Wednesday, August 31, 2011

Mahakama kuu yapingana na serikali juu ya wakimbizi nchini Australia.

Waumini wa dini ya Kislaam washerekea kumaliza mwezi wa Ramadhani.
Makka, Saud Arabia 31/08/2011. Waumini wa dini ya Kislaam duniani wamesherekea sikukuu ya Iddi baada ya kumaliza mwezi wa Ramadhani.
Sikukuu ya Iddi huwa inasherekewa na waumini wa dini ya Kislaam kwa kumaliza mwezi Ramadhani baada kufunga -kwa kujizuia kula kwa kipindi chote cha mwezi mzima ikiwa njia ya kuomba toba.
Mwezi huu wa Ramadhani, waumini wa dini ya Kislaam, huwa wanaamini ya kuwa nikipindi cha kufanya mema na kutafakali yale yote waliyo yafanya na pia kumwomba "Mungu awasamehe zambi kwa huruma yake." Pia kuangali ni kwa kiasi gani watajitahidi kufanya mazuri zaidi katika maisha yanayo fuata.
Mahakama kuu yapingana na serikali juu ya wakimbizi nchini Australia.
Sedney, Australia - 31/08/2011. Mahakama kuu nchini Australia imezuia amri ya serikali ya kutaka kubadilishana wakimbizi waliopo nchini humo na wakimbizi waliopo nchini Malaysia.
Uamuzi huo wa mahakama umekuja baada ya serikali ya Australia na Malaysia kukubaliana kubadilishana wakimbizi mapema mwezi May mwaka huu.
Makubaliano hayo yalikuja wakati mawaziri wakuu wa nchi hizo walipokutana na kujadili mbinu za kuzuia biashara ya kusafirisha watu kati ya nchi hizo.
Katika kutoa hukumu hiyo, mahakama ilisema "Malaysia siyo nchi mwanachama katika makubaliano ya maswala ya ukimbizi ya mwaka 1959 chini ya umoja wa mataifa na hivyo wakimbizi wanatakiwa wapewe haki sawa kwa kufatia sheria za kimataifa na zakitaifa."

Tuesday, August 30, 2011

Zimwi la vita vya Irak bado la mwandama Tony Blair.

Zimwi la vita vya Irak bado la mwandama Tony Blair.
London, Uingereza - 30/08/2011. Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair anakabiliwa na wakati mwingine mgumu baada ya aliyekuwa mkuu wa usalama wa MI5 kudai alimwonya kuhusu vita vya Iraq.
Blair anakabiliwa na wakati mgumu baada yaaliyekuwa mkuu wa usalama wa MI5 Baroness Manningham-Buller kusema ya kuwa alimtahadhalisha na kumtaka ashughulikie kwa ukaribu zaidi vita zidi ya kundi la Al Qaeda.
Manningham-Buller aliongea kwa kusema "nilimwonya nakumweleza ya kuwa kitendo cha kuimshambulia serikali ya Sadam Hussein kijeshi, kutafanya hali ya usalama wa nchi kuwa na matatizo na hasa kutaonekana kama kushambulia dini ya Kiislaam, na ingefaa tuelekeze nguvu katika kupambana na kundi la Al Qaeda ambalo lina maficho nchini Afghaistan, kwani Irak haikuwa tishio katika usalama wa Uingereza."
Barroness Manningam-Buller ambaye amestaafu kazi mwaka 2007, aliongezea kwa kusema "vita vya Irak vimevuga mkakati wa kupambana na kundi la AlQaeda."
Kufuatia kauli hiyo ya mkuu wa usalama wa MI5, kumefanya baadhi ya wanasiasa kuanza kuuliza maswali mengi kwanini Uingereza iliishambulia Irak.
Mke wa Gaddafi na watoto wake wakimbilia Algeria na wapinzani watoa onyo la mwisho.
Algiers, Algeria -30/08/2011. Mke wa pili wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amekimbilia nchini Algeria pamoja na watoto wake.
Habari kutoka ofisi ya wizara ya mambo ya nchi za nje zimesema " Safia Gaddafi aliwasi saa 08:45 na watoto wake Aisha, Hannibal na Mohammed na tumewapokea kiutu jambo ambalo kila mtu anahitaji kupewa."
Mahmud Shammam msemaji wa serikali ya mpito alisema " kitendo cha Algeria kuipokea famila ya Gaddafi ni kinyume na matwakwa ya Walibya na tutaomba warudishe nchini Libya waje wajibu mashitaka ya kutumia mali ya umma vibaya."
Serikali ya Algeria ilikuwa na uhusuano mzuri na serikali ya Muammar Gaddafi kwa kipindi kilefu na mpaka sasa imekataa kuitambua serikali ya mpito ya Libya.
Wakati huo jeshi la serikali ya mpito limetoa onyo la mwisho kwa wanajeshi ambao wanamuunga mkono Muammar Gaddafi kusalimu amri au kuwatayari kwa mapambano ikifika siku ya Jumamosi.
Onyo ilo limekuja wakati jeshi la wapinzani likiwa limezingira mji Sitre ambao unasadikiwa kuwa kuna nguvu nyingi za kijeshi na nimji alio zaliwa Muammar Gaddafi.
Mahakama ya haki za binadamu yakataa maombi ya Kenya.
Nairobi, Kenya -30/08/2011.Rufaa ya serikali ya Kenya kwenye mahakama ya kutetea haki za binadamu imekataliwa na mahakama iliyopo nchini Uhollanzi.
Rufaa hiyo ambayo ilikuwa imeitaka mahakama ya Hague kusimamisha kesi zidi ya washitakiwa sita akiwemo makamo wa waziri mkuu, mawaziri , mmoja wa mkuu wa polisi na viongozi wengine waliohusika katika kuchochea machafuko baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa mwaka 2007.
Kesi hiyo ina tarajiwa kuanza siku ya Alhamisi wiki hii, ambapo washitakiwa hao wanatakiwa kujibu mashitaka zidi yao kwa kuhusika na machafuko yaliyo sabaisha mauaji na mali nyingi kuteketea.
Kesi hiyo ilifunguliwa baada ya mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo Luis Moreno -Ocampo kumaliza uchunguzi wake aliyo ufanya nchini Kenya baada ya machafuko kutokea.
Serikali ya Zimbabwe yamfukuza balozi wa Libya.
Harare,
Zimbabwe - 30/08/2011. Serikali ya Zimbabwe imemfukuza balozi wa serikali ya mpito ya Libya baada ya kutamka ya kuwa anaunga mkono serikali ya mpito iliyo mpindua Muammar Gaddafi.
Taher Elmagrahi, alitangaza kuiunga mkono serikali ya mpito na kujiunga nayo baada ya serikali ya Muammar Gaddafi kung'olewa hivi karibuni na jeshi la wapinzani.
Simbarashe Mumbengegwi waziri wa mambo ya nchi za nje wa Zimbabwe alisema " Elmagrahi na wafanyakazi wote wa ubalozi wanatakiwa kuondoka nchini katika kipindi cha masaa 72."
Hata hivyo Taher Elmagrahi aliseme " mimi siyo mtu wa Muammar Gaddafi nipo kwa aajili ya Walibya na nawakilisha Walibya."
Serikali ya Zimbabwe na Libya zimekuwa na uhusiano wa karibu sana, hasa kati ya Muammar Gaddafi na rais Robert Mugabe.

