Thursday, October 30, 2008

Papa John Paul II alijeruhiwa na kisu, asema katibu wake"Ilikuwa siri".

Papa John Paul II alijeruhiwa na kisu, asema katibu wake" Ilikuwa siri".

Vatican,Vatican City - 26/10/08. Aliyekuwa katibu mkuu wa hayati Papa, John Paul II, Kadinali Staninislaw Dziwisz, amesema ya kuwa, hayati Papa John Paul II, alichomwa kisu mwaka 1982, lakini haikutangazwa. Tukio la kuchomwa kisu Papa John Paul II,lili tokea nchini Ureno, wakati wa ziara ya Papa, kutembelea hekalu la Fatima kwa ajili ya kutoa shukurani kwa kupona, baada ya kupigwa risasi na raia wa Uturuki Mehmet Ali Agca.
Katibu huyo, ambaye kwa sasa ni Kadinali wa Krakow nchini Poland, alisema ya kuwa, tukio hilo lilitokea wakati mmoja wa padri kutoka Uispani Juan Fernandez Krohn huku akiwa na kisu alimsogealea,Papa John Paul II,ali kumbusu na kumchoma, lakini walinzi wa Papa, walimuwahi kabla ya kumjeruhi vibaya.
Hata hivyo kisu likimchoma lakini hakikuleta mazara makubwa sana na Papa John Paul aliendelea na ziara yake kama kawaida.
Kadinali, Stanislaw Dziwisz, aliongeza kusema ya kuwa Papa John Paul II, alisema "Itakapo fikia wakati sitaweza sema au kuongea basi muda wangu utakua umefika wa kuondoka"Papa John Paul, aliaga dunia tarehe 2/4/2005.
Cadinali, Stanislaw Dziwsz, amekuwa katibu wa hayati Papa John Paul II kwa kipindi cha miaka 40.
Picha ya hapo juu anaonekan Papa John Paul II, akiwabariki watu wakati wa moja ya ziara zake enzi za uhai wake na chini wanaonekan maelfu ya watu wakiwa wamekuja kuomba Mungu pamoja naye.
Picha ya pili anaonekana Papa John Paul II, akiwa hospitalini kwa matibabu baada ya kupigwa risasi na Mehmet Ali Agca tarehe 13/05/1981, aliruhusiwa kutoka hospitalini baada ya wiki tatu.
Picha ya chini anaonekana hayati Papa John II, akiwa anamwangalia jiwa, anejaribu kutua kwenye mabega yake.
Makubaliano ya kuwa na biashara huru kuingiza mabilioni ya pesa.
Kampala, Uganda - 26/10/08. Viongozi wa bara la Afrika, wametiliana mkataba ili kushirikiana kibiashara hivi karibuni mjini Kampala.
Mkataba huo, ulioshirikisha nchi 26, unatarajiwa kuingiza mapato kwa kiasi cha $US 624 billion kila mwaka.
Mkataba huu ambao umekutanisha jumuiya zote za barala Afrika, ambazo zimekuwa zikijumuisha nchi zilizopo katika bara la Afrika kijografia.
Jumuiya hizo, ni SADC ( Southern Africa Development Community), EAC ( East African Community),COMESA (Common Market for Eastern and Southern Africa)
Picha hapo juu, zinaonekana baadhi ya nchi zitakazo faidika na mkataba huo.
Picha ya chini wanaonekana, viongozi wa nchi za Rwanda, Tanzania Uganda, Burundi na Kenya, ambao nchi zao zitafaniwa kutokana na mkataba huo.
Tofauti za siasa ndani ya Izrael zashindwa kupata atakaye kuwa waziri kuu" Uchaguzi kufanyika mkuu njiani"
Jerusalem,Izrael - 27/10/08. Kiongozi wa chama cha Kadima bi, Tzipi Livni, ambaye alitarajiwa kuwa waziri mkuu wa Izrael, ili kushika uongozi ulioachwa na aliye kuwa waziri mkuu wa Izrael, Ehud Olmert, ambaye alijiuzuru kutokana na kashfa ya kuhusika rushwa, amesema atamwomba rais wa nchi hiyo Shomon Peres kuitisha uchaguzi mapema iwezekanavyo.
Uamuzi hu wa kumwomba, rais, Shomon Peres kuitisha uchaguzi mapema, umekuja baada ya bi, Tzipi Livni, kushindwa kuunda serikali ya mseto.
Hata hivyo wachunguzi wa siasa nchini Izrael, wanasema ya kuwa mpinzani mkubwa wa bi Tzipi Livni, atakuwa aliyewahi kuwa waziri kuu wa Izrael, Benjamin Netanyahu ambaye ni kiongozi wa chama cha Likud.
