Monday, December 29, 2008

Rais wa Somalia aacha madaraka"Asema ameshindwa baadaya jitihada zake kugonga ukuta"

Nchi za Kiarabu zatakiwa kuongeza juhudi kutatua mgogoro wa Palestina na Israel "Katibu waUmoja wa mataifa ". Umoja wa Mataifa,Amerika-29/12/08. Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon,amezitaka Palestina na Israel kusimamisha mapigano mara moja , na kurudi katika meza ya majadiliano. Katibu huyo, Ban Ki-moon, akisitiza hayo,alizitaka nchi za Kiaarabu kufanya kila juhudi ili kuleta amani katika eneo hilo la Ukanda wa Gaza kwani juhudi wanazo zifanya hazisaidi, hivyo inabidi waongeze juhudi zaidi. Katibu Ban Ki-moon, alisema vita vilivyopo kwenye Ukanda wa Gaza, haukubaliki na jumuia ya kimataifa, hivyo lazima visimamishwe mara moja kwani vita hivyo vinaleta mazara makubwa kwa jamii na watu wa pande zotembili, Israel na Palastina kupoteza maisha yao. Picha hapo juu anaonekana, Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kikao na kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali alisi na nini kifanyike ili kuwepo na amani katika eneo la Ukanda wa Gaza. Umoja wa nchi za Afrika waonyesha makali yake"Guinea yasimamishwa uanachama".

Conakry,Guinea-29/12/08.Umoja wa nchi za Afrika (AU- African Union), umesimamisha uanachama wa nchi ya Guinea, baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi.
Mapinduzi hayo, yamekuja baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo ,Lansana Conte ambaye alitawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 24.
Picha hapo juu, ni ya bendera ya nchi za Umoja wa Afrika, ambapo jumuia hiyo, imesimamisha uanachama uanachama wa nchi ya Guinea.
Picha ya pili, anaonekana rais wa zamani wa Guinea, hayati, Lansana Conte wakati wa uhai wake akiwasalimia wanachi wakati akiwasili kwenye moja ya mikutano nchini humo.
Picha ya tatu, anaonekana, kiongozi wa sasa ambaye ni mwanajeshi, Kaptain, Moussa Dadis Kamara, akiwasalimia wanachi baadaya ya kutangaza ya kuwa rais wa nchi,(Guinea).
Picha ya nne, wanaonekna wanajeshi wakiwa wameka chini ya kifaru, baada ya jeshi kutwa madaraka, baada ya kifo cha rais, Lansana Konte.
Picha ya nne, linaonekana jeneza la rais, Konte,wakati mazishi ya kumwaga kwa mara ya mwisho, rais Lansana Konte yalifanyika jiji Konakri
Rais wa Somalia aachia madaraka"Asema ameshindwa baada ya jitihada zake kugonga ukuta".
Baidoa, Somalia-29/12/08.Rais wa Somalia, Abdullahi Yusufu Ahmed amejiuzuru nafasi yake ya urais wa kuingoza nchi hiyo ambayo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi.
Akiongea hayo, rais mstaafu, Abdallah Yusuf Ahmed,ali wakumbusha wabunge yakuwa, ikiwa ni tashindwa kazi, basi nita jiuzuru, na leo nimeamua kuikabidhi kazi mliyo nipa mikononi mwenu,na Spika wa bunge atachukua majukumu.
Picha ya hapo juu anaonekana, rais, Abdullah Yusuf Ahmed, akijifuta jasho, kwani kazi aliyo kuwa nayo hapo hawali ya kuwa rais wa Somali haikuwa nyepesi.
Picha ya pili, wanaonekana baadhi ya wapiganaji wa Kisomalia, wakiwa wameshikilia siraha, hali kama hii ilikuwa ngumu kwa raia kutimiza majukumu yake.
Amani yatoweka Ukanda wa Gaza, "Wapalestina na Waisrael, hakuna wa kutegua kitendawili"
Gaza,Ukanda wa Gaza-29/12/08.Mgogora wa Mashariki ya Kati yameingia hatua nyingine, baada ya serikali ya Israel kushambulia katika maeneo ya Gaza, kwa kutumia ndege zake, ili kuvunja kabisa nguvu la kundi la Hamas, ambalo linaongoza katika mapambano na serikali ya Israel.
Kwa mujibu wa masemaji wa serikali ya Israel,alisema imebidi kuchukua hatua hii,baada ya kundi la Hamas, kuvunja makubaliano ya kuendeleza mkataba wa amani, kwa kuanza kurusha roketi katika maeneo ya Israel.
Kufuatia vita hivyo, kiongozi wa kundi la Hamas,Khaled Meshaal, amesema atafanya mazungimzo na kundi la Fatah, kinacho ongozwa na rais rais, Mahamoud Abbas.
Picha hapo juu anaonekana, kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas, Khaled Meshaal, ametanga kwa kuwataka wafuasi wake kupigana kwa kujitoa muhanga.
Picha ya pili,anaonekana mmoja wa mkazi wa Gaza, akinyanyua juu, mwili wa mmoja wa mtoto aliye poteza maisha baada ya kupigwa na mabomu zilizo dondoshwa toka kwenye ndege za kijeshi za Israel.
Picha ya tatu, anaonekana mmoja wa mkazi wa Gaza, akiangali ni jinsi gani majengo ya maeneo hayo yalivyo haribiwa na na mabomu.
Picha ya nne, moshi unaonekana ukiwa umetanda juu,baada ya mashambulizi ya liyo fanyika Gaza.

