Tuesday, November 10, 2015

Rais Putin asema njama za Marekani zipo wazi.

Rais Putin asema njama za Marekani zipo wazi.

Moscow, Urusi - 10/11/2015. Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema kuwa Marekani na washirika wake wanampango wa kupunguza nguvu za kinyuklia za Urusi kwa kutaka kuweka mitambo ya siraha za kinyuklia barani Ulaya.

Akiongea na katika mkutano wa Sochi, rais Putin alisema " Iran na Korea ya Kaskazini zinatumiwa na Marekani kama kigezo cha kuwekwa mitambo ya kijeshi barani Ulaya. Lakini nia yake ni kujaribu kupunguza dhamira ya Urusi ya kuwekeza nguvu zake za kijeshi.

" Hivyo napenda kuwahakikishia kuwa Urusi haitakubaliana na kitendo hicho, na kwa sasa tunatengeneza siraha ambazo zitaweza kukabiriana na siraha hizo za Kimarekani." Alisisitiza raia Putin.

Mvutano wa kijeshi kati ya Urusi na Marekani, umekuwa wa muda sasa, tangu Marekani ilipo pendekeza kuweka mitambo yake ta Kijeshi barani Ulaya kwa madai kuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa NATO jambo ambalo Urusi inalipinga.

Tuesday, June 16, 2015

Urusi kuandaa kuwekeza siraha za kinyukia kiulinzi.

Mkuu namba 2 wa Al-Qaeda auawa.

Sanaa, Yemen - 16/06/2013. Kiongozi wa pili kwa uongozi katika kundi la Al-Qaeda, Nasir Wahishi, ameuawa kufuatia mashambulizi ya kutoka angani yaliyofanywa na ndege za kijeshi za Marekani.

Kuuawa huko kwa Nasir al- Wahishi, kunasadikiwa ni pigo la pili kubwa kwa kundi la Al-Qaeda,  kufuatia pigo la kwanza la kuuawa kwa kiongozi mkuu wa Al-Qaeda Osama bin Laden mwaka 2011.

Kutokana na kuuawa kwa kiongozi huyo namba mbili wa Al-Qaeda, Qassim al Raim, huenda akachukua kiti cha uongozi wa kundi hilo katika maeneo ya Peninsula.


Rais aliyepinduliwa nchini Misri ahukumiwa kifo.


Kairo, Misri - 16/06/2015. Mahakama kuu nchini Misri, imemuhukumu adhabu ya kifo rais aliye pinduliwa Mohamed Mosri.

Mahakama imemkuta na hatia bwana Musri kwa kuhusika katika makosa ya mauaji na makosa mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu. Pia hukumu kama hiyo ilitolewa kwa  wanachama  80 wa chama  cha Undugu wa Kislaam (Muslim Brotherhood), japokuwa hawakuwepo mahakamani.

Rais Mohamed Mosri,alipinduliwa kijeshi kutoka madarakani mnamo mwaka 2013 July, na toka hapo amekuwa chini ya ulinzi, nahuku mlolongo wa kesi zikimfuta, kutokana naaliyoyafanya wakati alipo kuwa madarakani.

Urusi kuandaa kuwekeza siraha za kinyukia kiulinzi.



Moscow, Urusi - 16/06/2015. Rais wa Urusi Vladmir Putin, amesema  Urusi itaweka mitambo yake ya kinyuklia 40, ikiwa ni njia ya  kuujiami kiulinzi.

Akiongea katika  sherehe za kuazimisha maonyesho ya kijeshi, rais Putin alisema "Mizinga 40  yenye uwezo wa kubeba siraha za nyuklia zitakuwa zimekwisha wekezwa ifikapo mwisho wa mwaka wa 2015."

   Matamshi hayo ya rais Putin, yamekuja baada ya Marekani kutamka hivi karibuni, itaongeza ulinzi wa kisiraha katika bara la Ulaya ikiwa nji ya kujihami kutokana na vitisho vinavyo wekwa na Urusi.

