Iran yatungua ndege aina ya drone ya Izrael
Tehran, Iran - 25/08/2014. Serikali ya Iran imetangaza kuwa imeangusha ndege inayo endeshwa kwa mtandao ''Drone'' ambayo ilikuwa imengia kwenye anga la Iran.
Akiongea kuhusu kuangashwa kwa ndege hiyo aina ya drone, Brigedia General Ramezan Sharif alisema '' Drone tuliyo iangusha inauwezo wa kuzunguka mduara wa kilomita 800 na kuruka urefu wa km 1,600 kutoka usawa wa bahari.''
''Hii drone tuliyo iangusha ni kutoka Izrael, naikikuwa inaelekea kwenye eneo la mitambo lenye mitambo ya kinyuklia ya Natanz, na bado tunaendelea kuchunguza zaidi nini kilichopo katika drone hii tuliyo idondosha.''
Kutunguliwa kwa drone ya Izreal nchini Iran, kumechukuliwa kama kitendo cha hatari kwa Iran, kwani Izrael ilisha dai kuwa ikibidi itafanya mashambulizi katika kituo cha mitambo ya kinyuklia cha Natanz.
Uturuki na Ujerumani za vutana juu ya ukachero.
Ankara, Uturuki - 25/08/2014. Serikali ya Uturuki, imeshutumu serikali ya Ujerumani, kwa kitendo cha kukachero mienendo ya serikali ya Uturuki kwa muda miaka 38.
Shutuma hizo zimetolewa kwa mara ya pili, baada ya zile za mwanzo zilizo lipotiwa na gazeti la Ujerumani la Der Spiege, ambalo August 17, liliripoti kuwa '' Ujerumani imekuwa ikikachero nchi ya Uturuki kwa niaba ya nchi za NATO.''
Akiongela suala hili, waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki Efkan Ala,alisema hiki kitendo cha ukachero ni cha hatari kati ya nchi marafiki
Hata hivyo habari zilizo toka ofisi ya mambo ya ndani ya Uturuki ziliasema ''kitengo cha usalama BND kimekuwa kikifanya shughuli ya ukachero zidi ya Uturuki tangu mwaka 1976, baada ya kuidhinishwa na aaliyekuwa Kansela wa Ujerumani Helmut Schmidt, ambaye alikuwa kiongozi wa SD - Social Demokratiki.''
Hata hivyo, serikali ya Ujerumani, hakuelezea kuhusu shutuma hizo za kutoka serikali ya Utiruki, bali msemaji wa serikali alisema '' Uturuki ni nchi mwana chama wa NATO, na nchi rafiki wa Ujerumani hii ndivyo mahusiano yaliyopo kati ya nchi hizi mbili.''
Nchini Ujerumani kuna watu zaidi ya millioni 3 wenye asili ya kutoka Uturuki, ambapo umekuwa ndiyo kiungo cha nchi hizi mbili kuwa na ukaribu kwa sana.
Urusi kupeleka tena misaada ya kiutu nchini Ukraine.
Moscow, Urusi - 25/08/2014. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi, ametangaza kuwa, nchi yake itapeleka misaada kwa mara nyingine nchi Ukraini, na kuzitaka nchi nyingine kuunga mkono jitihada hizo za Urusi.
Waziri Sergey Lavrov,aliyasema hayo wakati alipo kuwa akiongelea hali halisi ilivyo nchini Ukraine kwa kusema '' sisi tutaendelea kutoa misaada kwa watu wanao hitaji misaada, hiyo kwani hali iliyopo katika maeneo yaliyo shambuliwa na yanayo zidi kushambuliwa na jeshi la serikali ni mbaya sana.''
''Na msafara wa pili wa misaada unatarajiwa kuondoka wiki hii kwa kupitia njia ile ya mwanza, na tunaomba ushirikiano na kutoka kwa serikali ya Ukraine, kwani serikali ya Ukraine imefunga na kuzuia huduma zote za kibinadamu, jambo ambalo ni kinyume za haki za binadamu.'' Aliongezea waziri Lavrov
Ni wiki sasa, tangu Urusi ilipo iliamua kuingiza misaada nchini Ukraine, bila ruhusa kutoka kwa serikali ya Ukraine, jambo ambalo lililalamikiwa na washiriki wanao unga mkono serikali ya Kiev, lakini Urusi ilisisitiza kuwa ilikuwa inafanya hivyo kwa nia ya kusaidia watu waliokumbwa na maafa ya vita vya wenye kwa wenye vinavyo endelea nchini Ukraini.