Picha hapo juu anaonekana, Tzipi Livni , akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni.
Mvutano wa imani waleta utata,waumini wa dini tofauti kutoaminiana.
Borepang,India - 23/10/08. Mvutano wa kidini kati ya waumini wa dini ya Hindu na wale waumini ya dini ya Kikristu wamekuwa na wakati mgumu, kufuatia mvutano na ghasia zinazo letwa na waumini mwenye msimamo mkali kutoka pande zote za waumini wa dini hizi"Haya yalisemwa na mmoja wa mchunguzi wa maswala ya dini nchini India.
Kufuatia mvutano huu, kumeleta baadhi ya maeneo ambayo waumuni wa pande wa dini kutoka pande zote wamakuwa wanashindwa kwenda kusikia mahubiri, baada ya baadhi ya maadhi ya mahekalu na makanisa kuchomwa moto au kubomolewa.
Hata hivyo , msemaji wa serikali ya India, amesema yakuwa serikali ya India, inafanya kila jitihada kutatua matatizo haya.
Picha hapo juu,lianaonekana moja ya jengo la kanisa likiwa limeungua vibaya huku picha ya Yesu Kristu ikiwa imebakia imeninginia,baada ya kuchomwa moto na waumini wa dini nyingine ambao wanapinga kuwepo kwa dini ya Kikristu kwenywe eneo hilo.
Picha ya pili ni ya hekalu la waumini wa dini ya Hindu,likiwa lime aribiwa vibaya na moto mara baada ya kuungua na moto, ambao inasadikiwa waumini wa dini wapinzani ndiyo walio choma kanisa hilo.
Kesi ya Thomas Lubanga, bado yagonganisha vichwa vya sheria.
Hague,Uholanzi - 23/10/08. Mahakama ya kimataifa inayo shughulikia makosa ya jinai, ambayo inasikiliza kesi inayo mkabili aliyekuwa askari aliye ongoza vita zidi ya serikali ya Congo, hasa katika sehemu za Ituri bwana, Thomas Lubanga, imesema ya kuwa kuyumba kwa kesi yake kumeleta hali ya utata na kusababisha kusimamishwa kwa kesi hii.
Hata hivyo, Thomas Lubanga, ambaye anashutumiwa kuwatumia vijana wadogo kama askari wakati wa vita, ameamriwa na maakama kubaki kizuizini baada ya mahakama kukataa kuachiwa kwake huru.
Picha hapo juu anaonekana,Thomas Lubanga, akiwa ndani ya mahakama akisililiza kesi yake inayo mkabili.
Colin Powell's, asema atampigia kura, Baraka Obama"Sera za wagombea ndizo zilizo mpa uamuzi huu".
Washington, Amerika - 22/10/08. Aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Amerika, Colin Powell's, amempitisha mgombea wa urais wa Amerika, Baraka Obama kwa kusema atampigia kura katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mapema mwezi wa 11/2008.
Bwana, Baraka Obama, ambaye ndiye mgombea pekee wa urais kwa kupitia chama cha Demokratiki.
Colen Powell's, ambaye ni mwanachama wa chama cha Repablikani, na amefanya kazi na serikali iliyopo ya rais, George Bush kabla ya kujiuzuru.
Akiongea haya, Colin Powell's, alisema ya kuwa msimamo na mwelekeo wa baadhi ya viongozi waliomo ndani ya chama cha Repamblikani, na mwelekeo wa wagombea wote wanao gombea urais nchini Amerika, bwana, Baraka Obama na John MacCain's ndiyo zilizo mfanya achukue uamuzi huo wa kuamua kumpigia kura yake Baraka Obama.
Picha hapo juu, anaonekana, Colin Powell's akiongea kuidhinisha nia yake yakuwa atampigia kura Baraka Obama.
Picha ya pili wanaonekana, Baraka Obama mgombea urais kupitia chama cha Demokratiki kushoto na John MacCain's ambaye ni mgombea urais kupitia chama cha Repablikan kulia, wote wakiwa wanaeleza sera zao wakati walipo wekwa kiti moto mbele ya wananchi wa Amerika ili waweze kuchaguliwa kuiongoza nchi hiyo.

