Friday, April 29, 2011

William na Catherine wafunga pingu za maisha.

Mamia washuhudia William na Catherine walipokuwa wana wafunga pingu za maisha.
London, Uingereza 29/04/2011. Mamia ya wakazi wa jiji la London na dunia nzima wameshuhudia mjuukuu wa malkia Elizabeth, William akifunga ndoa na mchumba wake Catherine.
Harusi hiyo iliyo fungwa kanisani, na kuhudhuliwa na Malkia na familia yake, wazazi wa bibi harusi na familia yao, viongozi wa dini ,serikali na wageni wengine waalikwa.
Harusi hii ilitangazwa katika runinga kwenye nchi zaidi ya 108 dunia.
Bwana na bibi harusi William na Catherine wakipeana kisss, kuchuuum mbele za mamia kuashiria ya kuwa wao niwapendanao.
Bwana na bibi harusi William na Catherine wakionekana kwa mara ya kwanza mbele za mamia kama mke na mume mbele ya baraza katika makazi yao.
Mania walikuwepo kushuhudia kuchumooo kisss wa kukata na shoka.
Ishara ya yote kukamilika, bwana na bibi harusi walivalishana pete ikiwa ni haadi ya kuwa wamekuwa kama mke na mume
Picha hapo juu wanaonekana bwana hariusi William na bibi harusi Catherine wakiwa katika mkokoteni wa asili ambao unavyutwa na farasi njiani kueekea nyumbani kwa mapumziko , huku bwana harusi akikitoa tabasamukisi, baada ya kukabidhiwa mke wake na wazazi wa binti.
Hapa wanaonekana bwana harusi William na bi harusi Catherine wakila kiapo kwa pamoja mbele ya kasisi.
Baada ya harusi, bwana na bibi harusi wanatoka kanisani wakiwa kama mume na mke, na huku wakiwa wanatizamana kwa tabasamu la mahaba.
Picha hapo juu wanaonekana mke na mume wakiangaliana kwa furaha baada ya kumaliza kuimba nyimbo ya kumshukuru Mungu. hapa inaelekea Willy akimwambia mkewe, kumbe unajua kuimba hata nyimbo za dini.
Picha hapo juu anaonekana, William akimvalisha pete mke wake Catherine mbele ya kasisi, huku mkewe akitabasamu kwa furaha.
Picha hapo juu, baba wa Catherine, Middleton akimwakilisha mwanae mbele ya Kasisi tayari kula kiapo kumtwaa William kama mme wake, na huku kulia kwao mume wake Willy na mdogo wake Hurry wakimakini tayari kusikia habari njema toka kwa Catherine.
Picha hapo juu, wanaonekana bibi Malkia Elizabeth na kulia babu Philips wakiwa wamekaa tayari kungojea mjukuu wao kula kiapo mbele ya Mungu na kasisi ya kuwa anamchukua Catherine kama mke wake. mmm sasa mme wangu Willy anachukuliwa hivi hivi namwona , yaaa na mimi napata mke mwingine , hapo inaelekea bibi na babu wakiwa wanawaza.
Picha hapo juu anaonekana Catherine akielekea kuingia kanisani tayari kula kiapo cha kumpenda mume wake Willy.
Picha, hapa inaonekana mdogo wa Willy, Hurry akimwambia kaka yeke sasa unakwenda kuwa mme wa mtu, na kaka yake Willy akisema yaaa naenda kuanza maisha mapya mdogo wangu, hata hivyo wewe ni mgodo wangu na ndugu yangu milele.

Monday, April 25, 2011

Taliban wavunja jela na kutoroka.

