Saturday, January 29, 2011

Maandamano yafanya rais wa Misri kuvunja serikali.

Maandamano yafanya rais wa Misri kuvunja serikali.

Kairo Misri - 29/01/2011. Rais wa Misri amevunja serikali baada ya mandamano makubwa kufanyika kwa nchi nzima.
Rais Hosni Mubaraka, alisema " naelewa kwa jinsi gani wanchi wenzangu wanavyo sumbuka kutokana na hali zao za kiuchumi, mahitaji ya mabadiliko ya kisiasa na demokrasi, hivyo nitaunda serikali mpya ambayo itahakikisha yakuwa inatekeleza kwa vitendo hayo yote ili kuleta mabadiliko.
Wakati huo huo, rais wa Amerika Baraka Obama, amemtaka rais Hosni Mubara kufungua njia ya mabadiliko na kuacha demokrasi ichukue mkondo wake.
Rais Mubara, alihutubia taifa mara baada ya maandamano ya kupinga serikali yake kuwa makubwa na kuleta maafa karibu nchi nzima.
Picha hapo juu anaoekana rais Hosni Mubaraka akihutubia taifa na kuhaidi kuleta mabadiliko.

Friday, January 28, 2011

Serikali ya Misri ipo njia panda.

Nelson Mandela aruhusiwa kutoka hospital. Main Image Johannesburg, Afrika ya Kusin - 28/01/2011. Aliyekuwa rais wa kwanza baada ya kuanguka kwa utawala wa kibaguzi wa makaburu ameruhusi kutoka hospital Mill Park ambako alikuwa amekwenda kwa matibabu. Nelson Mandela mwenye umri wa miaka 92 alikuwa hospitalini kwa matibabu baada ya kutojisikia vizuri kiafya. Makamu wa rais Kgalema Motlanthe aisema " Mandela ana nafuu na alikuwa anataniana nasi na tuzidi kumwombea afya yake iwe nzuri." Picha hapo juu anaonekana Winnie Mandela akitokea hospital kumwangalia mumewe Nelson Mandela ambaye alikuwa amelazwa hospital. Serikali ya Misri ipo njia panda. Kairo, Misri 28/01/2011.Maelfu ya wananchi nchini Misri wameandamana kupinga serikali iliyopo madarakani na huku polisi wakipambana na waandamaji kwa kutumia gasi na maji.

Kwa mujibu wa mashaihidi waliokuwemo kwenye maandamano walisema watu wengi wamejeruhiwa wakiwemo wakinamama.
Katika maandamano hayo alikuwemo aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la kukagua na kumiliki mmatumizi ya nyuklia Mohamed ElBaradei.
Kufuatia maandamano hayo serikali imefunga matumizi yote ya mtandao, jambo ambalo jumuia ya kimataifa imelitilia mashaka kitendo hicho.
Picha hpo juu wanaonekana polisi wa kuzuia ghasia wakiwa wamesimama kuwazuia waandamanaji.

Wednesday, January 26, 2011

Uchumi wa dunia kujadiliwa tena Davos.

Uchumi wa dunia kujadiliwa tena Davos. Davos,Swiss - 26/01/2011. Viongozi wa serikali, wafanya biashara,,wanasiasa na wanauchumi, wanakutana nchi Uswisi ili kujadili mpangilio mzima wa uchumi dunia. Mkutano huo ambao utachukua siku tano, unatarajiwa kujadili mbinu za kuinua uchumi baada ya mtikiso mkubwa wa uchumi ulio ikumba dunia miaka miwili iliyo pita. Kwa mujibu wa wachunguzi wa maswala ya kiuchumi wanasema " inabidi katika mkutano huu viongozi, wanasiasa,wafanya biashara na wanauchumi watafute ufumbuzi wa kuinua uchumi na siyo kuweka ahadi ambazo zimekuwa ziki tawaliwa na mzunguko wa siasa na hai halisi ya kiuchumi. Picha hapo juu ni mji wa Davos, ambao viongozi wa nchi tofauti, wafanya biashara, wanasiasa na wanauchumi wanakutana kujadili hai halisi ya uchumi duniani.

