Saturday, November 28, 2009

Mvutano wa kisiasa nchini Pakistan kurudia tene ?

Mvutanao wa kisiasa nchini Pakistan kurudia tena? Karachi. Pakistan - 28/11/09. Mswada wa kisheria ambao ulikuwa umewekwa kwa ajili ya kumlinda rais wa Pakistan kufuatia shutuma za rushwa umekweisha hivi karibuni. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana kutoka Pakistan, zinasema rais, Asif Ali Zardari huenda akawa na wakati mgumu wa kisiasa katika uongozi wake. Wachunguzi wa mambo ya siasa za Pakistan, wanasema huenda Pakistan, ikakumbwa na mzozo wa kisiasa ambao ulikuwepo wakati wa rais Pervez Musharraf. Picha hapo juu anaonekana, rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari akiongea hivi karibuni na waandishi wa habari.

Saturday, November 14, 2009

Waumini wa dini ya Kislaam kuelekea Mecca Kuhijji

Waumini wa dini ya Kislaam kuelekea Mecca Kuhijji. Mecca, Saudi Arabia - 14/11/09. Mamilion ya waumini wa dini ya Kislaam wameanza kuelekea nchini Saudi Arabi, kwa ajili ya Kuhiji na kujiswafi nia zao na kufuata maagizo ambayo Mungu aliyaagiza kupitia Mtume Muhammad SW. Kwa mujibu wa serikali ya Saudi Arabia, hali ya usalama ipo katika hali nzuri na hakuna haja ya Waumini wa kuwa na wasiwasi. Picha hapo juu, wanaonekana waumini wa dini ya Kislaam wakiwa katika Hijja, kwa kujiswafi. Syria na Izrael huenda wakaanza mazungumzo ya amani. Paris,Ufaransa - 14/11/09. Rais wa Syria, Bashar Al Assad,amesema amekutana na rais wa Ufaransa,Nikolas Sarkozy, wakati alipo tembelea Ufaransa kwa ziara ya kiserikali. Katika ziara hiyo, marais hao walizungumzia, ni kwa jinsi gani wataanzisha mazungumzo ya kuleta amani kati ya Izrael na Syria. Hata hivyo, rais wa Siyria, aliseama yakuwa "hatafanya mazungumzo na waziri mkuu wa Izrael moja kwa moja, itabidi Izrael kutuma ujmbe wake na Syria itatuma wajumbe wake na hapo mazungumzo yanaweza kufanyika." Picha hapo juu anaonekana rais wa Syria, Bashar al Assad, akisalimiana na rais wa Ufaransa, Nikalas Sarkozy,wakati walipo kutana nchini Ufaransa.

Rais,Baraka Obama, kuudhulia mkutano wa viongozi wa Asia.
Paya Lebar, Singapore - 14/11/09. Rais wa America, Baraka Obama, amewasili Singapore, kuudhulia mkutano wa iongozi wa Asia na Pacific, ambao unatalajiwa kuaanza siku ya Jumapli.
Akiwa ziarani kwenye bara la Asia, rais Baraka Obama, alianza kutembelea nchini Japan, na kuahaidi yakuwa Amerika itashirikiana na nchi za Asia kwa ukaribu.
Picha hapo juu, anaonekana rais, Baraka Obama, akisalimia kabla ya kuelekea nchini Singapore kwenye mkutano.

Tuesday, November 10, 2009

Serikali ya China kuisaidia Afrika.

