Wednesday, March 27, 2013

Makubaliono ya kuundwa benki ya nchi za BRICS bado kufikiwa.

Makubaliono ya kuundwa benki ya nchi za BRICS bado kufikiwa.

Durban, Afrika ya Kusini - 27/03/2013.Viongozi wa nchi zinazo kua kiuchumi duniani wamekutana nchini Afrika ya Kusini ili kuangalia ni kwa kiasi gani nchi hizo zitashirikiana katika kukuza uchumi.
Viongozi wa nchi hizo zinazo julikana kama BRICS ambazo zinajumuisha nchi za Brazil, Urusi, India, China na Afrika ya Kusini wamekutana na kujadili  muundo wa benki ya nchi hizo na itakavyo weza  kushindana na mabenki ya nchi za Ulaya Magharibi ambazo zimekuwa zikitawala mfumo wa fedha wa dunia.
Katika kikao hicho, viongozi hao hawakufikia muafaka kamili juu  kuundwa kwa benki yao na kukubaliana kutoa muda wa kuliangalia swala hilo kiundani.
Mwenyekiti wa kikao hicho, rais wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma alisema " tunayo matumaini ya kuunda benki hiyo na kwa sasa ni wajibu wa viongozi kwenda kukaa, kupanga na kuliangalia jambo hili kiundani ili kulifanikisha."
Benki hiyo ambayo inatarajiwa kuhitaji pesa za euro billioni 50, ambazo zitachangwa na nchi hizo za BRICS ili benki hiyo iweze kufanya kazi kikamilifu.
Viongozi hao walikutana ili kutimiza mazungumzo yaliyo fanyika nchini India New Dheli, mwaka mmoja uliyo pita ambapo  azimio la kuundwa kwa benki hiyo  lilijadiliwa.

Korea ya Kaskazini yazidisha uhasama na Korea ya Kusini.

Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 27/03/2013. Serikali ya Korea ya Kaskazini imesimamisha mawasiliano ya aina zote  kati yake na serikali ya Korea ya Kusini.
Uhasama huo kati ya nchi hizi mbili umekuja baada ya Korea ya Kusini kuendelea kufanya mazoezi ya kijeshi na Marekani, jambo ambalo Korea ya Kaskazini imelitaja ya kuwa ni la kutishia usalama wake.
Habari kutoka Korea ya Kaskazini zilisema "kutokana na hali iliyopo tunaona  vita vinaweza kutokea muda wowote na hivyo kuanzia sasa mawasilino ya aina yoyote na Korea ya Kusini hayatakuwepo."
Msemaji wa serikali ya Marekani amesema "hiki ni kitendo ambacho hakitaijenga serikali ya Korea ya Kaskazini, na inabidi serikali ya nchi hiyo iangalie kama vitendo inavyo fanya ni sawa na havitasaidia katika kuleta uimara wa usalama katika eneo zima la Peninsula."
Korea ya Kaskazini imekuwa ikitishia kuishambulia Marekani na kusema ya kuwa kitendo cha kufanya mazoezi ya kijeshi kwenye Korea Peninsula kumevunja mkataba  uliyo wekwa wa vita wa mwaka 1950-53.

Sheria ya mlinda Abuu Qatada nchini Uingereza.

London, Uingereza - 27/03/2013.  Mahakama ya rufaa ya Uingereza imelitupilia mbali ombii la serikali  ya Uingereza la kutaka muhubiri maarufu wa dini ya Kiislaam arudishwe nchini kwao.
Abuu Qatada ambaye ni raia wa Jordan ameruhusiwa na mahakama ya Uingereza kuendelea kuishi nchini humo, japo serikali ya Uingereza kupitia ombi la waziri wa mambo ya ndani ya nchi hiyo Thereza May kutaka Abuu Qatada kuondolewa nchi Uingereza kwa madai anahatarisha usalama wa nchi.
Jopo la majaji wa mahakama ya rufaa lilitoa hukumu kwa kusema "hakuna ushahidi wa kutosha ya kuwa kesi inayo mkabili  Abuu Qatada nchini Jordani itaendeshwa kwa kufuata sheria na haki za binadamu."
Kufuatia uamuzi huo wa mahakama, waziri kimvuli wa mambo ya ndani, Yvette Cooper alisema " hii inasikitisha saana, na waziri Thereza anatakiwa kutumia kila sheria ili kufanikisha kuondelewa nchi kwa Abuu Qatada."
Abuu Qatada ambaye ni raia wa Jordan aliomba hifadhi nchi Uingereza mwaka 1993, baada ya jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Jordan kushindwa, na mwaka 1999 alikutwa na hatia  kwa kosa la uhaini nchini Jordan, baada ya kesi kuendelea japo hakuwepo nchini humo.

Sunday, March 24, 2013

Pervez Musharaf arudi nchini Pakistan.

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati aikimbia nchi.

Bangui, Afrika ya Kati - 24/03/2013. Kundi la waasi  linalo julikana kwa jina la Seleka, limevamia makazi ya rais wa  Jamuhuri ya Afrika ya Kati, na kumfanya akimbiliea nchini Kameron.
Rais Francois Bozize ambaye inasemekana amekimbia kwa kuvuka mto Oubangi baada ya waasi wa kundi la seleka kuchukua mji wa Bangui na baadaye kufanikiwa kuvamia ikulu ambapo alikuwa akiishi rais huyo.
Kufuatia mashambulizi hayo ya ikulu ya rais, Ufaransa imeomba kamati ya usalama ya umoja wa taifa kukutana ili kujadilli tukio hilo.
Hapo awali kundi la Seleka lilidai ya kuwa litamwondoa madarakani rais Bozize, kwani lilidai kwa kusema " haturiziki na jinsi serikali inavyo ongozwa na  hakutimiza makubaliano tuliyo saini pamoja."
Jamuhuri ya Afrika ya Kati imekuwa ikikumbwa na matatizo ya kisiasa na kusababisha zaidi ya wati 200,000 kukimbia nchi na wengine wengi kupoteza maisha yao.

