Sunday, April 29, 2012

Bomu lalipuka kanisani jijini Nairobi.

Uingereza kuimarisha ulinzi kabla ya michezo ya Olyimpiki jijini London.


London, Uingereza - 29/04/2012. Serikali ya Uingereza imetangaza ya kuwa itaweka mizinga ya kurushwa hewani na majini ikiwa katika harakagti za kuimarisha usalama kabla ya kuanza kwa mashindano ya Olimpiki hivi karibuni.
Mmoja wa mkazi wa jiji la London Brian Whelan alisema " nimeshtuka saana baada ya kujua karibu na maeneo tunayoishi yatafungwa mkitambo hiyo ya kijeshi, kwani eneo hili liona majengo mengi saana nasijui itakuwaje?
"Na ni kweli kuna swala la usalama jambo ambalo linabidi litizamwe kwa makini na linaleta mshawasha."
  Wizara ya ulinzi ya Uingereza imeamua kuweka mitambo hiyo ili m,kuweza kuimarisha usalama wa jiji la London ikiwa kutatokea majaribio ya mashambulizi ya ya kigaidi ya anga au majini.

Bomu lalipuka kanisani jijini Nairobi.


Nairobi, Kenya - 29/04/2012. Bomu limelipuka ndani ya kanisa wakati misa inaendelea jijini Nairobi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine kumia kijeruhiwa vibaya.
Mashambulizi hayo ambayo yalitokea katika kanisa lijulikanalo kama Nyumba ya Maajabu ya  Mungu katika kitongoji kijulikanalo kama Ngara.
Mmsemaji wa polisi Eric Kiraithe alisema "polisi wana habari ya kuwa mashambulizi hayo yametokea  na  bado wanaendelea na uchunguzi."
Jiji  la Nairobi limekuwa linakumbwa na mashambulizi ya mabomu, tangu kundi la Al Shabab la Somalia kutangaza ya kuwa wataishambulia Kenya kwa hali na mali, kutokana na kitendo cha jeshi la Kenya kuingilia kati mambo ya ndani ya Somalia na kuanzisha mashambulizi nchini Somalia.


Meli yakamatwa na siraha za wapinzani wa Syria.


Beiruti, Lebanoni - 29/04/2012. Serikali ya Lebanoni imekamata meli iliyo kuwa na na siraha ambazo zinasadikiwa zilikuwa zinaelekea kwenye kambi ya wapinzani wa serikali ya Syria.
Milos Strugar ambaye ni msemaji wa (UNIFIL) United Interim Force in Lebanon alisema " tumeweza kuizua meli hiyo ikiwa ni moja ya kazi zetu kuzuia uingizaji wa siraha kinyume cha sheria."
Meli ili ambayo imezuiliwa na mabaharia wake  11 imesemekana na ya kuwa meli hiyo imetokea nchini Libya ambapo kuna maghala ya siraha ambazo zilikuwa zimetumika katika kuuong'oa utawala wa Muammar Gaddafi.
Ofisi ya  mmiliki wa meli hiyo alisisitiza ya kuwa waliambiwa ya ,kuwa meli hiyo ilikuwa imeba mashine za mafuta na kwa mujibu wa sheria hawana ruhusa kufungua makontena hayo kuangalia ndani ,kuna nini.

Friday, April 27, 2012

Rais wa zamani wa Liberia akutwa na hatia.

Wake wa Osama bin Laden warudishwa Saudi Arabia.


Abbottabad, Pakistan - 27/04/2012. Wanawake waliokuwa wake wa kiongozi wa kundi la Al Qaeda, wamerudishwa nchi Saud Arabia.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikalini zinasema " wake hao wawili wa Osama Bin Laden wamerudishwa  nchini Saud Arabia pamoja na watoto 11."
Wake hao watatu wa Osama Bin Laden walikamatwa na kuwekwa kizuizini mara baada ya mume wao kuuwawa na jeshi la Marekani mwaka 2011 mwezi May.
 
Rais wa zamani wa Liberia akutwa na hatia.

Hague, Uhollanzi - 27/04/2012. Aliyekuwa rais wa Liberia  amekutwa na hatia ya kukiuka haki za binadamu wakati akiwa kiongozi  wa nchi kwa kusadia kundi la lililo sababisha mauaji, ubakaji na unyanyaswaji nchi Sierra Leone kati ya mwaka 1996-2002.
Charles Tylor alikutwa na hatia hiyo kwa kulisaidia kundi la Revolutionary United Front (RUF) and Army Revelutionary Council (AFRC).
Hata hivyo Charles Tylor amekanusha kuhusika na vitendo hivyo.
Kufuatia kukutwa na hatia hiyo, hukumu juu ya Charles Tylor itatolewa hivyi karibuni na anatarajiwa kutumikia kifungo nchi Uingereza.

Tuesday, April 24, 2012

Mahakama ya kutetea haki za binadamu kuichunguza Mali.

Waumini wa dini ya Kiislaamu hawapatiwi haki zao vyema barani Ulaya. 


London, Uingereza - 24/04/2012. Shirikisho la kimataifa la  kutetea haki za binadamu Amnesty International limedai ya kuwa waumini wa dini ya Kiislaam wanabaguliwa katika baadhi ya nchi za ulaya.
Katika repoti yake Amnesty International ilisema " Watu wenye imani na dini ya Kiislaam wamekuwa na wakati mgumu katika nyanja za elimu, zakikazi na hata kuwa vigumu kupata maeneo ya kusalia.
"Ubaguzi huu ambao ni wakunuiwa juu wa Waislaam hupo hasa katika nchi za Switzerland,Ufaransa, Spain,,Beligium na Uhollanzi.
Marco Perolini mtaalamu wa mambo ya jamii na ubaguzi katika shirikisho hilo aliongeza kwa kusema "Ubaguzi huu umekuzwa na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa katika kila kampeni za uchaguzi ili kupata kura na inajulikana ya kuwa sheria ilisha pitishwa na muungano wa nchi wanachama wa jumiya ya Ulaya  ya kuwa ni mafuku kumbagua mtu kwa kupitia dini, rangi na imani lakini sheria hiyo imekuwa haina nguvu katika nchi wanachama."
Mvutano wa dini, wageni na imani zao katika nchi za Ulaya umekuwa ukitumiwa na wanasiasa wengi hasa katika kampeni za kutaka kura katika kipindi cha miaka ya karibuni, jambo ambalo limekuwa linaleta hali ya wasiwasi kwa baadai ya wageni waamiaji na wenyeji.

