Thursday, June 30, 2011

Pakistan yaikataza Marekani kutumia kiwanja chake cha ndege.

Pakistan yaikataza Marekani kutumia kiwanja chake cha ndege.
Baluchistan, Pakistan-30/06/2011.Serikali ya Pakistan imeisimamisha jeshi la marekani kutumia basi yake iliyopo nchini humo kutumiwa kama kiwanja cha kuanzisha mashambulizi kwa kutumia ndenge aina ya drone ambazo zinaendeshwa kwa mtandao.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya Pakistani na kuthibitishwa na ofisi za jeshi zilizopo nchini humo zinasema " serikali ya Pakistan imesimamisha ruksa kwa jeshi la Marekani kutumia kituo cha Shamsi kilichopo kusini mwa jimbo la Baluchistan na kama ndege italuka kutoka eneo hilo itakuwa ya Pakistani."
Serikali ya Pakistani imekuwa ina wakati mgumu baadaya ya jeshi la Marekani kufanikiwa kumwua aliye kiongozi wa kundi la Al Qaeda Osama bin Laden nchini humo.
Umoja wa Afrika waingiwa na shaka na siraha kutoka Ufaransa kwa wapinzani.
Adis Abeba, Ethiopia - 30/06/2011.Umoja wa nchi za Kiafrika umeitaka serikali ya Ufaransa kuto dondosha na kusambaza siraha holera kwani kunaweza sababisha madhara makubwa hasa katika maswala ya usalama katika eneo hilo.
Kamishna wa Umoja huo Jean Ping akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Afrika alisema "siraha zinazo sambazwa kwa kudondoshwa toka angani na Ufaransa zinaishia kwenye mikono ya makundi yenye ushirikiano na Al-qaeda kutokana na ushahidi tulionao, na jambo ambo ambalo linaenda kinyume na swala zima la kulinda usalama wa eneo hilo."
Naye msemaji wa jeshi la Ufaransa Konel Thiery Burkhard alisema " kuna siraha kama lifles, mashine gun na roket mbazo zimedondoshwa kwenye eneo la kundi linalo pingana na serikali ya Gaddafi na inaweza kuwa hatari."
Hata hivyo Kanal Mokhtar Milad Fernana wa kikosi kinacho pingana serikali ya Gaddafi alikanusha madai hayo kwankueama " yoyote anaye dai kuwa tumepokea siraham basi haje hapa atupe ushaidi wa kuwepo kwa sirha hizo."
Udondoshwaji wa siraha kwenye maeneo ya wapinzani wa serikali ya Gaddafi yamekuwa yakifanyika karibu na mpaka wa Tunisi km100 kusini mwa mji wa Tripol.

Tuesday, June 28, 2011

Waziri wa fedha wa Ufaransa kuongoza -IMF- shirika la fedha.

Waziri wa fedha wa Ufaransa kuongoza -IMF- shirika la fedha.
New York, Marekani-28/06/2011. Shirika la kimataifa la fedha duniani IMF-International Monetary Fund, limemchagua waziri wa fedha wa Ufaransa kuwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo ili kushika nafasi iliyo achwa na Dominique Strauss-Kahn ambaye amejiudhulu kutokana na kuwa na kesi ya kijinsia.
Christine Lagarde, amechaguliwa kushika nafasi hiyo na kuwa mwanamke wa kwanza kushika kiti cha oungozi wa shirika hilo.
Kuchaguliwa huko kwa waziri wa fedha wa Ufaransa kumefanikwa baada ya kuungwa mkono na Marekani.Rasi wa Ufaransa, Nicola Sarkozy alisema " nivizuri kwani shirika hilo limepata kiongozi mwanamke kwa mara ya kwanza na ambaye anauwezo wakimataifa."
Serikali ya Ugiriki yapambana na wanaopinga uamuzi.
Athensi, Uguriki- 28/06/2011. Maelfu ya Wagiriki wameaandamana kupinga uamuzi wa serikali kutaka kugeuza sheria za kiuchumi nchini humo.
Habari kutoka ndani ya serikali zinasema "serikali ya Ugiriki upo na wakati mgumu wa kupambana maandamano ya nayo endelea na kuamua ni kwa jinsi gani itaweza kutuliza hasira na upinzani ambao serikali hiyo inakumbana nazo kutoka na hatua ya serikali kutaka kubana matumizi na kugeuza baadhi ya sheria za kiuchumi."
Maandamano hayo ambayo yameongozwa na vyama vya wafanyakazi kulekea katikati ya jiji la Athensi kwenye eneo la Syntagma yalikumbana na nguvu za polisi na kuleta ghasi kubwa na kusababisha maafa makubwa ya kijamii na mazingira.

