Viongozi wa dunia wakubaliana kuikomboa dunia kiuchumi.
Viongozi wa dunia wakubaliana kuikomboa dunia kiuchumi.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, April 02, 2009
0
comments
Mkuu wa Taliban, atangaza hali ya hatari kwa Amerika.
Washington,Amerika - 01/04/09 - Serikali ya Amerika imetangaz itatoa zawadi ya dola za Kiamerika $ 5 million, kwa mtu atakaye toa habari wapi alipo kiongozi wa Taliban, Baitullah Mehsud, ambaye ametangaza kuwa kundi lake litashambulia Amerika na kuishangaza dunia.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana, zinasema yakuwa kiongozi huyo wa Taliban, alisema ya kuwa kundi lake ndili lililo husika na ulipuaji wa kituo cha polisi mjini Rahore, siku ya jumatatu.
Baitatullah Mehsud, anashukiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Pakistani Bi Benazir Bhutto, na mashambulizi yaliyo tokea katika hotela ya Marriot iliyopo Islamabad.
Na inaaminika anauhusiano wa karibu na kundi la Al Qaeda.
Picha hapo juu ni ya, Baitullah Mehsud, ambaye anatafutwa akiwa hai au amefariki na serikali ya Amerika kwa kuwekewa zawadi ya US dola $ million 5 kwa mtu atakaye toa habari zake ili akamatwe.
Hatimaye Israel yapata waziri mkuu mpya.
Jerusalem, Israel - 01/04/09.Benyamin Netanyahu, ameapishwa rasmi kuwa waziri mkuu wa Israel, baada ya kupata baraka kutoka kwa bunge la nchi hiyo.
London,Uingereza - 01/04/09.Rais wa Amrika Baraka Obama, ameanza ziara katika nchi za Ulaya na ataudhulia mkutano wa kiuchuni ambao umeandaliwa na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown.
Doha,Katar - 31/03/09.Viongozi Latini Amerika na viongozi wa jumuia nchi wanachama wa nchi za Kiaarabu,wamekutana ili kujadili maendeleo na ushirikiano wakaribu.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, April 01, 2009
0
comments
Wapenzi wa soka wapotezamaisha"Fifa yataka maelezo".
Abdjan, Ivory Coast - 30/03/09. Zaidi ya watu 22 wamepoteza maisha baada ya kukanyagana wakati walipotaka kuingia uwanjani kuangalia mpira kati ya timu yao ya taifa na timu ya taifa ya Malawi katika kinyanganyiro cha kugombea nafasi ya kuingia katika fainali ya kombe la dunia litakalo fanyika nchini Afrika ya Kusini mwakani.
Mogadishu, Somalia - 30/09/09. Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia Abdirahman Ali, amenusurika kupoteza maisha baada ya gari alilo kuwa akisafiria kukanyaga bomu na kulipuka na kupoteaz maisha ya walinzi wake katika kitongoji kimoja katika mji wa Mogadishu.
Doha, Katar - 30/03/09. Mkutano mkuu wa kuwakutanisha viongozi na marais wa nchi wanachama wa nchi za Kiaarabu, umeanza rasmi nchini Katar, ili kutafuta ni jinsi gani nchi hizi zita weza kutatua matatizo yanayo zikabili nchi zao.
Rahore,Pakistan - 30/03/09 - Mashambulizi yametokea katika kituo cha kufunzia polisi kilichopo Rahore na kusababisha mauaji na majeruhi ya polisi walio kuwa katika majengo hayo.
Phnom Penh, Kambodia - 30/03/09.Mahakama ya ualifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa iliyopo nchini Kambodia, imeanza kusikiliza kesi ya mauaji ya kimbari yaliyo fanyika mapema miaka ya 1970s, ambapo zaidi ya watu wapatao million 1.7 waliuwawa na baadhi ya viongozi wa kundi la Khmer Rouge.
Posted by
Kibatala
at
Monday, March 30, 2009
0
comments
Rais wa Brazil, azilaumu nchi tajiri kwa mporomoko wa uchumi.
Moscow, Urussi-28/03/09.Serikali ya Urussi, imesema ipo ytayari kushirikiana na NATO,ili kuijenga Afghanistan.
Kartoum,Sudan-28/03/09. Serikali ya Sudan,imesema huenda mashambulizi yaliyo fanywa katika eneo moja lililopo kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, lilifanywa na Israel na kupoteza maisha ya watu 40.
