Tuesday, May 31, 2011

Mshukiwa wa mauaji ya Serbia,Meja Ratko Mladik kupelekwa Uhollanzi.

Mshukiwa wa mauaji ya Serbia, meja Ratko Mladik kupelekwa Uhollanzi.
Belgrade, Serbia - 31/05/2011.Mahakama kuu nchini Serbia imekataaa na kuitupilia mbali rufaa ya mshukiwa na muhusika mkuu wa mauaji ya liyo tokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo tokea miaka ya 1991-95.
Mtuhumiwa huyo Ratko Mladik, ambaye alikuwa mkuu wa majeshi anakabiliwa na mashitaka ya dhidi yake kwa kuhusika na mauaji ambayo yalisababishwa na vita hivyo, wakati yeye akiwa kama mkuu wa majeshi.
Kufuatia kukataliwa rufaa hiyo, mkuu wa majeshi huyo Ratko Mladik, anatarajiwa kupelekwa kwenye mahakama kuu ya kutetea haki za binandamu iliyopo nchini Hollanzi ili kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Hata hivyo kabla ya kupelekwa nchini Uhollanzi, Ratko Mladik, aliruhusiwa kutembela kaburi la mwanaye wa kike ambaye alijiua baada ya baba yake kushutumiwa ya kuwa anamehusika katika mauaji.

Monday, May 30, 2011

Rais wa Soka asema hakuna shaka ni matatizo ya muda.

Zurich, Switzaland - 30/05/2011 Rais wa shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu duniani FIFA, amekataa ya kuwa shirikisho hilo lipo na mvutano ndani ya uongozi wake.
Sepp Blatter, alisema "shirikisho hilo halina mvutano na matatizo yalito tokea ni kutokana na mlolongo wa shutuma ya kuwa ndani ya shirikisho hilo kuana milungura na rushwa ambazo zimefanyika na matatizo yaho ni ya muda yatatafutiwa uvunbuzi."
Rais huyo wa FIFA anatarajiwa kuwa mgombea pekee wa kiti cha urais baada ya mpinzani wake Mohamed bin Hammam kujitoa kutokana na shutuma hizo za rushwa.
Rais wa Afrika ya Kusini kutafuta suruhisho kati ya Walibya.
Tripol,
Libya 30/05/2011. Rais wa Afrika ya Kusini amewasili nchini Libya kutafuta njia mbadala za kuweza kuleta amni na kusimaisha vita vinavyo endelea kati ya kundi linalo pinga serikali ya Libya na ambalo lina ungwa mkono na serikali za Ulaya Mgharibi.
Kwa mujibu wa habari kutoka ofoce ya rais zinasema, "rais Jokob Zuma atakuwa nchini Libya ili kuongea na kujadiliana na kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ili kusimamisha mapigano.
hata hivyo kundi la upinzani lenye makao yake makuu Benghazi limesma" inaelekea kuwasili kwa rais wa Afrika ya Kusini kunaleta utata, kwani mpaka sasa hakuna dalili za au amelezo ya kuwa Muammar Gaddafi atatoka madarakani na kuondoka.".
Kuwasili kwa rais wa Afriaka ya Kusini nchi Libya kunatazamiwa kuleta maono tofauti ambayo huenda ya leta mabadiliko katika kampeni nzima ya kidemokrasi nchini Libya

Thursday, May 26, 2011

Viongozi wa nchi za G8 wakutana nchini Ufaransa.

Deauville, Ufransa - 26/05/2011. Viongozi na wakuu wa serikali wa kundi lijulikanalo kama G8 wamekutana nchi Ufaransa ili kujadili hali halisi ya mwenendo wa kiuchumi na kidemokrasia duniani. Wakihutubia nini la kufanya ili kuimarisha uchumi dunia na kuunga mkono mageuzi ya kisiasa duniani, viongozi na wakuu hao wamehaidi kutoa misaada tofauti kwa nchi tofauti kwa kuzingatia hali halisi za nchi hizo na kuhaidi kushirikiana kiuchumi kwa karibu. Vile vile viongozi hao walijadiliana kuhusu machafuko na vita vinavyoendela Libya jambo ambalo linapingwa na baadhi ya viongozi wanao udhuria mkutano huo wa G8 na mageuzi ya nayo endelea katika nchi za Kiarabu.

Hatimaye Ratko Mladic akamatwa.