Interpol yaombwa kumkamata rais wa Tunisia.
Tunis,Tunisia - 26/01/2011. Polisi wa kimataifa wameombwa kukamata aliye kuwa rais wa Tunisia, mkewe na washiriki wa karibu wa familia yake ili wajibu mashitaka mbele ya mahaakama.
Zine Kwa mujibu wa habari kutoka wizara ya sheria ya Tunisia zinasema "El Abidine Ben Ali, ambaye alikuwa rais wa Tunisi anakabiliwa na kesi za kuiba mali ya uma,kuiba pesa za nchi na kuziwekeza nje ya nchi kwa matumizi yake na familia yake."
Akisisitiza kuhusu habari hizo, Lazhar Karoui Chebbi, alisema tumeiomba Interpol kumkamata iliaje kujibu mashitaka ya kuhujumu mali umma.
Rais wa Tunisia alikimbia nchi baada ya wanchi wa Tunisia kuanamana kwa kutaka ajitoe madarakani kutona na serikali yake kushindwa kuwainua wanachi kiuchumi.
Umoja wa mataifa watakiwa kufungua mahakama za kiharamia.
New York, Amerika - 26/01/2011. Umoja a Mataaifa umeombwa kuchangia mbinu mbadala za kupambana na maharamia waliopo katika pwani ya Somalia hadi kufikia pwani za Afrika ya Mashariki na kuanzisha koti maarumu itakayo husika na kesi za kiaaramia.
Jack Lang, ambaye alikuwa waziri wa utamaduni wa Ufaransa, alisema " inabidi kuanzishwa koti ya kushughulkia kesi za kiaramia ili kukabili mlolongo wa watuhumiwa ambao huwa wanaachiwa huru.
Hadi kufikia sasa serikali ya Kenya na Ushelisheli ndizo zilizo weza kuwahukumu maharamia kwa kutumia sheria zilizpo nchini mwao.
Picha hapo juu wanaonekanaa baadhi ya maharamia wakinyoosha mikono mara baada ya kuwekwa chini ya ulinzi.

Tuesday, January 25, 2011

Serikali ya Palestina yakanusha kuridhia Waizrael.

Serikali ya Palestina yakanusha kuridhia Waizrael.
Ukanda wa Magharibi, Palestina - 25/01/2011. Serikali ya Wapalestina imekanusha vikali habari zilizo patikana ya kuwa uongozi huo umeridhia swala Wakimbizi wa Kipalestina.
Kwa mujibu wa habari zinasema "uongozi wa Wapalestina umekuwa na ukifikilia kukubaliana na serikali ya Izrael kuhusu swala la kurudi kwa wakimbizi wa Kipalestina waopo nje ya Palestina, ambapo zinasema itakuwa vigumu kwa wakimbizi wote kurudi Palestina."
Swala la kurudi kwa wakimbizi wa Kipalestina imekuwa moja mjadara unao letamvutano kati ya Waizrael na uongozi wa Wapalestina.
Picha hapo juu wanaonekana rais wa Amerika Baraka Obama katikati na kushoto ni Benyamin Netanyahu akitaka kupeana mkono na rais wa Wapalsetina Mahamoud Abbas mwaka jana wakati walipo kutana kujadii njia mbadala za kumaliza mgogoro kati yao.

Saturday, January 22, 2011

Tony Blair awelwa kiti moto tena.

Tony Blair awekwa kiti moto tena London, Uingereza - 22/01/2011. Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza wakati wa vita vya Irak na kumtoa madarakani hayati Saadam Hussein ameojiwa kwa mara nyingine tena na tume ya uchunguzi wa mwenendo mzima wa vita vya Irak. Tony Blair ambaye alikuwa waziri mkuu wa Uingereza, chini ya serikali yake alishirikiana na serikali ya Amerika iliyo kuwa ikiongozwa na rais George Bush na kumn'goa madarakani rais Saadam Hussein wa Irak. Akiongea mbele ya tume hiyo Tony Blair alisema " nasikitika kwa kwa wale wote waliopoteza maisha au kuathirika kutokana na vita hivi." Na nilimwahidi rais wa Amerika ya kuwa kutakuwa bega kwa bega katika vita hivi kwani niliamini Saadam Hussein alikuwa kiongozi hatri kwa jumuia ya kimataifa." Uingereza na Amerika kwa kushirikiana na washiriki wengine ziliongoza vita vilivyo vikia kungólewa madarakani kwa rais wa Irak, Saadam Hussein. Picha hpo juu ni ya aliye kuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair ambaye aalikuwa akijibu maswali kutoka katika tume ya kuchunguza mwenendo mzima wa vita vya Irak.

