Wednesday, October 8, 2014

Kesi ya Uhuru M Kenyatta njia panda kwa ICC.


Kesi ya Uhuru M Kenyatta njia panda kwa ICC.

 
 
Hague, Uhollanzi - 08/10/2014. Mwanasheria anaye mtete Uhuru M Kenyatta, ameiomba mahakama kutupilia mbali kesi inayo mkabili mteja wake, kwani haina ushahidi wakutosha.
 
Uhuru M Kenyatta ambaye anashitakiwa kwa kuhusika kwa njia moja au nyingine katika vurugu ambazo zilisababisha mauaji ya watu wasiopungua 1000 na mali nyingi kuharibiwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais wa mwaka 2007 nchini Kenya.
 
Steven Key, mwanasheria anaye mtete Uhuru M Kenyatta alisema " hii kesi in kesi ambayo haina ukweli na kila ukweli unapo ulizwa umekuwa hauwekwi mbele ya makahama."
 
" Nahivyo naiomba mahakama kuifuta kesi hii, kwani mpaka sasa upande wa mashitaka hauna cha kuonyesha kama ushahidi,na wamekubali hilo mbele ya mahakama."
 
Uhuru M Kenyatta alihudhurua kwenye kesi hiyo kama Uhuru Kenyatta, na siyo kama rais wa Kenya, baada ya kukabidhi wadhifa wa Urais wa Kenya kwa makamu wake William Ruto.
 
Kuhudhuria kwa Kenyatta katika kesi hiyo, kumekuwa ni kwa aina yake, kwani amekuwa ni mtu wa kwanza kuhudhuria akiwa kama rais aliyechaguliwa kuiogoza nchi, na kuamua kukabidhi madaraka yake kwa makamu wake na kwenda kwenye mahakama kama raia wa kawaida.
 
Ebola yaleta kitimtim bara la Ulaya.
 
Brussels, Ubeligiji - 08/10/2014. Umoja wa Ulaya umetaka upewe majibu kwanini ugonjwa wa Ebola umeruhusiwa kuingia katika bara hilo.

Swali hilo limetoke baada ya kutangazwa  kwa idadi ya watu wenye dalili za kugonjwa huo kuongezeka na huku Uhispania kuongoza baada ya watu wawili kukumbwa na ugaonjwa huo na mmoja wapo akiwa muuguzi aliyekuwa akimuuguza mtu aliyekuwa na ugonjwa huo ambaye alifariki dunia wakati akiwa katika matibabu.

Akiongea kuhusu kuingia kwa ugonjwa huo, mkurugenzi wa shirika la Afya duniani WHO Zsuzsanna Jakab amesema " itakuwa vigumu kuzuia ugonjwa wa Ebola kuingia nchi za Ulaya, kwani watu wanasafiri kutoka nchi ambazo zinaugonjwa huo na hivyo ipo haja ya kuwa na tahadhari kubwa."

Kuingia kwa ugonjwa wa Ebola katika bara la Ulaya, kumeleta mstuko mkubwa, kwani tangu ugonjwa huu ufahamike kuwepo katika bara la Afrika zaidi ya miaka 50 iliyopita na kuua watu wengi, nchi za bara la Ulaya zilikuwa hazitilii mkazo katika kuupambana nao, jambo ambalo limesababisha ugonjwa huu kusambaa kirahisi hadi kuingia bara la Ulaya.