Serikali ya Izreal kuendelea na ujenzi wa makazi.


Jerusalemu, Izrael - 24/04/2012. Serikali ya Izrael imepitisha muswada wa kuruhusu ujenzi wa makazi katika maeneo ambayo Palestina inadai ni ya Wapalestina.
Waziri Mkuu wa Izrael Benjamin Netanyahu alisema " uamuzi wa kujenga makazi katika maeneo ya Sansana, Rechelim na Bruchin yalipitishwa na serikali iliyo pita."
Hata hivyo Benjamini Netanyahu hakueleza kwa kirefu kuhusu uamuzi huo wa kuruhusu ujenzi wa makazi.
Saeb Erekat mwakilishi katika majadiliano ya kuleta amani kati ya Wapalestina na Waizrael alisema " serikali ya Izrael inabidi ichague amani au kuendelea na ujenzi wa makazi katika maeneo ya Wapalestina.
"Swali ni kwamba ikiwa kuna watu wanasema kuwe na mataifa mawili  majirani ya Wapalestina na Waizrael mbona ujenzi wa makazi bado unaendelezwa?
Nafikiri uamuzi wa kuendelea kujenga maeneo hayo kuna vuga mpango mzima wa kuleta amani."
Mazungumzo kati ya Wapalestina na Waizrael yamesimama baada ya viongozi wa Palestina kukataa kuendelea na mazungumzo kwa madai ya kuwa serikali ya Izrael isimamishe ujenzi wa makazi katika maeneo inayo yashikilia.

Mahakama ya kutetea haki za binadamu kuichunguza Mali.


Hague, Uhollanzi - 24/04/2012. Mahakama ya kimataifa inayo shughulikia kezi za ukiukwaji wa haki za binadamu na mauaji ya raia inaaangalia na kufuatiilia kiundani kama makoso ya ukiukwaji wa haki za binadamu yalifanyika nchini Mali wakati wa mapinduzi ya kuing'oa serikali ya nchi hiyo.
Habari zilizo patikana kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa mahakama hiyo zinasema " kunauwezekano mkubwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu yalifanyika, na ndo maaana inabidi uchunguzi ufanyike ili kujua ukweli."
Mali imekuwa na mvurugiko wa amani mara baada ya jeshi kuipindua serikali ya rais Amadou Toumani Toure na wakati huo huo  watu wa kabila la Taureg  wengi wao waliopo kaskazini mwa Mali wanataka nchi  igawanyike na wawe huru kutoka  serikali kuu ya Bamako.

Iran yazidi kujijenga kisiraha na nguvu za kijeshi.


Tehran, Iran - 24/04/2012. Jeshi la serikali ya Iran limedai yakuwa linauwezo wa kijeshi wa kulinda nchi ya Iran kwa kila namana na pia kuongezea ya kuwa siku si nyingi watazindua siraha ya kijeshi yanye uwezo wa kwenda mwendo wa kasi wa mita 100 kwa sekunde.
Kamanda wa jeshi hili  Rear Admiral  Ali Fadavi alisema " Iran itakuwa nchi ya pili kwa kuwa na uwezo huo wa kuwa na siraha ya kivita yenye uwezo wa kusari ndani ya maji kwa kasi ya mita 100 kwa sekunde.
Iran haita tikiswa na maadui zake kwani mafanikiyo yote ya kujilinda ni juhudi za wanasayansi wazalendo."
Mkuu huyo wa jeshi aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mizinga aina ya IRGC uliyo fanyika hivi karibuni.
Serikali ya Iran imekuwa ikishutumiwa na nchi za Ulaya Magharibi na Marekani kwa kuwa na nia ya kutengeneza siraha za kinyuklia, jambo ambalo Iran imekuwa inakanusha kwa madai yakuwa mradi wa kinyuklia ni kwa ajili ya maendeleo ya kisanyansi.

Monday, April 23, 2012

Nchi za jumuiya ya Ulaya zaondoa vikwazo kwa Myanmar.

Korea ya Kaskazini yaitaadhalisha Korea ya Kusini.


Pyongyang, Korea ya Kaskazini - 23/04/2012. Serikali ya Kora ya Kaskazini imetishia ya kuwa inauwezo wa kuisambaza serikali ya Korea ya Kusini kwa muda wa dakika nne.
Habari kutoka serikali ya Pyongyang zilisema kupitia luninga ya taifa " tunauwezo wa kuizamabaza Korea ya Kusini kwa madakika ikiwa majaribio ya mashambulizi yatafanywa katika maeneo ya nchi yetu."
Hali ya mvutanao wa kimalumbano kati ya Korea ya Kaskazini na Kusini zimetokea baada ya Korea ya Kaskazini kutofanikwa kurusha chombo cha kisayansi angani ambacho ilitarajia kukitumia kwa njia ya mawasiliano..


Nchi za jumuiya ya Ulaya zaondoa vikwazo kwa Myanmar.


