Afrika kuionyesha dunia ya kuwa soka iko damuni, soka ni furaha kama ngoma zetu.
Accra Ghana - Mashindano ya kombe la mataifa ya Kiafrika yamenza hivi karibuni nchini Ghana, huku kila nchi mshiriki wa mashindano haya ikiwa na matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa huu wa mwaka 2008.
Hii itakuwa ni kwa mara ya 26 mashindano haya yana chezwa kutafuta ni nani gwiji wa soka katika bara la Afrika.
Kwa kawaida mashindano haya huwa yanachezwa kila baada ya miaka miwili, hivyo basi bingwa huwa anawakilisha bara la Afrika katika mashindano ya mabingwa wa mabara yote sita ya dunia na bingwa wa soka wa dunia.
Hivyo roho za wapenzi wa soka zipo juju kutaka kujua kama nchi zao zitaweza nyakua ubingwa huu.
Pichani hapo juu wanaonekana mamia ya watu walio hudhuria siku ya ufunguzi wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika mjini Accra 2008.
Kama tunavyo jua Afrika, mpira wa miguu siyo tu huwa pekeyake bali husindikizwa na burudani kwa ujumla, hapo juu anaonekana mmoja wa shabiki wa soka akipiga ngoma, kusindikiza wachezaji waliopo uwanjani wacheze vizuri kama wana cheza ngoma.
Picha ya tatu mpaka ya sita, wanaonekana washabiki wa kiwa na shahuku kubwa kwa kufanya vitu vyao, ili kuwapa moyo wapenzi na wachezaji kwa ujumla.
Suharto afariki dunia, alikuwa kipenzi cha nchi za magharibi wakati fulani.
Jakarta, Indonesia - Aliyekuwa rais wa zamani wa Indonesia,bwana Haji Muhammad Suharto, amefariki dunia, baada ya kupata matatizo ya kiafya kwa muda mrefu.
Bwana Suharto, ambaye ameongoza Indonesia kwa miaaka isiyo pungua therasini (30), inasadikiwa alitawala kwa kutumia mkono wa chuma na hasa wakati wa vita baridi kati ya Komunisimu na Ubepari au kati ya NATO na USSR.
Bwana Suharto alikuwa akipendwa saana na kupata misaada kutoka nchi za ulaya magharibi na Amerika.
Bwana Suharto amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 86, huku alikuwa anashitakiwa kwa makosa mengi ya haki za binadamu.Lakini kutokana sheria za za Indonesia, pindipo mtu anapo aga dunia,basi kesi yake huwa inasimamishwa.
Pichani juu ni picha ya hayati Haji Muhammad Suharto, enzi hizo alipokuwa rais wa Indonesia.
Picha nyingine anaoneka hayati rais Suharto, alipokuwa rais wa Indonesia akiongea na rais wa zamani wa Amerika bwana Billy Clinton.
Na picha ya chini anonekana hayati,rais wa zamani wa wa Indonesia, akisalimiana na rais wa zamani wa Afrika ya Kusini bwana,Nelson Mandela walipokutana.
Wapalestina waonja raha ya kuwa huru,kiongozi mwasisi afariki dunia.
Gaza, Palestina - Raia wa Kipalestina wapatao makumi kwa mamia, walivuka mpaka na kuingia nchini Misri kwa wingi kwa mara ya kwanza, baada ya kundi la HAMAS kuvunja ukuta ulio kuwa umejengwa kuwazuia Wapalestina waishio katika mji wa Gaza.
Kuvunjwa kwa ukuta huo kuliwawezesha wanchi wa Palestina kuingia nchini Misri, na kujipatia mahitaji muhimu ambayo walikuwa wanaya kosa kwa muda mrefu.
Hali hii imekuwa ikilalamikiwa na Israel, na kuiagiza serikali ya Misri kuweka usalama zaidi ili kundi la HAMAS, lisipitishe siraha.
Wakati huo huo aliyekuwa mmoja wa wanachama na mwanzilishi wa PFLP- Popular Front for the Liberation of Palestine bwana George Habash amefariki dunia siku nya jumamosi 26-01-2008, kwa ugonjwa wa moyo.
Bwana,Habash ambaye alikuwa mtu wa karibu wa kiongozi wa PLO - Palestine Liberation Organasation, hayati Yasir Arafat.
Hayati George Habash alikuwa akiishi nchini Jordan, na atakumbukwa kwa mbinu zake za kuongoza utekwaji wa ndege,na utekwaji nyara kwa wapinzani wa Palestina.
Pichani juu wanaonekana waplestina wakivuka mpka na kuingia nchini Misri,na picha ya chini linaonekana katapira,likisaidia kubomoa kabisa ukuta ili wananchi wa Palestina waweze kuvuka bila matatizo.
