Thursday, March 12, 2009

Aliyemrushia kiatu rais Bush ahukumiwa miaka 3 jela.

Ufaransa na Ujerumani kudumisha ushirikiano zaidi. Berlin, Ujerumani 12/03/09. Kansella wa Ujerumani, Angela Merkel, amempongeza rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, kwa uamuzi wa nchi yake kurudi kikamilifu katika jumuia ya ulinzi ya NATO. Kansella,Angela Merkel, aliyasema haya, wakati alipo kutana na rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, ambaye yupo ziarani nchini Ujerumani,ili kujadili ni jinsi gani nchi hizi mbili zitashirikiana zaidi. Picha hapo juu wanaonekana rais, wa Ufaransa,Nicolas Sarkozy, akikaribishwa mjini Berlini na Kansella, Angela Merkel mapema leo. Madaktari na muuguzi watekwa nyara Darfur. Darfur, Sudan-12/03/09.Waanyakazi watatu wa shirika la madakitari wa sio na mipaka wametekwa nyara na watu wasiojulikana. Wafanyakazi hao wanao tokea, Kanada na Itali, waliingiliwa katika ofisi zao zilizopo,Saraf Umra na kuchukuliwa kwa nguvu huku mitutu ya bunduki ikiwa nyuma yao. Kuafuatia hali ya usalama kuwa mbaya katika eneo hilo la Darfur, shirika hilo limeamua kuamishia ofisi zake mjini Kartoum. Picha hpo juu, linaonekna moja ya gari, lililo kuwa likitumiwa na ma wafanyakazi hao waliotekwa nyara mapema leo.

Aliye mrushia kiatu rais Bush, ahukumiwa miaka 3 jela.
Baghdad, Irak-12/03/09. Mwandishi wa habari Muntadher al Zaidi, aliyemrushia kiatu aliyekuwa rai wa Amerika George Bush, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.
Wana habari huyo, Muntadher al Zaidi,mwenye miaka 30, alihukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kumshambulia na kumdhalilisha kiongozi wa kigeni aliye tembelea nchi hiyo.
Hata hivyo, mwakili wa Muntadher al Zaidi, wamesema watakata rufaa, kufuatia hukumu hiyo.
Picha hapo juu wanaonekana, baadhi ya watu wakiandamana kuelekea mahakamani huku wamebeba picha za Muntadher al Zaidi.
Picha ya pili anaonekana, Muntadher al Zaidi,anaonekana akirusha kiatu wakati, rais George Bush alipo tembelea nchini Irak.
Picha hapo juu,

Sunday, March 8, 2009

Dunia ina siku 100 kabla ya kuangamia "Mwana wa Malkia".

Wacko Jacko kupanda jukwaani tena kufanya vitu vyake.