Brussels, Ubeligiji - 23/04/2012.  Jumuia ya nchi za Ulaya EU zimekubaliana kwa pamoja kuitolea vikwazo nchi ya Myanmar ambavyo vilikuwa vimewekwa kwa muda mrefu.
Uamuzi huo wa nchi za jumuia ya Ulaya EU umekuja baada ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo walipo kutana Luxembourg.
Habari kutoka katika mkutano huo zinasema " hali inaanza kuwa ya kuridhisha nchi Myanmar, kwani wameonesha ngazi moja ya mageuzi ya kisiasa na kuna matumaini ya kuwa serikali iliyopo itaendelea kuleta magauzi bora."
Hata hivyo siyo vikwazo vyote vilivyo ondolewa, "bali vikwazo vya kuiuzia siraha Myanmar bado vitasimama palepale" ziliongezea habari kutoka mkutano huo.
Kutangazwa kwa kuondolewa vikwazo hivyo kwa nchi ya Myanmar kumekuja baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kufanya ziara ya kiserikali nchi humo hivi karibuni, na kuweza kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani Aung  Suu Kyi, ambaye alikuwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa miaka miaka mingi.

Misri yasimamisha kuiuzia Izrael gasi.


Kairo, Misri - 23/04/2012. Shirika linalo sambaza na mushughulikia masi nchini Misri limetangaza kusimamisha uuzaji wa gasi nchi Izrael kuanzai sasa.
Mohamed Shoeb ambaye ni msemaji wa kampuni ya usambazaji gasi nchini Misri - Egypt Natural Gas Company alisema " tumeamua kusimamisha uuzaji wa gasi nchini Izrael na uamuzi huo ni wa kibiashara na wala si wakisiasa."
Waziri wa fedha wa Izrael Yuval Steinitz alisema " uamuzi wa Misri kusimamisha uuzaji wa gasi ni wa kuangaliwa kwa makini kisiasa na kiuchumi.
"Hii ni hatari kwani kunakiuka mkataba wa amani na utulivu iliyopo kati ya Izreal na Misri na uamuzi huo siyo mzuri na haufai."
Swala la uuzaji wa gasi kati ya Misri na Izrael uliingia dosari mara baada ya kuangushwa serikali ya rais Husni Mubaraka, ambapo serikali yake ilikuwa na mawasiliano mazuri na serikali ya Izreal tangu achukue madaraka ya urais 1981.


Rais wa Sudan adai ni mtutu wa bunduki ni lugha itakayo tumika  kuanzi sasa.


Khartoum, Sudan - 23/04/2012. Rais wa Sudan amekataa kuwepo na usuruhishi na majadiliano ya kuleta amani kati ya serikali yake na serikali ya Sudani ya Kusini.
Rais Omar al Bashir alisema "hatuwezi kujadiliana na kusuruhishana na serikali ya Sudani ya Kusini, kwan awaelewi kitu, ila msemo wa mtutu bunduki ndiyo lugha wanayo elewa.
"Na mazungumzo yetu kwano ni mtutu uliyo jaa sisasi."
Shirika la habari la serikali ya Sudan limesema jeshi la serikali limefanikiwa kuwaua wanajeshi 1,200 wa jeshi la Sudan ya Kusini wakati wamapambano yaliyo tokea hivi karibuni.
Mzozo kati ya Serikali ya Sudani ya Kusini na Sudani  ulianza hivi karibuni kutokana na tatizo la mpaka kati ya nchi hizo mbili ambapo inasemekana kuna utajiri wa mafuta.

Tuesday, April 17, 2012

Baraka Obama aongoza katika kura za maoni zidi ya Mitt Romney.

Julian Assange aanzisha kipindi kwenye Luninga -TV ya Kirusi RT News.

Moscow, Urussi - 17/04/2012. Mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks ameanzisha kipindi cha mazungumzo katika luninga TV kupitia luninga TV ya kitaifa ya Urussi.
Julian Assange ambaye yupo chini ya ulinzi kwa kufungiwa kutokutembea huru, katika ufunguzi wa kipindi chake cha mazungumzo ya Luninga kwa mara ya kwanza amefanya mazungumzo na kiongozi wa kundi la Hezbollah Said Hassan Nasrallah ambaye hajawahi kufanya mahojiano na vyombo vya habari kwa muda mrefu.
Kipindi hicho kitajulikana kama The World Tomorrow, ambapo wageni mbali mbali wataalikwa kufanya mazunguzo naye.
Akiongea kabla ya kuanza kipindi hicho Julian Assange alisema "kwa kuwa na kifungo cha nyumbani, itakuwa vizuri kuweza kuongea na watu tofauti na kujifunza toka kwao."
Julian Assange yupo chini ya ulinzi kwa muda wa siku 500 sasa baada ya kesi iliyofunguliwa zidi yake ya kuhusika katika kubaka mwanadada mmoja wakati alipo kuwepo nchini Swiiden, jambo ambalo Assange anakanusha yakuwa hakumbaka mwana dada huyo.

Baraka Obama aongoza katika kura za maoni zidi ya Mitt Romney.

Washington, Marekani - 17/04/2012. Wachunguzi wa mambo ya kisiasa nchini Marekani wametoa matokeo ya utafiti wa kura za maoni wa ugombea urais ambao unaonyesha rais wa sasa Baraka Obama  anaongoza.
Kwa mujibu wa kura hizo za maoni, "Baraka Obama  wa chama cha Demokratic anaongoza kwa  52% na mpinzani wake Mitt Romney wa chama cha Republikan  kupata kura za maoni  43%." na wanacha wa chama Demokratik  kudai ya kuwa  Baraka Obama  ndiye kiongozi anayefaa kuingoza tena Marekani.
Matokeo hayo yamekuja baada ya  mgombea mwenza wa chama cha Republikan Rick Santorum kujitoa katika kinyang'anyiro cha kugombe kiti cha urais wa Mareakani na kumwachia nafasi mgombea pekee  kupitia chama hicho Mitt Romney.  
Pilika za kutaka kuwania kiti cha urais nchini Marekani zimeshaaanza kwa mwendo wa gia namba moja tayari kwa kila mgombea kujipanga wakati wa safari hiyo ndefu ya kutaka kuingia Ikulu ya Marekani.

