Saturday, July 31, 2010

David Cameron ataka Uturuki kuwa mwanachama wa EU.

David Cameron ataka Uturuki kuwa mwanachama wa EU.

Ankara, Uturuki - 31/07/2010. Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron, amesisitiza umuhimu wa Uturuki kujiunga na jumuia ya nchi za Ulaya.
David Cameron, aliyasema hayo wakti wa zira aliyo ifanya hivi karibuni nchini Uturuki. Akisisitiza waziri mkuu huyo wa Uingereza alisema "sionelei kama ni hekima kwa Uturuki kukataliwa kujiunga na jumuia ya Ulaya kwani ni mwanachama na mshiriki wa NATO, na inachangia vikamilifu katika NATO, naiweje tunalinda pamoja na baadaye mmjoa wetu alale nje ya turubai -tent." Kwa mujibu wa wachunguzi wa mambo ya kigeni wanasema Uturuki imekuwa inabadilisha mwelekeo wake baada ya kuona baadhi ya nchi za jumuia ya nchi za Ulaya hazifurahii au kukubali Ututuki kujionga na jumuia ya nchi za Ulaya. Vilevile huenda waziri mkuu wa Uingereza alipo wasiri nchini Amerika waligusia halisi na kuangalia ni wapi Uturuki inaelekea kwa sasa.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kulia akiwa na mwenyeji wake waziri mkuu wa Uturuki kushoto Recep Tayyip Erdogan, wakati alipo fanya ziara ya kiserikali hivi karibuni.
Taliban wasema. "Hatushirikiani na ISI- Pakistani."
Peshawar,Afghanistan - 31/07/2010. Kundi la Taliban limesema "" hakuna ukweli unaweza kuthibitishwa ya kuwa wanashirikiana na serikali ya aina yoyote katika vita wanavyo pigana."
Mmoja wa mtoto wa viongozi wa kundi la Taliban, Sirajuddin Haqqani, alithibitisha kwa kusema tupo kwenye vita, lakini hatushirikiani na majasusi wa Pakistan ISI, bali tupo tayari kupokea misaada kutoka kwa yoyote ili tuweze kutimiza matakwa yetu."
Sirajuddin Haqqani, alisema hayo mara baada ya kufahamika ya kuwa shirika moja la habari lilichapisha habari ya kuwa Taliban wana shirikiana na Pakistani ISI kwa ukaribu sana.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wapiganaji wa Taliban wakiwa wamebeba zana za kivita tayari kwa mashambulizi.
Naomi Campbell ajiaanda kikamilifu kuikabili mahakama.
London, Uingereza - 31/07/2010. Mwana mitindo maharufu duniani Naomo Campbell, amewaajili wanasheria maharufu duniani, kumtetea katika kutoa ushahidi kwenye koti ya mahakama inayo shughulikia kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu iliyopo jijini Hague, nchini Holland.
Kwa mujibu wa msemaji wa mwana mitindo huyo, "wanasheria watakao mwakilisha Naomi Campbell ni Sir Ken Macdonald ataongoza jopo la wanasheria katika kujibu shutuma ya kuwa aliyekuwa rais wa Liberia Charles Taylor alituma watu wampelekee almasi baada ya kumaliza kula chakula cha jioni na aliyekuwa rais wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela."
Kujiaandaa huko kumekuja mara baada ya mahakama kumtaka Naomi akajieleze kuhusu shutuma hizo zinazo mkabili.
Picha hapo juu ni ya mwanamama Naomi Campbell ambaye anasadikiwa alipewa almasi na rais wa Liberia.