Sunday, November 24, 2013

Mabaki ya mwanzilishi wa Kanisa Katoliki dunia yaonyeshwa.


Mabaki ya mwanzilishi wa Kanisa Katoliki dunia yaonyeshwa.


Vatican City, Vatican - 24/11/2013. Waumini wa Kanisa Katoliki duniani wameonyeshwa kwa mara ya kwanza mabaki  ya aliyekuwa mwanzilishi wa kanisa Katoliki Mtakatifu  Peter.

Mabaki hayo ya Mtakatifu Peter, yalionyeshwa kwa waumini hao huku yakiwa yamewekwa katika kisanduku katika misa  iliyo ongozwa na Papa Fransisco.

Kuonyeshwa kwa mabaki hayo kwa waumini wa Kikristu na hasa kwa waumini wa kanisa Katoliki inaaminika kutaongeza kukuza imani ya waumini wa kanisa la Katoliki, hasa baada ya kukubwa na  mikasa na utovu wa nidhamu ya kimaadili kwa wafanyakazi na wahudumu wa kanisa hilo katika sehemu tofauti duniani

Iran yafikia makubaliano na 5+1 juu ya Nyuklia.

Geneva, Uswis - 24/11/2013. Nchi 5+1 ambazo ni Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa,  China na Urusi, zimefikia makubaliano na Iran  kwa mara ya kwanza tangu kuanza mazungumzo kwa miaka kumi iliyo pita.

Katika makubaliano hayo Iran imekubali kusimamisha baadhi ya mikakati yake ya kuendelea kuzalisha madini ya kinyuklia na badala yake itapewa  kiasi cha $ dola za Kimarekani 7 billion ikiwa ni moja ya afuheni katika vikwazo ambavyo Iran ilikuwa imewekewa na jumuiya ya kimataifa kutokana na mpango wake wa kuzalisha madini ya kinyuklia ambao unashukiwa huenda yakatuka  katika kuunda siraha za sumu.


Akongea baada ya makubaliano hayo, rais wa Iran Hassan Rouhani amesema " hii ni historia na kwa wale ambao walikuwa wana nia tofauti na Iran, sasa watafahamu ya kuwa Iran inahaki ya kuuendelea na mpango wake wa amani wa kuzalisha nyuklia kwa matumizi ya  kisayansi na kijamii."


Kwenye makubaliano hayo ni kwamba Iran imekubali "kutokuzalisha madini ya Uraniam kupita kiasi cha asilimia 5% na kutoa ruhusa ya wakaguzi kutembelea na kukagua katika viwanda vya kufulia madini ya kinyuklia katika miji ya Natanz, Fordo na hakutakuwa na uendelevu wa uzalishaji wa na ufuaji wa madini ya kinyuklia katika kiwanda cha Arak."

Hata hivyo serikali ya Izrael haikupendezwa na makubaliano hayo na  waziri mkuu wa Benyamin Netanyahu amesema ya kuwa " kitendo cha kufikia makubaliano na Iran ni makosa ya kihistoria na Izrael haina imani na Iran, kwani tangu mwanzo Iran Ilisha sema yakuwa inataka kuifuta Izrael katika ramani ya dunia."

Makubaliano hayo hayataifanya Iran kusimamisha mpango wake wa kuzalisha nyuklia ambao imekuwa ikipigania toka kuanza kwa mazungumzo miaka kumi iliyo pita na vile vile makubaliano hayo yatakuwa katika mtazamo katika kipindi cha miezi sita kuanzia sasa.

Saturday, November 23, 2013

Mwili wa mwanzilishi wa Kanisa la Kikrisu Duniani kuonyeshwa hadharani.

Siri za Majasusi  wa kimataifa wa  za zidi fichuliwa.

Moscow, Urusi - 23/11/2013. Mashirika ya kijasusi ya Kimarekani na washiriki wake wamewekwa wazi tena na habari ambazo zimetolewa wiki hii katika mlolongo wa kufichuliwa  habari za siri na aliye kuwa mfanyakazi wa shirika la kijasusi la Marekani CIA na NSA.


Katika habari hizo ambazo zina kurasa tano, zimeonyesha nia ya mashika ya kijasusi ya Marekani na washiriki wake ya kuwa  yalikuwa na mpango endelevu wa kuendelea kuchunguza na kurekodi habari na nyendo za watu kwa muda mrefu zaidi.


Kurasa tano ambazo zipo mikononi mwa  gazeti la New York Times na kuthibitishwa na gazeti hilo zimesema " Makampuni hayo ya kijasusi yalikuwa na mpango wa kumrekodi, kumchunguza na kumfuatilia kila mtu mahali alipo na kwa muda wowote na hii ni kwa mujibu wa nyaraka za mwaka 2012."


"Habari hizi ambazo ni moja ya mikakati ya  mashika ya kijasusi kwa kuitwa PRISM na kueleza mpango wa miaka minne  2012 - 2016 wa NSA na kuita SIGNINT kwa jina na kiupelelezi."


Edward Snowden ambaye ndiye mwanzilishi wa mlolongo mzima wa kufichuliwa kwa siri za mashirika ya kijasusi ya Marekani na washiriki wake, umekuwa ikileta mtafaruku katika jamii ya kimataifa  na kukuza kutokuamniana katika jamii ya kijasusi ya kimataifa na kusababisha wakuu wa mashirika ya kijasusi kutoa maelezo ya kujitete kwa jamii za kimataifa ili kuweza kuimarisha na kurudisha imani kwa jamii nzima ya kimataifa.


Mwili wa mwanzilishi wa Kanisa la Kikrisu kuonyeshwa hadharani.

