekani na washiriki wake kwa kudai ya kuwa " Uchaguzi huo haukuwa wa maana na hakuwa wa halali na ni uchaguzi sifuri."

Hata hivyo Iran ambayo ni mshiriki mkuu wa serikali ya Syria imesema
"kitendo cha kuchaguliwa tena rais  Bashar Hafez al Assad ni pigo kwa wapinzani wa watu wa  Syria, na hasa ni kitendo cha aibu kwa Marekani na washiriki wake kwani hawapo kwa aajili faida ya watu wa Syria bali wanacho angalia ni maslahi yao"

Syria imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya wale wanao unga mkono serikali ya rais Bashar al Assad na wapinzania wake jambo ambalo limesababisha maelfu ya Wasyria kukimbia nje ya  nchi na mamia kupoteza maisha yao.

Rais Bashar al Assad, ameshinda uchaguzi huo ambao ulikuwa wa vyama vingi na anatarajiwa kushika utawala wa kiti hicho cha urais kwa muda wa miaka saba ijayo.

Rais  Vladmir Putini ataka ushahidi uonyeshwe hazarani.

Paris, Ufaransa - 05/06/2014. Rais wa Urusi amezitaka Marekani na washiriki wake kuonyesha ushaidi kwa jumuiya ya kimataifa kuwa majeshi ya Urusi yapo nchi Ukraine.

Rais Vladmir Putin aliyasema hayo wakati alipo kuwa akiongea na waandishi wahabari jijini Paris, ambapo amewasili nchini Ufaransa kwa ajili ya sherehe za kumbukumbu ya miaka 70 ya vita vya pili vya dunia.

Akiongea rais Putini alisema " ni jambo la kushangaza, ikiwa kuna wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine mbona mpaka sasa hawajaonyesha ushahidi"

" Dunia nzima inakumbuka wakati Marekani ilipo toa ushaidi kuwa Irak ina siraha za sumu, kuwa kuonyesha, malori na chupa zilizo kuwa na unga aina ya poda ambazo walidai sumu na ni za Saddam Hussein, na kwa kigezo hicho wakavamia Irak na baadaye Saddam Hussein alinyongwa, muda haukupita ikajulikana kuwa Irak haikuwa na siraha za sumu."

" Na ushahidi kuhusu Irak, ulitolewa mbele ya kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa, hivyo napenda kukumbusha kuwa, kuongea ni vyepesi na kutoa ushaidi wa huhakika ni hali nyingine."
 
Akisisitiza rais Putini alisema "baada ya mapinduzi ya serikali nchini Ukraine Februari mwaka huu,  Urusi iliunga mkono na kusimamia kura ya maoni ya jimbo Cremia kutaka kujiunga na Urusi, kwani hii niuamuzi wa watu wa Cremia na hii ipo katika kifungu cha 1 cha katiba ya Umoja wa mataifa."

Maelezo hayo ya rais  Putin yamekuja baada ya Marekani na washirika wake kudai kuwa Urusi ndiyo chanzo cha vurugu zinazo endelea nchi Ukraine.

Hata hivyo, rais Putin alisema kuwa yupo tiyari kukutana na kiongozi yoyote kuongea naye kuhusu  masuala ya kimataifa ikiwemo ya Ukraine wakati atakapo kuwa nchini Ufaransa, na kama rais wa Marekani yupo tiyari, basi yeye hanakipingamizi.

Wakuu wa G7 vichwa kuuma juu ya Urusi.

Brussels, Ubeligiji - 05/06/2014. Viongozi wa nchi za G7 au nchi zenye maendeleo ya kiuchumi wameionya Urusi kuwa huenda ikakumbwa na vikwazo zaidi ikiwa haita badili mwenendo wake kwa nchi ya Ukraine.

Onyo hilo lilitolewa na rais wa Marekani Baraka Obama , mara baada ya mkutano wa pamoja na viongozi wenzake wa G7 na uongozi wa jumuiya ya nchi za umoja wa Ulaya.

Rais Obama alisema " dunia inategemea uchumi shirikishi unaokuwa kwa pamoja, leo Urusi inajikuta haipo katika kuinuua uchumi wake, kwa ajili ya uchaguzi potofu unaofanywa na uongozi wa Urusi."

" Hivyo ipo haja ya Putin kuitambua serikali ya rais Petro Poroshenko na pia kusimamisha upelekeji wa siraha kwa wapinzani wa serikali ya Ukraine."

"Putin ananafasi ya kufuata sheria za kimataifa" Aliongezea rais Obama.

Mkutano wa wakuu wa G7, imefanyika baada ya ule mkutano  uliyokuwa ufanyike wa nchi za G8  kwenye mji wa Sochi Urusi kugomewa na Marekani na washiriki wake, kwa madai kuwa Urusi imejiingiza katika masuala ya Ukraine.


Wednesday, June 4, 2014

Marekani yahaidi kuwa karibu na Ukraine.

John Kerry afanya ziara ya kustukiza nchini Lebanoni.


Beiruti, Lebanoni - 04/06/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani amewasili nchi Lebanoni ili kujua ni kwakiasi gani Marekani itasaidiana na viongozi wa Lebanoni ili kutatua suala la wakimbizi.

Akiongea mara baada ya kufika Lebanoni na kujionea mwenyewe ni kwa jinsi gani serikali ya Lebanoni inavyo kabiliana na  hali ya wingi wa wakimbizi, waziri John Kerry alisema '' nimuhimu kwa serikali ya Lebanoni ikasaidiwa katika swala zima la kusaidia wakimbizi kwani hili nijukumu la kimataifa''

Kufatia zira hiyo ya John Kerry, Lebanoni inatarajiwa kupata msaada wa dola $51million ili kuweza kukabiliana na wimbi la wakimbizi wanaoingia nchi humo toka Syria ambapo bado vita vya kutaka kuing'oa serikali ya rais bashar al Assad.

