Tuesday, November 10, 2015

Rais Putin asema njama za Marekani zipo wazi.

Rais Putin asema njama za Marekani zipo wazi.

Moscow, Urusi - 10/11/2015. Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema kuwa Marekani na washirika wake wanampango wa kupunguza nguvu za kinyuklia za Urusi kwa kutaka kuweka mitambo ya siraha za kinyuklia barani Ulaya.

Akiongea na katika mkutano wa Sochi, rais Putin alisema " Iran na Korea ya Kaskazini zinatumiwa na Marekani kama kigezo cha kuwekwa mitambo ya kijeshi barani Ulaya. Lakini nia yake ni kujaribu kupunguza dhamira ya Urusi ya kuwekeza nguvu zake za kijeshi.

" Hivyo napenda kuwahakikishia kuwa Urusi haitakubaliana na kitendo hicho, na kwa sasa tunatengeneza siraha ambazo zitaweza kukabiriana na siraha hizo za Kimarekani." Alisisitiza raia Putin.

Mvutano wa kijeshi kati ya Urusi na Marekani, umekuwa wa muda sasa, tangu Marekani ilipo pendekeza kuweka mitambo yake ta Kijeshi barani Ulaya kwa madai kuwa ni kwa ajili ya ulinzi wa NATO jambo ambalo Urusi inalipinga.