Monday, May 31, 2010

Izrael yasimamisha meli za misaada.

Izrael yasimamisha meli za misaada.

Tel-Aviv, Izrael- 31/05/2010. Makomando wa Kiizrael wamesimamisha meli iliyo beba misaada ambayo ilikuwa ikielekea kwenye Ukanda wa Gaza.
Katika harakati za kuizuia masafara wa meli Freedom Flotilla, watu wapatao kumi na tisa wamefariki dunia.
Kufuatia tukio hilo nchi nyingi zike kiaani kitendo hicho kwa kuitaka serikali ya Izrael itoe maelezo kwa undani kisa cha tukio hilo.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wauguzi wa jeshi la Izrael wakiwa wanamshusha mmoja wa majeruhi wakati wa kuzizuia meli ambazo zilikuwa zikielekea Ukanda wa Gaza.
Picha ya pili hapo juu wanaonekena baadhi ya wapiganaji wa Izrael wakiwa wanakagua meli ambayo waliisimamisha ililp kuwa ikielekea Ukanada wa gaza.
China yaingilia kati kuleta amani kwa Wakorea
Beijing, China- 31/05/2010. Serikali za China, Japan na Korea ya Kusini zimekutana ili kujadili njia mbadala ya kutuliza hali ya mchafuko ambayo ulizuka baada ya meli ya serikali ya Korea ya Kusini kuzama kwa madai ya kuwa serikali Korea ya Kaskazini ndiyo iliyo izamisha.
Hata hivyo serikali ya Korea ya Kaskazini ilikana kufanya kitendo hicho.
Picha hapo juu wanaonekana wanajeshi wa waliopo katika mpaka unao tenganisha Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini wakiwa kazini kulinda mipaka yao.

Monday, May 17, 2010

Iran yasahini mkataba na kuruhusu madini kinyuklia kurutubishwa Uturuki.

Iran yasahini mkataba na kuruhusu madini kinyuklia kurutubishwa Uturuki.

Tehran, Iran 17/05/2010. Ssrikali ya Iran imekubali na kutia sahii mkataba wa kusafirisha madini ya ambayo yanatumika kuzalisha na kurutubisha madini ya nyuklia kupelekwa nchini Uturuki kwa uzalishaji wa madini ya nyuklia.
Mkataba huo ambao ulishuhudiwa na viongozi wa Brazil na Uturuki.
Hata hivyo Amerika na nchini za Ulaya Magharibi zikiongozwa na Uingereza na Ufaransa zinasema yakuwa mkataba huo lazima usimamiwe na shirika la IAEA - International Atomic Energy Agency.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wa Uturuki kulia Recep Tayyip Erdogan,katikati ni rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad na rais wa Brazil kulia Lula Inacio da Silva wakati walipo kutana nchini Iran.

Friday, May 14, 2010

Swala la mto Nile lafikiwa muafaka na nchi nne.

Swala la mto Nile lafikiwa muafaka na nchi nne.