Monday, August 29, 2011

Mbu wa malaria waelekea kupungua nchini Tanzania.

Serikali ya Marekani kukabiliana na maafa ya Irine.
Washington, Marekani - 29/08/2011. Kimbunga na mafuriko ambacho kimetokea nchini Marekani kimesababisha uaribifu mkubwa na kupoteza maisha ya watu kwa mujibu serikali.
Mafuriko hayo na kimbunga ambacho kilianza wiki iliyopita yamesababisha nyumba na barabara kubomoka na kufanya hali ya maisha na mawasiliano kuwa ngumu.
Craig Fugate mkurugenzi mkuu wa maswala ya maafa alisema" serikali ina kibarua kigumu na itajitahidi kuwasaidia wale wote waliokumbwa na kumbunga Irine na kiasi cha mamillioni ya dola zinahitajika haraka sana ili kuanza kutoa huduma."
Kimbunga na mafuriko yaliyo sababishwa na Irine kimefuatia kimbunga Katalina kilicho sababisha maafama makubwa miaka michache iliyopita nchini Marekani.
Mbu wa malaria waelekea kupungua nchini Tanzania.
Dar es Salaam, Tanzania - 29/08/2011. Watafiti wa malaria nchini Tanzania wamedai yakuwa mbu ambao wanasababisha ugonjwa wa malaria wanaelekea kupungua.
Wanasayansi wa Tanzania na Denmarki wamegundua upunguaji wa mbu hao baada ya kufatilia idadi ya mbu ambao walikuwa wanapatikana na viini vya ugonjwa huo.
Profesa Dan Meyrowisch, alisema " upunguaji wa mbu hao ni kitu ambacho kinatakiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi, ingawa inaweza sababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa na ukame."
Mpango wa kupambana na malaria umekuwa ikipewa kipao mbele ili kutokomeza malaria katika bara la Afrika ugonjwa ambao umekuwa unasababisha vifo vingi hasa kwa watoto wadogo.
Mshukiwa wa ulipuaji wa ndege ya Pan am jet anahali mbaya kuliko ilivyo zaniwa.
Tripol, Libya 29/08/2011. Mshukiwa ambaye inasadikiwa alihusika katika ajali ya ndege Pan Am Jet amekuwa na hali mbaya kiafya kuliko ilivyozaniwa na viongozi na wanasiasa wa Uingereza na Marekani.
Mohmed al Megrahi, ambaye aliachiwa huru mwaka 2009 na serikali ya Scotland na kurudi nchini mwake Libya baada ya kujilikana ya kuwa ana ugonjwa wa saratani- kansa ambayo itamfanya kutokuishi kwa muda mrefu.
Kuruhusiwa kwa Al Mergahi kumeleta mvutano kati ya wanasiasa na viongozi wa Uingereza na Marekani kwsa wengine kudai yakuwa arudishwe nchini Scotland kuendelea na kifungo.
Khaked al Megrahi, mtoto wa Mohmed Megrahi amesema " baba yangu ni mgojwa sana nahakuna mganga wala muhudumu ambaye tunawasiliana naye na hakuna msaada wowote tunapata, baba anatumia oksijeni na dawa zake zimekwisha hivyo tupo naye na hatujui nini la kufanya."
Waziri wa sheria wa serikali ya mpito Mohamed al Alagi alisema, hakuna Mlibya yoyote atakaye pelekwa nchi za magharibi ili kujibu mashitaka, hivyo Mohmed al Megrahi atapelekwa kokote."
Nayo serikali ya Scotland imesema " alifanya jambo la kiutu na Mohmed al Magrahi hatarudishwa nchini, na ushahidi umeonyesha yakuwa tulivyo amua kumuachia kwani hali yake sasa siyo nzuri."
Mashariki ya Uganda yakumbwa na maporomoko.
Kampala
,Uganda -29/08/2011. Mapoloka makubwa yameokea mashariki mwa Uganda na kusabaisha vifo vya watu na uharibifu mkubwa.
Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu Catherin Ntabade alisema " mvua kubwa iliyonyesha ndiyo iliyo sababisha maporokomo hayo na hadi sasa watu wapatao 23 wamepoteza maisha na watu wengine hawajulikani wapo wapi."
Serikali ya Uganda imepeleka kikosi cha waokoaji na misaada mingine ili kukabiliana na tukio hilo.
Maporooko kama haya yalitokea mwaka jana kwenye eneo karibu na mlima Elgon kwenye mpaka wa Kenya na Uganda na kuleta maafa makubwa kwa jamii na mazingira.

Sunday, August 28, 2011

Mapadri wazidi kujitoa katika Kanisa Katholiki nchini Kenya ili kuoa.

