Thursday, March 7, 2013

Korea ya Kaskazini yatishia kuishambuli Marekani.

Kambi ya Raira Odinga yalalamikia matokeo ya uchaguzi. 


Nairobi, Kenya - 07/03/2013. Uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya umeanza kuingia dosari baada ya kambi ya mgombea wa kiti cha urais Raila Odinga kudai ya kuwa kuna walakini kutokana na matokeo ya uchguzi huo yanavyo tolewa.
Kalonzo Musyoka ambaye ni makamu wa Raira Odinga katika uchaguzi huo wa rais nchini Kenya alisema "tunaushaidi ya kuwa matokeo ya uchaguzi yanayotolewa yana wizi ndani yake kwani kuna matokeo mengine yameonyesha  kura zimezidi zaidi ya waliojiandikisha."
"Na hatutaki maandamano kwani tupo ndani ya serikali ya shirikisho na niwajibu kufuata sheria."
Hadi kufikia sasa kambi ya Uhuru Kenyatta inaongoza kwa kura nyingi za urais zidi ya Raila Odinga na imepinga madai hayo ya kambi ya upinzani.
Hata hivyo kamati inayoshughulikia na kusimamia uchaguzi huo imezitaka kambi zote kusubiri matokeo ya mwisho, kwani nijambo la kushangaza kanza kulalamikia matokeo wakati bado kura bado zinahesabiwa.

Muuaji wa wapinga ubaguzi  wa Afrika ya Kusini afariki dunia.


Pretoria, Afrika ya Kusini - 07/03/2013. Kachero aliyekuwa wa serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini na ambaye alihusika katika kupanga mauaji ya wale wote waliyokuwa wanapingana na serikali ya kibaguzi amefariki dunia.
Dirk Coetzee 57, ambaye alikuwa akifanya mipango na mauaji hayo kwa kushirikiana na baadhi wa waafrika wa Afrika ya Kusini kwa kuwaingiza nchini Afrika ya Kusini kisiri na kuwapa kazi ya kuwakamata Waafrika wenzao na kuwaleta katika shamba la Vlakplaas mahali ambapo mauaji yalifanyika.
Dirk Coetzee alitubu hayo mara baada ya kurudi nchini Afrika ya Kusini na kutoa mfano kwa kutaja majina  ya  mauaji aliyo yafanya na kusema  "nilihusika katika mauaji ya wanachama wa ANC na wale wote waliokuwa wanapinga serikali"
Hata hivyo Coetzee alisamehewa makosa yake kwenye baraza la  ukweli na maridhiano  mwaka 1997 ambapo baadhi ya watu waliofanya makosa na mauaji katika serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini walisamehewa pia.

Aliyekuwa wazirimkuu wa Itali kwenda jela.


Milan, Itali - 07/03/2013. Aliyekuwa waziri mkuu wa Itali amehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kukutwa na hatia ya kurekodi mazunguzo yaliyokuwa yakifanyika katika mahakama kinyume na sheria mwaka 2006.
Silvio Berluscon 78, ambaye alishawahi kuiongoza Itali kama waziri mkuu, amehukumiwa kifungo hicho baada ya habari za kurekodi mazungumzo hayo kuvuja kutoka kwenye chombo cha habari ambacho kinasimamiwa na Paolo ambaye ni kaka ya Berlusconi.
Hata hivyo Silvio Berlusconi amekata rufaa zidi ya hukumu hiyo na kudai ya kwa kusema " hii ni mbinu za kutaka kunimaliza kisiasa na za kipendeleo."
Hivi karibuni Silvio Berlusconi alirudi kwenye uringo wa siasa na chama chake FrozaItalia kupata kura nyingi katika uchaguzi uliyofanyika hivi karibuni.

Maelfu wakusanyika kumuaga rais Hugo Chavez.


Karakas, Venezuela - 07/03/2013. Maelfu ya Wavenezuela wamakusanyika katika barabara kuu katika jiji la Karakas, ili kumuaga kwa mara ya mwisho aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hugo Chavez.
Huku wakilia na kusema ya kuwa kazi aliyo ianza Hugo Chavez wataiendeleza, maelfu ya watu hao walikusanyika kuanzia  hospital ya kijeshi ambayo rais Hugo Chavez alikuwa amelazwa na hadi katika kambi ya kijeshi, ambapo mwili wake utaifadhiwa hadi siku ya Ijumaa 08/03/2013 tayari kwa mazishi.
General, Jose Ornella, ambaye alikuwa pamoja na hayati rais Hugo Chavez alieleza kuwa  rais Chavez amefariki kwa ugonjwa wa moyo, na kabla ya kifo chake alisema   "nisingependa kufa na msinieche nikafa" na hayo ndiyo maneno yake ya mwisho.
Rais, Hugo Chavez 58, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa salatani, ambapo alikuwa katika harakati za matibabu nchini Kuba.
Viongozi mbali mbali na hasa wale walio kuwa karibu na Hugo Chavez wanatarajiwa kuhudhulia mazishi yake, na badhi ya viongozi wa karibu ni rais Cristina Kirchner wa Algentina, Evo Morales wa Bolivia na Jose Mejica wa Uruguay wamesha wasili nchini Venezuela tayari kwa mazishi ya kiongozi rafiki yao mpendwa.

Korea ya Kaskazini yatishia kuishambuli Marekani.


Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 07/03/2013.Serikali ya Korea ya Kaskazini  imetishia kuishambulia Marekani ikiwa kunamashambulizi yoyote yatakayofanywa kwenye nchi yake.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya nchi ya Korea Kaskazini  hambaye hakutajwa jina lake alisema"inavyo elekea ni kwamba Marekani ipo mbioni kuanzisha vita zidi ya yetu na huenda vikawa ni vya kunyuklia, na kwa minajili hiyo tunayo haki ya kujibu mashambulizi kwa njia itakayo tumiwa na adui yetu, ili kulinda nchi yetu."
Onyo hilo kutoka Korea ya Kaskazini limekuja  baada ya Marekani na Korea ya Kusini kupanga kufanya pamoja mazoezi ya kijeshi hivi karibuni.
Korea ya Kaskazini ilifanikiwa katika jaribio la kinyuklia lililo fanywa hivi karibuni na kufanya jumuia ya kimataifa kujadiliana ili vikwazo viongezwa kwa nchi hiyo.

Tuesday, March 5, 2013

Rais wa Venezuela Hugo Chavez aaga dunia.

Rais wa Venezuela Hugo Chavez aaga dunia.


