Friday, August 24, 2012

 Mauaji yatokea Kusini Mashariki mwa Kenya.
 

Nairobi, Kenya - 24/07/2012. Watu 48 wameuwawa na wengine kujeruhiwa ikisadikiwa kuwa ni kulipa kisasi kati vijiji viwili vinavyo pakana.
Mauaji hayo yaliyotokea katika eneo la  Reketa katika kijiji cha Tarassa Kusini Mashariki  maili 300 mwa mji wa Nairobi. na kuleta mstuko mkubwa tangu mauaji yaliyotokea miaka minne iliyopita wakati na baada ya uchaguzi mkuu nchi Kenya.
Msemaji wa polisi Chifu  Joseph Kitur alisema " watu walifariki kwa kukatwa na mapanga na wengine kuchomwa moto na pia nyumba zao kuchomwa moto jambo ambalo mpaka sasa bado tunalifanyia uchunguzi nini hasa kilifanyika hapo awali na kufikia kufanyika muaji ya kinyama kama haya."
Hata hivyo mkazi mmoja wa eneo hilo alisema hii mauaji haya yote yametokana na mvyutano wa mifugo kati ya wakazi wa vijiji vya Orma na Pokomo.

Angela Merkel na Antonis Samaras wakutana kujadili hali ya Ugiriki.
 
Berlin, Ujerumani - 24/08/2012.  Waziri mkuu  wa Ugiriki amekutana na Khansela wa Ujerumani katikaharakati za kutaka kujua ni kwa kiasi nchi ya Ugiriki inavyo fuata masharti ya kuimarisha uchumi.
Waziri Mkuu Antonis Samara na  Khansela Angela Markel walikutana na kujadili ni kwa kisi gani nchi za Jumuiya ya Ulaya zitashirikiana katika kuhakikisha Ugiriki inarudisha uimara wa uchumi wake.
Antonis Samara akiongea alisema " tunataka kuwahakikishia wenzetu tutafanya kila njia kuhakikisha uchumi wa Ugiriki unakuwa na tunachoomba ni muda zaidi."
Naye  Khansela Angela  Merkel alisema" naimani Ugiriki itatimiza yote yanayo takiwa ili kukuimarisha uchumi wa nchi hiyo na kutokana kwa kufuatia  makubaliano iliyo yafanya na nchi za jumuiya  Ulaya na ukizingatia Ugiriki ni nchi ambayo kwa upande wangu ni mwanachama wa nchi za jumuiya ya Ulaya na ningependa ieleweke kuwa naunga mkono nchi ya Ugiriki kubaki kuwa mwanachama wa nchi za jumuiya  Ulaya .
Nchi ya Ugiriki imekuwa nawakati mgumu katika haarakati za kutaka kuinua uchumi wake baada  ya kupewa mkopo wa pesa kutoka nchi za jumuiya za Ulaya na kutakiwa kufanya mrekebisho ya kiuchumi jambo ambalo limekuwa likileta msuguano kati ya serikali na wanchi wake.
  
Aliyefanya mauaji nchini Norway haukumiwa miaka 21 jela.

Oslo, Norway - 24/08/2012. Mahakama nchini Norway imemuhukumu kwenda jela mshitakiwa aliyehusika katika mauaji ya watu 77 na kufanya ushambulizi kutumia mabomu katika jiji la Olso.
Anders Breivik ambaye aliwavamia vijana waliokuwa katika kisiwa cha Utoya kwa ajili ya  mkutano wa kuhamasisha siasa na kuanza kuwapiga risasi amehukumiwa miaka 21 jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya makosa hayo.
Akiongea baada ya hukumu, mshitakiwa Anders Breivik alisema " nasikitika kwa wale wanachama wenzangu kwa kushindwa kufanya mauaji zaidi wakati ule."
Anders Breivik ambaye alidai ya kuwa ni mwanachama wa Temple Knight na alifanya mauuaji hayo kwani alikuwa anapinga kuwepo kwa wageni na kukua kwa dini ya Kiislaaam nchi Norway na Ulaya.. 