London Uingereza - 08/03/09.Bingwa wa muziki wa Pop duniani Michel Jackson, ametangaza ya kuwa atafaya onyesho lake la mwisho la kimziki nchini Uingereza wakati wa kipindi cha baridi kuisha barani Ulaya (Summer time).
Akiongea hayoa mbela ya wapenzi wake wa muziki, Michel Jackson, malisema ataimba nyimbo ambazo wapenzi wake wanazipenda na roho za wapenzi zitakongwa hadi mwisho wa onyesho hilo.
Kwa mujibu wa mtayarishaji wa onyesho hilo, Rob Hallet,alisema tiketi zitauzwa kwa kwa bei ambayo kila mpenzi wa Michael ataweza kununua.
Alisisitiza kwa kusema tiketi zitaanzia paudi 50 hadi Paundi 75.
Picha hapo juu anaonekana, bingwa wa muziki wa Pop, Michael Jackson akifanya vitu vyake katika muziki wa Thriller, muziki ambao ulimletea sifa kubwa ulimwenguni.
Picha ya pili, naonekana bingwa wa muziki wa Pop, Maichael Jackson akiwaaga wapenzi kwa kuwaonyesha vidole viliwili, mara baada ya kutangaza uamuzi wake wa kufanya onyesho la mwisho mjini London Uingereza, wakati wa kipindi cha jua.(Summer time) mwaka huu 2009.
Dunia ina siku 100,kabla ya kuangamia." Mwana wa Malkia
London, Uingereza - 08/03/09. Mwana wa Malkia Elizabeth wa Uingereza, Prinsi Charles, atauhutubia viongozi na wafanya biashara jijini Rio de Jeneiro nchini Brazil wiki ijayo.
Katika mkutano huo, Prinsi Charles, atawaelezea viongozi hao na wafanya biashara ya kuwa tunazo siki chache kuikomboa dunia katika janga la ukame, na uaharibifu wa mazingira.
Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya ufalme, Prinsi Charles atasisitiza saana kufanya kila njia kuikomboa dunia, kwai kwa mtazamo wake tunazo kama siki 100, kabla ya mazingira ya dunia kuaribika.
Akiwa ziaran katika nchi za Amerika ya Kusini, atatembela nchi za Chile,Equado na kisiwa cha Galapogos.
Picha hapo juu ni ya Prinsi Charles, ambaye anatatarajiwa kuwaomba viongozi wa duinia kuikomboa dunia, ambayo mazingira yake yapo hatarini.
Morocco ya vunja uhusiano na Iran"Imani ya Madhehebu yaleta mgogoro".
Rabat,Morocco - 08/03/09. Serikali ya Morocco imefunga uhusiano wa kibalozi na serikali ya Iran, kwa kile kinacho daiwa na serikali ya Morocco, ya kuwa serikali ya Iran, kuingilia maswala ya ndani ya nchi.
Kwa mujibu wa msema wa wizara ya mabo ya nje wa Morocco alisema, uhusiano na Iran, umevujwa tangu ijumaa 06/03/09.
Uhusiano wa Morocco na Iran umekuwa wakaeribu saana tangu mwanzo wa miaka ya 1990.Hadi hivi karibuni, baada ya yakuonekana ya kuwa kuana njama za kuendeleza wa Uislaaam wa Kishia nchini Morocoo, nchi ambapo nchini Morocco waumini waliowengi ni wa Waislaaam wa Suni.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Iran, nchi ambayo ina waumini wengi Waislaam Washia.
Picha ya pili, ni bendera ya Morocco, nchi ambayo ina waumuni wengi Waislaam Suni.
Ajali ya waziri mkuu wa Zimbabwe ni ajali kama ajali nyingine."Ubalozi wa sema"
Harare,Zimbabwe - 08/03/09.Ajali ya gari iliyokuwa imembeba waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai, kugongwa na lori la mizigo la USAIDA (United State Agency For International Development), haikuwa ajali ya kupangwa, ilikuwa ajali ya kama ajali nyingine zinavyotokea.
Kwa mujibu wa ofosi za ubalozi wa Uingereza, mjini Harare, zinasema lori hilo la mizigo, lilikuwa ni moja ya malori ya nayo tumiwa na serikali ya Uingereza kwa kushirikiana na serikali ya Amerika katika kutoa msaada kwa jamii.
Ajali hiyo ambayo ilitokea siku ya ijumaa, ilisababisha kifo cha mke wa waziri mkuu bi Suzan Tsvangirai, na waziri mkuu Morgan Tsvangirai na dereva wa gari hilo kupata majera kiasi.
Picha hapo juu, linaonekna gari lilolo mbeba, waziri mkuu wa Zimbabwe,likiwa libebinuka matairi juu,mara baada ya kupata ajali ya kugongwa na lori.
Picha ya pili, ni marehemu Bi Suzan Tsvangirai,amabye alipoteza maisha katika ajali ya gari, baada ya kugongwa na roli la USAID.
Picha ya tatu wanaonekana, waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai akicheza ngoma za asili na mkewe marehemu bi, Suzani wakati wa kampeni ya uchaguzi mkuu nchini Zimbabwe.
Picha ya tatu, anaokana rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, akiongea na waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, wakati alipo kwenda kumtembelea hospitali.
Amerika na Talibani kukaa meza moja.
Washington,Amerika - 08/03/09. Serikali ya Amerika huenda ikaanza kuongea na baadhi ya viongozi wa kundi la Taliban, ambao wanamwelekeo wa kati.
Akiyaongea hayo rais , Baraka Obama, aliyasema hayo, kabla ya makamu wa rais wa Amerika , Joe Biden, kuanza ziara ya katika bara la Ulaya, ili kukutana na viongozi kujadili hali ya Afghanistan.
Wakati huo huo, ofisi za ilikulu ya Amerika, zimesema, rais Baraka Obama, huenda akafanya ziara ya kiserikali nchini Uturuki mnamo mwezi wa nne mwaka huu 2009.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Amerika, Baraka Obama, akiongea hivi karibuni na waandishi wa kuhusu hali msimamo wa serikali yake hasa katika maswala yanoyo sera za kigeni.
Picha ya pili wanonekana wapiganaji wa jeshi la Amerika wakiwa wamepumzika, huku wakijipoza kwa sigara, baada ya ya kazi ngumu ya kupambana na kundi la Taliban nchi Afghanistan.

