Wednesday, June 23, 2010

Rasi Obama amteua mkuu wa majeshi mpya kuongoza NATO

Rais Obama amteua mkuu wa majeshi mpya kuongoza NATO.

Washington,USA - 23/06/2010. Rais wa Amerika Baraka Obama, ametangaza kujiudhulu kwa General Stanley McChrystal kuwa kiongozi mkuu wa majeshi ya NATO na kumteua General David Petraeus kuchukua nafasi yake.
Kutangazwa huko kunakuja baada ya General McChrystal kushutumu uongozi wa serikali ya USA kwa kuwa na myumbo katika kuendeleza vita nchini Afghanistan.
General Mc Chrystal aliyasema hayo wakati alipofanya mazungumzo na mahojiano na gazeti la Rolling Stone.
Rais Baraka Obama, alisema kujiudhuru huko kwa General McChrystal, hakuta badilisha msimamo wa USA nchini Afghanistan kupambana na kundi la Taliban. Picha hapo juu anaonekana General Stanley McChrystal akielekea ofisi za Ikulu ya Amerika kunana na rais Baraka Obama.
Picha ya pili anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama akielekea kutangaza kujiudhulu kwa General Stanley McChrystal, na nyuma anaonekana General David Petraeus akimfata rais kumtangaza rasmi kuwa kiongozi wa majeshi ya NATO.

Meli ya siraha yazuiliwa nchini Sypras.

Meli ya siraha yazuiliwa nchini Sypras. Nikosia,Syipras - 23/06/2010. Serikali ya Syipras imeizuia meli ijulikanayo kama Santiago ambayo inasadikiwa kubeba siraha kuelekea nchini Sudani. Waziri wa biashara Antonis Passchalides alisema, vifaa vilivyopo kwenye meli hii lazima vifanyiwe uhakiki. Uamuzi wa serikali ya Sypras kuzuia meli kufuatia vikwazo vilivyo wekwa zidi ya Sudan. Picha hapo juu inaonekana meli ambayo imezuiliwa nchini Sypras.

Saturday, June 12, 2010

Afrika ya ikaribisha dunia"Soka, Kombe la dunia

Afrika ya ikaribisha dunia "Soka, Kombe la duni."

Johannesburg, Afrika ya Kusini-12/06/2010. Mashindano ya kugombea kombe la dunia la mpira wa miguu yameanza rasmi nchini Afrika ya Kusini.
Mashindano hayo mbayo kwa mara ya kwanza yana fanykia barani Afrika tangi kuanzishwa yarifunguliwa rasmi na raia wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma na kuhudhuliwa na wageni waalikwa wakunchi,viongozi wa bara la Afrika na dunia nzima.
Picha hapo juu wanaonekana wachezaji wa timu ya taifa ya Afrika ya Kusini wakimenyana vikali na timu ya taifa ya Mexico katika mechi ya kwanza ufunguzi wa mashindano la kombe la dunia.
Picha ya pili wanaonekana rais wa FIFA Sept Platt na raia wa Afrika ya Kusini Jakob Zuma wakiwasalimia wananchi mara baada ya ufunguzi wa mashindano ya kombe la dunia.
Picha ya tatu wanaonekana maelfu ya watu walioudhulia kwenye sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia jiji Johannesburg Afrika ya Kusini.
Picha ya nne anaonekana mmoja ya wanachi wa Afrika ya Kusini akiwa ameinyanyua juu bendera ya Afrika ya Kusini nchi ambayo kwa mara ya kwanza imekuwa mwenyeji wa mashindano ya kombe la dunia katika bara la Afrika.
Mchungaji haukumiwa kifungo cha maisha.
Helsink, Finland-13/06/2010. Mahakama nchini Finland imemkuta na hatia Francois Bazaramba kwa kuhusika na mauaji ya kimbari yaliyo tokea nchini Rwanda 1994 na kumuhukumu kifungo cha maisha.
Francoi Bazaramba 59, ambaye alikuwa mchungaji amekutwa na kosa la kushirikiana watu wa jamii ya Kihutu katika mauaji wakati akiwa kiongozi wa dini.
Hata hivyo Francoi alikanana mashitaka hao, na wakili wake amesema watakata rufaa.
Pichani hapo juu anaonekana Francois Bazaramba akiwa mahakamani akisikiliza hukumu ya kesi yake.

Wednesday, June 9, 2010

Iran yaongezewa vikwazo.

Iran yaongezewa vikwazo.