Thursday, December 18, 2008

Hali ni ngumu kwa Joseph Koni,"Umoja wa matifa waomba kuunga mkono"

Muhusika wa mauaji ya halaiki ya Rwanda afungwa maisha.

Arusha, Tanzania - 18/12/08.Aliyekuwa mmoja ya maafisa wakuu wa jeshi la Rwanda, Theoneste Bagasora mwenye umri wa miaka 67, ameukumiwa kwanda jela maisha, baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika moja kwa moja katika mauaji ya halaiki yaliyo tokea nchini Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya watu 8,00,000, wengi wao wakiwa wa jamii ya Kitutsi na Wahutu wenye msimamo wawastani.
Picha hapo juu anaonekana, Theoneste Bagosora, akiwa mahakama kusikilaza hukumu yake.
Chini anaonekana, mlinzi wa mahakama, akimwelekeza yakuwa asimame, huku anaonekana Theoneste Bagasora, akimwangalia mlinzi tayari kunyanyuka kwenda kuanza kutumikia kifungo.
Nguvu za kijeshi za Kirusi bado zazunguka Latini Amerika.
Havana, Kuba - 18/12/08. Serikali ya Kuba, imezikaribisha nguvu za kijeshi kutoka nchi ya Urusi hivi karibuni, akiongea hayo,Capt. Igor Dygolo, alisema hii ni moja ya safari, ambapo ya melikebu za kijeshi zinafanya ziara katika maeneo ya Latini Amerika.
PIcha hapo juu,wanaonekana rais wa Urusi, Dmitry Medvedev akikaribishwa na mwenyeji wake rais wa Kuba Raul Castro, mapema walipo kutana mjini Havana.
Chini ni zinaonekana melikebu, zikiwa njiani kuelekea kwenye bahari ya Kuba.
Hali yawa ngumu kwa Joseph Koni"Umoja wa mataifa waombwa kuunga mkono'.
Kampala,Uganda - 17/12/08 . Mwakilishi maalumu wa anayeshughulikia suruhisho la kuleta amani nchini Uganda kati ya serikali na kundi linalo pinga serikali ya Uganda LRA Load Resistance Army , na ambaye ni rais wa zamini wa Msumbiji, Joachim Chissano, ameiomba Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa,kuunga mkono nguvu za kijeshi zilizoanza hivi karibuni kaskazini mwa Uganda,ili kumshinikiza Joseph Koni kutia saini mkataba wa amani.
Hata hivyo, Joseph Koni, alitoa sharti ya kuwa ni lazima,hati ya kukamatwa kwake na wenzake ifutwe, ndipo maswala mengine ya tufuatilia. Picha hapo juu ni ya rais wa zamani wa Msumbiji, ambaye ndiye msuruhishi wa matazizo yaliopo nchini Uganda.
Picha yapili anaonekana,Joseph Koni, akiwa amezungukwa na walinzi wake huko mafichoni.
Bei yamfuta kupunguzwa, wasema viongozi wa OPEC.
Oran,Algeria - 17/12/08 . Jumuia ya nchi zinazo toa mafuta duniani (OPEC) - Organisation of Petroleum Exporting Countries, zimekubaliana kwa pamoja kupunguza bei ya mafuta,ili kuweza kukizi mahitaji ya jamii.
Akiongea hayo,Chekib Khelil, ambaye ni rais wa OPEC, alisema nimatumaini yangu tumewashangaza wengi,na hii itasaidia kupunguza bei ya baadhi ya vitu vingine.
Picha hapo juu anaonekana, rais wa OPEC, Chekib Khelil, akiongea na waandishi wa habara baada ya mkutano mjini Oran.