Wednesday, March 4, 2009

Rai wa Sudan atakiwa akamatwe"Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa nchi kushitakiwa akiwa madarakani".

China ya ongeza matumizi yake katika sekta ya kijeshi. Beijing, China - 04/03/09. China imeongeza matumizi yake katika sekta ya kijeshi kufikia kiasi cha US $ 70.24 billion, ili kudumisha hali ya ulinzi na usalama. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, Li Zhaoxing alisema, China haita leta hali ya hatari na wala kutishia nchi yoyote,kwani matumizi hayo ni kwajili ya Wachina na usalama wao. Kufuatia hali ya China, kuongeza matumizi yake katika fani ya kijeshi, kunafuatia repoti iliyo tolewa na serikali ya Amerika ya kuwa China inaongeza matumizi yake kwenye sekta za kijeshi,hivyo inatakiwa kuwa wazi . Picha hapo juu wanaonekna wanjeshi wa China, wakiwa wanakula kwata, kati ya moja ya sherehe za kitaifa. Rais, Abbas na Bi Hillary Clinton, wakutana mjini Ramallah. Ramallah,Palestina - 04/03/09.Rais wa mamlaka ya Palestina , Mahamoud Abbas,amekutana na waziri wa mabo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton. Katika mkutano hu uliofanyika mjini Ramallah,Bi Hillary Clinton,alisema ya kuwa serikali ya Amerika ina muunga mkono rais Abbas,na serikali yake ndiyo inayo tambulika, na hivyo Amerika itajitahidi kwa kila hali kuleta amani, na kufikia lengo la kuwa na taifa la Wapalestina watakao ishi jirani na taifa la Izrael. Picha hapo juu wanaonekna, rais wa taifa la Palestina, Mahamoud Abbas kulia huku akiwa anatabasamu na kwa upande wa kushoto, ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton, wakati walipo kutana mjini Ramallah kujadili hali halisi ya eneo hilo. Rais wa Sudan atakiwa akamatwe" Hii ni mara ya kwaza kwa rais wa nchi kushitakiwa akiwa madarakani". Den Haag, Uhollanzi - 04/03/09.Mahakama ya kushughulikia kesi za makosa ya kimataifa, imetoa kibali cha rais wa Sudan Omar Al Bashir, akamatwe ili kujibu mashitaka. Kwa mujibu wa masemaji wa mahakama hiyo, rais Al Bashir, anakabiliwa na makosa ya kukuika haki za binadamu, na kuhusika kutokuwa na hali ya usalama kwenye eneo la Darfur, ambalo ni moja ya jimbo la nchi ya Sudan. Hata hivyo ,serikali ya Sudan, imesema haitambui kibali hicho cha kukamatwa kwa rais Al bashir, na haitashirikiana na mahakama hiyo. Picha hapo juu anaonekana rais wa Sudan, Omar Al Bashir, akisalimia wananchi, wakati akiwa katika ukaguzi wa maendeleo ya nchi hivi karibuni.