Kiongozi wa Al Qaeda atishia Wafaransa.
Paris,Ufaransa - 22/01/2011. Kiongozi wa kundi la Al Qaeda ametishia na kuitaka serikali ya Ufaransa kutoa wanajeshi wake aliopo katika nchi za Kiislaam.
Osama Bin Laden alisema kwa kupitia habari zilizo patikana katika vyombo vya habarai kwa kudai " ili raia wa Ufaransa waachiwe inategemea uamuzi wa serikali yao kutimiza moja ya masharti ambapo ni kwa serikali ya Ufaransa kutoa majeshi yake katika nchi za Kiislaam."
Kuongea huko kwa kiongozi wa Kundi la Al Qaeda kunaendana na kuungwa mkono m\na na kundi la AQIM ambalo ndilo kundi kubwa lililopo Kaskazini Magharibi mwa Afrika linalo shirikiana na Al Qaeda, na hivi karibuni limehusika katika mauaji na utekaji nyara wa wengi raia wa Ufaransa.
Picha hpo juu ni ya Osama Bin Laden, ambaye ni kiongozi wa kundi la Al Qaeda, na hajulikani mahali alipo au anapo ishi.

Wednesday, January 19, 2011

Ombi la kukamatwa kwa Tzipi Livni lakataliwa.

Odinga, Ouwattara na Gbagbo hakuna maelewano.