Monday, December 15, 2008

Ziara ya mwisho ya rais, George Bush nchini Irak ya kutwa na mkasa.

Mwanana mama mwenye umri wa miaka 70 ajifungua mtoto. Jimbo la Haryana, India-15/12/08. Mwanamke mwenye miaka 70,(amjaliwa kupata mtoto), kujifungua mtoto wa kike, akiwa ni mwanamke wenye uri mkubwa katika historia ya India na dunia. Mwanamke huyu, Rajo Devi, alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji, alisema ,mganga aliye muhudumia, Dr Anurag Bishnoi, na amganga alimalizia kwa kusema, bi, Rajo Devi yupo katika hali nzuri. Picha hapo juu, anaonekana mwamama, Rajo Devi na mume wake pamoja na mtoto wao wa kike baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini. Ziara ya mwisho ya rais, George Bush nchini Irak ya kutwa na mkasa.

Baghdad,Irak-14/12/08.Rais George Bush, wa Amerika,amefanya ziara yake ya mwisho kama rais wa Amerika nchini Irak na kukutwa na mkasa wa kihistoria.
Mkasa huo,ulimkuta rais, George Bush,wakati alipo kuwa akiongea na waandishi wa habari, mjini Baghdad, na mmoja ya wandishi wa habari kumtupia viatu na kudai ya kuwa hakutimiza haadi aliyo itoa wakati akiwa madarakani na sasa anaondoka na kuiacha Irak katika hali ngumu.
Rais, George Bush, aliendelea na ziara yake kama kawida, na kueleka nchini Afghanistan. Mwandishi wa habari huyo, ambaye julikana Muntazer al-Zaidi, amechukuliwa kama shujaa nchini Irak kwa kitendo chake hicho.
Hata hivyo, Muntazer al Zaidi, alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi.
Kufuatia kukamatwa kwa Muntazer al-Zaidi, kumefanya wananchi wa maeneo tofauti nchini Irak,kuandamana kudai ya kuwa Muntazer aachiwe huru.
Picha hapo juu wanaonekana, baazi ya wananchi nchini Irak, wakiandamana kudai ya kuwa Muntazer al-Zaidi, aachiwe huru.
Picha ya pili, inaonyesha matukio ya aina tofauti,wakati rais, George Bush na waziri mkuu Nuri al-Maliki wakati walipo kuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Picha ya tatu, anaonekana, Muntazer al-Zaidi akilusha kiatu kuelekea alipo simama rais , George Bush na waziri mkuu wa Irak Nuri al-Maliki.
Picha ya tatu, anaonekana waziri mkuu wa Irak,Nuri al- Maliki, akijaribu kuzuia kiatu bila mafanikio kisimfikie usoni rais George Bush,lakini hata hivyo kiatu hicho akikuweza kumzuru rais George Bush baada ya kukikwepa kiatu kilichotupwa na Muntazer al Zaidi.
Pakistan na Uingereza kushirikiana kupamabana na ugaidi"$ million 9 kutumika".
Islamabad,Pakistan-14/12/08.Waziri mkuu wa UIngereza, Gordon Brown, amehaidi ya kuwa serikali ya UIngereza itatoa msaada wa dola, $ 9 million, ilikuweza kupambana na ugaidi nchini Pakistan.
Waziri mkuu wa Uingereza, Gordo Brown, alitembelea pia, kiserikali za nchi za India,Afganistan na Pakistan.