Gaidi akamatwa nchi Venezuela.
Caracas, Venezuela - 25/04/2011. Maafisa wa usalama serikali ya Venezuela wamemkamata gaidi ambaye ameshukiwa kutaka kuhusika na kitendo cha kigaidi.
Kwa mujibu wa habari kutoka serikali ya Venezuela zinasema "gaidi huyo Joaquin Perez Becerra alikamatwa siku jumamosi baada serikali ya Kolombia kuwasiliana na serikali ya kuwa gidi huyo atapitia nchini"
Kukamatwa huko kwa Perez kuna kumekuja baada ya Interpol kutoa hati ya kukumatwa kwake wakati akitokea nchini German.
Huusiano wa serikali ya Venezuela na Kolombia umekuja baaada ya nchi hizo kukubaliana kushirikiana kiusalama baada ya rais mpya wa Kolombia Juan Manuel Santos kukutana na rais wa Venezuela Hugo Chavez na kuongea kumaliza uhasama kati ya nchi hizo mbili.
Taliban wavunja jela na kutoroka.
Kandahar, Afghanistan 25/04/2011. Zaidi ya wafungwa mianne wametoroka kutoka katika jela moja ambayo wengi wa wafungwa hao walikuwa wapiganaji wa kundi la Taliban.
Wafungwa hao ambao wametoroka kupitia shimo walio lichimba kwa urefu chini ya ardhi hadi kutoke nje gereza bila watu wausalama kutambua.
Msemaji wa Zabuillah Mujahed alisema " shimo hilo lilichimbwa kwa muda wa miezi mitano na walichukua masaa manne na nusu kutoka ndani ya jela hiyo.
NATO, alitibitisha habari hizi kwa kusema " tuna habari ya kuwa wametoraka kupitia shimo ambalo walilichimba kwa umbali wa zaidi ya mita 320.
Naye msemaji wa serikali ya Afghanistan, Waheed Omer kutoroka kwa wafungwa hao siyo picha nzuri kwa serikali , na tutahakikisha tunawakama wote waliotoroka."
Hii itakuwa ni mara ya pili wa wafungwa kutoka toka jela, baaada ya tukio kama hili mwaka 2008 ambapo wafungwa wapatao 1,000 walitoroka.
Makazi ya Muammar Gaddafi yashambuliwa.
Tripoli, Libya 25/04/2011.Ndege za jeshi la NATO limeshambulia makazi ya rais wa Libya ambaye majeshi yake yanapambana na majeshi ya upinzani yanayo ungwa mkono na Ufaransa, Uingereza na jumuia ya NATO.
Msemaji wa serikali Mussa Ibrahim amesema " ndege za jeshi la NATO lilishambulia makazi hayo kwa nia ya kutaka kumua rais wa sasa Muammar Gaddafi, ambaye nchi wanachama wa NATO zinataka atoke madaraka kwa kutumia nguvu za kijeshi jambo ambalo linaonyesha nini nia ya NATO."
Katika mashambulizi hayo, baadhi ya raia na wanajeshi waliokuwepo kwenye eneo hilo wanjeruhiwa vibaya na kuharibu kwa kiasi kikubwa majengo ya eneo hilo lililopo Ba el Azizia.

Friday, April 22, 2011

Ndege aina ya Drone kuanza kutumika nchini Libya.

Umoja wa Afrika waondolea vikwazo Ivory Coast.
Adis Abeba, Ethiopia -22/04/2011. Umoja wa Afrika umeondoa vikwazo amba
yo vilikuwa vimewekwa zidi ya nchi ya Ivory Coast.
Akiongea kuondolewa kwa vikwazo hivyo, mwenyekiti wa kamati ya amani ya Umoja wa Afrika alisema " tunapenda serikali iliyo chukua madaraka ihakikishe yakuwa ina imarisha usalama, haki na amani kwa watu wote katika misingi ya kidemokrasia na kuanzisha mpango mzima wa watu kusameheana."
Uamuzi huo umekuja baada ya aliye kuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kutolewa madarakani kwa nguvu na jeshi la Alassane Ouattara kwa kusaidiwa na jeshi la Ufaransa.
Wapinzani hao katika kiti kugombea kiti cha urais Laurent Gbagbo na Alassane Ouattara walianza kuvutana kisiasa baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa n a huku kila mmoja kudai ndiye aliye ibuka mshindi.
Ndege aina ya Drone kuanza kutumiwa nchi Libya.
Benghazi, Libya 22/04/2011. Aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais na ambaye pia ni mbuge wa chama cha Republikan cha Amerika amewasili nchini Libya.
John McCain, amewasili nchini Libya ili kuongea na viongozi wa upinzani ambao wanapingana na serikali ya Libya inayo ongozwa na Kanali Muammar Gaddafi.
Akijibu swali nini nia ya madhumuni ya ziara yake nchini humo, McCain alisema " nimekuja ili kuangalia hali halisi kutokana na matukio yanayo endelea."
Kuwasili huko kwa McCain kumekuja baada ya rais wa Amerika Baraka Obama kuruhusu matumizi ya ndege Drones ambazo zinatumia nguvu za mtandao katika kufanya mashambulizi zitumike katika vita zidi ya serikali ya Libya.