Serikali ya China kuisaidia Afrika. Sharm El Sheikh, Misri - 10/11/09. Serikali ya china imesema itazipatia nchi za Afrika billions 10 za dollah ya Kiamerika kwa ajili ya kuinia na kujenga jamii zao nchi zao na kuziwezesha nchi hizo kufanya biashara na China. Akiongea hayo mbele ya viongozi wa Afrika waliohudhulia mkutano uliofanyaka nchi Misri, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao,alisema wale wanao ikosoa na kuilaumu serikali ya China, waangalie kwani China inawataaalamu zaidi ya 15,000 katika bara la Afrika, ambao wanasaidia katika nyanja mbalimbali na China haitajihusisha na maswala ya ndani ya nchi yoyote. Serikali ya nchini imeseini mikataba ya kibiashara na nchi nyingi za Kiafrika na kufikia kiwango cha asilimia 33% ya kibiashara kwa mwaka. Picha hapo juu, amnaonekana, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, akiongea mbele ya viongozi na marais wa Afrika walioudhulia katika mkutano uliofanyaka katika mji wa Sharm El Sheikh nchini Misri. Charles Taylor, azilaumu nchi za Ulaya Mgharibi na Amerika. The Hague, Uhollanzi - 10/11/09. Aliyekuwa rais wa Liberial, Cherles Taylor, ameiambia mahakama ya kuwa kuondolewa kwake madarakani ulikuwa mpango wa serikali ya Amerika na nchi za Ulaya Magharibi ili ziweze kutawala upatikanaji wa mali ya asili iliyopo katiak eneo hilo. Akiongea kuelezea kukamatwa kwakwe, Charles Taylor, alisema hakuwa anaotoroka au kikimbia kutoka Nigeria,bali serikali ya Nigeria, ilishindwa kutimiza makubaliano yaliyo wekwa na rais wa wakati ule Olusegun Obasanjo yakuwa hakutakuwa na kesi zidi yake ikiwa atatoka madarakani lakini ikawa kinyume cha makubaliano yaliyowekwa. Uamuzi wa kesi hiyo huenda ikatolewa mwaka 2010 baada ya pande zote kutoa ushahidi wa kutosha mbele ya mahakama. Picha anaonekana rais wa zamani wa Liberia, Charles Taylor akiwa mahakamani tayari kusikiliza kesi ambazo zinamkabili. Korea ya kaskazini na Kora ya Kusini zatupiana risasi. Seoul,Korea - 10/11/09. Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini, zimelaumia baada ya wanajeshi wa nchi hizo mbili kutupiana risasi kwenye mpaka ulipo katika bahari Manjano. Mapambano hayo ambayo yalitokea 11:28 kwa saa za maeno hayo. Hata hivyo kwa mujibu wa masemaji wa serikali ya Korea ya Kusini , alisema, " Hakukua na majeruhi yoyote." Picha hapo juu, nimoj ya meli ya kivita ambayo inaaminika ilitumika kushambuliana katika ya nchi ya Korea ya Kusini na Korea ya kaskazini.

Monday, November 9, 2009

Hatimaye Lebanon kupata serikali.