Tuesday, March 3, 2009

Ulimwengu wa mchezo wa kriket waingia dao kubwa nchini Pakistan

Mke wa rais afungwa jela miaka mitatu. Lusaka, Zambia - 03/03/09. Mke wa rais wa zamani wa Zambia Frederick Chiluba, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na nusu, baada ya kukutwa na hatia ya kupokea pesa kinyume cha sheria. Ka mujibu wa mahakama,Bi Regina Chiluba,alipokea pesa hizo za serikali na kuzitumia kwa kujengea nyumba na kufanyia biashara wakati mume wake alipo kuwa rais. Wakati wa hukumu hiyo, rais huyo wazamani wa Zambia, Frederick Chiluba, alikuwepo mahakani, Hata hivyo rais huyo wa zamani wa Zambia, anakesi inayo mkabili kwa kutumia vibaya pesa za umma wakati akiwa madarakani. Picha hapo juu wanonekna, rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba na mkewe bi Regina Chiluba, wakiwa mahakamani siku chache kabla ya hukumu ya kwenda kutumikia kifungo cha miaka kwa miaka mitatu na nusu kwa bi Regina Chiluba kutolewa leo 03/03/09. Ulimwengu wa mchezo wa kriket waingia doa kubwa nchini Pakistan.

Lahore, Pakistan - 03/03/09.Wapakistan sita wamepoteza maisha yao na wachezaji sita wa timu ya Kriket ya Sri Lanka,kujeruhiwa vibaya baada ya watu wasiojulikana kushambulia msafara huo wa wachezaji karibu na uwanja wa Gaddafi, wakati tumu ya Pakistan ikicheza na Sri Lanka.
Mashambulizi hayo yaliyo fanywa kwa kutumia bunduki na pia kulipatikana bomu la kutupa kwa mkono ambalo halikulipuka.
Salman Taseer, mkuu wa jimbo la Punjab, alisema mashambulizi hayo yanafanana kama yale yaliyo tokea jijini Mumbai.
Picha ya hapo juu wanaonekana, polisi wa kiangalia kwa makini, kwenye kiti cha gari la polisi, ambalo lilishambuliwa wakati likisindikiza msafara wa wachezaji wa kriket wa timu ya Sri Lanka.
Picha pili hapo juu, wanaonekana kwa mbali baadhi ya watu wakiwa wameshilikia mitutu(bunduki) kuelekeza eneo la tukio.
Waziri mkuu wa Uingereza afanya ziara rasmi nchini Amerika.
Washington, Amerika - 03/03/09.Waziri mku wa Uingereza , Gordn Brown, amefanya ziara rasmi nchini Amerika, kwa mazungumzo ya kiserikali.
Waziri mkuu, Gordon Brown, amekuwa kiongozi wa kwanza, kufanya ziara nchini Amerika tangu rais, Baraka Obama, kuapishwa kuwa rais wa Amerika.
Ziara hiyo, imefanyika mapema, kabla ya kikao cha wakuu wa nchi 20 , kuudhulia kikao kitakacho fanyika njini London April 2 mwaka huu 2009.
Pichani hapo juu, wanaonekana rais, Baraka Obama na waziri mkuu wa Uingereza, wakisalimiana, mapema baada ya waziri mkuu, Gordon Brown kuwasili nchini Amerika.
Bi, Hillary Clinton, atembelea Izrael kwa mazungumzo.
Jerusalem,Izrael -03/03/09. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi, Hillary Clinton, amefanya mazungumzo viongozi wa Izrael,na kusisitiza yakuwa Amerika itashirikiana na Izrael kwa kila hali.
Hata hivyo , Bi, Hillary Clinton, alisisitiza ya kuwa swala la kuwepo kwa taifa la Palestina, ni njia moja ambayo Amerika inaliona ndiyo njia pekee ya kutatua mgogoro wa eneo hilo.
Picha hapo juu, anaonekana na mmoja wa viongozi wa Izrael , bwana, Benjamin Tetanyahu, wakati walipo kutana kwa mazungumzo.
Picha ya pili anaonekana rais wa Izrael, Shimon Peres na waziri wa mambo ya nje wa Amerika, Bi, Hillary Clnton kabla ya kuanza mazungumzo.

Monday, March 2, 2009

Rais wa Guinea Bissau, auwawa na wanajeshi"Hausishwa na kifo cha mkuu wa Jeshi"

Wafadhili na Wahisani wakutana kuchangisha ili kuijenga upya Ukanda wa Gaza.