Al Qaeda namba mbili auwawa.
Islambad, Pakistan - 28/02/2011.Kiongozi wapili kimadaraka katika kundi la Al Qaeda ameuwawa nchini Pakistani.
Atiya Abdul Rahman raia wa Libya ambaye inaaminika alikuwa muhimu katika kupanga mbinu zote za mashambulizi la kundi la Al Qaeda na alikuwa anawasiliana moja kwa moja Osama Bin Laden ambaye aliuwawa miezi michache iliyopita.
Kifo cha Atiya Abdul Rahman, kinasadikiwa ni pigo kubwa kwa kundi hilo, kwani ndiye mtu ambaye alikuwa "anaweza kumsaidia kiongozi wa sasa wa Al Qaeda Ayman al Zawahiri katika kuimarisha kundi hilo."
Kifo chake kimetokea baada ya ndege ya kijeshi inayo endeshwa na ongozwa na mtandao kushambulia eneo alilo kuwa amejificha.
Kundi la Al Qaeda lina ongozwa na Ayman al Zawahiri,baada ya kifo cha kiongozi wa kundi hilo Osama bin Laden.
Mapadri wazidi kujitoa katika Kanisa Katholiki nchini Kenya ili kuoa.
Nairobi, Kenya - 28/08/2011. Zaidi ya mapadri 40 wameamu kujitoa katika kanisa Katoliki na kujiunga na Kanisa la Ekumenikal Katholik ili waweza kuoa na kuwa nafamilia kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Askofu wa Kanisa la Ekumenikal Katholik, Geoffrey Shiundu, ambaye alijitoa katika kanisa mama la Katholik baada ya kuamua kuoa, alisema "kanisa la Ekumenikal linazidi kukua na mapadri wanadizi kujiunga nalo."
"Tutaweza kushirikiana na kanisa mama la Katholik kama Papa Benedikt XVI atakubali kubadili muundo wa kanisa kwa kuweka huru, ikiwa padri anataka kuoa aoe na kama hataki basi abaki bila kuoa." Alisisitiza.
Askofu Shiundu aliyasema hayo wakati wa sherehe ya kumweka wakfu mmoja wa mapadri kwenye mji wa Kitale.
Libya yarudishiwa uanachama na jumuiya ya nchi za Kiarabu.
Kairo
,Misri - 28/07/2011. Shirikisho la nchi za jumuiya ya Kiarabu remeirudishia uanachama wake Libya baada yakuangushwa kwa utawala wa Muammar Gaddafi.
Msemaji wa jumuiya hiyo Nabil Elarab alisema " bendela mpya ya serikali ya mmpito itawekwa na ile ya serikali ya Muammar Gaddafi ambayo ilikuwa na rangi ya kijani itatolewa."
Libya ilitolewa katika jumuiya hiyo baada ya serikali ya Muammar Gaddafi kuanza kupambana na wapinzani waliokuwa wanaipinga serikali yake mapema mwezi wa pili mwaka huu.

Friday, August 26, 2011

Mlipuko wa bomu watokea katika majengo ya ofisi za umoja wa mataifa.

Umoja wa Afrika wachanga pesa ili kusaidia maeneo yaliyo kumbwa na ukame.

Adis Abeba, Ethiopia - 26/08/2011. Viongozi na marais wa Umoja wa Afrika wamekutana jijini Adis Abeba na kubaliana na kutoa mchango wa fedha kiasi cha £215milioni ili kusaidia maeneo ambayo yamekumbwa na ukame katika bara la Afrika.
Akiongea katika mkutano huo wa kuchangisha fedha, katibu msaidizi wa umoja wa mataifa Asha Rose Migiro alisema " bado tunaitajika kutoa misaada kwa wananchi wengi ambao wamekumbwa na ukame ili kuzuia janga la vifo na kupoteza kizazi kijacho cha bara la Afrika, na uwezo tunao wa kuzuia hali hii isiendelee kama tukishirikiana."
Katika mkutano huo pia benki ya Afrika iliahidi kuongeza juhudi zake za kuimarisha uchumi kwa kuwekeza zaidi katika miradi itakayo leta maendeleo kwa wananchi.
Kufanyika kwa mkutano huo wakuchangisha pesa, umekuja baada ya mashirika ya kimataifa kudai ya kuwa "umoja wa Afrika hauja lipa kipao mbele swala la kame lililo likumba bara hilo."
Serikali ya Uganda yatupilia mbali hukumu ya vifo kwa mashoga.
Kampala, Uganda - 26/08/2011. Serikali nchini Uganda limetupilia mbali muswada wa kutaka mashoga na kwa wale wote ambao wanapenda kufanya mapenzi kijinsia moja kupewa adhabu ya kifo.
Waziri wa serikali za mitaa, Adolf Mwesige alisema " serikali inapinga kitendo hicho, na kwa sasa kunasheria za kutosha za kushughulikia swala hilo."
Mswada huo wa kuwapa adhabu kali mashoga na watu wenyekupenda kufanya mapenzi kijinsia moja ulipendekezwa na mwaka 2009 na mbuge David Bahati, jambo ambalo lilifanya dunia nzima kutupia mcho yake nchini Uganda ili kutetea haki za watu hao.
Hata hivyo asilimia 90 ya wananchi wa Uganda wanapinga tabia za mashoga.
Naye mmoja wa watu ambao wanaunga mkoo kutupiliwa mbali kwa muswada huo alisema " huu ni ushindi kwa aliye kuwa mtetezi wetu David Katto, ambaye aliuwawa katika harakati za kutete haki sawa kwa kila Mganda."
Hata hivyo habari kutoka bunge la Uganda zinasema, "rais Yoweli Museveni, aliwaambia wabunge yakuwa wapunguze munkali na swala la mashoga, kwani kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kufanywa katika kuinua maisha ya wananchi.
Mlipuko wa bomu watokea katika majengo ya ofisi za umoja wa mataifa.
Abuja, Nigeria -26/08/2011. Milipuko ya mabomu imetokea katika jengo ambalo kuna ofisi za umoja wa mataifa na kuleta maafa makubwa.
Kwa mujibu wa mashaidi walio ona tukikio hilo walisema" mlipuko huo ulitokea baada ya gari moja kuvuka kizuizi cha kuingilia katika jengo hilo."
Naye katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban ki - Moon amelaani kitendo cha kulipuliwa ofisi za umoja huo na muuaji wa kujitolea muanga kwa kusema " ni kitendo hambacho hakionyeshi nia njema kwa wale wote ambao wanajitolea kufanya kazi ya kusaidia jumuiya za kimataifa."
Kufuatia mlipuko huo katibu msaidizi Rose Migiro atawasili nchini Nigeria ili kuongea na viongozi serikali na kupata habari kamili kwa ajili ya kuziwakilisha kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa.
Naye msemaji wa polisi Yemi Ajavi alisema "watu kadhaa wameumia vibaya na wengine kupoteza maisha na inaonekana kama ni mauaji ya kujitolea muhanga na mpaka sasa bado tupo katika harakati za uokoaji kwani kuna baadhi ya watu bado wamekwama ndani ya jengo hilo."
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amelaani kitendo hicho na kusema " serikali itafanya kila njia kuwakamata wale wote walio husika katika mashambulizi hayo."
Kundi linalo julikana kama Bokaharamu limedai kuhusika na ulipuaji wa ofisi hizo za umoja wa mataifa, na kusema " uhu ni mwanzo wa kujibu mashambulizi baada ya serikali kutuma jeshi lake katika eneo la Kaskazini la Borno na kuna watu 100 ambao wapo tayari kujitolea muanga." Alisema msemaji wa kundi hilo Abu Darda.
Mlipuko huu wa bomu katika ofisi za umoja wa mataifa ni moja ya milipuko ya mabomu ambayo imekuwa ikitokea nchini Nigeria ambapo hivi karibuni bomu lililipuka katika ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi jijini Abuja.