Sunday, April 17, 2011

Serikali ya Kuba kufanya mabadiliko ya kisiasa.

Serikali ya Kuba kufanya mabadiliko ya kisiasa. Havana, Cuba -17/04/2011. Rais wa Kuba ametangaza mabadiliko ya kisiasa ambayo yatakayo fanyika nchini humo.

Rais wa Kuba Raul Castro akiwahutubia viongozi na wanachama tawala wapatao 1000 katika mkutano mkuu wa chama tawala alisema "tumefikia wakati wa kukubaliana na hali halisi ya mabadiliko ya kisiasa , kwa minajili hiyo tumekubaliana ya kuwa kiongozi wa nchi atakuwa anakaa madarakani kwa kipindi cha miaka hadi kumi tu.
rais Raul Castro alimekuwa mtawala wa nchi hiyo tangu alipo achiwa madaraka na kaka yake Fidel Castro
Iran yazindua gari mpya ya kifahari.
Tehran, Iran 17/04/2011.Serikali ya Iran imetangaza yakuwa inampango wa kujenga meli kebu ambayo itatumika katika kukagua na kulinda mipaka yake katika pwani ya kusini mwa nchi hiyo.
Mkuu wa jeshi la Iran, Admiral Amir Farhadi, alisema "meli kebu hiyo ambayo itakuwa na uzito wa tani 500 na itakuwa tayari kuanza kazi mwaka 2012 Julai."
Irani imekuwa ikipiga hatua za kisayansi na teknolojia na kuwa nauwezo wa kutengeneza mitambo na siraha za kijeshi.
Wakati huo huo kampuni ya kutengeneza magari ya Iran, imezindua gari mpya ya aina ya Dena ambayo inatarajiwa kuwa katika barabara hivi karibui, na wanunuzi wa magari kutoka Iran,nchi za Rusia,Syria, Turkey, iraq,Ukraine na Misri, wataaanza kuyatumia magari mwaka 2011.

Friday, April 15, 2011

Obama,Sarkoz na Kameron tutahakikisha Gaddafi anang'oka.

Obama, Sarkoz na Kameron tutahakikisha Gaddafi anang'oka.

London, Uingereza 15/04/2011. Viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Amerika wamekubaliana kwa pamoja kuundeleza mapambano dhidi ya kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Nikolas Sarkozi rais wa Ufaransa, waziri mkuu wa Uingereza David Kameon na rais wa Amerika Baraka Obama, kwa pamoja wamekubaliana kuhakikisha kiongozi wa Muammar Gaddafi anatoka madarakani.
Viongozi hao walitoa waraka wao wa pamoja na kusisitiza "sheria ya muswada ya kamati ya usalama ya umoja wa mataifa ya 1973, inataka jumuia ya kimataifa kulinda usalama wa raia na razima waitekeleze."
Waraka huo uliongezea " NATO na washiriki wake wataendelea na jukumu lao la kulinda raia na kuhakikisha Kanali Muammar Gaddafi anatoka na kuwapa uhuru wa na nchi wa Libya kujitawala wenyewe.
Hata hivyo baada ya waraka huo kutoka, kiongozi wa Libya alionoekana katika mitaa ya Tripoli akiwaslimia wanchi na wadau wanao muunga mkono, na huku mwanae wa kike Aisha Gaddafi aliwahutubia watu waliokuja Bab al Azizyah kuadhimisha miaka 25 tangu Amerika ilipo vamia Libya na kusema baba yake hataachia madaraka kwa kulazimishwa wala vitisho vya nchi za Magharibi na washirika wake.

Wednesday, April 13, 2011

Viongozi wakutana Katar kutathmin hali ya Walibya.

Nchi zinazo ongoza kukua kwa uchumi dunia zakutana nchini China. Hainan, China 13/04/2011. Viongozi wa serikali na mabenk wamekutana nchi China ili kuangalia kiundani njia bora ya kuimarisha sekta ya bishara ya kifedha na uchumi.

