Wednesday, March 30, 2011

Rais wa Syria ahutubia wananchi baada ya maandamano.

Rais wa Syria ahutubia na wanachi baada ya maandamano. Syria, Damascus - 30/03/2011. Rais wa Syria amelihutubia taifa siku kadhaa baada maandamano yaliyo fanyika nchini humo kutaka mageuzi.

Akiongea kupitia runinga na mbele ya bunge rais Bashar al Asad alianza kwa kusemasema " mimi ni Msyria na yoyote ambaye ni Msyria atakuwa anajidai kwa kutembea kifua mbela."
Najua Wasyria walikuwa wanasubiri maoni yangu, lakini ulinibidi nisubiri ili nipate picha kamili na huhakika wa hali halisi ili kuto wapa maadui wa Syria kutokana na hali iliyokuwawakati huo."
Naomba niwaeleze Wasyria wenzangu lazima tuwe na umoja na tutatue tofauti zetu bila magomvi na tuta shinda mbinu zinazo tumiwa na vyombo vya habari ambavyo vinatumika kudanganya dunia kuhusu hali ya nchi yetu."
Rais Al-Asad alikuwa akihutubia ili kuelezea ni kwa jinsi gani uongozi wake unavyo kabiriana na mageuzi yanato likumba bara la Waarabu.

Tuesday, March 29, 2011

Viongozi wakutana kujadili hali halisi ya Libya.

Viongozi wakutana kujadili hali halisi ya Libya.

London, Uingereza - 29/03/2011. Viongozi wa nchi za jumuia ya NATO na washiriki wake wanakutana jijini London ili kujadili hali halisi nchini Libya.
Akifungua mkutano huo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon alisema " tumekutana hapa ili kusaidia nia ya watu wa Libya na ambao wanataka kujenga nchi yao bila vitisho na kuhakikisha lengo lao linafanikiwa."
Mkutano huo ambao utakuwa na lengo la kupanga na tutathmini hali ya kisiasa nchini humo pindipo mageuzi ya takapo fanikiwa nchini Libya.

Friday, March 25, 2011

NATO kuongoza mapambano zidi ya Libya.

NATO kuongoza mapambano zidi ya Libya.

Brussels,Ubeligiji - 25/03/2011. Jumuia ya ulinzi na shirikisho la kijeshi la nchi wanachama wa
NATO zimekubaliana kuchukua majukumu na kuongoza vita zidi ya kiongozi wa Libya.
Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen aliongea na waandishi wa habari baada ya kikao cha viongozi hao kuamua kuchukua jukumu hilo kutoka kwa serikali ya Amerika.
Anders Fogh Rasmussen alisema " NATO itachukuwa majukumu yote ya kuhakikisha ya kuwa amri iliyo wekwa na umoja wa mataifa ya kumzuia kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kutumia jeshi la anga katika mashabulizi zidi ya wapinzani wake."
NATO ilianza mashabulizi nchi Libya baada ya kamati ya usalama ya umoja wa mataifa kupiga kura kumzuai kiongozi wa Libya kutumia jeshi la anga.
Wimbi la mageuzi ya kisiasa la aanza nchini Syria.
Daraa, Syria - 25/03/2011. Maafias wa usalama nchini Syria wamewashambulia waandamanaji ambao wanataka serikali ifanya mageuzi ya kisiasa.
Waandamanaji hao ambao waliandamana katika mji wa Daraa, walikutana na police na maafisa usalama wakati wakiwa njiani kuelekea kwenye ofosi za serikali.
Rais wa Syria Bashar al Assad ametangaza kuachiwa kwa wale wote walio kamatwa.
Maandamano yanayofanyikannchini Syria ni moja ya wimbi la mageuzi ambayo yana vuma katika bara la Kiarabu na nchi za Kiarabu pia.

Wednesday, March 23, 2011

Jerusalem ya kutwa na mlipuko wa bomu.

Jerusalemu ya kutwa na mlipuko wa bomu.