Monday, June 27, 2011

Mahakama ya Hague yataka Muammar Gaddafi akamatwe.

Mahakama ya Hague yataka Muammar Gaddafi akamatwe.
Hague, Uhollanzi - 27/07/2011. Mahakama ya makosa ya jinai na kutetea haki za binadamu nchini Uhollanzi imetoa kibali maalumu cha kutaka kiongozi wa Libya, mtoto wake wa kiume na afisa mkuu wa usalama wa taifa wakamatwe.
Jaji wa Sanj Mmmasenono Monageng, alitangaza ruhusa hiyo kwa kusema " kutokana na ushahidi uliyo tolewa na mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo ya kimataifa Louis Moreno-Ocampo zimeonyesha ushahidi wakutosha yakuwa kiongozi huyo wa Libya Muammar Gaddafi, mtoto wake Seif al Islam na afisa mkuu wa usalama wa taifa Abdullah Senussi wamahusika katika kukiuka haki za binadamu na hivvyo lazima wakamatwe."
Hata hivyo serikali ya Libya imesema haifanya makos hayo yanayodaiwa na makosa hayo ni ya jeshi la NATO.

Thursday, June 23, 2011

Marekani na Washiriki wa NATO kuondoa wanajeshi nchini Afghanistan.

Marekani na Washiriki wa NATO kuondoa wanajeshi nchini Afghanistan.
Washington, Marekani-23/07/2011. Rais Baraka Obama wa Amerika ametangaza kuwa serikali ya Amerika wanajeshi wapatao 33,000 watarudi nyumbani kutoka Afghanistan ifikapo msimu wa kiangazi wa mwaka 2012.
Kufuatia kutangazwa huko kwa serikali ya Amerika kupunguza wanajeshi nchini Afghanistan, nchi washiriki wa NATO nazo zimeanza kutangaza mpango wa kutaka kuondoa wanajeshi zikiongozwa na Uingereza.
Kufuatia uamuzi wa nchi za NATO kuanza kuondoa majeshi yake nchini Afghanistan, rais wa nchi hiyo Hamid Karzai ameunga mkono uamuzi huo kwa kusema kuanza kuondoka kwa wanajeshi wa NATO ni mwanzo wa Waafghanistani kuanza kuchukua madaraka ya ulinzi na kuwa mikononi mwao."
Hata hivyo habari kutoka ndani ya bunge la Amerika zinasema, rais Obama,ametoa kwa wingi jeshi hilo nchini Afghanistan na hawafahamu yambele yatakayo tokea.
Rais Hugo Chavez afanyiwa matibabu nchini Kuba.
Havana, Kuba 23/06/2011. Rais wa Venezuela anaendela kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji kwa ajili ya matibabu.
Rais Hugo Chavez 56 alikwenda nchini Kuba baada ya kusumbuliwa na pelvic abscess Juni 10.
Habari kutoka ofisi ya rais zinasema " rais Hugo Chavez anatarajiwa kurudi kazini muda si mrefu na makamu rais Elias Jaua anaongoza ofisi kwa sasa."
Kwanda huko kwa ajili ya matibabu kwa rais wa Venezuela kumekuja kutoka na uhusiano wa karibu wa nchi hizo mbili, japo inaaminika ya kuwa Kuba hali ya kufanyia kazi ya matibabu ni duni.
Kesi zidi ya mwanasiasa na kiongozi maarufu nchi Uhollanzi yafutwa.
Amsterdam,
Uhollanzi 23/06/2011. Mahakama ya jiji la Amsterdam imefutilia mbali kesi zidi ya mwanasiasa na kiongozi wa chama cha uhuru, ambayo ilikuwa imefunguliwa zidi yake kwa kukashifu,kuchochea utenganifu na hasira katika jamii.
Geert Wilders, ambaye alishiriki katika picha iliyo itwa "Fitna" ambayo ilitolewa mwaka 2008, na kuleta mvutano mkubwa kwa kusema " dini kislaama haina nafasi katika mila za Ulaya," jambo ambalo lilisababisha waumini wa dini ya Kislaam kukasirika.
Akiongea katika hukumu hiyo hakimu alisema" maneno aliyo yaongea Geert Wilders kuhusu dini ya Kislaam siyo makosa kufuatia sheria za nchi na hakuleta madhara katika jamii."
Akiongea nje ya mahakama Wilders alisema "nipo hapa kwa sababu ya yale niliyo yasema, nitaendelea kusema na sitakaa kimya.
Kesi zidi ya mwanasiasa huyo iliaanza mwaka 2010.