Picha hapo juu wanaonekana,rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari na waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, mapema walipo kutana mjini Islamabad.
Picha ya pili, wanaoneka madereva wa maroli yanayo chukua mizigo ya jumuia ya kijeshi ta NATO, wakiwa wamekaa chini, huku hawajui la kufanya, baada ya maroli yao kulipuliwa pamoja na baadhi ya magari ya kijeshi ya jumuia hiyo mapema hivi karibuni.
Picha ya tatu, wanaonekana waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, akiwa na waziri mkuu wa India, Monmohan Singh, wakati walipo kutana nchini India
Kongo na Rwanda zalaumiwa kwa machafuko ya liopo nchini Kongo.
New York,UN-14/12/08.Umoja wa Mataifa, umezilaumu serikali za Jamuhuri ya Kongo na Rwanda, kwa kutoleta amani katika maeneo tofauti nchini Kongo.
Katika repoti, iliyo wasirishwa kwenye Umoja huo,imesema yakuwa, serikali ya Kongo, imekuwa ikishirikiana na kundi moja la Kihutu, (FDLR) Force for the Liberation of Rwanda lililo kimbilia nchini Kongo, baada ya serikali inayo ongozwa na rais, Paul Kagame kuchukua madaraka.
Na ripoti hiyo, ilisema yakuwa serikali ya , Rwanda imekuwa ikimsaidia, mpinzani mkuu wa serikali ya Kongo, Laurant Nkunda, ambaye anatetea masrahi ya watusi waishio nchini Kongo.
Ripoti hiyo ilisema ya kuwa Kongo na Rwanda zinapigana vita kwa kutumia makundi haya na kusababisham madhara makubwa kwa wananchi na jamii nzima, hasa katika maeneo yenye vita.
Uingereza kuanza kutoa wanajeshi wake mapema mwaka 2009.
London,Uingereza-14/12/08. Serikali ya Uingereza ya kuwa itaanza kuwaondosha wanajeshi wake nchini Irak, kuanzia mwakani mwezi machi.
Hata hivyo, serikali ya Uingereza ilisema yakuwa, watakuwepo wanajeshi kati ya 300 hadi 400 watakao kuwa na kazi ya kulifundisha jeshi la Irak.
Hapo ujuu wanaonekana, baazi ya wanajeshi wa Uingerereza, wakiwa kazini katika eneo moja nchini Irak.
Israel ya wachia Wapalestina"Ishara ya kumuunga mkono rais.
Gaza,Palestina-15/12/08. Serikali ya Israel imewaachia zaidi ya Wapalestina 224, ambao walikamatwa katika vipindi tofauti wakati wa mapambano kati ya askaria wa Palestina na Wanajeshi wa Israel.
Kuachiwa kwa Wapalestina hao, kumekuja kama ishara ya kumuunga mkono rais wa Palestina, bwana, Mahmoud Abbas, ambaye anawakati mgumu kisiasa, hasa kwa kupata upinzani kutoka kwa chama cha Hamas.
Picha hapo juu wanaonekana wanachama wa Hamas,wakiandamana kwenye mji wa, Gaza kuazimisha miaka 21,tangu chama cha Hamas kilipo anzishwa.
Picha ya chini, wanaonekana Wapalestina, ambao wameachiwa wakikaribia kukutana na ndugu zao.
Picha ya tatu wanaonekana, wakina mama,wakishangilia kwa hali ya juu,wakati wafungwa wa Kipalestina walipowasili kwenye maeneo ya Wapalestina.

Tuesday, December 9, 2008

Pakistan yaweka ngumu kuwepeleka raia wake nchini India.