Karakas, Venezuela - 05/03/2012. Rais wa Venezuela Hugo Chavez amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu kutokana na ugonjwa wa saratani.
Akitangaza kifo cha rais Hugo Chavezi, makamu wa rais wa Venezuela Nikolas Maduro alisema" Wanachi wenzangu na marafiki wa Venezuela, rais wetu mpigania haki na mwanamapinduzi Hugo Chavez amefariki dunia.
Maadui wa Hugo Chavez walimpandikiza viini vya ugonjwa wa saratani., ambavyo vimeyaondoa maisha yake." 
Marehemu rais Hugo Chavez 58, amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa saratani, na alikuwa akifanyiwa matibabu nchi Kuba.
 Hugo Chavez ametawala nchi Venezuela kwa muda wa miaka 14 na alikuwa amechaguliwa kuiongoza Venezuela baada ya kufanyika uchaguzi mkuu hivi karibuni nchini humo,lakini kushindwa kuhudhulia sherehe ya kuwapishwa kwake kama rais kwani alikuwa katika matibabu nchini Kuba..
Kufuatia kifo cha rais Hugo Chavez, serikali ya Venezuela imewafukuza maafisa wa kijeshi wa Marekani kwa kuwapa masaa 24 kuondoka nchini Venezuela.
Kabla ya kifo cha rais Chavez, Venezuela na Marekani zilikuwa hazina uhusiano mzuri.

  Netanyahu ataka mbinu mpya kwa Iran.


 New York, Marekani -05/03/2013.Waziri mku wa Izrael ametahadharisha Marekani na washiriki wake ya kuwa Iran ipo inakaribia kuvuka mstari mwekundu katika harakati zake za  sayansi ya kinyuklia.
Benjamin Netanyahu akihutubia katika mkutano kwa kupitia mtandao kwa wajumbe wa ushirikiano wa Izrael na Marekani (American Izrael Public Affairs Committee - AIPAC) alisema. "vikwazo zidi ya Iran havifanyi kazi na Iran ipo inaendelea na mpango wake wa kutengeneza siraha za kimyuklia jambo ambalo ni la hatari kwa nchi majirani zake  na eneo zima la ukanda wa mashariki ya kati.
 "Inabidi hatua nyingine ziangaliwe ili kuizuia Iran na mpango wake wa kuendelea na uzalishaji wa nyuklia."
Mkutano wa AIPAC ni mkutano ambao huwakutanisha wajumbe wa Marekani na Izrael ili kujadili ni kwa jinsi gani watashirikiana kwa ukaribu ili kudumisha umoja wao.

Uhuru Kenyatta aongoza katika uchaguzi wa urais.

Nairobi, Kenya - 05/03/2013. Mgombea wa kiti cha urais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anaongoza katika  kura zidi ya mpinzani wake Raila Odinga.
Uhuru Kenyatta ambaye mpaka sasa anaongoza kwa asilimia 53% za kura zidi ya mpinza  wake Raila Odinga ambaye mpaka sasa amepata asilimia 42% za kura na huku kura nyingine bado zinahesabiwa.
Hata hivyo mkuu wa kamati ya uchaguzi mkuu amesema "bado kuna baadhi ya majimbo yanasubiriwa ili kuweza kupata idadi kamili ya kura zote."
"Napenda kuwataka Wakenya wote wawe na subira." 
Uchaguzi mkuu wa kumchagua rais na wabunge nchini Kenya umekuwa ukingaliwa kwa makini na jumuiya ya kimataifa , hii inataokana na vurugu zilizo tokea mwaka 2007-8 baada ya uchaguzi mkuu wa urais kufanyika ambapo watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha.  




Monday, March 4, 2013

Wakenya kuongea kupitia kura ili kumchagua rais.

 Wakenya kuongea kupitia kura ili kumchagua rais.

Nairobi, Kenya - 04/03/2013. Wananchi wa Kenya leo wanapiga kura kumchagua rais na kuwachagua wabunge ambao wataongoza nchi kwa kpindi cha miaka mitano.
Hata hivyo katika harakati za uchaguzi huo ambao umekuja na mtazamo tofauti kwa wananchi wa Kenya. Mjini Mombasa watu kumi natatu wameuwawa akiwemo polisi baada ya kutokea vurugu katika harakati za kuandaa uchaguzi.
Kundi la Mombasa Republikan Kanseli limeshukiwa kuhusika na mauaji hayo.
Wapinzani wakubwa katika kugombea kiti cha urais ni Raila Odinga na Uhuru Kenyatta, ambo kabla ya kuanza kwa uchaguzi kura za maoni zilionyesha kuwa wapo karibu sawa.
Uchaguzi mkuu wa Kenya unawekewa jicho ng'aavu, ili kuzuia mauaji yaliyo tokea mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha yao.

Jeshi la Nigeria lashambulia ngome ya Boko Haram

 Lagos, Nigeria - 04/03/2013. Jeshi la Nigeria limedai kuwaua wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika mashambulizi yaliyofanywa Kaskazini mwa Mashariki ya jimbo la Borno.
Msemaji wa jeshi amesema "jeshi la serikali limeweza kuwauwa wapiganaji 20 na mauaji hayo yalifanyika karibu na kijiji cha Mongono, siraha na vifaa vingine vya kijeshi vilikutwa katika eneo hilo."
Mashambulizi hao kwa kundi la Boko Haram, yamekuja huku mkuu wa kundi hilo Abubakar Shekau akikanusha kuwepo na mpango wa mazungumzo na serikali ya Nigeria. 
Kundi la Boko Haram limekuwa likilaumiwa kwa kuleta mchafuko wa amani nchini Nigeria kwa kuhusika na mashambulizi ya kigaidi yanayo tokea nchini humo mara kwa mara.
  
Makachero waliandaliwa kumua rais wa Syria.


Beirut, Lebanon - 04/03/2013.Gazeti la  moja nchi Lebanon limetangaza ya kuwa limepata nyaraka  zinazo oonyesha mpango wa Uturuki na Ufaransa wa kutaka kumua rais wa Syria Bashar al Assad.
Gazeti hilo la habari  Asianews lina ropoti ya kuwa nyaraka hizo zinaonyesha mpango na mbinu ambazo zingetumika katika kumua rais huyo wa Syria.
Kwa  mujibu wa gazeti hilo lilisema "makachero wa Kifaransa na Wakituruki walikuwa wameshapanga mbinu zitakazo tumika katika mauaji hayo ikiwa ni kuwaajili baadhi ya maafisa wanao fanya kazi katika ofisi ya rais Bashar al Assad."
Wakati huo huo rais Bashar al Assad amesema "Uingereza ipo mbioni kuwauzia siraha waasi wa serikali ya Syria na hatutarajii ya kuwa Uingereza inaweza kuwa msuruhishi."
 Naye waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Syria Walid al Muallem alithibitisha kuwepo kwa mpango  na kudai yakuwa "Saudu Arabia inajua mipango yote pamoja na washiriki wake.
Mapigano nchini Syria ya kutaka kumngóa madarakani rais Bashar al Assad yamekuwa yakiendelea na huku mamia ya watu kupoteza maisha yao, mali za nchi kuharibiwa vibaya na raia wengine wa Syria kuikimbia nchi yao. 