Lebanon imekuwa katika myumbo wa kisiasa kwa muda mrefu, na tatizo la ongezeko la wakimbizi kukimbilia nchini humo limefanya jamii ya Walebanoni kuwa na upinzani mkubwa kwa kuwepo kwa wakimbizi wanao ingia nchini humo wengi wao kutoka Syria.

Marekani yahaidi kuwa karibu na Ukraine.

Warsaw, Poland - 04/06/2014. Serikali ya Marekani imehaidi kuongeza misaada kwa serikali ya Ukraine, ili kuweza kupambana na wapinzani wanaotaka kuigawa nchi hiyo.

Haadi hiyo ilitolewa na rais wa Marekani Baraka Obama wakati alipo kutana na rais wa Ukraine Petro Poroshenko jiji Warsaw.

Rais Obama alisema '' kitendo cha wanachi wa Ukraine kumchagua Petro Poroshenko ni cha busara kwani  ni mtu atakaye waongoza kwa bora zaidi.''

'' Na serikali ya Marekani itatoa pesa kiasi cha dola billion 5$ ili kusaidia Uikraine kutokana na hali iliyopo ili kulinda usalama wake''  Tangu mwezi Machi serikali ya Marekani imesha toa dola $23million kwa Ukraine.

Kabla ya kuchaguliwa kuwa rais katika uchaguzi uliyofanyika May 25, Petro Poroshenko, alikuwa mfanya biashara ambaye alikuwa akishughulika na uuzaji wa vyakula hasa chololati na bidhaa zinazo endana na mikate na kupewa jina la Mfalme Chokolati.

Tuesday, June 3, 2014

Abdul Fattah al Sisi ashinda uchaguzi wa Urais nchini Misri.

Rais Obama atangaza msaada kwa NATO.

Warsaw, Poland - 03/06/2014. Serikali ya Marekani imetangaza kutoa pesa ili kusaidia   kuikuza NATO kiulinzi kwenye bara la Ulaya.

Hayo yalisemwa na rais Baraka Obama wakati alipo kuwa akihutubia jiji Warsaw, Poland wakati wa alipokutana na wanajeshi wa Kimarekani waliopo nchini humo.

Rais Obama alisema "tukiwa marafiki na washirika wakubwa ni jukumu letu kujilinda kwa pamoja, na naomba wabunge wa kongresi waunge mkono wito wakukubali kutoa dola billion moja ilikuweza kufanikisha lengo hili kwani usalama wa washiriki na marafiki zetu ni usalama kwetu pia."

 |April mwaka huu wanajeshi 150 wa Kimarekani waliwasili nchini Poland, baada ya hali ya machafuko kuongezeka nchini Ukraine.

Rais Baraka  Obama alipokelewa na mwenyeji wake rais Poland Bronislaw Komorowsiki kwenye uwanja wa Kijeshi ambapo ndipo waliongea na kutoa hotuba kwa pamoja.

Baada ya kumaliza ziara yake nchi Poland rais Obama atatembelea  nchi Ubeligiji na baadaye pia kuwasili Ufansa ili kuhudhuria sherehe ya miaka 70 tangu kuisha vita vya pili vya dunia.

 Waziri mkuu wa Uturuki akemea CNN.


Istambul, Uturuki - 03/06/2014. Waziri mkuu wa Uturuki ameyalaumu mashirika ya habari ya nchi za magharibi kwa kutangaza habari kwa kupendelea na pia kuwa kama makampuni ya makachero.

Waziri mkuu  Recep Tayyip Erdogan aliyasema hayo wakati alipo kuwa akihutubia katika mkutano wa wanachama wake wa chama cha AK  na kutoa mfano kuwa  CNN ni moja ya shirika la habari ambalo limekuwa likifanya kazi yake kama ofisi ya kikachero.

Akiongea waziri mkuu Erdogan alisema "CNN ilitumia masaa nane wakati wa siku ya kumbu kumbu ya Gezi, na mwaka huu wamekamatwa na kuonyesha kuwa hawafati maadili ya uandishi na kazi yake ni kuchangia kuvuruga nchini."

"Ni jukumu langu kuhakikisha Uturuki inakuwa salama kwa kila mtu, na polisi wanatakiwa kufanya kazi yao bila kuingiliwa ili kuleta usalama na nitawalinda kwa hali na mali."

"Mbona hawaonyeshi yanayo fanywa na polisi nchini Marekani au Uingereza?" 

Waziri mkuu Tayyip Erdogan, alilitaja shirika la habari la CNN kuwa katika ripoti yake ya vurugu zilizo tokea mwaka 2013 katika kiwanja cha Taskim, ilikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya nchi za kigeni na mpaka sasa bado mashirika hayo yanania ya kukuza mvugo wa amani nchini Uturuki. 

Kuongea huko kwa waziri Erdogan umekuja baada ya mmoja wa waandishi wa habari wa CNN kukamatwa wakati wa maandamano na baadaye kuachiwa  huru baada ya kuwekwa chini ya ulinzi kwa muda wa zaidi ya dakika 45.

Abdul Fattah al Sisi ashinda uchaguzi wa Urais nchini Misri.



Kairo, Misri - 03/06/2014. Matokea ya uchaguzi nchini Misri yamempa ushindi mkubwa Abdul Fattah al Sisi ambaye alikuwa anagombania kiti cha urais.

Sisi ambaye alikuwa mkuu wa majeshi na kuachia magwanda Machi 26 2014, ameshinda kwa wingi wa kura za asilimia 96.91 katika uchaguzi mkuu uliyo fanyika Misri.

Ushindi huo wa Sisi, umekuja miezi tisa tu, baada ya kuhusika katika mapinduzi ya serikali ya rais Mohammed Morsi  na  ambaye alimchagua Sisi kuwa mkuu wa majaeshi. 

Tangu kuangushwa kwa serikali ya Hosni Mubara mwaka February 11/ 2011, Misri imekuwa na misukosuko ya kisiasa na kupelekea kuvuruga  nchini humo, jambo ambalo Sisi amehaidi kulipatia jibu na pia kusema "itachukua miaka 25 ili kuleta demokrasi kamili nchi Misri."