Sharm El Sheikh,Misri - 02/03/09.Wafaziri na Wahisani wanakutana nchini Misri, kwa ajili ya mkutano wa kuchangisha pesa za kuijenga upya Ukanda wa Gaza.
Akiongea hayo, rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas,amesema ujenzi wa Ukanda wa Gaza utahitaji zaidi ya $ 5billion.
Akiongea na washiriki, Wahisani na Wafadhili, rais,Mahmoud Abbas,alisema yakuwa Wapalestina wataungana katika kuijenga maeneo yao.
Wahisani na Wafadhili hao, wanaotoka nchi 40, wanakutana mjini Sharm El Sheikh, wamesema pesa zote zitakazo tolewa zisipitie kwenye mikono ya Hamas.
Picha hapo juu, anaonekana waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Bi Hillary Clinton, akisalimiana na katibu mkuu wa Muungano wa Ulaya, bwana Javier Salana,wakati alipo wasili mjini Sharm El Shekh.
Picha ya pili ni ya moja ya jengo likiwa limebomolewa vibaya, kutokana na vita vilivyo tokea mwisho wa mwaka 2008 hadi mapema 2009 katikati ya mwezi wa Januari.
Rais wa Malawi, akamatwa na polisi.
Lilongwe, Malawi - 02/02/09. Polisi nchini Malawi, wamemkamata aliyekuwa rais wa nchi hiyo, bwana Bakili Muluzi, kwa kushukiwa kutumia pesa zipatazo million 11, pesa zilizo tolewa na wahisani.
Rais, Bakili Muluzi,ambaye alitawala Malawi tangu mwaka 1994 hadi 2004, analaumiwa kwa kuzitumia pesa hizo kwa matumizi yake binafsi.
Kesi ya mauaji ya, Rafiki Hariri, yafunguliwa nchini Uhollanzi.
The Hague,Uhollanzi - 02/03/09.Umoja wa mataifa, umefungua koti ya kimataifa itakayo shughulika kesi ya mauaji ya aliye kuwa waziri mkuu wa Lebanoni, Rafiki Hariri.
Waziri mkuu, Rafiki Hariri, aliuwawa kwa bomo mnamo tarehe, 14/02/05 na watu wengine 22 walipoteza maisha yao pia.
Kuuwawa kwa bwana , Hariri, kulisabababisha Syria, kujiondoa toka Lebanoni,baada ya kuwepo nchini humo kijeshi kwa miaka mingi.
Picha hapo juu, linaonekana moja ya gari likiwa limeshika moto,baada ya kulipuliwa na bomu, na kutokana na ajari hiyo, waziri mkuu, Rafiki Hariri alipoteza maisha.
Picha ya pili, anaonekana hayati, waziri mkuu wa Lebanoni, enzi za uhai wake.
Rais wa Guinea Bissau,auwawa na wanajeshi "Hausishwa na kifo cha mkuu wa Jeshi".
Bissau, Guine Bissau - 02/03/09. Rais wa Guinea Bissau,Joao Bernardo Vieira,ameuwawa kwa kupigwa risasi wa wanajeshi wakati akiwa nyumbani kwake mapema leo hasubuhi, 02/03/09.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, Zamora Induta, alisema mauaji haya yamefanyika na wanajeshi wa karibu wa aliyekuwa mkuu wa majeshi, Generali Tagme Na Waie, aliye uwawa mapema siku ya jumapili, baada ya risasikwa kufyatuliwa na mlipuko wa bomu kutokea karibu na eneo alilo kuwa amekaa.
Hata hivyo, msemaji huyo wa jeshi, alisema yakuwa , rais,ni moja ya watu waliohusika katika mauaji ya Generali,Tagme Na Waie.
Picha hapo juu, ni ya rais wa, Guinea Bissau, Joao Bernardo Vieira,anaonekana enzi za uhai wake, akitoa saluti , wakati jeshi lilipo pita mbele ya katika moja ya sherehe za kitaifa.
Kemikal Ali - (Chemical Ali) ahukumiwa kunyongwa.
Baghdad,Irak-02/03/09.Jaji wa mahakama kuu nchini Irak, Mohammed Al Uraibi, amemuhukumu kunyongwa aliyekuwa aliyekuwa waziri wa ulinzi, wakati wa hayati rais Saddam Hussein, bwana Ali Hassan Al Majid.
Bwana, Ali Al Majid, aliyejulikana kama Kemikal Ali(Chemical Ali),alihukumiwa kunyongwa baada ya hakimu,Mohammed Al Uraibi, kumkuta na hatia ya kuu ruhusu mauaji ya Wairak wa jamii ya Kishia mnamo mwaka 1999.
Picha hapo juu,anaonekana, bwana, Ali Al Majid ( Chemical Ali), akijieleza mbele ya jaji, kabla ya kkuhukumiwa kunyongwa.