Thursday, February 28, 2013

Papa Benedikt ajiudhuru rasmi uongozi wake wa Kanisa Katoliki.

Papa Benedikt ajiudhuru rasmi uongozi wake wa Kanisa Katoliki.

Vatican City, Vatican - 28/02/2013.Papa Benedikt wa XVI amewaaga rasmi waumini wa Kanisa Katoliki duniani kwa misa maaalumu aliyo iongoza.
Papa Benedikti 85, ambaye amongoza Kanisa Katoliki kwa muda wa miaka nane alitangaza kujiudhuru wadhifa wake huo mwanzoni mwa mwezi huu kutokana na hali ya afya yake kuto mruhusu kuendelea na kazi hiyo ya kuliongoza Kanisa Katoliki lenye waumini wapatao 1.2 billion.
Akihutubia waumini waliokuja kuudhuria misa ya kumuaga, Papa Benedikti alisema "nawatakiwa baraka za Mungu ziwe nanyi na nawashukuruni sana na tuzidi kuendalea katika njia apendayo Mungu."
Papa Benedikti ambaye alizaliwa na kubatizwa kwa jina la Joseph Ratzinger amekuwa Papa wa kwanza  kujiudhuru madaraka yake tangu ilipotokea miaka 600 iliyopita. 

Marekani kutoa kifedha kwa wapinzani wa serikali ya Syria.

 Washington, Marekani - 28/02/2013. Serikali ya Marekani imetangaza kuongeza msaaada wa kifedha kwa kundi linalo pingana na serikali ya Syria.
Akiongea katika mkutano uliofanyika nchi Itali Roma ambao ulijulikana kama mkutano wa marafiki wa Syria. waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Marekani John Kerry alisema " kiasi cha dola za Kimarekani $60millioni zitatolewa kwa kundi Syria National Coalition (SNC) ."
"Pesa hizo zitakuwa kwa ajili ya misaada ya kiutu" aliongezea waziri John Kerry.
John Kerry yupo katika ziara za kikazi baada ya kuapishwa kuchukua wadhifa wa waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Marekani .
Hadi kufikia sasa maelfu ya Wasyria wamekubwa na hali mbaya kiuchumi na kijamii tangu kuanza vita  vya kutaka kuun'goa utawala wa rais Bashar al Assad.

Tuesday, February 12, 2013

Korea ya Kaskazini yaitikisa dunia kwa kufanikiwa jaribio la nyuklia.

 Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 12/03/2013. Serikali ya Korea ya Kaskazini imetangaza kufanikiwa  katika jaribio la kulipua bomu la kinyuklia.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya Korea ya Kaskazini zimesema " tumefanikiwa katika jaribio la kinyuklia  ambalo lilifanyika chini ya ardhi na tumetumia teknolojia ya kisasa na yenye ujazo mdogo."
Jaribio hili ni la tatu, na kiongozi wa Korea ya Kaskazini amesema "majaribio mengine kama hayo yatafuata."
Idara ya sayansi na nyuklia ya umoja wa mataifa iliyopo Vienna imesibitisha  kuwepo kwa mlipuko mkubwa  kuliko ile wa kwanza 2009 ambao ulifanywa na serikali ya Korea ya Kaskazini.
Kufuatia kufanikiwa kwa serikali ya Korea ya Kaskazini, kamati ya usalama ya umoja wa mataifa imeitisha mkutano wa dharula mjini New York ili kujadili kitendo hicho cha Korea ya Kaskazini.

John Kerry akaribishwa  kitendawili cha Iran.

 Washington, Marekani - 12/03/2013. Waziri wa mambo ya nje wa Marekani ameitaka Iran  kusimamisha mpango wake wa kuendelea kuzalisha nyuklia.
John Kerry ambaye amechukua nafasi iliyo achwa wazi na Hillary Clinton alisema " jumuia ya kimataifa ipo tiyari ikiwa Iran itakuwa tayari kwa mazungumzo."
Mazungumzo hayo ya John Kerry yamekuja baada ya Marekani kuona Iran inazidi kuwa kichwa ngumu kwa jumuiya ya kimataifa katika mpango wake wa kuendelea na miradi ya kinyuklia na kudai nikwaaajili ya matumizi ya kisayansi na siyo kwa vita.

Monday, February 11, 2013

 Papa Benedikti XVI atangaza kujiudhulu.


Vatican, Vatican City - 11/02/2013.Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani ametangaza kujiudhulu wazifa wake kutokana na hali ya kiafya kuto mruhusu kuendelea na kazi za kiinjili.
Akitangaza kuhusu habari hizi,  Federico Lombardi ambaye ni msemaji wa Vatican alisema Papa Benedikti wa XVI atajiudhulu  wadhifa wake kama mkuu wa kanisa Katoliki duniani  tarehe 28/02/2013.
Papa Benedikti mwenye miaka 85, ambaye alitawazwa kuwa mkuu wa kanisa Katoliki April 19, 2005 amekuwa ni kiongozi wa kanisa Katoliki wa 265.
Kufuatia kujiudhulu huko kwa Papa Benedikti, Makadinali watakutana katika ya mwezi Machi ili kumchagua kiongozi mpya wa kanisa hilo.
  
Libya yavutana na ICC juu ya washitakiwa kutoka nchini Libya


 Tripol, Libya - 11/03/2013. Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia makosa ya jinai (ICC) imeitaka serikali ya Libya kumkabidhisha mikonino mwa mahakama hiyo aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa Libya wakati wa utawala wa rais Muammar Gaddafi.
Abdullah Senussi  ambaye alikamatwa nchini Mauritania mwezi Machi mwaka jana, hadi sasa yupo mikononi mwa serikali ya Libya, na anakabiliwa na mashitaka ya kukiuka haki za binadamu wakati akiwa kama mkuu wa upelelezi wa Libya.
Kwa mujibu wa habari kutoka makao makuu ya koti (ICC) iliyopo Hague nchini Netherlands, zinasema " serikali ya Libya inatakiwa kumkabidhi haraka iwezekanavyo Abdulah Senussi mikononi mwa ICC kabla sheria haijachukua mkondo wake"
Kesi zidi ya Senussi imekuwa inaleta mvutano kati ya ICC na serikali ya Libya jambo ambalo limeifanya ICC kutishia kutumia mbinu mbadala baada ya serikali ya Libya kuzidi ng'ang'ania azma yake ya kumzuia mtuhumiwa huyo.
  
