Tuesday, November 30, 2010

Mkutano wa utunzaji wa mazingira waanza kwa mashaka.

Google kufanyiwa uchunguzi na jumuia ya Ulaya. Brussel, Umoja wa Ulaya - 30/11/2010. Kitengo cha uchunguzi cha jumuia ya muungano wa umoja wa Ulaya kinachunguza malalamiko yaliyo tolewa dhidi ya Google kwa kukutumia vibaya umezo wake. Kwa mujibu wa makampuni mengine ya kimtando yamsema "google inavunja ushindani wa kiimtandao dhidi ya makampuni washindani." PIcha hapo juu inaonekana picha ya mtandao wa Google ambao unalalamikiwa na washindani wake kwa kuvunja ushindani. Mkutano wa kutunza mazingira waanza kwa mashaka. Cancun,Mexico - 30/11/2010. Mkutano wa kutunza mazingira unaofanyika nchini Mexico umeamza kwa vishindo huku kila nchi muhusika akitaka matakwa yake yatimizwe. Akiongea katika mkutano huo mwakilishi wa serikali ya Amerik Jonathan Pershinga alisema " tunataka kuwepo na makubaliano ya pamoja katika kudhibiti uaribifu wa mazingira duniani" Hata hivyo msimamo huo wa Amerika umeonekana kutiliwa mashaka na baadhi ya washiriki kwa kudai kuwa hakutaleta matokeo mazuri. Pichani hapo juu aanonekana mmoja ya washiriki wa mkutano wa mazingira unaofanyika Mexico akichora kapicha kuashiria ishara kuhusu matokeo ya mikutano iliyo fanyika hapo awali kabla wa sasa unaofanyika Cancun Mexico ambapo wajumbe wa nchi tofauti wanakutana kujadili mazingira. Venezuela yapewa mkopo na Urussi kwa ajili ya kuimarisha maswala ya kiulinzi. Carakas, Venezuela 30/11/2010. Serikali ya Venezuela imesema ya kuwa serikali ya Urussi itaipa mkopo wa $4 billion ambazo zitaiwezesha nchi hiyo kukuawa siraha ili kuimarisha maswala ya kijeshi na ulinzi. Akiongea katika sherehe ya miaka 90 ya jeshi la anga rais wa Venezuela Hugo Chavez alisema " Tumeamua kufanya hivyo ili kuendelea kulinda nchi yetu na maadui." Picha hapo anaonekana rais wa Venezuela Hugo Chavez wakati wa kuadhimisha sherehe za maiaka 90 ya jeshi la anga ambalo ilitaongezewa nguvu. Radi yaleta maafa na vifo ya watu nchi Afrika ya Kusini. Kwa Zulu Natali, Afrika ya Kusini - 30/11/2010.Watu wapatao saba na wengine kujeruhiwa baada ya radi kuwashambulia wakati wakiangali jengo lilijenge kwa turubai kwaajili ya Krismas. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali anayeshughulikia maafa Mthokozisi Duza alisema "watu walio jeruhiwa apo hospitali kwa matibabu." Picha hapo juu inaonyesha miali ya moto iliyo tokana na radi ikishambulia Kwa zulu Natal na kusababisha maafa ya kijamii na kwa mazingira. Rais wa Urussi atoa onyo ikiwa hakuna makubaliano na NATO.