Iran yadai Saudi Arabia haina uwezo wa kuziba pengo la mafuta.


Tehran, Iran - 17/04/2012. Waziri madini nishati na mafuta wa Iran amedai yakuwa Saudi Arabia haitaweza kukamulisha ahaadai yake ya kutoa mafuta zaidi ambayo yataitosha dunia.
Waziri Rostam Qaesem alisema " Saudia Arabia inaweza kutoa mafuta hayo kwa muda mfupi, lakini kwa kipindi kirefu hawataweza na matokeo ya ahaadi hiyo yataleta mashaka katika dunia."
Maelezo hayo ya Iran yamekuja baada ya serikali ya Saudi Arabia kuhaidi yakuwa inauwezo wa kuziba pengo la mafuta litakalo tokea baada ya Iran kuwekewa vikwazo kwa kuzalisha mafuta zaidi.
Iran imewekea vikwazo vya uuzaji wa mafuta, benki na biashara katika masoko ya nchi za Ulaya  Magharibi na Marekani, baada ya Iran kuendelea na mpango wake wa mradi wa kinyukilia.

Monday, April 16, 2012

Tanzania moja ya nchi itakayo simamishiwa misaada na Kanada

Mshitakiwa wa mauaji ya kustisha nchini Norway afikishwa mahakamani.

Oslo, Norway - 16/04/2012. Mtuhumiwa  aliye husika katika mauaji ya kutisha ya kihistoria nchini Norway amefikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Anders Behring Breivk 33 alifikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka ya mauaji ya watu 77 aliyo yafanya mwaka 2011 Julai.
Akijibu baada ya kusomewa mashitaka yake Anders Breivk alisema " natambua kitendo nilicho fanya, lakini sioni kama ni kosa, kwaini nilikuwa najitete kwa kujilinda na kitendo cha Waislaam kuivamia Ulaya, na si itambui mahakama hii kwani mmepata maagizo kutoka kwa serikali ambayo ina unga mkono mchanganyiko wa watu kutoka sehemu tofauti na dini zao."
Hata hivyo Wanorway walio wengi wanahisi yakuwa Anders Breivk atatumia mahakama hiyo ili kukuza  itikadi za watu wa lengo wa kulia wanao pinga wageni na Waislamu na hasa kupitia majarida 1,500 ambayo yalichapishwa kwenye mitandao kabla ajafanya mashambulizi hayo.
Kwa mujibu wa wansheria wa Norway wanadai yakuwa Anders Behring Breivk ikiwa atakutwa na hatia huenda akahukumiwa kwenda jela miaka 21 ambayo huenda ikaongezwa na akakaa jela maisha.


Tanzania moja ya nchi itakayo simamishiwa misaada na Kanada.


Dar - es- Salaam, Tanzania - 16/04/2012. Tanzania itakuwa moja ya nchi ambazo zitakumbwa na hatua ya serikali Kanada kuamua kusimamisha kutoa misaada kwa kipindi cha miaka mitatu.
Serikali ya Kanada imeamua kusimamisha utoaji wa misaada hiyo ya kifedha yenye thamani ya dola million 400 za Kimarekani kupitia mpango unaojulikana CIDA - Canadian International Development Agency
Habari kutoka serikali ya Kanada zinasema "nchi zote  ambazo zina husika katika mradi huo zitafahimishwa kuhusu uamuzi huo siku chache kuanzia sasa."
Nchia  nyingine ambazo zitaathirika na kusimamishwa kwa kutolewa misaada hiyo ni Afghanistan, Bolivia, Mozambique na Pakistan.


Boko Haram kutishia kuangusha serikali ya Goodluck Jonathan.


Lagos, Nigeria - 16/04/2012. Kundi linalo pingana na serikali ya Nigeria na lenye itikadi kali ya kidini nchini Nigeria limetishia kuiangusha serikali ya nchi hiyo.
Mmoja wa viongozi kundi hilo Boko Haram alisema katika video ilyopatika " tutaiangusha serikali ya Goodluck Jonathan katika kipindi cha miezi mitatu."
Tishio hilo limekuja baada ya serikali ya Nigeria kupata msukumo kutoka serikali ya Marekani ili kupambana na makundi ambayo yanaleta mvurugo wa amani nchi Nigeria.


Benki ya dunia yapata rais mpya.


Johannesburgh, Afrika ya Kusini - 16/04/2012.  Matumaini ya nchi za Afrika kupata rais wa benki hya dunia ya mefutwa,baada ya Dr Jim Yong Kim kuchaguliwa kuwa rais wa benki hiyo.
Dr Jim Yong Kim, raia wa Marekani mwenye asili ya kutoka  Korea, alichaguliwa na kuwaacha wapinzani wake walio kuwa wakigombea kiti hicho kwa udadisi mkubwa.
Bara la Afrika lili kuwa limempendekeza Bi Ngozi Okonjo Iweala ambaye ni waziri wa Afya wa Nigeria kugombea kiti hicho, lakini hakufanikiwa kutoka na upinzani ulikuwepo katika kinyanganyiro hicho cha kugombea kazi ya juu ya kimataifa katika kusimamia mswala ya fedha.
Kabla  ya matokeo hayo, Bi Okonjo Iweala alisema " uchaguzi wa urais wa benki ya dunia haukufanyika kimsingi."
Uongozi katika benki ya dunia umekuwa ukielezewa ya kuwa unaupendeleo wa aina fulani kwa uongozi huo huwa unapelekwa kwa nchi zilizoendelea, jambo ambalo linatoa mthiani kwa bara la Afrika na uongozi wake.

Umoja wa Mataifa walaani kitendo cha Korea ya Kaskazini kukiuka sheria za kimataifa.