Tuesday, August 21, 2012

Waziri mkuu wa Ethiopia aaga dunia.

Waziri mkuu wa Ethiopia aaga dunia.

Addis Ababa, Ethiopia - 21/08/2012. Wananchi wa Ethiopia wameaanza maombelezi baada  ya waziri mkuu wa nchi hiyo Meles Zanawi kufariki nchini Belgium kwa matibabu.
Msemaji wa serikali   Simon Bereket  akiongea baada ya habari za kifo cha Meles Zanawi alisema " makamu wa waziri mkuu Hailemariam Desalegn ataogoza hadi hapo uchaguzi mwingne mwaka  2015."
Waziri mkuu Meles Zanawi  alifariki dunia alipokuwa katika matibabu nchini Belgium na alichukua madaraka ya uongozi baada mapinduzi yaliyopelekea kuangushwa kwa Haile Mariam mwaka 1991.

 Sergie Lavrov aonya mashambulizi zidi ya serikali ya Syria.

Moscow, Urussi - 21/08/2012. Urussi imeonya na kusema kitendo chochote cha kufanya mashambulizi nchini Syria hakitakubalika.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urussi Sergie Lavrov aalionya kwa kusema " haitakiwi kuingilia maswala ya ndani ya nchi huru yoyote ikiwemo Syria, na nikinyume na sheria za kimatafa na nimekuwa nasisitiza hilo kila wakati na naonya ya kuwa kitendo chochote cha kuishambuli Syria kitaleta maafa katika jamii nzima ya maeneo hayo."
Waziri Sergie Lavrov aliyasema hayo baada ya kauli ya rais Baraka Obama kudai kuwa upo uwezekano wa nguvu za kijeshi kutumika ikiwa serikali ya Syiria itatumia siraha za sumu zidi ya wapinzani wanaopigana vita na serikali ya rais Bashar al Assad.

Waliotenda makosa ya jinai kunyongwa hivi karibuni asema rais wa Gambia.

Banjul, Gambia - 21/08/2012. Rais wa Gambia ametangaza kuwa watu wote waliukumiwa kunyonwa nchini humu watapata adhabu hiyo ufika mwezi wa Septemba.
Rais Yahya Jammen akiongea katika siku kuu ya kuadhimisha mwisho wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani alisema." ningependa kuthibitisha  ya kuwa wale watu waliohukumiwa vifo baada ya kukutwa na makosa kama ya uuaji, ubebajiwa wa madawa ya kulevya, ushoga, na makosa mengine ya jinai basi adhabu zao zitatekelezwa kwa mujibu wa sheria za nchi inavyo eleza.
""Serikali inabidi kuonyesha makali yake kwa wale wote ambao wanakiuka sheria na kuvuruga amani ya nchi  kwa njia moja au nyingine."
Rais Jammen ambaye alichukuwa madaraka mwaka 1994 baada yamapinduzi ya kijeshi na amekuwa akilaumiwa kwa kuongoza nchi kwa vitisho jambo ambalo serikali yake imekuwa ikilikana.

Monday, August 20, 2012

Machimbo ya madini yafunguliwa baada ya mauaji.

Uchaguzi wa rais wa Somalia wakwama.

Mogadishu, Somalia - 20/8/2012. Uchaguzi wa kumchagua rais wa Somalia umesimapishwa kwa mdai yakuwa wananchi wa Somalia hawakuwa tayari kwa upigaji wa kura.
Uchagu huo ambao ulikiwa kufanyaka leo 20/08/2012 umeesimamishwa kwa madai ya kuwa kuna baadhi ya matakwa ya uchaguzi lazima  yatekelezwe kwanza.
Serikali ya mpito iliyopo  ambayo iliteuliwa kwa msaada wa nchi za Ulaya Magharibi inamaliza leo mnuda wake rasmi kisheria.
Kufuatia umuzi huo, uongozi wa nchi ya Somalia utasimamiwa na viongozi 225 walioteuliwa kwa baraka za viongozi wakiasili na kuapishwa rasmi leo.
Somalia nchi ambayo tangu mwaka 1991 imekuwa ikikumbwa na mvurugiko wa amani na kusabisha vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Machimbo ya madini yafunguliwa baada ya mauaji. 