Moscow, Urussi - 30/11/2010. Rais wa Urussi Dimtri Medvedev amesema ikiwa nchi yake aitafikiana makubaliano na NATO katika swala la kujenga mitambo ya kiulinzi basi nchi yake itajihami zaidi kiulinzi. Akilihutubuua taifa, rais Medvedev alisema "swali lililopo ni kwa NATO kukubaliana nasi katika swala zima la ujenzi wa mitambo ya ulinzi au ikiwa hakuna makubaliano basi katika kipindi cha miongo ijayao basi tutaamua kuweka mitambo yetu wenyewe ya kiulinzi na kufufua mashindano ya kisiraha." Pia rais Medvedev, aliwataka wanachi kuongeza kizazi kwa katika kipindi cha miaka ijayo taifa litakuwa na watu wachache na haitakuwa vizuri kwa ujenzi wa taifa." Picha hpo juu anaonekana rais wa Urusi Dimri Medvedev akihutubia taifa na kuongelea maswala ya kitaifa na kimataifa kwa ujumla. China inamatumaini ya kuwa ipo siku kutakuwa na Korea moja.
Beijing China 30/11/2010. Habari zilizo patikana kutoka kwa mtandao wa Wiki Leaks zinasema ya kuwa baadhi ya viongozi wa serikali ya China wanapendelea kuunga mkono na kuungana kwa Korea ya Kusini na ya Kaskazini.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "balozi wa China nchini Kazakhstan alisema wanamatumaini siku za mbaleni kutakuwa na Korea moja ingawa kwa sasa bado nchi hizo zinajulikana kama zilivyo Korea ya Kusini na Korea ya Kaskazini."
Picha hapo juu ni bendera ya Korea ya Kaskazini nchi ambayo imekuwa ina vutana na jumuia ya Kimataifa kuhusu ukweli wa swala la kinyuklia na mshiriki wa karibu wa China.
Picha ya pili ni ya bendera ya Kora ya Kusini nchi ambayo imekuwa haina ushirikiano mzuri na serikali ya Korea ya Kaskazini.

Monday, November 29, 2010

Serikali ya Amerika ya shutumu uchapishwaji wa habari za siri kwenye vyombo vya habari.

Serikali ya Amerika ya shutumu uchapishwaji wa habari za siri kwenye vyombo vya habari. Washington, Amerika - 29/11/2010. Serikali ya Amerika imeshutumu kitendo cha kuchapishwa habari za siri ambazo zimesambazwa kwenye vyombo vya habari tofauti. Akiongea mbele ya waanshishi wa habari, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika Hillary Clinton alisema "kitendo hicho ni kibaya na kinahatarisha usalama wa raia katika jumuiya ya kimataifa na maelezo yaote yalio elezwa katika habari hizo siyo msimamo wa serikali ya Amerika na watu wake." Akiongea kwa kusisitiza Hillry Clinton aliendelea kwa kusema kuwa "ushirikiano uliopo kati ya serikali za kimataifa na Amerika utazidi kudumishwa na kushinda kitendo hicho ambacho siyo kizuri cha kusikitisha." Picha hapo juu anaonekana waziri mambo ya nje wa Amerika Hillary Clinton akiongea na waandhishi wa habari kuhusu uchapishwaji wa habari za siri kwenye vyombo vya habari zilizo tolewa na WIKI LEAKS. Serikali ya Iran yazishutumu nchi za Magharibi mara baada ya mauaji ya mwansayansi wake. Tehran, Iran 29/11/2010. Rais wa Iran ameshutumu serikali za magharibi baada ya kutokea mauaji ya mwanasayansi wake wa kinyuklia ambaye ameuawawa na bomu lililo tengwa kwenye gari lake.

Akiongea mbele ya waandishi rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad alisema " hizi ni njama za serikali za magharibi na njama hizi hazitafanikiwa kusimamisha maendeleo ya sayansi ya kinyuklia." Rais wa Iran akiongelea kuhusu kuchapishwa kwa habari za siri za aliseama " habari hizo hazitaisumbua Iran, kwani ni njama za Amerika katika harakati zake za kijasusi na kwa Iran hili hatazitilia maanani na tutaendelea kushirikiana na nchi za jirani kama kawaida kwa habari zilizomo zinania ya kuharibu uhusiano wa Iran na majirani zake."
Picha hapo juu anaonekana rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad akiongea na waandishi wa habari.

Sunday, November 28, 2010

Wiki Leaks yaja na habari mpya za kustusha.