Kampala, Uganda - 14/05/2010. Serikali za nchi za Rwanda, Uganda, Ethiopia naTanzania zimetialiana sahii mkataba ili kuanza kuangalia ni kwa jinsi gani nchini hizi zitaanza kufaidika na malia asili ya mto Nile kwa manufaa ya nchi hizo na kutengua mkataba uliwekwa na ukoloni wa Uingereza mwaka 1929 ambapo Misri ilipewa haki ya kutumia maji ya mto huo kwa wingi kuliko nchi zote ambazo mto huo unatoka au kupita.
Wakiongea kwa nyakati tofauti mawaziri wa maliasili wa Ethiopia Asfaw Dingamo alisema " naamini hatimayake nchi zpte zitakubaliana kimsingi kuhusu swala zima la matumizi maji ya mto Nile."
Naye waziri wa maliasi wa Rwanda, Stansilas Kamanzi alisema " inasikitisha baadhi ya nchi ambazo mto una pita hazikuwepo kutokana na hali halisi ya swala lenyewe."
Kufuatia kitendo hicho, serikali ya Misriimepinga na kudai haikuwa haki na huenda ikachukua hatua za kisheria.
Picha hapo juu inaonyesha vyanzo vya mto Nile kutoka Afrika ya mashariki na kuishia nchini Misri.
Picha ya pili inaonyesha picha ya maji ya mto Nile ambayo yamekuwa yakitumiwa kwa njia mbalimbali na wanchi wa Misri kwa asilimia kubwa.
Rais wa Urussi akutana na kiongozi wa Hamas.
Dumuscas,Syria - 14/05/2010. Rais wa Urussi, Dmitry Medvedev amekutana na kiongozi wa kundi la Hamas aliyepo ukimbizini nchini Syria Khaled Meshaal wakati wa ziara yake aliyo ifanyanchini humo.
Kufuatia mkutano huo, ofisi za mambo ya nje ya Izrael zimesema"hazikufurahishwa na kitendo hicho."
Hata hivyo habari kutoka ofosi za serikali ya Urussi zinasema" kiongozi huyo huwa nakutana au kuwasialiana viongozi wengi wakiwemo wa serikali ya Amerika ila kutokana na sababu fulani huwa hawatangazwi kama walikutana au kuwasiliana na kiongozi huyo."
Picha hpo juu ni ya rais wa Urussi, Dmitry Medvedev, ambaye alikutana na kiongozi wa kundi la Hamas aliyepo ukimbizini nchini Syria.
Rais Obama, ataka muswada wa kutengenezwa mitambo ya ulinzi upitishwe.
Washington, Amerika - 14/05/2010. Rais wa Amerika Baraka Obama, amelitaka bunge la Congress kupitisha muswada wa pesa $205million kwa ajili ya kuisaidia Izrael kutengeneza mitambo ya kuzuia mashabulizi ya mabomu.
Mpango huo unao julikana kama "Iron Dome" utakuwa na mazumuni ya kuzuia mashambulizi kutokea nchini za jirani hasa Lebanon na Ukanda wa Gaza ambapo huwa mabomu mengi huwa yanarushwa upande wa Izrael kutokea sehemu hizo.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Amerika, Baraka Obama akiongea hivi karibuni kuhusu hali halisi ya Mashariki ya Kati.
Taliban wataka utawala wa Pakistan ung'olewe.
Karachi, Pakistan - 14/05/2010.Kiongozi mmoja wa kundi la Taliban liloponchini Pakistan Azam Tarik amelitaka kundi lake kuingusha serikali ya Pakistan na kusema ya kuwa nia na mipango ya Amerika haitafanikiwa.
Kiongozi huyo ambaye pia ni msemaji wa kundi hilo alisema "kundi lake halijahusika na milipuko ya mabomu iliyo tokea hivi karibuni katika maeneo yanayo kaliwa na raia, na ni mbinu za kutaka kulichafua kundi hilo."
Akisisitiza Azam Tarik, "hivi sasa umefika wakati wa kuwaondowa kwenye madaraka wale wote wanao shirikiana katika kupinga Uislaam na wananchi wa Pakistan."alimalizia kwa kusema.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Pakistan, Asif A Zardari, ambaye yupo madaraka na hali ya usalama wa Pakistani imekuwa nawakati mgumu kutona na tishio la kundi la Taliban.

Wednesday, May 12, 2010

Uingereza yapata serikali mpya ya shirikisho.

Uingereza yapata serikali mpya ya shirikisho.

London, Uingereza - 12/05/2010. Wananchi wa Uingereza wamepata viongozi wapya watakao iongoza serikali ya nchi hiyo baada ya makubaliano ya kimsingi kufikiwa kati ya chama cha Liberal Demokratik na Conservative.
Serikali hiyo mpya shirikisho itaongozwa na waziri mkuu mpya wa Uingereza David Cameron wa chama cha Conservative na makamu wa waziri mkuu atakuwa Nick Gregg wa chama cha Liberal Demokratik.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi wapya wa serikali ya Uingereza, David Cameron kushoto akiwa na Nick Gregg kulia wakielekea kuingia ofisini kuanza kazi ya uongozi rasmi.
Picha ya pili, wanaonekana Nick Cregg kulia na David Cameron kushoto wakiwasalimia wananchi na waandishi wa habara mara baada ya kukubaliana kimsingi kuunda serikali ya shirikisho ya Uingereza.
David Miliband atangaza kugombea uongozi wa chama cha Labour.
London, Uingereza - 12/05/2010. Aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza David Miliband ametangaza kugombe kiti cha uenyekiti cha cham cha Labour.
David Miliband ambaye ameshawahi kushika madaraka tofauti katika serikali iliyokuwa ikiongozwa na chama cha Labour kabla ya kuteuliwa kuwa waziri wa mabo ya nje wa Uingereza.
Picha hapo juu anaonekana David Miliband ambaye ametangaza kugombea uongozi wa chama cha Labour.
Picha ya pili anaonekana aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown akishuka kutoka kwenye gari baada ya kutoka kumwona Malkia wa Uingereza ya kuwa anaikabidhi serikali kwa chama cha Conservative na Libaral Demokratik.
Urusi na Uturuki kushirikiana kwa ukaribu.
Ankara, Uturuki - 12/05/2010. Serikali ya Urussi imetiliana sahii mkataba na serikali ya Uturuki wenye thamani ya $20 billion kwa ajili ya kujenga mitambo ya kinyuklia na miradi mingine.
Kwa mujibu wa wasemaji wa serikali zote mbili walisema "nchini hizo pia zimeondo visa kwa raia wa nchi hizo na kurahisisha shughuli nyingine za kujenga mahusiano kati ya nchi hizo mbili."
Picha hapo wanaonekana rais wa Urussi kulia Dmitry Medvedev na waziri mkuu wa Uturuki Tayyip Erdogon wakitia sahii mikataba kwaniaba ya nchi hizo mbili.
Ndege yaanguka na kuuwa abiria 103 nchini Libya.
Tripoli, Libya - 12/05/2010. Ngede iliyo kuwa ikitokea nchi Afria ya Kusini kuelekea nchini Libya imeanguka na kupoteza maisha ya watu 103 na kijana mmoja wa Kihollanzi ndiye aliye nusirika katika ajali hiyo.
Kwa mujibu wa habari zina sema "ndege hiyo ilianguka karibu na kiwanja cha ndege wakati inataka kutua."
Ndege hiyo ya shirika la ndege la Afriqiya ilikuwa katika safari zake za kawaida kutoka jijini Johannesburg kuelekea jijini Tripoli.
Picha hapo juu yanaonekana mabaki ya ndege la Afriqiya ambayo ilianguka mapema alfajiri siku ya Jumatano ikitokea nchini Afrika ya Kusini.

