Friday, October 28, 2016

Tony Blair ateta lake juu ya Brexit



London Uingereza - 28/10/2016. Waziri wa zamaniwa Uingereza Tony Blair, ameongelea wasiwasi wake kuhusu madhara ambayo huenda yakatokea baada ya Uingereza kuanza rasmi mazungumzo ya kujitoa katika jumuiya ya muungano wa nchi za umoja wa Ulaya.

Akiongea na BBC 4 radio, Blair alisema "Ikiwa tutatoka katika jumuiya ya Ulaya, basi madhara yake yatakuwa makubwa kijamii na kiuchumi."
Blair aliyasema hayo kwa kusisitiza kuwa watu 48% ya wakipiga kura walipiga kura ya kubaki ndani ya Umoja wa Ulaya na kwani walijua umuhimu wake.

"Wananchi wanatakiwa wapewe nafasi ya kuliangalia hili suala kwa undani, ikibidi kuwepo na kura ya nyingine kuhusu Uingereza kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya."

Hata hivyo Maria Caulfield, mbunge wa chama tawala cha Conservative na mmoja wa viongozi wanao shughulikia Uingereza kujitoa katika muungano wa umoja wa Ulaya amesema " Blair anatakiwa  kutoa mawazo ya kuijenga Uingereza iliyo amua kuwa nje ya jumuiya ya nchi za Ulaya na siyo vinginevyo"

"Blair anapinga demaokrasi, wanachi walishaamua na matakwa yao lazima sisi kama viongozi tuyatekeleze." Alisisitiza  Caulfield.

Maoni hayo ya Tony Blair yamekuja kufuatatia maswali mengi yanayo ulizwa kuhusu nafasi ya Uingereza baada ya kujitoa rasmi katika muungano wa jumuiya ya nchi za Ulaya na kushuka kwa thamani ya fedha ya Uingereza tangu Waingereza kupiga kura ya kukataa kuwa jumuiya ya Ulaya.