Pervez Musharaf arudi nchini Pakistan.

Karachi,Pakistan- 24/03.2013.   Rais wa zamani wa Pakistan  amerudi nyumbani baada ya kuwa nje ya nchi kwa kipindi miaka minne na miezi kadhaa.
Pevez Musharraf  69, ambaye alishawahi kuwa rais wa Pakistan alikuwa akiishi nchini Dubai tangu alipo achia madaraka ya urais na kuondoka nchini humo.
Pervez Mushar ambaye amerudi nchini  Pakistan ili kujiandaa kugombea kiti cha urais,  amehaidi ya kuwa akichaguliwa kuwa rais atapambana na wale wote ambao wanavuruga amani nchini Pakistan.
Hata hivyo makundi ya Taliban na  na Alqaeda yametishia kuwa watatuma watu wakujitolea muhanga ili kupoteza maisha yake Pervez Musharraf.
Pervez Musharraf anakabiliwa na kesi ya kutotoa ulinzi wa kumlinda aliye kuwa kiongozi wa chama cha upinza marehemu bibi Benazir Bhutto, ambaye aliuwawa na mlipuko wa wa mabomu wakati alipo kuwa katika kampeni ya uchaguzi katika mji wa Rawalpindi.

Thursday, March 21, 2013

Baraka Obama Wapalestina na Waizrael lazima wafikilie upya ili amani iwepo.

Baraka Obama  Wapalestina na Waizrael lazima wafikilie upya ili amani iwepo.

Ramallah, Palestina - 21/03/2013. Rais wa Marekani amewataka viongozi wa Palestina na Izrael kukutana tena ili kuongelea swala la kuwepo na kuundwa taifa la Wapalestina litakalo pakana na Izrael.
Rais Baraka Obama akiongea kwenye mkutano  wa pamoja na waandishi wa habari, alisema "Inabidi viongizi wote lazima wafikilie upya ili kuweza kufanikisha kupatikana kwa amani kati ya Waizreal na Palestina na ni haki kwa Wapalestina kuwa na Taifa lao ili waweze kujenga maisha yao ya baadaye kwa kizazi kijacho."
Naye rais wa Wapalestina Mahamoud Abbas akichangia katika mkutano huo alisema " kikwazo kikubwa ni kuendelea kujengwa kwa makazi ya Kiyaudi katika eneo letu sisi Wapalestina na inabidi ujenzi huu usimamishwe na hali hii imekuwa ikipingwa na kulaaniwa na jumuiya ya kimataifa na hata umoja wa mataifa umesha piga kura zaidi ya mara 13 kupinga ujenzi huo."
"Hivyo ujenzi wa makazi lazima usimame ili kufanikisha mazungumzo na Waizrael."Alisema rais Abbas.
Ziara ya rais Obama katika eneo la Westbank ni ya kwanza tangu kuwa rais wa Marakani na kbla ya kuonana na viongozi wa Wapalestina aliongea kwanza na viongozi wa Izrael ambao walisisitiza nia yao ya kutaka mazungumzo ya amani kati yao na Wapalestina yaendelee.

Tuesday, March 19, 2013

Kadinali Jorge Mario Bergoglio asimikwa rasmi na kuitwa Papa Fransisko.

Kadinali Jorge Mario Bergoglio asimikwa rasmi na kuitwa Papa Fransisko.

Vatican, Vatican City - 19/03/2013. Maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki, viongozi wa serikali na marais wameudhuria kusimikwa kwa Kadinali Jorge Mario Bergoglio kuwa mkuu wa Kanisa Katoliki duniani.
Kabla ya kuongoza misa Kadinali Jorge Mario Bergoglio 76, alisimikwa uongozi huo na kupewa cheo cha Upapa kwa jina alilo chagua la Fransisko na kuwa ni Papa wa kwanza kutoka katika bara la Amerika.
Papa Fransisko akiongea baada ya kusimikwa na kuongoza misa alisema " nawaomba  wale wote wenye madaraka   wawajibike vyema katika nyazifa zao za kiuchumi, siasa na kijamii ili tuweze kulinda na kujenga jamii bora na mazingira yake."
Papa Fransisko, amechuku jina la Fransisko wa Assis ambaye alikuwa mtoto wa tajiri, lakini aliamua kwenda kuishi  na watu masikini wakati wa karne ya 13, na hivyo Papa Fransisko kusisitiza ya kuwa kanisa ni kanisa la watu masikini.
Papa Fransisko ni mzaliwa wa Argentina.

Wazimbabwe wakubaliana katika kura ya muda wa urais.

Harare, Zimababwe - 19/03/2013. Wananchi wa Zimbabwe wamepitisha kwa wingi wa kura kuunga mkono sheria itakayo tumikika kumruhusu rais kuongoza nchi kwa mihula miwili ikiwa atachaguliwa baada ya kumaliza awamu ya kwanza.
95% ya watu walio piga kura walikubaliaana na sheria hiyo ambayo itaanza kutumika baada ya uchaguzi mkuu wa urais utakao tarajiwa kufanyika  mwaka huu mwezi wa Julai.

 Siraha za sumu zatumika katika vita nchini Syria. 