Wakaribbean waomba rais mteule wa Amerika, Baraka Obama, kuondoa vikwazo kwa serikali ya Kuba. Saint John's,Barbuda - 09/12/08.Jumua ya nchi za Karibbien, zimemwomba rais mchaguliwa wa Amerika, Baraka Obama, kuondoa vikwazo vilivyo wekwa kwa serikali ya Kuba. Akiongea hayo, waziri mkuu wa Antigua na Barbuda, W Baldwin Spencer,ambaye ni mwenyekiti wa jumuia ya nchi za Karibbien, amesema hayo wakati wa mkutana wa viongozi wa nchi hizo ulio fanyika Santiago de Kuba. Hata hivyo , rais mteule wa Amerika, Baraka Obama, alisema yakuwa serikali yake itapunguza baadhi ya vikwazo kwa wananchi wa Kuba,lakini vikwazo vitabakia mpaka hapo serikali ya Kuba itakapo badilisha msingi wake wa kisiasa. Picha hapo juu, anaonekana rais mtuele wa Amerika, Baraka Obama, akisikiliza kwa makini wakati alipo udhulia moja ya mikutano ya kampeni ya kugombania urais wa Amerika,na aliahaidi mabadiliko makubwa katika serikali yake ikiwa atachaguliwa kuwa rais wa Amerika na kukuza ushirikiano na jumuia ya kimataifa ili kurudisha hazi ya Amerika na wanachi wake. Mamia ya waumini wa dini ya Kiislaam, wamaliza kutimiza moja ya nguzo za dini. Mecca,Saudi Arabia - 09/12/08.Maelfu ya waumini wa dini Kiislaamu,wametiza wajibu na nguzo za dini ya Kiislaamu, baada ya kukamilisha hija kwa kufuata njia zote alizo fanya Mtume Muhammad ( S . A . W). Kwenda Hija, ni muhimu kwa kila Muislaamu, endapo atajaliwa kufanya Hija wakati uzima wake, alisema, mmoja ya Mahujaji. Picha hapo, juu wanaonekana baadhi ya waumuni wa dini ya Kiislaamu wakiwa wamepumzika karibu na mlima Arafat. Picha ya pili wanaoneka, baba na mtoto wake wa wakitupa mawe, ikiwa ni ishara ya kumpiga shetani na mambo yake yote. Picha ya tatu,wanaonekana mamia ya waumini, wakizunguka mnara wa Kabba, ambao nu moja ya jiwe ambalo limebakiwa ambalo lilijengwa na Mtume Abraham( Ibrahim), na nimuhimu kwa kila Muislaamu akijaliwa kulitenda na kutimiza katika uzima wake. Pakistan yaweka ngumu kuwapeleka raia wake nchini India.