Sunday, February 1, 2015

Mmoja wa waandishi wa habari wa Aljazeera aachiwa.

Rais Robert Mugabe mwenyekiti wa AU.


Adis Ababa, Ethiopia - 01/02/2015. Rais Robert Mugabe , amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa jumuiya ya muungano wa nchi za Afrika  AU, baada ya mwenyekiti wa sasa rais wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kumaliza muda wake.

Akiongea mara baada ya kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti, rais Mugabe alisema " kazi yangu ni kuhakikisha yote yaliyo azimiwa yanatimizwa, hivyo kama nchi za Ulaya na washiriki wake watasema kuhusu kuchaguliwa kwangu, hilo haliniusu."

"Lengo ni kuhakikisha tunatumikia wananchi wa Afrika, na hasa kuinua hali ya wanawake, japo tupo tofauti kimaumbile, wanawake wanaweza fanya kazi fulani na kuna kazi nyingine wanaume hawawezi kufanya kama kubeba motto tumboni, hivyo tunaangalia ni njinsi gani wanawake wasaidiwe katika jamii ili kuchangia ujenzi wa bara hili kiuchumi."

"Zimbawe leo tuna majaji na marubani wanawake, hivyo tunajua umuhimu wa wanawake katika jamii nzima ya kiaafrika."

Rais Robert Mugabe, ndiye rais mkubwa kiumri, na ambaye amekuwa akisifiwa na kupendwa sana katika bara la Afrika kama mginaji halisi wa Wafrika, na hasa kwa kupinga na kufokea hadharani  tabia za baadhi ya nchi zinazo taka kuleta muvurugo na kuiba mali zilizopo katika bara la Afrika kiujanja ujanja.

Mmoja wa waandishi wa habari wa Aljazeera aachiwa.
 
Kairo, Misri - 01/02/2015. Peter Greste, mwandishi wa habari wa shirika la habari la Aljazeera, ameachiwa huru na kusafirishwa kwao nchini Australia, wakati waandishi wenzake Baher Mohamed, na Mohamed Fanny wakiwa bado jela.

Greste Muaustralia na wenzake Baher na Fanny, wamekaa jela siku 400, tangu mahakama jijini Kairo kuwahukumu vifungo, baada ya kushatakiwa kukisaidia kihabari chama kilicho tolewa madarakani cha Muslim Brotherhood  kwa nguvu na rais wake Mohammed Mosri kukamatwa.

Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema kuwa " Greste alipakizwa kwenye ndege ya shirika la ndege la Misri leo hasubuhi, akiwa na kaka yake.

Mostefa Soug, mkuurugenzi mkuu wa  Aljazeera akiongea kuachiwa kwa Peter Grste alisema "tunafurahi kuwachiwa kwa Peter Greste, lakini hata hivyo bado tunasisitiza Baher na Fanny lazima waachiwe huru, na hatuta pumzika mpaka waachiwe."

Kuachiwa huko kwa Greste kumekuja kutokana na msukomo wa kimataifa unao isukuma serikali ya Misri ya kutaka kuachiwa kwa waandishi wa habari wa Aljazeera waliopo ambo mmoja wao Peter Greste kuachiwa  huru na wenzake Beher Mohammed na Mohamed Fanny bado wapo jela.

Wakwepa kodi nchini Ugiriki walikuwa kitisho kwa serikali.

Athens, Ugiriki - 01/02/2015. Mkuu wa umiliki na ukusanyaji wa kodi nchini Ugiriki Nikos Karavitis Theoharis, alilazimika kujiudhuru, baada ya kupokea vitisho kutoka kwa wakwepa kodi.

Akiongea, mara baada ya kuchaguliwa kwa serikali mpya ya Siryiza,  Theoharis alisema " Nilikuwa napokea  simu za vitisho ofisini kwangu na ujumbe kupitia mitandao yakuwa ni Euro 5,000 zitatumika kuvunja miguu yangu."

