Wauaji wa kujitolea muhanga watishia amani Urusi.
Wauaji wa kujitolea muhanga watishia amani Urusi.
Posted by Kibatala at Wednesday, March 31, 2010 0 comments
Kanisa Katoliki "Vyombo vya habari vinanchafua jina la Kanisa." Vatican, Vatican City - 26/03/2010. Msaidi wa Papa Benedikt XVI amelaumu vyombo vya habari kwa kujaribu kuharibu jina na kuchafua Kanisa Katoliki na uongozi wake. Akiongea baada ya habari kutolewa ya kuwa Papa Benedict wakati akiwa Kadinali alifutilia mbali malalamiko yaliyoletwa ya kuwa baadhi ya mapadri walikuwa wananyanyasa waumini kijinsia "yanalengo la kuaribu Kanisa na uongozi wake." Kanisa Katoliki limekuwa na wakati mgumu baada ya waumini na wanafunzi waliosoma katika shule za Kanisa hilo kulalamika ya kuwa walinyanyaswa kijinsia wakati wakiwa masomoni katika shule hizo. Picha hpo juu anaonekana Papa Benedikt VXI, akiwasalimia waumini waliokuja kusali na kuomba Mungu kwa pamoja katika moja ya sikuku za Kikristu ndani ya la jiji Vatican. Nchi za Kiaarabu kuchanga pesa kuwasaidia Wapalestina. Sirte, Libya - 26/03/2010. Mawaziri wa mabo ya nchi za nje wa nchi za Kiarabu wamekubaliana kutoa na kuchangisha kiasi cha $500million kwaajili ya kuwasaidia Wapalestina wanao ishi Jerusalem. Mawaziri hao wanaokutana kabla ya mkutano mkuu wa wakuuwa nchi za Kiarabu, umesema "mchango huyo ni kwaajili ya kukabiliana na ujenzi ambao unaendelea katika eneo hilo la Jeruusalemu. Picha hapo juu wanaonekana mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiaarabu wakiwa katika kikao katika mti wa Sitre. Iyad Alawi ashinda uchaguzi wa Irak.
Posted by Kibatala at Friday, March 26, 2010 0 comments
Baraka Obama atia saini muswada mpya bima ya afya kwa Waamerika.
Washington, Amerika - 23/03/2010. Rais wa Amerika amesaini muswada wa bima ya afya na kufanyiwa mabadiliko ambayo itawawezesha Waamerika wapatao million 32 watapata matibabu bila matatizo.Posted by Kibatala at Tuesday, March 23, 2010 0 comments
Serikali ya rais Obama ya weka historia
Posted by Kibatala at Monday, March 22, 2010 0 comments
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa atemelea Gaza.
Posted by Kibatala at Sunday, March 21, 2010 0 comments
Tiger Woods,apata mthiani mwingine.
Orlando, Amerika - 20/03/2010. Mcheza gofu na bingwa wa mashinado makubwa ya mchezo huo Tiger Woods na wanasheria wake wanajaribu kuzuia visanamu vya mwan gofu huyo visiuzwe. Kwa mujibi habari zilizo patikana, zinansema, visanamu hivyo vya kimapenzi, vinamleta wakati mgumu Tiger Woods, kwani ni muda ameweza kuweka sawa unyumba wake, baada ya kuyumba kwa muda. Hata hivyo kampuni ambayo inafanya mpango wa kuuza visanamu hiivyo Pipedream ahija eleza lolote kutokana na swala hilo. Picha hapo ni ya Tiger Woods,ambaye alikuwa na matatizo ya kifamili siku za nyuma na sasa ameyamaliza baada ya kuomba msamaha kwa mke wake, famili kwa ujumla na washabiki wake. Pope aomba msamaha kwa niaba ya Kanisa.Posted by Kibatala at Saturday, March 20, 2010 0 comments
Zuma ashinda kura za maoni. Cape Town, Afrika ya Kusini -18/03/1020. Rais wa Afrika ya Kusini ameshinda kura za maoni ambazo zilikuwa zimepigwa hivi karibuni, baada ya vyama vya upinzani kudai kura hizo zipigwe. Vyama vya Congre of people na Democratic Alliance ndivyo viliongoza kwa kutakura za maoni zipigwe. Kura za maoni zilizo pigwa 241 zili kubali uongozi rais Jakob Zuma, na 81 zilipinga uongozi wake. Kura hizo ni za kwanza tangu Afrika ya Kusini kutoka katika serikali ya kibaguzi mwaka 1994. Picha hpo juu anaonekana rais wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma, katikati akiwa anashiriki katika mila na utamaduni wa kabila lake la Zulu ambapo huwa anashiriki kikamilifu bila kuficha. Anyongwa kwa makosa ya kifedha. Pyongyang, Korea ya kaskaziani - 18/03/2010. Serikali ya Korea ya Kaskazini ilimuhukumu kifo na kumyonga afiasa mmoja aneye shughulika na mswala ya fedha na uchumi baada kubainika alikuwa anakwenda kinyume na sheria. Afisa huyo Pak Nam-ki, aliuwawa kwa kupigwa risasi. Hata hivyohabari kutoka Korea ya Kusini zinamsema , kuuwawa kwa bwana Pak kunakuja baada ya kubainika alikuwa anapingana na sera za serikali ya mapinduni ya Korea ya Kusini. Picha hapo juu, ni ya bendera ya Korea ya Kaskazini, nchi ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa kukiuka haki za binadamu kila wakati. Kitendawili cha Iran jibu bado kwa Amerika na Urusi.
