Wapalestina na Waizrael bado kukubaliana kimsingi haki zao
Jerusalem Mashariki, Izrael - 25/10/09. Polisi wa Izrael wamevamia msikiti wa Al Aqsa na kupambana na waumini wa Kiislaam wengi wao wa kiwa Wapalestina.
Kufuatia kuvamia eneo la msikiti huo wa Al Aqsa, waumini wa dini ya Kiislaam wengi ambao ni Wapelestina walianza kutupa mawe na huku polisi wa Izrael wakitumia mabomu ya kutoa machozi.
Kwa mujibu wa shirika la kuktetea haki za binanadamu, limesema ya kuwa kuna baadhi ya watu walikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.
Picha hapo juu anaonekana mmoja wa kijana wa kipalestina akirusha jiwe kuelekea walipo polisi na huku wapiga picha wakiwa kazini kupata picha kamili ya matukio.
Jeshi la serikali la kamata miji iliyokuwa chani ya Taliban.
Islamabad, Pakistan -25/10/09.Serikali ya Pakistan, imetangaza yakuwa imekamata mji wa Kusini mwa Waziristan ambao umezungukwa na milima.
Kwa mujibu wa masemaji wa jeshi, alisema yakuwa waliweza kupambana na kundi la Taliban na mshiriki wake Al-qaed kwa muda wa wiki moja na kufanikiwa kukaribia mji amabo kiongozi wa Taliban, Hakimullah Mehsud.
Kufuatia mapambano hayom, maelfu ya watu wamekimbia maeneo yao kwa ili kuokoa maisha yao.
Picha hapo juu wanaonekana wanachi wakiwa wanakimbia kuepuka kipigo kutoka kwa mmoja wa wanajeshi ambaye ana jaribu kuwatuliza wakimbizi waliokimbia vita vinavyo endelea nchini Pakistan kupambana na ugaidi nchini humo.
Kansellar Angel Markel ateua serikali mpya.
Berlin, Ujeruman - 25/10/09. Kansellar Angel Markel, ametangaza serikali mpya itakaoyo iongoza Ujerumani hasa katika kipindi hiki cha kupapamba na kuinua uchumi wa nchini hiyo.
Serikali mpya chini ya uongozi wa Bi, Angel Markel imeteua Wolfgang Schauble kuwa waziri wa fedha amabye atakuwa na kibarua kigumu cha kujaribu kuangali maswala ya pesa na kupunguza kodi za mapato kuanzia mwezi januari mwakani.
Picha hapo juu, anaonekana Bi, Angel Markel akiongea mbele ya wanachama wa chama chake mapema wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mapema mwaka huu.
Baghdad yashutushwa na hali ya milipuko ya mabomu.
Baghdad,Irak - 25/10/09. Mabomu yamelipuka karibu na ofisi za serikali ya Irak na kupoteza maisha ya watu 108 na kujeruhi watu wasiopungua 512.
Kwa mujibu wa habari , huenda idadi ya watu watakao poteza maisha ikaongezeka kutokana na milipuko hiyo ya mabomu.
Serikali ya Irak, imelaaani kitendo hicho na kudai yakuwa ni kitendo cha kulaani wa na jumuia ya kimataifa na lazima kupigana na hali hii kwa hali na mali.
Picha hapo juu, unaonekana moshi ukielekea juu, baada ya bomu kulipuka karibu na ofisi za serikali.
Sunday, October 25, 2009
Kansellar Angel Markel ateua serikali mpya.
Posted by
Kibatala
at
Sunday, October 25, 2009
0
comments
Friday, October 23, 2009
Uchumi wa China wapata nafuu.
Uchumi wa China wapata nafuu.
Beijing, China 23/10/09. Serikali ya China imetangaza ya kuwa hali ya uchumi wa nchi hiyo umepanda kwa kiasi cha asilimia 8%, kwa muda mfupi tangu dunia kukumbwa na tetemeko la kiuchumi.
Kwa mujibu wa serilikali, kupanda kwa hali ya kiuchumi, kumekuja baada ya matumizi ya nje na ndani kuelekea kufanya vizuri kibiashara.
Picha hapo juu ni ya bendera ya China, nchi ambayouchumi wake na maendeleo yake ya kiuchumi duniani yamekuwa yakienda vizuri.
Wanchi wa Kenya waishitaki Uingereza kwa makosa ya miaaka ya 1950-60s.
London, Uingereza - 23/10/09. Raia wa Kenya watano wameishitaki serikali ya Uingereza kwa kosa la kuwatesa na kuwanyanayasa wakati wa miaka 1950 - 60, wakati wa harakati za kugombea uhuru wa Kenya.
Posted by
Kibatala
at
Friday, October 23, 2009
0
comments
Monday, October 19, 2009
Mwaka 2009 hakuna kiongozi bora wa Afrika.
