Thursday, July 24, 2014

China ya wekeza nchini Kuba kwa vishindo.

Mkuu wa upelelezi enzi ya rais Muammar Gadaffi akataliwa rufaa yake.

Tripo, Libya - 24/07/2014. Mahakama ya kimataifa inayo shughulikia makosa ya jinai na ukiukwajai wa haki za binadamu imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa mkuu wa maswala ya usalama nchini Libya

Abdullah Senoussi ambaye alikuwa mkuu wa maswala ya usalama wakati wa utawala wa rais Muammar gadaffi , alikata rufaa kwa kutaka kesi yake isikilizwe  nchini Uhollanzi katika mji wa Hague kwani  anahofia kuwa mahakama ya Libya haitakuwa na usawa katika uendeshaji wa kwsi nzima kwa kuzingatia kazi aliyokuwa aliifanya.

Katika uamuzi wake huo, mahakama hiyo imesema kuwa " Libya ipo na uwezo wa kuendesha kesi hiyo  baada ya kumaliza kufanya uchunguzi na kwani kesi hiiyo ilisha anzishwa nchini Libya."

Abdullah Sonoussi alishitakiwa mwaka 2011kwa makosa ya mauaji, utesaji na kuhusika katika kupinga kuangushwa kwa serikali ya Muammar Gadaffi 2011. 

China ya wekeza nchini Kuba kwa vishindo.

Havana, Kuba - 24/07/2014.China na Kuba zimesaini mikataba ya kimaendeleo kati ya nchi hizo, kufuatia ziara ya rais wa Chini nchini humo.

Rais Xi Jinping ambaye hii ni ziara yake ya kwanza, tangu kuwa rais wa Chinaa  alikutana na viongozi wa serikali ya Kuba  na kuzungumzia  ni kwa jinsi gani  nchi hizi mbili zitaendelea kudumisha uhusiano.

Ziara hiyo ya rais wa China kwa nchi  Kuba imefanyika, akiwa katika moja ya mpango wa China kutaka kuimarisha uhusiano wakaribu  na nchi zilizopo katika nchi za Karibiani.

Mikataba iliyo sainiwa kati ya  China na Kuba itahusisha sekta ya kilimo ambapo itaghalimu kiasi cha $115 millioni za Kimarekani na pesa nyingine za Kimarekani $600million zitatumika kwa kununulia madini  ya aina ya chuma ya nikele kutoka Kuba na vile vile kujenga bandari nchi Kuba.

 Mikataba ya China na Kuba imekuja siku chache baada ya rais wa Urusi Vladmir Putin kumaliza kufanya ziara nchini Kuba na kusaini mikataba katika sekta tofauti za kiuchumi.


Friday, July 18, 2014

Kuanguka kwa ndege ya Malasyia kwazua msuguano wa kisiasa.

 Kuanguka kwa ndege ya Malasyia kwazua msuguano wa kisiasa.

Moscow, Urusi - 18/07/2014. Waziri wa mambo ya nje wa Urusi, ametahadharisha kuwa hali iliyopo nchi Ukraine kutokana na kuangushwa kwa ndege ya Malasyia, kunaweza sababisha Urusi kuangalia kwa undani nini cha kufanya zidi ya serikali ya Kiev.

Ndege ya Malasyia  boeing 777 iliyokuwa ikitokea Amsterdam kuelekea Malasyia ilitunguliwa na bomu katika jimbo la Donetsk ambalo linashikiliwa na  kundi linalo wapinzani wa serikali ya Kiev, nao ambao wamekanusha kuhusika na kuangushwa kwa ndege hiyo na kudai kuwa ndege hiyo iliangushwa na jeshi la serikali.

Akiongea Lavrov alisema " Ikiwa Kiev haitabadirisha mwenendo wake wa kufanya mashambuli kwenye maeneo ya Urusi, basi Urusi inauwezo wa kushambulia na kuharibu maeno ambayo yanatumika kwa kufanya mashambuli yanayo milikiwa na serikali ya Kiev."

