Wednesday, November 28, 2007

Mazungumzo, au kuongea,ni dawa ya kumaliza uhasama"Korea,Kusini/Kaskazini.

Nyota ya Denzil Washigton yazidi kung'ara, "kumbi za sinema kurindima".

New -York. Amerika . Mcheza sinema, bora na maarufu duniani Denzil Washington, ametokea kuwa kipenzi cha watazamaji wa sinema ulimwenguni. Denzil Washington, ambaye amcheza sinema inayoitwa American Gangstar, ambayo hadi hivi sasa, ndiyo gumzo la wapenda sinema. Akiongea katika ufunguzi wa maandalizi ya sinema mpya itakayo julikana Great Debaters, mmoja ya wasimamizi wa sinema hii, amesema nyota ya Denzil Washington itazidi ngara. Sinema hii Great Debeters inatarajiwa kuingia kwenye kumbi za sinema muda si mrefu. Kwenye sinema hii, itaelezea hali halisi na jinsi gani 1930s mambo yalivyo kuwa enzi hizo. Denzil Washington amshinda zawadi nyingi za kimataifa kama mcheza sinema, Denzil Washington alizaliwa ndani ya Jijini la New York. 28/12/1954. Kocha mkuu na mkurugenzi wahojiwa na polisi" Mirungura na kabumbu". London, Uingereza - Kocha mkuu wa Portsmouth, bwana Harry Redknap na mkurugenzi wake mkuu, wamekamatwa na polisi , kwa ajili ya mahojiano. Viongozi hawa wa Portsmouth, wanashukiwa kuhusika katika ulaji mrungura,wakiwemo watu wengine hambao mpka sasa majina yao hayajulikani. Msemaji mmoja wa polisi,alisema msako huu, ni moja katika uchunguzi unaoendelea kuchunguza mirungura katika kabumbu. Hapo juu ni kocha mkuu wa Portsmouthm Harry Redknap, akiangalia kwa makini wakati timu yake ikipambana moja ya lgi zinazo endelea nchini Uingereza.
Hali bado ngumu vita zidi ya Taleban, ajari katika mapambano.
Kopenhagen,Denmark- Ofisi ya jeshi la ulinzi, nchini Denmark, imesema ya kuwa wanajeshi Uingereza, wamewaua wanajeshi wa jeshi la Denmark.
Vifo vya wanajeshi hawa vilitokea september 26, wakati walipo shambuliwa na na wanajeshi wa uingereza, katika harakati za kupambana na askari wa jeshi la Taleban
Msemaji mmoja wa jeshi, alisema bado uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.
Nawakai huo huo, wanajeshi wa jeshi la Amerika, wameshambulia basi dogo lililo kuwa limebeba wafanyakazi wa benki, ambao walikuwa wakielekea kazini.
Msemaji wa jeshi la Amerika, alisema tukio hili, lilitokea maeneo ya Shaab kaskazini ma Baghdad.
Tukio hili, limekuja wakati serikli ya Iraki, ina jadili jinsi gani kushirikiana na jeshi la Amerika ili kupunguza matukio kama haya yasiongezeke.
Pichani, ni askari( wanajeshi) wa NOTO, wakiwa mstari wa mbele kupambana na Taleban.
Mazungumzo au kuongea, ni dawa ya kumaliza uhasama"Korea. Kusini/Kaskazini.
Seoul,Korea Kusini - Serikali ya Korea ya Kusini na Serikali ya Korea ya Kaskazini, zimeanza mazungumzo, katika kuboresha uhusiano, mbao zaida ya miongo mitano zimekuwa zi uhasama.
Mazungumzo hayo yatawakutanisha, waziri wa ulinzi wa Korea ya Kusini bwana Kim Jang-soo ,
mkuuwa maswala ya usalama wa Korea ya kaskazini bwana Lee Jee-joung.
Katika ziara yake bwana Kim Jang-soo na Lee Jee-joung,wataongelea jinsi ya kutatua mgogoro wa mpaka unaotenganisha nchi hizo mbili, na atatembelea maeneo ya viwanda.
Uhasama huu,wanchi hizi mbili ulianza baada ya kusaini mkataba wa amani mwaka 1950-53, baada ya vita kuisha katika njia isiyo yakawaida.
Pichani anaonekana waziri wa ulinzi wa korea ya Kusini bwana Kim Jang - soo alipokuwa anaelekea Korea ya Kaskazini, huku akiashiria kwa dole gumba ya kuwa mabo yote yatakuwa mazuri.
Ukweli umweka mtu huru,ujanani nilifanya mambo haya"Baraka Obama".
Washingtone. USA - Mgombe wa kiti cha urahisi, kupitia chama cha Demokratiki, nchini Amerika, bwana baraka Obama, amekubali ya kuwa alishawahi kutumia madaya ya kulevya wakati wa ujana wake.
Akizungumza wakati wa kampeni ya uchaguzi, bwana Obama alikubali ya kuwa wakati yupo sekondari alisha wahi kutumia madawa ya kulevya, na anajuta ni kwanini alifanya kitendo hiki.
Bwana, Baraka Obama, aliongeza kusema ya kuwa umri wa ujana, wakati mgumu saaana, kwani unaweza fanya mambo ambayo huja ukajuta baadaye.Lakini ni vizuri kueleza ukweli, kwani hta rasi Billy Clinton, alikubali yakuwa ujanani aliwahi kutumia au kuvuta mjani(marijuana).
La muhimu ni kuacha tabia hiyo kabla ujahathirika na maisha ya baadaye.
Pichani ni picha ya bwana Baraka Obama, alipo kuwa akijibu maswali wakati wa kampei ya uchaguzi, mjini Hampshire.
Uingereza na Robert Mugabe,moto wazidi kukolea.Nani wa kuuzima?
London, Uingereza - Waziri mkuu wa Uingereza bwana Gordon Brown, amesema hatahudhuria mkutano ,utakao kutanisha viongoozi wa Afrika na Ulaya, mwezi wa desemba.
Bwana Brown,alisema haya baada ya rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kuhaidi ya kuwa atahudhulia mkuto huu.
Nia na madhumuni ya mkutano huu, kudumisha uhusiano kati ya bara la Afrika na Ulaya. Lakini hata hivyo, rais wa Umoja wa Ulaya, bwana Jose Barroso, alilisitiza mazungumzo ndiyo suruhisho la kila jambo ,na siyo matatizo ya kibinafsi.
Vile vile wajumbe wa Umoja wa Ulaya, wanona ya kuwa mkutano huu, utazidi kukuza uhusianao uliopo ka ya Afrika na Ulaya kiuchumi na Kijamii. Hapo juu pichani ni waziri mkuu wa Uingereza, bwana Gordon Brown, aliye susia kuhudhulia mkutano utakao fanyika nchini Ureno.
Hakuna "Sharia laws" Uchaguzi wa ibuka na maswala ya dini.
Nairobi, Kenya - Shirikisho la Waislamu nchini Kenya, limekanusha vikali ya kuwa, chama cha upinzani nchini Kenya, kinacho ongozwa na Raila Odinga, pindipo kikishinda uchaguzi unaotarajiwa kufanyaika mwezi wa desemba 2007, kita ruhusu maeneo fulani ya nchi Kenya kuwa na Sharia Law."Amri za kisharia".