Wiki Leaks yaja na habari mpya za kustusha

Washington, Amerika- 28/11/2010. Serikali ya Amerika imekilaani kitendo cha shirika la habari lijulikanalo kama Wiki Leaks kwa kutoa habari za siri kwanye mtandao wake na kusambaza kwa mashirika mengine ya habari.
Kwa mujibu wa habari kutoka Washington zinasema " kitendo cha Wiki Leaks kutoa habari hizo za siri zitahatarisha usalama wa maisha ya jamii.
Hata hivyo mwanzilishi wa shikika hilo Jualian Assange aliema "kutolewa kwa habari hizo kutaleta mabadiliko makubwa katika jamii." "Picha hapo juu anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama na kwa nyuma anaonekanaka waziri wa mambo ya nje wa Amerika Hillary Clinton ambapo serikali ya Amerika ina hitahusishwa kwa kiasi kikubwa kwenye habari za siri zilizotolewa na Wiki Leaks.

Saturday, November 27, 2010

Waziri mkuu wa Lebanoni awasili nchini Iran

Waziri mkuu wa Lebanoni awasili nchini Iran.

Tehran, Iran 27/11/2010. Waziri mkuu wa Lebanoni amewasili nchini Iran kwa ziara ya kiserikali. Saad Hariri amewasili nchini Iran ili kudimisha husiano na serikali hiyo. Katika ziara yake Saad Hariri, atakutana na rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejadili kujadili njia za kudimisha ushirikiano wa karibu zaidi. Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Lebaboni, Saad Hariri akichuka ndani ya ndege nchini Iran tayari kuanza ziara na mazungumzo na viongozi wa serikali ya Iran jinsi ya kushirikiana kikamilifu kwa karibu sana. Korea ya Kaskazini yaonya mazoezi ya kijeshi ya pamoja.
Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 27/11/2010. Serikali ya Korea ya Kaskazini imeonya kwa kusema ya kuwa "kitendo cha serikali ya Korea ya Kusini kufanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja na majeshi ya Amerika yanaweza kuleta tukio lisilo tabilika"
Hata hivyo serikali ya China imeitaka serikali ya Amerika kuangalia kwa makini kitendo chake cha kutaka kufanya mazoezi ya kijeshi pamoja na Korea ya Kusini.
China nchi ambayo inaushirikiano wa karibu na serikali ya imetuma ujumbe kwa serikali ya Korea ya Kusini ili kujadili swala hili.
Picha hapo juu zinaonekana ndege za kijeshi za Kiamerika zikiwa kwenye melikebu tayari kwa mazoezi.
Picha ya pili wanaonekana baadhi ya wananchi wa Korea ya Kusini wakiwa wamekusanyika mbele ya ofisi ya ulinzi kudai serikali ichukua hatua dhidi ya Korea ya Kaskazini.

Saturday, November 20, 2010

Iran yasema yafanikwa kutengeneza roketi ya ulinzi

Iran yasema yafanikwa kutengenza roketi ya ulinzi. Tehran,Iran 20/11/2010. Maofisa wa kijeshi wa serikali ya Iran wamedai wamafanikiwa kutengeneza roketi ya kiulinzi na kuifanyia majaribio wakati wa mazoezi ya siku tano ya kijeshi. Akiongea Brigedia Meja General Mohammad Hassan Mansouria alisema " kwa kutumia maalifa ya wanasayansi wa hapa nyumbani tumeweza kutengeneza roketi kwa jina S-200 ambayo ni kwa ajili ya ulinzi na inauwezo sawa na ile ya Urussi S-300. Akisisitiza zaidi Brigadia huyo alisema katika mazoezi hayo tuliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katuika maswala ya ulinzi na mashambulizi ya maadui. Mazoezi ya kivita ya Irani yalianza siku ya Jumanne kwa madhumuni ya kuangalia ni kwa jinsi gani jeshi hilo tiyali kwa mashambulizi ya aina yoyote. Picha hapo juu inaonekana moja ya roketi ya Kiiran ikipaakuelekea angani baada ya kulipuliwa wakati wa mazoezi ya kivita ya jeshi la Iran.