Wanaharakati na Wapalestina wavunja ukuta. Qalandiya, Palestina - 09/11/09. Wapalestina hukun wakishirikiana na wanaharakati wa kigeni wamebomoa ukuta uliojengwa kutenganisha Wapalestina na Waizrael katika eneo la mji wa Qalandiya. Wanaharakati hao na wapalestina walitumia roli na kuvuta ukuta kwa umbali wa mita mbili, kabla ya polisi wa Izrael, kuja kuwazuia. Mmoja wa wanana harakati hao, Abdullah Abu Rahma, alisema wanaona ukuta huo ni sawa ule wa Berlin, "na ikiwa leo wanaadhimisha miaka 20 tangu kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin, basi waliona ni bora kuvunja ukuta huo kwa kuadhimisha sherehe hiyo." Picha hapo juu wanaonekana, baadhi ya wanaharakatina Wapalestina wakiwa juu ya ukuta unaotenganisha Izrael na Palestina. Hatimaye Lebanon kupata serikali. Beiruti, Lebanon - 09/11/09. Waziri mkuu wa Lebanon , Saad Hariri, amkabidhi majina ya mawaziri amabo wataunda serikali ya Lebanon kwa rais wa nchi hiyo Michel Sleiman. Kuteuliwa kwa mawaziri hawa kumekuja baada ya mazungumzo marefu yaliochukuwa miezi kadhaa, kujadiliana na vyama vya upinzani ambavyo vilikataa uteuzi uliofanyaka mara ya kwanza. Serikali hiyo itakuwa na mawaziri 30,ambapo chama cha Hezbollah kimepata wizara 10. Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa vyama tofauti wakiwa katika mazungumzo ya kuunda serikali ya Lebanon itakayo apishwa kuongoza serikali. Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ,azitaka nchi za Kislaam kuisaidia nchi yake. Istambul,Turkey- 09/11/09. Rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, amezitaka nchi wanachama shirikisho la nchi za Kiislaam kuisaidi Afghanistan kiuchumi na kijamii. Akiongea hayo , rais wa Hamid Karzai, alisema wananchi wa Afghanistan, wanaitaji msaada mkubwa kwa sasa, kutokana na hali halisi ya nchi hiyo, ambapo imekuwa na matatizo ya kivita kwa muda mrefu. Picha hapo juuanaonekana, rais wa Afghanistan, Hamid Karzai, alipo wasili katika jiji Istambul. Maaelfu washangilia miaka 20 tangu kuvujwa kwa ukuta wa Berlin. Berlin, Ujerumani - 09/11/09. Wanachi wa Ujerumani pamoja na viongozi mbali mbali duniani wameungana kwa pamoja kushangilia miaka 20 ya kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin. Wakiongozwa na , Kanselar, Angela Markel na rais wa Ujerumani,Horst Koehler,na huku mvua kubwa ikinyesha viongozi hao na wananchi wali tembelea eneo ambalo ukuta wa ulikuwa umejengwa. Baadhi ya watu waliokuwepo kipindi hicho cha kuvunjwa kwa ukuta wa Berlin, wamekuwa wakisikika wakisema "hawaamiani kama sasa ni miaka 20 imepita tangu kuvunjwa kwa ukuta huo na kuifanya nchi ya Ujerumani kuwa moja." Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya watu wakiwa juu ya ukuta wa Berlini, huku wakishangilia kuvunjwa kwa ukuta huo mwaka 1989.

Thursday, November 5, 2009

Rais wa Wapalestina atangaza kutogombea urais mwakani.

Rais wa Wapalestina, atangaza kutogombea urais mwakani. Ramal, Palestina 05/11/09 - Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, ametangaza rasmi yakuwa hatagombea uchaguzi wa rais ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao 2010. Akitangaza mbele ya waandishi wa habari, alisema ameamua hivi kufuatia vikwazo ambavyo vinakwamisha kuwepo kwa amani kati ya Waizrael na Wapalestina. Picha hapo juu, anaonekana rais wa Wapalestina, Mahmoud Abbas, akijianda kuongea mbele tya waandishi wa habari kuhusu uamuzi wake wa kutogombea kiti cha urais . Wafanyakazi umoja wa mataifa nchini Afghanistan matatani. Afghanistan, Kabul - 05/11/09. Umoja wa Matifa,umetangaza ya kuwa wafanyakazi wake wote waliopo nchini Afghanistan waondoke nchini humo kutokana na hali ya usalama kuwa tata. Uamuzi huo unakuja baada ya wafanyakazi watano wa umoja wa mataifa kuuwawa hivi karibuni. Hata hivyo mwakilishi wa umoj wa matifa Kai Eide,alisema yakuwa haina maana umoja wa matifa utasimamisha misaada yake kwa Afghanistan. Picha hapo ju ni moja ya gari la umoja wa matifa, ambalo lilishabuliwa hivi karibuni.

Monday, November 2, 2009

Umoja wa Matifa waismamisha misaada ya kijeshi nchini Kongo DRC.

Umoja wa Mataifa kusimamisha misaada ya kijeshi nchi Kongo DRC.

