Saturday, February 20, 2010

Wakazi wa Kigali wastuliwa na milipuko ya mabomu.

Wakazi wa Kigali wastuliwa na milipuko ya mabomu.

Kigali, Rwanda - 20/20/2010. Milipuko ya mabomu imetokea sehemu tatu tofauti katika jiji la Kigali na kusababisha kifo cha mtu mmoja na watu zaidi ya 18 kujeruhiwa na watano kati ya majeruhi hao vibaya. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, watu wawili wamekamatwa "hawa watu walio kamatwa ni kati ya wale watu wanaotaka kuleta vurugu kwa kutishia amani na ni watu wa kundi la Interahamwe" alisema msemaji huyo. Hata hivyo serikali ya Rwanda imeanza uchunguzi mara moja kuhusiana na milipuko hiyo ya mabomu. Milipuko hiyo imekuja wakati wananchi wa Rwanda wanajiaanda kufanya uchaguzi wa kumchagua rais mnamo mwezi wa August. Picha hapo juu ni ya bendara ya Rwanda nchi ambayo miaka kumi na nane iliyo pita kulitokea mauaji kati ya watu jamii ya Watutsi na watu jamii ya Wahutu na watu wengi welipoteza maisha. Matokea ya uchaguzi Ukrain shwali. Kiev, Ukrain - 20/02/2010. Mgombea wa chama pinzani katika kiti cha urai wa Ukrain bi Yulia Tymoshenko amefuta kesi ya malalamiko ya madai ya kutaka matokeo ya uchaguzi kurudiwa kuhesabiwa, baada ya mpinzani wake Victor Yanukovych kushinda katika uchaguzi wa urais ulio fanyika mapema mwaka huu. Akiongea na waandishi wa habari bi Yulia Tymoshenko alisema "Haina haja ya kuendela na kesi kwa hali halisi ya koti inajionyesha yakwa hakuna kitu kitabadilisha matokeo." Bi Yulia Tymoshenko, alifungua kesi kwa madai ya kuwa kulikuwa kunaukiukwaji wa sheria wakati wa uchaguzi na wakati wa kuzihesabu kura. Picha hapo juu anaonekana, bi Yulia Tymoshenko akiondoka ndani ya mahakama baada ya kusikia kesi ya madai aliyo yaleta mbele ya koti inayo shughulika kesi za sheria ya uchaguzi. Rais wa Niger angolewa madarakani na jeshi. Niamey, Niger - 20/02/2010. Malfu ya wananchi wameandamana jijini Niamey kuunga mkono kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mamadou Tandja. Maandamano hayo ambayo yaliishia katika majengo ya ukumbi wa bunge la Niger kwa kuonyesha shukurani kwa jeshi kwa uamuzi wa kumtoa madarakani rais huyo, ambaye alijiongezea muda wa kuongoza nchi. Hata hivyo jeshi la nchi hiyo limehaidi kuanda uchaguzi muda si mrefu na kurudisha madaka kwa serikali ya kiraia.. Picha hapo juu wanaonekana wanajeshi wakiwa wanaangalia usalama wakati wa maandamano. Saga la Afghanistan lasababisha kuvunjika kwa serikali.

Hague,Netherland - 20/02/2010.Serikali ya muungano nchini Netherland imevunjika baada ya kutotokea makubaliliano kuhusu jeshi la Netherland lililoponchini Afghanistan. Kuvunjika huko kumekuja baada ya waziri mkuu msaidizi Wouter Bos, kupinga kuongezewa muda wa kuwepo kwa jeshi la Netherland nchini Afghanistan, wakati waziri mkuu Jan Peter Belkenende, anataka jeshi la Netherland liongezewe muda baada ya NATO kuiomba serikali ya Netherland kufikilia ombi hilo. Majadiliano hayo amabayo yalichukua karibu masaa 16 haya kufikiwa muafaka wa pamoja na kulazimisha serikali kuvunjika, kwani chama cha PvdA kinacho ongozwa na Wouter Bos kinapinga ombi hilo la NATO. Picha hapo juu,wanonekana Wouter Bos kushoto na Jan Peter Belkenende kulia enzi zao wakiwa viongozi wa ambao waliongoza nchi kwa kauli moja.

Thursday, February 18, 2010

Hali ya usalama wa rais wa Niger mashakani.