Msemaji mmoja wa shrikosho hilo amesema hayo, baada ya viongozi wa dini ya kikristu, kutaka kujua kama habari hizi ni kweli.
Hii inakuja baada kuhaidi kulinda na kufuatili upya jinsi gani watu ambao ni wafuasi wa dini ya Kislamu wanavyo nyimwa baadhi ya haki zao, na vilevile matokeo ya kura za maoni kuonyesha ya kuwa bwana Odinga yupo, mbele kwa 45% zidi ya mpinzani wake rais wa sasa bwana Mwai Kibaki.
Nchni Kenya watu amabo ni wafuasi wa dini ya Kislamu wengi wao wanaishi maeneo ya Pwani ya Mombasa, Lamu na wachache wapo kanda za nyanda za juu.
Pichani ni waumini wa dini ya kislamu nchini Kenya wakiwa wana omba Mungu msikitii.
Wazee wa Afrika waliotimiza malengo yao,mengine yalikuwa ya ziada, kwa ubaya na kwa uzuri.
Hapo juu, ni wazee wetu wa kwanza kujua kutea haki na tamani ya mtu,katika ulimwengu wa sasa, walipigania uhuru, kwa kila namna, nakuhakikisha ya kuwa Afrika imekuwa huru.
Ijapokuwa walipo kuwa wakipigania uhuru, walikuwa na nia tofauti,jambo la maana walilo fanya ni kuakikisha kila mtu, atokeae Afrika, anakuwa huru, uweza wa kisiasa,au wakiuchumi.
Hawa viongozi wa kwanza wa Afrika, walipambana na mambo mengi,hasa kwa kuzingatia mazingira yaliyo kuwepo wakati ule.
Kitu ambacho wana wa Afrika, "hasa viongozi wa sasa", tunapashwa kujua yakuwa deni tulilo nalo ni kubwa saana, kwani viongozi hawa waliweka na kujitolea maisha yao ili kila mwafrika awe huru na kuleta usawa kwa wote.
Kama inavyo eleweka, kila binadamu anaasili ya uchoyo na uoga,awe kiongozi au raia wakawida, awe mwafrika, mzungu, mchina, au watu kutoka bara la Asia na Amerika.
Hii inategemea ni kwa kiasi gani uchoyo na uoga huu anaweza ukaishinda nafsi ya mtu.
Hali huwa ni mbaya hasa, inapotokea, mtu,watu,au kundi la watu, (aliye)au walipoewa uwezo na Baba Mola, kuwaongoza watu wenzao, kushindwa kujizuia hii tabia ya uchoyo na woga, na hapo huwa ndiyo chanzo chakuwa na matabaka,ya walio nacho na wanaotafuta kila siku.
Jambo la muhimu lazima tukumbuke, viongozi hawa wa Afrika waliotetea na kupigania uhuru, lengo lao kuu, walilikamilisha, na ndiyo maana, leo hii kila Mwafrika anatembea kifua mbele, macho mita mia.
Ni kweli, viongozi hawa walipo kamirisha kazi zao za kupigania uhuru,iliwabidi waanze kupambana na hali halisi ya kuichumi na ongezeko la watu katika kila nchi ya Afrika.
Hali hii ilipelekea jamii, kuanza kuulizana ni kwanini,mambo yanaanza kubadilika.
Tukiangalia kiundani, siyo kama viongozi hawa, hawakujua haya matatizo haya, lakini hawakuwa na mbinu mpya za kutatua matatizo haya.
Kipindi cha kupigania huru wa Afrika , dunia nzima kwa ujumla ilikuwa na wakati wa mageuzi, tukiangalia Ulaya ilikuwa inajijenga taratibu baada ya vita vya pili vya dunia, Amerika ilikuwa ian zidi kujiimarisha kwa kuwekeza vitega uchumi karibu dunani kote., kujenga uhusianao mzuri na bara la Ulaya.
Kwa kweli kipindi cha miaka ya 60s, kilikuwa kipindi cha nani anaupeo zaidi wa kuonambele, ili kumtumia mwingine kwa manufaa yake.
Wakati viongozi wa Afrika, wanafikiri nini la kufanya, dunia na walimwengu wakawa wanabadilika kimawazo, kivitendo kila kukicha, na kukatoke vishawishi ya kila namna irimradi (kila mtu),au nchi ipate inacho ona kitanufaisha jamii yake na wananchi wake.
Vile vile lazima tukumbuke, ya kuwa binadamu yoyote, awe, mwafrika, mzungu, mwarabu, mchina, muhindi au kutoka jamii yoyote, akitaka au kunia kitu, atatumia kila mbinu, vitisho, ulaghai,na kuua ili afaikiwe malengo yake.Ya huyu ndiye binadamu alivyo.
Kutokana na hayo yote, ikapeleka, baadhi ya viongozi wa Afrika, kushindwa kujizuia na tabia ya uchoyo na uoga, naikawa raisi kusahahu na kukumbuka nini walihaidi wakati wa uhuru.
Kwa kuona hivyo, (watu)au nchi ambazo zilikuwa zina hitaji kujijenga, zikapata mwanya wa kuendelea kujijenga zaidi, kwa kutumia mbinu zote walizoona zinafaa kupata mandeleo na hali hii inaendelea mpaka leo hii katika kila jamii.
Hii yote isiwe sababu, inabidi tuelewe ya kuwa, hasili ya binadamu anaependa kwanza apate yeye, na ndiyo ataweza kuangalia mwingine kama anacho cha kutosha.
Na hii inamaanisha ya kuwa hatuna haja ya kulaumiana, kwa kushutumumiana, kwani wanabinadamu wamebarikiwa na Baba Mola, kuwa na mtu au watu fulani ambao wataweza kuwaongoza wenzao, ili waweze kuwajenga kimaisha, kiuchumi na kifikra hapa duniani.
Swali la kujiuliza Je viongozi wa sasa, wanaweza kujitolea kupoteza maisha yao? Kama walivyofanya viongozi waliopigania uhuru. Je viongozi hawa wasasa wanatimiza majukumu yao ya kupenda na kujenga vya kwao, na nchi zao?
Lazima kujifunze ni jinsi gani tutatue makosa yaliofanywa na viongozi wetu siyo kubakia kuwa na choyo na woga, ambavyo ndiyo chanzo cha matatizo yote yaliopo.
Viongozi hawa waliopigaia uhuru walitimiza lengo lao, mengine yaliyo tokea baadaya ya uhuru yalikuwa ni ya ziada, mazuri kwa mbaya.
Viongozi wote dunia, kumbukeni, yakuwa mnalakujibu mbele ya Baba Mola, kama hamkutimiza yale yote yaliyo pashwa myatimize kama viongozi, kwani mpaka leo, hakuna aliye rudi kutuelezea huko wanapokwenda watu milele, kuna nini.
Ni bora tuamini Mungu yupo, kwani tukiaga dunia, natukaenda huku wanapo kwenda watu wengine wasio rudi na tusimkute, ni salama kwetu. Lakini je tukienda tukamkuta yupo tutafanya nini?
Kwani siku zote baba mzuri ni yule anayependa na jenga nyumba yake. Hayo ni maoni ya Muhariri ya kila mwezi. Mungu atubariki.Amina

Saturday, November 24, 2007

Polisi wa Brazil wachanganya madawa, msichana wa miaka 15, aona cha moto.