Abidjan, Ivory Coast-19/01/2011. Msuruhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast ambaye pia ni waziri mkuu wa Kenya ameondoka nchi humo bila kupata suruhisho la mgogoro huo.
Raila Odinga ambaye alipewa jukumu la kusuruhishwa mgogoro huo wa kisiasa aliwaambia waandishi wa habari ya kuwa imekuwa vigumu kufikia muaafaka kati ya pande zote mbili za kisiasa.
Akisisitiza Odinga alisema "muda wa mazungumzo ya hiyari unazidi kuwa finyu."
Hata hivyo msemaji wa serikali ya rais Laurent Gbagbo alisema "hatutakubali tena kuongea na Raila Odinga kwani anapendelea upande mmoja wa bwana Ouawattara na hatuko tayari kumpokea."
Picha hapo juu anaonekana Raila Odinga akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na Laurent Gbagbo pichani kulia na Alassana Ouwattara pichani kushoto.
Amerika na China kushirikiana kwa karibu zaidi.
Washington, Amerika- 19.01/2011. Serikali ya Amerika na Uchina zimekubaliana kushirikiana katika usalama wa maswala ya kinyuklia na sekta za kibiashara. Kufuatia mikataba hiyo China itanunua ndege za aina ya boingi 200 na kuwekeza nchini Amerika vitega uchumi katika kilimo,mawasiliano. Wakiongea mbele ya waandishi wa habari marais hao walisema kukutana kwao kumeweka msingi mzuri ambao nchi zote mbili zitanufaika." Picha hapo juu wanaonekana rais wa Amerika Baraka Obama kushoto na rais wa China Hu Jintao wakiwasalimia wanchi waliokuja kuwalaki kabla ya kuanza mazungumzo rasmi kati yao jinsi ya kushirikiana kwa ukaribu zaidi. Watunisia watakiwa kuungana. Tunis, Tunisa- 19/01/2011. Rais wa kipindi cha mpito nchini Tunisia ametangaza yakuwa atahakikisha maswala yaliyo leta kutokuelewana na kunyanyasa wanachi hayatarudiwa tena na kutaka wanchi wa Tunisia kufungua ukurasa mpya. Fouad Mebazaa, akitangaza kupitia TV na vyombo vingine vya taifa na kimataifa alisema, sisi sote kwa pamoja tunaweza kuiongoza na kuijenga nchi yetu na hivyo tufungue ukurasa mpya ili kuijenga nchi yetu ambayo imeyumba kisiasa na kiuchumi." Hata hivyo bado kunahali ya mvutano wa kisiasa nchini Tunisia huku wanchi wakudai ya kuwa bado serikali hiyo inaviongozi waliokuwa wakati wa utawala wa rais Zine Ben Ali ambaye ameikimbia nchi baada ya wanachi kutaka atoke madarakani. Nayo serikali ya Swissi imezizuia mali zote za aliyekuwa rais wa Tunisia Zine Ben Ali. Picha hapo juu anaonekana rais wa mpito wa Tunisia Fouad Mebazaa akishuka kutoka kwenye gari, huku akiwa analindwa vikali na walinzi wake tayari kuelekea ofisini kuanza kazi rasmi ya kuongoza nchi. Ombi la kukamatwa kwa Tzipi Livni lakataliwa. Pretoria, Afrika ya Kusini- 19/01/2011. Serikali ya Afrika ya Kusini imekataa ombi la kutaka akamatwe aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Izrael ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini humo. Ombi hilo lilitolewa na Shirika la Uhusiano la Wapalestina, kwa adai ya kuwa aliyekuwa waziri wa mamboya nje wa Izrael Tzipi Livni alihusika katika wakati jeshi la Izrael lilipo shambulia eneo la Gaza mwidho wa mwaka 2008 hadi mwanzoni mwa mwaka 2009. Mclntosh Polela ambaye ni msemaji wa ofisi ya usalama na makosa ya jinai alisema "tumepata ombi la kutaka kukamatwa kwa aliyekuwa waziri wa mambo ya njee wa Izrael na hatutachukua hatua hiyo na Tzipi Livni hatakamatwa kwani hakuna ushahidi wa kutosha zidi yake." Picha hapo juu ni ya Bi Tzipi Livni, ambaye alikuwa waziri wa mambo ya njee kati ya miaka ya 2009-9.
Mtoa siri za benki za Swisi ahukumiwa.
Zuriki, Uswisi - 19/01/2011. Mahakama jijini Zuriki imemkuta na makosa aliyekuwa mfanyakazi wa benki aliyehusika kutoa nyaraka za siri kwa Wikileaks ambazo zinaonyesha majina ya watu ambao wameweka pesa katika benki nchini humo.
Mshitakiwa huyo Rudolf Elmer alihukumiwa kwa kutozwa faini ya kiasi cha Swiss 7,200 ($7,505) na kuwa chini ya uangalizi kwa muda wa miaka miwili.
Akitoa hukumu hiyo hakimu alikataa ombi la mwasheria kwa upande wa mashitaka kwa kutaka adhabu ya kifungo itolewe kwa bwana Ridolf Elmer.
Rudolf Elmer alikubali makosa yake kabla ya hukumo hiyo kutolewa.
Picha hapo juu anaonekana Ridolf Elmer ambaye alikutwa na hatia ya kutoa nyaraka za siri za benki kwa mtandao wa habari wa Wikileaks. Jumuiya za nchi za kiarabu za tahadhalishwa.
Sharm el Sheikh, Misri-19/01/2011. Viongozi wa nchi za Kiarabu wamekutana nchini Misri ili kutasmini hali halisi ya jumuiya hiyo na kujadili wimbi la magauzi ambalo linaelekea kuzikumba nchi za Kiarabu.
Amir Mussa ambaye ni katibu mkuu wa jumuia ya nchi za Kiaarabu waliwaambia viongozi wa nchi wanachama ya kuwa hali ya kiuchumi katika nchi hizo inabidi ziangaliwe kwa undani sana, na "inatakiwa kuwepo na mabadiliko ya kiuchumi kwa serikali hizo kuwekeza rasilimali vitega uchumi ilikuinua maisha ya wanchi wa nchi hizo."
Akiongezea Amr Mussa alisema "mapinduzi yaliyo tokea nchini Tunisia lazima ma yaangaliwe kama mfano kwa serikali za nchi hizo."Na aliwataka wanchi wa nchi za Kiarabu kuwa pamoja ili kujenga nchi zao na eneo zima kwa ujumla.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Misri Hosni Mubaraka akipokea ujumbe toka kwa moja ya washuri na huku katibu Amr Muoussa, akiangalia kwa makini.

Saturday, January 15, 2011

Rais wa Tunisia akimbia nchi.

Rais wa Tunisia akimbia nchi.

Tuinis, Tunisia 14/01/2011. Rais wa Tunisia amekimbilia nchini za Uarabuni baada ya hali ya kisiasa kuwa katika hali mbaya kwa upande wa uongozi wake.
Zine El Abidine Ben Ali ambaye ametawala nchini Tunisia kwa zaidi ya miongo miwili na nusu alikimbia nchi huku hali ikiendelea kuwa mbaya kufuatia maandamano yalifanywa na wanchi wa Tunisia kupinga hali ya kiuchumi kuwa ngumu.
Kufuatia kuondoka nchi kwa rais huyo, spika wa bunge Fouad Mebezaa ameapishwa kuwa rais wa muda ili kuiongoza Tunisia mpaka hapo uchaguzi mpya utakapo fanyika.
Picha hapo juu anaonekana rais wa zamani wa Tunisia enzi zake wakati alipo kuwa akiwasalimia wananchi mara katika moja ya sheehe za kitaifa.