Thursday, February 26, 2009

Fedha za rais wa Gabon zafilisiwa nchini Ufaransa.

Fedha za rais wa Gabon zafilisiwa nchini Ufaransa.

Paris,Ufaransa - 27/02/09. Uongozi wa serikali ya Ufaransa, umefirisi fedha za rais wa Gabon, Omar Bongo Ondimba,
Uamuzi wa kufirisi fedha zake umekuja baada ya koti iliyopo Bordeaux kutoa uamuzi wa kutaka rais, Omar Bongo, kulipa fedha zilizo ingia kwenye akaunti yake, ili mfanya biashara wa Kifaransa, Rene Cardona aachiliwe kutoka jela.
Pesa zipatazo Us-$580,000, zilitolewa na mtoto wa mfanya biashara huyo, ili babayake aachiwe kutoka jela.
lakini hata hivyo koti, iliamua ya kuwa fedha hizo zilitolewa kinyume cha sheria, na kuamuliwa zirudishwe mara moja.
Picha hapo juu anaonekana rais, wa Gaboni, Omar Bongo Ondimba, akicheza muziki kusherekea miaka 70, tangu kuzaliwa kweke.
Picha ya pili anaonekana,rais, Omar Bongo, alipo kuwa moja ya mikutano ya kimataifa hivi karibuni.
Syria na Amerika kuanza mazungumzo hivi karibuni.
Washington, Amerika 27/02/09 - Ofisi ya Syria kwenye umoja wa Mataifa, imesema yakuwa serikali ya Amerika na Syria zitaanza mazungumzo hivi karibuni ili kujadiri hali ilivyo mashariki ya Kati.
Mazungumzo hayo yata wakutanisha balozi wa Syria wa nchini Amerika na viongozi wa Amerika wanaoshughulikia maswala ya mashariki ya Kati.
Katika mkutano hu watazungumzia swala la amani na hali halisi ya Mashariki ya kati kwa ujumla.
Picha hapo juu inaonekana bendera ya nchi ya Syria, nchi ambayo imekuwa inalaumiwa na Amerika kwa kujihusisha na kuyumba kwa hali ya usalama katika eneo hilo, hasa kwa kuunga mkono makundi ya Wapalestina ya nayo pingana wa Waizrael.
Picha ya pili, ni ya bendera ya Amerika, nchi ambayo imekuwa haina uhusiano mzuri na nchi ya Syiria.
CIA yasema Kim Jongo Il, bado ashikilia uskani.
Pyongyang,Korea ya Kaskazini - 27/02/09.Shirika la Kijasusi la Amerika -CIA- limesema ya kuwa kiongozi wa Jamuhuri ya Korea ya Kaskazini,Kim Jong Il, bado anaongoza nchi, japokuwa imeripotiwa hali yake ya afya siyo nzuri.
Haya yalisemwa na Leon Panetta wakati alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari, kuhusu nia ya Korea ya kaskazini, kutaka kurusha mizimga ya ke ya masafa marefu kwa majaribio.
Picha hapo juu anaonekana kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Kim Jong Il,akiongea na baadhi ya viongozi wa Korea ya Kaskazini,kabla ya kuwa kwenye matibu kwa kipindi kilefu sasa.
Vyama vya Wapalestina kukubaliana kushirikiana kimsingi.
Kairo,Misri - 27/02/09. Makubaliano ya kimsingi yamefikiwa kati ya vyama pinzani vya Fatah na Hamas ambayo vinaongoza Wapalestina ili kujadili jinsi gani vinaweza shirikiana.
Baada ya mkutano huo uliofanyika Misri, mmoja ya kiongozi wa Fatah,Ahamed Qurei, alisema uamuzi huo ni kwa ajili ya Wapalestina wote waishio Ukanda wa Gaza na West Bank.
Hata hivyo, kiongozi huyo akuelezea kiundani zaidi nini makubaliano yapi watajadili.
Picha hapo juu, ni ngao ya bendera ya Fatah, chama ambacho kimekuwa kikipigania haki za Wapalestina tangu kianzishwe mwaka 1954.
Picha ya pili ni ya ngao ya chama cha Hamas, chama ambacho kimekuwa kikipigania Wapalestina, huku kikiwa na mwelekeo tofauti na Fatah.