Thursday, October 23, 2008

Matunda ya uongozi bora wa nchi ya mpa nishani ya heshima"Rais wa zamani wa Botswana."

Matunda ya uongozi bora wa nchi ya mpa nishani ya heshima''Rais wa zamani wa Botswana."

Gaberone, Botswana-23/10/08. Rais wa zamani wa Botswana, Festus Mogae, ametunukiwa nishani ya kuwa kiongozi aliye tumikia taifa lake vizuri hasa kwa kupiga vita ugonjwa wa ukimwi wakati wa utawala wake.
Nishani hii iliyo anzishwa na mfanya biashara maarufu wa Afrika Mo Ibrahim, kwa madhumuni kuwafanya viongozi wa nchi za Afrika kufanya kazi vizuri na kwa uadililifu wanapo kuwa madarakani.
Nishani hiiyo itaambatana na donge nono la fedha zipatazo US$ Million 5, ambazo atazipa kwa kipindi cha miaka kumi.
Hapo juu anaonekana, Mo Ibrahim, akipiga makofi kumshangilia rais wa zamani wa Botswana, Festus Mogae, wakati wa kutinikiwa nishani
Picha pili, anaonekana rais, Festus Mogae, ambaye wakati wa uongozi wake nchini Botswana, serikali yake ilijitahidi kupapambana na ugonjwa wa ukimwi.
Umwagaji wa madawa yenye sumu yaleta madhara nchini Ivory Coast.
Abidja, Ivory Coast- 23/10/08. Watu wawili wafanyakazi ya kampuni ya Tommy, wamehukumiwa kwenda jela kwa kosa la kuruhusu madawa ya sumu kumwagwa maeneo ya wazi nchini Ivory Coast.
Akiongea mara baada ya hukumu hiyo, wakili wa serikali, alisema ya kuwa alikuwa ameomba washitakiwa wahukumiwe vifungo vya maisha, lakini mahama imewahukumu watuhumiwa jumla ya miaka 25 jela.
Watuhumiwa hao bwana, Salomon Ugborugbo, ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampuni wa kampuni ya Tommy, amehukumiwa kwenda jela miaka 20 na bwana Desire Kouao amehukumiwa miaka 5 jela.
Picha hapo juu wanaonekana wachunguzi wa mazingira wakiangalia kwa makini ni kiasi gani sumu imeathiri mazingira.
Picha yapili wanaonekana wataalamu wa kusafisha mazingira, wakimwagia dawa kusafisha na sumu iliyo mwagwa sumu ambayo imeleta mazara kwa jamii na mimea.
Picha ya tatu anaonekana mwanamke mmoja , ambaye inasemekana aliathirika kutokana na kumwagwa kwa sumu karibu na maeneo aliyokuwa akiishi.
Meya wa mji ajiunga na taliban.
Herat, Afghanistan-18/10/08. Aliyekuwa meya wa mji wa Herat, Ghullamu Yahya Akbari, amejiunga tena na kundi la Taliban.
Ghullamu Yahya Akbari, ambaye ni mmoja wa viongozi na wapiganaji wa Taliban, ambaye alikuwa mstari wa mbele kupigana na wanajeshi wa Shirikisho la jumuia za nchi za Urusi ya zamani, alisema ya kuwa atarudi katika mazungumzo ikiwa majeshi ya kigeni yatatoka ndani ya nchi yake.
Picha hapo juu kushoto, anaonekana akiwa amezungukwa na wapiganaji wake.
Waingereza wawili wahukumiwa jela kwa kukiuka sheria za nchi.
Dubai,Jumuia ya Nchi za Kiarabu- 16/10/08. Raia wawili wa Uingereza, wameukumiwa kifungo cha miezi mitatu na kulipa faini yaUs $ 272 kwa kila mmoja wao baada ya kukutwa wakifanya mapenzi kwenye maeneo ya wazi.
Raia hao majina yao yamehifaziwa, walifunguliwa kesi, kwa kosa la kuvunja sheria ya kufanya mapenzi nje ya ndoa na kulewa hadharani.
Akizungumza hukumu hiyo, hakimu Hamdi Mustafa Abu el Khair, alisema ya kuwa watuhumiwa hao wakimaliza hukumu yao, wanatakiwa warudishwe nchini kwao Uingereza.
Hata hivyo, raia hao wa Uingereza, walikanusha mashitaka yao na walitolewa nje kwa dhamana.
Uingereza kupanga mkakati mpya wa kulinda usalama wa nchi.
London,Uingereza-18/10/08. Serikali ya Uingereza inafikiria kuanzisha muundo mpya wa kuwa na mtambo ambao utajumuisha mawasiliano ya kutumia simu na mtandao ili kudhibiti ualifu na ugaidi.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana katika ofisi ya mambo ya ndani ya Uingereza iliyo chini ya Jacqui Smith, zilisema hii itawasaidia polisi katika kazi zao.
Hata hivyo, wazo la serikali kuwa na mitambo hiyo, ilipingwa na Lord Carle, kwa kusema yakuwa serikali isiruhusiwe kuwa na stoo ya kulundikia habari za watu.
Picha ya hapo juu ni ya serikali ya Uingereza, nchi ambayo inafikilia mbinu mpya ya kupambana na ualifu na ugaidi.
Jumuia ya Ulaya yazidi kukuna kichwa na hali halisi ya Bulgaria.
Sofia,Bulgaria-19/10/08. Jumuia ya Ulaya imeitaka serikali ya Bulgalia, kufanya jitihada ili kukomesha uraji rushwa, ambao matokeo yake huwa inaatarisha hali ya usalama kwa wana siasa na wafanya biashara.
Kwa mujibu wa wa jumuia ya Ulaya,Bulgaria ni moja ya nchi katika jumuia ya Ulaya, ambayo uraji wa rushwa umefika kiwango cha hali ya juu,na kuifanya jumuia hiyo kukuna kichwa kila wakati kwa kuangalia ni jinsi gani watakomesha ulaji huu wa rushwa ambao umeota mizizi kwa muda mrefu.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya walinzi,wakiwa nje ya jengo moja ,kulinda hali ya usalama kwa viongozi na wafanya biashara,walipo kutana hivi karibuni.