Johannesburg, Africa ya Kusini - 20/08/2012. Machimbo ya madini ya platinum yaliyopo nchini Africay Kusini yamefunguliwa baada ya kufungwa kutokana na vurugu kati ya polisi na wafanyakazi jambo ambalo lilipekea watu 44 kuuwa kutokana na kupigwa risasi. 
Kampuni inayosima mchimbo hayo Lonmin ilisema" machimbo ya Marikana yamefunguliwa na theruthi moja ya wafanyakazi 28,000 wa machimbo hayo wamerudi kazini."
Machimbo hayo ambayo yamekuwa katika habari baada ya mauaji yaliyotokea kati ya polisi na wafanyakazi wa machimbo hayo kutupiana risasi. 
Kufuatia mauaji hayo rais Jacob Zuma ameteua kamati maalumu ili kuchunguza chanzo cha muaji hayo ambayo yametokea tangu serikal ya kibagu ya Afrika ya Kusini kung'olewa.


Izrael kutumia ujumbe wa siku kwa kutoa tahadhali.

Jerusalem, Izrael - 20/08/2012. Serikali ya Izrael imekamilisha na kufanikiwa kutuma ujumbe kwa kupitia simu za mkono kuwajulisha wanachi wake ikiwa kama kunashambulizi lolote la kijeshi.
Zoezi hili ambalo lilifanyika kwa mudawa siku tano nakjuisha hivi karibuni limefanyika huku kukiwa kuna hali ya utata ya kati ya Izrael na Iran nchi ambazo zimekuwa zikilumbana kwa vitisho vya kivita jambo ambalo serikali ya Marekani ikiingilia kati ili kuituliza Izrael baada  ya kutilia mashaka ya kuwa huenda serikali ya Izrael kaamua kufanya mashambulizi bila kushauriana na washiriki wake.
Lakhadar Brahim adai kazi ni kubwa juu ya amani ya Syria.

Algies, Algeria - 20/08/2012.  Mkuu mpya ambaye ameteuliwa kusimamia uletwaji wa amani nchi Syria amesisitiza yakuwa kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha amani inarudi nchini  Syria.
Lakhdar Brahimi ambaye ni raia wa Algeria alisema "kwa sasa nchini Syria kuna vita vya wenyewe kwa wenyewe na inahitaji kazi ya ziada ilikuweza kusimisha vita hivyo kwa jirani anamuua jirani yake na wakati mwingine kaka namuua kaka yake."
Hata hivyo waziri wa mambo wa mambo ya nje wa Syria amekanusha madai ya  Lakhdar Brahim
na kusema "serikali ya Syria ina pambana na magaidi ambao wanasaidiwa na nchi zenye kutaka serekali ya iondoke madarakani na kuweka vibaraka wao ambao watatumikia."
Lakhdar Brahim amechukua nafasi ya Kofi Annani ambaye amejiudhulu katika kazi hiyo ya kusimamia kuleta amani nchini Syria.

Nchi za Amerika ya Kusini zaunga mkono uamizi wa Ekwado kwa Julian Assange.