Belgradi, Serbia- 26/05/2011. Serikali ya Serbia imetangaza kukumatwa kwa aliyekuwa mkuu wa jeshi Bosnia Serbi ambaye anakabiliwa na mashitaka ya mauaji wakati wa vita vilivyo tokea mwaka 1992-95. Generali Ratko Mladic ambaye alikuwa natafutwa ili ajibu amshitaka dhidi yake, alipotea mara baada ya kesi dhidi yake kufunguliwa na mahakama ya kimataifa. Akitangaza kuhusu kukumatwa huko, rais wa Serbia Boris Tadic alisema "kwaniaba ya wanchi wa Serbia napenda kuwatangazia ya kuwa Ratko Mladic amekamatwa, na kuanzia sasa tunafungua kitabu kipya ambacho kitatuwezesha kusamehena na kukubaliana kuishi pamoja." "Na tunahaidi wale wote wafanyao mabaya lazima watajibu mashitaka"alimalizia kwa kusema haya rais wa Serbia Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "Ratko Mladic hakuwa na matata au kuleta kipingamizi wakati wakukamatwa kwake na inasemekana anamatatizo katika moja ya mkono wake."

Serikali ya Libya kuitaka Uhispania katafuta njia ya luleta amani.

Madrid, Uhispania - 26/05/2011.Serikali ya Uhispania imepokea maombi kutoka serikali ya Libya ya kutaka kuwepo na mazungumzo ya kusimamisha vita vinavyo endelea nchini Libya. Habari kutoka ofosi ya waziri mkuu wa Uhispania, zinasema " tumepokea mswaada kutoka serikali ya Libya ambao unaomba kuwa na mazungumzo ya kuleta amani nchini Libya." Akiongea mbele ya waandishi wa habari, waziri mkuu wa Libya Al-Baghdadi al Mahmoud "alisema serikali ya ke ingependelea kuanza mazungumzo ya kuleta amani na kusimamisha mashambulizi nchini Libya yanayofanywa na NATO." "Na Muammar Gaddafi bado na atakuwa kiongozi wa LIbya, na kama Gaddafi akiondolewa kwa kutumia nguvu, basi hakutakuwepo na Libya watu wanayo tarajia." Hata hivyo, kundi la upinzani linalo pinga serikali ya Gaddafi, linadai lazima kiongozi huo ataoke madarakani na ndipo amani ipataikane.

Wednesday, May 25, 2011

Obama na Cameron kupambana na Gaddafi hadi mwisho.

Obama na Cameron kupambana na Gaddafi hadi mwisho.
London, Uingereza - 25/05/2011. Waziri mkuu wa Uingereza na rais wa Amerika wakubaliana kwa pamoja yakuwa wataendelea kusisitiza kwa kila hali ili kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kutoka madarakani.
Wakiongea pamoja, wakati walipo wakiongea na waandishi wa habari, rais wa AAmerika Baraka Obama na David Cameron, walisema, tunaamini zipo nguvu za kutosha za kuhakisha Muammar Gaddafi anaachia madaraka.
Wakati huo huo serikali ya Afrika ya kusini, imesema inafanya mmpango wa kutaka kuleta amani nchi Libya na kuandaa njia ya kutoka madarakani kwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.
Rais Baraka Obama yupo ziarani katika nchi za Ulaya kwa muda wa siku sita.
Kwa mujibu habari kutoka serikali ya Afrika ya Kusini, zinasema, rais wa Jacob Zuma atatembelea Libya ili kutafuta suruhisho katika nchi hivyo ambao, imekuwa na mapigano kati ya serikali ya Libya na wale wanaoipinga.
Libya imekuwa ikishambuliwa na ndege za majeshi ya NATO, ili kupunguza mashambulizi yanayofanywa na serikali ya Gaddafi zidi ya wapinzani wanaopinga serikali.
Serikali ya India kuimarisha uhusiano na bara la Afrika.
Adis Abeba
, Ethiopia - 25/05/2011. Waziri mkuu wa India amehaidi yakuwa serikali yake itakuwa karibu na Afrika, ili kusaidia kujenga uchumi wa bara zima.
Akiwahutubia katika mkutano ulio wakutanisha viongozi wa Afrika na India, waziri mkuu Manmohan Singh alisema, " kuna mafanikio ya kiuchumi ambayo yanaendelea barakani Afrika, na India itashirikiana kikamilifu na bara la Afrika, kwa kuzingatia India na Afrika kunauhusiano mkubwa kihistoria.
Serikali ya India, imekuwa mbioni kuimarisha uhusiano wake na bara la Afrika kwa kuwekeza zaidi ya $5billion, na hii inaonekana ni katika kukabiliana na mataifa kama China, na Umoja wa nchi za Ulaya ambazo zimekuwa zijaribu kushirikiana na serikali za Afrika.