New-York, Amerika- 09/06/2010. Kamati ya usalama ya umoja wa mataifa imepitisha makubaliano ya kuwekewa vikwazo kwa serikali ya Iran.
Mswaada huo ambao ulipitishwa kwa kura 12 na mbili kupinga mswaada huo na moja kutopiga kura. Nchi ambazo zilipinga mswaada huo ni Brazil na Uturuki nchi ambazo ziliongoza mazungumzo na kuifanya Iran kukubali kuruhusu baadhi ya madini yanayo timika kutumika kuzalisha nguvu za nyuklia.
Hata hivyo serikali ya Iran imekilaani kitendo hicho na kusema, "Hatuta hathirika na vikwazo hivyo kwa kuto kuendelea na mpango wetu wa kuendeleza nyuklia ya kisayansi."
Picha hapo juu wanaonekana wanasayansi wa Iran wakiwa wanajadili maendeleo ya mitambo ya kuzalisha nguvu za nyuklia.
Picha ya pili wanaonekana wajumbe wa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa wakiwa katika mkutano kujadili mswaada wa Iran.

Friday, June 4, 2010

Mafua ya nguruwe yaleta saga WHO

Mafua ya nguruwe yaleta saga WHO. London,Uingereza - 04/06/2010. Gazeti linalo toa ripoti za kiafya za binadamu nchini Uingereza limesama '' kunaukweli ya kuwa wataalamu wa liotoa habari za kuoenea kwa ugonjwa wa mafua ya nguruwe walizidisha vitisho katika kuelezea hatari ya ugonjwa huo.'' Kwa mijibu wa gazeti hilo lilisema ''yakuwa wataalamu hao walikuwa wanahisa katika uuzaji wa madaya ya kutibu na kukinga ugonjwa huo'' Ugonjwa huo unaojulikana kama H1N1 virus ulitishia dunia nzima hata kusababisha baadhi ya nchi kuingiwa na wasiwasi kwatumia pesa zaidi kununu madawa ya kutibu ugonjwa kwa wingi. Kuthibitisha hali hiyo kamati ya kiafya ya Ulaya melilaumu shirika la afya dunia WHO kwa kutofanya uhakiki wa habari wakati zilipo tolewa na wataalamu hao. Picha hapo juu wanaonekana badhi ya watu wakipata chanjo wakati wa kuvuma ugonjwa wa mafua ya nguruwe.

Tuesday, June 1, 2010

Uturuki ya laani vikali kitendo cha Izrael.

Umefikia afrika kuwa na kiti ndani ya UN. Nice,Ufaransa- 01/06/2010. Rais wa Ufaransa Nicalas Sarkozy amesema "umefika wakati wa bara la Afrika kuwa na kiti maalumu katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa." Rais, Sarkozy aliyasema hayo wakati alipo kutana na viongozi wa bara la Afrika kwa kusisitiza ya kuwa "hatuwezi kuongea habari za ulimwengu na dunia bila kuhusisha bara la Afriaka"

Mkutano huo ambao uliitishwa na Ufaransa, na kwa mara ya kwanza ulizishirikisha nchi zilizo kuwa makoloni ya Mwingereza ili kuzidisha uhusiano wa karibu na nchi za bara la Afrika.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi kutoka bara la Afrika pamoja na rais wa Ufaransa, wakati walipomaliza mkutano na serikali ya Ufaransa ili kudumisha uhusiano.
Uturuki ya laani vikali kitendo cha Izrael.
Ankara, Uturuki-01.06/2010. Waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amelaani kitendo cha jeshi la Izrael ni la kinyama na yamefanywa kinyume cha sheria za kimataifa.
Akiongea na viongozi wa serikali na kutangazwa karibu dunia nzima na mashirika tofauti ya habari waziri mkuu huyo alisema, "Asitokee mtu kuijaribu uvumilivu wa Waturuki, kwani tuna heshimu marafiki, na kukosanana na Waturuki ni gharama kwa mtu huyo na hatuacha kuisaidia watu wa Gaza na tutazidi kukemea vitendo vya Izreal."
Waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan, alikatisha ziara yake nchini Chile, mara baada ya tukio hilo kutokea.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, akihutubia kuhusu kitendo cha Waizrael kuvamia msafara wa misaada ya kibinadamu iliyo kuwa ikielekea Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo na majeruhi katika msafara huo.
Picha ya pili anaonekana kijana mdogo akiwa amebebwa kwenye mabega wakati wa harakati ya kupinga kitendo cha Izrael kuvamia meli iliyo kuwa ilielekea Ukanda wa Gaza.
Al-Qaeda namba tatu asadikiwa kuuwawa.
Pakistan, Lahore - 01/06/2010. Jeshi la Amerika na washiriki wake wamesema, "wamefanikiwa kumua anayesadikiwa kuwa namba tatu wa kundi la Al-Qaeda Mustafa Abu al-Yazid au kwa majina mengine Sheikh Sa'íd al Masri."
Kuuwawa huku kwa Mustafa Abu al-Yazid kulitokea kaskazini mashariki mwa Pakistan, kwa shirikiana na majeshi shiriki.
Picha hapo juu anaonekana Mustafa Abu al Yazid, ambaye inasadikiwa aliuwawa wakati wamashambulizi yaliyo fanywa na jeshi la Amerika na washiriki wake hivi karibuni.