Polisi wa Moroko na kundi la Sahrawi zashambulia na kusabisha vifo.
Sahara ya Magharibi, Morokko - 20/11/2010. Serikali ya Morokko imetetea kitendo cha serikali yake kuvamia kambi za wananchi ambao wanaishi katika maeneo ya Sahara ya Magharibi na kudai yalikuwa ya kuleta amani.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa Waziri wa mambo ya ndani zilisema " kitendo hicho cha polisi kuvamia kambi hiyo kilifanywa baada ya kundi la Sahrawi kumuua polisi."
Hata hivyo msemaji wa Sahrawi alisema " uvamizi katika kambi hiyo kulisababisha vifo vya watu wapao 36 na watu wengine 163 kuwekwa kizuizini kwa kudai haki za kila siku za maisha yao kama kazi na matibabu na vulugu hizo zilisababishwa na polisi wenyewe."
Picha hapo juu wanaonekana polisi wakiwa katika kambi ya wakimbizi wa Polisalio mara baada ya kumaliza kufanya kazi yao.
NATO kuangalia mipango mipya ya kukabidhi ulinzi kwa Afghanistan.
Lisboa, Ureno 20/11/2010. Viongozi wa NATO wanakutananchini Ureno ili kujadili na kupanga mipango ya kukabidhi maswala ya ulinzi kwa Wananchi wa Afghanistan.
Mkutano hu ambao umeudhuliwa na viongozi wapatao 28, katibu mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na viongozi wote ambao nchi zao zinashiriki kikamilifu katika vita vinavyo endelea nchini Afghanistan.
Akiongea wakati waufunguzi wa makutano huo katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussena alisema "mafanikio ya mkutanao huu ni kuhakikisha wananchi wa Afghanistan wanaweza kuongoza na kulinda nchi yao na kukabidhi madaraka yote ya ulinzi kuwa mikononi mwa. na kuendelea kudumisha ushirikiano na wananchi wa Afghanistan."
Picha hapo juu anaonekana rais wa Afghanistan Hamid Karzai kushoto akisikiliza mazungumzo yanayo tolewa na katibu mkuu wa NATO kulia Anders Fogh Rasmussen wakati wakikao cha ufunguzi kuhusu masawala ya Afghanistan.

Wednesday, November 17, 2010

Mamiliioni ya Waislaam washerekea sikukuu ya Hajji

Mamilioni ya Waislaam washerekea sikukuu ya Hajji

Makka, Saud Arabia 17/11/2010.Mamilion ya Waumini wa dini ya Kiislaam wamasherekea siku ya Iddi Al Hajj.
Kuazimisha siku kuu ya Hajj, baadhi ya Waislaam ambao wamejaliwa kwenda Kuhiji Makka huwa wana swali na kumkana shetani na mambo yake yote na kuomba masamaha kwa Mungu muumba wa vitu vyote tuvionavyo na tusivyo viona.
Picha ya kwanza ni ya kitabu Kitukufu Kuraan kitabu ambacho ni nguzo na msingi wa dini ya Kiislaam.
Picha ya pili ni ya Sura ya kwanza ya kitabu Kitukufu Kuraan Surat al Fatiha ambayo ni wajibu wa kila Mwislaam kuitambua.
Picha ya tatu inaonyesha siku ya Hajj ni siku ambayo Waislaam wote huwawana wanashirikiana wa kila kitu ili kuwa karibu na Mungu na katika picha wanaonekana Maelfu ya Waislaam waliokwenda Kuhijji wakiwa wana zunguka Al Kabba kukmilisha Hijja zao.
Rais wa Irak akataa kusaini hukumu ya kifo cha Tari Aziz.
Baghdad, Irak 17/11/2010.Rais wa Irak Jalal Talabani amsema hatasaini ruhusa ya kutaka kunyongwa aliye kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje na naibu waziri mkuu Tarik Aziz.
Rais, Jalal Talabani alisema"sita saini kifo cha Tarik Aziz, kwasababu mimi ni mjaamaa na Tarik ni mkristu na ni mzee na najisikia huruma juu yake."
Picha hapo juu anaonekana rais wa Irak, Jalal Talabani akitoka kuzungumza na waandishi wa habari na kuelezea hali halisi ya Irak kwa ujumla.
Tutafanya kazi na wanachi pamoja asema Aung San Suu Kyi.
Rangoon, Myanmar - 17.11/2010.Kiongozi ambaye anatetea demokras nchini Myanmar ana aliye achiwa huru kutoka kizuizini ameomba jumuia za kimataifa kuondoa vikwazo ambavyo vilikuwa vimewekwa zidi ya nchi yake.
Aung San Suu Kyi, ambaye alikuwa kizuizini kwa kipindi cha zaidi ya miaka kumi alisema " Nataka kusikia wananchi wa Myanmar wakisema ya kuwa wanauwezo wa kusema na kufnya vitu kwa maamuzi yao bila woga, na tutafanya kazi ya kuinua maisha ya kila mwananchi, na haki za binadamu zitalindwa na kutekelezwa kisheria."
Aung San Suu Kyi aliyasema hayo mbele ya wanachama wa chama DeNational League for mocracy(NLD) walipo kuja kumlaki mara baada ya kuachiwa kutoka kizuizini.
Picha hapo juu anaonekana bi Aung San Suu Kyi akiwasalimia watu waliokuja kumlaki mara baada ya kuruhusiwa kutoka kizuizini.