Damascus, Syria - 19/03/2012. Serikali ya Syria  imelaumu vikundi vinavyo pigana na serikali kwa kutumia siraha zenye sumu.
Msemaji wa serikali ya rais Bashar al Assad  alisema' wapiganaji wanaopigana naserikali wametumia siriha zenye sumu katika mji wa Aleppo."
Hata hivyo msemaji wa kundi linalo pigana na serikali alikanusha madai hayo kwa kusema " huu ni uzishi mtupu, na tunaamini jeshi la serikali limetumia mabomu aina ya scud ambayo huenda ya na sumu."
Kufuatia habari hizi serikali ya Urusi imeonya na kulaani na kusema  linabidi lichunguzwe ukweli wake kwani " ikiwa  siraha za sumu zimeanguka mikononi mwa wapiganaji basi hali inaweza kuwa mbaya zaidi."
Habari hizi za matumizi ya siraha za sumu zimekuja baada ya wapinzani wa serikali ya Syria kufanya uchaguzi na kumchagua Ghasssa Hitto, kuwa waziri mkuu wa serikali inayo pingana na rais Bashar al Assad katika uchaguzi uliyofanyika nchini Uturuki jijini Instambul.
Ghasssan Hitto ambaye alikuwa akiishi nchi Marekani amesema  " hakuna  majadiriano na serikali ya Bashar al Assad."
Syria ina limbikizo la siraha za sumu na za kinyuklia ambazo kama zikitumika katika vita hivi vya wenye kwa wenye huenda eneo zima la bara Arabu likawa katika hali mabaya. 

 Irak bado mabomu yalipuka na ni miaka 10 tangu kuangushwa kwa Saddam Hussein

Baghdad, Iraq - 19/03/2013. Watu zaidi ya 48 wamepoteza maisha yao na zaidi ya watu 120 kujeruhiwa vibaya, baada ya mfululizo wa mabomu kulipuka wakati Wairak wanatimiza miaka 10 tangu kuangushwa kwa Saddam Hussein.
Mashambulizi hayo ya mabomu ambayo yalitokea katika masoko, holetini nakwenye kituo cha basi katikati ya jiji la Badhdad kwenye eneo linalo kaliwa na  watu jamii ya Kishia.
Uvamizi nchini Irak uliongozwa na Marekani mwaka 2003/19, kwa madai ya kuwa Saddam Hussein alikuwa amelimbikiza siraha hatari za sumu ya kinyuklia.
Tony Blair ambaye alikuwa waziri mkuu wa Uingereza na aliye unga mkono na kushirikiana na serikali ya Marekani katika uvamizi nchini Irak amesema " hajutii uamuzi wake wa kushiriki katika kung'oa  Saddam Hussein madarakani kwani hata kama vuguvugu hili la mapinduzi inalo endelea katika bara la Waaraabu lingefenikiwa kumuondoa madarakani Saddam Hussein, basi ingekuwa ni tukio ambao linge jawa na majuto makubwa kwa jumuiya ya kimataifa kwa kuzingatia ni nini kinacho endelea nchini Syria,  ambapo rais Bashar al Assad anavyo wafanyia wananchi wake."
Vita vya kuivamika Irak vilipoteze maisha ya Wairak zaidi ya 100,000 na wengi kujeruhiwa na mali nyingi za Wairak kuharibika.

Monday, March 18, 2013

Papa Fransis aombwa kutatua mgogoro wa Kisiwa cha Falkland.

Bosco Ntaganda ajisalimisha mikononi mwa ofisi za Kibalozi nchini Rwanda.

Kigali, Rwanda - 08/03/2013. Kiongozi wa kundi la waasi wanaopigana na serikali ya Kongo Kinshasa amejisalimisha katika ofisi za ubalozi za Marekani zilizopo nchini Rwanda.
Bosco Ntaganda ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataifa tangu mwaka 2006,  ili kujibu kesi zidi yake, alijipeleka mwenyenyewe kwenye ofisi za ubalozi wa Marekani na kutaka apelekwe kwenya mahakama ya kimataifa.
Hapo awali habari kutoka serikali ya Kongo Kinshasa zilisema ya kuwa Bosco Ntaganda amekimbilia Rwanda baada ya kundi lake kuzidiwa nguvu na kundi la M23 ambalo pia linapingana na serikali ya Kinshasa.
Viktoria Nuland ambaye ni msemaji wa ubalozi wa Marekani nchi Rwanda alisema " Bosco Ntaganda amewasili katika ofisi zetu leo hasubuhi na ameomba apelekwe mahakama ya kimataifa ya iliyopo nchini Uhollanzi,
" Na sasa serikali ya Rwanda na Marekani kwa kushirikana na mahakama ya kimataifa iliyopo nchini Uhollanzi zipo katika mazingumzo  ili kukuamilisha maombi ya Bosco Ntaganda."
Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Louise Mushikiwabo kwa kuthibitisha kuwepo kwa Bosco Ntaganda   kwenye ubalozi wa Marekani alisema "serikal ya Rwanda bado inalishughulikia swala hilo na ni kweli Bosco Ntaganda yupo katika ubalozi wa Marekani,"
Bosco Ntaganda mwenye asili ya Kitutsi  na aliyejulikana kwa jina la "Teminata - Terminator "alijiunga na jeshi mwaka 1990 akiwa na miaka 17, na kujisalimisha huko kwakwe kunaleta maswali mengi hadi sasa.

Mahakama yaombwa kufuta kesi zidi ya Uhuru Kenyatta.
Hague, Uholanzi - 18/03/2013. Mwanasheria anayesimamia kesi inayo mkabili rais mchaguliwa wa nchi Kenya ameitaka mahakama ya kutetea haki za binadamu iliyopo nchi Uholanzi kufuta kezi zidi ya mteja wake.
Mwanasheria Stephen Kay, ameimbia mahakama ya kuwa "ikiwa shahidi huyo wanne na  ambaye alitoa maelezo tata kuhusu mteja wake Uhuru Kenyatta basi kesi hiyo ifutwe kwani ushahidi huo ni dhaifu."
" Na hata hivyo tunekosa uaminifu na ushahidi uliyopo, kwani ushahidi uliyo kuwepo zidi ya Muthaura hauna tofauti na Uhuru Kenyatta."  
Uhuru Kenyatta amechaguliwa kuwa rais wa Kenya hivi karibuni kufuatia uchaguzi mkuu uliyofanyika nchini humo japo ana kesi inayo mkabili katika makahama ya kimataifa ya makosa ya jinai iliyopo nchini Uholanzi.