Wednesday, June 22, 2011

ilvio Berlusconi ashinda kwa mara nyingine kura za maoni.

Ban Ki-moon achaguliwa tena kwa muhula wapili.
New York, Marekani - 22/06/2011. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amechaguliwa te na kwa mara nyingine kuwa katibu mkuu na wajumbe wa umoja wa mataifa.
Ban Ki-moon, ambaye alitangaza rasmi wiki mbili zilizo pita kutaka kuendelea kuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa baada ya ya muhula wake kuisha mwaka huu,
Katibu alipata kura 192 za wajumbe wa umoja wa mataifa ambazo zilimwezesha kuchaguliwa tena kuwa katibu mkuu kwa muhula wa pili utakao anza mwaka 2012 .
Ban Ki-moon 67 alikuwa mgombea pekee katika kiti hicho cha ukatibu mkuu wa umoja wa mataifa.
Silvio Berlusconi ashinda kwa mara nyingine kura za maoni.
Rome, Itali 22/06/2011. Waziri mkuu wa Itali ameshinda kura ya imani na serikali yaye ambayo ilipigwa ili kuthibitisha kama bado anaaminika kuongoza kutokana na misukosuko inayo mkabili yeye binafsi.
Silvio Berlusconi ambaye alishinda kwa kupata kura za maoni 317 kwa 293.
Hata hivyo waziri mkuu Berlusconi anakabiliwa na wakati mgumu, kibinafsi kusafisha jina lake katika milango na maswala ya kisiasi kutokana na kashfa zinazo muandama.

Sunday, June 19, 2011

Mvutano wa siasa nchini Somalia, waziri mkuu ajitoa madaarani.

Mvutano wa siasa nchini Somalia, waziri mkuu ajitoa madaarani.
Mogadishu, Somalia-19/06/2011. Waziri mkuu wa Somalia ametangaza kujiudhulu baada ya kukubaliana na rais na spika wa bunge.
Waziri Mohamed Abdulahi Mohamed alisema " kufuatia mtazamo wangu kuhusu hali halisi ya nchi yetu na makubaliano yaliyowekwa Kampala Uganda na napenda kumshuruku rais na wanchi wenzangu kwa massada walionipa wakati wa uongozi wangu.
Mapema mwaka huu waziri mkuu wa huyo ambaye ailtakiwa kujihudhulu lakini alikataa kwa kutaka kuwepo na kura ya imani zidi yake.
Somalia nchi iliyopo kwenye pembe ya Afrika Mashariki imekuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu kuanguka kwa rais Mohamed Siad Barre mwaka 1991 na imekuwa ikizaniwa ya kuwa ni moja ya makazi ya kundi la Al Qaeda.
Mameya wa miji nchini Marekani wataka vita kusimamishwa.
Balttimore, Marekani - 19/06/2011. Mameya wa miji ya nchini Marekani wamekutana katika mji wa Baltimore na kulitaka bunge la nchi yao kupitisha mswada wa serikali kusimamisha vita nchini Afghanistan na Irak ambavyo vinaitia hasara taifa kifedha na kijamii.
Wakiongea katika hotuba ya pamoja ambayo ilisomwa na Elena Temple alisema " Mkutano mkuu wa Mameya wa Marekani unaliomba bunge la nchi kusimamisha vita na kuelekezea fedha zinazo tumika katika vita hivyo kwenya sekta za kijamii ili kuinua uchumi wa nchi."
Vita vinavyo endelea hadi sasa vimekuwa vikitumia zaidi ya mamillion kwa mwaka na kuleta maafa makubwa katika jamii.

Saturday, June 18, 2011

Rais wa pili wa Zambia Fredrick Chiluba afariki dunia.