Bolton wavunja mwiko, Alex Ferguson aamriwa kuwa mtazamaji. London.Uingereza - Kwa mara ya kwanza, kwa kipindi kisicho pungua miaka 20. timu ya Bolton Wanders, wameweza vunja mwiko kwa kuwafunga Man United goli moja kwa bila kweye uwanja wa nyumbani. Mara ya mwisho Bolton kushinda uwanja wa nyumbani ilikuwa desembe 1978. Goli la ushindi, lili fungwa na mshambuliaji hatari Nikalas Anelka kwenye dakika ya 11 kipindi cha kwanza. Matokeo ya mchezo huu yamewaza kuipa huai timu ya Bolton,kuepuka kuwa moja ya timu zinazo elekea kushuka daraja. Kufutia hali hii, kulimfanya kocha wa timu ya Man United, bwana Alex Ferguson, kutolewa kwenye benchi la wachezaji,na kuamriwa kuwa mtazamaji, baada ya kujibishama kimaneno na mwamuzi wa mchezo huo. Pichani anaonekana kocha wa Man United, Alex Ferguson,akielekea kujiunga na watazamaji, baada ya kutolewa kwenye benchi la wachezaji.

Wakati ni mgumu kwa mshambuliaji wa Kibrazil"Aingi kambini"
Milani.Itali - Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil na Inter Milan Adriano, anatarajiwa kuanza mazoezi hivi karibuni,baada ya kuwa na matatizo binafsi.
Adriano anatarajiwa kuanza mazoezi ya peke yake huku kwao, ili kuwa tayari kuingia uwanjani tena.
Mshambuliaji huyu Adriano mwenye miaka 25, amekuwa na matatizo ya kutokuwa madhubuti kiakili, kimwili,na matatizo ya kifamilia, na wakati mwingine kunywa pombe kupita kiasi.
Hata hivyo huenda asirudi kwenye klabu yake Inter Milan,kutokana na sababu zisizo julikana.
Andriano huenda akajiunga na Man City au Arsenal, hapo atakapo kuwa madhubuti kimwili na kiakili.
Merry Jones afungiwa miaka miwili, na kutakiwa kurudisha fedha zote.
Monte Calro,Monaco-Mwana riadha maarufu wa mbio fupi duniani kwa upande wa wanake, Merry Jones, amefungiwa kukumbia au kushiriki mashindano ya aina yoyote ya riadha ya shilikisho la riadha la dunia kwa kipindi cha miaka miwili na kuvuliwa ubingwa wa dunia na kunyang'anywa medali zake alizo shinda kwenya mashindano ya olyimpiki yaliyo fanyaika Sydney Australia.
Vile vile amatakiwa kurudisha fedha zipatazo US$ 700,00 alizo pewa kama tunzo.
Merry Jones, alitangaza kujiuzuru kukumbia, baada ya kukubali yakuwa alitumia madawa yakuongezea nguvu mwilini wakati wa mashindano ya olympiki ya Sydney. Pichani hapo juu ni Mery Jones, akitoa machozi,baada ya kukili makosa yake, na picha nyingine Merry Jones akiingia ndani ya koti kusikia hukumu dhidi yake.
Rais wa zamani wa Ufaransa afunguliwa kesi za uchunguzi.
Paris. Ufaransa - Mahakama nchini Ufaransa, imefunga kesi ya uchunguzi zidi ya rais wa zamani wa Ufaransa bwana Jacques Chirac.
Kesi hii inahusu, kuajiliwa watu hewa, na matumizi ya fedha za umma wakati alipo kuwa meya wa jiji la Paris.
Kesi hizi hazikuweza kufunguliwa, wakati wa urais wake, kutokana na sheria za Ufaransa za kumlinda rais wa nchi kushitakiwa akiwa madarakani.
Hapo juu pichani ni rais wazamani bwana, Jacques Shirac akihutubia taifa.
Ili kujenga nchi upya, Somalia yapata waziri mkuu mpya.
Baidoa. Somalia- Baada ya rais Abdullahi Yusuf, kumteua bwana Hassan Hussen kuwa waziri mkuu mpya wa Somalia, amepitishwa na bunge la serikali ya Somalia na kuapishwa.
Kuteuliwa kwa bwana Hassan Hussen, ni katika kujenga uhusiano wa kimakabila nchini humo, nakuleta uhusiano wa karibu na serikali ya rais Abdillahi Yusuf, ambayo inawakati mgumu wa kuijenga upya nchi ya Somalia,baada ya kuaribika kiuchumi na kimazingira kwa kutokana na vita vya wenyewe kwa wenye.
Bwana Hassan Hussen au kwa jina jingine Nur Adde, anatokea kwenye koo Hawiye, moja ya koo kubwa ambazo ndizo zilizo na nguvu nchini Somalia.
Hapo juu ni picha ya waziri mkuu mpya wa Somalia bwana Nur Adde.
Wateka nyara wa FNL, wanataka madai yao yatimizwe na serikali.
Bujumbura. Burundi -Kikundi kinacho pingana na serikali ya Burundi, The Force for National Liberation (FNL) kimewateka nyara maafisa wa serikali.
Msemaji mmoja wa kundi hilo, bwana Pasteur Habimana, amedai wamewateka nyara mafisa wawili, mmoja ni afisa usalama wa jimbo la Cibitoke, na afisa wa polisi anaye shughulikia uchunguzi na usalama wa Bujumbura.
Msemaji huyu aliongeza kwa kusema, wameaua kufanya hivi, ili serikali iwapatie wanachama wao ambao wamafungwa katika majela ya serikali. Pichani hapo juu ni askari wa jeshi la serikali wakiwa kazini , na chini ni picha ya askari wa serikali akiangalia miili ya watu walio kufa, baada ya mapambano na wapinzani wa serikali wajulikanao kama The Force of National Libaration (FNL)
Serikali yarudi nyuma, walala hoi"Chingas warudi mitaani"
Dakar. Senegal -Baada ya serikali ya Senegal kujaribu kuwafukuza,wafanya biashara wadogo wadogo wanao uza mitaani, hasa ndani ya jiji la Dakar kwa kutumia nguvu zake za dola, imeamua kuruhusu tena wafanya biashara hawa kuendelea na biashara zao kama kawaida.
Kufuatia maelezo ya benki ya dunia,asilimia 95% ni wafanyakazi wadogo wadogo(Chingas),na kunapunguza uzururaji na ukosefu wa kazi nchini humo.