Abdul Fattah al Sisi anatarajiwa kuapishwa kuwa rais siku ya Jumapili wiki hii.

Mwizi wa kimtandao atafutwa kwauvumba na ubani.


Washington, Marekeni - 03/06/2014. Marekani inamsaka raia wa Urusi ambaye alifanikiwa kuingia katika mfumo mzima wa kimtandao na kuiba mamilioni ya pesa katika mabenki tofauti duniani.

Evgenivy Bagacgev 30 ambaye ametajwa kama mtuhumiwa wa wizi wa kimitandao, anatakiwa kujibu mashitaka ya kuhusika na kutengeneza mfumo wa kimtandao ambao uliweza kutengua mfumo mama wa kiulinzi wa kibenki na kuweza kupenyeza na kuiba pesa tangu 2006. 

Akiongea mara baada ya kutoa wajihi wa mtuhumiwa, mmoja  wa mkuu wa kitengo cha usalama wa mitanndao wa  Marekani Leslie Caldwell  alisema "mfumo aliyotengeneza Bagacgev ni wa hali ya juu na ilikuwa vigumu kuugundua, na hii tuliweza kugundua kwa kushirikiana na nchi 10 ambazo zilikumbwa na matatizo haya na hivyo lazima atafutwe kwa uvumba na ubani"

Evegenivy Bagacgev anasemekana kwa mara ya mwisho alionekana katika maeneo ya Black See kwenye kitongoji cha Anapa akijiliwaza .

 Wapalestina wapata serikali mpya.


Ramallah, Palestina - 03/06/2014. Wapelestina wamepata serikali ya muungano, ambayo itakuwa na kazi kubwa ya kuuanda matayarisho ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge.

Serikali hiyo ambayo imeunganisha vikundi vya Hamas na Fatah, itakuwa na viongozi 17 kutoka pande zote. 

Kuundwa huko kwa serikali ya muungano, kumekuja baada ya majadiliano yaliyo chukua wiki tano na kufanikiwa kufikia tamati kwa makubaliano ambayo yalifanyika April 23 mwaka huu.

Akiongea mara baada ya kuundwa na kula viapo kwa viongozi wapya wa Kipalestina, rais wa Wapelestina Mahamoud Abbas alisema "serikali hii itakuwa ya mpito, na maswala ya ukombozi wa Wapalestina katika majadiliano ya amani na Izrael yapo chini ya PLO - Palestina Liberation Organasation, na serikali hii kama serikali zilizo pita, itafuata na kutii sheria zilizo sainiwa hapo awali."

Hata hivyo kitendo cha Fatah na Hamas kuungana na kuunda serikali, kimepingwa vikali na Izrael, na kuitaka Marekani kutounga mkono serikali hoyo.

Uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi kwa Wapalestina unatarajiwa kufnyika mwaka 2015

Mfalme wa Uispania kuachia madaraka.

Madrid, Uispania - 03/07/2014.Mfalme wa Juan Carlos Uispania ametangaza kuachia kiti cha ufalme, baada ya kukikalia kwa miaka arobaini.

Akiongea kumwakilisha Mfalme Juan Carlos, waziri mkuu wa Uspania Mariano Rajoy alisema " Mfalme Juan Carlos ameamua kuachia uongozi wa kifalme, ili kutoa nafasi kwa kizazi kipya na pia nakuwa na matumaini katika kurekebisha makosa ambayo yametokea katika harakati za  kuijenga na kuimarisha Uispania"

Mfalme Juan Carlos, amependekeza kuachia kiti hicho kwa mwanae 46 Prince Phillipe, ambaye anatazamiwa kuwa mfalme wa kizazi cha kisasa na kuwa na majukumu  magumu ya kuimarisha ufalme, kutokaa na baadhi ya kashfa kuzuka katika ufalme huo.
 Na vile vile kutokea upinzani wa hapa na pale  wakupinga uongozi wa Kimfalme nchi Uispania

Saturday, May 24, 2014

Papa Francis aanza ziara nchi za Mashariki ya Kati.

Jacob Zuma ala kiapo kuwa rais kwa mara ya pili mfululizo.

Pretoria, Afrika yaKusini - 24/05/2014. Rais Jacob Zuma  ameaapishwa kwa mara nyingine kuwa rais wa Afrika ya Kusini ikiwa ni muhula wake wa pili kama rais wanchi hiyo.

Baada ya kuapishwa rais Zuma  alisema " kipindi hiki cha uongozi wangu wa miaka mitano tutahakikisha tunainua uchumi na maisha ya jamii kwaujumla."

Katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi, rais Jacob Zuma, amelaumiwa kwa kukosa kuinua maisha ya wananchi walio wengi ambao inasadikiwa hali ya umaskini imekuwa ikiongezeka kwa haraka kila kukicha.

Katika sherehe hiyo, marais na viongozi mbali mbali waliudhulia kuapishwa huko wakiwemo, rais Robert Mugabe wa Zimbabwe na Goodluck Jonathan.

Rais Jacob Zuma amechukua kiti cha urais chini ya chama cha ANC ambapo kilishinda uchaguzi mkuu uliyofanyika Mei 7 na kuwa chama pekee kinacho ongoza nchi tangu Afrika ya Kusini tangu kukomeshwa kwa serikali ya ubaguzi wa rangi miaka 20 iliyopita.

ICC Hague yatoa hukumu jela miaka 12 kwa German Katanga

Hague, Uhollanzi - 24/05/2014.Mahakama ya kimataifa ICC, inayo shughurikia makosa ya jina na ukiukwaji wa haki za binadamu imemuhukumu kwenda jela aliyekuwa mkuu wa majaeshi ya upinzani nchi Kongo DRC, German Katanga.

German Katanga 36, ambaye alikutwa na makosa ya kuuza siraha ambazo zimetumiwa katika mauaji ya mamia ya watu manamo  mwaka 2003.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Bruno Cotte alisema " mahakama inakuhukumu miaka 12 kwenda jela kutokana na makosa ambayo umekutwa nayo."

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo, wakili wa Katanga amekata rufaa kupinga uamuzi huo wa mahakama.