Monday, November 15, 2010

NATO kuanza kuukabidhi usalama na ulinzi kwa Waafghanistan.

NATO kuanza kuukabidhi usalama na ulinzi kwa Waafghanistan. Washington,Amerika - 15/11/2010. Serikali ya Amerika pamoja wa washiriki wake wa NATO zimeaanza kupanga plani ya ulinzi nchini Afghanistan kabla ya kwa kipindi cha miezi 18- 24. Kwa mujibu wa habari kutoka ofisi za serikali jijini Washington zinasema " kuna police wapatao 260,000 ambao watakuwa tayari kuchukua majukumu ya ulinzi na usalama na inatarajiwa kufukia 2014 maswala ya usalama na ulinzi yatakuwa chini ya Waafghanistan wenyewe." Picha hapo juu wanaonekana polisi wa Afghanistan akiwa katika ulinzi ikiwa ni moja ya mikakati ya ulinzi kwa msaada wa NATO.

Saturday, November 6, 2010

Kikwete aapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa miaka mitano mingine.

Kikwete aapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa miaka mitano mingine.

Dar es Salaam, Tanzania - 06/11/2010.Watanzania wameshuhudia kuapishwa kwa mara nyingine tena kwa Jakaya Kikwete kuwa rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akigombea kiti hicho cha urais kwa kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) alishinda kura kwa asilimia 61zidi ya wapinzani wake.
Mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi Jakaya Kikwete alisema "nitahakikisha wanachi wana kuwa na amani na kukuza uchumi wa nchi."
Picha hapo juu anaonekana rais wa sasa wa Tanzania Jakaya Kikwete akiongea na waandishi wa habari kabla ya kampeni za uchaguzi wa rais wa 2010 kuanza.
Picha ya pili anaonekana rais Jakaya Kikwete akiingia uwanjani tayari kuapishwa kuwa rais wa Tanzania kwa mara nyingine.
Picha ya tatu wanaonekana viongozi wa nchi tofauti walioudhulia sherehe za kuapishwa rais Jakaya Kikwete.
Picha ya mwisho anaonekana rais Jakaya Kikwete akiongea na rais mstaafu Benjamin Mkapa, wakati wa moja ya mkutano ya chama cha Mpinduzi ambacho ni cham tawala.

Wednesday, November 3, 2010

Baraka Obama na Demokratik wazidiwa kete na Republikan.

Baraka Obama na Demokratik wazidiwa kete na Republikan.