 Papa Fransis aombwa kutatua mgogoro wa Kisiwa cha Falkland.

 Rome, Itali - 18/03/2013. Rais wa Argentina amemumba kiongozi mteule wa Kanisa katoliki duniani kusaidia kutafuata suruhisho la mgogoro wa Kisiwa cha Falkland ambacho kinagombaniwa Uingereza na Argentina.
Rais Cristina Fernandez Kirchner alisema " nimeongea na Papa Fransis asaidie kutatua mgogoro wa kisiwa cha Falkland.
"Kwani hali inavyo kwenda tunaweza kujikuta nguvu za kijeshi zikatumika tena," alioongezea rais Kirchner.
Mazungumzo kati ya Papa Fransis na rais Cristina Fernandez Kirchner yalichukua dakika 20 kabla ya kufanyika sherehe rasmi  ya kumsimika wadhifa kamali wa Upapa Jorge Mario Bergoglio 76 na kuwa Papa Fransis ambayo viongozi na marais watahudhuria hapo  kesho.
Papa Fransis ni mzaliwa wa Argentina, na kabla ya kuteuliwa kuwa Papa alikuwa  Kardinali wa jiji la  Bueno Aires
  
India na Itali zavutana kidiplomasia.

 India, New Delhi, - 18/03/2013. Jaji mkuu nchini India amekataa takwa ya kuwa balozi wa Itali nchini India ana sheria inayo mlinda kutokana madaraka aliyo nayo.

Jaji Altamas Kabir alisema " mahakama imekosa imani na serikali ya Itali kwa kitendo walichofanya cha kushindwa kutimiza agizo ambalo serikali mbili zilikubaliana."
Jibu hilo la mahakama limekuja baada ya balozo wa Itali nchini India, Daniel Mancini kukataliwa kuondoka nchini India kwa madai ubalozi wa Itali nchini India uliweka dhamana ya kuwa washutumiwa hao wa wawili wangerudi nchini India ili kujibu mashitaka yanayao wakabiri ya mauaji ya raia wa Waindia walioku wavuzi wa  samaki.
Balozi Mancini alichukua dhamana ya kuachiwa kwa raia hao wa Itali na kuhaidi watarudi ili kijibu mashita yao, lakini wakati ukipo fika wa raia hao wa Itali kurudi nchini India hawakufanya hivyo, jambo ambalo serikali ya India imesema ni kunyume na makubaliano na sheria zilizopo.

Viongozi wa Jumuiya ya Ulaya kuachia madaraka 2014

Brussels, Ubelgiji - 18/03/2013. Viongozi wakuu wawili wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya wametangaza kuchia madaraka yao ifikapo mwaka 2014.
Wakiongea kwa nyakati tofauti, Herman Van Rompuy 65, ambaye alisha wahi kuwa waziri mkuu wa Ubelgiji and Catherine Ashton 56, ambaye ni mwanachama wa chama cha Labour cha Uingereza walisema ya kuwa umefikia wakati wa kuwapa watu wengine nafasi kuongoza.
Viongozi hao ambao walichaguliwa kushika nyazifa hizo mwaka 2009, wamekuwa wakishirikiana katika harakati nyingi za kudumisha jumuiya ya Ulaya  ili kuhakikisha umoja huu unakuwa imara zaidi.

Thursday, March 14, 2013

Botswana yaiomba msamaha Kenya.

Botswana yaiomba msamaha Kenya.


Gaberone, Botswana - 14/03/2013. Waziri wa mambo ya nje wa Botswana ameomba msamahaa kwa rais aliyechaguliwa hivi karibuni nchini Kenya.
Pandu Skelemani aliomba msaahaa huo baada ya kusema " serikali ya Bostwana itamzuia kuingia nchi rais mtarajiwa wa Kenya Uhuru Kenya ikiwa hatashirikiana na mahakama ya kimataifa ICC Hague, iliyopo nchini Uhollanzi. "
Hapo awali  serikali ya Kenya ili ilaumu Botswana kwa kuingilia mambo ya serikali nyingine."
Waziri Skelemani alisema " naomba msamaha kwa watu wa Kenya kutokana na kauli yangu ya hapo awali na serikali zetu zitakuwa kwa ukaribu bila wasiwasi."
Botswana imesha wahi pia kutoa onyo kwa rais wa Sudan Omar al Bashir ya kuwa ikiwa ataingia nchini humo atakamatwa.

China wapata rais mpya.

Beijing, China - 14/03/2013. Bunge nchini China limememchagua Xi Jinping kuwa rais wa nchi hiyo.
Xi Jinping 59, ambaye hapo awali alikuwa amesha apishwa kuwa mkuu wa majeshi atakuwa na kofia mbili za kuongoza nchi.
Uchaguzi huo ambao ulifanywa na wabunge 3000, na kura tatu hazikupigwa.  
Rais huyo mpya wa China anatarajiwa kufanya ziara yake ya kwanza nchini Afrika ya Kusini ifikapo mwisho wa mwezi Machi.