German Katanga amekuwa ni kiongozi wa pili kuhukumiwa na mahakama ya ICC baada ya mahakama hiyo kumuhuku jela aliyekuwa mkuu wa majeshi ya upinzani Thomas Lubanga mwaka 2012.

Papa Francis aanza ziara nchi za Mashariki ya Kati.

Amman, Jordan - 24/05/2014. Mkuu wa kanisa Katoli dunia Papa Francis amewasili nchi Jordan ikiwa ni moja ya nia yake ya kukuza uhusiano wa karibu na wakazi wa Mashariki ya kati.

Akiongea mara baada ya kuwasili nchini Jordani na kuongoza ibada katika uwanja mkubwa ulipo Amman  Papa Francis alisema " nimatumaini yangu kuwa amani na utulivu utakuwepo kwa wakazi wa eneo zima la Mashariki ya Kati na dunia nzima, na nawashukuru wananchi wa Jordani kuwa mstari wa mbele katika kuleta amani na kutoa msaada na vile vile kuwa weka kilauhudi ili kumaliza mzozo wa Waizrael na Wapalestina."

Papa Francis alipokelewa na  Mfalme wa Jordan Abdullah II wakati alipo wasili nchi Jordani na baadaye alitembelea katika hekalu la waumini wa Orthodox na vile vile kutembelea kambi ya wakimbizi kutoka  Syria.

Papa Francis katika ziara yake hiyo, ameambatana na wakuu wa dini ya Kiislam na Kiyahudi kutoka  Argentinana ikiwa ni katika jitihada zake za kutaka kuwepo na uhusiano wa karibu na waumini wa dini nyingine.

Siku ya Jumapili atatembelea mji wa Bethlehem - West Bank na kuongoza ibada katika eneo ambalo inaaminika ni mahali alipo zaliwa Yesu Kristu.

Thursday, May 22, 2014

Iran yadai ipo tiyari kwa majibu ya kivita.

Uchaguzi wa urais nchi Malawi wawa tumbo joto kwa rais Joyce Banda.

Lilongwe, Malawi - 22/05/2014. Rais wa Malawi Joyce Banda na ambaye anagombania tena kiti cha urais, amekutwa na wakati mgumu  baada ya kashfa kuibuka  kuwa wa Malawi imepoteza mamilioni ya pesa kutoka hazina kuu wakati wa uongozi wake.

Huku akiwa anasubiri mataokeo ya uchaguzi mkuu ambapo  zaidi ya watu wapatao millioni 7 wamepiga kura, rais Joyce Banda alilalamikia mfumo mzima wa uchaguzi kwa kudai kuwa ''kumekuwa na ukiukwaji wa kimsingi wa mwenendo mzima wa uchaguzi na mitandazo ya kuhesabia kura kuvurugwa kimakusudi.''

''Na mimi sihusiki na wizi wa millioni ya dola za Kimarekani zinazo tajwa.''

Malawi inakadiliwa kupoteza zaidi ya dola  million 30, na pia serikali ya rais Joyce Banda iliwekewa vikwazo vya misaada na na pesa kutoka nchi wafadhili tangu kutokea sintofahamu katika uongozi wake.

Hata hivyo msimamizi wa uchaguzi mkuu wa Malawi Maxon Mbendera amepinga kauli hiyo ya rais banda kwa kusema '' hakuna ukiukwaji wa sheria uliovunjwa na mitandao ipo safi, na kama ingetokea tatizo basi tunayo plan B ya kluhesabu kura kwa mkono.''

Rais Joyce Banda, amekuwa na wakati mgumu kutoka kwa wapinzani wake ambao wanaongozwa na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Malawi  Peter Mutharika Uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kwa pamoja nchini Malawi ulinafanyika siku moja kwa mara ya kwanza tangu Malawi kupata uhuru 1962.

Iran yadai ipo tiyari kwa majibu ya kivita.

Tehran, Iran - 22/05/2014. Serikali ya Iran imesema kuwa  itakuwa ni makosa makubwa kwa Izrael kufanya mashambulizi nchini Iran kwani  majibu ya Iran baada ya kushambuliwa yatakuwa hayana mfano.

Onyo hilo limetolewa na mkuu wa maswala ya kijeshi na ushirikiano wa kiulinzi Brigedia Ramezan Sharif kwa kusema ''Natumaini Izrael haitafanya makosa kama hayo, na wakuu wa wanchi hiyo wenye busara wanajaribu kuzuia hatua hiyo kwa kujua kuwa Iran itajibu mashambulizi ambayo dunia nzima itastuka.''

Kuongea kwa mkuu huyo wa jeshi la Iran, kumekuja baada ya kudai kuwa vitisho vinavyo fanywa na baadhi ya viongozi wa Izrael vinaangaliwa kwa makini.

Mvutano na vitisho kati ya Iran na Izrael vimekuwa vimekuwa vikiendelea huku Izrael ikidai Iran izuiwe kuendelea na mradi wake wa kinyukilia kwa madai unania ya kutengeneza mabomu yatakayo tioshia amani kwa Irzael na mashariki ya kati nzima.

Na wakati huo huo Iran kudai kuwa mradi wake wa kimnyuklia ni wa kimaendeleo ya kisayansi, na pia kudai Izrael kuweka wazi kuwa ina siraha za kinyuklia jambo ambalo mpaka sasa Izrael haija liweka wazi.

China na Urusi zawaweka ngumu Umoja wa mataifa.

Washington, Marekani - 22/05/2014. China na Uruusi zimepiga kura ya veto kwa kupinga muswada wa kutaka serikali ya Syria kupelekwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC.

Kura hiyo ya veto immepigwa  baada ya Ufaransa  kuwakilisha muswada huo ambao unaishutumu serikali ya Syria kuhusika na ukiukwaji wa haki za minadamu na makosa ya jinai.
Muswada huu ambao uliungwa mkono na nchi 58, uligonga mwamba uliowekwa na China na Urusi kwa madai kuwa ulikosa baadhi ya ukweli.