Urusi haina mpango wa kuzuia box linalotumika kwa kuhifadhia habari lilipo  kwa sasa kwenye mikono ya kundi linalo pingana na serikali ya Kiev na wale wote wanao fikiria au kusema hivyo nawashauri wangoje uchunguzi ufanyike kwanza." Aliongezea waziri Lavrov

Hali ya kuvutana kimaneneo imezuka tena upya kutoka nchi za Magharini kwa kusema kuwa "Urusi lazima iwekee mkazo katika suala la amani nchi Ukraine, kwani inauwezo wa kufanya hivyo.


Wednesday, July 16, 2014

Bashar al Assad aapishwa tena kuwa rais wa Syria.

Bashar al Assad aapishwa tena kuwa rais wa Syria.

Dumascus, Syria - 16/07/2014. Wananchi wa Syria wameshuhudia kuapishwa kwa rais Bashar al Assad rais ili kuwa kiongozi wa nchi hiyo.

Rais Bashar al Assad, amechukua madaraka ya urais kwa mara ya tatu baada ya kushinda uchaguzi wa urais, huku wapinzani wake wa ndani na nje ya nchi wakiwa bado vichwa vinawauma jinsi ya kumtoa madarakani.

Akiongea mara baada ya kuapishwa rais Assad alisema " muda si mrefu, mapinduzi halali yatapatikana, na wale wote ambao wanazani kuwa kutumia nguvu ni dawa, basi wajue kuwa haitapita muda watayaona malipo yao."

Kuapishwa kwa rais Bashar al Assad kuridhuriwa na viongozi wa dini zote  waliopo nchi Syria na wageni wengine  rasmi na baadaye kukagua gwaride la heshima.

Rais Bashar al Assad alishinda uchaguzi kwa kupata kura zenye wingi wa asilimia 89 wakati wauchaguzi mkuu uliyofanyika nchi humo 3/June/2014.

Monday, July 14, 2014

Ujerumani ya vunja mwiko na kuwa bingwa wa Dunia wa mchezo wa soka.

Vita ukanda wa Gaza hatari kwa afya ya baaadaye.

Gaza, Palestina - 14/07/2014. Mapigano yanayo endelea kati ya jeshi la Izrael na kundi la Hamas la Kipalestina yametakiwa yasimamishwe mara moja kwani mesababisha maafa  na uharibufu wa mali kwa pande zote mbili.

 Akiongelea hali halisi inayosababishwa na mapigano hayo, muuguzi kutoka Norway  Dr Erick Fosse ambaye yupo katika mji wa Gaza amesema " siraha zinazo tumika zinahathari kubwa kwani madini yaliyo tumika kutengenezea siraha hizo huwa yanasababisha ugonjwa wa saratani ( kansa)."

"Na madhara yake yatakuwa ni kwa kizazi kijacho" Aliongezea Dr  Fosse.

Mauaji na uharibifu wa mali ambao unazidi kutokea kwa pande zote mbili, huku uongozi wa Izrael ukidai ni kulinda nchi yao dhizi ya ugaidi na huku makundi ya Kipalestina yanayo ongozwa na kundi la Hamas kudai kuwa yanatete haki za Wapalestina zidi ya Waizrael ambao wamechukua adhi yao kinguvu,  jambo ambalo hadi sasa jumuiya ya kimataifa imeshindwa kupatia usuruhisho.

 Ujerumani ya vunja mwiko kwa kuwa bingwa wa Dunia wa mchezo wa soka.

Rio de Janeiro, Brazil - 14/07/2013. Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya ujerumani kwa upande wa wanaume, imetwaa kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu Ujerumani mbili kuungana.

Ushindi huo ulikuja katika dakika 113 ya kipindi cha ziada, baada ya dakika 90 za kawaida kuisha bila kuzaa matunda  wakati mchezaji  Mario Gotze alipo tuliza mpira kifuani na kwa ustadi baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa mchezaji mwenzake Andre Schurrle na kuupachika kimiani huku kipa wa Argentina, Romero akiwa anaruka kulia na mpira kumpita kushoto.

 Ushindi huo wa Ujerumani ndani ya bara la Amerika ya Kusini ni wa kwanza kihistoria tangu kuanzishwa kwa kombe la dunia 1930, kwani haijawai kutokea  kwa kombe la dunia kutwaliwa na timu ya bara la Ulaya wakati mwenyeji ni nchi ya Amerika ya Kusini.