Thursday, January 13, 2011

Wahaiti wakumbuka siku ya tetemeko la ardhi.

Wahaiti wakumbuka siku ya tetemeko la ardhi. Port au Prince, Haiti - 13/01/2011. Maelfu ya wananchi wa Haiti wamekutana katika jiji la Port au Price kukumbuka siku ambayo tetemeko la ardhi lilitkea na kupoteza maisha ya watu na kuleta maafa makumbwa kwa kila jamii kiuchumi na kiafya. Tetemeko hilo ambalo lilipoteza maisha ya watu wapatao 316,000 kupoteza maisha yao na wengine kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa mashirika tofauti yanayotoa misaada nchini Haiti yamesema " hadi kufikia sasa hali nchini humo bado siyo ya kulizisha na juhudu zinatakiwa kuongezeka ili kuijenga nchi hiyo na kuinua hali ya misha ya watu wake." Picha hapo juu ni misaraba ikiwa inawakilisha watu waliopoteza maisha wakati wa tetemeko la ardhi lililo tokea mapema mwaka 2010. Waamerika waombwa kuungana na kushirikiana. Tucson, Amerika - 13/01/2011. Rais wa Amerika amewataka Waamerika wote kuungana na kuishi kwa ushirikiano ijapokuwa kunatofauti za kisiasa. Rais, Baraka Obama aliyasemahayo wakati alipo udhulia siku maalumu ya kuwakumbuka watu walioshambuliwa kwa risasi na kupoteza maisha ya kwenye jimbo la Arizona. Baraka Obama alisema " mambo mabaya hutokea na nilazima tujitahidi kuwa wavumilivi hasa tukizingatia tumepoteza watu sita kutokana na ukatili uliofanyaka." Mtu anayehusika na mauaji hayo Jared Lougher 22 anashikiliwa kutokana na kufanya kitendo hicho cha kikatili. Picha hapo juu wanaonekana rais Baraka Obama akiwa na mke wake Micheel wakishika kwenye ndege kuelekea kuhudhulia siku maalumu ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha wakati wa mashambulizi ya kikatili.

Wednesday, January 12, 2011

Kesi ya Julian Assange yaanza kusikilizwa.

Kesi ya Julian Assange yaanza kusikilizwa.

London, Uingereza - 12/01/2011. Mwanasheria wa mwanzilishi wa WikiLeaks ameiambia mahakama ya kuwa mteja wake atahukumiwa kifo ikiwa atapelekwa nchini Amerika. Mwanasheria huyo, alisema " ikiwa Julian Assange atapelekwa nchini Sweden, basi kunauwezekano mkubwa wa mteja wake kupelekwa nchini Amerika na kuhukumiwa adhabu ya kifo." Julian Assange, ambaye anatakiwa nchini Sweden kwa kosa la kufanya mapenzi rubuni amekuwa anapinga na kuwa alifanya kitendo hicho kama kinavyo elezwa.
Picha hapo juu anaonekana Julian Assange,akielekea mahakamani kusikiliza kesi yake.
Mafuriko yazidi kuleta athari kubwa nchini Australia.
Brisbane, Australian - 12/01/2011. Maelfu ya wakazi wa mji wa Brisbane wamehama mji mara baada ya mji mzima kukumbwa na mafuriko ya kihistoria.
Anna Bligh, alisema "zaidi ya makazi 20,000 huenda yakakumbwa na mafuriko na kuwaacha wakazi wake bila kitu."
Hali ya mafuriko nchini Australia imekuwa ikeendelea kwa kasi na kusabababisha hasara kubwa sana kwenye maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya waokoaji wa huduma ya kwanza wakiwa ndiani ya boti tayari kutoa msaada.
Serikali ya Rebanon yavunjika.
Beiruti, Lebannon - 12/01/2011. Serikali ya Lebanon imevunjika baada ya washiriki katika serikali ya muungano Hezbollah kujitoa.
Kuvunjika huko kwa serikali kumekuja baada ya kuzuka mabishano makubwa jinsi ya kupiga kura ili kuunga mkono matokeo ya uchunguzi wa mauaji aliyekuwa waziri mkuu Rafik al Hariri
mwaka 2005.
Serikali ya Lebanon imevunjika wakati waziri mkuu wa Saad Hariri akiwa ziarani Amerika kukutana na rais Baraka Obama.
Katibu mkuu wa umoja wa Matifa Ban Ki-moon alisema " ningependa kuwataka Walebanon kutatua maswala yao kwa amani na huru na umoja wa mataifa upo pamoja nao."
Hadi kufikia sasa uchunguzi wa kessi hiyo na matokeo yake yamekuwa yakipingwa na kundi la Hezbollah kwa madai ya kuwa matokeo yaina yoyote yatakuwa ya kisiasa hivyo haita yatambua.
Picha hapo juu ni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Rafik al Hariri ambaye aliuwawa na bomu lililolipuliwa na watuwasiojulikana.