Rais wa pili wa Zambia Fredrick Chiluba afariki dunia.
Lusaka, Zambia 18/06/2011. Aliye kuwa rais wa pili tangu Zambia kupata uhuru na kuchaguliwa kupitia kura zilizo shirikisha vyama vingi nchini humo amefariki dunia.
Fredrick Jacob Titus Chiluba 68, ambaye ametawala Zambia kwa muda wa miaka kumi na kubadilisha muundo mzima wa serikali uliyo kuwa umewekwa na rais wa kwanza wa Zambia Keneth Kaunda.
Akitangaza kufariki kwa Fredrick Chiluba, rais wa sasa wa Zambia Rupiah Banda alisema " aliyekuwa rais wetu Fredrick Chiluba amefariki dunia mapema leo 18/06/2011, na kwaniaba ya serikali napenda kutoa salamu za rambirambi kwa familia, ndugu marafiki na jamaa wote."
Hayati Fredrick Chiluba alisifiwa sana kwa kuleta mageuzi ya kisiasa hasa na nchi za Ulaya Magharibi.
Ujerumani na Ufaransa wakubaliana kuisaidia Ugiriki.
Berlin, Ujerumani - 18/06/2011. Viongozi wa serkali ya Ujerumani na Ufaransa wamekubaliana kwa pamoja kuisaidia Ugiriki kifedha ili kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Kansela wa Ujerumani Angel Merkel na rais wa Ufaransa Nicalas Sarkozy walikubaliana bila kipingamizi kuipa Ugiriki kwa kusema " wakati huu ni wakati wakuonyesha ushirikiano wetu."
Kufuatia myumbo wa kiuchumi waziri mkuu wa Ugiriki, alibadilisha baraza la mawaziri ili kuleta msimamo mmoja ndani ya serikali.
Ugiriki ambayo ianayumba kiuchumi,inatakiwa kupewa mkopo wa kiasi cha 12 billioni ili kuinua uchumi wa nchi hiyo.
Marekani na Taliban wakutana kujadili usalama wa Afghanistan
Kabul, Afghanistan - 18/06/2011. Rais wa Afghanistan ametangaza ya kuwa serikali ya Marekani inafanya mazungumzo na kundo la Taliban.
Rais Hamid Karzai alisema " wakuu wa siasa na wakijeshi kutoka serikali ya Marekani wamekuwa wakiongea na viongozi wa kundi la Taliban ."
Hivi karibuni waziri wa ulinzi, Robert Gates alisema " huenda kukawa na amzungumzo na Taliban, ili kuleta suruhisho kupitia siasa."
Mazungumzo hayo na kundi la Taliban yamekuja huku serikali ya Marekani ikiwa inajiandaa kuondoa majeshi yake taratibu, tayari kukabidhi madaraka kwa serikali ya Afghanistan ifikapo mwaka 2014.

Friday, June 17, 2011

Viongozi wa Argentina na Uingereza watupiana maneno juu ya Falkland.

Viongozi wa Argentina na Uingereza watupiana maneno juu ya kisiwa cha Falkland.
Bueno Aires
, Argentina- 17/06/2011. Rais wa Argentina amemshambulia kwa maneno waziri mkuu wa Uingereza kufuatia mvutano ulipo kuhusu kisiwa cha Falkland.
Rais wa Cristina Fernandez, alisema "maoni ya waziri mkuu wa Uingereza ni aibu, hayasemeki na hayaendani na ukwli ulipo kuhusu kisiwa cha Falkland.
Na nitazidi kusisitiza ukweli kuhusu kisiwa cha Falkland katika ngazi za kimataifa, ili tuweke wazi umilikaji wa kisiwa hiki."
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron akiongea ndani ya bunge, alisema wananchi wa kisiwa cha Falkland ndiyo watakao amuakama wanataka kuwa chini ya Uingereza au hapana"
Mvutano wa kisewa cha Falkland ambao ulisababisha vita vilivyo chukua wiki kumi kati ya Argentina na Uingereza mwaka1982 wakati wa utawala wa waziri mkuu Margret Hilda Thatcher na kisiwa hicho kuwa chini ya mwingereza.

Thursday, June 16, 2011

Nokia yashinda kesi zidi ya Appple.