Tuesday, October 14, 2008

Syiria kufungua uhusiano wa kiserikali na serikali ya Lebanon.

Nigeria kubadirisha majina ya mitaa,na kuyapa majina mapya."Malcos Garvey jina lake kutumika"

Abuja,Nigeria-10/10/2008. Serikali ya Nigeria, imepanga kuyapa majini mapya baadhi ya mitaa na barabara kubwa nchini humu na majina mengine kubadirishwa.
Akiongea hayo, waziri wa serikali mitaa Aliyu Umar, yakuwa baadhi ya mitaa ilipewa majina kinyume,namatakwa , mila na utamaduni wa nchi.
Msemaji wa serikali, alisema baadhi ya mitaa itapewa majina ya wanamichezo na watu mashuhuri waliochangia kwa njia moja katika kuinua uchumi wa nchi na kutetea haki za binadamu.
Kati ya watu, ambo majina yao yatatumika kama majina ya mitaa, hayati Bob Marley, Fela Anikulapo Kuti, Martin Luther King, Malcom X na Malcus Garvey.
Kwa upande wa michezo majina ya wanasoka, JJ Okacha, Kanu Nwankwo na Mery Onyali, majina yao yatatumika kama majina ya mitaa.
Picha hapo juu , ni mwanamuziki maarufu wa muziki wa raggae, hayati Bob Marley, ambaye muziki wake umekuwa kama mshawasha wahisia za kutete haki za wanyonge duniani duniani.
Picha ya pili, ni ya hayati , Fela Anikulapo Kuti, mwanamiziki ambaye musiki wake, ulikuwa unaelezea kinaga ubaga hali halisi ya maisha ya watu katika kupambana na maisha ya kila siku.
Picha ya tatu, anaone mtetezi wa haki za binadamu na usawa kwa wote nchini Amerika, Martin Luther King,akihutubia mamia mnamo miaka ya sitini.
Picha ya mwisho, anaonekana mwana harakati wa usawa wa binadamu nchini Amerika, Malcom X, akiongea katika moja ya mikutano wakati wa harakati za kutetea haki za binadamu.
Bunge la Uingereza la pinga, "Waziri mkuu asisitiza msimamo wake mpaka ufanikiwe".
London,Uingereza-14/10/2008. Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brawn, amesema atahakikisha yakuwa siku za kuwekwa kizuizini kwa watu wale wanao shukiwa wanajihusisha na ugaidi nchini Uingereza zina ongezwa hadi kufikia siku 42.
Waziri mkuu, Brawn, alisisitiza hayo mara baada ya matokea ya kura zilizo pigwa katika bunge la Uingereza kukataa mswaada wa kuongeza siku za watu kukaa kizuizini kwa washukiwa wanao jihusisha na ugaidi nchini Uingereza.
Kura za kukubaliana na mswaada ambazo zilikuwa 118 na zile zinazo pinga mswaada huo kuwa 308, hivyo kuweka mswada huo katika wakati mgumu, hasa kwa serikali ya waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brawn.
Picha hapo juu ni ya bunge la Uingereza, ambalo limekataa mswaada wa kuongeza siku toka siku 28 hadi 42, baada ya kura kupigwa.
Picha ya pili anaonekana waziri mkuu wa wa Uingereza Gordon Brawn, akionyesha kwa ishara yakuwa kunahaja ya kufungua macho zaidi na kuona kwa makini nini ugaidi unafanya katika jamii.
Syiria kufungua uhusuiano wa kiserikali na serikali ya Lebanon.
Damascus, Syiria-14/10/2008.Rai wa Syiria, Bashar Al- Assad, ametandaza rasmi yakuwa serikali yake itafungua ofisi za kibalozi nchini Lebanon.
