Papa Benedikt ajiudhuru rasmi uongozi wake wa Kanisa Katoliki.
Papa Benedikti 85, ambaye amongoza Kanisa Katoliki kwa muda wa miaka nane alitangaza kujiudhuru wadhifa wake huo mwanzoni mwa mwezi huu kutokana na hali ya afya yake kuto mruhusu kuendelea na kazi hiyo ya kuliongoza Kanisa Katoliki lenye waumini wapatao 1.2 billion.
Akihutubia waumini waliokuja kuudhuria misa ya kumuaga, Papa Benedikti alisema "nawatakiwa baraka za Mungu ziwe nanyi na nawashukuruni sana na tuzidi kuendalea katika njia apendayo Mungu."
Papa Benedikti ambaye alizaliwa na kubatizwa kwa jina la Joseph Ratzinger amekuwa Papa wa kwanza kujiudhuru madaraka yake tangu ilipotokea miaka 600 iliyopita.
Marekani kutoa kifedha kwa wapinzani wa serikali ya Syria.
Washington, Marekani - 28/02/2013. Serikali ya Marekani imetangaza kuongeza msaaada wa kifedha kwa kundi linalo pingana na serikali ya Syria.
Akiongea katika mkutano uliofanyika nchi Itali Roma ambao ulijulikana kama mkutano wa marafiki wa Syria. waziri wa mambo ya nje ya nchi wa Marekani John Kerry alisema " kiasi cha dola za Kimarekani $60millioni zitatolewa kwa kundi Syria National Coalition (SNC) ."
"Pesa hizo zitakuwa kwa ajili ya misaada ya kiutu" aliongezea waziri John Kerry.
John Kerry yupo katika ziara za kikazi baada ya kuapishwa kuchukua wadhifa wa waziri wa mambo ya nje ya nchi ya Marekani .
Hadi kufikia sasa maelfu ya Wasyria wamekubwa na hali mbaya kiuchumi na kijamii tangu kuanza vita vya kutaka kuun'goa utawala wa rais Bashar al Assad.