Washington, Marekani - 16/04/2012. Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imelaani kitendo cha Korea ya Kaskazini kurusha roketi kinyume cha sheria.
Laana hiyo kutoka katika kamati ya usalama ya umoja wa Matifa, imekuja baada mtambo wa kisayansi wa Korea ya Kaskazani kuharibika baada ya kurushwa hivi karibuni.
Kamati hiyo ya usalama ya umoja wa Mataifa ilisisitiza pia vikwazo lazima viwekwe kwa viongozi na makampuni yaliyopo Korea ya Kaskazini,ili kuifanya serikali ya Korea ya Kaskazini kubadili msimamo wake wa kinyuklia.
Mvutano wa kinyuklia kati ya  nchi za Magharibi na hasa Marekani kwa kudai yakuwa Korea ya Kaskazini ilikuwa na mpango wa kurusha roketi ili baadaye wajaribu bomu la nyuklia.

Friday, April 13, 2012

Mtambo wa Korea ya Kaskazini washindwa kufika mwezini.

Serikali ya Baraka Obama kuimarisha vitega uchumi barani Afrika.

Washington, Marekani - 13/04/2012. Wachumi,wafanyabiashara na wanasiasa wa Marekani wameitaka serikali izidishe kuwekeza vitega uchumi katika bara la Afrika.
Maagizo hayo yamekuja baada ya muswada kupitishwa ili kuimarisha na kuzidisha vitega uchumi katika bara la Afrika na kusema  "kwani kwa kufanya hivyo kutaimarisha uhusiano kati ya Waafrika na Wamarekani."
Uamuzi huo wa kupitishwa muswada huo wa kuwekeza vitega uchumi barani  Afrika umekuja ili kuweza kuikabili China ambayo imeisha jiweza na kuimarika katika bara la Afrika kwa muda sasa.
Muswada huo ambao umepitishwa katika serikali ya Baraka Obama utafatilia miswada mingine iliyopitishwa wakati wa utawala wa George Bush na Billy Clinton ambapo serikali hizo zilipitisha miswaada ya kiuchumi na kiutu ili kuimarisha maisha ya watu wa Afrika na kuinua uchumi kwa jumla.

Hali shwari nchini Syria na UN kupeleka wawakilishi wake.

Damascus, Syria - 13/04/2012. Umoja wa Mataifa umechagua watu 30 ambao watakwenda nchini Syria, ili kusimamia hali ya amani nchini humo.
Wawakilishi hao  ambayo bado kutajwa, watakuwa nchini Syria ili kuhakikisha amani inakuwepo na kusimamia mpango mzima wa majadiliano ya kisiasa " alisema Kofi Annan ambeye ni mwakilishi mkuu wa umoja wa Mataifa katika kusuruhisha ugomvi kati ya serikali ya Bashar al Assad na wapinzani ambao wanasaidiwa na nchi marafiki wanao pinga serikali ya Assad.
Leo ni siku ya pili tangu mswada wa kusimamisha mapigano kati ya majeshi ya serikali na ya upinzani  kutimizwa, baada ya Kofi Annan mwakilishi wa umoja wa Matifa kuzitaka pande zote mbili kuachana na mapambano ya kivita na kukaa chini kujadiliana kuhusu hali haya kisiasa na demokrasia ambayo itawanufaisha wa Syria wote.

Rais Robert Mugabe hana matatizo ya kiafya. 


Harare, Zimbabwe - 13/04/2012. Rais wa Zimbabwe amerudi Zimbabwe baada ya  ziara isiyo ya kiserikali nchini Singapore.
Kurudi huko kwa rais Robert Mugabe, kumetuliza habari zilizo kuwa zimeenea kuhusu hali yake ya kiafya, ambapo ili semekena ya kuwa " alikuwa anaumwa sana na yupo huko kwa matibabu."
Waziri wa habari Webster Shamu alisema " nafikiri mumemwona rais yupo imara kama chuma cha pua, nafikiri kutangaz habari za uongo siyo vizuri na tunajua hizi ni mbinu za mabepari."
Rais Robert Mugabe aliambatana na mkewe Grace huku Singapore ambapo habari kutoka serikalini zilisema " rais yupo huku kwaajili ya kuashughulikia maswala ya shule ya mtoto wake Bona."
Mugabe alionenekana akicheka na kufurahi na viongozi waliokuja kumpokea wakatia alipo wasili nchini Zimbabwe jana.


Mtambo wa Korea ya Kaskazini washindwa kufika mwezini.


Pyong Yang, Korea ya Kaskazini - 13/04/2012. Serikali ya Korea ya Kaskazini imekili ya kuwa mtambo a kisanyansi ambao waliurusha angani kwenda mwezini umeharibika kabla ya kufika huko.
KCNA-Shirika la habari za Korea ya Kaskazini liripoti "mtambo ambao ulirushwa angani umeshindwa kufika  baada ya kutokea matatizo ambayo hayajajulikana na kuanguaka baharini.
Wataalamu wameanza uchunguzi wa chanzo cha kuanguka kwa mtambo huo."
Mtambo huo ulikuwa umerushwa ili kumbatana na miaka 100 ya shereha ya kuzaliwa kiongozi mwasisi wa Korea ya Kaskazini Kim Ill Sung na kumkumbuka kiongozi mwingine Kim Ill Jung ambaye alifariki mwezi  Desemba 2011.



Tuesday, April 10, 2012

Serikali ya mpito ya Libya yapingana na mahakama ya Kimataifa.

Zintan, Libya - 10/04/2012. Serikali ya Libya imeitaka mahama ya kimataifa inayo shughurikia makosa ya jinai na kutetea haki za binadamu kutoa muda ili kuweza kuaanda kesi ya mtoto aliyekuwa mtoto wa rais wa Libya Muammar Gaddafi.
Serikali ya mpito ya Libya iliomba kwa kusema " Libya haitampeleka Saif al Islam Gaddafi nchi Uhollanzi kwani serikali ya Libya inauwezo wa kuendesha kesi zidi yake."
Seif al Islam Gaddafi ambaye alikamatwa baada ya baba yake Muammar Gaddafi kuangushwa kutoka katika kiti cha urais na kuwawa, anashutumiwa kwa kuhusika katika kukiua haki za binadamu wakati wa utawala wa baba yake.