Li Wuwei, makamu wa mwenyekiti na mshauri wa mambo ya kisiasa alisema, " nchi wanachama zimejitahidi na kushirikiana katika kuinua hali ya kiuchumi baada ya ya myumbo wa kiuchumi kutokea na zitaendele kufanya hivyo hasa katia nchi zinazohitaji kuinuka kiuchumi ili ziweze kukidhi mahitaji ya jamii zao."
Mkutano huo unaojulikana kama BRICS unajumuisha nchi za Brazil, Urussi, China na Afrika ya kusini nchi ambazo zinaongoza katika kukua kwa uchumi kwa haraka zaidi.
Rais wa zamani wa Misri na watoto wake wawekwa chini ya ulinzi wa polisi.
Kairo, Misri 13/04/2011. Rais wa zamani wa Misri amewekwa kizuizini pamoja ya watoto wake wawili wa kiume, ilikuwezesha uchunguzi zidi ya kesi inayo wakabili ya rushwa na unyanyasaji.
Kwa mujibi wa wakili wa serikali alisema " Hosni Mubaraka na watoto zake Gamal na Alaa watakuwa kuzuizini kwa muda wa siku15 wakati uchunguzi unaendelea zidi yao."
Hosni Mubaraka 82, ambaye ametawala Misri kwa miaka zaidi ya miongo mitatu alitolewa madarakani na maandamano ya watu waliotaka aachie madaraka mapema mwanzoni mwa mwaka huu..
Habaria zinasema rais Hosni Mubaraka anamatatizo ya moyo na hivi sasa yupo hspitali amelazwa kwa uchunguzi zaidi wakati watoto wake wako chini ya ulinzi wa polisi.
Viongozi wakutana Katar kutathmini hali ya Walibya.
Doha,Katar - 13/04/2011. Viongozi wa kundi la upinzani linalo pingana na serikali ya Libya wamekutana na viongoziwa nchi tofauti nchi Katar ili kujadili hali halisi ya mapambano yanayo endelea ili kung'oa madarakani kiongozi wa Libya MuammarGaddafi.
Akiongea mbele ya viongozi walioudhuria mkutano huo waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague amesema, "nilazima tuhakikishe tunafanya kila njia ili tunasaidia kundi la upinzani ili kuliwezesha kuimarisha demokrasi nakuhakikisha Muammara Gaddafi anakubaliana na matwakwa ya wanchi wa Libya."
Msemaji wa kundi la upinzani linalo mpinga serikaliya Mahmud Shamman alisema, " tungependa tutambulike kama wawakilishi wa serikali mpya ya Libya ambao tupo kwa ajili ya kuijenga Libya kwa kila Mlibya."
Mkutano wa huu umefanyika ili kuangalia ni kwa kiasigani jumuiya ya kimataifa itaweza kuisaidia Libya.

Monday, April 11, 2011

Jeshi la Alassane Ouattara la mkamata Laurent Gbagbo.

Jeshi la Alassane Ouattara la mkamata Laurent Gbagbo. Abidjan, Ivory Coast -11/04/2011.Jeshi la upinzani linalo ongozwa na Alassane Ouattara, kwa kushirikiana na jeshi la Ufaransa limefanikiwa kumkamata aliyekuwa rais wa Ivory Coast baada ya kuvamia makazi yake.

Rais huyo wa Ivory Coast Laurent Gbagbo,alikamatwa baada ya mashambulizi kati ja jeshi lake na jeshi la Ouattara kwa msaada wa Ufaransa na vifaru huku helkopta zikisaidia kuhakisha ya kuwa Gbagbo na jeshi lake hawawezi kuendeleza mashambulizi.
Msemaji wa Alassane Ouattara, Affaoussy Bamba alisema, " Laurent Gbagbo amekamatwa na sasa yupo mokononi mwa jeshi letu.
Hata hivyo , msemaji wa Laurent GbagboToussaint Alain , alisema jeshi la Ufaransa limemkamata Gbagbo baada ya kuvamia makazi yake.
Kufuatia madai hayo, waziri wa ulinzi wa Ufaransa alikanusha madai hayo na kusema ,"Gbagbo alikamatwa na jeshi la Alassane Ouattara."
Kukamatwa huko kwa Laurent Gbagbo, kumekuja baada ya rais huyo kudai yakuwa yeye ndiye mshindi wa matokeo ya uchaguzi, na huku mpinzani wake Alassane Ouattara akidai yeye pia ameshinda uchaguzi na umoja wa mataifa kuunga mkono.
Kundi la upinzani la kataa mpango wa kuleta amani nchini Libya.
Benghazi, Libya - 11/04/2011. Kundi la upinzani linalopigana na serikali ya Libya limepinga mpango uliopitishwa na umoja wa Africa ili kusimamisha mapigano.
Msemaji wa kundo hilo lili na makao yake makuu Benghazi, Mustafa Jabiri alisema " hatuwezi kushirikiana na uongozi wa Muammar Gaddafi, na lazima uachie madaraka yeye na familia zao, na tutakufa nao au tuchukue ushindi kwa mtutu wa bunduki."
Uamuzi wa kundi hilo kukataa mpango wa umoja wa Africa ili kuleta amani kati ya serikali ya Libya na wapinzani wake ulikuja baada ya viongozi wa jumuia hiyo chini ya rais wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma kukutana na Muammar Gaddafi ili kujadili mpango wa kuleta amani.