Pichani ni mwela wa kupambana na vurugu, wakiwa wanamalizia kazi yao ya kuwafukuza (Chingas), kabla ya kruhusiwa kurudi mitaanai kuendelea na biashara zao kama kawaida.
Polisi wa Brazil, wachanganya madawa,"Msicha wa miaka 15 aona cha moto."
Sao Paulo. Brazil -Kutokana na wingi wa uarifu, unaosababishwa na ukosefu wa kazi, kumepelekea kujaa wa watu walio fungwa jela.
Hali hii imesababisha, polisi kwenye jimbo moja la Para, wamefanya kitendo cha kushutua jamii ya wa Brazil na ulimwengu kwa ujumla, baada ya kumuweka mahabusu msichana mmoja wa miaka 15 na wafungwa wengine wa kiume wapatao 20.
Kutokana na kitendo hicho, cha polisi kumweka pamoja na wanaume kulipelekea msichana huu kubakwa na kunajisiwa na mahabusu wenzake wa kiume.
Uchunguzi wa kesi hii bado unandelea, na wote walio husika na uzembe huu watachukuliwa haua, msemaji wa polisi alisema.
Hapo juu ni picha za lupango nchini Brazil,ambazo zinasadikiwa kujaa, huduma ni duni.
Mimi na wewe mpaka milele, lakini siyo kama ilivyo. " Nchini Misri"
Cairo.Egypt - Zaidi ya ndoa 240, huwa zinavunjika,au wapendanao kuachana, hii ni kutokana na na achunguzi wa maswala ya jamii.
Hii ni kuwa kila siku, ndoa moja huvunjika kwa kipindi cha dakika sita (6), kwa kipindi cha mwaka wa kwanza wa ndoa, na kukadiriwa ya kuwa kuna idadi ya ndoa 2,5 millioni kwa mwaka huvunjika.
Wengi ya wanaodai taraka ni wanawake,au kupewa taraka na waume zao kutokana na sababu mbali mbali, hasa wanaume wengine kutaka kuongeza mke mwingine ndani ya nyumba.
Ingawaje kuvunjika kwa ndoa huchukua muda, hasa kuzingatia muda wa kufatilia uamuzi wa mahakama.
Lakini msemaji alisema ya kuwa kunandoa nyingi, ambazo huvunjika bila habari zake kujulikana. Hapo juu ni vifungo ya chuma vya maisha ambavyo wapendanao huwa wanafungana ili waishi milele, lakini mara wanakata kwa msumeno vifungo hivi...................................... mambo yaha
Australia yapata waziri mkuu mpya, je vita Iraq mashakani?
Sydney. Australia -Waziri mkuu wa Australia bwana John Howard,ameshindwa kupita kuwa tena waziri mkuu wa nchi hiyo kwa kipindi kingine.
Bwana Howard ambaye ameiongoza Australia kwa kipindi cha miaaka 11 kama waziri mkuu chini ya chama chake Liberal Part .
Matokeo ya uchaguzi huu, yamepa bwana Kevin Rudd ushindi mkubwa na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya chama chake cha Labor Part kushinda kura, kwa asilimia 53%, zidi ya chama cha cha bwana Howard ambacho kimepata asilimia zipatazo 47%.
Bwana Kevin amehaidi kuleta mabadiliko, na kuangalia upya kuhusu vita vya Iraq. Pichani ni picha mbili tofauti, picha ya juu anaonekana bwana Kevin Rudd, akiangalia kwa tabasamu baada ya mataokeo.Picha nyingine anaonekana bwana John Howard aki waaga wanachama wenzake baada ya kukubali mtokeo ya uchaguzi
Nimeishi kwa kunywa aja ndogo na majani ya pori"Mfanyakazi wa mbuga za wanyama"
Nairobi.Kenya - Mfanyakazi mmoja, anayefanayakazi kwenye mbuga za wanayama karibu na mlima Kenya uliopo km110 kaskazini mwa mji wa Nairobi, bwana Solomon Nyanjui ameponea chupuchupu baada ya kuanguka na helikopta. Bwana Solomon Kinyanjui, ambaye ni mfanya kazi wa Kenya Wildlife Service (KWS), amekuwa ana fanya kazi ya kuendesha helikopta, kwa kipindi cha miaka 27. Baada ya ajali kumkuta, bwana Solomoni Kinyanjui, alisema, aliweza kuishi porini na majeraha, na kwa kula majani na mkojo wake mwenyewe hadi hapo wanajeshi wa jeshi la Kenya walipo kuja kumuokoa. Hii ni mara ya pili bwana Kinyanjui anaponea chupuchupu,mara ya kwanza alipata na ajali kama hii 1995 wakati alipo kuwa akikagua mbuga za wanyama. Pichani, ni mmoja wa kifaru, ambaye bwana Solomon Kinyanjui na wafanayakazi wenzake huwa wanawalinda, na kuwafatilia kwa makini ili wasimalizwe kabisaa, na wawindaji haramu ambao huwaua na kuchua pembe zao tayari kwa mauzo. Zim dolla, kuchapishwa upya, Irani na Zimbabwe ushirikiano wa mzuri zaidi.
Harare. Zimbabwe - Gavana wa benki kuu ya Zimbabwe, bwana Gideon Gono, ametangaza ya kuwa serikali, imetoa noti mpya, hivi karibuni.
Hali hii inakuja, kutokana na kushuka kwa thamani ya pesa ya Zimbabwe, ijulikanayo kama Zimbabwe dollar.
Akiongea na waandishi wa habari, gavana Gideon Gono, lindelea kwa kusema kwa kuwashutumu baadhi ya wafanya biashara na wale watu wanao shikilia pesa, wanaombwa wa zibadilishe kwa haraka, kabla ya kupoteza thamani yake, na akaagiza benki ziongeze maasaa, ili kukabiliana na mabadiliko haya.
Wakati huo huo, ushirikioano wa Zimbabwe na Iran unazidi shamiri,baadaya viongozi wa nchi hizi mbili kukutana na kuongea wakati rais Robert Mugabe, alipo tembelea hvi karibuni nchin Iran. Pichani ni rais wa Iran, Mahamoud Amadinejad na rais Robert Mugabe, wakikagua gwaride rasmi lillilo andaliwa kwaajili ya rais Mugabe.

Friday, November 23, 2007

2million paundi kama kiinua mgongo, kiti moto cha timu ya taifa ya Uingereza kiko wazi.