Al-Qaida wamteua Ayman al Zawahri kuwa kiongozi mkuu.
Islamabad, Pakistan- 16/06/2011. Kundi la Al Qaida limemteua aliyekuwa makamu wa kundi hilo kuwa kioongozi mkuu wa kundi hili kufauatia kifo cha kiongozi wao hivi karibuni
Ayman al Zawahri ameteuliwa rasmi baada ya majadiliano yaliyo chukua wiki sita tangu kuuwawa kwa kiongozi wa Al-Qaida Osama bin Laden na jeshi la Amerika nchi Pakistan.
Akiongea baada ya uteuzi huku bunduki ikiwa pembeni yake, Ayman al Zawahri alisema " tutaendelea mapmbano yetu kama kawida na kuonya ya kuwa wale Amerika itakumbana na upinzani ambao hapo mwazo haukuwepo."
Ayman al Zawahri ambaye ni rai wa Misri alijiunga na Al-Qaida mwaka 1986 baada ya kukutana na aliye kuwa kiongozi wa kundi hilo hayati Osama bin Laden katika mji wa Peshawar nchini Pakistan.
Kiongozi wa aliyeshukiwa kuongoza mauaji ya Bali afungwa.
Jakarta, Indonesia - 16/06/2011. Mahakama kuu jijini Jakarta imemuhukumu aliyekuwa mkuu wa kundi la Jemaah Islamia kwa kosa lakuwafadhili wapiganaji wa kundi la Aceh wanaopingana na serikali ya Indonesia.
Abu Bakar Bashir, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 15 baada ya kukutwa ya kuwasaidia wapinzani wa serikali wa kundi la Aceh, ambao wao walitaka kumwua rais .
Wakati wa hukumu hiyo, polisi na wana usalama walikuwa makini ili kuzua machafuko ambayo yangeweza kutokea kwenye maeneo ya mahakama hiyo.
Abu Bakar Bashir, anashutumiwa pia kwa kuhusika katika milipuko ya bomu iliyo tokea Bali mwaka 2002 na kusababisha mauaji ya watu wasiopungua 200 wengiwao wakiwa watalii.
Nokia yashinda kesi zidi ya Appple.
Helsink, Finland - 16/06/2011. Shirika la utengenezaji wasimu za aina ya Nokia lenye makao yake makuu nchini Finland limeshinda kesi zidi shirika la Apple mpinzani wake mkuu katika kuuza na kutengeneza simu la Apple.
Ushindi huo umekuja baada ya kesi iliyo funguliwa na Nokia mwaka 2009,kwa madai Apple imekuwa ikitumia baadhi ya teknolojia zake.
Akiongea mara baada ya kupata ushindi wa kisheria, mkurugenzi mkuu wa Nokia Stephen Elop, alisema " tunafurahi kuona sas Apple wamejumuika katika kutumia teknologia za Nokia na hii ni mwanzo wa na sisi wote tunaweza kuundelea na biashara bila matatizo."
Hata hivyo malipo ambayo yanatakiwa yalipwe na Apple,hayakuweza kupatikana kutokana na makubaliano yaliyo wekwa kati ya mashirika hayo mawili.

Sunday, June 12, 2011

Huwa nasoma Kuraan na Biblia asema Tony Blair.

Afrika ya Kusini ya muaaga mama wa ukombozi zidi ya Ubaguzi wa rangi.
Soweto, Afrika ya Kusini-13/06/2011. Wananchi wa Afrika ya Kusini wamekumbwa na huzuni na msiba mkubwa baada ya kuondokewa na mwanaukombozi na mama wa Afrika ya kusini aliye pigana kidete kupinga ubaguzi wa rangi.
Albertina Sisulu, ambaye alikuwa mke wa hayati Walter Sisulu 92 alifariki dunia nyumbani kwake jijini Johannesburg.
Watu wapatao 40,000 walikuwepo kwenye misa ya kumuuga hayaati Albertina iliyo fanyika kwenye uwanja wa mpira wa SOWETO.
Rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, amesema "msiba wa kuondokewa Albertina ni wa kitaifa na takumbukwa kwa mchango wake wa kuung'oa ubaguzi wa rangi."
Nelson Mandela, ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Afrika ya kusini baada ya kuung'oa ubaguzi wa rangi alisema katika waraka wale uliyo somwa na mke wane Graca, " Albetina ulikuwa sehemu ya maisha yangu wewe na mumeo Walter na nitawakumbuka milele na ningependa kuwepo kukuaga kwa mara ya mwisho na najaribu kufikiria ya kuwa Albertina anakwenda kutana na wapigania uhuru wenzake Oliver Tambo. Walter na Heren Joseph nakushukuru kwa yote tuliyo fanikwa niee salaamu zangu kwa mashujaa wenzangu." Mabida
Albertina Sisulu amepumzishwa karibu na hayati mume wake Walter Sisulu.
Huwa na soma Kuraan na Biblia asemaTony Blair.
London, Uingereza -12/06/2011. Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza amekubali ya kuwa miaka ya 70 dunia nzima ilikuwa haina mawazo ya kutosha kupambana na hali halisi na tangu kutoka madarakani ameweza kujua hali halisi kwa kusoma vitabu hasa vya dini.
Tony Blair aliseme " hali imekuwa ngumu kimaisha na ipo nia ya kuhakikisha yakuwa matajiri kuwasidia watu wasiona uwezo. Kwani itakuwa siyo haki kwa mtu mmoja kuwa na utajiri mwingi na wengi wanishi katika haki mbaya."
Akiongeza Tony Blair "kuwa na imani ni muhimu saana kwani kunakuwezesha kujua ukweli wa mabo yanayotokea duniani na huwa nasoma bibilia na Kuraani ambavyo vinanisaidia kuelewa kiundani hali halisi."
Tony Blair ambaye ni kiongozi anayesimamia kupunguza mgogoro uliyoko kati ya Izrael na Palestina amekubali pia tangu atoke madarakani amelewa kiundani hali halisi kati ya Wapalestina na Waizrael.