Thursday, August 25, 2011

Zawadi nono kutolewa kwa atakaye toa habari alipo Gaddafi akiwa mzima au amekufa.

Jean-Pierre Bemba kugombea urais wa Kongo DR.
Kinshasa, Kongo DR - 25/08/2011. Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Kongo, naambaye yupo chini ya mahakama ya kimataifa ya kuzuia hualifu amehaidi kugombea kiti cha urais katika uchaguzi unao tarajiwa kufanyika mwisho wa mwaka 2011.
Jean Pierre Bemba ambaye ni kiongozi wa chama- MLC, Movement Liberation of Congo amesema hayo kupitia mwanasheria wake Aime Kilolo ya kuwa "atagombani kiti cha urais ijapokuwa yupo na kesi."
Memba ambaye alikamatwa 2008 nchini Uberigiji na kufunguliwa kesi ya kukiuka haki za binadamu kwenye mahakama ya kutetea haki za binadamu iliyopo Hague nchini Uhollanzi wakati wa jeshi lake lilipo kuwa linapambana na jeshi la serikali kati ya mwaka 2002 na 2003
Habari zilizo patikana zinamsema akiwa kizuizini Jean Pierre Bemba ameweza kutana na wakongo wengi wakiwemo viongozi wa upinzani Etiene Tshisekedi, Vital Kamerhe na Leon Kengowa Dondo.
Zawadi nono kutolewa kwa atakaye toa habari alipo Gaddafi akiwa mzima au amekufa.
Benghazi,
Libya -25/08/2011. Serikali ya mpito ambayo inapambana katika kuing'oa madarakani serikali ya Libya imetangaza kutoa zawadi ya fedha kwa mtu yoyote atakaye toa habari wapi yupo kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi ili akamtwe akiwa mzima au amekufa.
Guma el Gamaty ambaye ni mmoja wa viongozi wa serikali ya mpito, alisema " hii ni nafasi ya dhahabu ya $ 1.7million zitatolewa ikiwa mtu yoyote atatoa habari za kupatikana kwa Muammar Gaddafi"
Zawadi hii imetolewa na wafanya biashara kwa kusaidia na serikali ya mpito ambayo wapiganaji wake wanapigana na serikali ya Muammar Gaddafi.
Nayo serikali ya Itali imekubali kuachilia pesa za zilizo kuwa za serikali ya Muammar gaddafi ili kusaidia serikali ya mpito.
Hadi sasa Muammar Gaddafi na familia yake hawajulikani wapo wapi, baada ya kundi la upinzani kuingia katika jiji la Tripoli hivi karibuni.

Wednesday, August 24, 2011

Muammar Gaddafi ahaidi kufa au kupata ushindi.