Homa ya zidi panda 2010, dunia itakubali Afrika ina uwezo"Soka la dunia" Pretoria. Maandalizi ya kombe mpira wa miguu la dunia yatakayo fanyika nchini Afrika ya Kusini 2010, yamekadiliwa kuighalimu serikali kiasi kikubwa cha fedha kuliko kilivyo kadilikiwa hapo awali. Kiasi hicho huenda kikapanda hadi kufikia Us$ million 500, ni sawa na asilimia 20% la ongezeko, toka mashindano ya takapo anza na kumalizika. Akiongea, waziri mdogo wa fedha wa Afrika ya Kusini bwana Jabu Moleketi,alisema hii inatokana na kuwepo mabadiliko ya bei na mahitaji ya vifaa vitakavyo kamilisha uandaaji huu mkubwa katika historia ya soka barani Afrika. Alihaidi dunia nzima itakubali kuwa, Afrika tunao uwezo wa kuandaa mashindano haya. Hapo juu ni picha ya nembo au alama itakayo tumika wakati wa mashindano ya kombe la soka au kandanda la dunia nchini Afrika ya Kusini 2010. 2million paundi kama kiinua mgongo, kiti moto cha timu ya taifa ya Uingereza kikowazi. London. Uingereza. Kufuatia kushindwa kuingia kwenye mashindano ya kugombea kikombe cha ubingwa Ulaya, kocha mkuu wa Uingereza kibarua chake kiliota majani. Kocha huyo bwana Steve MacClaren,ametimuliwa na chama champira cha nchi ya Uingereza yeye pamoja na jopo lake la walimu. McClaren, tangu achukue timu ya taifa ya Uingereza miezi 18 iliyo pita, alisema kuondoka kwangu kama kocha wa timu ya taifa ni uchungu mkubwa katika maisha yake, na kuongezea ya kuwa amejifunza mengi kwa kipindi alicho kuwa kocha wa Uingereza. Bwana McClaren, ameondoka na kitita cha paundi million 2 kama kiinua mgongo. Hata hivyo kuondoka kwa bwana McClaren kumeleta, kufunguka milango kwa makocha kadhaa, maarufu duniani, akiwemo, kocha wa zamani wa Real Madrid, bwana Fabiano Capello, kocha wa zamani wa Chelsea bwana Jose Mourinho . Lakini , bwana Mourinho, amesema hawezi kuwa kocha au kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza. Pichani hapo juu, anaonekana aliyekuwa kocha bwana Steve McClaren na mke wake bibi Kathryn wakitokea ndani baada ya kuongea na waandisi wa habari, "huuu" kuachana na kiti moto cha timu ya taifa ya Uingereza. Waziri mkuu wa Rhodesia afariki dunia,ubaguzi ulikwisha alipotoka madarakani. Johannesburg. Afrika ya Kusini. Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Zimbabwe bwana Ian Smith, amefarika dunia hivi karibuni. Chanzo cha kifo chake hakijajulikana,lakini watu wake wakaribu walisema bwana Smith alikuwa anaugua kwa muda mrefu. Ian Smith, aliongoza kufukuzwa kwa Uingereza nchini Zimbabwe 1965, na kuongoza serikali ya wazungu wachache na kuwakandamiza wana wa Afrika waliowengi nchini Zimbabwe enzi ikijulikana kama Rhodesia. Pichani hapo juu, anaonekana Ian Smith akiongea na waandishi wa habari, wakati wa enzi zake kama waziri mkuu wa Rhodesia. Wasichana wa Uingereza kuonja lupango nchini Ghana.

Accra. Ghana, wasichana wawili raia wa Uingereza waliokamatwa na polisi julai, 2/07,wakati wakijaribu kupenyesha 6kg ya madawa ya kulevya ili kuyapeleka Uingereza kupitia kiwanja cha ndege cha Acrra wamekuta na hatia. Wasichana hawa,Yasmine Vatansever na menzake Yatunde Diya wamekutwa na makosa na wanaweza kufungwa kwa kipindi cha miaka mitatu au zaidi kufuatia sheria za kuwafunga vijana wasio timia miaka 18 nchini Ghana. Hukumu ya kesi yao inatarajiwa kutolewa desemba 5/07. Kukamatwa kwa wasichana hawa, kunakuja kuokana na ushirikiano kati ya polisi wa Ghana na Uingereza, ili kuzuia biashara hii ambayo imeshamiri saana kupitia nchi za Afrika ya magharibi na kuingizwa nchini Uingereza. Pichani ni mmoja wa wasichana na uchungi kichwani,akielekea kwenye ndinga lamwela kurudi mung'aanda kungojea kazi ya muheshimiwa bwana Pilato,ambaye hawajui atawapa mvua ngapi. Hali ya usalama, na ushindani wa kibiashara barani Afrika"Shell kuachia ngazi?" River Delta. Kutokana na kuokuwa na hali ya usalama, na mashindano ya biashara kataika uchimbaji wa mafuta eneo la mto Delta nchini Nigeria,kampuni kubwa dunia ni ya uchimbaji na uuzaji wa mafuta na gasi Shell imetangaza huenda ikauza baadhi ya hisa zake kwa kampuni moja ya kichina. Habari zilizo patikana, zimesema yakuwa,kutokuwepo usalama katika eneo hili la Delta ni chanzo kikubwa cha kudhohofisha uzalishaji wa mafuta na gesi, na hivyo kupelekea shell kufikilia kuuza hisa zake zilizopo eneo hilo. Hali yakuto kuwa na usalam, inakuja baada ya wakazi kutoona faida ya uwekezaji huu, hasa kwa kukosekana mahitaji muhimu kama, maji safi , shule, hospitali na barabara. Hata hivyo, sababu nyingine ni makampu ya kichina yamekuwa yanaleta ushindani mkubwa katika kuwekeza hisa, na kusababisha bei kupanda. Lakini ata hivyo msemaji wa shell, alikataa kuongea chochote kutokana na habari hii. Hapo juu pichani, ni makaazi mmoja wa eneo la Delta, akiangalia kwa makini jinsi uchimbuzi wa mafuta na gasi unavyo endelea.