"Vitisho nilivyo kuwa nikipokea, vinaonyesha ni kwa kiasi gani wakwepa kodi walivyo kuwa wanaibia nchi bila uwoga, na hivyo baada ya kuona nipo imara ndipo walipo nitisha na kwa usalama ikabidi  nijiudhuru."
"
 
"Lakini naamini serikali iliyo ingingia madarakani, itakuwa shubiri kwa wakwepa kodi. kwani vitisho walivyo kuwa wakivitumia havita saidia"

Theohari,s aliyaongea haya baada ya kushinda kuwa kama mbuge, na ambaye anaunga mkono serikali mpya iliyo chaguliwa nchini Ugiriki, inayo pinga mbinyo na makato ya serikali kwa wananchi ili kulipa madeni ya nchi. Hatua ambayo inadhaniwa huenda ikaleta mtafaruku katika jumuiya ya umoja wa Ulaya.




Thursday, January 1, 2015

Mamilioni washerekea kuanza kwa mwaka mpya.

Mamilioni washerekea kuanza kwa mwaka mpya.

 Mungu Baba tunakushukuru, utubariki, utulinde, utuzidishie kwa kila jambo tulifanyalo na utufanye tuzidi kukuomba na kukutegemea wewe Muumba kwa kila jambo. Amina.


 Wapalestina wajiunga na Mahamakama ya Kimataifa.
Ramalhah, Palestina - 01/01/2015. Rais wa Palestina Mahamoud Abbas, ametia siani mkataba wa makubaliano wa kujiunga rasmi kuwa mwanachama wa mahakama ya kimataifa inayo shughulikia  makosa ya jina na ukiukwaji wa haki za binadamu ICC, masaa machache baada ya kamati ya usalama ya umoja wa mataifa kushindwa kupitisha ombi la uhuru wa Wapalestina.

Akiongea baada ya kumaliza kusaini kujiunga na ICC, rais Mahmoud Abbas alisema " wanatushambulia kila siku, angani, majini na kila sehemu, wapi tutapeleka malalamiko yatu? Ikiwa kakati ya usalama ya umoja wa mataifa imetukataa."

Akiunga mkoni kitendo cha rais Abbas kusaini kujiunga na ICC, Hanan Ashrawi, ambaye  ni mwanadiplomasia alisema " tumekuwa watu wapole katika majadiliano tangu 1991, wakati mpango wa kuwa na mataifa mawili ya Kipalestina na la Kizrael kuzikwa, hivyo hiki kitendo cha leo ni muhimu kwa Wapalestina."

Kufuatia kujiunga kwa Wapalestina na ICC, kumetoa uwezo kwa mahakama ya kimataifa kuweza kuchunguza mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo yamefanyika katika maeneo ya Wapalestina.

Kufuatia kujiunga kwa Wapalestina kwenye koti ya ICC, waziri mkuu wa Izrael, Benjamin Netanyahu amesema " Kitendo cha Abbas, kutawafanya Wapalestina kushitakiwa, kutokana na vitendo vyao vya kigaidi na hasa kwa kuunga mkono kundi la Hamas.
"Sisi kwa upande wa Izrael hatukubaliani na uamuzi wa Wapalestina, na tutalinda haki za Waizrael."

Uamuzi huu wa Wapalestina kujiunga na ICC, kumekuja baada ya kamati ya Usalama ya umoja wa mataifa kushindwa kupitisha muswaada ulioletwa na Wapalestina, baada ya Marekani na Australia kupinga muswaada huo, ambao ulikuwa unadai Izrael kusimamisha kitendo cha kuchukua ardhi ya Wapalestina kwa nguvu na kurudisha wanazo kalia kwa kufuata mipaka ya makubaliano ya mwaka 1967.