Friday, June 10, 2011

Waziri wa ulinzi wa Amerika, alezea wasiwa wake juu ya NATO.

Taasisi yaonya kuhuku uuzwaji wa Ardhi barani Afrika.
Oakland,New-Zealad 10/06/2011. Taasisi ya uchunguzi wa iliyopo nchini New-Zealand, emetoa repoti na kusema shirika la fedha la lijulikanalo kama HEDGE FUND, limekuwa likinunua ardhi katika bara la Afrika kwa njia ambazo hazistahilina, na mpaka sasa imesha nunua ardhi yenye ukubwa mita miasita million katika ba
ra la Afrika.
Repoti ilyotolewa na Oakland Institute inasema Hedge fu
nd imekuwaikinunua ardhi kupitia kwa viongozi wala rushwa na hata wakati mwingine kuwarubuni machifu na viongozi wa vijiji kukubali kuuza ardhi kwa kutiliana mikataba inaruhusu kwa ardhi zao kutumika kulimia biofuel mazao mafutana na maua. Na nchi ambazo zimetajwa katika repori hiyo ni Ethiopia, Sudani ya Kusini, Mali,Sierra Leone na Tanzania.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo inasema iliwa hali hii itaendelea basi hali ya upatikanaji wa chakula utakuwa mgumu hasa katika nchi hizo na dunia kwa ujumla.
Waziri wa ulinzi wa Amerika, alezea wasiwa wake juu ya NATO.
Brussel, Ubeligiji -10/06/2011.Serikali ya Amerika imelezea wasiwasi mkubwa ambo huenda kuleta utata kati ya nchi wanachama wa NATO.
Akiongea wakati wa mkutano wa maswala ya kiulinzi ambao umeandaliwa ili kuangalia, na kutathmini hali ya kiulinzi kati ya nchi wanachama, waziri a mambo ya nje wa Marekani Robert Gate alisema "kutokuwepo na msukumo na nia katika kuchangia hasa katika maswala ya kivita kwa baadhi ya nchi wanachama kunaleta wasiwasi mkubwa hasa kwa kizazi kijacho cha nchi wanachama wa NATO."
Akiendelea kusisitiza " kutokuwepo na ukaribu wa ukachero na uchache wa vifaa vya kiulinzi lazima yafanyiwe mabadiko."
Waziri Robert Gate, ambaye anatarajiwa kujiudhulu kutoka madarakani hivi karibuni, ameyasemahayo wakati serikali ya Marekani ikiwa nafikilia njia mbadala ya matumizi ya kijeshi.

Friday, June 3, 2011

Ratko Mladik afikishwa mahakamani.

Hague,
Uhollanzi 03/06/2011.Mahakama ya kutetea haki za binaamu na makosa ya kivita imeanza kusikiliza kesi zidi aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Bosnia Serb, RatkoMladik, ambaye anashutumiwa kwa kuhusika na mauji yaliyo tokea mwaka 1992-95 mjini Sarajevo.
Jaji anayeongoza katika kusikiliza kesi hiyo , Alphons Orie, alimsomea makosa 11 ambayo Ratko Mladika yanamkabili mbele ya mahakama, na kutaka kujua kama anafahamu kese inayo mkabili, alijibu ya kuwa anataka muda zaidi ili kujibu swala swala hilo.
Akiongea mara baada ya kumaliza kumsomea mashitaka Jaji alphons Orie alisema "tarahe , 4-Julai, kesi itaendelea kusikilizwa na anatakiwa kutoa jibu la kukubali makosa au kukataa."
Ratko Mladik alikamatwa 26 Mai, baada kingia mafichoni kwa muda wa miaka isiyo pungua 16.