Kuwepo kwa hari ya hatari,kwa pelekea kusimamishwa uanachama"Pakistani"
Islamabad. Koti nchini Pakistani, limetupilia mbali mashitaka yoye yaliyo kuwa yana mkabili rais,Gen. Pervez Musharaf. Koti hiyo ikiongozwa na jaji mpya aliyechaguliwa,baada ya rais, Gen Musharaf kuwafukuza kazi jaji mkuu na wenzake waliokuwepo hapo mwanzo. Kesi hiyo ilkuwa inakataa matokeo ya uchaguzi wa rais wa Pakistani, ambao ulifanyaika mwezi wa oktoba, kwa kudai ya kuwa uchaguzi huu, ulifanyika, wakati rais, Gen Musaraf alikuwa bado amiri jeshi mkuu. Kufuatiaa hali hii, rais, Gen Musharaf alitangaza hali ya hatari, na kuwaweka viongozi wa upinzani chini ya ulinzi kwa muda na baadaye waliruhusiwa kuwa huru. Hata hivyo matokeo ya koti, yamepingwa vikali na vingozi wa vyama vya upinzani, na kutishia kususia uchaguzi ujao, ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwakani. Hali hii ya hatari, imepelekea Pakistani, kanzia tarehe 22/11/07, kusimamishwa uanachama wa jumuia ya Commonwealth. Uamuzi huu umechukuliwa na mawazili wa jumuia hii, katika mkutano ulio fanyika nchini Uganda. Hapo juu anaonekana rais, Gen Pervez Musharaf akisisitizia kurudi kwa mani na utulivu Uchimbuzi wa mali ya asili waleta mvutano na wakazi, na afya zipo hatarini. London. Makampuni yanayo jihusisha na uchimbaji wa madini katika bara la Afrika, yamelaumiwa kwa kukiuka haki za binadamu. Makampuni hayo makumbwa kama Anglo American, AngloGold Ashanti, Anglo Platinum, an Vendata, ambayo ndiyo kiini cha biashara na mikataba ya madini katika nchi nyingi za Afrika. Wasemaji wa haki za bnadamu, walisema hapo mwanzo, serikali ya Uingereza, ilikataa kuingilia.,kwani ni maswala ya biashara Kulingana na habari zilizo tolewa, zilsema ya kuwa makampuni haya yamekuwa yana sababisha mgongano katika jamii, hasa kwa wenyeji ambao waishio karibu na maeneo hayo ya madini, Wengi wao wamekuwa wakiamishwa kwa nguvu bila kulipwa maslahi yoyote. Kuthibitisha haya, waziri wa maliasiali wa Zambia,ameishutumu kampuni moja uchimbaji wa madini Konkola Copper Mines( KCM) ambayo ina ubia na Vendeta kawa 51%, kwa kuchafua mazingira karibu na mato wa Kafue. Lakini msemaji wa makampuni aya amesema wanatilia maanani kwa sana na kufuata hai za binadamu, nawataendelea kushirikiana na serikali ktatua matatizo haya.

Wednesday, November 21, 2007

Tumeshikwa na mshangao, butwaa na mshituko" Wafanyakazi wa CNN"

Baada ya kuonja lupango tena, natubu makosa yangu" Mike Tyson"

Bingwa wa zamani wa ndondi wa dunia, Mike Tyson, amemaliza kifungo cha siku moja jela.
Tyson, alihukumiwa kifungo hiki baada ya kukamatwa na mihadharati na kuendesha gari, wakati akiwa amelewa na alikubali makosa haya kabla ya hukumu hiyo haijatolewa.
Hata hivyo Mike Tyson mwenye miaka 41, kumalizia kifungo hicho, siyo mwisho wa hukumu, bali itambidi atumike bwelele(bure),kwenye maeneo ya umma kwa masaa 360 kadha, ili kumalizia adhabu hii.
Pichani ni Mike Tyson, alipokuwa amudhulia tafrija moja mjini Mesa, Arizona, kabal ya hukumu hiyo.
Sampras ang'ala, lakini nyota ya sasa yazidi kung'ara"Tenisi"
Seoul. Bingwa wa zamani wa dunia wamchezo wa tenisi, Peter Sampras, alishindwa kuonyesha umail wake.
Sampras, alishindwa vibaya,na bingwa wa sasa wa dunia wa mchezo wa tenisi Roger Federer, ambaye alitawala vipindi vyote viwili vya mchezo huu kwa kushinda 6-4 6-3 machezo uliyo chukua dakika zipatazo 60.
Wakiongea na waandishi wa habari baada ya mcheo huu, Sampras, alisema kwa pande wake ni kwamba anafurahi kwani alicheza vizuri kwa kiwango chake, ingawaje uzito wa mwili bado una mletea utata kiasi, na kuahaidi mechi ijayo, ambayo watarudiana anaweza fanya mavitu yake.
Na kwa upande wa Feder, alisema amefurahi kwa kucheza na bingwa wa zamani, na Sampras ame dhihilisha ya kuwa alikuwa nyota enzi zake alimalizia kwa kuseama Federer.
Pichani hapo juu, anaonekana akifanya vitu vyake alipo pamabana na Federer.
Wanasiasa wa Ulaya Magharibi wanataka kuichafua nchi yetu" Rais Putin"
Moscow. Rais wa Russia, Vladamil Putin, amewashambilia, wanasiasa wa ulayamagharibi, kwa kuingilia maswala ya kisiasa ya nchi ya Russia, wakati wa kampeni za uchaguzi wa wabunge ambao utafanyika dec, 2-2007.
Rais, Putin alisema ya kuwa wanasiasa wa ulaya magharibi wanataka kudhoofesha hali ya nchi.
Kampeni hii, ambao rais Putin,ana ongoza chama chake cha United Russia, kinatarajiwa kushinda.
Walio kuwa na makosa,na watendaji wakati wa ubaguzi wa rangi wasamehewe"Rais Mbeki"
Cape Town. Rais wa Afrika ya Kusini, Thabo Mbeki, amesema ya kuwa watu ambao waliofanya makosa ya kisiasa kabla ya 1999, wakati serikali ya ubaguzi wa rangi, anaweza kuomba kupata msamaha.
Rais Mbeki, alisema kufuatia na hali hii, ambayo haikuisha, wa katia wa kusema ukweli na kusamaeheana( Truth and Renconciliation),ambayo iliwekwa ili kusameheana, ili kujenga upya Afrika ya kusini.
Kamisheni, liyokuwa ikiongozwa na wa kanisa la Kingrikana nchini Afrika ya Kusini, askofu Desmond Tutu iliwasamehe watu wapatao 1000 ambao walifanya makosa wakati ya serikali ya Ubagizi wa rangi. Rais Mbeki, alisema watu hawa, wanatakiwa uanza kuomba msamaha kuanzia januari 15, 2008, na kabla ya msamaha uhuu kutolewa, mazungumzo yatafanyika kwa wahusika wote.
Hapo juu, ni picha ya rais, Thabo Mvuyelwa Mbeki,ambaye anakaribia kumaliza muda wake kama mwenyekiti wa chama tawala ANC ( Afrikcan National Congress).
Tumeshikwa na mshangao, butwaa,na kustuka,"Wafanyakazi wa CNN"
Atlanta.Daktari aliye usika katiak upasuaji wa mama ya mwana muziki, Kanye West, Dr Jan Adam, alikatisha mahojiano na mtangazji maarufu wa CNN.
Mahojiano hao yaliyo takiwa kufanyika katika studio za CNN Atlanta, kati ya Dr Jan Adam na bwana Larry King, yalisimama baada ya Dr Jan Adama kupata ujumbe ya kuwa asimamishe nahijiano hayo, ambayo yange husu hali halisi kuhusu upasuaji wa wa marehemu Dr Donda, mama ya mwana muzuki maarufu Kanye West.
Hali hii ili washangaza na kuwashutua wafanyakazi wa CNN, hasa bwana Larry King, kwani walikuwa wameshajiandaa kwa matangazo haya.
Pichani ni Dr Adam akitoa kiongela sauti( Microphone) tayari kunyanyuka kutoka ndani ya studio ya CNN Atlanta.
Fungueni mipaka ya Afrika Mashariki kwa muda wa masaa 24 kila siku.
Kampala. Rais, Poul Kagame ameziomba nchi wanachama wa jumuia ya Afrika mashariki, kuwa na mpango maalumu wa kufungua mipaka kwa muda wa masaa 24.
Rais Kagame aliendelea kwa kusema, ya kuwa kutokana na hali ya uchukuzi na barabara, inakuwa ni vigumu kwa wafanya biashara, na magari yanayo beba mizigo, kwani usafirishaji huchukua siku tatu hadi tano kabala ya kumfika kule unapo hitajika.
Na ameomba kulegeza mashariti katika sekta tofauti, ili kuweza kuajili watu wenye ujizi kataika kila nchi.
Aliongezea kwa kusema ya kuwa, hivi sasa nchini Rwanda, watu wenye ujuzi na wataalamu, wanapewa kipao mbele na hakuna vikwazo tena.
Na hii inasaidia kukuza soko la kazi na biashara pian aliyaongea haya alipo kuwa akihudhuria mkutano wa kibiashara ulioandaliwa na rais wa Uganda bwana Joweri Kaguta Mseven.
Kuba bado ni mshiriki muhimu wa Afrika, katika nyanja zote za kimandeleo.
Gaberone.Serikali ya Botswana na serikali ya Kuba zimesaini mkataba wa , kibiashara, uchumu, sayansi, elimu, ufundi,michezo na afya
Akiongea wakati wa kuadhimisha miaaka 30 ya ushirikiano, balozi wa Kuba , bwana Jorge Tormo, alisema uhusiano huu wa nchi hizi mbili, umeleta maendeleo kwa pande zote, hasa kataka sekta ya elimu na afya.
Baada ya miongo minne kupita, Malkia akanyagatena ardhi ya Uganda.
Kampala.Mkutanao wa nchi wanachama wa (Commonwealth) au nchi zote zilizokuwa koloni la Mwingereza, ziananza mkutano wa pamoja kuzungumzia, maswala ya kijamii , kisiasa ,na kiuchumi.
Uganda ambaye ndiye mwandaaji wa mkutano huu ambao utafunguliwa na Malkia wa Uingereza, malkia Elizabeth II siku ya ijumaa.
Malkia ameshawasili nchini Uganda tayari kwa ufunguzi huu.
Malkia Elizabeth II, kwa mara ya mwisho alikuwa nchi 1954, kabla ya Uganda aijapata uhuru.
Malkia ameongozana na mumewe Prince Philips the Duke of Edinburg.Prince Philips ambaye 1954 aliongozana na Malkia Elizabeth, walipoembela Uganda wakati uo.
Pichani juu anaonekana rais Yoweli Kaguta Mseven, akiangalia maandalizi ya mkutano kama yana enda sawa.