Sunday, January 9, 2011

Wasudan wapiga kura kuamua muungano wa nchi yao

Wasudan wapiga kura kuamua muungano wa nchi yao.

Juba, Sudan - 09/01/2011. Wananchi wa Sudan wamepiga kura ili kuamua kama nchi yao itabaki moja au kugawanyika kuwa Sudan ya Kusini na Sudan ya Kaskazini.
Kwa mujibu wa wasimamizi wa uchaguzi huo wamesema wanchi wa Sudan wameudhulia katika vituo vya kula kwa wingi.
Salva Kiir ambaye ni kiongozi wa Sudan ya Kusini alisema " upigaji wa kura waleo ni kumaizia kazi iliyo anzwa na kiongozi wetu John Garang na inathibitisha kazi yake haikupotea bure.
Picha hapo juu anaonekana kiongozi wa Sudan Kusini Salva Kiir akipiga kura katika moja ya vituo vya kupigia kura.

Friday, January 7, 2011

Al Shabab walaumiwa kwa kuzuia misaada ya utu.

Al shabab walaumiwa kwa kuzuia misaada ya utu. Mogadishu, Somalia - 07/01/2010. Serikali ya Somalia inalimaumu kundi la Al Shabab kwa kuzuia misaada ya kiutu ambayo inatolewa ja jumuiya ya kimataifa. Habari kutoka wizara ya mambo ya ndani ya nchi zinasema ' inakuwa vigumu kusambaza misaada ya kiutu kutokana na hali ya kutokuwepo kwa usalama kwa wafanyakazi wanaohusika katika kutoa misaada." Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Somalia ni moja ya nchi ambayo ilikubwa na hali ya ukame, kiasi cha kuhatarisha hata mifugo. Picha hapo juu inaonyesha ni kwa kiasi gani hali ya ukame ilivyo hasili maisha ya watu na na wanyama.

Mabalozi wa Kanada na Uingereza watakiwa kuondoka nchini Ivory Coast.
Abidjan, Ivory Coast - 07/01/2010. Rais wa Ivory Coast amewataka mabalozi wa Uingereza na Kanada kuondoka mara moja nchini humo.
Uamuzi huo wa uongozi wa Ivory Coast kuwafukuza mabalozi hao, umekuja mara baada ya serikali hizo za Uingereza na Kanada kuwataka mabalozi wa Ivory Coast waliopo katika nchi hizo "kuondoka mara moja."
Hata hivyo wakati uongoziwa rais Laurent Gbagbo unavutana na jumuiya ya kimataifa, mpinzani wake Lassane Ouattara ameitaka jumuiya ya ECOWAS kutumia nguvu za kijeshi kumwondoa madarakani rais Gbagbo.
Picha hapo juu ni ya rais wa sasa wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo ambaye amekuwa anavutana na jumuiya ya kimataifa mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa.

Tuesday, January 4, 2011

Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wakubali kukutana.

Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wakubali kukutana.

