Oliver Kahn ,nyota ya makipa ya Ujerumani, ameliaga rasmi lango la milingoti mitatu maeneo yake.
Munchen, Ujerumani - Aliyekuwa golikipa namba moja wa timu ya bayen Munchen, naaliyewahi kuwa golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Ujerumani, Oliver Kahn, hivi karibuni alicheza mechi yake ya mwisho na timu yake ambayo amechezea kwa kipindi zaidi ya muongo mmoja.
Oriver Kahn, ambaye alianza kudakia timu ya Karlsruher SC,wakati akiwa na miaka 18 na baadaye msimu wa 1993-94, kuamia Bayen Munchen.
Kahn alilikuwa na wakati mgumu na wakati wafuraha wakati wote alipokuwa kipa namba moja wa Buyen Munchen na timu ya taifa ya Ujerumani.
Picha ya kwamza hapo juu anaonekana kipa Oliver Kahn, akifanya vitu vyake kumnyima kaptain wa timu ya Kamerooni Rigobert Song, kufunga goli wakati wa mashindano ya kombe la dunia yaliyo fanyika Japan -Korea ya Kusini mwaka 2002.
Picha ya pili anaonekana Oliver Kahn,akiangalia bila matumaini jinsi gani nyavu zinavyo cheza, baada ya Ronaldo kufanya vitu vyake 2002 kwenye kombe la dunia lililo fanyika Japan - Korea ya Kusini.
Picha nyingine ya kati anaonekana, Oliver Kahn akitoka nje baada ya kufanya vitu vyake kulinda lango la timu yake Buyen Munchen.
Picha ya nne, anaonekana Oliver Kahn, akitokwa na damu kwenye kipaji cha uso baada ya kugongwa na kitu kisicho julikana,.
Picha ya chini anonekana Oliver Kahn, akiokoa mpira usielekeendani ya lango lake 1999, wakati timu yake Bayen Munchen ilipo pambana na Man United katika fainali za klabu bingwa za Ulaya mwaka 1999 na pembeni wanaonekana mshambuliaji wa Man United, Andy Cole na beki wa Bayen Munchen Sammy Kofour wakiangalia kwa makini.
Jimmy Carter "Amerika ifikilie kuongea na Iran" mabomu ya nyuklia "Carter", ayakadilia idadi yake duniani.
London, Uingereza - Rais wa zamani wa Amerika, bwana Jimmy Carter, amesema ya kuwa itabidi rais atakaye chaguliwa kuiongoza Amerika , kuongea moja kwa kwa na serikali ya Iran, ili kuishawishi kuacha mpango wake wa kuendelea na ujenzi wa mitambo ya nyuklia.
Akiongea haya, nchini Uingereza, bwana Carter alisema yakuwa nchi kama Amerika, Uingereza , Ufaransa, Urusi na Israel, ambazo zina mabomu ya nguvu za kinyuklia.
Aliongezea yakuwa Amerika ina siraha za nyuklia zisizo pungua 12,000, na nchi nyingine kama Ufaransa,Uingereza zina zaidi ya mamia na Israel ina zaidi ya 150 ya siraha hizo.
Picha hapo juu, anaonekana bwana, Jimmy Carter, alipo kuwa amepokea zawadi za nishani ya amani.
Picha nyingine anaonekana bwana, Jimmy Carter, akisaidia kujenga jamii hivi karibuni, ikiwa ni moja ya kazi anayo ifanya kusaidia kuinua maisha ya watu walio na kipato cha chini.
Kiongozi mpya wa bunge la Iran, aonya IAE, baada ya ripoti kutolewa.
Teheran, Iran - Bunge la Iran, limemteua aliyekuwa kiongozi wa Iran katika mazungumzo ya kinyuklia bwana Ali Larijani kuwa kiongozi wa bunge la Iran ( Spika wa Bunge).
Baada ya uteuzi huu, bwana, Ali Larijani alionya ya kuwa nchi yake Iran, itafikilia tena kushirikiana na shirika la kuchunguza nguvu za nyuklia duniani (IAE) International Atomic Energy.
Bwana, Ali Larijani ,alisema haya baada ya ripoti ya shirika hilo la IAE kutoa ripoti yake na kudai ya kuwa Iran haijashirikiana kikamilifu na shirika hilo.
Picha hapo juu ni picha ya bwana, Ali Larijani muda mfupi kabla ya kuchaguliwa kwake kuwa spika wa bunge la Iran.
Picha ya pili ni picha ya bwana Ali Larijani, enzi hizo alipokuwa akiongelea jinsi gani nchi yake Iran na swala la nyuklia mbele ya jopo la wataalamu wamaswala ya nyuklia mjini Viena.