Mwaka 2009 hakuna kiongozi bora wa Afrika.
London,Uingereza - 19/10/09.Shirika linalo simamiwa na mfanyabiashara mwafrika, Ibrahim Mo, limetangaza mwaka 2009 halitatoa zawadi kwa kiongozi yoyote wa Afrika.
Akiongea leo jijini London, Ibrahim Mo, alisema kamati inayo simamia uchaguzi wa viongozi bora wa Afrika, imekosa kiongozi wa Kiafrika ambaye amekamilisha matakwa ya kiongozi kupewa zawadi na shirika hilo.
Zawadi hiyo hutolewa kwa viongozi wa Afrika ni kiasi cha dola za Kiamerika Milllion tano na dola laki lakimbili killa mwaka hutolewa kimaisha mpaka hapo mteuliwa watakapo aga dunia.
Picha hapo juu anaonekana, Ibrahim Mo, akiongea leo mbele ya wajumbe wa kamati waliokuja kushuhudia ni nani amechaguliwa kuwa kiongozi bora wa Afrika wa mwaka 2009, alitangaza yakuwa mwaka 2009 hakupatikana kiongozi aliye fikisha matakwa ya kuwa kiongozi bora wa Afrika.
Mauji nchini Iran yaleta kushutumiana na nchi majirani.
Kabul,Afghanistan - 19/10/09. Kamati inayosimamia uchaguzi nchini Afghanistan ambayo ipo chini ya Umoja wa Mataifa, imetangaza yakuwa uchaguzi uliofanyika nchini humo ulikuwa na ukiukwaji washeria.
Posted by
Kibatala
at
Monday, October 19, 2009
0
comments
Wednesday, October 14, 2009
China na Urussi kutiliana mkataba wa kibiashara.
Wanajeshi kuongezwa nchini Afghanistan"Waziri mkuu wa Uingereza atangaza".
London, Uingereza - 14/10/09. Waziri mkuu wa Uingereza,Gordon Brown,ametangaza yakuwa serikali ya Uingereza itapeleka wanajeshi wapatao 500, nchini Afghanistan.
Beijing, China -14/10/09. Waziri mkuu wa Urussi, Vladamir Putin, na waziri mkuu wa China Wen Jiabao,wametiliana mkataba wa kibiashara kati ya nchi hizi mbili zenye thamani ya 3.5billion.
Brussel, Ubeligiji - 14/10/09.Muungano wa Umoja wa Ulaya, umetoa wito yakuwa kiongozi wa kijeshi aliopo madarakani chini Guinea, Kaptain, Mussa Kamara, kufikishwa mbele ya sheria ili kukabiliana na mashitaka ya kukiuka haki za kibinadamu, wakati wa kuzuia maandamano,ambayo yaliandaliwa vyama vya upinzani.
Baghdad, Irak 14/10/09.Wizara inayo shughulikia haki za binadamu, imesema watu wapatao 85,000, wamepoteza maisha yao kati ya mwaka 2004- 2008, kutokana na vita vilivyo pelekea kung'olewa madarakani, aliyekuwa rais wa Irak, hayati , Saddam Hussein.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, October 14, 2009
0
comments
Thursday, October 8, 2009
Swala la nyuklia lawa kitendawili.
Swala la nyuklia lawa kitendawili.
Washington, Amerika 08/10/09.Rais wa Amerika, Baraka Obama,amekubali kuiruhusu serikali ya Izrael kuweza kufunga milango yake ya kufanyiwa uvchunguzi wa kinyuklia kwa muda wa miaka 40.
Jerusalem, Izrael - 08/10/09. Mjumbe wa serikali ya Amerika,George Mitchell, ambaye anashughulikia maswala ya kuleta amani, Mashariki ya Kati, kati ya Izrael na Palestina, amekutana na waziri wa mambo yanje wa Izrael leo Avigdor Lieberman.
Kabul, Afghanistan - 08/10/09.Jiji la Kabul, limekubwa tena na mstuko wa bomu, ambalo lililipua ofisi za ubalozi wa India.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, October 08, 2009
0
comments
Saturday, October 3, 2009
Rio de Jainero, wenyeji wa michezo ya Olyimpik 2016"Kwa mara ya kwanza katika udongo wa Amerika ya Kusini.
Rio de Janeiro, wenyeji wa michezo ya Olyimpik 2016."Kwa mara ya kwanza katika udongo wa Amerika ya Kusini".
Copenhagen, Denmark - 03/10/09.Jiji la Rio de Janeiro, limekabidhiwa rasmi kuwa mwenyeji na mwandaaji wa mashindano ya michezo ya Olyimpiki ya mwaka 2016.