Mozambique na Ureno zazungumzia utata wa bwawa la Cahora Bassa.


Maputo, Mozambique - 10/04/2012. Serikali ya Mozambique na Ureno zimekubaliana kudumisha ushirikiano wa karibu zaidi ili kweza kushirikiana kwa kila nyanja za kiuchumi na biashara.
Makubaliano hayo serikali ya Mozambique na Ureno yamekuja baada ya ziara ya waziri mkuu wa Ureno  Pedro Passos kufanya ziara nchini  Mozambique  na kubaliana kuangalia upya ni kwa jinsi gani mzozo wa bwawa la Cahora Bassa ambao ulikuwa haujatafutiwa ufumbuzi.
Mozambique ilikuwa koloni la Ureno kabla ya kupata uhuru mwaka 1975 chini ya chama cha FRELIMO.
na uhusiano kati ya nchi hizombili kupungua kwa muda mrefu.

Mtuhumiwa wa mauaji ya Norway adaiwa ni mzima wa akili.


Oslo, Norway - 10/04/2012. Wachunguzi wa afya ya akili  walio mfanyia  mtu aliye husika katika  mauaji ya kutisha yaliyo tokea nchini Norway mwaka 2011/ Julai/22 wametoa majibu kuhusu hali ya akili ya mshutumiwa huyo .
Anders Behring Breivik 33 ambaye aliwauwaa watu 77 na kutega mabomu ambayo yalileta maafa makubwa ameripotiwa na wachunguzi wa afya ya akili yakuwa akili yake haipo katika hali ya kufanya unyama na ni mzima.
Majibu kuhusu ali ya kiafya ya kiakili juu ya Breivek yamekuja baada ya uchunguzi zaidi kufanywa kuhusu afya yake.
Awali mtuhumiwa Anders Behring Breivik alidhaniwa ya kuwa anamatatizo ya akili, jambo ambalo lilifany wakili kufikilia ni kwa jinsi gani watashughurikia kesi ya muaaji huyo.

Iran yadai kuwakamata majasusi waliotaka kufanya mashambulizi hivi karibuni.


Tehran, Iran - 10/04/2012. Wizara ya usalama ya Iran imetangaza yakuwa imewakamata watu kadhaa na kufanikiwa kuvunja nguvu za majasusi ambao walikuwa wamepanga kufanya mashambulizi nchini humo hivo karibuni.
Kwa kujibu wa habari zinasema " baada ya kukamatwa kwa watu hao, ushahidi umeonekana ya kuwa kuna nchi za Ulaya Magharibi  Marekani na washiriki wake wanahuzika katika ujasusi huo.
Idadi ya siraha na mabomu na mitambo mingine ya kijeshi ilikamatwa wakati baada ya wapelelezi wa Iran kupata uhakika kamili."
Kufuatia kukamatwa kwa watu hao, serikali ya Iran imedai ya kuwa habari nyingine zitafuatia hivi karibuni ili kuthibitisha mpango huo wa majasusi.ulikuwa ni wa kweli.
Iran imekuwa inavutana na nchi za Magharibi, hasa katika swala  la utengenezaji nguvu za kinyuklia, ambapo Iran inadai ni haki yake kuwa na uwezo wa kutengeneza nguvu za nyuklia.

Sunday, April 8, 2012

Joyce Banda aapishwa kuwa rais wa Malawi.

Mamia waudhuria misa ya Pasaka Vatican City.

Vatican City, Vatican - 08/04/2012. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani ameongoza misa ya sikukuu ya Pasaka na kwa kuomba amani na utulivu kutawa nyoyo za binadamu.
Papa Benedikt XVI akiongoza misa alisema" tukiwa tunasherekea kufufuka kwa Yesu Kristu aliyeshinda mauti, tunaomba ufufuo wake ulete amani  kwenye maeneo yote duniani yanayo kabaliwa na vita na ukame.
Kuanzia nchi za Mashariki ya Kati, Syria, Izrael Palestina Irak na kwa wale wote walio kumbwa na matatizo ya vurugu katika bara la Afrika."
Papa Benedikt pia aliwatakiwa waumini wote duniani Pasaka njema yenye furaha na amani.
Siku ya leo Wakristu duniani kote wansherekea siku ambayo Yesu Kristu alifufuka baada ya kuhukumiwa na Pilato na baadaye kutundikwa msalabani ili maandiko yatimie.

Joyce Banda aapishwa kuwa rais wa Malawi.
Lilongwe, Malawi - 08/04/2012. Makamu wa rais wa Malawi ameapishwa kuwa rais wa nchi hiyo kufuatia kifo cha rais Bingu wa Mutharika  kilichotokea siku ya 05/04/2012.
Joyce Banda 61, atakuwa rais wa kwanza mwanamke kuchukua madaraka hayo ya juu ya kuongoza nchi  Malawi na katika ukanda wa Kusini na Mashariki ya Afriaka.
Rais Joyce Banda alisema haya baada ya kuapishwa "nitafanya kazi yangu kama inavyo sema katiba ya nchi na kuitumikia Malawi kwa moyo wangu wote, na napenda tuwe na matumaini mema na umoja, kwa imani naamini hakutakuwa na mwanya wa kulipizana visasi, na kwakuwa sisi ni taifa linalo muamini Mungu basi hatutashindwa kutimiza aliyo agiza."
Rais Banda alisisitiza utulivu hasa katika kipindi hiki cha malombelezi ya kuondokewa na aliye kuwa rais wa Malawi Bingu wa Mutharika.