Wagombea urais Kenya wawekwa kiti moto kupitia Luninga.

Nairobi, Kenya - 11/02/2013. Wananchi na kaaazi wa Kenya watapata kwa mara ya kwanza fursa ya kuwa ona wanasiasa  wanaogombania urais wakijadili na kuongea sera zao za kisiasa na kiuchumi kwa kutangazwa moja kwa moja kupitia luninga na redio za kitaifa.
Mdaharo huo wa kisiasa ambao utachukua  muda wa masaa mawili, utawakutanisha wanasiasa  ambao ni viongozi wa vyama  wanagombania kiti cha urais kupitia vyama hivyo ili kuelezea wananchi  wa Kenya ni kwa kiasi watainua maisha ya Wakenya kiiuchumi na kijamii.
Wananchi nchini Kenya watapiga kura 4 mwezi Machi 2013, ili kumchagua rais na wabunge. 


Sunday, February 10, 2013

Muuaji wa kujitolea muhanga afa nchini Mali

Muuaji wa kujitolea muhanga afa nchini Mali

Gao, Mali - 10/02/2013. Mapigano ya kivita kati ya wapiganaji wa makundi ya Kiislam na majeshi ya serikali chini ya usaidizi wa jeshi la Ufaransa yameendelea katika eneo la Kaskazini  mwa  Mali.
Habari kutoka kwa msemaji wa kijeshi zinasema " mapigano hayo yaliaanza karibu na kituo cha polisi na baadaye muuaji wa kujitolea  kujilipua karibu na kizuizi kilicho wekwa barabarani."
Mji wa Gao ambao hapo awali ulikuwa umerudishwa mikononi mwa jeshi la serikali unaelekea kuwa kituo cha waasi hao wa Kiislam kwani inaaminika bado wapo katika baadhi ya vijiji vilivyopo kwenye mji huo.  

Wairan wapo imara asema rais Mahmoud Ahmadinejad.

Tehran, Iran - 10/02/2013.Rais wa Iran amesisitiza ya kuwa Wairan hawata tikiswa na mtu yoyote na lolote wanalo fanya ni kwaa ajili ya kuendeleza nchi yao na si kwaa ya kutishia nchi nyingine.
Rais Mahmoud Ahmedinejad aliyasema hayo wakati akuhutubia maelfu waliokusanyika  katika bustani ya  Azadi ili kuadhimisha miaka 34 tangu mapinduzi ya kuuong'oa utawala wa uliokuwa unakubalika na serikali za Magharibi.
"Leo maadui wanafanya kila njia ili kuzuia taifa la Iran kufanya maendeleo ya kisayansi kwa kutumia kila njia  ,kalini hadi sasa wameshindwa na tutazidi kuendeleza uwekezaji wa kisanyansi ili kizazi cha  Wairan wajao wawe na msingi imara." Aliongezea rais Ahmadinejed
Iran imekuwa na mvutano na serikali za magharibi kuhusu mpango wa mradi wake wa kinyuklia., jmabo ambalo serikali za magharibi zi na shukia ya kua Iran inampango wa kutengeneza siraha za kinyuklia na huku serikali ya Iran ikipinga shukuma hizo.



Sunday, February 3, 2013

Majeshi ya Ufaransa kuondoka nchini Mali.

 Wapinzani nchini Misri walia na rais Mosri.

 Kairo, Misri - 03/02/2013. Polisi nchini Misri wamekuwa na kashfa nyingine tena, baada ya kuonekana katika picha za luninga wakimpiga mmoja ya waandamanaji wakiwa "uchi" bila nguo.
Kufuatia tukio hilo vyama vya upinzani nchini Misri vimedai rais Mohamed Mosri ashitakiwe, kwani tangu achukue madaraka zaidi ya watu 60 wamekwisha uwawa kufaatia ghasia zinazo endelea nchi humo.
Mmoja wa kiongozi wa vyama vya upinzani akisikika akisema " kitendo kilicho fanywa na polisi kimekiuka haki za binadamu na tunataka rais atolewe madarakani kwani yale tuliyo yakataa wakati wa utawala wa Husni Mubaraka Mosri ndiyo anayayenda."
Hali ya amani nchini Misri imekuwa ya kuyumba saana tangu kuingia serikali mpya ya  Mohammed Mosri  chini ya chama cha Muslim Brotherhood, jambo ambalo lilimfanya rais Mosri kutangaza hali ya tahadhali katika baadhi ya miji mikuu nchini  Misri, kitu ambacho kiliwafanya wanachama wa vyama vya upinzani kupinga na kuanzaa maaandamano kupinga tahadhali hiyo.

Majeshi ya Ufaransa kuondoka nchini Mali.

 Bamako, Mali - 03/02/2013. Rais wa Ufaransa Francois Hollande amewaahakikishia Wamali ya kuwa jeshi la Ufaransa lipo nchini Mali ili kusaidia kurudisha amani nchini humo.
Akiongea na wahandishi wa habari rais Hollande alisema " jeshi la Ufaransa lipo kwa ajili ya kurudisha amani  na pindipo kazi hiyo itakapo kamilika, jeshi hilo litarejea nyumbani."
Wakati akiongea na waandishi wa habari rais Hollande, majeshi ya Ufaransa kwa kushirikiana na majeshi ya Mali yamezidisha mashambulizi zidi ya waaasi wa kundi linaloshirikiana na Al Qaeda na kulifanya kundi hilo kutokomea kabisa na kuachia mji wa Timbuktu ambao ulikuwa chini ya waaasi hao.
Rais Hollande alifanya ziara ya kiserikali nchini Mali ikiwa ni jitihada ya Ufaransa kuonyesha kuunga mkono serikali ya Mali na kuwapa moyo wanajeshi wa Ufaransa waliopo nchini Mali.




Thursday, January 31, 2013

Izrael yaishambulia Syria.

Harakati za uchaguzi zaanza rasmi nchini Kenya.