Kinshasa, DRC - 02/11/09. Umoja wa Mataifa umesimamisha misada iliyokuwa inatoa kulisaidia jeshi la Kongo (DRC) kwa kudai yakuwa kuan baadhi ya wanajeshi wa jeshi hilo la serikali wanakwenda kinyume na sheria za kijeshi kwa kuhusika na kutesa , kunyanya na hata kuua raia.
Akiongea, msemaji wa UN, anayeshughulikia maswala ya amani, Alain Le Roy, amesema yakuwa raia wamekuwa hawapati kulindwa na jeshi hilo, na badala yake jeshi limekuwa likienda kinyume.
"ata hivyo serikali ya Kongo DRC, imesema imekuwa inafanya uchunguzi wa kesi hisi,na haitakuwa jambo la busara kwa UN kusimamisha kulisaidia keshi la Kongo kwani kutafanya hali ya usalama kuwa mbaya"alisema waziri wa habari wa wa Kongo DRC, Lambert Mende.
Picha hapo juu, ni bendera ya Umoja wa mataifa, ambapo UN, imetangaza kusimamisha kuisaidia Kongo DRC kijeshi.
Picha ya pili, anaonekana rais wa Kongo DRC, Joseph Kabila, ambye serikali yake imekuwa inawakati mgimu wa kuijenga upya Kongo DRC,na kupambana na makundi ya wapinzani wanao pigani malia ya asili ya Kongo DRC.
Korea ya Kaskazini na Amerika bado zavutana.
Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 02/11/09. Serikali Korea ya kaskazini,imeitaka serikali ya Amerika kufikiara kutoa uamuzi wa haraka kama itakubali mazungumzo ya nchi hizo mbili kufanyika.
Habari kutoka wizara ya mambo ya nje ya Korea ya kaskazini,zilisema ya kuwa Korea ya Kaskazini imeweka bayana ya kuwa inataka kuzungumza na serikali ya Amerika moja kwa moja, na kama haitafanyika haraka, basi korea ya Kaskazini itaamua ni nini la kufanya.
Hata hivyo serikali ya Amerika, imekuwa inasisitiza mazungumzo yafanyike kuwa kuhusisha nchi za China, Urussi, Japan,Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini.
Picha hapo juu, wanaonekana wanajeshi wa Korea ya kaskazini wakiwa wanakula kwata katika moja ya sherehe za kimataifa za nchi hiyo.
Hamid Karzai kuwa rais wa Afghanistan.
Kabul Afghanistan - 02/11/09. Kamati ya uchaguzi wa Afghanistan, imetangaza rasmi ya kuwa Hamid Karzai kuwa mshindi wakiti cha urais kutokana na uchaguzi wa uliofanyika mapema mwezi wanene tarehe 20, ambapo matokeo ya uchaguzi huo yalionekana yakuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi.
Uamuzi wa kumtangaza Hamid Karzai kuwa rais wa Afghanistan, kumekuja , baada ya mpinzani wake Dr Abdullah Abdullah kujitoa katika uchaguzi wa marudio ulikuwa umepangwa kufanyika tarehe 07/11/09 kwa kudai yakuwa hautakuwa wa haki, kutokana na baadhi ya mahsrti waliyo taka kutotimizwa.
Picha hapo juu, ni ya bendera nchi ya Afghanistan, nchi ambayo hali ya kisiasa imekua katika mutata kwa muda mrefu sasa.
Picha ya pili ni kushoto, Dr Abdullah Abdullah,ambaye amejitoa katika uchaguzi wa rais na kumpa nafasi ya kutangazwa Hamid Karzai kulia kuwa rais wa Afghanistan.
Iran yataka mkataba wa nyuklia utazamwe upya.
Tehran, Iran - 03/11/09. Serikali ya Iran imetaka shirika linalo shughulikia maswala ya nguvu za kinyuklia kutizamwa upya.
Akiongea na waandishi wa habari, waziri wa mabo ya nje wa Iran, Monouchehr Mottaki, alisema ya kuwa Iran,imelitizama kiundani swala la kuitaka Iran, kupeleka nje madini yanayo tumika kutengenezea nguvu za nyuklia nje ya Iran, ili kuihakishia dunia yakuwa aina mpango wa kutengeneza bomu la nyuklia.
hata hivyo Iran, imekuwa ikisisiti yakuwa haina mpango wa kutengeneza mabomu ya nyuklia.
Picha hapo ju ni moja ya kiwanda cha kutengenezea na kuchuja madini ambayo yanatumika kutengeneza nguvu za nyuklia.