Ufunguzi wa ofisi za ubalozi wa Syiria nchini Lebanon, kumekuja tangu mwaka 1948, wakati Lebanon ilipo pata uhuru kutoka kwa Ufaransa.
Uhusiano wa nchi hizi mbili, umekuja baada ya rais wa Lebanon Michel Sleiman, kutembela Syiria mapema mwezi wa nane mwaka huu.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Lebanon, amesema ya kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Lebanon, Fawzi Salloukh, atafanya ziara ya kiserikali nchini Syiria hivi karibuni.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Syiria, ofisi za kibalozi kati ya nchi hizi mbili funguliwa kabla ya mwisho wa mwaka.
Picha hapo juu wanaonekana, marais wa Lenbanon Michel Sleiman na rais Bashar Al Asaad wakieleka kwenya kukagua gwaride la heshima wakati rais wa Lebano alipo tembelea Syiria.
Picha ya chini wanaonekana rais Bashar Al Saad wa Syiria na rais wa Lebanon Michel Sleiman wakikagua gwaride la heshima wakati wa ziara ya kiserikali ya rais wa Lebanon mapema mwezi wa nane mwaka huu.
Fedha zilizo tolewa na serikali ya Jumuia ya Ulaya na Amerika zainua hali ya masoko.
Brussel, Belgium-14/10/2008. Masoko ya hisa karibu kote duniani yame anza kurudi katika hali yake ya kawaida, baada ya serika ri za jumuia hii ya Ulaya kutoa pesa ili kuzisaidia benki, ambazo zimepata mtikiso kutokana na mporomoko wa biashara wa kifedha.
Na wakati huo huo, rais wa Amerika George Bush, amatangaza rasmi yakuwa serikali itatoa pesa zipatazo dola billion 250,ili kuinua masoko ya nchi hiyo.
Mtikisiko na mporomoko wa hisa ulitokea siku za nyuma, baada baadhi ya mabenki makubwa kushindwa kuhimiri mzunguko wa hisa hizo katika masoko ya dunia kwa kuanzia jijini Tokyo hadi New York.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Amerika nchi ambayo kuporomoka kwa soko la hisa, kulisababisha tikisiko na mporormoko wa masoko duniani kote.
Picha ya pili ni ya bendera ya jumuia ya Ulaya, jumuia ambayo imekuwa ya kwanza kutoa fedha ili kuchangia fedha kusaidia kuinia mabenki na soko la hisa katika jumuia hiyo, na matokeo yake kusaidia kuimasoko kurudi katika hali yake yakawaida.
Mgogoro wa ardhi mpakani huenda ukaleta mvutano mkubwa.
San Pedro,Paraguai-14/10/2008.Uchaguzi uliofanyika mwezi wa april nchini Paraguai umekuwa ni kinyume na matarajio ya wakulima hao.
Kwa mujibu wa msemaji wa wakulima hao,alisema' yakuwa maeneo yao ya asili yamekuwa yakikaliwa na wanchi wakulima kutoka nchi ya Brazil.
Mvutano huo wa kugombea ardhi kati ya wananchi wa nchi hizi mbili, umekuwa ukijadiliwa na viongozi wa serikali zote mbili kwa kipindi kirefu, na mpaka sasa bado mvutano huo haujapatiwa uvumbuzi".
Mgogoro huu wa kugombea ardhi,katika maeneo yanayo pakana nchi hizi mbili, umekuwa ni mkubwa na sasa ni sisi wananchi tunazidi nyanyaswa.
Msemaji huyo alisema kuchaguliwa kwa rais, Fernando Lugo, kulikuwa ndiyo matumaini yao, lakini matumaini haya yamekuwa ni ndoto.
Picha hapo juu ni baadhi ya wakulima wakiwa wameweka kambi karibu na barabara ili kuonyesha kutorizika kwao na serikali ya rais Fernando Lugo kwa kuto timiza haadi yake.