Rome, Itali -23/11/2013. Kanisa Katoliki duniani limepanga kuionyesha kwa waumini wa dhehebu la Katoliki dunia mabaki ya mifupa ya Mtakatifu Peter, ambaye inaaminika ndiye mwanzilishi wa Kanisa la Kikristu.

Aliongea kabla ya kuonyeshwa kwa mabaki hayo ya Mtakatifu Peter, Askofu Rino Fisichelle amesema " kitendo hiki kitakuwa ni kitendo cha kitamaduni na cha asili ya Kikanisa  katika kuonyesha uhalisia wa wale wote walio toa misha yao kwa ajili ya kumumika Mungu."


Inaaminika ya kuwa Mtakatifu Peter aliuwawa baada ya kutundikwa kichwa chini miguu juu jijini Roma mwaka wa 64 baada ya  Kristu na kuzikwa katika  mjini Rome na baadaye  Mfalme  Constantine kujengea hekalu mahali alipo zikwa katika karne ya (4) nne.

Kanisa Katoliki chini ya uongozi wa Papa Fransisco limekuwa likijitahidi kufanya mabadiriko ili kuweza kurudisha imani  kwa waumini wa Kikristu na hasa kwa Wakatoliki duniani , na hii inatokana na kupungua kwa waumini waendao makanisani  baada ya imani  kupungua kwa baadhi ya waumini wa Kikristu.


Mabaki hayo ya mifupa ya Mtakatifu Peter, yamekuwa ni kitendawili kwa muda mrefu na hivyo kitendo cha Kanisa kuamua  kuonyesha mabaki hayo ikiwa ni ishara na nia ya kukuza imani ya waimini ya wa Kikristu ambayo kwa sasa imekuwa inakubwa misuko suko kutokana na baadhi ya watumishi wa Kanisa hilo  kukumbwa na kashfa ya kuvunja maadili ya Kikristu katika jamii.

Hali ya Nelson Mandela kiafya njia panda.

Johannesburg, Afrika ya Kusini - 23/11/2013. Rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini na mpigania uhuru wa Afrika ya kusini, bado yupo katika hali tete kiafya.
Nelson Mandela ambaye  yupo katika matbabu na hadi sasa hawezi kuongea na anawasiliana kwa kutumia ishara.

Akiongea na waandishi wa habari, Winnie Madigizela Mandela alisema " Hali ya Nelson Mandela ni tete, na  pale alipo nyumbani kwenye kitanda ni sehemu ambayo tunaweza kuita kama ICU ( Chumba cha wagonjwa wadharula na uangalizi wa hali ya juu) na mipira ambayo amewekewa kusaidia kusafisha mapafu inasaidi kutopa magojwa mengine kirahisi na anaendelea kupata hauheni kila kukicha."

Nelson Mandela 95, alilazwa  June 8  kwa ugonjwa wa mapafu na amekuwa anaumwa kwa muda mrefu na kwa sasa yupo nyumbani kwake Houghton moja ya kitongoji kilichopo katika jiji la Johannesburg.

Mandela ambaye alikuwa amefungwa jela miaka 27 na serikali ya kikaburu na kuachiwa mwaka 1990 na 1994 kuchaguliwa kuwa rais wa kwanza mzawa wa Afrika ya Kusini  chini ya chama cha ANC (African Nation Congres) had alipomaliza kipindi chake mwaka 1999.

Ujerumani yadai bado kazi ngumu kuhusu Iran na  nyuklia.



Berlin, Ujerumani - 23/11/2013.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani amesema kuwa  mazungumzo ya kidiplomasia kati ya Iran na jumuiya ya Ulaya na washiriki wake kuhusu mpango wa kuendelea na uzalishaji wa kinyuklia ambayo jumuiya ya kimataifa inautilia wasiwasi.

Waziri Guido Westerwelle alisema " Kunauwezekano makubaliano yakafikiwa, lakini kazi ya ziada inatakiwa kufanyika".

Mazungumzo kati ya Irani na mpango wake wa  kuendeleza uzalishaji wa kinyuklia na jumuiya ya kimataifa umekuwa ukileta vichwa kuuma  kwa jumuiya ya kimataifa, kwani tangu mazungumzo hayo kuanza hayajawahi kuleta jibu kamili au kufikia muafaka.

Rais wa Nigeria apata nafuu.



London. Uingereza- 23/11/2013 Rais wa Nigeria anaendelea kupata nafuu baaada ya kulazwa hospital jijini  London.
Rais Goodluck Jonathan 56, alilazwa baada ya kuzidiwa wakati alipokuwa akijiindaa kuudhuria mkutano wa  kamati ya wakuu wa kiuchumi ambao alitakiwa kuwepo kwenye mkutano huo tangu siku ya Jumatano.

Akiongea katika mkutano wa kuvutia  wawekeshaji, rais Jonathan  alisema " kwanza napenda kuomba kuwaomba radhi kwa kushindwa kuudhuria mkutano huu tangu kwanza, na ningependa kuwahakikishia yakuwa Nigeria chini ya uongozi wangu tumeweka mikakati na mipango madhubuti ambayo itarahisisha wawekezaji kuweza kuwekeza kwa unafuu."

Hii ni mara ya kwanza kwa rais Jonathan kuuugua na kushindwa kuudhuria mkutano wa kimataifa, na itakumbukwa kuwa Goodluck Jonathan alishinda uchaguzi wa urais mwaka 2011 na kuapa kuiongoza Nigeria nchi ambayo ina utajiri mwingi wa malighafi mafuta ambayo ni moja ya kitega uchumi cha nchi ya Nigeria.