Islamabad,Pakistan - 08/12/08. Serikali ya Pakistan, imesema ya kuwa haita wapeleka washukiwa wa maafa ya ulipuaji wa mabomu na kusababisha mauaji ya watu 172 na zaidi ya 300, walijeruhiwa.
Serikali ya Pakistan,imesema yakuwa imeamua hivyo ,baada ya kupatikana habari yakuwa serikali ya India,ilikuwa nampango wa kubomu baazi ya maeneo yalipo ndani ya Pakistan, ambapo inasadikiwa ni makazi ya kundi la kigaidi la Lashkae -e-Taiba, ambalo linasadikiwa kuhusika na mlipuko ulio tokea hivi karibuni nchini India.
Hata hivyo, waziri wa mambo ya nje wa Pakistan, Shah Mehmood Qureshi,amesema ya kuwa hawakufanya hivyo,kwa vitisho bali wapo kwa ajili ya kuleta amani kati ya nchi hizi mbili siyo kuleta vita.
India na Pakistan, zote zina nguvu za kijeshi zenye uwezo wa kinyuklia na zimekuwa zikitazamwa kwa karibu na jumuia ya kimataifa na kuagiza lazima zishirikiane katika kupiga vita ugaidi waaina yoyote..
Jumuia ya Ulaya yakubali kuwapa hifazi wakimbizi wa Irak.
Brussels, Belgium - 2/12/08.Jumuia ya Ulaya, imekubaliana kwa pamoja kuwapokea na kuwapa hifazi wakimbizi, 10,000 kutoka nchini Irak, waliopo kwenya makambi ya kikimbizi nchini Syria na Jordan.
Uamuzi huo umekuja baada ya kikao cha mawaziri wa mambo ya ndani ya jumuia hii, walipo kutana mapema tarehe, 28/11, mjini Brussel.
Uamuzi huu umekuja , baada ya shirika la kuudumia wakimbizi la umoja wa mataifa ,kuziomba nchi wanachama wa jumia hiyo kuwapa hifazi wakimbizi hao wa kutoka Irak
Hata hivyo, nchi kama Greesi na Cyprus, zilipinga makubaliano hayo kwa kudai, zina wakimbizi wengi katika nchi zao.
Picha hapo juu, anaonekana nyota ya Holly Wood, mcheza sinema na balozi wa kujitolea wa unoja wa mataifa, bi, Angelina Jolie, akiangalia kwa uchungu, jinsi gani, mama mmoja wa Kiirak, akingojea kupewa posho, wakati balozo huyo alipokwenda kuwatembelea wakimbizi hao mwaka, 2007.
Picha ya pili , ni moja ya makazi ya wakimbizi,mbele ya anaonekan binti, mdogo akiwa amembeba mtoto,hatima yake mtoto huyu na dada yake watapa mahali pazuri na kuweza kwenda shule kama watoto wengine.
Kutovaa kitamba cha kichwa sio kukiuka haki za binadamu"Mahakama ya sema".
Brussels, Ubeligiji - 6/12/08. Mahakama ya haki za binadamu ya jumuia ya Ulaya - European Court of Human Rights (ECHR), imesema kufukuzwa kwa wanafunzi wa kike wawili waliokataa kufua vitambaa vya kichwa, halikuwa tendo la kukiuka haki za binadamu.
Kesi ya wasichana hao, iliyo wakilishwa na jumuia za kutetea haki za binadamu kutokea nchini Uturuki, ambao walifukuzwa shule nchini Ufaransa,baada ya kukataa kuvua vitambaa hivyo vya kichwa wakati wa kipindi cha kufanya mazoezi ya viungo.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wasichana wakiwa wamevalia vitamba vya kichwa ikiwa ndiyo moja ya mtindo wa mavazi ya wakaazi wengi wanaotokea katika jamii ya nchi jumuia za kiarabu na baadhi ya maeneo duniani kote, ikiwa ni ishara ya kutunza heshima ya mwanamke mbele ya jamii.
Picha ya pili, ananonekana mwana mama, akiwa amevalia kitamba kichwani na kufunika uso wake, lakini mavazi kama haya yamekuwa vigumu, kukubalika katika jumuia za nchi za Ulaya na baadhi ya maeneo mengina duniani.

Monday, December 8, 2008

Wafanyakazi wa kampuni ya ulinzi na usalama ya Blackwater, kizimbani kujibu kesi ya mauaji.

O.J.Simpson,akutwa na hatia na kufungwa miaka 15 jela.