Quito, Ekuado - 20/08/2012. Mawaziri wa mabo ya nchi za nje wa serikali za Amerika  ya Kusini wameagiza kuanzishwa kwa mazungumzo kati ya serikali ya Ekuado na Uingereza ilikutataua mzozo uliotokea kati ya nchi hizo mbili juu mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Juliane Asange.
Mawaziri hao kwa pamoja walikubaliana na kuiunga mkono Ekuado kwa uamuzi wake wakumpa hifadhi ya kiutu Julian Assange ambaye anakabiliwa na shutuma za ubakaji nchi Swedeni, jambo ambalo anakusha.
Julian Assange ambaye aliongea kwa mara ya kwanza huku akiwa kasimama katika dirisha la ubalozi wa Ekuado iliyopo jiji London Ungereza ambapo alikimbilia kwa madai upo mpango ukiopo wa kumrudisha nchini Swedeni ni wa kutaka apelekwe nchini Marekani ambapo anadai amefunguliwa mashitaka kwa kutoa habari za kisiri za Marekani katika mtandao wake wa Wikileaks.

Friday, August 17, 2012

Bingwa wa Marathon 2012Londoon apokelewa kwa shangwe nchini.


Bingwa wa Marathon 2012Londoon apokelewa kwa shangwe nchini.

Kampala, Uganda - 16/08/2012. Mwanariadha aliyeshinda mbio za Marathon za michezo ya Olympics London alikalibishwa kwa shangwe na kupewa heshima ya kupata kuonana rais Yoweri Museven.
Stephen Kiprotich aliyeshinda medali ya dhahabu katika mashindo ya michezo Olympics iliyofanyika London, alikaribishwa na rais Yoweri Museven katika chakula ambacho aliandaa kwa ajili ya mwanariadha huyo kwenye Ikulu ya rais ya Entebe.
Rais Yoweri Museven akimkaribisha Kiprotich, alisema' "ningependa kumpongeza kwa ushindi huu, na wale wote ambao wamehusika katika kumsaidia Stephen Kiprotich kuiletea ushindi Uganda."
Stephen Kiprotich  alipewa $800,000 na rais Museven na ameiwezesha Uganda kupata medali ya dhahabu baada ya miaka 40 ambapo marehemu Akii-Bua aliipatia Uganda medali ya dhahabu katika mchezo wa mbio za kuruka viunzi 400 meta.

Wednesday, August 1, 2012

Sweden yaweka ngumu kwenda ubalozi wa Ekuado.
London, Uingereza - 31/07/2012. Serikali ya Sweden imekata ombi la serikali ya Ekuado la kutaka serikali hiyo kuja kumuhoji mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks ambaye yupo ukimbizini kwenye ubalozi wa Ekuado uliopo London.
Julian Assange ambaye ndiye mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks alikimbilia katika ubalozi wa Ekuado baada ya siku zake za rufaa kukaribia kuisha, jambo ambalo linge mfanya arudi jela na huenda angesafirishwa nchi Sweden ili kujibu mashitaka yanayo mkabili ya uubakaji, jambo ambalo Assange analikataa na kulikanusha.
Assange aliamua kuomba ukimbizi ubalozi wa Ekuado uliopo London, baada ya kuhisi ya kuwa kama angerudishwa Sweden, basi angepelekwa nchi Marekani ili kujibu mashitaka ya kuchapisha nyaraka za siri za nchi ya Marekani.

Rais w Syria atakiwa kuachia madaraka.

Tunis - Tunisia - 31/07/2012.Waziri wa ulinzi wa Marekani amemtaka rais wa Syria kuachia madaraka kama anataka kuilinda familia yake.
Leon Panetta alisema " Marekani na jumuiya ya kimataifa hawatavumilia, na inabidi Asad atoke madarakani kwa kuiokoa nchi yake."
"Pia hatutafanya makosa kama tuliyo yafanya nchini Irak, na nia yetu n kuleta amani na uimara wa eneo zima kwa ujumla."
Agizo la waziri Panetta liomekuja wakati akiwa ziarani nchini Tunisia na huku vita kati ya jeshi la serikali la Syria lililo chini ya rais Asad linapambana vikali na jeshi la upinza linalo pata misaada toka nchi za nje.