Samuel Eto'o avunja rekodi ya dunia kuwa mchezi wa mpira wa miguu kwa kulipwa pesa nyingi.
Dagestan, Urussi 24/08/2011. Mchezaji maharufu wa mpira waamiguu wa timu ya taifa ya Kameroon na Inter Milan Samuel Eto'o amevunja rekodi ya duia kwa kuwa mchezaji atakeye lipwa pesa nyingi baada ya kusaini mkataba na timu ya Anzhi Makhachkala iliyopo katika jimbo la Dagestan.
Samuel Eto'o , ambaye ameshinda kombe la ligi ya vilabu bingwa vya ulaya wakati akichezea timu Barcelona na Inter Milan, anatarajiwa kupokea kiasi cha 28.8million kwa muhula baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kuchezea timu hiyo.
Eto'o atakuwa anapokea kiasi cha 350,000 kwa wiki kuliko wacheza wengine maarufu dunia ambao ni Wesley Snijder anapokea 250,000 kwa wiki, Christian Ronaldo 210,000 na mchezaji bora wa dunia Lionel Messi 180,000.
Akiongea baada ya kusaini mkataba Eto'o alisema " napenda kuwashukuru wapenzi na viongozi wa Inter Milan kwa kuonyesha mapenzi na ushirikiano kwa kipindi chote nilipo kuwa mchezaji na mkazi wa jiji la Milani.
Mapambano ya kikabila kutishia amani Kusini mwa Sudani.
Juba, Sudani ya Kusini -24/08/2011.Shirika la umoja wa mataifa -UNMISS - linaloshirikiana na serikali ya Sudani ya Kusini-,limeonya ya kuwa mauaji ya kikabila bado yanaendelea katika jimbo la Jongle.
Katika ripoti iliyo tolewa na shirika hili zinasema " watu wa jamii ya Murle na Lou Nuer wamekuwa wakipigana katika harakati za kutaka kila jamii iwe na mifugo mingi jambo ambalo ilinatishia amani katika eneo hilo"
Ripoti hiyo imeongezea ya kuwa katika maeneo hayo "bado kuna uhaba wa mahitaji muhimu ya kijamii."
Hata hivyo habari kutoka serikali ya Sudani ya Kusini zinasema " eneo hilo limeanza kupewa kipao mbele na itachukua muda kukamilisha miradi yote kutokana na mazingira ya kijiografia."
Sudani ya Kusini iliundwa baada ya kura ya maoni ya kutaka eneo hilo lijitenge kutoka serikali ya Kartoum, na kujitangazia utawala wake hivi karibuni.
Muammar Gaddafi ahaidi kufa au kupata ushindi.
Libya, Tripol -24/08/2011.Kiongozi wa Libya amelihutubia taifa kwa kutumia redio, huku mahali alipo ajulikani baada ya jeshi la wapinzani kuchukua makazi ya kiongozi huyo ya Bab al Aziziya na karibu maeneo ya jiji la Tripol.
Kanali Muammar Gaddafi, alisema "tunapigana vita zidi ya wasaliti wa Libya na katika mapambano haya kuna mambo mawili kufa au ushindi, na kitendo cha mimi kutoka hapo Bab al Aziziya ni mbinu za kujipanga tayari kwa mashambulizi, kwani tulijua ya kuwa NATO walikuwa wanataka kushambulia eneo hilo."
Naye msemaji wa serikali ya Libya, Mussa Ibrahim, akisisitiza kwa kupitia TV kutoka eno lisilo julikana alisema " Libya itakuwa na mlipuko wa volkano, majivu na moto na tunauwezo wa kupigana kwa muda mrefu."
Hata hivyo viongozi wa serikali ya mpito wamedai yakuwa "Muammar Gaddafi ameshaangushwa na tunampango wa kuamishia ofisi zote jijini Tripoli muda si mrefu na tunaendelea kumsaka hadi tu mkamate na ndipo Walibya watakuwa huru."
Hadi kufikia sasa Muammar Gaddafi na familia yake awajulikani wapo wapi jambo ambalo bado lina leta mashaka kwa serikali ya mpito.
Makampuni ya mafuta kusuguana vichwa baada ya kuanguka kwa Gaddafi
Paris
,Ufaransa 24/08/2011.Viongozi na wafanya biashara wa maampuni ya mafuta wamekuwa wakivutana nyuma ya ukuta na kusuguana vichwa, katika majadiliano ya keweza kukubaliana na serikali ya mpito ya Libya ni kwa jinsi gani uchimbaji na upatikanaji wa mafuta utakavyo kuwa.
Hali hii inakuja baada ya serikali ya mpito kutangaza ya kuwa itaaangalia mikataba yote iliyo wekwa na serikali ya Muammar Gaddafi.
Habari kutoka ndani ya serikali hiyo ya mpito zinasema, " makampuni yote ambayo yanatoka kwenye serikali ambazo hazikushiriki katika kuunga mkono kung'olewa kwa Gaddafi huenda mikaaba yao ikafutwa."
Kufuatia habari hizi baadhi ya serikali zilizo tiliana mikataba na serikali ya Gaddafi "zimeshaanza mikakati ya kutaka kulinda mikataba hiyo kwa kila hali."
Libya ni moja ya nchi yenye utajiri mkubwa wa mafuta na tangu kuanza kwa vita nchin humo bei katika soko la mafuta imekuwa ikiyumba.

Tuesday, August 23, 2011

Kesi zidi ya Dominik-Strauss Kahn yafutwa na aachiwa huru.

Kesi zidi ya Dominik-Strauss Kahn yafutwa na aachiwa huru.
New York,
Marekani - 23/08/2011. Jaji wa mahakama amefuta kesi zidi ya aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la fadhe la kimataifa baada ya kesi hiyo kutokuwa na ushaidi wa kutosha.
Jaji Michel Obus aliamua kufuta kesi hiyo baada ya mwanasheria kwa upande wa mashitaka kudai ya kuwa "kesi zidi ya Dominik Strauss-Kahn haina ushaidi wa kutosha kwa kuzingatia ukweli wa bi Diallo ambao ameusema alipo wasili nchini Marekani."
Mwanasheria Kenneth Thompson ambaye anamtete mshitaki alisema" mwanasheria wa serikali ameamua kutokubaliana na haki ya mwanamke asiyekuwa na makosa kuweza kupata haki yake kutokana mambo yaliyomtokea."
Baada ya uamuzi wa mahakama kufuta kesi, familia ya Strauss-Kahn ilisema " kipindi chote cha kesi hii familia yetu ilikuwa aina furaha na kuanzia sasa tunaweza kuanza upya maisha ya kujenga familia yetu ."
Kufuatia uamuzi wa mahaka kufuta kesi, Dominik Strauss-Kahn yupo huru na anaweza kusafiri kurudi nchini kwake Ufaransa.
Dominik Strauss-Kahn alifunguliwa mashitaka baada mfanyakazi katika hotel aliyo kuwa amefikia kufungua kesi ya ubakwaji zidi yake.

Vita vya LIbya vyaingia sura mpya na Saif al Islaam yupo huru.