Sunday, November 1, 2009

Uchaguzi wa Afghanistan waingia doa, mpinzani ajitoa kushiriki uchaguzi.

Waasi wa Nigeria watishia kuvunjika kwa makubaliano ya amani. Niger Delta, Nigeria - 01/11/09. Msemaji wa kundi MEND Henry Okah ambalo linapinga kuwepo kwa makampuni ya kigeni ambayo yanachimba mafuta katika eneo hilo limesema linataka makampuni yote yaliopo eneo hilo yaondoke. Akuiongea, Henry Okah, alisema yakuwa serikali ya Nigeria imekuwa haitimizi matakwa ya wanachi na wakazi wa Niger Delta, basi haitachukua muda hali itakuwa mbaya katika eneo hilo. Picha ya kwanza hapo juu wanaonekana wapiganaji wanaotete haki zao katika eneo la Niger Delta wakiwa wamshikilia siraha na wanatishia kuvunjika kwa makubaliano ya amani yaliyopo. Picha hapo juu, ni ya bendera ya Nigeria ya Nigeria, nchi ambayo eneo la Niger Delta linaleta kichwa kuuma kwa serikali ya Nigeria. Raia wa Afrika ya Kusini kuchunguzwa. Johannesburg, Afrika ya Kusini - 01/11/09. Serikali ya Afrika ya Kusini, inafanya uchunguzi ili kujua ni raia gani wa Afrika ya Kusini walishiriki katika vita vya Wapalestina na Waizrael mapema mwisho wa mwaka 2008. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema yakuwa ikiwa kuna raia wa Afrika ya Kusini alishiriki,hatachukuliwa hatua za kisheria, kwani serikali ya Afrika ya Kusini hairuhusu raia wake kushiriki vita bila ruhusa ya serikali. Picha hapo juu, wanaonekana, wapiganaji wakiwa wamepiga picha pamoja. Uchaguzi wa Afghanistan waingia doa, mpinzani ajitoa kushiriki uchaguzi. Kabul, Afghanistan - 01/11/09. Mgombe uchaguzi wa urais wa Afghanistan ,Dr Abdullah Abdullah, amesema hatashiriki katika marudio ya uchaguzi yanayo tarajiwa kufanyika tarehe 07/11/09. Uamuzi wa mgombea huyo, Abdullah Abdullah, alisema ameamua kutoshiriki, kwa uchaguzi huo hautakuwa wa haki. Hata hivyo, uamuzi huo, umekuja baada ya serikali kukataa kuwafukuza kazi baadhi ya viongozi ambao chama cha Dr, Abdullah Abdullah kiliwataka viongozi hao wafukuzwe kazi, kwa kukosa imani nao. Akiongea, mbele ya wadau na waandishi wa habari, alishangiliwa na baadaye kujibu maswali baadaye. Picha hapo juu, anaonekana, Dr, Abdullah Abdullah akiongea mbele ya waandishi wa habari kutoshiriki kwakwe katika uchaguzi mkuu wa rais utakaofanyika 07/11/09. Amerika bado kupata jibu la Wapalestina na Waizrael kuwa na amani.

Jerusalem,Izrael - 01/11/09.Waziri wa mambo ya nje wa Amerika Bi, Hillary Clinton, amemaliza ziara yake mashariki ya kati bila yakuwa na mafanikio makubwa ya kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael.
Hali hii inakuja baada ya viongozi wa Palestina na Izrael kuzidi kuvutana kufuatia madai tofauti ya kila upande, ambayo yamefanya hali ya amani katika eneo hilo kuwa na utata.
Picha hapo juu, anaonekana kushoto Bi, Hillary Clinton, na kulia ni rais wa Palestina, Mahmoud Abbas wakati walipo kuta mapema jana.
Picha ya pili anaonekana, waziri mkuu wa Izrael, Binyamin Netanyahu kushoto akiwa na Bi, Hillary Clinton wakati walipo kuwa wanaongea na waandishi wa habari.