Akiongea baada ya kura hiyo ya veto, balozi wa umoja wa mataifa wa Urusi Vitaly Churkin alisema '' uamuzi wa kupiga kura ya veto ni mzuri kwani unania ya kupunguza mlolongo wa kuendelea vita nchini Syria ambao umekuwa ukichochewa kila kukicha.''

Syria imekuwa katika vita vya wenyewe kwa kwa kipindi cha miaka mitatu na zaidi na inakadiriwa watu zaidi ya 175,000 wamecha poteza maisha na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa.


Wednesday, May 21, 2014

China na Urusi zasaini mkataba wa karne.

China na Urusi zasaini mkataba wa karne.

Beijing, China - 21/05/2014. Urusi na China zimesainia mkataba wa biashara wa malighafi mafuta ambao utatudu kwamuda wa miaka 30.

Makubaliano hayo  kufanya biashara pamoja katika sekta ya malighafi mafuta yamechukua miaka kumi ya majadiriano na hatimaye  kufikia makubaliano, ambapo kuanzi sasa  shirika la uzalishaji wa malighafi mafuta la Urusi Gazprom na la China CNPC kwa pamoja yatafanya bishara ambayo itagharimu $ 400 billion.

Mkurugenzi mkuu wa Gazprom Aleksey Miller lisema " mkataba wa makubaliano na matumzi yatakavo fanyika itabaki ni kati ya Gazprom na CNPC katika makubaliano ya kibiashara."

Mkataba wa Urusi na China umeitwa mkataba wa karne, kwani utasaidia nchi hizi mbili kuwa karibu zaidi jambo ambalo nchi za muungano wa Ulaya na Marekani zitauchunguza na kuwa makini na nchi  hizi mbili.

Kitendo cha Urusi kusaini mkataba na China  kibiashara ya malighafi mafuta kimetafsiliwa kuwa  ni ushindi mkubwa kwa rais Vladmir Putin, kwani kutokana na mgogoro wa Ukraine, Urusi imejikuta ikivutana na nchi za muungano wa jumuiya ya Ulaya na Marekani na hata kufikiwa Urusi kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Friday, May 16, 2014

Kenya yashambuliwa tena na mabomu.

Kenya yashambuliwa tena na mabomu.

Nairobi, Kenya - 16/05/2014.Wakazi wa jiji la Nairobi walishikwa na mstuko mkubwa baada ya milipuko ya mabomu kutokea kwenye soko la Gikomba ambalo ni la pili kwa ukubwa na maarufu kwa uuzaji wa nguo na bidhaa ndogo ndogo.


Akiongea baada ya tukio hilo, rais wa Kenya. Uhuru Kenyatta amesema "tutawatafuta pale walipo wale 
wote wanao husika au kuandaa kuvurga amani nchi Kenya, kwani wanafanya vitendo vya kishetani "

" Naamini kwa ushirikiano wa pamoja tutashida vita hivi zidi ya ugaidi." Asisitiza rais Kenyatta.

Milipuko hiyo ya mabomu ambayo imesababisha mauaji ya wati 12 na kujeruhi watu 90, imetokea wakati wananchi wa Kenya hasa wakazi wa jiji la Nairobi wakiwa bado na jeraha la kulipuliwa kwa eneo la maduka ya kisasa la Westgate ambapo watu 67 waliuwawa mwishoni kwa mwaka jana baada ya wapiganaji wa Al Shabab kuvamia eneo la maduka hayo.

Kenya imekuwa inakumbwa na milipuko ya mabomu ambayo kundi la Al Shabab limekuwa likidai kuhusika na  na mashambulizi yanayo tokea nchini humo ikiwa ni kupinga kitendo cha serikali ya Kenya kupeleka jeshi lake nchi Somalia ili kupambana na kundi la Al Qaeda

Hata hivyo serikali ya Kenya imekasirishwa na kitendo cha Uingereza kuwakataza raia wake kutokwenda Kenya na kuwataka wale walipo Kenya kuondoka kwa madai kuwa hakuna uhakika wa usalama wa raia hao wakati watakapo kuwa  Kenya.

Nchi mwenyeji wa kombe la dunia 2014 yavutana na wananchi.

Sao Paulo, Brazil - 16/05/2014.Waandamanaji wamepambana na polisi nchi Brazil kwa kupinga kitendo cha serikali kuaandaa michuano ya kombe la dunia, huku wanachi   walio wengi wakiwa na maisha ya kimasikini.

Maandamano hayo ambayo yamefanyika katika miji tofauti nchi humo, kuliwafanya polisi kutumia mabomu ya machozi ili kupambana na waandamanaji waliokuwa na asira huku waki imba kudai maisha bora na huku wakipindua magari yaliyokuwa barabarani pia kuvunja baadhi ya maduka.

Mmoja wa waandaji wa maandamano hayo Luana Gurther alisema " serikali inatakiwa kutumia pesa katika kujenga hospitali, shule, nyumba na kusaidia kuinua maisha ya watu, badala ya kutumia mamilioni ya pesa kwa ajili ya kombe la dunia."

Maandamano hayo yamekuja baada ya hali ya maisha kuwa juu, na huku bei ya vitu kupanda bei kwa asilimia 50% .

Brazili itakuwa mwenyeji wa kombe la dunia  la mwaka huu wa 2014 na pia michuano ya michezo ya  Olimpiki ya 2016.

Umoja wa mataifa wadai ukiukwaji wa haki za binanadamu ni mkubwa nchini Ukraini.

Geneva, Uswisi - 16/05/2014. Umoja wa mataifa mestushwa na hali ya  uvunjwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchi Ukraini,  baada ya kupokea  ripoti yenye kurasa 37 ambayo imetolewa na shirika la kutete haki za binadamu la Umoja wa mataifa.

Akiongea kuhusu hali hiyo, mkuu wa kitengo cha kutete haki za binadamu Navi Pillay amesema " uvujwaji wa haki za binadamu nchi Ukraine umekuwa ukifanywa kwa wale watu ambao wamekuwa wakiandamana bila kufanya vurugu na pia na wale wasiohusika katika vurugu na huku polisi wa serikali wakiwa wanaangalia au wakati mwingine kushiriki katika kufanya matendo ya unyanyasaji."