Afrika ya Kusini na Burundi zasahini mikataba ya kiuchumi.
Bujumbura, Burundi -23/08/2011. Serikali za Afrika ya Kusini na Burundi zimetiliana sahii mikataba ya kiuchumi kati ya nchi hizo ili kuimarisha maendeleo na kukuza ukaribu zaidi
Mikataba hiyo ilisainiwa wakati rais wa Afrika ya Kusini, Jakob Zuma alipo fanya ziara ya kiserikali nchini Burundi, ili kudumisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo mbili, na kwa kuzingatia rais Jacob Zuma alikuwa mmoja wa wasuruhishi katika jitihada za kuleta amani nchini Burundi.
Katika mikataba hiyo nchini hizo zitashirikiana katika sekta za kilimo,usafiri na kifedha, ambapo kutaongezea nguvu kiuchumi hasa kwa nchi ya Burundi ambayo ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu hadi vilipo kwisha hivi miaka ya karibuni.
Vita vya Libya vyaingia sura mpya na Saif al Islaam yupo huru.
Tripoli
, Libya - 23/08/2011.Mtoto wa kiume wa kiongozi wa Libya ameonekana na kuongea na waandishi wa habari, masaaa machache baada ya kundi la upinzani kutangaza yakuwa wame mkamata yeye na ndugu zake.
Huku akishangiliwa na wadau na wale wanao muunga mkono baba yake, Saif al-Islaam alisema " mimi nipo na kundi la wapinzani limekwisha na utiwake wa mgongo umesha uvunja. Na baba yangu yupo salama na tutashinda zidi yawale wanaotaka mali ya Libya."
Pia alimalizia kwa kusema" kesi zidi ya mahakama ya kimataifa ya Uhollanzi hainisumbui kichwa na kwasasa kundi la upinzani limekwisha na jiji la Tripol lipo chini ya mikono yetu."
Kufuatia kuoneana kwa Saif al Islaam, viongozi wa kimataifa wamekuwa wakitoa maelezo tofauti na kusisitiza yakuwa muda si mrefu utawala wa Muammar Gaddafi utaporomoka na Libya itakuwa huru.
Saif al Islaam ambaye alizaniwa kuchukua madaraka ya baba yake, amekuwa ndiye msemaji mkuu wa serikali ya baba yake na kuhaidi yakuwa serikali ya baba yake itashinda.

Monday, August 22, 2011

Serikali ya Tanzania yaonya viongozi wanaoshiriki biashara ya madawa ya kulevya.

Serikali ya Tanzania yaonya viongozi wanaoshiriki biashara ya madawa ya kulevya.
Dar es Salaam, Tanzania - 22/08/2011. Serikali ya Tanzania imeonya yakuwa wale viongozi wa dini na serikali wanao tumia madaraka yao katika kufanya biashara ya madawa ya kuleva watakamatwa muda si mrefu.
Akiongea na waandishi wa habari, mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya
Godfley Nzowa alisema "tumepata majina ya watu wanaohusika na biashara hizo na bado tunafanya kazi ya uchunguzi zaidi ili kuwakamata wahusika wate. Na kunabaadhi ya majina tuliyo nayo ni yaviongozi wa dini na serikali wanaohusika katika biashara hiyo haramu."
Akijibu shutuma hizo kiogozi wa kanisa Katoliki, Kadinal Polycarp Pengo aliomba serikali iwataje viongozi hao wa dini ili kuthibitisha ukweli huo na kujenga imani kwa wananchi.
Onyo hilo limekuja baada ya ripoti kutoka ofisi za umoja wa mataifa zinazo shughulika na kupambana na madawa ya kulevya kuelezea ya kuwa "eneo la Afrika Mashariki limekuwa nikitovu cha kupitishia madawa ya kulevya kutokea Pakistani na sehemu tofauti duniani na kuwa ndio biashara kubwa inayo fanywa na wafanya biashara wakubwa na kukuza uharifu katika nchi za maeneo haya."
Serikali ya Afrika ya Kusini kuwa mwenyeji mkutano wa hali ya hewa na mazigira.
Durban, Afrika ya Kusini - 22/08/2011.Idara inayoshughulikia haliya hewa na mabadiliko yake ya umoja wa mataifa imeaanza maandalizi ya mkutano utakao fanyika nchini Afrika ya Kusini kuanzia Desemba 4 mwaka huu.
Kwa mujibu wa habari zinasema, "mkutano huo utawakusanyisha wajumbe wapatao 20,000, viongozi na wakuuu wa nchi wapatao 100."
Mkutano huo ambao ni moja ya mikutano ya kujadili hali halisi ya mabadiliko ya hali ya hewa,utajadili mikakati ya kupambana na uharibifu wa mazingira unaofanywa duniani kote.
Jiji la Tripoli lazungukwa na milio ya risasi baada ya jeshi la wapinzani kuingia.
Tripoli, Libya 22/08/2011.Jeshi la kundi la upinzani linalo pingana na serikali ya Libya limeingia jiji Tripoli kwa mara ya kwanza na kukamata badhi ya maeneo katika jiji la Tripoli.
Msemaji kundi hilo la kijeshi Guma El- Gamati alisema " Wapiganaji wetu wanashikilia karibu sehemu zote za jiji la Tripoli na jeshi la serikali lina shikilia maeneo matatu ambayo ni hospital, kambi ya kijeshi na Rixo Hotel na baadhi ya wapiganaji wa jeshi la Libya wamekuwa katika mazungumzo ya kusalimu amri ili kujisalimisha kwa jeshi letu."
Na habari kutoka kwa kiongozi wa jeshi la upinzani zinasema " mtoto wa Muammar Gaddafi ,Saif al Islam Gaddafi amekamatwa na jeshi hilo la upinzani na sasa yupo chini ya ulinzi wao."
Hata hivyo hakuna habari kutoka serikali ya Libya juu ya kukamatwa kwa mtoto huyo wa Muammar Gaddafi, ila msemaji wa serikali Mussa Ibrahim alisema mashambulizi yalyofanywa siku ya jumapili yameua zaidi ya raia 1,00 na zaidi ya 5000 kujeruhiwa vibaya."
Kufuatia kuingia kwa kundi hilo la upinzani jijini Tripoli, milio ya risasi imekuwa ikisikika karibu kila eneo ndani ya jiji hilo.
Mapigano kati ya jeshi la kundi la wapinzani na serikali ya MuammarGaddafi yalianza mapema mwezi machi na hadi sasa yameshafikisha miezi sita.