Siasa yaingia kindumbwendubwe, waziri mkuu atakiwa ajiudhuru.
Jerusalem, Israel - Waziri wa ulinzi wa Israel, bwana Ehud Barak, amemtaka waziri mkuu wa sasa wa Israel bwana Ehud Olmert kujihudhuru kutoka serikalini kama waziri mkuu kufuatia kashfa za kupokea rushwa.
Waziri huyu wa ulinzi bwana Ehud Barak, alisema ya kuwa waziri mkuu bwana, Ehud Olmert hawezi kuongoza serikali kwani kashfa za rushwa zitakuwa zinamzonga kila wakati.
Hata hivyo waziri Olmert, alisema ya kuwa pesa hizo zilitolewa kama kama mkopo kwakwe, na hivyo ikiwa atakutwa na makosa basi atajihuzuru.
Picha hapo juu ni picha ya waziri mkuu wa sasa wa Israel bwana Ehud Olmert.
Picha ya chini ni picha ya waziri wa ulinzi wa Israel bwana, Ehud barak, ambye anataka bwana Olmert kujihuzuru.
Amani ya Lebanon, "Uongozi mpya utaleta atulivu?" Siniora arudi ofisini.
Beiruti, Lebanon - Waziri mkuu wazamini wa Lebanon, bwana Fuad Siniora, ataendelea tena kuliongoza bunge la nchi hiyo.
Uteuzi huo, umefanywa na rais mpya wa Lebanon bwana, Michel Sleiman, na aliyekuwa kiongozi wa jeshi, bwana Michel Sleiman.
Hata hivyo kundi la Hezbollah, halikufurahishwa na uteuzi huo, lakini limesema yakuwa watashirikiana na serikali ya sasa, ili kuleta amani na utulivu nchini humo.
Bwana, Fuad Siniora, ambaye anapendelea serikali ya Lebanon, ishirikiane na nchi za Ulaya Magharibi.
Pichani hapo juu ni picha ya bwana, Fuad Siniora ambaye amechaguliwa kuliongoza serikali mpya la Lebanon.
Pichani hapo juu ni picha ya rais wa sasa wa Lebanon, bwana Michel Sleiman.
Japan kufuata mkondo wa China, "Afrika soko la marighafi kwa dunia".
Yokohama, Japan - Serikali ya Japan, imetangaza ya kuwa itatoa zaidi ya $ 4billion kwa nchi za Afrika, ili ziweze kujijenga kiuchumi na kijamii kwa kipindi cha miaka mitano itakayo fuata.
Akiongea haya kiongozi wa Japan, Yasuo Fukuda, alisema ya kuwa pesa hizo zitatolewa kwa njia ya mikopo yenye riba nafuu, ili kuinua maendeleo ya bara la Afrika.
Hata hivyo, viongozi wa Afrika, walionyesha sononeko lao kuhusu, bei za bidhaa za Afrika kukuso soko katika nchi za Magharibi, hata kukabiliana na vikwazo vya kibiashara ambavyo vimewekwa na nchi hizi za magharibi.
Picha hapo juu, ni picha ya bendera ya Japan, ambayo ina taka kuingia Afrika kibiashara, ili kushindana na nchi kama China, ambayo imejijenga kiuchumi na kibiashara na nchi zilizopo barani Afrika.
Picha ya chini ni picha za viongozi na marais wa Afrika, ambao wapo Japani katika mkutanao wa kibiashara na serikali ya Japan.
Rais Muammar Gaddafi, azishutumu nchi za magharibi" Wazamisha mashua na watu hupoteza maisha".
Tripol, Libya - Kiongozi na rais wa Libya,bwana Muammar Gaddafi , amelaani kitendo cha kuwazamisha kwa makusudi baharini, Waafrika ambao hutumia njia ya bahari kufika Ulaya.
Rasi Gaddafi, alisema hay hivi karibuni na kudai nchi za Ulaya zimekuwa zikifanya hivyo kwa makusudi, na hivyo vita dhidi ya Waafrika katika bahari ya Mediteranian ni kwaajili ya kujilinda na nchi za Ulaya zinafanya kila njia kuzuia watu Waafrika wasifike ulaya kwa kudai kuwa bashua zao zimezama.
Rais, Gaddafi, hakutaja ni nchi gani, wakati alipo kuwa akiongea na wakati wa mkutano wa kibiashara
Pichani hapo juu ni picha ya rais Muammar Gaddafi,ambaye ni rais wa Libya.