" Hii pia imekuwa ikitokea kwa waandishi wa habari kupigwa kutekwa nyara na hata jeruhiwa kwa makusudi." Aliongezea Pillay.

Naye aliyekuwa Kansela wa Ujerumani kati ya 1074-1982 Helmut Schmidt, ameilaumu  muungano wa nchi za Ulaya kwa kusema " Nchi za muungano wa Ulaya zinavyofanya katika mgogoro wa Ukraini zinatishia kuzuka kwa vita na Urusi, kwani  kadri siku zinavyo kwenda na hali hii inazidi kuwa mbaya  na hali kama hii ilitokea mwaka 1914."

Mazungumzo hayo ya kuzilaumu nchi za muungano wa Ulaya yaliyo fanywa wakati  Kansella Helmut Schmidt alipo ongea  na gazeti la Bild hivi karibuni, ili kuona mwono wake wa hali halisi ya ushiriki wa muungano wa nchi za Ulaya katika mgogoro wa Ukraini.

Marekani yadai ikoma macho na Iran.

Al-Quads, Izrael - 16/05/2014. Marekani imeihakikishia Izrael kuwa haitaruhusu Iran kutengeneza bomu la nuklia.

Matamshi hayo yaliongewa na waziri wa Ulinzi wa Marekani  Chuck Hagel, ambaye yupo nchini Izrael kwa ziara ya kiserikali wakati  apokutana na waziri mkuu wa Izrael  Benjamin Netanyahu katika jiji la Jerusalem ambalo kwa kiarabu linajulikana kama Al-Quads.

"Napenda kuwahakikishia kuwa  Marekani ipo macho kwa kila hali ili kuhakikisha Iran haitengenezi bomu lolote la nyuklia, na kama Iran itaendelea kutosikia basi hatua kali zitachukuliwa kufuatia sheria za kimataita."

Akizungumzia kuhusu matamshi hayo ya waziri Chuck Hagel, mtaalamu wa maswala ya kidiplomasia na mwandishi wa habari wa Iran Hamid Golpira amesema"Izrael imekuwa ikikanusha kuwa haina mabomu ya nyuklia wakati ukweli unajulikana kuwa Izrael ina mabomu ya nyukila yapatayo 200, na mpaka sasa haitaki kuweka wazi japo jumuiya ya kimataifa inalikua hili, ikiwemo  Marekani."

Mvutano kati ya Marekani , washiriki wake na Iran kuhusu masuala ya kinyuklia umekuwa ukipigwa danadana katika kila vikao vinavyo fanywa vya  5+1  vya nchi za Iran, China, Ujerumani, Marekani, Ufaransa na Uingereza. kwa kutoa majibu ya sintokubaliana kila baada ya mikutano

Wednesday, May 14, 2014

Umoja wa mataifa waingia doa na mapambano ya Ukraine.

Jaji aamuru mwanariadha akapimwe akili.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 14/05/2014. Jaji  anayesikiliza kesi ya mauaji nayo mkabili mkiambiaji Oscar Pistorius, ametoa amri ya kuchunguzwa akili kwa mwanariadha huyo ili kuweza kupata kufahamu uwezo wake wa akili na ufahamu.

Akitoa amri hiyo Jaji Thokozile Masipa alisema " mshitakiwa anatakiwa kuangaliwa kiakili kwani, itasaidia mahaka kujua ni kwa kiasi gani haya makosa yalifanyika, kwa maana hali ya kutambua akili na ufahamu wa mtu si kazi ya mahakama."

"Matatizo ya akili yanatakiwa kuangaliwa na siyo jambo la kulifumbia macho." Aliongezea Jaji Masipa.

Uamuzi huo wa Jaji Masipa wa kutaka Oscar Pistorius kuchunguzwa akili umekuja baada ya kusikiliaza mwenendo mzima wa kesi na pia kwa upande wa utetezi kutaka uchunguzi huo ufanyike kwa kutokana na historia ya maisha ya mshitakiwa.

Oscar Pistorius, ambaye ni mwanariadha wa kwanza kushiriki katika mbio za Olimpiki jumla za mwaka 2012 London akitumia miguu bandia, alikili kumwua bila kukusudia mpenzi wake Reeva  Steenkamp katika siku ya wapendanao dunia.

Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael ahukumiwa kwenda jela.


Jerusalem, Izrael - 14/05/2014. Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael amehukumiwa kwenda jela kwa muda wa miaka sita na kutakiwa kulipa faini ya Euro 210,000.

Ehud Olmert ambaye alikuwa waziri mkuu mwaka 2006, alikutwa na hatia ya kuhusika katika kula  rushwa wakati alipo kuwa meya wa jiji la Jerusalem.

Akitoa hukumu, Jaji David Rosen alisema, " kuwa kiongozi anaye ongoza jamii na kukabidhiwa dhamana ya wananchi ni lazima awemfano bora kwa jamii, na kitendo cha kukubali kula rushwa lazima kikomeshwe kwa kiongozi yoyote aliyehusika kwa kuadhibiwa vikali."

"Makosa aliyokutwa nayo Olmert yalikuwa kukubali kula mlungura katika harakati za kuandaa mipango mji, na pia pesa nyingi kutumika kiholera katika kutangaza baadhi ya miradi na vilevile kutoa unafuu wa kodi kinyume na sheria na hata kushinikiza baadhi ya sheria kuundwa ili kutoa ubukheri kwa wahusika katika ujenzi wa  jiji la Jerusalem."

Kesi ya Ehud Ormert imechukua zaidi ya miaka miwili,na uchunguzi  ulianza rasmi kufanyaki mwaka 2010 na baadaye kuonekana  Olmert alikuwa muhusika mkuu katika suala zima la matumizi mabaya ya pesa wakati wa utawala wake kama meya wa jiji la Jerusalem na kumfanya alijiudhuru 2008 uwadhifa wake wa uwaziri mkuu, baada ya polisi kuanza matayarisho ya kumfungulia kesi.