Posted by Kibatala at Thursday, March 18, 2010 0 comments
Sony yaingia mkataba tena na (Michael Jackson) Jackson Estate. New York, Amerika - 16/02/2010.Kampuni ya msiki ya Sony, imetiliana mkataba na Michael Jackson estate ili kuimiliki albamu kumi za marehemu Michael Jackson. Mkataba huo wenye thamani ya $250 million ambao ni wa miaka saba. Kwamujibu wa wachinguzi wa mabo ya muziki wanasema Sony itaweza pata faida kubwa hasa wakati wa kuazimisha siku ya kukumbuka ya kifao cha Michael Jackson. Picha hapo juu ni ya Michael Jackson akifanya mavitu ya kujiandaa na maonyesho, enzi za uhai wake.
Posted by Kibatala at Tuesday, March 16, 2010 0 comments
Rais wa Zimbabwe aunga mkono cham cha Consevertive.
Posted by Kibatala at Sunday, March 14, 2010 0 comments
India na Urussi kushirikiana katika kuendeleza nguvu za kinyuklia. New Delhi, India - 13/03/2010. Serikali ya India na Urussi zimetilia sahihi mkataba wa kuanzisha ujenzi wa mitambo ya nguvu za nyuklia nchini India. Mkataba huo ulifanyika jiji Delhi wakati waziri mkuu wa Urussi, Vladimir Putin alpo tembela nchini India. Akiongea kuhusu mkataba huo waziri mkuu wa Urussi, Vladimir Putin alisema" tunajenga uhusiano na India hasa katika sekta ya Nyuklia." Naye waziri mkuu wa India Manmohan Singh, alisema " uhusianowetu na Urussi ni wa uhakika katika nyanja tifauti." Picha hapo juu wanaonekana waziri mkuu wa Urusi, Vladimir Putin kushoto akiongea na waziri mkuu wa India Manmoham Singh kulia wakati walipo kutana jijini Delhi hivi karibuni. Kanisa Katoliki lakumbwa na kashfa nyingine nchini Ujeruman. Munich, Ujeruman -13/03/2010. Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki nchni Ujerumani ameomba masamahaa kwa niaba ya kanisa kutokana na matukio na matendo yaliyo tokea miaka ya nyuma. Askofu,Robert Zollitsch,aliyasema" Kanisa lita yafanyia uchunguzi madai yote, litawapatia huduma za kiushauri wale wote walioathirika na matukio hayo." Kuomba msamaha huo kunakuja baada ya Kanisa Katoliki kukumbwa na kashfa shutuma kubwa kufuatia malalamiko yaliyo letwa na watu ambao waliathilika na matukio hayo yaliyo tokea ndani ya Kanisa Katoliki. Picha hapo juu anaonekana, Askofu Mkuu Robert Zolliisch akiongea kuhusu matukio yaliyo toke ndani ya kanisa.
Posted by Kibatala at Saturday, March 13, 2010 0 comments
Kupinga kuvaa hijab haku mkomboi mwanamke. Strasbourg, Ufaransa - 11/02/2010. Kiongozi mwandamizi wa shirika la kutetet haki za binadamu katika bara la Ulaya, Thomsas Hammarberg amesema " sheria za kutaka kuwazuia wakina mama kuvaa hijab za aina yoyote katika baadhi ya nchi za ulaya ni kukandamiza haki za wanawake na zinaweza kuleta athatari siku za baadaye." Aliyaongea haya wakati wa siku ya wanawake duniani. Akiongezea Thomsas Hammerberg, alisema "kuwazuia wanawake hao kuvaa hijab hakutaleta ukombozi wa wanawake na kunaenda kinyume na maadili ya demokrasi na hasa swala zima la uhuru wa mtu binafsi kuingiliwa katika maaamuzi yake yanayo mfaa. Picha hapo juu wanaonekana, baadhi ya wanawake waliopa katika bara la Ulaya wamevalia hijabu amabzo zinataka kupigwa marufuku.
Posted by Kibatala at Thursday, March 11, 2010 0 comments