Monday, May 10, 2010

Gordon Brown asema "Nangátuka madarakan."

Gordon Brown asema "Nangátuka madarakani."

London,Uingereza - 10/05/2010. Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema atajiudhuru uongozi katika chama chake cha Labour, na kuwaomba wanachama wenzake kujiandaa kumchagua kiongozi mwingine atakaye kiongoza chama cha Labour.
Akiongea mbele ya wandishi wa habari Gordon Brown alisema "nita jiudhuru uongozi wa chama ifikapo wa mwezi Septemba" Na kwa sasa kiongozi wa Liberal Demokratic, Nick Clegg,ameniambia ya kuwa angetaka kuongea na chama cha Labour wakati anaendelea kujadiliana na chama cham Consevative."
Akimalizi katika hotuba yake Brown alisema "Katika kipindi chote nitakacho kuwa kiongozi kabla ya kujiudhulu nitahakikisha mabadiliko ya kiuchumi yanakwenda haraka na kukamilisha yale yote yanayotakiwa kufanywa kwa maendeleo ya Waingereza wote."
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown akiongea mbele ya waandishi wa habari mikakati na muda gani atajiudhulu uongozi.

Friday, May 7, 2010

Uchaguzi wa Uingereza wawa patupu.

Uchaguzi wa Uingereza wawa patupu. London Uingereza - 07/05/2010. Matokeo ya uchaguzi yaliyotolewa nchini Uingereza yameiacha nchii hiyo na wakati mgumu wa kisiasa baada ya matokeo hayo kutompa mgombea yoyote wa vyama vya, Conservatives, Labour na Liberal Demokrati ushindi kamili wa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo. Matokeo hayo ambayo Conservatives ilipata viti 306 au asilimia 36%, Labour viti 258 asilimia 29% na Liberal demokrati 23%. Kufuatia matokeo hayo ya uchaguzi, serikali ya Uingereza itabidi iundwe na chama zaidi ya kimoja tangu hali hii ilipo tokea mwaka 1974. Picha hapo juu wanaonekana wagombea wa uongozi wa Uingereza wakati wa kampeni ya uchaguzi hivi karibuni, kutoka kushoto, David Cameroon, Nick Clegg na Gordon Brown. Taliban na Al Qaeda washirikiana zaidi.

Islamabad, Pakistan - 07/05/2010. Habari kutoka katika ofisi kuu za kijasusi za kimataifa zinasema yakuwa "kundi la Taliban na Al Qaeda zimekuwa na huusiano wa karibu zaidi kuliko hapo mwanzo na kuongea hali ya usamala kuwa wa mashaka kwa wanchi wa Afghanistan na nchi zinazo pakana na nchi hiyo."
Wachunguzi wa mambo ya kijasusi walizidi kusisitiza habari hizi hasa kwa kuzingatia uwezo wa mwanzo wa kundi la Taliban.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wapiganajiwa kundi la Taliban ambao wamekuwa wanapigana na majeshi ya kimataifa nchini Afghanistan.

Thursday, May 6, 2010

Nigeria yapata msiba mkubwa.

Nigeria yapata msiba mkubwa.