Thursday, October 9, 2008

Angola yaitaka Ufaransa kufuta kesi inayo wakabili ya viongozi wake.

Aliyetaka kuzindua kitabu kumuelezea ,Baraka Obama, arudishwa kwao. Nairobi, Kenya-07/10/2008.Raia mmoja wa Amerika, bwana Jarome Corsi, amerudishwa kinguvu nchini Amerika, baada ya kuingia nchini bila kutimiza sheria. Bwana, Corsi, ambaye alikuwa nchini Kenya, kuzindua kitabu chake (The Obama Nation), ambacho kilikuwa na makusudio ya kumuelezea kiundani, kimaisha na maisha ya kisiasa ,mgombea pekee wa kiti cha urais wa Marekani,kwa kupitia cham chama cha Demokratiki, bwana Baraka Obama, alikutwa kwenya hotel na kupelekwa kiwanja cha ndege. Picha hapo juu ni ya bwana Jarome Corsi, akisindikizwa kiwanja cha ndege, tayari kurudi kwao Amerika kabla ya kuzindua kitabu chake( the Obama Nation ). Askofu Mkuu, Ameritus Desmond Tutu,awapa kitendawili wananchi wa Afrika ya Kusini.

Cape Town,Afrika ya Kusini-08/10/2008. Askofu mkuu wa Kanisa la Kianglikana nchi Afrika ya Kusini, Askofu Desmond Tutu, ameseama wananchi wa Afrika ya Kusini, wamekuwa kama isemavyo bibilia, ya kuwa wale waliovuka mto Jordani, na kusahahu ya kuwa mahali walipo sasa, wamefika baada ya kuvuka mto huo wa Jordan.
Askofu, Desmond Tutu ambaye mshindi wa nobeli ya zawadi ya utetezi wa amani duniani ,aliyaongea haya wakati wa kusherehekea miaka 77 ya tangu kuzaliwa kwake,mapema mwanzo mwa wiki hii mjini Cape Town.
Picha hapo juu ni kitabu Kitakatifu ambacho katika moja ya maandiko ya ke matakatifu, wana Israel walivuka mto Jordan, na baadaye walianza kuuliza maswali mengi na kufikia hata kukorofishana.
Picha ya pili anaonekana, Askofu Desmond Tutu, akiongea hivi karibuni. Picha ya chini, wanaonekana baadhi ya wananchi, wakimuunga mkono rais Thabo Mbeki, aliyekuwa rais wa Afrika ya Kusini, ambaye amejiuzuru kutokana ma mgogoro ndani ya chama tawala cha ANC - ( African national Congress )
Matumizi ya makaa ya mawe, kupunguzwa katika jumuia ya Ulaya.
Brusells, Belgium-09/10/2008.Jumuia ya Ulaya imepanga mkakakati wa kupunguza matumizi ya makaa ya mawe na mitambo yote inayo chafua hali yahewa kupunguzwa ifikapo mwaka 2013.
Kwa mujibu, wa msemaji wa jumuia hiyo, upunguzwaji wa matumizi hayo ya makaa ya mawe,kutakuja baada ya makampuni kutakiwa kulipa kwa kila kiasi cha hewa chafu kiwanda kitakacho chafua.
Kufuatia hali hii, viwanda vinavyo tumia makaa ya mawe, vitalipa kiasi cha $ million 56 kwa mwaka, na huenda kukaongeza bei ya umeme.