Umoja wa mataifa waingia doa na mapambano ya Ukraine.

New York, Marekani - 14/05/2014. Umoja wa Mataifa umekutwa na wakati mgumu wa kujibu maswali baada ya helikopta yenye nembo ya UN kuonekana kutumika katika mashambulizi nchi Ukraini.

Habari kutoka katika ofisi ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon zimesema, " nikinyume na sheria kutumia vifaa au helikopta ya umoja wa mataifa katika mapambano yoyote na hii inaleta sura potofu kwa jamii nzima ya kimataifa kuhusu ufanisi wa umoja wa Mataifa."

"Vifaa, ndege na helikopta za Umoja wa Mataifa huwa vinatumika katika kusaidia na kuokoa watu walio katika hali ya hatari na maafa, hivyo serikali ya Kiev imevunja sheria na kwenda kinyume na mkataba wa umoja wa amataifa na tunalaani itendo cha kutumia vifaa vya Umoja wa Mataifa katika mapambano ya kivita."

Hata hivyo waziri wa ulinzi wa  Ukraine imekanusha kutumia helikopta ya umoja wa mataifa katika mapambano yake na wapinzani ambao wanataka kujitenga na serikali ya Kiev, na alipo ulizwa kuhusu helikopta yenye nembo ya UN kuonekana kufanya mashabulizi akili kataa kulizungumzia swala hilo tena.

Helikopta yenye rangi nyeupe Mil Mi-24 imeonekana ikitumika katika mashambuzi ya kuwashambulia wapinzani wa serikali  ya Ukraine, ambo wanapinga uhalali wa serikali ya sasa ambayo iliingia madarakani baada ya mapinduzi yaliyo mng'oa rais Victor Yanukovych  Februari mwaka huu 2014.

Mapambano ambayo yanaendelea nchi Ukraine yamekuwa baada ya majimbo ya Donetsk na Lugansky kupiga kura ya maoni ya kujitenga na serikali ya Kiev, jambo ambalo Kiev inalipinga.

Tuesday, May 13, 2014

Msuruhishi wa machafuko ya Syria atundika madaruga juu.

Waumini wa dini waajiliwa kupigana na ugaidi nchi Marekani.


New York, Marekani - 13/05/2014. Polisi katika jiji la New York wamekuwa wakiwaajili watu wenye imani na dini Kislaam tangu kutokea mashambulizi ya Septemba 11.

Likilipoti habari hizi, gazeti la New York Times  limeandika "Kamati ya usalama iliamua kuwaa ajili waumini hao wa dini ya Kiislaam katika hotel na kwenye Miskitiili kuweza kujua na kupata habari mapema kabla, kwani  maeneo hayo yamekuwa yakitumika katika mikutano na pia kuajili watu kujiunga na makundi ya kigadi."

Likiongeza katika ripoti hiyo limeandika kuwa " wengi wa waajiliwa wamekuwa wale wanao toka nje ya Marekani."

Akithibitisha kwa kuwepo kwa uajili huo, mkuu wa kitengo cha kupamana na ugaidi John Miller alisema " Tunaangalia watu ambao wanaweza kutupatia undani wa ugaidi kutoka sehemu tofauti duniani jambo ambalo litasaidia kupambana na ugaidi kwa urahisi."

Hata hivyo kufuatia uamuzi wa polisi kuajili watu wenye imani na dini ya Kiislaam, malalamiko yamekuwa yakitolewa na wahusika kwa kudai inabidi washirikiane na polisi kwani hawana njia nyingine.

Gazeti la New York Times limelipoti habari hizi kufuatia sheria ya uhuru wa habari.

Msuruhishi wa machafuko ya Syria atundika madaruga juu.


New York, Marekani 13/05/2014.Lakhdar Ibrahimi ambaye  aliyeteuliwa na umoja wa mataifa kuwa mkuu katika kusuruhisha suala la uleteji wa amani na mapatano katika myumbo wa kisiasa na vita kati ya Wasyria ametangaza kujiudhuru ifikapo mwisho wa tarehe 31/05/2014.

Akitangaza kutaka kujiudhuru huko katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema "Lakhdar Ibrahimi atajiudhuru"

Hata hivyo Ban Ki-moon haueleza ni nini kilicho mfanya msuruhishi huyo kutaagaza kujiudhuru wakati hali ya Syria bado ni tete.

Akiongea baada ya habari kutangazwa Lakhdar Ibrahimi alisema " nimekuwa nafikirika kujiudhuru  kila kukicha na sasa muda umefika wa kutangaza rasmi siku ya kujiudhuru kwangu."

Lakhdar Ibrahimi toka kuteuliwa kwake kushughulikia suala la machafuko ya Syria amaekuwa na wakati mgumu wa kuwapatanisha wapinzani wa serikali na serikali ya rais Assad, jambo ambalo lilimfanya akili na kuomba radhi kwa wananchi wa Syria kuwa hali bado ni tete katika kufikia makubaliano kwa pande zote mbili.

Kujiudhuru kwa Ibrahimi kumekuja wakati serikali ya rais Bashaar Assad imekuwana nguvu zaidi kuliko wapinzani na kufanikiwa kuuchukua mji wa Alepo ambao ulikuwa makao makuu ya wapinzani wa serikali na huku rais Bashar Asaad akiwa katika kampeni ya kugombea tena kiti cha urais kwa miaka saba ijayo, ambapo anatarajiwa kushinda kwa wingi wa kura.

Matokeo ya kura za maoni nchini Ukraine yawa kitendawili.


Moscow, Urusi - 13/05/2014. Matokeo ya kura ya maoni ya kutaka kujitawala kwa majimbo ya  Donitsk na Lugansk yamezidi kuleta kicha kuuma kwa uongozi wa nchi za jumuiya ya Ulaya na Marekani na huku Urusi ikiwa inachukua muda kutathmini nini kitatokea.