Iceland yasumbua vichwa vya wafadhili wake.

Iceland yasumbua vichwa vya wafadhili wake.

Hague, Netherland - 11/04/2011. Serikali ya Uingereza na serikali ya Netherland zimeishitaki serikali ya Iceland baada ya kutoke mgogoro wa kulipa deni.
Uamuzi huo wa serikali hizo kuishitaki Iceland limekuja baada ya wanchi wa Iceland kupinga kitendo cha serikali yao kulipa deni la pesa ambazo ziliazimwa kwa Iceland ili kusaidi serikali ya nchi hiyo baada ya myumbo wa Mabenki nchini humo.
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Iceland alisema " serikali ya Iceland haina wasiwasi n aitalipa dei hilo, hata kama wanachi hawapendelei kitendo hicho."
Serikali ya Iceland ilipewa pesa na serikali za Uingereza na Netherland ili kuimarisha mabenki yake baada ya kutokea kwa myumbo wa kipesa na kutishia uchumi wa Iceland.

Thursday, April 7, 2011

Mahakama ya Hague yaanza kesi za machafuko ya Kenya.

Mahakama ya Hague yaanza kusikiliza kesi za machafuko ya Kenya.

Hague, Netherland -07/04/2011. Viongozi wa siasa kutoka nchini Kenya wamefikishwa mahakamani kufuatia machafuko yaliyo tokea wakati na kabla uchaguzi.
William Ruto,Henry Kosges ambao walikuwa mawaziri na mtangazaji Joshua Arao Sang wanashita kwa kuchochea machafuko ya kikabila yaliyopo nchini Kenya.
Hata hivyo bado kuna watuhuniwa wengine wanatarajiwa kufikishwa mahakani kujibu mashitaka kama haya.
Uchaguzi wa urais wa mwaka 2007 nchini Kenya ulileta machafuko ya kisiasa na hata kupelekea kumwagika kwa damu na watu kupoteza maisha yao.
Japan yakumbwa na tetemeko la ardhi jingine.
Tokyo, Japan -07/04/2011. Tetemeo kubwa la ardhi limeikumba tena Japan baada ya tetemeko la kwanza ambalo limeleta maafa makubwa.
Tetemeko hili lililo tokea kaskazini mwa Japan, limepelekea jamii nzima ya maeneo imetakiwa kuondoka kwani kunawasiwasi tsunami kutokea.
Wataalamu wa mambo ya kiyasansi ya ardhi na hali ya hewa wamesema "tete hilo limekuwa na nguvu za uwezo wa 7.1 magnitude."
Hata hivyo mpaka sasa hakuna habari zaidi kimaafa na watu kupoteza maisha.

Wednesday, April 6, 2011

Uingereza ya kubali baadhi makosa.

Uingereza ya kubali baadhi ya makosa.

Islamabad, Pakistani - 06/04/2011. Waziri mkuu wa Uingereza amewahutubia waandishi wa habari wanafunzi na viongozi wa serikali wa Pakistan na kukubali yakuwa Uingereza inatakiwa ibebe lawama kutokana na machafuko katika eneo hilo.
David Cameron alisema " Uingereza imekuwa ni chanzo cha matatizo katika eneo hilo na tumekuwa tukihusika katika sehemu tofauti hapo mwanzo.
"Ukiangalia kiundani utaona historia ina husisha Uingereza kwa njia moja au nyingine."
Waziri mkuu wa Uingereza yupo ziarani nchini Pakistani ili kukuza uhusiano na nchi hiyo ambayo ni mshiriki mkubwa katika vita zidi ya ugaidi.

Tuesday, April 5, 2011

Mke wa Ratko Maladic aiambia mahakama mume wake huenda amefariki.