Tuesday, May 17, 2011

Luis Moreno Ocampo ataka Muammar Gaddafi afikishwe mahakamani.

Den Haag, Uhollanzi , 16/05. 2011. Wakili wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi zidi ya kukiukwa haki za binadamu, amewaomba majaji wa mahakama hiyo watoe rukhsa ya kukumatwa kwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, mtoto wake wa pili Saif al Islam na mkuu wa usalama wa taifa Abdullah Senussi. Luis Moreno Ocampo, aliyasema haya mbele ya waandishi wa habari, kwa kusema " upo ushaidi wa kutosha ya kuwa haki za binadamu zimekiukwa na serikali ya kiongozi huyo tangu kuanza kwa mvumo wa kutaka aaondoke madarakani." Akiwakilisha na kuonyesha kurasa zipatazo 74 ambazo ameziwakilisha katika mahakama jijini Den haag (Hague), na zimeelezea ushaidi wa kutosha wa kukiukwa kwa haki za binadamu nchi libya na uongozi wa Muammar Gaddafi. Muamar Gaddafi ambaye ametawala Libya zaidi ya miaka 40, amekumbwa na wimbi lililotokea kwemye maoenao ya Afrika ya Kaskazini baada wanachi kutaka demokrasi na mageuzi ya kisiasa. Mkurugenzi mkuu wa IMF akataliwa dhamana na mahakama. New York, Marekani - 16/05/2011. Halimu wa mahakama jijini New York amemkatalia kumpa dhamana mkurungenzi mkuu wa shirika la fedha duniani (IMF) Internaltional Monetary Fund. Mkurugenzi hyo kwa IFM, Dominik Strauss-Kahn, amekataliwa dhamana hiyo na jaji kwa madai huenda akaondoka nchini humo kwa kutumia ndege. Dominik Strauss anakabiliwa na shitaka la kutaka kumbaka mmoja wa mfanyakazi wa hotel aliyo kuwa amelala na anatarajiwa kurudi mahakamani Mei 20.

Sunday, May 15, 2011

Serikali ya Amerika kuchunguza shirika la ulinzi la raia wa Amerika. Abudhabi, UAE - 15/02/2011. Serikali ya Amerika imeanza uchunguzi zidi ya mwanzilishi wa shikika la ulinzi lililo julikana kama Blackwater na sasa kama Xe, baada ya ya habari kuenea yakuwa amekodishwa ilikutoa ushauri wa kiulinzi na kuunda majeshi katika nchi tofauti. Erick Prince, ambaye ndiye mwanzilishi wa shirika la ulinzi la Blackwater, anesemekana amtiliana sahii mkataba na nchi za Kolombia na nchi nyingine ili kampuni yake ijulikanayo kwa sasa Xe kusaidia kupambana na wale wote wanaopinga serikali hizo. Kwa mujibu habari kutoka serikali ya Amerika zinasema " inaangalia sheria ipi iliyo vyunjwa kwa raia wa Amerika kutoa mafunzo ya kijeshi nje ya Amerika." Vile vile kunahabri nyingine ambazo zinasema "shirika hilo aliwaajili watu wenye imani ya Kiislaam kwa kuofia ya kuwa watu waimani hiyo hawatakuwa tayari kushambuliana waislaam wenzao." Shirika hilo ambalo limekuwa linato ajira kwa walinzi na wapiganaji walio acha kazi za kijeshi na ulinzi lili wahi kukumbwa na kashfa ya kuuhusika katika mauaji yaliyo tokea nchi Irak mwaka 2007.

Mkurugenzi wa IMF akabiliwa na shitaka la ubakaji.