Nairobi, Kenya - 31/01/2013. Viongozi wa siasa nchini Kenya wameanza kampeni za uchaguzi kupitia vyama vyao tayari kujiandaa kwa uchaguzi mkuu utakao fanyika Machi 4/ 2013.
Harakati kubwa za uchaguzi zitakuwa ni katika kinyang'anyiro cha kiti cha urais ambapo kamati ya uchaguzi imeyapitisha majina ya  waziri mkuu Raila Odinga na Uhuru Kenyatta  kuwa baadhi ya wagombea wa kiti cha urais.
Uchaguzi wa viongozi hao umekuja baada ya rais wa sasa Mwai Kibaki kumaliza muda wake kama rais wa Kenya.
Odinga amemchagua makamu wa rais Kalonzo Musyoka kuwa makamu wake na Uhuru Kenyatta amemchagua waziri wa elimu William Ruto kuwa makamu wake.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Raila Odinga na Uhuru Kenyatta walisema " tunatumaini uchaguzi utakuwa wa haki na yale yaliyo tokea 2007/2008 hayatatokea tena."

Izrael yaishambulia Syria.

Damascus, Syria - 31/01/2013. Serikali ya Syria imetishia kuchukua hatua kali dhizi ya Izrael.
Tishio hilo la serikali ya Syria limekuja baada ya ndege za kijeshi za Izrael kufanya mashambulizi ndani ya Syria.
Kwa mujibu wa serikali ya Syria, ndege nne za kijeshi za Izrael zimefanya mashambulizi karibu na jiji la Damascus na kuua watu wawili na watano kujeruhiwa.
Kufuatia mashambulizi hayo, jumuiya ya nchi za kiarabu limelaani kitendo hicho kwa kusema ni kinyume  na sheria za kimataifa na kuizaraurisha jumuiya hiyo.
Hata hivyo habari kutoka Washington zimethibitisha yakuwa ndege za Izrael zimeshambulia msafara wa kijeshi nchini Syria.
Nayo Iran imeunga mkono serikali ya Syria kwa kudai ya kuwa ipo bega kwa bega na serikali ya Syria na  ipo tayari kutoa msaada wa kila hali kwa Syria.
Hata hivyo serikali ya Izrael haijathibitisha mashambulizi hayo.

Wednesday, January 30, 2013

Seneta John Kerry kuchukua kiti cha Hillary Clinton.

 Seneta John Kerry kuchukua kiti cha Hillary Clinton.


Washington, Marekani - 30/01/2013. Wabunge wa seneta la Marekani wamepiga kura kwa wingi na kupitisha jina la Seneta John Kerry kwa wingi wa kura 94-3 na kumpa nafasi ya kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
John Kerry 69, ambaye alisha wahi kugombea kiti cha urais kupitia chama cha demokrasi cha Marekani anachukua nafasi ya bibi Hillary Clinton ambaye alishikilia nyazifa hiyo kwa miaka minne iliyo pita.

Rais wa Misri awasili nchini Ujerumani.

 Bonn, Ujerumani - 30/01/2013. Rais wa Misri Mohammed Mosri amefanya ziara ya kikazi nchini Ujerumani katika harakati za kutaka kuijenga nchi yake kiuchumi na kutafuta uvumbuzi wa changamoto ya  kisiasa iliyopo nchini mwake.
Akiongea baada ya kumkaribisha mgeni wake, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel  alisema " wanachi wa  Misri wanatakiwa kukaa katika meza ili kusuruhisha changamoto ya kisiasa iliyopo nchini humo.
Naserikali ya Ujerumani itachangia kwa hali na mali mpaka wananchi wa Mirsi wanapata demokrasi kamili.
Rais Mohammed Mosri amefanya ziara hiyo siku chache baada ya kutangaza hali ya tahadhali ili kurudisha usalama na amani nchini Misri. na kudai yakuwa hakutakuwa na serikali mpya hadi hapo kipindi cha uchaguzi wa wa wabunge kitakapo fika.

Tuesday, January 29, 2013

Iran yafanikwa kutuma nyani mwezini.

Hali ya amani nchini Misri yazidi kuwa tete.

 Ismailia, Misri - 29/01/2013. Waelfu ya wakazi wa mji wa Ismalia  wamekiuka amri ya serikali iliyo wataka kukaa majumbani kwao ili serikali iweze kukabiliana na vurugu zinazo endelea nchi Misri.
Wakazi hao wa mji wa Ismailia na mji wa Suez Kanal walipinga na kuvunja amri hiyo huku wakidai ya kuwa wanacho taka ni haki zao kwani " wamesha tuonea vya kutosha wameua watoto zetu, wake zetu na hali inazidi kuwa mbaya kila kukicha"
Navyo vyama vya upinzani nchini humo vipepinga vikali hatua hizo za serikali za kuweka dharula yakiusalama katika miji hiyo. 
Rais wa Misri Mohammed Musri alitangaza hali ya dharula ya liusalama katika miji yote ambapo vurugu zinaendelea.
Nchi ya Misri imekuwa na wakati mgumu kiamani tangu kufanyaka maandamano ya liyo mtoa rais Husni Mubaraka.

Waethiopia wapigwa sindano za kuzuia kuzaa kwa wingi  chini Izrael.


 Jerusalemu, Izrael - 29/01/2013. Waziri wa afya wa Izrael amekubali ya kuwa serikali ya Izrael imekuwa ikiwachoma sindano za uzazi wa majira wageni wa Kiithiopia ikiwa ni katika harakati za kudhibiti ongezeko la wahamiaji.
 Kukubali huku kwa serikali ya Izrael kumekuja baada ya gazeti la Haaretz kuandika habari hizo kufuatia maelezo na malalamiko yaliyo tolewa na shirika la kufuatilia haki za binadamu likujulikanalo kama Association for Civil Right in Izrael (ACRI) kuitaka sererikali isimamishe mara moja zoezi hilo, kwa kudai ya kuwa wakinamama wanako pigwa sindano hizo hawajui madhara yake hya hapo baadaye.
Sindano hiyo inayo julikana kwa jina la Depo-Provera imekuwa ikitumika kuwadunga wakina mama wa Kiithiopia na wakina mama wanao tumia dawa hiyo huwa wanatakiwa kupiga sindano hiyo kila baada ya miezi mitatu.
Kwa mujibu wa wachunguzi wa kisayansi dawa hiyo aina ya Depo- Provera huwa inaleta madhara ya  kuumwa na kichwa, kupoteza nywele, mzunguko wa kike kutokuwa wa kawaida, kupungukiwa uzito  na ngozi kuwa na madhara.

 Iran yafanikwa kutuma nyani mwezini. 