Washington, Amerika - 03/11/2010. Matokeo ya uchaguzi nchini Amerika yamemalizika nchini Amerika na chama cha Republikan kupata ushindi dhidi ya chama cha Demokratik.
Matokeo hayo ya uchaguzi yameweza kuipa chama cha Republikan kupata viti vingi katika bunge ambapo inaaminika yakuwa matokeo hayo huenda yakampa wakati mgumu rais Baraka Obama katika uongozi wake kwa kipindi kilichobakia.
Akiongea baada ya matokeo hayo rais wa Amerika wa Amerika Baraka Obama alisema " nina wajibika na matokeo yote ya kushindwa kwa uchaguzi kwa chama cha Demokras na hii imeonyesha ni kwa kiasi gani bado wananchi hawajaridhika na juhudi zetu, na hivyo kuna haja ya kuongeza juudi zaidi kufikia malengo ya kuinua uchumi wa Amerika."
Obama aliongezea kwa kusema "pia nitashirikiana kikamilifu na viongozi wa chama cha Republikan ili kuendeleza na kukamilisha malengo ya kuinua uchumi wa Amerika."
Picha hapo juu inaonyesha viti vya bunge na kulia vyene rangi nyekundu ni viti vya wabunge wa chama cha Republikan amba wamepata kura zaidi na kushoto ni viti vya wabunge wa Demokratik ambao wamepoteza kura na viti katika bunge.
Picha ya pili anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama wakati wa kampeni cha uchaguzi wa wabunge hivi karibuni.
Picha ya tatu anaonekana Bi Hillary Clinton akisalimiana wa watu akiwa katika kampeni za uchaguzi wa wabunge hivi karibuni.
Izrael kufikiria upya mazungumzo na Uingereza.
Tel Aviv, Izrael - 03/11/2010. Serikali ya Izrael imesema haitafanya mazungumzo na Uingereza kutokana na sheria ambayo inaruhusu mahakama kuwashitaki maafisa wa Izrael ambao watatembelea Uingereza kwa kuhusishwa na makosa ya kivita..
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana zinamsema "nchi hizo mbili huwa zinafanya mazungumzo katika maswala ya ulinzi kila mwaka."
Picha ya kwanza hapo juu ni ya nchi ya Uingereza nchi ambayo ina ushirikiano wa karibu na Izrael.
Picha ya pili ni ya nchi ya Izrael nchi ambayo inaitaka serikali ya Uingereza kubadilisha sheria ambayo ina weza kuwashitaki raia wa Izrael ambao wanashukiwa kuwa na makosa ya kivita.
Rais wa zamani wa Amerika ajianda kutoa kitabu chake.
Washington, Amerika - 03/11/2010. Aliyekuwa rais wa Amerika George Bush anatarajiwa kutao kitabu chake ambacho kiteelezea hali halisi wakati wa uongozi wake mpaka hapo alipo mwachia ofisi rais wa sasa Baraka Obama.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema rais huyo wa zamani George Bush alisema "huwa wakati mwingine anajisikia vibaya kwa kukuso kuzipata siraha za maangamizi ya jamii ambazo zilikuwa ndiyo kiini cha kuanza kwa vita hivyo."
Picha hapo juu anaonekana rais wa zamani George Bush enzi zake alipokuwa rais wa Amerika kuelekea kuhutubia bunge.

Tuesday, November 2, 2010

Somalia yapata waziri mkuu mpya.

Somalia yapata waziri mkuu mpya.