Geneva,Uswisi - Serikali ya Iran, imekubali kuruhusu shirika linalo shughulikia ukaguzi wa nyuklia duniani, IAEA, kwenda nchini Iran kuchunguza, kiwanda cha pili kilichopo miji wa Qom.
Jerusalem, Izrael - 03/10/09.Serikali ya Izrael imewaachia huru wanawake 19, ambao ilikuwa imeshikilia kwa muda mrefu.
Paris, Ufaransa - 03/10/09. Serikali ya Ufaransa imeongeza maouzo yake ya silaha kwa kufikia asilimia 13% tangu mwaka 2000..
Posted by
Kibatala
at
Saturday, October 03, 2009
0
comments
Monday, September 28, 2009
Miaka ya 1980s,dunia ingepatwa na mstuko mkubwa.
Miaka ya 1980s,dunia ingepatwa na mstuko mkubwa.
Havana, Kuba 28/09/09.Miaka ya 1980s, ambapo Amerika na Kuba, zilikuwa katika hali ya hatari karibu kupigana kivita,hakukuzaniwa ya kuwa hali hii,ilifikia hadi rais, wazamani wa Kuba ,Fidel Catro kuimba Urussi, kuisaidia Cuba ,kuishambulia Amerika kwa bomu la nyuklia, pindipo vita vitaanza.
Margarita, Venezuela - 28/09/09. Rais wa Venezuela, Hugo Chavez ,amewataka viongozi wa Afrika na Amerika ya Kusini, kushirikiana kikamilifu ili kuepuka kuzitegemea nchi za Ulaya na Amerika.
Konakry,Guinea - 28/09/09. Watu kadhaa wameuwawa na wengine kujeruhiwa baada ya polisi kupamabana na waandamanaji wanaopinga uamuzi wa mkuu wa jeshi, kugombea kiti cha urais
Posted by
Kibatala
at
Monday, September 28, 2009
0
comments
Bi, Angel Markel, kuongoza usukani tena nchini Ujerumani.
Ndugu wawili ,Wakijerumani ndiyo waanzilishi wa makampuni za viatu maarufu duniani.
Furth, Ujerumani - 28/09/09.Kampuni ya viatu ya adidas na Puma, zimetimiza miaka 60 tangu zianzishwe nchini Ujerumani na watoto wa baba mmoja Adi Dassler na Rudolf Dassler.
Rome Itali - 28/09/09. Serikali ya Itali imesema ya kuwa, kundi la mamafia waliopo nchini Itali wamekuwa wakitumia mamba ili kuweza kufanya biashara zao.
Paris,Ufaransa - 28/09/09.Waziri mkuu wa zamani wa Ufaransa, Dominique Villepin, amefungua kesi zidi ya rais wa sasa wa Ufaransa,Nikolas Sarkozy.
Berlin,Ujerumani - 28/09/09. Kansella wa Ujerumani, Bi, Angel Markel na chama chake CDU- Christian Demokrat Union wamshinda uchaguzi mkuu uliofanykia mapema jana jumapili, kuvishinda vyama vingine kwa kupata kura nyingi kwa asilimia 33.8,wakati vyama vya SD - Social Demokrat kilipata asilimia 23 na vyana vingine vilipata asilimia chini ya 20.
Tehran,Iran - 28/09/09.Serikali ya Iran, imejaribu makombora yake ya masafa marefu aina Shabab 3 yenye uwezo ya kwenda km , 2000 namakombora mafupi aina ya shabab 1 na shabab 2 ambayo yanaweza kwenda umbali wa km 300-700.
Posted by
Kibatala
at
Monday, September 28, 2009
0
comments
Thursday, September 24, 2009
Nchi zenye nguvu za kubaliana kupunguza siraha zake za nyuklia.
Nchi zenye nguvu za kukubaliana kupunguza siraha zake za nyuklia.
UN, Amerika - 24/09/09. Kamati ya ulinzi na usalama ya umoja wa Matifa,umekubaliana kwa pamoja kupunguza nguvu za siraha za nyuklia duniani chini ya rais wa Amerika Baraka Obama.
Umoja wa Mataifa, Amerika - 24/09/09. Waziri mkuu wa Izrael, Binyamin Netanyahu, ameuambia yakuwa serikali yake, na Waizrael wote nanacho taka ni kwa Wapalestina kukubali kuwepo kwa taifa la Izrael, ambao wataishi kama majirani.
UN, Amerika - 24/09/09. Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, ameilaumu nchi tajiri na zenye nguvu kwa kusababisha vita, umwagaji wa damu, kukuza ugaidi na kutishia amani, kwenye eneo la Mashariki ya Kati na Afghanistan.