Umoja wa mataifa waagiza kutotupa vyakula ovyo. Hong Kong, China - 15/05/2011. Shirika la umoja wa mataifa linalo shughulikia maswala ya kilimo na chakula duniani limeagiza tabia ya kutupoteza au kuharibu vyakula usimamishwe mara moja. Kwa mijibu wa shirika hilo limesema, "nchi tajiri na watu matajiri ndiyo huwa wanatupa au kuharibu vyakula kwa wingi kuliko wale watu masikini na nchi masikini." Kwa kuongea habari hizo zimesisitiza zaidi ya asilimia thelathini, huwa kuharibiwa karibu kila mwaka duniani kutokana na kutokuwa makini. Mkurugenzi wa IMF akabiliwa na shitaka la ubakaji. New York, Amerika - 15/05/2011. Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la kutathmini maswala ya fedha namisaada ya kifedha -Internaltional Monetary Fund(IFM) amefunguliwa mashitaka. Dominik Strauss Kahn, alikamatwa na polisi baada ya muhudumu mmoja katika hotel aliyo kuwa amefikia kudai yakuwa alisumbiliwa kijinsia na mkurugenzi huyo. Msemaji wa polisi, Ryan Sesa alisema, Dominik Strauss Kahn, amekamatwa na polisi wakati akiwa njiano kuelekea uwanja wandege. Hata hivyo mwansheria wa Dominik Strauss, amesema "mteja wake atakana shitaka hilo." Domink Strauss, ambaye inasemekana alikuwa mmoja ya wale viongozi waliokuwa wamepanga kugombe akiti cha urais wa Ufaransa mwaka 2012 ili kuchuana na rais wa sasa. Marekani ya sema Walibya ndiyo wataamua uongozo wao Washington, Marekani - 15/05/2011. Viongozi wa serikali ya upinzani wa Libya wameondoka kwa shingo upande baada ya selikali ya Amerika kushindwa kuikubali kimsaada wa hali na mali. Kwa mujibu wa habari kutoka ikulu ya Marekani zinasema, "serikali ya Amerika haiwezi kuitambua au kuuutambua uongozi huo, kwani uamuzi huo upo mikononi mwa wanachi wa Libya kuwachagua viongozi wao." Hata hivyo serikali ya Amerika, imesisitiza msimamo wake wake wakuunga mkono wanchi wa Libya katika harakati za kuleta mabadiliko ya kisiasa na demeokrasia. Wakati huo huo wataalamu wa mabo ya kisiasa, kidiplomasia na uchumi, wanasema "vita vinavyo endelea nchini Libya, vinasababishwa na nchi zenye hisa nchini humo, nahasa nia kubwa ni kuhakikisha Urussi na China zisitawale maeneo hayo kiuchumi."

Sunday, May 1, 2011

Papa John Paul afanywa kuwa mteule.

Vatican City,Vatican - 01/05/2011. Kanisa Katoliki limetangaza rasmi yakuwa aliye kuwa Papa John Paul wa Pili amekuwa mteule rasmi. Kufanywa huko kuwa mteule kumekuja baada ya ushahidi kutolewa ya kuwa alikuwa ni mtu wa aina ya pekee. Mmoja ya watu waliotoa ushahidi huo, ni sista wa Marie Simon Pierre ambaye alisema yakuwa "alitibiwa na Papa John Paul kupitia maombi." Sherehe hiyo iliudhuliwa na viongozi wa serikali na wakidini akiwemo rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkewe.

Mashambulizi ya jeshi la NATO laua mtoto wa Gaddafi.

Tripol, Libya- 01/05/2011. Ndege za jeshi la NATO zimeshambulia makazi ya rais wa Libya na maisha ya watu waliokuwepo katika jengo hilo. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Moussa Ibrahim, amesema " Mashambulizi yaliyo fanywa na NATO yameuwa mtot wa mwisho wa kiume Saif al Arab Gaddafi wa Kanali Muammar Gaddafi na wajukuu zake watatu." "Kijana aliye uwawa alikuwa anasoma nchini Ujerumani na hakuwa anahusika na mambo ya kisiasa na hii inaonyesha yakuwa NATO na washiriki wake wanataka kumwua kiongozi wetu. Lakini hata hivyo Koingozi Kanali Muammar Gaddafi yeye na mke wake ni wazima." Mashambulizi dhidi ya serikali ya Libya yalinza li kusinikisha kiongozi wa nchi hiyo kuacha kuwashambulia raia wa Bhengazi na kuachia madaraka ambayo amekuwa akiyashikiria zaidi ya miaka arobaini.