Nyota ya sinema ya big mama, atimiza miaka 43 ya kuzaliwa.
Holly Wood, Los Angels - Masani maarufu duniani Lawrance Martin, leo ametimiza miaka 43 tangu kulzaliwa.
Martin Lawrance, ambaye alizaliwa tarehe 16/4/1965, nchini Ujerumani Frankfrut,ametokea kuwa msanii maarufu ambaye amecheza sinema nyingi, na vilele amecheza sinema na wasanii kama,Willy Smith na wasinii wengi duniani anasifika kwa kuchekesha saana hasa hawapo jukwaani.
Pichani anaonekana akiwa anafanya vitu vyake kwenye sinema ya big momma.
Picha nyingine anaoneka,Martin Lawrence,akiwasalimia baadhi ya washabiki wake.
Hapo juu anaonekan Martin Lawrence, akiwa ametana shati.
Vatican haitaruhusu vitendo vingine vya aibu kutokea"Pope"
New York, Amerika - Pope Benedict, amewasili nchini Amerika kwa ziara rasmi,ili kuimarisha uhusiano kati ya serikali ya Amerika na Vatikani.
Kufanyika kwa ziara hii ya Pope Benedict kumetonesha donda kwa baadhi ya watu ambao, wanadai yakuwa,baadhi ya watumishi wa kanisa hili la Katoliki kutuhumiwa kuwalawiti baadhi ya waumini wao.
Pope Benedict , alihaidi atahakikisha ya kuwa Vaticani haita ruhusu tena hali hii kutokea.
Hata hivyo,Pope Benedict, atarajiwa kuzungumzia swala hili na swala la Iraki,pindipo watakapo kutana na rais wa Amerika bwana George Bush.
Na wakati huo huo, Pope Benedict, atasherekea siku yake ya kuzaliwa kwenywe Ikuru ya Amerika, sherehe hizi zimeandaliwa na George Bush,na inatarajiwa kuhudhuriwa na watu wasiopungua 9,000
Picha anaonekana,Pope Benedict, akisalimia baadhi ya waumini waliokuja kuudhulia misa hivi karibuni.
Chini ni picha za Pope Benedict tangu alipo kuwa kijana na mpaka anatimiza miaka mwaka 81 leo.
Urusi yataka zidi kutanua misuri yake, Georgia yawa na homa.
Moscow, Urusi - Serilakai ya Urusi imetangaza ya kuwa itaanzisha uhusiano na majimbo ya Kusini mwa Ossetai ,na Abkhazia, yaliyopo Georgia.
Uhusiano huu na majimbo haya utakuwa wa kiuchuni, kijamii na pamoja na kisayansi mbinu.
Hata hivyo serikali ya Georgia, imesikitishwa na kitendo hicho, kwani imedai inakwenda kinyume cha sheria za kimataifa alisema waziri wa mambo ya nje ya Georgia bwana David Bakradze.
Pichani zinaonekana baadhi ya nguvu za serikali ya Urusi, zikionekana amabzo zinaipa homa nchi ya Georgia.
Hapa anaonekana rais wa Georgia,ametangaza ya kuwa atahakikisha yakuwa hali hii aita endelea.
Tuache kutumia pesa za Amerika, US dollar, tuanzishe benki zetu,
Teheran,Irani - Rais wa Iran, bwana Mohmoud Ahamadinejad amewataka wanachama wa OPEC, waache kutumia ($dollar), pesa inayo tumika nchini Amerika katika kufanya biashara.
Akiongezea, ameagiza ya kuwa lazima waanzishe benki itakayo milikiwa na wanachama na pesa zao.
Mvutano kati ya serikali ya Iran na Amerika umekuwa wamuda mrefu, na Iran kuungana na baadhi ya nchi kama, Venezuela, na Syiria,zinazo pingana na sera za serikali ya Amerika.
Wakati huo huo, serikali ya China imaeanza mazungumzo na serikali ya Irani na kwa kuongoza mazungumzo kuhusu swala zima la kuwepo kwa nyuklia na mitambo yake nchini Irani.
Mazungumzo haya yamekuja , baada ya serikali ya Iran kutangaza ya kuwa imewekeza zaidi viini vya nyuklia vipatavyo 6,000.
China ni nchi ambayo inafanya biashara na Iran, japo baadhi ya nchi za magharibi zimeweka vikwazo kwa serikali ya Irani.
Baadhi ya wananchi wa Irani wakiwa wameshikilia bango lenye picha za maris ambao wanapinga sera za nje za serikali ya Amerika.
Pichani hapo juu, wanaonekana marais wa Venezuela bwana Hugo Chavez na Iran bwana Mahmoud Ahamadinejad wakionyesha ushirikiano wao ulivyo komaa.
Picha nyingine wanaonekana rais wa Syiria bwana, Bashar al Assad na rais wa Irani, Mohamoud Ahamadnejad walipokutana hivi karibuni.
Picha nyingine wanaokena baadhi ya wajumbe wa serikali ya China na Iran walipo tia saini baadhi ya mikataba ya kibiashara hivi karibuni.
Ajali ya ndege, nchini Jamuhuri ya Kongo, yaleta wasiwasi kuhusu ubora wa ndege .
Goma, Jamuhuri ya Kongo - Serikali ya Jamuhuri ya Kongo, imetangaza ya kuwa ajali ya ndege iliyo tokea mjini Goma,imesababisha zaidi vifo vya watu wasiopungua 40 kupoteza maisha yao.
Ndege hiyo ambayo inasemekana ya kuwa ilipata itilafu kwenya tairi lake moja, ambolo inaaminika ndiyo chamzo cha ajalihiyo.
Kutokana na ajari hii, kutokea hivi karibuni, kuna leta wasiwasi kuhusu hali nzima ya usalama wa ndege hizi, kwani kampuni inayo miliki ndege hizi ijulikanayo kama Hewa Bora, ni moja ya kampuni ambayo imefungiwa na mashirika ya kimataifa kwa ndege zake kutumika kwenye anga za kimataifa.
Pichani hapo juu wanaonekana baadhi wenye huruma wakiwa katika harakati za kuwaokoa watu ambao wamo ndani ya ndege hii iliyo pata ajali.
Picha nyingine, inaonekana sehemu ya ndege hii ambayo imepata ajali, na kuuwa zaidi ya watu wasiopungua 40.