Abidjan, Ivory Coast - 04/01/2011. Mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast huenda ukapata njia muafaka mara baada ya rais wa sasa na mpinzani wake kukubali kukutana ili kuongea kiundani tofauti zao za kisiasa zilizo letwa tangu kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais. Akiongea na waandishi wa habari, mwakilishi wa Umoja wa Afrika ambaye ni waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alisema, "Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara wamekubali kukutana mara baaada ya kukutana na viongozi hao." Raila Odinga na baadhi ya viongozi wa ECOWAS wamekuwa wakifanya kila juhudi kuleta suruhisho la kisiasa kati ya viongozi hao, ili kuiepusha Ivory Coast na machafuko na vurugu ambazo huenda zikapelekea kuleta vita kati ya wadau wa Ouattara na Gbagbo. Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa ECOWAS na mjumbe wa Umoja wa Afrika Raila Odinga kulia wakatiwalipo kutana Alassane Ouattara.
Rais wa Sudan ahahidi kuunga mkono matokeo ya kura za maoni.
Juba, Sudan ya Kusini - 4/01/2011. Rais wa Sudan ametembelea Sudan ya Kusini siku chache kabla ya kufanyika kura za maoni ambazo huenda matokeo yake ya kasababisha kuigawa Sudan.
Rais Omar Al Bashir alisema " ningependelea kuwepo kwa umoja wa wanachi wa Sudan. lakini ikiwa matokeo ya kura yatapelekea kugawa Sudan, basi nitakuwa wa kwanza kuwa kuunga mkono matokeo hayo."
Omar al Bashir aliyasema hayo mbele ya wabunge wakati alipo kutana nao mjini Juba.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Sudan wakati alipowasili mjini Juba ili kuongelea hali halisi ya matokea ya kura ya maoni itakayo pigwa hivi karibuni.

Sunday, January 2, 2011

Brazil wapata rais wa kwanza mwana mke.

Brazil wapata rais wa kwanza mwanamke. Brasilia, Brasil - 02/01/2011. Wananchi wa Brazil wameshuudia kuapishwa kwa rais mpya wa nchi yao, baada ya muda wa rais wa sasa Luiz Lula da Silva kumalizika. Dilma Rousseff aliapishwa mbele ya watu wapatao 70,000 wakiwemo wageni waalikwa kutoka nchi tofauti duniani. Rais Dilma aisema " nitajitahidi kulinda na kuendeleza yale yote ambayo rais Luiz Inacio Lula Da Silva aliyo fanya katika kuinua uchumi wa wanchi wa Brazil na kuinua kiwango cha kila mwanchi kiuchumi." Picha hapo juu anonekana rais wasasa wa Brazil Dilma Rousseff kushoto akiwa na rais aliye mwachia ofisi Luiz Inaci Lula da Silva kwa pamoja wakiwa wamenyanyua mikono mara baada ya kuapishwa kwa Dilma Rousseffe kuwa rais wa kwanza mwanamke. Urussi yaaanza kuiuzia China mafuta.

Moscow, Urussi - 02/1/2011. Serikali ya Urussi kupitia makampuni yake ya mafuta imeaaza kusafirisha mafuta nchini China.
Usafirishaji huo wa mafuta utapitia Mashariki ya Siberia ambapo mitambo ya kusafirishia mafuta imewekezwa na itakuwa na urefu km 50,000.
Igor Dyomin ambaye ni msemaji wa kampuni ya kusafirisha mafuta Transneft alisema mitambo hiyo itakuwa na uwezo wa kusafirisha tani zamafuta 43,000 kwa siku.
Urussi ni nchi ambayo ni moja ya nchi inayo uza zao la asili ya mafuta na gasi katika nchi mbalimbali za ulaya.
Picha hapo juu ni ya bomba la mafuta likielekea nchini China ambapo imeaanza kununua mafuta kutoka Urussi

Saturday, January 1, 2011

Dunia nzima yashangilia kuanza mwaka 2011

Dunia nzima yashangilia kuanza mwaka 2011.

London, Uingereza -01/01/2011. Wananchi duniani kote wameshangilia kwa furaha kuanza mwaka 2011.
Miji tofauti duniani ilikuwa na shangwe na mataa yenye rangi tofauti na ving'ola kulia kuashilia kuanza kwa mwaka 2011.
Mwaka 2010 utakumbukwa kwa matukio tofauti ambayo yameleta maafa makubwa katika jamii.
Matukio hayo ni tetemeko la adhi nchini Haiti, mtikisiko wa uchumi na mlolongo wa mafuriko, barafu kwa wingi na jua kuwa kali hasa nchini Argentina.
Picha hapo juu zinaonekana taa zikiwashwa kusherekea kuanza kwa mwaka 2011.