 Rais wa Ufaransa ataka vikwazo viondolewe kwa wapinzani wa serikali ya Syria

Paris, Ufaransa - 14/03/2013. Rais wa Ufaransa, amezitaka nchi wanachamwa jumuiya ya Ulaya kutoa vikwazo vya siraha kwa wapiganaji wanao pingana na serikali ya Syria.
Rais Francois Hollande aliyasema haya saa chache baada ya waziri wa mambo ya nje Laurent Fabius kusisitiza hipo haja ya jumuiya ya Ulaya kuondoa vikwazo kwa wapiganaji wanao pingana na serikal ya rais Bashar al Assad.
Waziri Laurent Fabius alisema " njia iliyo bakia ni kuwapa siraha wapiganaji hao, ambapo kutasaidia kufikia suruhisho la kisisa, kwani serikali ya Syria imekuwa ikipewa siraha na Iran na Urusi" 
"Na Ufaransa na Uingereza zipo tiyari kuondoa vikwazo hivyo bili kupata ruhusa kutoka kwa nchi wanachama wa Ulaya."Aliongezea waziri Fabius.
Hata hiyo kauli hizo za viongozi hao wa Ufaransa zitakuwa na wakati mgumu kupenya kwenye vichwa vya nchi wanachama wa Ulaya, kwa kuzingatia Ujerumani imekuwa ikisita kuunga mkono uamuzi huo.

 Benjamin Netanyahu aunda serikali ya muungano.

Jerusalem, Izrael - 14/03/2013. Waziri mkuu wa Izrael amefikia makubaliano na chama cha upinzani ili kuunda serikali.
BenjaminTetanyahu chini ya chama chake cha Likud-Yisrael Beitenu amefikia makubaliano na chama cha Yeshi Atid na Hatnua na chama kingine cha Kiyahudi.
Kuundwa kwa serikali ya Izrael kumekuja baada ya wiki tano kupita kufuatia uchaguzi mkuu uliyonfayika mwezi January 22, ambapo chama cha waziri mkuu Netanyahu hakikuweza kupata kura za kumwezesha kuunda serikali bili chama wapinzani.
Serikali ya Izrael imeundwa wakati rais wa Marekani Baraka Obama anatarajiwa kufanya ziara nchi Izrael.

Wednesday, March 13, 2013

Habemus Papam kwa waumini wa Kanisa Wakatoliki.

Habemus Papam  tamko rasmi la Makadinari. 
 
  
Kengere na moshi mweupe watokea na kuashiria ya kuwa waumini wa Kanisa Katoliki wapata Papa mpya.

Vatican City, Vatican - 13/03/2013. Kadinari Jorge Mariao Bergoglio 76 mzaliwa wa Argentina ameteuliwa kuwa mkuu wa kanisa Katoliki duniani.
Jorge Mario Bergoglio atajulikana kwa jina la Papa Fransis na kuwa mkuu wa kanisa Katoliki wa 266 na amekuwa ni Papa wa kwanza kutoka nje ya bara la Ulaya  tangu miaka 1000 kupita.
Papa Fransis akiongea kuwashukuru  waumini na wale wote walio husika katika kufanikiasha kuteuliwa kwake alisema "Nawashukuru sana kwa  Makadinari wezangu kwa kunichagua kutoka mbali na kunileta hapa na ninge waomba muniombe."

Makadinari walichukua siku mbili katika maombi na kufanikiwa kumchagua Papa Fransis.

Tuesday, March 12, 2013

Makama ya kimataifa yamwachia mmoja wa watuhumiwa kutoka Kenya.
 
The Hague, Uhollanzi - 12/03/2013. Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai imefuta kesi ya mmoja ya washukiwa wa vurugu na mauaji yaliyo tokea nchini kenya kati ya mwaka 2007-8. baada ya uchaguzi mkuu na watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha.
Francis Muthaura ambaye ni mmoja wa washitakiwa alifutiwa kesi, baada ya kushindwa kupatikana ushahidi wa kutosha.
Mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo Fatou Bensouda alisema " hadi sasa hakuna ushaidi kamili unaweza kutumika ,kwani mashahidi hawajajitokeza japo jitihada zimetumika ili kupata ushahidi, na wengine waneshindwa kutoa ushahidi kwa kuofia maisha yao."
Baada ya kufutwa kwa kwesi hiyo ya Muthaura, mwanasheria anaye mwakilisha Uhuru Kenyatta  amesema "anabidi pia kesi zidi ya Uhuru ifutwe pia."
Kufutwa kwa kesi hiyo, kumekuja siku mbili baada ya Uhuru Kenyatta kushinda kiti cha urais wa Kenya kufuatia kura zilizo pigwa hivi  karibuni nchini humo.
 
Hali ya kidpomasia kati ya Venezuela na Marekani yaingia sura mpya.
 
 
Washington, Marakani - 12/03/2013. Serikali ya Marekani imewafukuza wafanyakazi wa kibalozi wa Venezuela ambao walikuwa wakifanya kazi nchini humo.
Uamuzi huo wa kuwafukuza wafanyakazi hao umekuja baada ya serikali ya Venezuela  kuwafukuza  waambata wa kijeshi wa Marekani waliokuwa wakifanya kazi nchini Venezuela.
Venezuela na Marekani zimekuwa na mahusiano yanayo yumba, tangu enzi za uhai wa rais Hugo Chavez ambaye aliishitumi Marekani kwa kudai ilitumia mamluki kutaka kuipindua serikali yake.
Ofisi za ubalozi za Marekani zilizopo nchini Venezuela zimekuwa wazi baada ya hayati rais Hugo Chavez kumkataa balozi aliye pendekezwa na serikali ya Marekani.
 
Malkia wa Uingereza akosa kuhudhuria siku ya Commonwealth.
 