Posted by
Kibatala
at
Thursday, September 24, 2009
0
comments
Wednesday, September 23, 2009
Viongozi wa dunia tukubali kuwajibika"Asema rais ,Baraka Obama"
Viongozi wa dunia tukubali kuwajibika" Asema rais, Baraka Obama"
Umoja wa Mataifa,Amerika - 23/09/09.Rais wa Amerika, Baraka Obama, amewataka viongozi wa dunia, kukubali kuwa tayari na kukabiliana na mageuzi ya dunia ya sasa,kwani ina mapambano makubwa sana.
Akiongea, rais Obama,alisema, nilazima kila kiongozi awajibike,kwani Amerika pekee yake haitaweza kutatua matatizo ya dunia nzima,ambayo yanasababishwa na matatizo yanayo ikabili dunia, na hatimayake kunapelekea kuwepo na watu wenyer itikadi kali na baadeye wanakuwa magaidi, wauwaji , wavurugaji wa amani na umasikini kuongezeka na hata kuharibu hali ya hewa na mazingira yake.
Rais , Obama, alisema tangu kuchukua ofisi,yeye pamoja na uongozi wake wamejitahidi kupambana na ukweli wa hali halisi inayo ikabili dunia ya leo.
Hii ndiyo hali halisi ambayo tunakabiliwa nayo.
Kuhusu, hali ya amani ya Mashariki ya Kati, rais, Obama, alisema yakuwa uongozi wake utajitahidi kwa hali mali kuhakikisha amani inapatikana kati ya Wapalestina na Waizrael.
Kwani wakatai umefika kukuzungumza bila kuwekeana vikwazo wala masharti, kwani wanaoumia ni wanachi wa Izrael na Wapalestina na siyo wanasiasa, "akijionyeshe yeye mwenyewe".
Picha hapo juu, anaonekana rais , wa Amerika, Baraka Obama, akiwahutubia viongozi walioudhulia mkutano wa 64 wa umoja wa Mataifa jijini New York Amerika, ili kujadili hali ya dunia nzima inavyobadirika kimazingira na swala la kuwepo amani duniani kote.
Rais wa Libya Muammar Gaddafi, ashambulia umoja wa matifa, "Adai mabadiliko ya kikatiba ya UN".
UN,Amerika - 23/09/09. Rais wa Libya, Muammar Gaddafi, amelishambuli umoja wa Matifa kwa kusema ya kuwa linakwenda kinyume na katiba ya umoja huo.
Akisisitiza, kwa undani, rais Gaddafi, alisema ya kuwa kamati ya usalama ya umoja wa matifa, haitakiwi kuwa baadhi ya nchi wanachama tu, bali kila nchi mwanachama lazima ihusishwe, kama hakutafanywa hivyo,ni kukiuka katiba ya umoja huu.
Rais, Gaddafi, alisema yakuwa nchi ambazo zina viti vya kudumu, katika kamati ya usalama ya umoja wa mataifa , zina nyanyasa nchi ndogo na masikini,kwa kutumia kura zake za veto,na kwani katiba ya umoja huo,inasema ya kuwa nchi zote ni sawa ndogo hadi nchi kubwa.
Akiongezea, rais Gaddafi, alisema yakuwa,inabidi umoja huu uundwe upya kikatiba ambayio itaipa kila nci hakisawa.
Kuhuusu swala la amani mashariki ya kati,rais Gaddafi,alisema yakuwa Waarabu na Waizrael hawana uadui, bali ni mgongano wa kisiasa unao sababisha kutokuwepo na amani.
Kwa kumalizia, rais wa Libya, Muammar Gaddafi, alisema yakuwa swala la kuleta amani duniani ni la kila kiongozi kuwajibika kikamilifu.
Picha hapo juu, anaonekanana raia wa Libya, Muammar Gaddafi, awaaga viongozi wa nchi waliokuwa wakimsikiliza hotuba yake iliyo chukua saa moja na dakika 27,kuelezea kiundani wa UN.
Lazima tutumize malengo tuliyo yaweka kwenye karne ya 21"Asema katibu mkuu"
Umoja wa Mataifa,Amerika - 23/09/09.Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa,Ban Ki moon,amefungua rasmi, baraza kuu la mkutano wa umoja wa mataifa la 64, na kusisitiza viongozi wa nchi zote kuungana kutimiza agizo la kupambana mabadiliko ya hali ya hewa na kuleta amani duniani, ili kufikia malengo ya karne ya 21.
Katibu huyo, Ban Ki moon,ameagiza pia viongozi waasimamishe umwagikaji wa damu, huko mashariki ya Kati na Afghanistan,kupamabana na umasikini,kulinda haki za wanawake,kudumisha demokrasi,na kupunguza nguvu za nyuklia na bila kusahahu Somalia na Sudan.
Picha hapo juu, anaonekanana, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon,akihutubia wakuu wa nchi walioudhulia mkutanao wa Umoja wa Mataifa wa 64, jijini New York.
Posted by
Kibatala
at
Wednesday, September 23, 2009
0
comments