Picha hapo juu ina onyesha moja ya kiwanda kinacho tumia makaa ya mawe, katika moja ya nchi wanachama wa jumuia ya Ulaya, inaonyesha ni jinsi gani hali ya hewa inavyo anavyo chafuka.
Angola yaitaka Ufaransa, kufuta kesi inayo wakabili ya viongozi wake.
Paris,Ufaransa-07/10/2008.Serikali ya Angola, imeitaka serikali ya Ufaransa, kusimamisha kesi inayo wakabili baadhi ya viongozi wa Angola,kwa kuhusika na rushwa wakati wa ununuzi wa siraha mnomo miaka ya 90.
Kwa kufatia kufunguliwa kwa kesi hiyo,serikali ya Angola, imesema kuendelea kwa kesi hiyo, kutahatarisha ulinzi na usalama wa Angola.
Picha hapo juu ni ya bendera ya Ufaransa, nchi ambayo kesi imefunguliwa kuwashitaki baadhi ya viongozi walio husika katika ununuzi wa siraha mapema miaka ya 90.
Chini ni bendera ya nchi ya Angola, nchi ambayo viongozi wake wana tuhumiwa kwa rushwa wakati wa kununua siraha.
Mkuu wa jeshi , asema ipo haja ya Taliban kushirikishwa kuleta amani nchini Afghanistan.
London,Uingereza-06/10/2008.Brigedia Mark Carleton-Smith, ambaye ni mkuu jeshi,amesema yakuwa ushindi vita zidi ya kikundi cha Taliban, utakuwa ni mgumu na kuna haja ya kushirikisha kikundi hiki katika kuleta amani nchini Afghanistan.
Alisisitiza ya kuwa, ikiwa Taliban watakuwa tayari kukaa na kuzungumza, basi ipo haja ya wao kushirikishwa kisiasa, na hii ita leta kusimamisha vita nchini humo.
Kwani kuijenga Afghanistan kunahitajika kufanya kazi ya ziada,kisiasa,uchumi na kijeshi pia.
Picha hapo juu ni ya moja ya wapiganaji wakiwa wanapiga doria, katika moja ya miji nchini Afghanistan,ambapo wamekuwa wanapambana na kikundi cha Taliban.
Mlipuko wa bomu watokea karibu na makazi ya Mfalme wa Swaziland.
Mbabane,Swaziland-07/10/2008.Watu wawili walifariki dunia hivi karibuni, baada ya bomu kuripuka karibu na makazi ya mfalme wa Swaziland.
Msemaji wa serikali, alisema ya kuwa watu hao walisadikiwa kufanya uhaini, lakini bomu lililipuka kabla ya matakwa yao kutimia.
Nchini Swaziland, kumekuwa na mvutano wa kisiasa, na kusababisha baadhi ya viongozi wa siasa kuwekwa chini ya ulinzi wa serikali.
Mfalme Muswati III ametawala Swaziland tangu mwaka 1986, chini ya uongozi wake amekuwa akilaumiwa kwa kutofatilia maswala ya nchi hasa ugonjwa wa ukimwi.
Picha hapo juu ni picha ya Mfalme wa Swaziland , Mfalme Mswati III, ambaye bomu lililipuka karibu na makazi yake.