LasVegas,Amerika,05/12/08.O.J Simpson, aliyejuwa mchezaji maarufu wa mipira wa watu wenye misuri-American Football, amehukumikwenda jela miaka 15, baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria na kuhatarisha maisha ya jamii.
O.J. Simpson, alikutwa na hatia,baada yeye na rafiki yake kuamua kwenda kuchukua vitu walivyo dai ni vya O.J . Simpson katika duka moja lilipo mjini humo.
Hukumu ya O.J. Simpson na mwenzake, ilitolewa na jaji Jackie Glass.
Hata hivyo wanasheria wa O.J.Simpson, walidai watakata rufaa, kwani kuna baadhi ya vifungu vya sheria vilikiukwa wakati wakuendesha kesi hii.
Picha hapo juu anaonekana, jaji, Jackie Glass, akiongea kabla ya kutoa hukumu ya kifungo kwa O.J.Simpson cha miaka 15 jela.
Picha yapili, Inatimiza ule usemi useamao,msiba kwa jilani kuna shibe ya muda,hapo anaonekan mmoja ya wachuuzi wa biashara ndogo ndogo, akiuza vichika funguo vikiwa na picha za O.J.Simpson.
Picha ya tatu anaonekana, O.J. Simpson, akiongea mbela ya jiji, kwa kudai yakuwa alikuwa anachukua malizake, na hakujua kama alikuwa nanafanya makosa ama kuvunja sheria.
Wafanyakazi wa kampuni yaulinzi na usalama ya Blackwater, kizimbani kujibu mashitaka ya mauaji.
Utah,Amerika,08/12/08.Wafanyakazi watano wa kampuni ya ulinzi na usalma ya Blackwater, wamejisalimisha wenyewe kwenye vyombo vya usalama mjini Utah, ili kujibu mashitaka ya zidi yao zidi ya mauaji ya rais nchini Irak, wakati wakiwa kazini.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa wafanyakazi hawa,alisema ya kuwa wateja wake walikuwa kazini wakati wa mashambulizi hayo yalipo tokeana walikuwa wanajilinda na mashambulizi, baada ya kushamuliwa na watu wasio julikana.
Picha hapo juu wanaonekana,wafanyakazi wa kampuni ya usalama na usalama, ambao wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji.
Picha pili ni ya gari, ambayo ilikuwa moja wapo lililo kutwa kati ya mashambulizi ya wafanyakazi wa Blackwter.
Poland yawa na wasiwasi kufuatia mkataba wa usalama wa kulinda NATO.
Slupsk, Poland,04/12/08.Wachunguzi wa mambo ya kiusalama nchini Poland, wamesema yakuwa kupitishwa kwa makubaliano kati ya serikali ya Poland na serikali ya Amerika, ili kuwekwa mitambo ya kivita nchini humo kumeleta wasiwasi na hisia tofauti.
Akisema haya, ni mmoja ya wanajeshi wa Poland, Bronislaw Nawak, alisema yakuwa ,ikiwa makubaliano haya yata endelea kama yalivyo kubaliwa, basi Poland itakuwa ndiyo chambo cha mashambulizi yoyote yatakayo tokea kwa kuzingatia na maelezo yaliyo tolewa na uongozi wa mjini Moscow,alimaliza kwa kusema Bronislaw Nawak.
Hata hivyo, jumuia ya Ulaya, imekubaliana kwa pamoja kuwekwa kwa mitambo hiyo ya kivita nchini Paland.
Picha hapo juu ni picha ya mizimga ya kivita ambayo huenda zikaweka nchini Poland,ambapo serikali ya Washington inadai ya kuwa mizinga hiyo ni kwa ajili ya kulinda NATO na mashambulizi kutoka Iran na Korea ya Kusini.
Serikali ya Afghanistan, yataka muda maarumu wa kuwepo kwa jeshi la kimataifa.
Kabul,Afganistan - 29/11/08. Rais wa Afghanistan,Hamid Karzai,amesema ya kuwa itakuwa ni muafaka endapo majeshi ya kimataifa yatewaka muda maarumu wa kuwepo nchini humo.
Akiongea mbele ya ujumbe wa kamati ya usalama wa umoja wa mataifa, ya kuwa endapo kutakuwepo na muda maarumu utakao wekwa kwa majeshi haya kuondoka ili kuweza kupanga ni jinsi gani kutakuwepo na makubaliano ya kisiasa kati ya makundi yanayo pingana na serikali.
Nchini Afghanistan, kundi la Taliban, ndilo kundi kubwa linalo ongoza mashambulizi zidi ya serikali na majeshi ya kimataifa.
Picha hapo juu, anaonekana rais, Hamid Karzai, akiongea mbele ya wajumbe wa kamati ya usalama ya umoja wa mataifa.
Picha ya chini, ni mmoja ya mwanajeshi wa jeshi la kimataifa, akiwa anakura doria katika moja ya mji nchini Afghanistan.