London, Uingereza - 12/03/2013. Malkia wa Uingereza amehairisha kuhudhuria sherehe za nchi wanachama wa Commonwealth.
Malkia Elizabeth II 86, ambaye alikuwa amelazwa hivi karibuni  kutokana na kusumbuliwa na tumbo na kufanyiwa matibabu baadaye kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa mapumziko.
Kwa mujibu wa habari kutoka Buckingham Palace makazi aishio Malkia zinasema  " Malkia Elizabeth II anaendelea vizuri."
Japokuwa Malkia hakuhudhulia sherehe hiyo, aliweza kusaini kitabu ambacho kinahusisha mamlaka na mahusiano ya nchi wanachama wa Commonwealth.
Ni miaka 20 imepita tangu Malkia Elizabeth II kushindwa kuhudhulia sikuku ya nchi wanachana wa Commonwealth,
Nchi wanachama wa umoja huo ni nchi zilizo kuwa makoloni ya Mwingereza kabla ya nchi hizo kupata uhuru.
 
Nelson Mandela atoka hospital.
 
Johannesburg, Afrika ya Kusini -12/03/2013. Rais wa zamni wa Afrika ya Kusini ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kumalizika kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.
Nelson Mandela 94,  alikuwa amelazwa siku ya Jumamosi, ili kuangalia kiundani mwenendo wake wa kiafya   na  aliruhusiwa  na kurudi nyumbani.
Mwezi Desemba, Nelson Mandela, alilazwa hospital kwa wiki tatu, baada ya kuwa na matatizo katika mapafu na kufanyiwa upasuaji mdogo.
Msemaji kutoka ofisi ya rais Jakob Zuma alisema "kulazwa huko kwa Mandela, ni moja ya hatua ya kutizama afya yake, kutokana na umri aliyo nao."
Nelson Mandela mmoja wa viongozi wa Afrika ya Kusini waliopigana katika kuutokomeza ubaguzi wa rangi na kufanikisha kuleta haki sawa kwa wazalendo wa Afrika ya Kusini.





Sunday, March 10, 2013

Wavenezuela kupiga kura upya kumchagua atakaye ziba pengo la Hugo Chavez.

Walinzi wa UN waliotekwa nchini Syria waachiwa huru.


Aman, Jordan - 10/03/2013. Walinzi wa kutunza amani wa umoja wa mataifa ambao walikuwa wametekwa nyara  katika eneo la Golan Height na wapiganaji wanao pinga serikali ya Syria wameachiwa huru.
Walinzi hao 21, ambao ni raia wa Phillipines waliwasili nchini Jordan jana Jumamosi jioni baada ya jitihada za serikali ya Phillipines kwa kushirikiana na umoja wa mataifa kuwalazimisha wapiganaji hao kuwaachia huru walinzi hao.
Akithibitisha kuachiwa huko, mwakilishi wa umoja wa mataifa aliyepo Damascus Mokhtar Lamini alisema " walinzi wa umoja wamataifa kutoka Philipines  ambao walikuwa wametekwa nyara wameachiwa huru na wamesha wasili nchini Jordan."
Hapo mwanzo wapiganaji hao walisema" hatuta waachia walinzi hawa wa umoja wa mataifa mpaka hapo jeshi la serikali litakapo acha mashambulizi katika maeneo yetu."
Hata hivyo madai wapiganaji hao hayakutimizwa, na jeshi la serikali ya Syria, chini ya uongozi wa rais Bashar al Assas bado lina yanashambulia maeneo yote yanayo shikiliwa na wapiganaji hao.

Wavenezuela kupiga kura upya kumchagua atakaye ziba pengo la Hugo Chavez. 
Karakas, Venezuela, 10/03/2013.Masaa machache baada ya kuapishwa kwa Nikolas Maduro kuwa rais wa Venezuela, serikali ya nchi hiyo imetangaza rasmi siku ya kufanyaka uchaguzi mkuu wa urais.
Wavenezuela watapiga kura tarehe tarehe 14, Aprili/2013, tayari kumchagua rais mpya , ili kukamilisha katiba ya nchi hiyo inavyo sema "lazima uchaguzi ufanyike siku 30 baada ya kifao cha rais."
Viongozi watakaogombea kiti hicho cha urais ni  Nikolas Maduro ambaye alikuwa makamu wa rais wa Venezuela kabla ya kifo cha rais Hugo Chavez, na amehaidi kuendeleza mipango yote iliyo achwa na rais Chavez. Na  Henrique Capriles ataongoza kambi ya upinzani kwa kugombea tena kiti hicho cha urais kwa mara ya pili, baada ya kushindwa hayati rais Hugo Chavez kwenye uchaguzi uliyo fanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Polisi wa Afrika ya Kusini walio husika kumburuza kwa gari raia wa Msumbuji kushitakiwa.

Johannesburg, Afrika ya Kusini - 10/03/2013.Watu wapatao 2000 wameudhuria mazishi ya dereva wa taxi Mido Macia 26,  raia wa Msumbiji ambaye alifia kituo cha polisi baada ya kukamatwa.
Kufuatia kifo hicho, polisi tisa, wamefunguliwa mashitaka kutokana na  kifo Mido Macia ambaye walimburuta barabarani kwa kutumia gari la polisi wakati wakifanya doria.
Mido Macia raia wa Msumbiji alikutwa katika kituo cha polisi cha Devyton mnamo tarehe 27/02/2013 na  majeraha ya kichwani, na kuamika ya kuwa chanzo cha kifo cha Mido Macia kilitokana mateso ya kuburuzwa barabarani na polisi hao.
Kitendo cha polisi hao kumburuta Mido Macia barabarani, kilionyeshwa kwenye mitandao  na kuleta mshituko mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa na pia kulaaniwa vikali na rais  wanchi hiyo Jacob Zuma.

Saturday, March 9, 2013

Uhuru Kenyatta ashida uchaguzi wa rais Kenya.

Uhuru Kenyatta ashida uchaguzi wa rais Kenya.