Monday, October 6, 2008

Chama tawala nchini Afrika ya Kusini kina mvutano" Hali si shwali"

Mkuu wa Polisi ajuuzulu baada ya msukumo wa meya wa jiji.

London, Uingereza-02/10/2008.Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Uingereza, amejiuzulu kazi yake,baada ya meya wa jiji la London kumtaka afanya hivyo
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi, alisema , bwna Ian Brair, amjiuzulu nafasi hii kwa manufaa ya jeshi la polisi.
Hata hivyo kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya meya wa jiji la London,alisema ya kuwa meya wa jiji hilo hakuwa na imani na mkuu huyo wa polisi, uenda wangeitisha kura ya maoni kuhusu uongozi bwana, Ian Brair.
Kujiuzuru kwa bwana, Ian Brair, kumekuja , baada ya mvutano mkubwa uliotokea kati ya jeshi la polisi na familia ya hayati Charles de Manezes.Ambapo jeeshi la polisi, lilimua kwa kumpiga risasi, hayati Charles de Manezes kwa makosa kwa kumfananisha na mmoja ya watu wanao shukiwa ni magaidi katika kituo kimoja cha treni(Metro) jijini London.
Izrael yatakiwa iyaachie baadhi ya maeneo" Asema Ehud Olmet".
Jerusalemu, Izrael-29/09/1008.Aliyekuwa waziri mkuu wa Izrael, Ehud Olmert, amesema yakuwa ina bidi Izrael ijitoe kwenye maeneo ya Ukingo wa Magharibi, Jerusalemu Mashariki ili kufanikisha mpango wa amani kati ya Izrael na Palestina.
Bwana , Olmert alisistiza kwa kusema, yeye sikiongozi wakwanza kutaha amani iwepo kwenye ukingo huo,basi umefikia wakati wa kusema hali hii kwa jamii na kuwafahaimisha vizuri.
Makomandoo wawakomboa watekwa nyara" Wote wazima"
Kairo, Misri-29/09/2008. Makomandoo wa kutoka serikali ya Sudani na Misri walifanikiwa kuwakomboa mateka waliokuwa wametekwa nyara na kundi la watu wasiojulikana.
Watu waliotekwa nyara walikuwa raia wa Misri 8 , raia wa Ulaya 11.
Kundi hilo lililo wateka nyara, lilikuwa likidai pesa ili watu hao waachiwe huru.
Watu hao waliokuwa ni watalii, walitekwa nyara karibu na mpaka na nchi ya Libya, Sudan na Misri, waliokolewa na wote ni wazima, kwa mujibu wa msemaji wa serikali ya Misri.
Picha hapo juu ni picha ya watu walio tekwa nyara wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi mjini Kairo.
India na Amerika zakubaliana kushirikiana katika nguvu za kinyuklia.
Washington, Amerika- 02/10/2008. Serikali ya India na serikali ya Amerika, zimetiliana makubaliano ya kuwa serikali ya Amerika na India kusaidiana katika kuimarisha nguvu za kinyuklia.
Katika makubaliano hayo, serikali ya India itawajibika kuruhusu, wakaguzi wa umoja wa mataifa kukagua shughuli zote za kinyuklia nchini India, na Amerika itatoa misaada ya kiufundi na maarifa kwa India.
Picha hapo juu wanaonekana,waziri mkuu wa India kushoto,bwana Manmohan Singh,akiwa na rais wa Amerika George Bush,wakati walipokutana mjini Washington.
Wateka nyara watishia kulipua meli" Wadai lazima masharti yao yatimizwe.
Mogadishu, Somalia-02/010/2008.Kikundi kimoja kinacho shikilia meli moja yenye shehena ya mizigo ambayo waliiteka nyara, wamedai yakuwa watailipua meli hiyo ikiwa hawata timiziwa masharti yao, kikundi hicho kinacho julikana kama (Somalia Islamist Militants).
Mmoja wa viongozi hawa alisema" meli hiyo ilikuwa imebeba siraha, zinazo elekea nchini Ethiopia, na kwamba hawataiachia meli hii, kwani siraha hizi zitatumika katika kuwashambulia wao".
Picha hapo juu ni ya meli ambayo imetekwanyara na mmoja ya kundi linalo pigana na serikali ya Somalia.
Chama tawala nchini Afrika ya Kusini kina mvutano,"hali si shwali".
Johannesburg,Afrika ya Kusini-03/10/2008.Viongozi kadhaa wanachama hai wa chama tawala cha ANC- African National Congress, wamesema kuna mgawanyiko ndani ya chama hicho, na hali hii inatishia mshikamano katika chama hicho.
Haya yalielezwa, baada ya aliyekuwa waziri na mwenyekiti wa ANC, Mosiuoa Lekota, kusema ya kuwa haina haja kuwa kimya kwani,kwani viongozi wa juu wa chama hicho cha ANC ni wa kulaumiwa kwa kukiuka misingi, mila na desturi ya chama hicho cha ANC.
Picha hapo juu anaonekana,Mosiuoa Lekota,alipo kuwa akiongea hivi karibuni katika moja ya mkutano.
Chini ni ya picha ya bendera ya chama cha ANC-African National Congress, chama ambacho kinatawala nchi Afrika ya Kusini.
Bolivia na Venezuela, zawekwa katika nchi zinazo pinga kushirika katika vita zidi ya madawa ya kulevya.
Washington, Amerika- 23/09/08. Serikali ya Amerika imetangaza rasmi yas kuwa imeiweka nchi za Bolivia , Burma na Venezuela katika nchi ambazo hazisirikiani na jumuia ya kimataifa kupinga au kuzuia uuzaji wa mada ya kulevya.
Hata hivyo serikali za Bolivia na Venazuela, zimesema hii inakuja kutokana na kutokuelewana kiserikali kati ya Washington na serikali hizi.
Na wakati huo huo, serikali ya Venezuela imeomba msaada wa kusaidiwa kujengewa mitambo ya kinyuklia kwa ajili ya nguvu za umeme na serikali ya Urusi. Hapo juu anaonekana rais wa Venezuela ,Hugo Chavez, akiwa ameshikilia pesa ya Amerika,wakati alipo kuwa akihutubia katika moja ya mikutano nchini Venezuela.
Picha ya pili ni ya bendera ya Amerika , nchi ambayo ina mvutano serikali ya za Venezuela na Bolivia.