Jerusalem, Izrael 23/03/2011. Mlipuko wa bomu umetokea katika jiji la Jerusalem kwenye maeneo ya al Quads.
Msemaji wa polisi alisema " mlipuko huo ulisababishwa na bomu lenye uzito wa kati ya kili 1-2 na ulipakiwa katika sanduku dogo."
Mlipuko huo umesababisha watu wapatao 30 kujeruhiwa na mtu mmoja kupoteza maisha.
Waziri mkuu wa Benyamin Netanyahu amelaani kitendo hicho na kukatiza safari yake ya kiserikali nchini Urussi.

Monday, March 21, 2011

Vladmil Putin alaani mashambulizi zidi ya LIbya.

Vladmil Putin alaani mashambulizi zidi ya Libya. Moscow, Urussi 21/03/2011. Waziri mkuu wa Urussi amezilaumu nchi za magharibi kwa kitendo chake cha kuishambulia Libya.

Vladamil Putin alisema " mashambulizi yanayo endelea nchini Libya ni ya kishetani na Amerika na washiriki wake wanafanya mashambulizi bila hata kufikilia mbele."
Na hii inaashiria ya kuwa lazima tuongeze uwezo wetu wa kijeshi ili kuendana na hali ahalisi."
Wakati huo huo, mtoto wa kiongozi wa Libya Saif al Gaddafi amesema "rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy anatakiwa kurudisha pesa zote ambazo serikali ya Libya ilimsaidia wakati wa kampeni zake za Urais, kwani malipo yake ni kuongoza na kuwa kinara wa kutushambulia kivita na kusahahu misaada yote na tunao ushahidi."
Hata hivyo msemaji wa rais Nikolas Sarkozy amekanusha maelezo hayo yaliyo tolewa na mtoto wa Muammar Gaddafi.

Sunday, March 20, 2011

Mashambulizi nchini Libya ya zidi kupamba moto.

Mashambulizi nchini Libya ya zidi kupamba moto.

Paris, Ufaransa - 20/03/20. Jeshi la Ufaransa kwa kushirikiana na washiriki wake wanaenedelea na mashambulizi kwa kutumia jeshi la anga ilikuzuia jeshi la Muammar Gaddafi.
Mashambulizi hayo ambayo yameshachukua siku mbili yameanza kuchukupicha tofauti baada ya maafa kutokea na kuleta hisia tofauti.
Akiongea kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alisema " vita vilivyo anzishwa na nchi za Magharibi na washirika wake vitakuwa na maafa makubwa kwa jamii nzima ya kimataifa na itachukua muda mrefu kuliko walivyo dhania."
Mmoja wa mkuu wa jeshi la Amerika Admiral Mike Mullen amesema "mashambulizi nchini Libya hayana maana ya kumtoa madarakani kiongozi wa nchi hiyo."
Wakati huo huo jumuia ya nchi za Kiarabu imelaumu mashambulizi yaliyo fanywa na Ufaransa na washiriki wake, akiongea katibu mkuu wa jumuia hiyo Amr Mussa alisema "majeshi ya Ufaransa na washiriki wake yanafanya kinyume na makubaliano ambayo ni kulizuia jeshi la Libya lisitumie jeshi la anga, lakini sasa mashambulizi yanaelekea kuleta maafa kwa raia."
Mashambulizi nchini Libya yameanza baada ya Umoja wa matifa kupigakura na kukubali kuingilia kati matatizo ya wenyewe kwa wenye kati ya watu wanaomuunga mkono Muammar Gaddafi na ya wapinzani wake.

Monday, March 14, 2011

Saudu na washirki wake wavamia Bahrain.

Saudia na washiriki wake wavamia Bahrain.