 Watu wapatao 74,738 waliokuwapo ndani ya uwanja wa Marakana, hii ikiwemo wakuu wa nchi za BRICS ambao wapo nchi Brazili kikazi.

Wednesday, July 9, 2014

Wakuu wa nchi za BRICS kuanzisha benki ya unafuu.

Wakuu wa nchi za BRICS kuanzisha benki ya unafuu.

Moscow, Urusi - 09/07/2014. Nchi  wanachama wanao julikana kama BRICS zinakaribia kuunda benki yake ili kuepukana mvutano wa kifedha na benki ya dunia na shirika la fedha la kimataifa-IMF katika utoaji wa mikopo na riba.

Benki hiyo itajulikana kama Benki mpya ya Maendeleo ambayo imeundwa kwa nia ya kuwa  na kazi ya kutoa mikopo nafuu na kuunda miradi mbali mbali ya kukuza uchumi kwa nchi masikini.

Akiongea kuhusu kuundwa kwa benki hiyo, waziri wa fedha wa Urusi, Anton Siluanov amesema "Benki itaanzishwa kwa mtaji wa billioni 10 kifedha na 40 billion zitakuwepo kwa dharula, na kila mwanachama wa nchi za BRICS atachangia kiasi sawa kifedha."

"Urusi itachangia 2 billion katika kuimarisha benki hiyo kwa muda wa miaka saba ijayo na benki hii itaanza kazi rasmi ifikapo mwaka 2016."Aliongezea waziri Siluanov.

Mazungumzo ya kuanzishwa kwa benki hii mpya ya nchi za BRICS yamekuja kabla ya kikao cha wakuu wa nchi za BRICS kinacho tarajiwa kufanyika nchini Brazil Julai 15-16.

Nchi za BRICS ni Brazilm India, China na Afrika ya Kusini.

Benki hii pia itaruhusu nchi wanachama wa umoja wa Mataifa kujiunga na hazitaruhusiwa kuwekeza zaidi ya asilimia 45

Kuanzishwa kwa benki ya nchi wanachama wa BRICS, kunatoa changa moto kubwa kwa IMF na benki ya dunia, ambapo zimekuwa zikilaumiwa kwa kuwa hazipo kwa aajili ya nchi masikini na zimekuwa zikiweka masharti magumu kwa nchi inayo taka mkopo toka kwa mashirika hayo ya kifedha. 

Nchini Irak siraha za sumu zaangukia mikononi mwa ISIS.
 
Baghdad, Irak - 09/07/2014. Serikali ya Irak, imetoa taarifa kwa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa kuwa eneo lenye siraha za sumu limetekwa na kundi la ISIS linalo pingana na serikali ya waziri mkuu Nour al Malik.


Ujumbe huo wa serikali ya Irak kwa umoja wa mataifa ulikabidhiwa kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki Moon na balozi wa Irak wa umoja wa mataifa Mohamed Al Alkhakim wenye kuandikwa " eneo lenye kuhifadhi siraha zenye sumu la Muthanna limekuwa chini ya kundi la ISIS tangi Juni 11 mwaka huu."

Siraha hizo zenye sumu, ambazo zilitengenezwa  kabla ya vita vya Gulf vya mwaka 1991 na zinasadikiwa kuwa ni roketi 2,500 ambazo zina sumu aina ya sarin na tani 180 za aina tofauti za siraha za sumu ambazo zikitumika zinaweza kuuwa mamia ya watu kwa kuwa na uwezo wa kuharibu misuri ya ufahamu katika mwili wa binadamu.

Naye aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza  Tony Brair aliyeongoza vita vya kuondoa serikali ya Irak iliyokuwa chini ya rais Saadam Husseini, amemtaka waziri mkuu wa Irak Nour al Maliki kubadili mwenendo wake wa uongozi ama kama hawezi ajiudhuru.

Waziri mkuu wa Irak Nour al Maliki amekuwa akilaumiwa kwa kuwa kinara katika kuongoza mgawanyiko wa Wairak, hasa kimakundi ya kidini ya Shia na Suni.


 


Monday, July 7, 2014

Papa Francis aomba msamaha.