Nairobi, Kenya - 08/03/2013. Makamu wa waziri mkuu wa Kenya amechaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo baada kupata kura nyingi zaidi ya mpinzani wake.
Uhuru Kenyatta ameshida uchaguzi huo kwa kupata kiasi cha kura za asilimia 50.07% kutoka kwa wapiga kura 6,173,433,  kati ya wapiga kura 12,330,028  waliojiandikisha  kupiga kura.
 Kamati iliyo simamia uchaguzi huo imesema "86% ya watu  ndiyo waliopiga kura  kutoka idadi ya wapiga kura wote walio jiandikisha na hakuna wizi uliotokea na tunaomba wagombea wote waheshimu matokeo ya uchaguzi."
Baada ya kutangazwa uchaguzi huo, kambi iliyo simamia uchaguzi na kuhakikisha ushindi wa Uhuru Kenyatta imetoa ujumbe kwa kusema "tunawashukuru Wakenya wenzetu kwa kukubaliana na mipango yetu na ujumbe wetu."
Hata hivyo kambi ya mgombea aliyeshindwa uchaguzi huo Raila Odinga imesema "hatukubaliani na matokeo hayo na tupo mbioni kufuata sheria ili kupinga matokeo hayo ya kura."
Uhuru Kenyatta atakuwa rais wa nne, tangu Kenya kupata uhuru mwaka 1963 na atafuata nyayo za marehemu baba yake Mzee Jomo Kenyatta ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Kenya.
Kenya imekuwa ikiangaliwa na jumuiya ya kimataifa ni kwa jinsi gani mpango mzima wa kupiga kura utakavyo kwisha, hii inatokana na vurugu zilizo tokea wakati na baada ya uchaguzi wa rais mwaka  2007-8, ambapo watu zaidi ya 1000 walipoteza maisha yao na mali nyingi kuharibiwa napia kusabaisha hasara kwa jamii nzima ya Kenya.

Rais Nikolas Maduro kufuata nyayo za hayati Hugo Chavez.


Karakas, Venezuela - 08/03/2013. Makamu wa rais wa Venezuela ameapishwa kuchukua kiti cha urais kilicho achwa wazi na hayati rais Hugo Chavez.
Nicolas Maduro aliapa kwa kusema " na apa kuwa mwaminifu na kufuata nyayo za komredi Hugo Chavez, kuhakikisha ya kuwa kazi aliyo ianza tunaitimiza kufuatia katiba na kwa kushirikiana na wananchi wa Venezuela, Mungu nisaidie."
Hata hivyo kiongozi wa chama cha upinzani nchini humu, Henrique Kaplies kupitia msemaji wake amesema " tunapinga kuapishwa kwa Nikolas Maduro kuwa rais kwani inakwenda kinyume na sheria."
Baada ya kuapishwa, rais Nikolas Maduro alisema " uchaguzi mkuu unahitajika ufanyike mapema iwezekanavyo ili kutimiza katiba inavyo sema."
Wavenezuela bado wapo kwenye maombelezi baada ya kifo cha rais wao Hugo Chavez kilichotokea hivi karibuni.

Vatican yatangaza siku rasmi ya kuanza ibaday ya kumchagua Papa.


Vatican City, Vatican - 08/07/2013. Baraza la kamati ya Makadinali limechagua siku rasmi ya kuanza ibada ya kumchagua mkuu mpya wa kanisa Katoliki duniani.
Habari zinasema uamuzi huo ulichukuliwa siku ya Ijumaa usiku baada ya kuwasili kwa Kadinali 115 ambaye alikuwa akisubiriwa.
Siku ya Jumanne wiki ijayo itakuwa siku rasmi ya kuanza ibada ya kumchagua Papa- mkuu wa kanisa Katoliki duniani lenye waumini wapatao 1.2 billioni,
Ibada hiyo ya kumchagua mkuu mpya wa kanisa Katoliki inafanywa, baada ya Papa Benedikt XVI kujiudhuru wadhifa wake huo mwisho wa mwezi Februari mwaka huu 2013.

Makao makuu ya soka yachomwa moto nchini Misri.


Kairo, Misri - 08/03/2013. Mamia wa watu wenye asira wamevamia makao makuu ya  ya shirikisho la soka la Misri kufuatia uamuzi wa mahakama kuwahukumu azabu ya kifo mashabiki 21 kutokana na vurugu zilizo tokea mwaka 2012.
Watu hao wenye hasira wengi wakiwa wapenzi na washabiki waliunguza jengo la ofisi hiyo ya shirikisho la soka ikiwa ni moja ya kupinga  adhabu iliyo tolewa na mahakama kwa mashabiki wa soka walio husika katika vurugu na kusabaisha vifo wakati timu za Al - Masry na Al-Ahly ya Kairo zilipo kutana kwenye mechi iliyofanyika kwenye mji wa Port Said.
Hata hivyo mahakama iliwaachia watu 25 ambao hawakukutwa na hatia.
Misri imekuwa ikikimbwa na maandamamo ya kila mara tangu kufanyika mapinduzi ambayo yalimn'goa madarakani rais Husni Mubaraka Februari 2011.

Friday, March 8, 2013

Mwili wa Hugo Chavez kuhifadhiwa kwa kumbukumbu.

Mwili wa Hugo Chavez kuhifadhiwa kwa kumbukumbu.

 Picha hapo juu inaonyesha tangu kuzaliwa kwa rais wa Venezuela Hugo Chavez hadi alipo fariki dunia na mambo ambayo alipitia na kufanya.
 
 Wengi walilia kwa uchungu kiasi cha kuchanganyikiwa , kuto kuamini na kuzimia  wakati wa mazishi ya kumwaaga rais Hugo Chavez.

Picha hapo juu ni za marais tofauti ambao wamekuwepo katika mazishi ya kumuaga hayati rais Hugo Chavez. 