Wednesday, February 25, 2009

Ajari ya ndege yatokea nchini Uhollanzi.

Amani ya Somalia ni mthiani mgumu kwa Jamii ya kimataifa.

Mogadishu, Somalia - 25/02/09.Watu wapatao 48, wameuwawa,huku vita vikendelea katika maeneo ya jiji Somalia kati ya makundi ya kijeshi kwa kushirikiana na jeshi la Muungano la Afrika na kundi kubwa la Al Shabab.
Katika vita hivyo wanajeshi wa muungano wa jeshi la Afrika, pia limewapoteza wanajeshi wake sita ambao wanatokea nchini Burundi.
Kufuatia hali hii, inampa wakati mgumu, rais mpya wa Somalia, Sharif Ahmed, kuweza kuunda serikali ya muungano.
Picha ya hapo juu wanonekana, baadhi ya wanajeshi wa wa muungano wa Afrika, wakiwa katika doria.
Picha ya pili wanonekana baadhi ya wapiganaji wa moja ya kikundi kinacho pinga serikali ya ya Somalia wakiwa katika moja ya maeneo yao,huku wakiwa wamebeba siraha tayari kwa vita pindipo vikitokea.
Ajari ya ndege yatokea nchini Uhollanzi.
Amsterdam,Uhollanzi-2/02/09.Watu wapatao tisa, wamepoteza maisha baada ya ndege ya shirika la Usafiri la Uturuki kuanguka,nchini Uhollanzi karibu na kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Amsterdam.
Katika ajari hiyo, watu wengine wapatao 50, wamajeruhiwa vibaya kati ya abiria 135 walio kuwemo kwenye ndege hiyo.
Ndenge hiyo namba TK1951, iliyo kuwa ikitokea jijini Instambul kuelekea Amsterdam, ilipotea njia ya kutulia na kuanguka na kukatika vipande vitatu.
Hata hivyo, wataalaam wa mambo ya usalama wa ndege wanaendelea na uchunguzi kujua nini chanzo cha ajali hiyo.
Picha hapo juu, inaonekana ndege ya shirika la ndege la Uturuki, ikiwa imeharibika vibaya sehemu za nyuma ya ndege hiyo.
Picha ya pili ineonesha, ndege ikiwa imeanguka karibu na maeneo ya makazi ya wanachini

Friday, February 20, 2009

Kesi ya aliyemrushia kiatu aliyekuwa rais wa Amerika ya hairishwa.

Papa wapunguza mashambulizi kwa binadamu"Wasema wataalaamu".

