Sunday, September 29, 2013

Marekani na Urusi zavutana kuhusu muuza siraha raia wa Urusi.

 Rais wa Iran akumbwa na maandamano tofauti.

Iran, Tehran - 29/09/2013. Rais wa Iran amerudi nyumbani na kukaribishwa na mapokezi tofauti, baada ya kumaliza ziara ya kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi wa kila mwaka wa umoja wa mataifa.

Akiwa amewasili kwenye uwanja wa ndege wa  Mehrabad, rais Hassan Rouhani, alipokelewa na ba baadhi ya makundi yaliyo kuwa ya kipiga ukelele kupinga Marekani na Izrael na wengine wakimuunga mkono kwa kusema "aksante rais Hassan Rouhani"
Katika msafara wake kutoka uwanja wa ndege, gari la rais Rouhani lilipigwa na viatu  na kurushiwa mayai.

Rais Rouhani amekutwa na mapokezi hayo tofauti baada ya kufanya mazungumzo ya kihistoria na rais wa Marekani Baraka Obama kwenye simu kwa muda wa dakika 15, na kuwa nikitendo cha kihistoria tangu serikali ya mapinduzi ya Irani ilipochukua madaraka baada ya kuupindua uongozi wa kifalme Shah ambao ulikuwa unaurafiki na serikali ya Marekani na marafiki zake.

Marekani na Urusi zavutana kuhusu muuza siraha raia wa Urusi.



 Moscow, Urusi - 29/09/2013. Serikali ya Urusi imelaani kitendo cha serikali ya Marekani na mahakama ya nchi hiyo kukataa rufaa iliyo ombwa na raia wa Urusi Victor Bout ambaye anahusishwa na kosa la kuuza siraha kinyume cha sheria.

Victor Bout anashutumiwa kwa kuuza siraha na kuhatarisha vitega uchumi na masrahi ya Marekani, alikamatwa nchi Thailand na kuamishiwa nchi Marekani ili kujibu mashitaka ya kufanya biashara ya kuuza sirha kinyume na sheria  na kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela mwaka 2012 April, jambo ambalo serikali ya Urusi inalipinga kwa madai ni uamuzi wa kisiasa umeshinikiza maaamuzi hayo ya mahakama.

Kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya Marekani Victor Bout, alihusika katika kuuza siraha kwa kundi la Revolutionary Army Force of Colombia ambalo limetangaza kuwa kundi la kigaidi na serikali ya Marekani.

 Boko Haram wafanya mashambulizi tena kwa wanafunzi.


Jimbo la Yobe, Nigeria - 29/09/2013. Kundi linalo pingana na serikali ya Nigeria la Boko Haram limefanya  mauaji katika chuo kilichopo katika mji wa Damaturu kwenya jimbo la Yobe wilaya ya Gujba.
Akiongea kuhusu mauaji hayo msimamizi wa Molima Idi Mato alisema " watu zaidi ya 50 wameuwawa baada ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram kushambulia kwa bunduki na kuchoma moto mabweni ambayo wanafuni walikuwa wamelala wakati wa usiku."

Naye msemaji wa serikali katika jimbo la Yobe, Laarus Eli amesema " hadi kufikia hivi sasa tumesha kusanya adi ya miili ya watu 50 na polisi bado wanaendelea na kutafuta miili ya watu wengiene."
Akiongezea Lazarus Eli alisema " zaidi ya wanafunzi 1,000 walikimbialia mafichoni, mara baada ya kuanza mashambulizi hayo"

Shambulio hilo la Boko Haram limefuatia mashambulizi yaliyofanywa na kundi hilo mwezi wa Kuni ambapo walishambulia shule mbili katika eneo hilo.