Mogadishu, Somalia - 02/11/2011. Bunge la serikali ya Somalia limekubali kwa pamoja kumpishatisha waziri mkuu mpya. Mohamed Abdullahi Mohamed ambaye aliteuliwa na rais wa sasa wa Somalia Sharif Sheikh Ahmed mapema 14 Oktoba ili kuchukua nafasi iliyo achwa wazi na waziri mkuu aliyeziudhuru Omar Abdirashid Sharmarke Septemba 21. Akiongea mara baada ya kupitishwa kuwa waziri mkuu wa Somalia, Mohamed Abdillah Mohamed alisema "majukumu yangu ya kwanza ni kupambana na ugaidi ili kuleta usalama kwa Wasomalia." Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu mpya wa Somalia Mohamed Abdillah Mohamed akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuteuliwa na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu. Vikwazo vyaendelea kuwekwa zidi ya serikali ya Sudan.
Washington, Amerika - 02/11/2010. Serikali ya Amerika imeendelea kuiwekea vikwazo serikali ya Sudan. Kwamujibu wa habari zilizo patikana zinasema "vikwazo hivyo vinania ya kurazimisha serikali ya Sudani kupitisha swala kura ya maoni ambalo uenda likaigawa nchi hiyo katika sehemu mbili." Picha hapo juu anaonekana mmjoja ya kijana akiwa ndani ya basi akiangalia kitu fulani wakati nchi yake bado inaendelea kuwekewa vikwazo.
Waingereza na Wafaransa watiliana sahii katika maswala ya ulinzi.
London, Uingereza - 02/11/2010. Serikali za Uingereza na Ufaransa zimetiliana mikataba ya maswala ya ulinzi hivi karibuni jijini London. Mikataba hiyo ambayo itaifanya serikali zote kushirikiana kikamilifu katika maswala ya ulinzi wa kinyuklia na ushirikiano wa mambo ya kijeshi kwa ujumla
Mkataba huu ambao ulisainiwa na rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron wakati walipo kutana jijini London.
Akiongea mara baada ya kumaliza kutia saini mikataba hiyo ya ulinzi waziri mkuu wa Uingereza alisema "leo tumefungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika maswala ya ulinzi kati ya nchi hizi mbili."
Picha hapo juu wanaonekana waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kulia akiongea na rais wa Ufaransa Nokolas Sarkozy mara baada ya kutiliana sahii mikataba hiyo.
Waamerika wapiga kura kuwachagua wabunge.
Washington, Amerika - 02/11/2010. Wananchi wa Amerika wameanza kupiga kura kuwachagua wabunge ambapo inasadikiwa matokeo ya uchaguzi huo huenda yakaleta mabadilikio makubwa ya kisiasa kati ya vyama vya Demokratic na Republikan.
Kwa mujibu wa ripoti zilizo patikana zinasema "chama cha Republikan huenda kikapata viti vingi katika bunge,"
Picha hapo juu anaonekana mke wa rais wa Amerika bi Michelle Obama akiwa katika kampeni kuwahamasisha wananchi wapige kura na kupigia chama cha Demokratik.

Monday, November 1, 2010

Wabrazil wamchagua rais mwanamama kuingoza nchi yao

Wabrazil wamchagua rais mwanamama kuiongoza nchi yao

Rio De Janeiro, Brazil - 01/11/2010. Wananchi wa Brazil wamemchagua kwa mara ya kwanza rais mwanamama kuiongoza nchi yao.
Dilma Vana Rousseff, 62, alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata asilimia kura 55.5% kwa kumshinda mpinzani wake Jose Serra aliyepata asilimia 44.5 za kura zpte zilizo pigwa.
Akiongea mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Brazili, Rousseff alisema "kama nilivyo haidi nitatekeleza yale yote na hasa kupigana na ufukara na umasikini na kuakikisha nchi yetu inakuwa kimaendeleo."
Dilma Rousseff, anatarajiwa kuapishwa kuwa rais mapema mwaka 2011, na kuchukua madaraka ya rais wa sasa Luiz Inacio Lula da Silva.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Brazil nchi ambayo kwa mara ya kwanza imemchagua rais mwanamke kuiongoza nvhi hiyo.
Picha ya pili anaonekana kulia Dilma Vana Rousseff, akiwa na wadau wakipata ghahawa wake wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais hivi karibuni.
Mizigo yote kufanyiwa ukaguzi wa hali ya juu.
Sanaa, Yemen - 01/11/2010. Serikali za nchi tofauti duniani zimeanza kufikiria njia mpya ya kukabiliana na mbinu za makundi ya kigaidi kwa kuangalia mbinu gani watatumia kuimarisha ukaguzi wa mizigo katika viwanja vyote vya kimataifa.
Uamuzi huo wa kuongea usalama na ukaguzi wa mizigo, umekuja baada ya kundi la kigaidi chini uongozi wa Alqaeda waliweza kupitisha mizigo ambayo ilikuwa imebeba mabomu ambayo yangetumika kulipua na kuaribu maeneo yaliyo kusudiwa na kundi hilo.
Kwa mujibu wa kiongozi mmoja wa shirika la ndege la Ryanair alisema " kufuatia hali ya tukio lililo tokea Yemen litasababisha hali ambayo wasafiri watabidi waizoee, hii ni kwa ajili ya usalama wa abiria na jamii kwa jumla."
Picha hapo juu zinaonekana baadhi ya ndege za kubebea mizizigo zikiwa zimepaki tayari kwa kubeba mizigo ambayo kuanzia sasa mizigo yote itafanyiwa ukaguzi wa hali ya juu.