Frolida, Amerika - 20/02/09.Wataalamu wa tabia ya viumbe viishivyo baharini ,wamesema mashambuli ya papa kwa binadadmu yamepungua kwa kiasi kikubwa katika mwaka 2008kwa kulinganisha miaka mitano iliyo pita.
Akiongea hayo, mwanasayansi anayeshughulikia tabia za papa, alisema mwaka 2008, papa walipunguza mashambuli kwa binadamu,kwani ni watu wawili walipoteza maisha kutokana na kujeruhiwa na papa, nchini Mexico, Amerika mmoja na Australia mmoja.
Picha hapo juu anaonekana papa, akiwa amemza binadamu maara baada ya kushambulia.
Picha ya pili, anaonekna papa, akiluka juu ya maji tayari kushambua kitu chochote anacho hisi kipo mbele yake.
Kesi ya aliye mrushia kiatu aliyekuwa rais wa Amerika ya hairishwa.
Baghdad,Irak-20/02/09. Wanachi wa Irak, wamshuhudia Muntedar al Zaidi mwenye miaka 30, akifikishwa mahakamani kwa kosa la kumtupia kiatu aliyekuwa rais wa Amerika, George Bush, wakati alipo fanya ziara nchini Irak, kabla ya muda wake wa kuwa rais wa Amerika kuisha.
Muntader al Zaidi, alifika mahakamani, hasubuhi ya siku ya alkhamis 19/02/09, huku akishuhudiwa na ndugu ,jamaa, marafiki, wanasheria, wanasiasa na wanchi wengine.
Katika kesi hiyo,watu walisikika wakipiga kelele, ambazo zilimpa wakati mgumu hakimu na kuchukua muda zaidi ya saa na dakika 15.
Hata hivyo, hakimu alihairisha kesi hadi 12/machi/2009
Zimbabwe yaitaji billion 5$- dola,"Asema waziri mkuu"
Harare,Zimbabwe - 20/02/09. Waziri mkuu mpya wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, amesema,ili kujenga na kunyanyua uchumi wa Zimbabwe,kunaitajika zaidi ya billion 5$ - dola.
Na hii inaitakuja kutoka na vitega uchumi vitakavyo wekwa na wawekezaji.
Waziri mkuu, huyo wa Zimbabwe, aliyasema haya wakati alipo kuwa baada ya kukutana na rais wa Afrika ya Kusini na waziri wa fedha,ili kujadili ni njia zipi zita tumika kusaidia kunyanyua haraka uchumi wa Zimbabwe.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Zimbabwe, nchi ambayo imekuwa katika hali mbaya ya kiuchumi tangu kuanza matatizo ya kisiasa,baada ya uchaguzi mkuu wa uliofanyka mapema mwaka 2008.
Picha ya pili anaonekana waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, akiongea huku akiangali kwenya faili lake lililo juu ya kijukwaa, nakujaribu kuafafanua kwa undani, huku akionyesha mikono juu, kuashiria hali ya uchumi ya Zimbabwe, inahitaji kujengwa upya.
Kiongozi wa Likud, Benjamin, Netanyahu, atakiwa kuunga serikali.
Jerusalem, Izrael- 20/02/09 - Rai wa Izrael, Shimon Peres, amembomba kiongozi wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu kuunga serikali ya muungano kwa muda usiopungua wiki sita.
Rais, Shimon Peres, alimuomba, bwana Benjamin Netanyahu, wakati walipo kutana, na baadaye kuongea katika mkutano uliofanyika Jerusalem.
Katika, mkutano huo, bwana, Benjamini Netanyahu, aliwaomba viongozi wa vyama pinzani kuungana kwa pamoja, ili kuweza kuunda serikali kwa ajili ya wana nchi Izrael.
Picha ya hapo juu wanaonekana, rais, Shimon Peres na kiongozi wa chama cha Likud, bwana Benjamin Netanyahu, wakisalimiana muda mfupi kabla ya kuanza mazungumzo.
Picha ya pili, anaonekana, kiongozi wa chama cha Likud, Benjamin Netanyahu, akiongea kwa kusisitiza lazima waungane ili kujenga Izrael.
Tamil Tager washambulia ndani ya jiji la Kolombo"Hali si swali Sri Lanka"
Kolombo, Sri Lanka - 20/02/09. Watu wapatao 50 wamjeruhiwa vibaya na wengine wawili kuuwawa baada ya ndege za kijeshi la kundi la Timil Tiger, kushambulia ndani ya jiji la Kolombo.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Sri Lanka,Kaheliy Rambukwella, alisema yakuwa ndege hizo zilishambulia majengo ya serikali.
Hata hivyo moja ya ndege hizo za kijeshi, ilishambuliwa na ndege za jeshi la serikali.
Mapambano kati ya jeshi la serikali na kundi la Tamil Tiger ambalo linagombani kujitenga na serikali.
Picha hapo juu, zinaonekna gari zikiendeshwa kwa kasi ili kuepuka milipuko, mara ya milipuko kusikika karibu na mojo ya majengo yenye ofisi za serikali.
Picha ya pili ni ramani ya Sri Lanka, nchi amboyo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, tangu mwazo wa mwaka 1983.