Kenya yatangaza kuwa na mafuta katika ardhi yake.
Nairobi, Kenya - 27/03/2012. Serikali ya Kenya imetangaza kugunduliwa kwa mafuta nchini humo katika maeneo ya Kaskazini Magharibi mwa Turkana.
Rais Mwai Kibaki alisema" hii ni habari jema kwani ni kwa mara ya kwanza Kenya inagundulika ya kuwa ina mafuta"
Ugunduzi wa mafuta hayo umefanywa na kampuni inayo julikana kama Tullo Oil ambayo pia imedai yakuwa mafuta yenye uboara kama haya ya Kenya yamegunduliwa nchini Uganda.
Uchimbuzi wa mafuta hayo nchini Kenya unatarajiwa kwenda kina cha umbali wa mita 2,700 ifikapo mwezi wa Mei.
Papa Benedikt XVI awasili nchini Kuba.
Havana, Kuba- 27/03/2012. Kiongozi wa madhehebu ya Kikatoliki duniani amewasili nchini Kuba kwa ziara ya siku tatu nchini humo.
Papa Benedikt wa Kumi na Sita - XVI, aliwasili nchini Kuba baada ya kumaliza ziara yake nchini Mexico.
Rais wa Kuba Raul Castro katika kumkaribisha Papa Benedikt alisema " Kuba inatambua umuhimu wa Kanisa Katiliki nchini Kuba na Wakuba wapo pamoja na Kanisa katika kulinda haki za Wakuba na kwa kushirikiana na Kanisa Wakuba watailinda Kuba."
Papa Benedikt allsema " nawaomba wa Kristu wenzangu kumwamini Mungu na kupingana nakila aina ya njia za shetani kwani ndiyo njia pekee ya kushinda umasikini na ubaya wa ubinadamu."
Katika ziara hiyo Papa Benedikt anatarajiwa kukutana viongozi wa serikali ya Kuba ili kujadili hali halisi ya kiimani nchini humo.
Korea ya Kaskazini bado kitendawili kwa Marekani.
Seoul, Korea ya Kusini - 27/03.2012. Serikali ya Marekani imeitaka serikali ya Korea ya Kaskazini kuachana na mpango wake wa kuendeleza mradi wa kinyuklia.
Onyo ilo lilitolewa baada ya rais wa Marekani, Baraka Obama yupo ziarani nchini Korea ya Kusini na ameuhduria kikao cha viongozi wa dunia ili kujadili udhibiti wa matumizi ya sirha za kinyuklia.
Rais Obama alisema "Korea ya kaskazini lazima iachane na mradi wa kinyuklia kwani kitendo cha serikali ya Korea ya Kaskazini kuendelea na mpango wake wa kuendeleza vitisho vya kinyuklia kwa kujaribu mabomu havita saidia ila vina ifanya Korea ya Kaskazini kutengwa zaidi."
Serikali ya Korea ya Kaskazini imekuwa ikivutana na jumuiya ya kimataifa katika harakati zake za kinyuklia kwa muda sasa baada ya mazungumzo kukwama miaka michache iliyo pita.
Iran bado yasisitiza yakuwa itajibu mashambulizi.
Tehran, Iran - 27/03/2012. Mmoja wa viongozi wa ya Iran amedai ya kuwa kitendo chochote cha kuishabulia Iran kitakuwa cha kujutiwa.
Ayatollah Seyyed Ahmad Khatami alisema " ikiwa Izrael au nchi yoyote kuishambulia Iran, basi wajuwe yakuwa majibu yetu Iran yatakuwa ya kuiwezesha dunia kutambua ya kuwa tunachosema huwa tunatekeleza.2
"Kwani kumekuwa na vitisho vingi vya kuishambulia Iran, Izrael imekuwa ikiishawishi jumuiya ya kimataifa kuamini ya kuwa Iran ni adui wa jamii, jambo ambalo si la kweli.
"Iran hajawahi kuishambulia nchi yoyote na kitendo cha kuishamblia Iran kitakumbwa na majibu ambayo yatafanya jamii isituke na uenda ikawa fundisho kwa wale wote wanao taka kutumia nguvu kwa ajili ya manufaa yao."
Iran imekuwa ikishutumiwa na Mareakani na washiriki wake yakuwa inampango wa kutengeneza siraha za kinyuklia kinyume na sheria, jambo ambalo Iran imekanusha vikali kwa kudai yakuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa ajili ya maendeleo ya kisayansi.