 
 Picha hapo juu yaonyesha baadhi ya watu walikuja kumwaga marehemu rais Hugo Chavez, na wengine wakilia kwa uchungu.

Karakas, Venezuela - 08/03/2013.Maelfu wamekusanyika katika mazishi ya aliyekuwa rais wa Venezuela Hugo Chavez aliyefariki dunia hivi karibuni.
Viongozi kutoka mataifa mbalimbali 55 wameudhuria mazishi yao na huku wanachi wa Venezuela wakizidi kuja mahali ambapo mwili wa hayati  rais Hugo Chavez umelazwa.
Makamu wa rais  Nicolas Maduro alisema" serikali imeongeza siku saba zaidi za kuaga mwili wa Hugo Chavez, ili kumpa fursa kila mwananchi wa Venezela kuweza kuja kumuaga kwa mara ya mwisho rais wetu mwana mapinduzi na alipigania haki zetu sote."
"Vile vile mwili wa hayati rais Hugo Chavez utahifadhiwa katika eneo ambalo mapinduzi ya kijeshi ya kutaka kumtoa madarakani ya mwaka  2002  kushindwa na eneo hilo litaitwa kumbukumbu ya mapinduzi." alisema
Inakadiriwa zaidi ya watu million mbili huenda wakahudhulia kumuaga hayati rais Hugo Chavez.
Kuhifadhiwa mwili huo  kwa hayati Hugo Chavez kunafanana  wanamapinduzi wengine  kama,  Lenin wa Urusi, Ho Chi Mihn wa Vietnam na Mao Zedong wa China. 
Rais wa Urusi Vlamdir Putin katika kukumbuka huusiano kati ya Venezuela na Urusi alisema" Hugo Chavez alikuwa mtu shujaa na mtu ambaye alikuwa mwaminifu na mwangalifu katika kila jambo alifanyalo na kupanga kwa makini.
"Kiukweli alikuwa anataka kuendeleza kuinua maisha ya wananchi wake, amekuwa kinara katika ukumbozi  wa Latin Amerika, na wakati yupo hali alikuwa kama Simon Bolivar, Fidel Castro na Che Guevara." Aliongezea rais Putin.
Kufuatia kifo cha rais Hugo Chavez, makamu wa rais Nicolas Maduro, ataapishwa kuchukua kiti cha urais na ambapo anatarajiwa kuitisha uchaguzi mkuu wa urais katika kipindi cha siku 30 baada ya kifo cha rais kwa mujibu wa katiba ya Venezuela.

Kadinali aliyekuwa akisubiriwa awasili Vatican.
 
Vatican City, Vatican - 08/03/2013. Makadinali wote  wamewasili Vatican City, tayari kwa kuanza ibada ya kumchagua atakaye kuwa kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki duniani.
Kadinali Jean Baptiste Phan Minh Man kutoka Vietnam aliwasili akiwa wa mwisho jana na kukamilisha ya makadinali 115 ambao watahusika katika kumchagua Papa - mkuu wa waumini wa kanisa la Katoliki.
Kuwasili kwa Kadinali huyo kutoka Vietnam, kutawezesha kupangwa tarehe maalumu ya kuanza ibada ya uchaguzi huo.
Uchaguzi wa mkuu mpya wa kanisa la katoliki, umekuja baada ya Papa Benedikt XVI kujiudhuru wadhifa wake huo kutokana na sababu za kiafya.

Korea ya Kaskazini yasimamisha mkataba wa amani na jirani yake.

PyongYang , Korea ya Kaskazini - 08/03/2013. Korea ya Kaskazini imesimamisha makubaliano ya amani kati yake na Korea ya Kusini baada ya umoja wa mataifa kuongeza vikwazo kwa nchi hiyo.
Habari kutoka kwa shirika la habari la Korea ya Kaskazini zilisema " tunasimamisha mkataba wa amani na Korea ya Kusini na shambulizi lolote la kushambulia nchi yetu litajibiwa kwa vishindo."
Kutangazwa kwa habari hizi kulikuja baada ya kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un, kutembelea kambi ya jeshi ambayo ilifanya mashambulizi mwaka 2010, katika kisiwa cha  Yeonpyeong ambacho kinamilikiwa na Korea ya Kusini, na kuwataka kuwa tayari kwa vita.
Kufuatia kauli hiyo, Korea ya Kusini, imefanya mkutano wa dharula ili kujadili hali ya usalama wa nchi hiyo.
Korea ya Kaskazi imewekewa vikwazo zaidi na  umoja wa mataifa, baada ya kufanya jaribio la siraha ya nyukia hivi karibuni.

Walinzi wa UN bado mateka kwa wapinzani wa serikali ya Syira.

Golan Heights,Izrael - 08/03/2013. Wapiganaji wanaopingana na serikali ya Syria wamekataa kuwaachia walinzi wa amani wa umoja wa mataifa walio wateka nyara sikumbili zilizo pita.
Walinzi hao 21, waliopo chini ya umoja wa mataifa wa  kulinda amani katika eneo la Golani Height amabo wanatokea Philippine, walitekwa nyara na wapiganajihao katika eneo la Golan Height, eneo  ambalo walinzi hao wa umoja wa mataifa huwa wanalilinda baada ya eneo hilo kuwahi kuleta mzozo kati ya Izrael na Syria.
Wapiganaji hao waliamua kuwateka nyara Waphillipines hao, ikiwa ni  njia moja ya kutaka jeshi la serikali ya Syria kuacha kushambulia maeneo ambayo wapiganaji hao wanayashikilia karibu na Golan Height.
Tangu kuanza kwa vita vya wenye kwa wenye nchini Syria, mamia ya watu wameuwawa, wengine kuikimbia nchi na baadhi ya nchi kuwaondoa raia wake ambao walikuwa wanafaya kazi nchini humo.