Rais Uhuru Kenyatta kichwa kuuma kwa Raila Odinga  

Nairobi, Kenya - 07/07/2014. Mamia ya watu wameandamana katika jiji la Nairobi, baada ya vyama vya upinzani kuandaa maandamano hayo ili kuishawishi serikali kubadili mwelekeo.

Huku wakiwa wanaimba na kuwa na mabango ambayo yanataka rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kujiudhuru, kwa madai kuwa ameshindwa kuimarisha maisha ya wananchi wa Kenya na pia kuimarisha usalama wao.

Mmoja wa viongozi kutoka kambi ya upinzani na muhusika katika maandalizi ya maandamano hayo Seneta Bonny Khalwale alisema " Leo tuna sema kuwa rais ameshindwa hivyo lazima aondoke madarakanani."

Hata maandamano hayo yalikkwisha salama, na polisni wapatao 15,000 walikuwa katika ulinzi ilikuwa tayari kupambana na watu watakao leta vurugu.

 Hata hivyo kabla ya maandamano hayo, CORD ambacho ni muungano wa vyama pinzani nchini Kenya, wameitaka pia serikali ya Kenya iyaondoe majeshi yake nchini Somali. Baada ya kundi la Al-shabab kuongeza mashambuliz yake tangu majeshi ya Kenya kuingilia kazi vita vinavyo endelea nchini Somalia.

 Naye msemaji wa Raila Odinga ambaye ni mkuuwa vyama vya upinzani amesema kuwa maandamano yaliyofanyika leo ni mwanzo tu, kwani yapo mengi yatafuata.

Raila Odinga ambaye alikuwa waziri mkuu wakati wa serikali ya rais Mwai Kibaki, alirudi hivi karibuni Kenya, baada ya kutokuwepo kwa muda wa nchini Kenya  na kudai anataka kukutana na rais Uhuru Kenyatta ili  wafanye zungumzo yanayo husu usalama wa Kenya.

Papa Francis  aomba msamahaa.

Vatican City, Vatican - 07/07/2014. Mkuu wa kanisa Katoliki dunia amelitaka kanisa kujutia makosa iliyo yafanya na kuwa tayari kujirekebisha.

Papa Francis, aliyasema hayo wakati alipo kutana na watu waliofanyiwa matendo  ya kubakwa kimapenzi na baadhi ya wafanyakazi na wahubiri wa dini hasa kutoka kanisa la Katoliki.

Akisema Papa Francis "Upendo  wa kanisa uliingiliwa na uchafu na sumu ambayo watu ambao walikuwa wanatakiwa kufanya kazi ya kanisa na kuhubiri neno la Mungu wamekuwa wanakwenda kunyume."

"Watu hao walimeli tia sumu kanisa na wanatakiwa watubu."

"Napenda kuomba msaamahaa kwani niaba ya kanisaa, kwani vijana wakiume na wasichana walio  bakwa wakati walikopokuwa na imani na watu wakanisa ili kuwasaidia kiroho na kimahitaji na matokro yake haikuwa hivyo. Hivyo naomba watusamehee."

"Na nahaidi kupambana na wale wote wanao haribu huduma za kanisa kwa jamii."

Papa Francis aliyaongea haya baada ya kukutana na watu waliobakwa na wafanyakazi wa kanisa Katoliki wakati alipo kutana nao mjini Vatican City.

Thursday, July 3, 2014

Kundi la Al Qaeda lawa na mbinu mpya za kupitisha mabomu viwanja vya ndege.

Polisi wa watawanya waandamanaji nchini Afrika ya Kusini.



Pretoria, Afrika ya Kusini - 03/07/2014. Polisi wamepambana na wafanyakazi na wanachama chama cha wafanyakazi wa viwanda vya chuma NUMSA ambao walikuwa wanadai ongezeko la posho.

 NUMSA chama ambacho kinawafanyakazi wanachama  waapatao 220,000 kiliitisha mgomo kwa wafanyakazi wake ilikiwa ni njia ya kushirikiza ombi lao lakutaka kuongezewa posho toka asilimia 12 hadi 15.

Msemaji wa polisi, Ronel Otto alisema "maandamano hayo yanafuata mgomo ambao umechukuliwa na wanachama wa NUMSA, na pia  ilibidi polisi kutumia mbinu za kiulinzi ili kutuliza ghasia baada ya baadhi ya wafanyakazi kuzuia mlango mkuu wa kuingia katika kampuni ya kufua umeme ya Eskom iliyopo Midupi Kaskazini mwa jimbo la Limpompo."