Saturday, November 17, 2007

Pakistani yaibuka mshindi." Ya ngoswe wa mwachia ngoswe .

Mfalme wa tenis bado kuwa yule yule, hakuna wa kumshinda kwa sasa.

Shangai. Mchezaji wa tenis bora duniani Roger Federer amezidi kuonyesha umaili wake baada ya kushinda mpinzani wake mkuu kutoka Spaini David Ferrer kwa pointi 6-2,6-3,6-2. Mechi hiyo iliyo chukua dakika zipatazo 98. Dakika hizi zilikuwa kama moto kwa bwana Ferrer, na kumpa nafasi Feder kushinda kikombe hiki kwa mara ya pili. . Pichani hapo juu anaonekana Roger akishangilia kwa nguvu baada ya kushinda mechi mjini Shanghai. Na picha nyingine Roger na Ferrer wanaingia uwanjani huku muziki wa nguvu ukiwasindikiza kumenyana kwenye kinyanganyiro hicho ambacho Feder alibuka na ushindi na kudhihilisha ni mwamba wa tenis. Pakistani yaibuka mshindi , Ya ngoswe wa mwachia ngoswe.
Islamabad. Timu ya kriketi ya Pakistani imezidi kuimarisha ushindi wake , baada ya kuwashinda waasimu wao wakuu India na kuonyesha ya kuwa michezo na siasa ni njia mbili tofauti.
Nyota mpya ya Pakistani katika mchezo huu wa kriketi, bwana Shoab Malik, ndiye aliye kuwa mwiba kwa wana kriketi wa India baada ya kushinda ponti nyingi ambazo ziliwawezesha Pakistani kushinda kwa mizunguko 3 na India mizunguko 2.
Hapo juuu anaonekana nyota ya timu ya kriketi ya Pakistani bwana Shoab Malik akipongezwa na wenzake baada ya kushinda pointi nyingi zaidai ya wachezaji wote katika mpambano huo..
Hali ya hatari itakuwepo mpaka hali itakapo kuwa shwari" Rais Gen Musharraf"
Naibu katibu mkuu wa Amerika , bwana Negroponte, amemwomba, rais Gen Musharraf , kuondoa hali ya hatari ailiyo iweka nchi nzima.
Negroponte aliyasema hayo alipo kutana na rais Gen Musharraf, hivi karibuni wakati naibu katibu huyu alipo tembelea kikazi nchini Pakistani ili kutatua mgogoro wa kisiasa uliopo kati ya rais Gen Musharraf na wapinzai wake wanao ongozwa na bibi, Bhuto.
Hata hivyo rais Gen Musharraf ali haidi ya kuwa tarehe 9 january ni siku ya uchaguzi nchini Pakistani, na kuhaidi kuendelea kupigana na magaidi wote waliopo Pakistani.
Rais Gen Musharraf,amesema kuweka amri ya hali hatari , nikataika kurudisha utulivu na amani nchini humo, na halia hii iata tolewa pindipo hali itakapo kuwa shwari.
Pichani hapo juu ni bwana Negroponte,alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari.

Ugonjwa wa ajabu wauwa na kuacha kitendawili nchini Angola.