Sunday, August 21, 2011

Serikali ya Kenya yakasirishwa na Luis Moreno Ocampo.

Serikali ya Kenya yakasirishwa na Luis Moreno Ocampo.
Nairobi, Kenya - 22/08/2011. Serikali ya Kenya imekasirishwa na kitendo cha mwanasheria mkuu wa mahakama ya makosa ya jinai iliyopo nchini Uhollanzi, kwa kuihusisha ikulu katika machafuko ya kisiasa yaliyo tokea nchini humo.
Habari kutoka ikulu zinasema, "ofisi ya rais imekasirishwa sana na Luis Moreno Ocampo kuwahusisha wafanya kazi wa karibu wa rais Mwai Kibaki katika machafuko ya kisiasa."
Hata hivyo habari kutoka ofisi ya Luis Moreno Ocampo zinasema " ripoti hiyo haikuwahusisha rais na waziri mkuu wa Kenya."
Ripoti hiyo ya Luis Moreno Ocampo imekuja baada ya uchunguzi uliyo fanywa na ofisi yake nchini Kenya, baada ya machafuko yaliyo leta hasara kwa raia na mamia kupoteza misha kabla na baada ya uchaguzi mkuu uliyofanyika nchini humo mwaka 2007 .
Wamarekani wahukumiwa kwenda jela nchini Iran.
Tehran,
Iran -22/08/2011. Mahakama nchini Iran imewahukumu raia wawili wa Marekani kwenda jela kwa kosa la kuingia nchini humo kinume cha sheria na kufanya ukachelo wa niaba ya serikali ya Marekani.
Watuhumiwa hao, Josh Fattal na Shane Bauer walihukumiwa kwenda jela miaka minane kila mmoja, baada ya ya mahakama kuwakuta na hatia na kuamua kuwahukumu miaka mitano kila mmoja kwa kosa la kufanya ukachelo na miaka mitatu kila mmoja kwa kosa la kuingia nchini Iran kinyume cha sheria.
Mwanasheria anaye wawakilisha wa Marekani hao alisema " natumani wateja wangu wataachiwa kwa msamaaha wa serikali, baada ya wazazi wa watuhumiwa hao kuiomba serikali ya Iran kuwaachia kwa kuzingatia ni mwezi mtukufu wa Ramdhani, kwani hawakufanya makosa yoyote"
Josh na Shane walikamatwa 31/Julai/2009 baada ya serikali ya Iran kudai walikuwa wamevuka mpaka na kuingia nchini humo kutokea eneo la Kikurdish lililopo nchini Irak.

Friday, August 19, 2011

Rais wa zamani wa Ivory Cost afunguliwa mashitaka.

China na Marekani zakutana kujadili mabadiliko uchumi.
Beijing, China 18/08/2011. Serikali za China na Marekani zimekubaliana kuendelea kufanya biashara ingawa kuna baadhi ya vikwazo ambavyo vipo kati ya nchi mbili hizo.
Makamu wa rais wa China akimkaribisha mgeni, wake makamu wa rais wa Marekani Joe Biden,ambaye yupo ziarani nchini China, Xi Jinping alisema "Marekani ni nchi ambayo inatakiwa kuimarika kiuchumi,kwani uchumi wake ni kiungo cha duniani."
Makamu wa rais Joe Biden yupo nchini China ilikujadili maswala ya kiuchumi na biashara na serakali ya China .
Hata hivyo habari kutoka serikali ya China zinasema, makamu wa rais Xi Jinping atazungumzia swala la Marekani kutaka kuuzia Taiwani zana za kijeshi.
Rais wa zamani wa Ivory Coast afunguliwa mashitaka.
Abidjani
, Ivory Coast 12/08/2011.Rais wa zamani wa Ivory Coast amefungulia mashitaka ya kutumia mali ya umma vibaya wakati akiwa madarakani .
Laurent Gbagbo, ambaye alitolewa madarani kwa nguvu na jeshi la rais wa sasa Alassane Outtara, anakabiliwa kujibu mashitaka ya kutumia fedha na mali za serikali kabla na baada ya uchaguzi kwa manufaa ya kumsaidia kubaki madarakani.
Hata hivyo wasemaji wa kutetea haki za binadamu, hawakulizika na kesi hiyo kwa madai ni "haina uzito kulinganisha na mauaji na uharibifu uliyo tokea wakati wa vita kati ya wanajeshi wa Gbagbo na Outtara mara ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa baaada ya Laurent Gbagbo kudai yakuwa yeye ndiye alishinda uchaguzi.

Friday, August 12, 2011

Katibu mkuu umoja wamataifa awa na wasiwasi juu ya wanchi wa Libya.

Uingereza yapata hasara ya mamilion kutokana na vurugu za uvunjaji.

London, Uingereza- 12/08/2011. Serikali ya Uingereza imekadilia uaharibifu uliyo fanywa wakati wa machafuko na uvunjaji ulio tokea hivi karibuni huenda ukafikia £100 million.
Hata hivyo waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amehaidi ya kuwa serikali itawasaidia wale wote waliopata hasara kutokana na uvunjaji huo na kuhidi kwa kusema " serikali itafanya kila njia kuwakamata wale wote waliofanya vitendo hivyo ili waaadhibiwe kisheria."
"Na serikali itahakikisha inaweka mbinu mbadala ili kuzuia vitendo kama hivyo visitokee tena hapo baadaye." Alimalizia waziri mkuu David Cameron.
Hadi kufikia sasa zaidi ya watu 900 wameshakamatwa kwa kuhusika na machafuko hayo ambayo yame wame wapa mashaka wakazi wa Uingereza.
Katibu mkuu aumoja wa mataifa awa na wasiwasi juu ya wanchi wa Libya.
New York, Marekani - 12/08/2011. Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa amelezea wasiwasi alionao katibu mkuu,kufuatia ripoti ya kuwa raia wa kawaida wamekuwa wakipoteza maisha kwenye vita vinavyo endelea nchini Libya.
Msemaji huyo alisema, katibu mkuu amezitaka pande zote mbili zinazo pigana chini humo kutafuta suruhisho lili kusimamisha umwagaji wa damu.
Nayo serikali ya Libya imelilaumu jeshi la NATO kwa kushanmbulia maeneo ya raia kila inapo fanya mashambulizi yake.
Hata hivyo jeshi la NATO limesema " huwa linafanya mashambulizi kwenye kambi za majeshi ya Libya na siyo maeneo ya raia.