Kufuatia matokeo ya kura za maoni katika majimbo hayo,  serikali za majimbo hayo yameitaka Urusi kukubali kuziunganisha katika serikali ya shirikisho na kuwa sehemu ya Urusi.
Naye msemaji  wa rais Dmitry Peskov akjibu kuhusu maombi ya majimbo hayo amesema "Urusi Urusi bado natafakali kwa makini juu ya maombi hayo."

Matokeo ya kura katika majimbo hayo ya Donietsk na Lugansk yame pelekea viongozi wa majimbo hayo kutangaza kusimamisha maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao ulitarajiwa kufanyika hivi karibuni jambo
ambalo Marekani imetishia kuwa " ikiwa hakutafanyika uchaguzi mkuu, vikwazo zidi ya Urusi vitazidishwa."

Kura zamaoni ambazo  zilipigwa siku ya Jumapili na  kwa wingi wa kura za asilimia 90 za kuunga mkono kwa majimbo ya Donetsk na Lugansk kujitenga na serikali ya Kiev,yameleta mitazamo tofauti.

Urusi imeshiria msimamo wake kuwa machafuko na mauaji yanayo endelea nchi Ukraine ni sababu ya serikali ya Kiev kushindwa kujua la kufanya, kwani imekuwa ikiongozwa na nguvu za nje badala ya kukaa na kufanya mazungumzo na wapinzani wa serikali na wakati huo huo Marekani na washiriki wake wakuu jumuiya ya Ulaya, kupinga na kulaani matokeo pia kutanganza kutoyatambua,

Monday, May 12, 2014

Wanajeshi wa kukodiwa watumika nchi Ukraine


Serikali ya Nigeria yapinga matakwa ya kundi la Boko Haram.

Maiduguri, Nigeria - 12/05/2014. Kundi la kigaidi la Boko Haram, limesambaza na kuzimeonyesha video za wasichana wa shule iliyowateka karibuni wiki nne zilizo pita.
Video ya kwanza ilikabidhiwa kwa shirika la habari la Ufaransa AFP na baadaye kuanza kuonekana katika mitandao tofauti ambapo wasichana hao walionekana wa kiswali.

Akiongea baada ya kuonyeshwa kwa video hiyo ya wasichana hao, mkuu wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau alisema " wasichana hawa watashikiliwa hadi hapo wanachama na wapiganaji wa Boko Haram watakapo achiwa huru"

 Naye mwakilishi wa BBC aliyepo Nigeria John Simpson amesema "kubadili nia huko kwa kundi hilo la Boko Haram kumeo nyesha kuwa kundi hilo lipo tiyari kuongea kuhusu kuachiwa kwa wasichana hao."

Kundi la Boko Haram lilianzishwa mwaka 2002 na toka hapo limekuwa likifanya mashambulizi zidi ya raia na ikiwa ni njia ya kuonyesha kupingana na mwenendo wa serikali ya Nigeria.

Jina Boko Haram linamaana ya kuwa  elimu na utamaduni wa kutoka nchi za Magharibi ( Ulaya na Marekani) ni marufuku kufuatwa na  wanchi wa Nigeria hasa wale walipo katika jimbo la Maiduguri

Wanajeshi wa kukodiwa watumika nchi Ukraine.


Donetsk, Ukraini - 12/05.2014. Maafisa usalama wa jimbo la Donetsk wamethibitisha madai yaliyotolewa na gazeti la Bild am Sonntag la Ujerumani   kuwa wanajeshi mamluki wa kukodiwa kutoka shirika la ulinzi  linaloitwa Xe Services lenye makao yake nchini Marekani  wameletwa nchi Ukraine ili kusaidiana na jeshi katika harakati za kupambana na wanapingana wanaopingana na serikali ya sasa ya nchi hiyo.

Mapema April 29/2014 gazeti la Bild  am Sonntag lililipoti kuwa kitengo cha usalama cha Ujerumani (BND) kilimpa maelezo Kansela Angela Merkel kwa kumweleza kuwa wanajeshi wa kigeni wa kutoka shirika la Xe zamani lililo julikana kama Blackwater na washiriki wake wapo nchi Ukraine tayari kusaidiana na serikali ya Kiev.

Maafisa hao wa usalama wamesema kuwa kuna idadi ya wanajeshi 400 mamluki ambao wapo nchi ni Ukraine na baadhi yao wameonekana kushiriki katika operesheni nzima ya kupambana na  wapinzani wa serikali ambao serikali ya Kiev inadai kuwa wanaungwa mkono Urusi, japo Urusi imekuwa ina kana kuhusika na hali ya machafuko yaliyopo nchini Ukraine na kwa kudai serikali iliyopo ndiyo ya kulaumiwa kutokana na machafuko yaliyopo nchini humo.

Nguvu za kisayansi katika jeshi la Iran za zidi kuonekana.


Tehra, Iran -12/05/2014. Iran imefanikiwa kutengeneza ndegeaina ya drone, ndege ambazo huwa zinaendeshwa bila rubani  ikiwa ni njia moja ya nchi hiyo ya kuweza kwenda sambamba na nchi nyingine ambazo zina ndege za aina hiyo.

Ndege hiyo ilionyeshwa kwa wataalamu wa kijeshi kutoka Urusi ambao walikuwa nchi Iran kikazi na kuelezwa kuwa "drone hiyo ambayo imetengenezwa kwa kufanana  na za Kimarekani, itakuwa na uwezo wa kurekodi maelezo ya picha na mienendo yoyote itakayo agiziwa kufanya na wataalamu wa  drone hizo"

Iran imekuwa na mikakati mikubwa ya kujiendeleza kisayansi na kiteknologia na vile vile kuhakikisha inaongeza nguvu zake za kijeshi tangu nchi hiyo ilipo kuwa na vita na Irak katika miaka ya 1980-89, na baadaye kuwekewa vikwazo na nchi za Magharibi.

 Na kutokana na vikwazo hivyo, Iran ilianza kuonyesha umairi wake wa kisayansi katika kijeshi mnamo mwaka wa 1992 baada ya kufanikiwa kutengeneza vivaru cha kivita, mizinga na ndege za kivita ikiwa kama njia ya kujihami.