Uchaguzi mkuu wa Zimbabwe kuwa machi 29," Wapinzani wanamashaka"
Harare, Zimbabwe - Wapinzani wa chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe wanao ongozwa na bwana Morgan Tsvsngirai, wamelalamikia hatua ya serikali kuamua kuweka tarehe ya uchaguzi mkuu wa nchi tarehe 29 mwezi wa machi.
Msemaji wa MDC, alisema kutangazwa kwa tarehe hiyo ni kinyume, na hii inahashiria ya kuwa serikali na ZANU-PF, wanakiuka baadhi ya makubaliono, hasa kwa wasuruhishi wa mgogoro huu wa kisiasa kutoka Afrika ya Kusini wakiongozwa na rais Thabo Mbeki.
Viongozi wa MDC,wameomba uchguzi huu usogezwe mpaka mwezi wa juni.
Picha hapo juu anaonekana bwana Morgan Tsvangirai, akiutubia wananchi katika moja ya kampeni za kuimarisha chama cha MDC.
Picha chini, wanonekana vijana wanachama wa MDC wakiandamana hivi karibuni mjini Harare.
Wapiganaji (MEND) wa mwalika George Clooney, kujionea mwenyewe hali ya Niger Delta.
Niger Delta,Nigeria - Wapiganaji wa nao pigania haki zao katiaka ukanda wa mafuta wa Niger Delta, wamemwalika mcheza sinema, mwana amani na mtetezi wa haki za binadamu bwana George Clooney kutembelea eneo la Niger Delta.
Eneo la Niger Delta, ni eneo ambalo linatoa mafuta kwa wingi nchini Nigeria, limekuwa katika hali ya mashaka kila kukicha.
George Clooney mwenye miaka 46, amekuwa akijitahidi na kuiomba dunia kusiammisha vita vya Darfur, na mwalikoko huu wa watu wa Niger Delta,kumeonyesha ni jinsi gani bwan Clooney alivyo muhimu katika harakati za kuleta amani.
Wachunguzi wa mambo wamedai ya kuwa kama hali iliyopo Niger Delta, atafanyiwa kazi sasa, basi huenda ikawa na ubaya zidi kwa binadamu, kulikono hali hilivyo sasa Darfur.
Pichani anaonekana bwana George Clooney aliongea na waandishi wa habari kuhusu hali mbaya inayao sababishwa na vita hasa katika bara la Afrika.
Picha ya chnini wanaonekana wapiganajiwa wa Niger Delta(Emanicipation of the Niger Delta) mwakiwa na siraha tayari kupamabana na yoyote wanaye ona anakwenda kinyume na matakwa yao.
Makubaliano ya amani ya mjini Goma,kuwa ni mwanzo wa kuisha vita?
Kivu,Jamuhuri ya Kongo - Wapiganaji wa jeshi linalo ongozwa na Mej Laurant Nkunda, wametia mkataba wa amani hivi karibuni na serikali ya Kinshasa.
Makubaliano haya yaliyo fanyika mjini Goma, makao makuu ya Kivu Kaskazini. yalihudhuliwa na rais wa Kongo Kinshasa bwana joseph Kabila.
Kutiwa mkataba huu wa makubaliano, unakuja baada ya mazungumzo yaliyo chukua zaidi aya wiki mbili.
Kuweko kwa makubalianao haya, huenda kukumaliza mapambano ambayo yameshukua zaidi ya miaka kumi.
Kutokana na machafuko haya, inadadikiwa ya kuwa zaidi ya watu wasiopungua 1,500,hufa kila siku, kwa kukosa mahitaji ya muhimu.
Picha ni hapo juu ni picha ya kiongozi wa kundi la jeshi la wapinzani wa serikali ya Kongo Kinshasa Mej Laurant Nkunda.
Picha chini ni picha ya wapiganaji wa jeshi ka serikali wakiwa mstari wa mbele kupambana na wapinzani wa serikali hivi karibuni.
Singa singa, wadai ya kuwa haki zao za kidini zimevunjwa"Hii ni kinyume cha katiba"
Paris,Ufaransa - Wananchi wa jamihii ya Singa singa waishio nchini Ufaransa, walianadamana hivi karibuni, kupinga kuzuiliwa kuvaa vilemba vyao vya kichwani kwenye maeneo ya serikali na kwenye mashule.
Wakiongea, mmoja wa viongozi wa jamihii ya Singa singa, alisema ya kuwa kuzuiliwa kuvaa vilemba vyao, kunaingilia na kuvuruga imani ya dini yao. Kwani hata katiba inaruhusu kila mtu anayo haki kuabudu na kuomba Mungu bila kuingiliwa nakuzuiliwa kutekeleza amri za dini.
Hapa juu, wanaonekana wananchi wa jamii ya aina ya Singa singa, wakiandamana kupinga kuzuiliwa kuvaa vilemba vyao, na huku wakiwa wameshikiria picha ya kiongozi (rais ) wa Ufaransa.