Wednesday, August 3, 2011

Hosni Mubaraka afikishwa mahakama kujibu mashitaka zidi yake.

Serikali ya Marekani yaruhusiwa kukupo.
Washington, Marekani 03/08/2011. Bunge nchini Marekani limepitisha muswada kwa serikali kuweza kukopa jambo ambalo lilikuwa linatishia uchumi wanchi na hasa wafanyakazi waserikali.
Kura zilizo kubali mswada huo ni 74 na zilizo kataa 26 na mswada huo ulikuwa unahitaji kura 60 ili uweze kupitishwa.
Kufuatia kupitishwa muswada huo, rais wa Marekani Baraka Obama amesaini muswada huo, ili kuiwezesha serikali kuweza kukopa kwa ajili ya kuendesha shughuli zake na hasa kuweza kulipa mishahara ya wafanyakazi wake.
Hata hivyo wataalamu wa mambo ya uchumi wanadai yakuwa muswada huo hautakuwa jibu la kutatua matatizo ya kiuchumi nchini humo kwa kipindi kirefu kijacho.
Serikali ya Marekani ilikuwa inasubiri muswada huo kupitishwa, jambo ambalo kama muswada huo usingepita siku ya Jumanne 03/08/2011, uchumi wa nchi hiyo ungekuwa katika hali mbaya na kuathiri duniani kote.
Hosni Mubaraka afikishwa mahakama kujibu mashitaka zidi yake.
Kairo
, Misri - 03/08/2011. Aliyekuwa raia wa Misri amefikishwa mahakani ili kujibu mashitaka yanayo mkabili zidi yake, ambayo yamefunguliwa ili kujibu kutokana na uongozi wake kura rushwa na mauaji katika kipindi chote cha utawala wa rais huyo.
Hosni Mubaraka , watoto wake na viongozi waliohusishwa katika kesi hizo waliwasilishwa katika mahakama iliyopo jijini Kairo huku maelfu ya wanchi wakingoja kwa hamu kuona jinsi kesi hiyo itakavyo endeshwa.
Hosni Mubaraka aliwasilishwa kwa ndege kutokea mji wa Sharm el Sheikh ambako andipo anapoishi tangu kutolewa madarakani miezi sita iliyopita na nguvu zawananchi.
Hata hivyo Hosni Mubara ambaye anasumbuliwa na magonjwa aliwasili akiwa kwenye kitanda cha kubebea wagonjwa ili kusikia kesi zidi yake.
Kesi zidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Misri itandelea tena tarehe 15, baada ya jaji kuhairisha kesi kwa siku ya leo.

Tuesday, August 2, 2011

Rwanda na Uganda kuimarisha ushirikiano uliyopo.

Rwanda na Uganda kuimarisha ushirikiano uliyopo.
Kigali,Rwanda - 02/08/2011. Marais wa Rwanda na Uganda wamehaidi kuimarisha uhusiano uliyopo kwa ajli ya wananchi wa nchi hizo na jumuiya nzima ya Afrika Mashariki.
Marais hao Paul Kagame na Yoweri Museven waliyaongea haya wakati walipo kutaka kwenye chakula cha jioni kilichoandaliwa na mke wa rais Paul Kagame.
Rais Yoweri Museven alifanya ziara nchini Rwanda ili kudumisha uhusiano na nchi hiyo kwa ukaribu na kujadili mikakati ya kuimarisha jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hugo Chavez amuunga mkono Muammar Gaddafi.
Karakas, Venezuela - 02/08/2011. Rais wa Venezuela ameliambia taifa ya kuwa amepokea barua kutoka kwa rafiki yake mwanamapinduzi kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Rais, Hugo Charez alisema " nimeisoma barua hiyo na kuilewa na nitaendelea kumuunga mkono kiongozi mwana mapinduzi Muammar Gaddafi ambaye anapigania haki ya wanchi wake na nakutakia maisha marefu Muammar Gaddafi."
"Nawale note ambao wanamwaunga mkono wapinzani wa Gaddafi hawajui nimakosa wamefanya."
Rais Hugo Chavez ambaye alikuwa amenyoa nywele, aliyaema haya wakati alipo kutana na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kutoka nchi Kuba kwa matibabu ya kansa.
Na habari kutoka nchi Libya zinasema kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi amemshukuru rais wa Venezuela kwa kuwanaye pamoja wakati wa shida na ameonyesha ni rafiki wa kweli."
Iraka yatakiwa kufanya uamuzi wa haraka kuhusu jeshi la Marekani.
Baghdad,
Irak - 02/08/2011. Mkuu wa majeshi ya Marekani ameitaka serikali ya Irak kufanya uamuzi wa haraka katika kuamua kuhusu kuendelea kuwepo kwa jeshi la Marekani nchi humo.
Admiral Mike Mullen alisema " inawabidi viongozi wa Irak kuamua kama wanataka jeshi la Amerika liendelee kuwepo nchini humo baada ya Desemba 31 kwani muda unakwenda haraka."
"Na inabidi wanajeshi wa Amerika wapewe huakika wa kisheria ikiwa wataiendelea kuwepo nchini Irak" alisema Admiral Mike Mullen.
Hata hivyo habari kutoka serikali ya Irak zinamsema " viongozi wa serikali ya Irak wapo na wakati mgumu hasa kutoka kwa wanachi wanchi hiyo na jumuiya ya kimataifa kutokana na hali halisi iliyopo nchini humo, hasa katika swala zima la usalama."
Marekani bado inawanajeshi wapatao 46,000 ambao bado wanaendelea na kazi ya kulisaidia jeshi la Irak katika maswala ya ulinzi.