Mke wa Ratko Mladic aiambia mahakama mume wake huenda amefariki. Belgrade,Serbia - 05/04/2011. Mke wa aliyekuwa kiongozi kivita vilivyo tokea nchi za Balkan amefikishwa mahakani ili kujibu mashitaka ya kukutwa na siraha. Bosijlika Mladik, ambaye alifikishwa mahakamani, aliiambia mahakama ya kuwa siraha hizo ziliwekwa na mumewe na aliwazuia kugusa kabati hilo.

Akiongelea kuhusu swala la mume wake Bosijlika Mladik alisema " mume wangu aliondoka nyumbani mwaka 2001 siku ambayo Slobadan Milosoevik alikamatwa na tangu siku hiyo hatujamwona na huenda amesha fariki kwani alikuwa anatumia vidonge kwa ajili ya matibabu na nivigumu kuishi bila kutumia vidonge hivyo."
Ratko Mladic ambaye alikukuwa mkuu wa majeshi wakati wa vita hivyo vilivyo tolekea katika nchi za Balkani
Haiti ya mchagua aliyekuwa msanii wa muziki kuwa rais wao.
Port-au-Price, Haiti 05/04/2011.Matokeo ya uchaguzi nchi Haiti yametangazwa na aliyekuwa mwanamusiki maharufu nchini humo kushinda katika kiti cha kugombania uchaguzi wa rais.
Michel Martelly au Sweet Micky, ameshinda uchaguzi huo baada ya wadau na wapenzi wa mwanamziki Wyclies Jean kumpigia kura kwa wingi .Wyclif Jean ambaye hapo mwanzoni aligombea kiti hicho lakini kujitoa kutokana na sababu za kiufundi.
Akiongea baada ya matokeo hayo Michel Martel, alisema" nitajitaidi kuijenga upya Haiti na kuzidisha mshikamano na ushirikiano katika jamii ya Wahaiti."
Uchaguzi huo wa Haiti utawezesha nchi hiyo kujengwa upya baada ya kukutwa na janga la tetemeko la Ardhi ambalo lilisababisha uharibufu mkubwa karibu nchi nzima.

Sunday, April 3, 2011

Mahaka ya kimataifa yakataa kesi iliyofunguliwa na Georgia.

Mahakama ya kimataifa yakataa kesi iliyo funguliwa na Georgia. Hague, Uhollanzi - 03/04/2011. Mahakama ya kimataifa ya umoja wa mataifa imekataa kesi iliyo letwa na serikali ya Georgia zidi ya Russia.

Habari kutoka mahakama hiyo zinasema " mahakama haiwezi kuendelea na kesi kutokana na baadhi ya mazungumzo haya kufanyika na kuchunguzwa."

Kesi hiyo ulifunguliwa na serikali ya Georgia baada ya jeshi la Urussi kuivamia Georgia ili kuzuia mauaji dhidi ya wakazi wa Abkhazia na Kusini Ossetia.

Jeshi la Ufaransa la zuia kiwanja cha ndege.
Abidjan, Ivory Coast -03/04/2011.Jeshi la Ufaransa limeshikilia kiwanja cha ndege cha jiji la Abidjan.
Jeshi hilo la Ufaransa ambalo lipo chini ya Umoja wa Mataifa huku majeshi ya rais wa sasa wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na mpinzani wake Alassane Ouattara ya kiendelea kupigana.
Machafuko ya kisiasa nchini Ivory Coast yalianza baada ya uchaguzi mkuu wa kumchagua rais kuingia mgogoro dhidi ya Gbagbo na Ouattara kufuatia matokeo yaliyo tangazwa.

Friday, April 1, 2011

Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa wavamiwa.

Wafanyakazi wa Umoja wa mataifa wavamiwa. Mazar-el-Sharif, Afghanistan -01/04/2011. Ofisi za umoja wa mataifa nchini Afghanistan zimevamiwa na waandamanaji ambao walikuwa wanapinaga kitendo cha mchungaji mmoja kuchoma Kuraan.

Waandamanaji hao walivunja jengo la umoja wamataifa na kuwavamia wafanyakazi waliokuwemo katika eneo hilo na kusababisha vifo vya wafanyakazi wanane wa umoja wa mataifa.
Masemaji wa polisi alisema " baadhi ya waandamanaji walivamia majengo ya umoja wa mataifa kwa nguvu na kupanda juu ya ofisi hizo na kuleta madhara makubwa."
Maandamano hayo yalifanyika baada ya swala ya ijumaa ili kupinga kitendo cha mchungaji mmoja kuchoma kitabu cha dini.