  Tehran, Iran - 29/01/2013. Wana sayansi wa Iran wamefanikwa kutuma nyani mwezini ikiwa ni moja ya matayarisho ya kutuma binadamu kwenda mwezini ifikipo 2019.
Msemaji wa kisayansi wa Iran alisema " hii ni atuha muhimu katika maendeleo ya kisanyansi nchini Iran na kila tukifanyacho ni kwaa ajili ya matumizi ya Wairan na binadamu wate kwa ujumla na tunashukuru nyani huyo amewasili bila matatizo yoyote."
Kufuatia kitende hicho, baadhi ya mashirika ya kimataifa yametilia wasiwasi kwa kudai ya kuwa ni kitendo kilicho kiuka sheria za kimataifa.
Marekani na washiriki wake wamekuwa wakitilia mashaka kuhusu mpango mzima wa Iran katika maswala ya kinyuklia kwa kudai "Iran inampango wa kutengeneza bomu la nyuklia."

Malkia wa Netherlands kujiudhulu wadhifa wake.

 The Hague, Netherlands - 29/01/2012. Wananchi na wazalendo waishio Netherlands wamepatwa na mishituko  yenye mawazo na maoni tofauti baada ya Malkia Beatrix kutangaza kuachia nyazifa zake za kwa mwanaye Prinsi William-Alexander.
Akiongea kupitia luninga ya taifa huku wananchi, wazalendo na wakazi wanao ishi nchini Netherlands, Malkia Beatrix  ambaye anatimiza miaka 75 siku ya Alkhamisi 31/01/2013 alisema " Nawashukuru kwa kuwa pamoja nami katika kila hali, na leo imefikia wakati wa kuachia kizazi kipya kuiendeleza nchi."
Napenda kuwatangazia ya kuwa tarehe 30/4/2013 mwanangu William-Alexander atachukua kiti cha kifalme.
Netherlands imekuwa na utamaduni wa wafalme kujiudhuru tofauti na nchi nyingine zenye uongozi wa kifalme.







Tuesday, January 22, 2013

Baraka Hussein Obama achukua ofisi kwa mara ya pili.

Washington Marekani - 22/01/2013. Wananchi na wakazi wa Marekani kwa mara nyingine tena walikusanyika ili kushuhudia kuapishwa kwa Baraka Hussein Obama kuchukua kiti cha urais kwa mara ya pili baada yab kushinda uchaguzi mkuu uliyofanyika Marekani mwaka jana.
Baraka Hussein Obama mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa Marekani kwa mara ya pili alihutubia taifa  na kusema"Safari yetu haijakamilika mpaka hapo mama zetu, wake zetu, mabinti wentu wataka;po kuwa na haki sawa katika jamii na pia haki kwa kila mtu inatimizwa na kulifanya taifa hili la Marekani kuwa taifa lenye kutoa nafasi kwa kila mtu aishiye nadani ya nchi hii."
Kabla ya kuapishwa mbele ya kadamnasi ya Wamarekani rais Baraka Obama aliapishwa katika Ikulu kwani kisheria siku ya kushika ofisi iliangukia siku jumapili na ikabidi aapishwe ili kukamilisha sheria ya nchi.

Wajerumani na Wafaransa wakumbuka siku mkataba wa ushirikiano kwa nchi zao.


Berlin, Ujerumani - 22/01/1213.Wananchi wa Ufaransa na Ujerumani wanasherekea mkataba uliyowekwa na  uliyo wekwa kati ya viongozi wa nchi hiyo miaka 50 iliyopita.
Mkataba huo unao julikana kama mkataba wa Elysee ambapo ulisainiwa kati ya  rais wa Ufaransa Charles de Gaulle na Kansela wa Ujerumani Konrad Adenauer siku ya tarehe 22 Januari 1963.
Wakiongea katika kuadhimisha sherehe hiyo  viongozi wa Ufaransa na  Ujerumani walisisitiza kuendeleza uhusiano huo na kuhakikisha ya kuwa wanajenga msingi imara kwa kizazi kijapo cha nchi hizo.                         

Friday, October 26, 2012

Silvio Berluscon haukumiwa kwenda jela.

 Silvio Berluscon haukumiwa kwenda jela.

 Milan, Itali - 26/07/2012. Aliyekuwa waziri mkuu wa Itali amehukumiwa  kwenda jela na kuzuiliwa  kushiriki katika maswala ya kiofisi baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kodi za malipo.
Hukumu hiyo imetolewa baada ya kukutwa kuhusika katika biashara kinyume na sheria.
Silvio Berlusconi ambaye alikuwa waziri mkuu wa Itali, amehukumiwa kwa mara ya kwanza, japo hapo awali alishafunguliwa kesi tofauti zidi yake.
Baada ya hukumu hiyo, Berlusconi alisema "hukumu haina maana na haikufuata haki"
Hata hivyo Silvio Berlusconi  amekata rufaa baada ya hukumu hiyo.

Rais wa Marekani apiga kura mapema.
 
Chicago, Marekani - 26/10/2012. Rais wa Marekani amepiga katika mji wake Chicago ikiwa ni moja ya kampeni za kutaka wapiga kura wajitokeze kwa wingi.
Rais  Baraka Obama, alipiga kura huku kura za maoni zikiwa zimesimama katikati baada ya mpinzani wake  Mitt Romney kujivuta juu katika kura za maoni zilizo tolewa hivi karibuni.
Upigwaji wa kura hizo ni moja ya mpangilio ya uchaguzi uliyopo nchini Marekani.
Mara baada ya kumaliza kupiga kura Baraka Obama, aliendelea na ziara ya kampeni ya kutaka raia wa Marekani kumpigia kura hasa katika  miji ya Ohio Virginia  na Florida.



Sunday, September 9, 2012

Mtoto wa Muammar Gaddafi kuondoka nchini Niger.

Mtoto wa Muammar Gaddafi kuondoka nchini Niger.


Niamey, Niger - 09/09/2012. Mtoto wa aliyekuwa rais wa Libya Muammar Gaddafi anatarajiwa ,kuondoka nchini Niger.
Saadi Gaddafi mtoto ambaye alikimbilia nchini Niger baada ya serikali ya baba yake Muammar Gaddafi kuangushwa na baadaye kuuwawa.
Kwa mujibu wa habari zinasema " Waziri wa mambo ya nje wa Bazoum Mohamed ameshatoa rukhusa kwa Saadi Gaddafi kuondoka nchini Niger."
Habari zilizo patikana zimedai ya kuwa huenda Saadi akaamia nchini Afrika ya Kusini, japo hadi sasa hakuna  habari za huakika kutoka katika serikali ya Afrika ya Kusini.