Tokyo, Japan-28/03/09.Serikali ya Japan, imepitisha amri ya kulitaka jeshi la ulinzi wa anga kujiandaa kuzuia chombo cha anga kitakacho rushwa na Korea ya Kaskazini.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, March 29, 2009
0
comments
Mchezaji wa mpira wa miguu apigwa risasi kiwanjani.
Beijing, China, 22/03/09.Makubaliano kati ya China na Muungano wa Ulaya, kuhusu ujenzi wa pamoja wa chombo cha kuruka angani Galileo, kutoleta zao mafanikio, yameifanya China kuamua kujenga chombo chakuruka angani peke yake .
Jerusalem. Israel 22/03/09.Habari zinazo endele kutolewa na baadhi ya askari wa jeshi la Israel, kuhusu hali halisi ya vita kati ya Israel na Palestina, mapema mwisho wa mwaka 2008 hadi mwazo wa mwaka 2009, zinazidi kuleta hali ya wasiwasi na mvutano hivyo na kuleta mjadala mkubwa katika jamimii nzima ya Israel na kuhusu imani na ulinzi wa nchi.
Hii ina kuja baada ya ya baadhi ya watu kujadili kuwepo kwa vita hivi kwani vinakwenda kinyume na matakwa ya kidini,na wengine wana sema hii ni lazima kulinda taifa la Israel,kwani ni taifa teule na ni lazima walilinde kwa hali na mali.
Khartoum,Sudan 22/03/09. Shule moja ya kidini nchini Sudan imemshauri rais wa Sudan,Omar Al bashir , kuto safiri nchini Katar, kuhudhuria mkutano wa nchi wanachama wa jumuia ya nchi za nchi za Kislam unaotarajiwa kuanza 30,03/09.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, March 22, 2009
0
comments
Nchi zaanza kulegeza vikwazo nchini Zimbabwe."Misaada yaanza kutolewa".
Stockholm, Sweden - 21/03/09.Serikali ya Sweden, imesema itatoa kiasi cha million $ 10.5 kwa serikali ya Zimbabwe, kwa ajili ya kusaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu.
Tehran,Iran 21/03/09.Kiongozi mkuu wa Iran,Ayatollah Ali Khamenei, amesema yakuwa Iran ipo tayari kushirikiana na Amerika, ikiwa Amerika itabadilisha mwelekeo wake kuhusu Iran.
Darfur,Sudan 20/03/09. Mmoja ya walizni wa amani kwenye maeneo ya Darfur, amepigwa risasi na kufa wakati wakiwa ulinzi kwenye kwenye maeneo ya Nyala.
Prague,Czech -20/03.09.Viongozi wa muungano wa Ulaya, wamekubaliana kwa pamoja kuongeza mara dufu, fedha ili kuinua hali ya kiuchumi inalo likabili bara hili.
Viena,Austria - 20/03/09.Mahakama ya mji wa St Poelten, imemuhukumu kifungo cha maisha Josef Fritzl mwenye miaka 73, kwa kumkuta na hatia ya kumteka nyara, kumfanya mtumwa na kumweka kinyumba mtoto wake wa kike kwa kipindi kisicho pungua miaka 24 na kumzalisha watoto na mmoja ya watoto hao kufa kutokana na kukusa matibabu.
Posted by
Kibatala
at
Saturday, March 21, 2009
0
comments
Jaji arudishwa ofisini" Maandamano na siasa za mvutano bado nchini Pakistan.
Lahore,Pakistan-18/03/09.Kurudishwa madarakani kwa aliyekuwa jaji mkuu wa zamani wa Pakistan, Iftikhar Chaudhry, kumeleta hali ya joto katika siasa ya Pakistan.
Antananarivo, Madagasca-Mahakama nchini Madagasca,imepitisha Andy Rajoelina kuwa rais wa Madagasca, siku moja baada ya kupewa madaraka ya kuwa rais wa nchi hiyo.
Moscow, Urussi- 18/03/09.Rais wa Urussi, Dmitry Medvedev, ameagiza ongezeko la kujenga na kuimarisha nguvu za kijeshi la Urussi lifanyike ili kukabilina na ongezeko la nguvu za NATO.
Prague,Czeck-18/02/09.Serikali ya Czeck imetangaza kusimamisha mpango wake wakuirusu serikali ya Amerika, kujenga mitambo ya kunasia mawasiliano na mitambo mingine ya kijeshi.
Yaounde,Kameroon-17/03/09.Papa Benedict wa XVI, amewasili nchini Kameroon, ikiwa ni moja ya ziara yake katika bara la Afrika.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, March 18, 2009
0
comments