Manama, Bahrain - 14/03/2011. Mamia ya wanajeshi na askari wa nchi jumuia Gulfu wameingia nchini Bahrain ilikusaidia serikali ya nchi hiyo.
Uamuzi huo wa jumuia ya nchi za Gulfu ulikuja baada ya serikali ya Bahrain kuomba msaada ili kupambana na waandamanaji ambao wanataka mageuzi ya kisiasa.
Uamuzi huo wa kuvamia Bahrain umelaumiwa na wanasiasa na shirika la kutetea haki za binandamu na kutaka umoja wa matifa uingilie kati.
Japan yakumbwa na tetemeko la ardhi na tsunami.
Tokyo, Japan 14/03/2011. Wanachi wa Japan wapo katika hali mshtuko baada ya tetemeko la ardhi kutokea na kusababisha tsunami.
Tsunami hiyo ilisababisha maafa makubwa na inasadikiwa watu wapatao elfu kumi na tano wamepoteza maisha yao kwa kuzingatia huaribifu uliofanywa na tsunami kuvamia na kuaribu makazi ya watu na kuleta hasara ya zidi ya mabilion ya pesa.
Kufuatia tsunami hiyo ambayo ilisababisha milipuko katika visima vya mitambo ya nyuklia.

Thursday, March 10, 2011

Dalai Lama kuachia madaraka hivi karibuni.

Dalai Lama kuachia madaraka hivi karibuni. Dharamshala,India - 10/03/2011.Kiongozi wa kiimani ambaye ni mzaliwa wa himaya za Tibeti ametangaza atajiudhulu maswala yote ya kisiasa.

Dalai Lama, ambaye amekuwa kiongozi wa wananchi wa Himaya za Tibeti alitangaza habari hizo kwa kusema" nafikili umefika wakati wa kumchagua kiongozi mwingine atakaye waongoza wana Tibeti na umefika wakati wa kutoa nafasi hiyo."
Dalai Lama ambaye anaishi ugenini nchini India baada ya kukumbi kutoka himaya za Tibet baada ya mapinduzi kushindwa zidi ya serikali ya China mnamo miaka ya mwisho ya hamsini.
Ufansa yaitambua serikali ya wapinzani wa Muammar Gaddafi.
Paris, Ufaransa - 10/03/2011. Serikali ya Ufaransa imekuwa nchi ya kwanza kuitambua serikali ya upinzani inayo mpinga kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Akiongea mbele ya ujumbe na viongozi wa upinzani rais wa Ufaransa Nicolas Sozy alisema " tunaelewa umuhimu wa kuwaunga mkono watu wa Libya."
Uamuzi huo wa Ufaansa umekuja baada ya Amerika, na washiriki wake kutaka kuwepo na uzuizi wa anga ili kumdhibiti kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kutumia anga katika mashambulizi zidi ya wapinzani wa serikali.

Saturday, March 5, 2011

Waganda waombeleza kutokwa na kiongozi wao.

Waganda waombeleza kutokwa na kiongozi wao

Kampala Uganda - 05/03/2011. Aliye kuwa rais wa Uganda kwa muda wa siku tatu amefariki dunia baada ya kuungua kwa muda mfupi.
Walter Ochora Odoch ambaye alikuwa mmoja wa wamajeshi walio ongoza mapinduzi ya kumng'oa madarakani hayati rais wa Uganda Milton Obote.
Akiwa na cheo cha Kanal, Walter Ochora alikuwa kiongozi wa mstari wa mbele kuleta amani katika maeneo ya kaskazini mwa Uganda na hasa aliopo ongozi katika mazungumzo na mpinzani wa serikali ya Uganda Joseph Kony
Marehemu Walter Ochora ameshe wahi kushika nyazifa mbalimbali za serikali enzi za uhai wake.
Jeshi la serikali la Libya kuanza mashambulizi zidi ya wapinzani.
Tripol, Libya - 05/03/2011. Jeshi la serikali ya Libya limeanza mashambulizi zidi ya makundi ya wapinzani ambayo yanapinga serikali.
Mapigano ya kuipinga serikali ya Libya inayo ongozwa na Muammar Gaddafi yalianza mara baada ya kiongozi huyo kukutaa kutoka madarakani.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema " jeshi linalo muunga mkono Muammar Gaddafi limefanikiwa kukamata baadhi ya maaeneo ambayo yalikuwa mikononi mwa makundi ya upinzani.
Chamzo cha kutaka mapinduzi dhizi ya serikali ya Libya yalianzia katika mji wa Benghazi na kuenea sehemu tofauti nchini LIbya.