Moscow yaonya mashabulizi zidi ya Iran.
Moscow, Urusi - 09/09/2012. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi ametoa onyo ya kuwa kitendo chochote cha kuishambulia Iran kijeshi kitaleta madhara makubwa.
Akiongela swala hilo makamu wa waziri wa mambo ya ndani y Urusi  Sergey Ryabkov alisema "tunapenda kuonya ya kuwa mashambulizi ya kijeshi zidi ya Iran yataleta maafa makubwa ambayo yatavuka mipaka ya nchi za Mashariki ya Kati,  na napenda kusisitiza suala la Iran na nguvu zakinyuklia nivizuri kujadiliwa katika meza kuliko kutumia nguvu za kijeshi."
Mazungumzo hayo yamekuja huku nchi za Ulaya na Marekani zikiwa zimezidisha jitihada za kutaka Iran iwekewe vikwazo vya kiuchumi ambavyo vitaifanya nchi hiyo kuachana na mradi wake wa kinyuklia.

Friday, August 24, 2012

 Mauaji yatokea Kusini Mashariki mwa Kenya.
 

Nairobi, Kenya - 24/07/2012. Watu 48 wameuwawa na wengine kujeruhiwa ikisadikiwa kuwa ni kulipa kisasi kati vijiji viwili vinavyo pakana.
Mauaji hayo yaliyotokea katika eneo la  Reketa katika kijiji cha Tarassa Kusini Mashariki  maili 300 mwa mji wa Nairobi. na kuleta mstuko mkubwa tangu mauaji yaliyotokea miaka minne iliyopita wakati na baada ya uchaguzi mkuu nchi Kenya.
Msemaji wa polisi Chifu  Joseph Kitur alisema " watu walifariki kwa kukatwa na mapanga na wengine kuchomwa moto na pia nyumba zao kuchomwa moto jambo ambalo mpaka sasa bado tunalifanyia uchunguzi nini hasa kilifanyika hapo awali na kufikia kufanyika muaji ya kinyama kama haya."
Hata hivyo mkazi mmoja wa eneo hilo alisema hii mauaji haya yote yametokana na mvyutano wa mifugo kati ya wakazi wa vijiji vya Orma na Pokomo.

Angela Merkel na Antonis Samaras wakutana kujadili hali ya Ugiriki.
 
Berlin, Ujerumani - 24/08/2012.  Waziri mkuu  wa Ugiriki amekutana na Khansela wa Ujerumani katikaharakati za kutaka kujua ni kwa kiasi nchi ya Ugiriki inavyo fuata masharti ya kuimarisha uchumi.
Waziri Mkuu Antonis Samara na  Khansela Angela Markel walikutana na kujadili ni kwa kisi gani nchi za Jumuiya ya Ulaya zitashirikiana katika kuhakikisha Ugiriki inarudisha uimara wa uchumi wake.
Antonis Samara akiongea alisema " tunataka kuwahakikishia wenzetu tutafanya kila njia kuhakikisha uchumi wa Ugiriki unakuwa na tunachoomba ni muda zaidi."
Naye  Khansela Angela  Merkel alisema" naimani Ugiriki itatimiza yote yanayo takiwa ili kukuimarisha uchumi wa nchi hiyo na kutokana kwa kufuatia  makubaliano iliyo yafanya na nchi za jumuiya  Ulaya na ukizingatia Ugiriki ni nchi ambayo kwa upande wangu ni mwanachama wa nchi za jumuiya ya Ulaya na ningependa ieleweke kuwa naunga mkono nchi ya Ugiriki kubaki kuwa mwanachama wa nchi za jumuiya  Ulaya .
Nchi ya Ugiriki imekuwa nawakati mgumu katika haarakati za kutaka kuinua uchumi wake baada  ya kupewa mkopo wa pesa kutoka nchi za jumuiya za Ulaya na kutakiwa kufanya mrekebisho ya kiuchumi jambo ambalo limekuwa likileta msuguano kati ya serikali na wanchi wake.
  
Aliyefanya mauaji nchini Norway haukumiwa miaka 21 jela.

Oslo, Norway - 24/08/2012. Mahakama nchini Norway imemuhukumu kwenda jela mshitakiwa aliyehusika katika mauaji ya watu 77 na kufanya ushambulizi kutumia mabomu katika jiji la Olso.
Anders Breivik ambaye aliwavamia vijana waliokuwa katika kisiwa cha Utoya kwa ajili ya  mkutano wa kuhamasisha siasa na kuanza kuwapiga risasi amehukumiwa miaka 21 jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya makosa hayo.
Akiongea baada ya hukumu, mshitakiwa Anders Breivik alisema " nasikitika kwa wale wanachama wenzangu kwa kushindwa kufanya mauaji zaidi wakati ule."
Anders Breivik ambaye alidai ya kuwa ni mwanachama wa Temple Knight na alifanya mauuaji hayo kwani alikuwa anapinga kuwepo kwa wageni na kukua kwa dini ya Kiislaaam nchi Norway na Ulaya.. 


Tuesday, August 21, 2012

Waziri mkuu wa Ethiopia aaga dunia.

Waziri mkuu wa Ethiopia aaga dunia.

Addis Ababa, Ethiopia - 21/08/2012. Wananchi wa Ethiopia wameaanza maombelezi baada  ya waziri mkuu wa nchi hiyo Meles Zanawi kufariki nchini Belgium kwa matibabu.
Msemaji wa serikali   Simon Bereket  akiongea baada ya habari za kifo cha Meles Zanawi alisema " makamu wa waziri mkuu Hailemariam Desalegn ataogoza hadi hapo uchaguzi mwingne mwaka  2015."
Waziri mkuu Meles Zanawi  alifariki dunia alipokuwa katika matibabu nchini Belgium na alichukua madaraka ya uongozi baada mapinduzi yaliyopelekea kuangushwa kwa Haile Mariam mwaka 1991.

 Sergie Lavrov aonya mashambulizi zidi ya serikali ya Syria.

Moscow, Urussi - 21/08/2012. Urussi imeonya na kusema kitendo chochote cha kufanya mashambulizi nchini Syria hakitakubalika.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urussi Sergie Lavrov aalionya kwa kusema " haitakiwi kuingilia maswala ya ndani ya nchi huru yoyote ikiwemo Syria, na nikinyume na sheria za kimatafa na nimekuwa nasisitiza hilo kila wakati na naonya ya kuwa kitendo chochote cha kuishambuli Syria kitaleta maafa katika jamii nzima ya maeneo hayo."
Waziri Sergie Lavrov aliyasema hayo baada ya kauli ya rais Baraka Obama kudai kuwa upo uwezekano wa nguvu za kijeshi kutumika ikiwa serikali ya Syiria itatumia siraha za sumu zidi ya wapinzani wanaopigana vita na serikali ya rais Bashar al Assad.