Uingereza yapiga marufuku kuweka wazi sigara madukani.

London, Uingereza - 08/04/2012. Serikali ya Uingereza imepiga marufuku na kuagiza maduka yote nchini humo kuziba na kufunika sigara zilizopo madukani.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikalini zinasema "kwa kuziba na kufunika sigara zilizopo madukani kutasaidia kupunguza kishawishi cha kuvuta sigara na vilevile huenda tabia ya kuona sigara na kutaka kuvuta ikapungua."
hata hivyo baadi ya wafanyabiashara na raia wamesema "kitendo hicho hakita saidia kwani kila mvuta sigara anajua nini sigara gani anavuta."
Uamuzi huo wa serikali ya Uingereza kupiga marufuku kuweka sigara wazi madukani umekuja baada ya kampeni kubwa ya kupambana na magonjwa yanayo husiana na uvutaji wa sigara kuongezeka.

Friday, April 6, 2012

Jeshi la China latakiwa kupuuzia uvumi wa kisiasa.

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika afariki dunia.


Blantyre, Malawi - 06/04/2012. Rais wa Malawi amefariki dunia baada ya kuupata matatizo ya moyo siku ya Alhamisi 05 April wakati akiwa katika shughuri zake za kiofisi.
Bungu wa Mutharika 78 ambaye alichaguliwa kuiongoza Malawi mwaka 2004 na kuchaguliwa tena kwa mara ya pili mwaka 2009 kuwa rais wa  Malawi na mwaka 2011 kukumbwa na mvutano wa kisiasa na Uingereza hivi karibuni jambo ambalo lilisababisha uhusiano kati ya Malawi na Uingereza kudorola.

Watuareg wajitangazia uhuru ndani ya Mali.

Timbuktu, Mali - 06/04/2012. Kikundi la upinzani lililopo nchini Mali la Tuareg limetangaza kujitawala badaa ya kuchua eneo kubwa nchini Mali.
Kundi hili linalo julikana kama (MNLA)-The National Movement for the Liberation of Azawad ambalo lilifanikiwa kuchukua eneo kubwa nchini Mali, lili tangaza ya kuwa linataka lijulikane kama "Azawad."
Hata hivyo Umoja wa Afrika umepinga swala hilo na kuagiza kuwa jumjuiya ya kimataifa kutokubaliana na kundi hilo.
Nayo serikali ya Ufaransa imeunga mkono ombi la Umoja wa Afrika na kusema "Ufaransa haitaitambua ombi hilo la MNLA na Mali ni nchi moja na tunataka Mali kuwa nchi moja.

Mahakama ya Hague ya Uhollanzi yamtaka Saif al-Islaama Gaddafi. 

Hague, Uhollanzi - 06/04/2012.  Mahakama inayo shughulikia makosa ya jinai na kutetea haki za binadamu iliyopo Uhollanzi imetaia serikali ya Libya kumpeleka mtoto wa Muammar Gaddafi nchini Hollanzi.
Mahakama hiyo ya Hague ambayo ilitoa hati ya kukamatwa Saif al-Islaam Gaddafi ambaye yupo chini ya mikono ya serikali ya mpito ya Libya tangu alipo kamatwa  mwaka 2011 Novemba wakati akiwa katika harakati za kutoroka.
Naye mwanasheria anaye mtetea Saif al-Islaam Gaddafi alisema " tangu Saif kakamatwa amekuwa ananyanyaswa, kunyimwa haki zake na kufungiwa kwenye vyumba vya giza."
Serikali  ya Libya imekuwa ikivutana na mahakama ya Hague, kwa madai wanataka kesi dizi ya Saif al-Islaam Gaddafi  ifanyike nchi Libya.

Wakuba washerekea kwa mara ya kwanza sikukuu ya Ijumaa Kuu tangu mwaka 1959.

Havana, Kuba - 06/04/2012. Wanchi wa Kuba wamesherekea kwa mara ya kwanza siku ya kumbukumbu ya kuteswa kwa Yesu Kristu msalabani.
Siku ya Ijumaa Kuu siku ambayo haikuwa katika sikukuku za serikali ya Kuba kwa muda wa miaka mingi, ilisherekewa na waumini wa dini ya Kikristu wa Kuba, baada ya Papa Benedikt XVI kuiomba serikali ya kuitambua rasmi siku hiyo.
Ombi hilo la Papa limefuatia ombi la kwanza lililo fanywa na marehemu Papa John Paul II aliye iomba serikali ya Kuba kufanya siku ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu - Krismas kuwa siku ya mapumziko na kusherehekewa kitaifa.
Serikali ya Kuba ilipiga marufuku sikukuu za kidini mwaka 1959 baada ya kufanyika mapinduzi.


Jeshi la China latakiwa kupuuzia uvumi wa kisiasa.


Pyong Yang - China - 06/04/2012. Jeshi la China limewataka wanajeshi nchini humu kutilia maanani swala la ulinzi wa nchi na kuachana na uvumi ya kuwa kulikuwa kuna mpango wa kufanywa mapinduzi.
Habari hizi zimetolewa na gazeti la jeshi la China, kwa kuripoti " wanajeshi wa China wanatakiwa kuzuia na kulinda propaganda za aina yoyote, kwani zinaleta kelele zisizo na maana na hazitasaidia lolote kwa ni uvumi wa kisiasa."
Wanchi wa China wana tarajia kuona mabadiliko ya uongozi wa kisasa kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Thursday, April 5, 2012

Rais wa Malawi alazwa hospitali.

Raia wa Urussi haukumiwa miaka 25 jela nchini Marekani.

