Sunday, June 16, 2013

Wairan wapata rais mpya.

Rais wa Urusi aweka wazi nani mwenye damu ya za Wasyria.



London, Uingereza -  16/06/2013. Rais wa Urusi Vladmir Putin  amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa wakuu wa G8 ambao utafanyika katika mji wa Enniskillen uliyopo Ireland ya Kaskazini.

Wakiongea na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo ya faragha, viongozi hao wa Uingerza na Urusi, wamepishana kuhusu hali halisi ya matukio yanayo tokea nchini Syria.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alisema "rais wa Syria Bashar al Assad mikono yake imejaa damu inayo mwagika nchini Syria na lazima awajibike na ataoke maarakani."

"Na wale wanaopigana na serikali ya Assad tunawasaidia ili kuweza kuikomboa nchi yao na baadaye waweze kujenga nchi yenye misingi ya kidemokrasi."Alimalizia Waziri mkuu Cameron

Naye rais wa Urusi Vladmir Putin alisema " Damu inayo mwagika nchi Syria ni damu ambayo impo mikononi mwa wale wote wanao pigana vita nchini humo. Na hao wanaopigana na serikali ya Assad ni watu ambao wanakula viungo vya watu, je hawa ndiyo watu wanaotakiwa kuisaidiwa?" Alihoji rais Putin.

"Serikali ya Urusi imekuwa ikitoa siraha kwa serikali halali ya Syria  na hakuna sheria ambayo imemevunjwa kimataifa na hilo linajulikana katika sheria za kimataifa." Alimalizia rais Putin.

Mkutano kati ya rais Putin na waziri mkuu David Cameron  umeonyesha kuwa kwenye mkuutano wakuu wa G8 wa mwaka huu, ambao utawakutanisha wakuu wa  nchi za Kanada, Japan,  Ujerumani, Itali Urusi, Marekani Ufaransa na Uingereza huenda ukawa na changamoto kubwa katika maamuzi yao kwa kuzigatia kuwepo na  misimamo tofauti ya nchi hizo kuhusu hali ilivyo nchini Syria.

Wairan wapata rais mpya.


Tehran, Iran - 1/06/2013. Wananchi wa Iran wamemchagua Hassan Rouhani kuwa rais mpya wa Iran, baada ya kupata  kura nyingi kuliko wapinzani wake katika uchaguzi mkuu wa kumchagua rais uliyofanyika nchini humo tarehe 14/06/2013.

Hassani Rouhani alishinda kwa kupata kura  millioni 18.6 zidi ya wapinzani wake Mohammad Baqer Qalibar aliyepata kura millioni 6.07  na Saeed Jalili aliyapata kura million 4, na hivyo kutangazwa rasmi ya kuwa atashika kiti cha urais kilicho achwa wazi na rais Mohmoud Ahmedinejad baada ya kumaliza muda wake wa urais.

Akiongea mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais, Rouhani alisema "nawashukuru ndugu zangu wa Iran kwa kunipa fursa ya kuwa kiongozi, na nitamtumikiwa kila Muiran kwa moyo wangu wote ili kuleta maendeleo kwa nchi yetu Iran."

Hassani Rouhani anajulikana kuwa mmoja ya watu wanaosimamia mageuzi ya kimaendeleo na alisha wakuwa kiongozi katika majadiliano ya kinyuklia kati ya Iran na shirika linalo shughulikia maswala ya kinyukilia hapo mwanzo kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa rais wa Iran.

Moto wa Snowden bado wawaka ndani ya Kongesi ya Marekani.


Washington, Marekani - 16/06/2013.  Gazeti la serikali nchini Marekani  limetoa ripoti kamili ya idadi ya simu ambazo zilisikilizwa,  kuufuatia  kutolewa siri  yakuwa serikali ya Marekani ilikuwa ikizichunguza na kusikiliza kwa siri simu zote zilizo kuwa zikiingia na kutoka nchini Marekani.

Gazet hilo la serikali lilisema yakuwa  ni simu 300 tu ndizo zilizo sikilizwa kwa msimu wa mwaka jana kati ya mamilioni ya simu na email ambazo zilikuwa zikifuatiliwa na (NSA) shirika la usalama la Marekani.

Kutangazwa kwa idadi ya simu zilizosikilizwa kumekuja baada ya aliyekuwa mmoja wa mfanyakazi
 wa shirika la usalama Edward Snowden kutoa siri ya kuwa Marekani ilikuwa inazisikiliza simu na kusoma email zote zilizo kuwa zikingia na kutoka nchini humo.

Hata hivyo viongozi wahusika katika maswala ya usalama wa Marekani, wamelaani kitendo cha Snowden na kusema kuwa kimehatarisha usalama wa Marekani na washiriki wake katika harakati za kupambana na ugaidi  duniani.

Korea ya Kaskazini yatoa mthiani kwa Marekani.



Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 16/06/2013. Serikali ya Korea ya Kaskazini ipendekeza kwa serikali ya Marekani kuandaa mazungumzo mapya ambayo yatafaidisha pande zote mbili.

Kwa mijibu wa habari kutoka Korea ya Kaskazini zinasema "tunapendekeza mazunguzo na serikali ya Marekani ili kuweza kuzungumzia hali ya usakama katika eneo la Korea ya Peninsula na kuweza kupata suruhisho litakalo leta amani ya kudumu."

Hata hivyo baada ya pendekezo hilo kutoka kwa Korea ya Kaskazini, serikali ya Marekani haijatoa jibu lolote.

Korea ya Kaskazini imesisitiza ya kuwa pendekezo hilo ni muhimu kwa Marekani kulifikiria kwani ni nafasi muhafaka ili kufikia makubaliano kati ya nchi hizo mbili kuhusu hali ya usalama katika eneo la Korea Peninsula.

Uhusiano wa Misri na Syria wazidi kuwa  mchungu.


Cairo, Misri - 16/06/2013.  Rais wa Misri ametangaza kufunga mahusiano ya kidiplomasia na Syria na kuangiza ofisi za kibalozi zilizopo nchini Misri na Syria kufungwa.

Rais Mohamed Mosri, aliyasema hayo mbele ya maelfu ya watu waliokusanyika ili kumuunga mkono na serikali yake ambayo imetimiza mwka tangu kuchukua madaraka Juini 30/2012.

Akizungumza katika hotuba hiyo Mosri alisema " lazima jumuiya ya kimataifa kukemea kitendo cha  jeshi  la Hezbollah katika harakati zake za kumsaidia   Bashar al Assad na kundi la Hezbollah lazima lifahmu yakuwa halina nafasi nchi Syria."

Akiongezea Mosri alimtaka rais wa Syria Bashaar al Assad kuondoka madarakani,  na vile vile aliukuunga mkono nia ya Marekani yakutaka kuwekewa vikwazo kwa serikali ya Syria kutokutumia anga lake katika vita zidi ya makundi ya kivita yanayo pingana na rais  Assad.