Waliotenda makosa ya jinai kunyongwa hivi karibuni asema rais wa Gambia.

Banjul, Gambia - 21/08/2012. Rais wa Gambia ametangaza kuwa watu wote waliukumiwa kunyonwa nchini humu watapata adhabu hiyo ufika mwezi wa Septemba.
Rais Yahya Jammen akiongea katika siku kuu ya kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani alisema." ningependa kuthibitisha  ya kuwa wale watu waliohukumiwa vifo baada ya kukutwa na makosa kama ya uuaji, ubebajiwa wa madawa ya kulevya, ushoga, na makosa mengine ya jinai basi adhabu zao zitatekelezwa kwa mujibu wa sheria za nchi inavyo eleza.
""Serikali inabidi kuonyesha makali yake kwa wale wote ambao wanakiuka sheria na kuvuruga amani ya nchi  kwa njia moja au nyingine."
Rais Jammen ambaye alichukuwa madaraka mwaka 1994 baada yamapinduzi ya kijeshi na amekuwa akilaumiwa kwa kuongoza nchi kwa vitisho jambo ambalo serikali yake imekuwa ikilikana.

Monday, August 20, 2012

Machimbo ya madini yafunguliwa baada ya mauaji.

Uchaguzi wa rais wa Somalia wakwama.

Mogadishu, Somalia - 20/8/2012. Uchaguzi wa kumchagua rais wa Somalia umesimapishwa kwa mdai yakuwa wananchi wa Somalia hawakuwa tayari kwa upigaji wa kura.
Uchagu huo ambao ulikiwa kufanyaka leo 20/08/2012 umeesimamishwa kwa madai ya kuwa kuna baadhi ya matakwa ya uchaguzi lazima  yatekelezwe kwanza.
Serikali ya mpito iliyopo  ambayo iliteuliwa kwa msaada wa nchi za Ulaya Magharibi inamaliza leo mnuda wake rasmi kisheria.
Kufuatia umuzi huo, uongozi wa nchi ya Somalia utasimamiwa na viongozi 225 walioteuliwa kwa baraka za viongozi wakiasili na kuapishwa rasmi leo.
Somalia nchi ambayo tangu mwaka 1991 imekuwa ikikumbwa na mvurugiko wa amani na kusabisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Machimbo ya madini yafunguliwa baada ya mauaji. 

Johannesburg, Africa ya Kusini - 20/08/2012. Machimbo ya madini ya platinum yaliyopo nchini Africay Kusini yamefunguliwa baada ya kufungwa kutokana na vurugu kati ya polisi na wafanyakazi jambo ambalo lilipekea watu 44 kuuwa kutokana na kupigwa risasi. 
Kampuni inayosima mchimbo hayo Lonmin ilisema" machimbo ya Marikana yamefunguliwa na theruthi moja ya wafanyakazi 28,000 wa machimbo hayo wamerudi kazini."
Machimbo hayo ambayo yamekuwa katika habari baada ya mauaji yaliyotokea kati ya polisi na wafanyakazi wa machimbo hayo kutupiana risasi. 
Kufuatia mauaji hayo rais Jacob Zuma ameteua kamati maalumu ili kuchunguza chanzo cha muaji hayo ambayo yametokea tangu serikal ya kibagu ya Afrika ya Kusini kung'olewa.


Izrael kutumia ujumbe wa siku kwa kutoa tahadhali.

Jerusalem, Izrael - 20/08/2012. Serikali ya Izrael imekamilisha na kufanikiwa kutuma ujumbe kwa kupitia simu za mkono kuwajulisha wanachi wake ikiwa kama kunashambulizi lolote la kijeshi.
Zoezi hili ambalo lilifanyika kwa mudawa siku tano nakjuisha hivi karibuni limefanyika huku kukiwa kuna hali ya utata ya kati ya Izrael na Iran nchi ambazo zimekuwa zikilumbana kwa vitisho vya kivita jambo ambalo serikali ya Marekani ikiingilia kati ili kuituliza Izrael baada  ya kutilia mashaka ya kuwa huenda serikali ya Izrael kaamua kufanya mashambulizi bila kushauriana na washiriki wake.
Lakhadar Brahim adai kazi ni kubwa juu ya amani ya Syria.

Algies, Algeria - 20/08/2012.  Mkuu mpya ambaye ameteuliwa kusimamia uletwaji wa amani nchi Syria amesisitiza yakuwa kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha amani inarudi nchini  Syria.
Lakhdar Brahimi ambaye ni raia wa Algeria alisema "kwa sasa nchini Syria kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe na inahitaji kazi ya ziada ilikuweza kusimisha vita hivyo kwa jirani anamuua jirani yake na wakati mwingine kaka namuua kaka yake."
Hata hivyo waziri wa mambo wa mambo ya nje wa Syria amekanusha madai ya  Lakhdar Brahim
na kusema "serikali ya Syria ina pambana na magaidi ambao wanasaidiwa na nchi zenye kutaka serekali ya iondoke madarakani na kuweka vibaraka wao ambao watatumikia."
Lakhdar Brahim amechukua nafasi ya Kofi Annani ambaye amejiudhulu katika kazi hiyo ya kusimamia kuleta amani nchini Syria.

Nchi za Amerika ya Kusini zaunga mkono uamizi wa Ekwado kwa Julian Assange.

Quito, Ekuado - 20/08/2012. Mawaziri wa mabo ya nchi za nje wa serikali za Amerika  ya Kusini wameagiza kuanzishwa kwa mazungumzo kati ya serikali ya Ekuado na Uingereza ilikutataua mzozo uliotokea kati ya nchi hizo mbili juu mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Juliane Asange.
Mawaziri hao kwa pamoja walikubaliana na kuiunga mkono Ekuado kwa uamuzi wake wakumpa hifadhi ya kiutu Julian Assange ambaye anakabiliwa na shutuma za ubakaji nchi Swedeni, jambo ambalo anakusha.
Julian Assange ambaye aliongea kwa mara ya kwanza huku akiwa kasimama katika dirisha la ubalozi wa Ekuado iliyopo jiji London Ungereza ambapo alikimbilia kwa madai upo mpango ukiopo wa kumrudisha nchini Swedeni ni wa kutaka apelekwe nchini Marekani ambapo anadai amefunguliwa mashitaka kwa kutoa habari za kisiri za Marekani katika mtandao wake wa Wikileaks.