Maandamano na mgomo wa wafanyakazi wa NUMSA  umelalamikiwa na viongozi wa mashirika yanayo husika na zualishaji wa chuma kwa kudai kuwa lika siku Rand 300 millioni zinapotea na hivyo kuwataka wafanyakazi warudi kazini.

Jonh McCain aja na sera mpya ya Irak na Syria.



Arizona, Marekani - 03/07/2014. Mbunge wa Seneti la Marekani, ameshinikiza na kusisitiza kuwa inatakiwa kuwapa siraha wapiganaji wa wanaopingana na serikali ya Syria ambapo pia watatumia siraha hizo kupambana  na na kundi la ISIL lililopo nchini Irak.

Seneta John McCain aliyasema hayo wakati alipo kutana kiongozi wa mambo ya kigeni wa kundi linalo pingana na serikali ya Syria wakati alipo kuwa  ziarani nchini Uturuki.

Akiongea Seneta McCain alisema " kutokuwepo na niya ya kuwasaidia kisiraha wapinzani wa serikali ya Syria, kunahatarisha maslahi ya Marekani."

" Napia hili kundi la ISIL lililopo Irak lisipo kabiriwa haraka litakuwa ni hatari kwa katika eneo zima la Mashariki ya Kati jambo ambalo litasababisha hali ya usalama na ulinzi kwa Marekani na mafao yake kuwa katika hali tete."

Akiongezea Seneto John McCain alisema kuwa "Iraq na Syria zimekuwa nchi ambazo ni hatari na zitakuwa hatari zaidi hapo baadaye katika manufaa ya Wamarekani kama hazitazibitiwa mapema."

Hata hivyo habari kutoka ndani ya kundi hilo la ISIL zimesema kuwa
"wapiganaji wake wengi walikuwa wakipata mafunzo kwa kipindi cha miaka miwili nchi Jordan, ili kuwan
tayari kupambana na serikali ya Syria, lakini waliamua kubadirika toka kwenye mwelekeo huo."

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyo endelea nchini Syria na Irak, vimekuwa vikiwapa vicha kuuma viongozi na wataalamu wa maswala ya ulinzi na usalama, kwani kuna baadhi ya raia kutoka nchi za Magharibi  wapo katika makundi hayo ya kivita na inahofiwa huenda raia hao wakaja kuwa tishio pindipo watakapo rudi makwao.

Kundi la Al Qaeda lawa na mbinu mpya za kupitisha mabomu viwanja vya ndege.

London, Uingereza - 03/07/2014. Serikali ya Uingereza imeweka hali ya tahadhari katika viwanja vyake vya ndege, baada ya kutahadharishwa kuwa kuna uwezekano wa mabomu kupita.

Habari kutoka ofisi ya waziri wa usafiri zinasema kuwa "ulinzi umeimarishwa baaada ya serikali ya Marekani kuitaadharisha Uingereza kuwa mabomu ambayo si chuma cha kuonekana kwa mitambo yameaandaliwa kupita katika viwanja vya Uingereza kuelekea Marekani kwa ajili ya mashambulizi."

Hali ya tahadhari katika viwanja vya ndege nchini Uingereza imekuja, baada ya kuaminika kuwa "raia wa Ulaya ndiyo watakao beba mabomu hayo, kwani hawaitaji visa kuingia nchin Marekani."

Kuthibitisha ukweli huo wa kuwepo kwa aina hiyo ya mabomu, maafisa usalama wa Marekani wamesema kuwa "kundi la Al-Qaeda ambalo linamakao nchini Yemen na Syria ndilo linalo husika katika kutengeneza mabomu hayo."

Akizungumzia kutokana na habari hizi, makamu wa waziri mkuu wa Uingereza Nick Clegg ameonya kuwa Uingereza imejiaandaa kikamilifu katika swala la ulinzi, na hasa katika viwanja vyake vyote.

Kufuatia tahadhari hiyo, abiria wameonekana wakisubiri kwa muda zaidi ili kuweza kukaguliwa  katika viwanja vyote vya ndege nchini humo.