Wednesday, June 1, 2011

Kaptain Sepp Blatter kuongoza Shirikisho la Soka FIFA tena.

Zuriki, Uswizi - 01/06/2011. Wajumbe wa shirikisho la soka duniani FIFA,wamemchagua tena rais wa shirikisho hilo kushikiria kiti hicho kwa kipindi kingine cha miaka minne.
Wajumbe hao waliweza kumchagua Sepp Blatter kwa wingi wa kura zipatazo 186 kati ya kura 203 zilizo pigwa.
Sepp Blatter, ambaye alikuwa mgombea pekee katika kiti hicho, baada ya mpinzani wake Mohamed bin Hammam kujitoa kutokana na kashfa za rushwa.
Hata hivyo, uchaguzi huo ulifanyika baada ya Uingereza kushindwa kuwashawishi nchi wanachama wa shirikisho hilo kupiga kura ya kutaka uchaguzi huo usimamishwe kwa muda, ili achaguliwe mpinzani dhidi ya Sepp Blatter, lakini matokea ya kura hizo yalipinga maombi ya Uingereza kwa 172 kutaka uchaguzi ufanyike na 17 kuunga mkono Uingereza.
Kuchaguliwa kwa Sepp Blatter, kumeaandamana na misukosuko mingi iliyo ikuta shirikosho hilo baada ya kashfa za rushwa kuandama uongozi mzima wa shirikisho hilo FIFA.
Akiongea baada ya matokeo ya uchaguzi, rais huyo wa FIFA Sepp Blatter alisema "Mimi ni kaptain ambaye naongoza jahazi lililo kumbwa na mawimbi na tuta hakikisha shirikisho la soka litakuwa mairi na kulinda heshima ya mchezo huu, kuweka wazi kila jambo na kuhakikisha matatizo yaliyo tokea hayatotokea tena, na nahaidi kwa baraka za Muumba na uzima atakao nipa basi tuta fanikiwa kuhakikisha shirikisho hili lina kuwa swafi na imara."
Mtuhumiwa wa mauaji ya Bosnia Serbi Ratko Mladik awasilishwa Hague kujibu mashitaka.
Hague, Uhollanzi -01/06/2011.Aliyekuwa mkuu wa majeshi wa Bosnia Serbia ambaye anashutumiwa kwa kuhusika na mauaji yaliyo tokea wakati wa vita 1992-95 nchini humo amewasilishwa kwenye mahakama ya kutetea haki za binadamu ili kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Ratko Maladik, atafikishwa mahakamani siku ya Ijumaa tayari kuanza kusikiliza kesi yake itakayo endeshwa jaji kutoka Uhollanzi.
Kwa mujibu wa habari kutoka mahamani zinasema "Mladik anakabiliwa kujibu mshitaka yaziyo pungua 11."
Ratko Mladik, alikamatwa baada ya kukumbia mafichano kwa muda usiyo pungua miaka 16 iliyo pita.
Hussein Mubaraka na watoto wake wawili kufikishwa mahakamani.
Kairo, Misri 01/06/2011. Serikali ya Misri imetangaza ya kuwa aliyekuwa rais wa zamani wa nchi hiyo atafikishwa mahakamani yeye na watoto wake kujibu mashitaka ya kusababisha maafa yaliyo tokea wakati wa maandamano ya kutaka ang'olewe madarakani kwa rais huyo.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikali zinasema " Hussein Mubaraka na watoto wake wawili wa kiume watafikishwa mahakamani kuanzia tarehe 13, mwezi wa nane."
Habari hizo pia zilisisitiza yakuwa ikiwa "Hussein Mubaraka atakutwa na hatia ya kuhusika na machafuko yaliyo sababisha mauaji wakati wa kutaka atolewe madarakani baada ya kutawala Misri kwa muda wa miaka 30, basi huenda akaukumiwa adhabu ya kifo."
Rais Hussein Mubaraka alitolewa madarakani baada ya maandamano yaliyo chukua siku 18 ya kutaka atoke madarakani.