New York, Marekani - 05/04/2012. Jaji wa mahakama katika jiji la New York amemuhukumu kwenda jela miaka 25 raia wa Urussi ambaye alikuwa mfanya biashara wa kuuza siraha.
Voktor Bout 44 ambaye alipiga ukelele kwa kusema " huu ni uongo" alikutwa na hatia ya kuhusika na njama za kuhatarisha maisha ya Wamarekani na kwa kutaka kuuza siraha kwa magaidi.
Pia inaaminika mtuhumiwa Viktor Bout, alihusika katika kuuza siraha nchi za Rwanda, Angola na Congo.
Hata hivyo upande wa utetezi wa Viktor Bout ulidai yakuwa mteja wao alikuwa akiuza ndege mbili za mizigo zanye thamani ya $5million.

Pakistani yataka ushahidi kamili kutoka na madai ya  Marekani.

Islamabad, Pakistan - 05/04/2012. Serikali ya Pakistani imeitaka serikali ya Marekani kutoa ushahidi kamili wa madai yakuwa raia wa Pakistan alihusika katika milipuko iliyotiokea nchini India 2008.
Habari kutoka ofisi ya mambo ya nje ya Pakistani zinasema "tungependa tupate ushahidi wa kutosha ili tuanze kufuata sheria badala ya kuongelea kwenye mitandao na njia tofauti.
Mohammad Saeed alisema " nipo naishi maisha yangu ya kila siku bila shida na kama kuna mtu ananihitaji basi tuwasiliane nipo sina shaka."
Madai hayo yamekuja baada ya serikali ya Marekani kutangaza kitita cha dola $10 million kwa mtu atakaye toa habari zitakazo fanya kukamatwa kwa Mohammad Saeed ambaye Marekani inasema alihusika katika milipuko ya ugaidi ya mwaka 2008 na kuu watu 166.

Rais wa Malawi alazwa hospitali.


Blantyre, Malawi - 05/04/2012. Rais wa Malawi amelazwa hopsitali baada ya kukutwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo.
Rais Bingu wa Mutarika 78 alianguka wakati akiwa katika shughuli zake za kiserikali.
Kwa mujibu wa habari kutoka ofodi ya rais zimasema " kumekuwa na mshituko mkubwa kwani nchini nzima kutokana na tukio hilo."
Malawi ni nchi ambayo imekumbwa na misukosuko ya kiuchumi kwa muda sasa na hasa pale mauaji ya watu 19 yalipo tokea mwaka 2011 na kusababisha nchi za Ulaya Magharibi kulaani kitendo hicho  na nyingine kupunguza misaada kwa kudai serikali ya Malawi ifanye mabadiriko haraka  iwezekanavyo.




Monday, April 2, 2012

Senegal yapata rais wa nne tangu kupata uhuru.

Miaka 30 yatimia tangu vita vya Falkland.

London, Uingereza - 02/04/2012. Miaka 30 imefikia leo tangu Uingereza kuvamia visiwa vya Falklands, ilikuling'o jeshi la Argentina lililo chukua kisiwa hicho.
Katika kuadhimisha kumbukumbu hiyo, waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alisema "leo ni siku ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha katika vita hivyo, na Uingereza itaendelea kuwalinda Wanafalkland hadi hapo watakapo amua wao wenyewe.
Naye rais wa Argentina Christina Fernandez alisema "kitendo cha Uingereza kuendelea kukishikilia kisiwa hicho ni kinyume cha sheria na lazima wakiachie kisiwa hicho ni cha Argentina."
Mvutano wa Argentina na Uingereza zimekuwa zikivutana nani anamiliki kisiwa hicha kwa muda sasa jambo ambalo halijapatiwa jibu.


Chama cha Aung San Kyi chashinda viti vya bunge. 


Myanmar. Naypyitaw - 02/04/2012. Chama cha mwana harakati wa mapinduzi ya kisiasa nchini Myanmar kimetapa ushindi mkubwa katika uchaguzi uliyo fanyika hivi karibuni.
Chama cha Aung San Kyi NLD-National League for Democrcy kilipata viti 44 katika uchaguzi huo.
Aung San Kyi alisema " huu ni mwanzo wa mageuzi nchini mwetu, vita bado vinaendelea ili kuleta haki na usawa, na tunamatumaini ya kuwa ushindi huu utaliwezesha bunge kufanya kazi kwa manufaa ya wananchi."
Katika harakati za uchaguzi huo serikali ya Mynmar imedai ya kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na wasimamizi wa kimataifa waliruhusiwa kuangalia uchaguzi huo unakwenda kihalari.


Senegal yapata rais wa nne tangu kupata uhuru.


Dakar, Senegal - 02/04/2012. Wananch wa Senegal wameoata rais mpya, ambaye amepishwa wiki moja baada ya matikeo ya uchaguzi kutolewa.
Macky Sall 50, aliapishwa kuwa rais wa Senegal baada ya kumshinda aliyekuwa rais wa nchi hiyo Abdullaye Wade katika uchaguzi uliofanyika mara ya pili baada ya uchaguzi wa kwanza kutotoa mshindi.
Macky Sall alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura asilimia 66% na Wade alipata asilimia 34%.


Serikali ya Syria yakubaliana na Koffi Annan.


Damascus. Syria - 02/04/2012. Serikali ya Syria imekubaliana na mpango wa amani uliopendekezwa na mwakilishi wa umoja wa mataifa Koffi Annan.
Rais wa Bashar al Assad, amekubaliana ya kuwa tarehe 10/April itakuwa siku ya kuanza mpango mzima wa kusimika muhimiri  amani uliyo pendekezwa.
Koffi Annan ambaye ni msimamizi wa kuleta amani nchini Syria alisema " lazima kamati ya ulinzi ya umoja wa Matifa ifikirie mpango wa kuandaa wajumbe ambao watakuwa na majukumu ya kusimamia na kuangalia hali ya usalama.
Mpango huo ambao  wa 10/April unatarajiwa kutoa ruhusa kuwepo kwa amani na jeshi la Syria litaanza kutoka katika miji ambayo ipo chini ya jeshi hili.