Lagos, Nigeria 06/05/2010. Aliyekuwa rais wa Nigeria,Umuru Yar'Adua amefariki dunia leo baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Marehemu, Umuru Yar'Dua alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa na hata aliweza kwenda nchi za Kiaarabu kwaajili ya matibabu zaidi na baadaye aliweza kurudi nchi Nigeria mapema mwezi wa Februari.
Kufuatia kifo hicho, aliyekuwa makamu wa rais Jonathan Goodluck ameapishwa kuwa rais wa Nigeria baada ya kifo cha aliyekuwa rais umuru Yar'Dua. Picha hapo juu anaonekana hayati raia wa Nigeria, Umuru Yar'Dua enzi za uahai wake akiongea katika mkutano mmoja wapo.
Picha ya pili wanaonekana wanajeshi wa Nigeria, wakiwa wamebeba mwili wa marehemu rais wa Nigeria Umuru Yar'Dua kuelekea kijijini kwa ambapo alipewa pumuziko la milele mbele ya familia, ndugu,wananchi na raia wa sasa Goodluck Jonathan.
Picha ya tatu anaonekana akiapa kuwa rais wa Nigeria baada ya kutangazwa ya kuwa rais Umuru Yar'Dua amefariki dunia.
Jeshi la Urussi laokoa meli ya iliyotekwa nyara.
Moscow, Urussi - 06/05/2010. Jeshi la wanamaji la Urussi limeikomboa meli iliyo kuwa imetekwa na maharamia wa Kisomalia siku chache zilizo pita katika maeneo ya bahari ya Ghuba ya Uajemi.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi alisema "Katika harakati za kutaka kuikomboa meli hiyo maharamia 10 walifariki dunia na wengine walikamatwa."
Meli hiyo ambayo ilikuwa inawafanyakazi wapatao 23 ambapo meli hiyo ilikuwa imebeba mafuta yenye thamani ya $52 million kuelekea nchini China.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya maharamia wa Kisomalia wakiwa katika ufukwe wa wa pwani ya Somali.

Saturday, May 1, 2010

Nchi ya Chad kukumbwa na janga la ukame na njaa.

Omar al Bashir ahaidi kutumikia Wasudani wote. Khatoum, Sudan - 01/05/2010. Rais mchaguliwa wa Sudan, Omar al Bashir, amwataka wananchi wa Sudan kushirikiana katika kukabiliana matatizo ambayo yanaikabili nchi hiyo.Omar al Bashir aliyasema hayo baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa kugombea kiti cha urais uliofanyika mapema mwezi uliopita nchini Sudan. Uchaguzi huo wa kushirikisha vyama vingi ulifanyika huku baadhi ya vya kususia uchaguzi huo Kwa upande wake Omar al Bashir, alisema " mmenichagua kuwa kiongozi wenu na hivyo nitaingoza nchi yangu kwa manufaa ya wananchi wote wa Sudan." Picha hapo juu ni picha kubwa ya rais Omar al Bashir, aliyechaguliwa kuiongoza tena Sudan huku chini ya picha wanaonekana wanchi ambao wanamuunga mkono rais Omar al Bashir wakishangilia baada ya ushindi kura kutangazwa. Nchi ya Chad kukumbwa na janga la ukame na njaa. N'djamena,Chad-01/05/2010. Shirika moja la kimataifa linalo shughulika na kutoa misaada limedai nchi ya Chad inahali mbaya kutokana na ukame ambao unendelea kuikumba nchi hiyo. Hata hivyo shirika hilo limesema " Wanachi wa Chad, wanakabiliwa na hali hiyo ikichangiwa na vita ambavyo vimechangia kuwepo na wakimbizi wengi wa ndani ya nchi na kusababisha hali ya uzalishaji kuwa mgumu hasa kwenye sehemu zile ambazo kuna unafuu wa hali ya ukame." Picha hapo juu anaonekana mama akiwa na mtoto wake ambaye anaonekana kutokuwa na afya nzuri kutokana na utapia mlo. Madawa yatakiwa kurudishwa" Hayakufikia kiwango"

New York. Amerika - 01/05/2-10. Kampuni ya kutengeneza madawa imeitisha madawa ambayo yalikuwa tayari kutumika kutibu, baada ya kufahamika yahakuwa yamefikia kiwango cha bora.
Kwa mujibu wa msemaji wa McNEil, " imebidi dawa zote za aina ya,Tylenol,Zyrtec, Motrian na Benadryl zirudishwe ili kutathmini na kuzihakiki."
Nchi zitakazo athirika ni Amerika-US,Canada,Jamuhuri ya Dominika, Guan, Guatemala,Jamaika, Puerto Rico, Panama, Trinida & Tobago,Kuwait na Fiji.
Picha hapo juu zinaonekana baadhi ya madawa ambayo yanatakiwa yarudishwe kwaajili ya kutathminiwa upya na wataalamu wa madawa.