Luanda. Shirika la afya ulimwenguni,WHO limetangaza ya kuwa, ugonjwa usiojulikana ambao uliibuka nchini Angola, huenda umesababishwa na sumu.
WHO, imesema bado inafanya uchunguzi zaidi ili kupata utatuzi wa madhara haya, kwani mpaka sasa watu wapatao 368, wamesha ugua kutokana na sumu hii, na wengine wa 6 wamasha aga dunia
Bado yupo imara, yote yamekuwa muruha- (gado),"Msemaji wa Wackojaco"
Califonia. Mwana muziki maarufu wa muziki wa pop na kuruka majoka Michael Jackson, amaepuka kupoteza eneo na nyumba yake Neverland.
Hali hii ya kupoteza Neverland ilikuja baada ya habari kuvuma ya kuwa kwa sasa Michael ana pambana na ukwasi.
Lakini msemaji wa Michael,amesema ingawaje eneo hili Neverland lili kuwa katika utata, lakini utata huo umekwisha
Michael Jackson, ambaye tangu kuisha kwa kesi amekuwa akiishi Ireland,Dubai na Las Vegas. Pichani hapo juu ni Michael kwa sasa ,na picha nyingine chini ni Michael enzi hizo mwaka 47
Wakadogo wakombolewa na Unincef,hali yadizi kuwa mbaya. "UN"
Kinshasa.Chirika la kuhudumia watoto Unicef, limesema limekomboa askari watoto wapatao 232 kutoka kwenye makundi yanayo pigana nchini Kongo.
Watoto hawa ambao walikuwa maaskari, wengi wametoke kundi la Mayi mayi lililopo kusini mwa mji wa Kivu
Kukombolewa kwa watoto hawa, kumekuja kutokana na msaada wa UN na vyama vingine vya kusaidia watoto.
Kutokana na msemaji wa Unicef, amesema kutokana na vita vilivyo ibuka hivi karibuni, ongezeko la watoto kufanywa askari kunazidi kuongezeka
Pichani hapo juu ni askari watoto wakiwa wameshika mitutu,kushiriki kwenye vita vinavyo endelea mpaka hivi sasa.
Uzembe na kuto wajibika kwa waganga wa hospitali. "Wachangaya madawa".
Dare es Salaam.Waziri wa afya wa erikali ya Tanzania ameomba msamaha kwa familia na wananchi kwa ujumla baadaya ya upasuaji wa kimakosa ulio fanyaika katika hospitali kuu ya Muhimbili.
Uzembe huu ulifanywa na waganga wa upasuaji hospitalini Muhimbili iliyopo jijini Da er Saam, kwa kumfanyia upasuaji wa kichwa bwana Emanuel Didas, badala ya upasuaji wa goti.
Pichani ni bwana Emmanuel Didas akiwa amepumzika kitandani baada ya upasuaji wa kichwa.
Wala mirungula na kudai kitu kidogo kaeni chonjo" Sierra Leone"
Freetown. Rais mpya wa Sierra Leone, bwana Ernest Bai Koroma amepishwa hivi karibuni na kuhaidi kupigana na rushwa kwa kutumia kila aina ya siraha.
Bwana Ernest Bai Koroma, alisema inatakiwa kwa kipindi cha miaka mitatu ya kipindi cha utawala wake lazima kuwe na mabadilko na maendeleo, na hali za watu lazima zibadilike.
Aliwaagiza polisi waache mchezo wa kuomba kitu kidogo kwa raia, na walimu wasiwanyase wanafunzi kwa kuwalazisha kuwafanyia biashara. Hapo juu pichani ni bwana Ernest Bai Koroma wakati wa kampeni zake za kuwania kiti cha uraisi.
Joto la jiwe la Kisomalia kuwageukia wanajeshi wa AU" Sheikh Aden"
Mogadishu. Kiongozi wa wapinzani wanao pinga serikali ya mpito nchini Somalia Sheik Aden Hashi Ayrow, amewaagiza wapiganaji wake waanze kuwashambulia wanajeshi wa jeshi la Umoja wa Afrika waliopo nchini humo.
Navile vile ame waomba wapiganaji wengine kujiunga na kundi lake lijulikanalo kama Al Shabab
Hali hii imekuwa ngumu kwa serikali ya mpito ya Somali inayao ongozwa na rais Abdullah Yusuf , kujenga nchi ya Somalia ambayo imekuwa na vita vya wenyewe kwa wenye kwa zaidi ya miongo mmoja. Pichani hapo juu wanaonekana maskari na kifaru cha wanajeshi AU wakila doria mjini Mogadishu.
Nyeti za jela ya Guantanamo Bay zimepenyezwa hadharani
New York. Mafaili ambayo yamekusanya siri na jinsi ya kuwatunza wafungwa, ambao wanao ishi au kuletwa kwe jela ya Guantanamo.
Mafaili haya yenye kurasa zaidi ya 238, zimechapishwa kwenye mtandao na zinaonyesha jinsi gani ya kuwatunza wafungwa wanao daiwa ni magadi.
Moja ya nyeti hizi, nikuhusu ni mfungwa yupi anaruhusiwa kutembelewa na wafanayakazi wa msalaba mwekundu na nani hasiruhusiwe.
Kambi ya Guanatanamo ambao ilifunguliwa mwaka 2002,kwa ajili ya kuwaweka kizuizini magaidi wa nao saidia na Al Qaeda au Taliban . Pichani ni wanajeshi wanaolinda jela ya Guantanamo wakila doria ndani ya jela ya G'mo Bay.
Siraha ya kupunguza nguvu ya ondosha maisha ya abiria kwenye uwanja wa ndege Vancovour"Polisi mashakani"
Kanada. Polisi wa uwanja wa ndege wa Vancuvour, wamejikuta katika hali isiyo ya kawaida,baada ya kuu bila kukusudia wakati walipo tumia bunduku inayo tumia mionzi ya umemem kumtuliza raia mmoja wa Polandi bwana, Robert Dziekanski aliyekuwa na miaka 40.
Bwana, Robert Dziekanski ambaye alikuwa ana elekea nchini Kanada kuuungana na mama yake anayeishi na kufanya kazi jimbo moja lilipo magharibi ya mji wa British Columbia.
Hapo juu wanaonekana polisi wakiwa katika haakai za kumuliza marehemu Robert Dziekanski.
OJ Simpson, kizimbani tena kwa kutuhumiwa kutumia nguvu na siraha.
Nevada, Las Vegas, mchezaji wa zamani wa Amerikani football, OJ Simpson, na wenzake wanne wanakabiliwa na mashitaka ya kuchukua vitu kwa nguvu,kutoka kwenye duka mmoja karibu na kasino mjini hapo, amabalo linauza vitu vya wachezaji wa zamani na maharufu wa Kiamerika.
OJ Simpson, alikwenda kwenye duka hilo, kuchukua vitu vyake alivyodai ya kuwa viliibiwa kutoka kwenye makazi ya bwana OJ Simpson, na mwenye duka hilo ndiye aliye vinunua, na vilikuwa kwenye duka hilo.
Lakini mwenye duka hilo alidai OJ na wenzake walitumia nguvu na walikuwa na mitutu, an waitumia mitutu hiyo kuwatishia.
Hapo juu ni bwana OJ Simspson akiwa anaangalia kwa makini jinsi mwanasheria wake anavyo ongea.