Hali ya usalama wa rais wa Niger mashakani. Niamey,Niger - 19/02/2010. Jeshi nchini Niger limemteka nyara rais wa Niger Mamadou Tandja, baada ya kuvami makazi yake. Kwa mujibu wa watu waliona tukio hilo walisema" walisikia milio ya risas wakti inaaminika rais alikuwa akiongoza mkutano. Habari zinasema jeshi limemchukua rais ili atangaze kujiudhulu urais. Niger imekuwa katika mvutano wa kisiasa, tangu rais Tandja alipo jitangazia kujiongezea madaraka, jambo ambalo halikukaribishwa na jumuia ya kimataifa. Picha hapo juu anaonekana rais wa Niger, Mamadou Tandja, akihutubuia wanachi hivi karibuni kabla ya kukamatwa. Rais wa Amerika akutana na Dalai Lama. Washington, Amerika - 19/02/2010. Rais wa Amerika Baraka Obama, amekutana na kiongozi mwana harakati wa kutetet haki za Watibeti katika Ikulu ya Amerika leo. Viongozi hawa wawili walikutana licha ya China kupinga mkutano huo wa kiongozi wa Watibeti na rais wa Amerika. Picha hapo juu, kulia ni kiongozi wa Watibeti Dalai Lama na kulia ni rais Baraka Obama, ambao wamekuta kwa mazungumzo ya faragha katika ofisi za Ikulu. Interpol watoa picha za washukiwa. Riyadh, Saudi Arabia - 18/02/2010.Police wa kimataifa Interpol imetoa picha na majina ya watu ambao wanashukiwa kuhusika katika mauaji ya aliyekuwa kamanda masaidizi wa kundi la Hamas, Mahmoud al Mabhouh wakati alipo kuwa nchini Dubai. Kwa mujibu wa Intarpol "watu walio husika na mauaji hayo watakamwa kutokana na ushirikiano wa nchi tofauti." Hata hivyo watu hao wanashukiwa kwa kutumia paspoti zisizo halisi na inasadiwa paspoti hizo ziliibiwa au kutolewa kinyume cha sheria. Picha hapo juu ni zawatu wanaoshukiwa katika mauaji ya aliyekuwa kamanda wa wa kundi la Hamas hivi karibuni.

Wednesday, February 17, 2010

Ufaransa yafuta deni la Haiti.

Ufaransa yafuta deni la Haiti. Port-au-Prince,Haiti. 17/02/2010. Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy amewasili nchi Haiti kwa ziara ya kiserikali na kuthmini hali halisi ya uaribufu ulio fanywa na tetemeko la ardhi lililo tokea mwamzono mwa mwaka huu. Akiongea na viongozi wa serikali na wananchi alisema Ufaransa imefuta deni lenye thamani $ 77millions na $450 kuchangia ujenzi wa Haiti baada ya kuathirika na tetemeko la ardhi. Picha hapo juu, anonekana rais wa Ufaransa kulia na mwenyeji wake rais wa Haiti. akikagua gwaride mapema alipo wasili nchini Haiti kuangli uharibu ulio fanywa na tetemeko la ardhi. Argentina yaweka malipo kwa meli zote ziingiazo kwe visiwa vyake.

Buenos Aires, Argentina - 17/02/2010. Rais wa Argentina,Christina Kerchner ametia sahihi sheria itakayo lazimisha kila meli ambayo itakuwa inapita katika visiwa Malivinas na Falkland kupata ruhusa kutoka serikali ya Argentina.

Kufuatia kutiwa sahihi sheria hiyo, serikali ya Uingereza, imemwita balozi wa Argentina nchini Uingereza kujibu maswali ya kuhusu sheria hiyo mpya.

Picha hapo juu anaonekana rais wa Argentina,akiongea kuelezea hali halisi ya visiwa vya Argentina.

Saturday, February 13, 2010

Rais wa zamani wa Amerika aruhusiwa kutoka hospitai.

Rais wa zamani wa Amerika aruhusiwa kutoka hospitali.

New York, Amerika - 13/02/2010. Aliyekuwa rais wa Amerika, Billy Clinton ameruhusiwa kutoka hospital baada ya kufanyiwa operasheni ndogo ya ili kuruhusu damu iweze kufanya kazi yake mwilini vizuri.
Operasheni hiyo iliyo fanywa kwenye moyo, ilifanyikia katika hospital New York.
Billy Clinton, aliyekuwa rais wa Amerika kwa miaka minane 1993-2001, alionekana akitokea hospitali kuelekea nyumbani.
Picha hapo juu, ni yaaliye kuwa rais wa amerika Billy Clinton,ambaye amefanyiwa operasheni wa moyo hivi karibuni.
Picha hapo juu,ni ya Dr Schwartz akiongea na wandishi wa habari, mara baada ya kumaliza operasheni ya aliyekuwa rais wa Amerika Billy Clinton.
Wasudan kuanza kampeni ya kumchagua rais nchi.
Khartoum, Sudan - 13/02/2010. Kampeni za uchachaguzi zimeanza nchini Sudan kugombea kiti cha urais wa Sudan.
Wagomea urais wapatao 12 wanafanya kampeni ya kugomea kiti hicho ambacho kwa sasa kina shikliwa na rais Omar Al Bashir.
Uchaguzi huo utakaofanyika April 11,utafungua njia ya kupiga kura ya maoni mnamo mwaka 2011.
Mpinzani mkubwa wa rais, Omar Al Bashir,ni Yasser Arman 49, ambaye alisha wahi kuwa waziri mkuu na mwanacham wa Umma Party.
Picha hapo juu wanaonekana kulia rais wa sasa wa Sudan Omar Al Bashir na mpinzani wake mkuu Yasser Arman, ambaowatachuana vikali kugombe kiti cha urais wa Sudan.
NATO yapania kuukomboa mjiwa Marjah.
Marjah, Afghanistan-13/02/2010. Jeshi la NATO na jeshi la Afghanistan, chini ya uongozi wa US limeanza kampeni ya kuukomboa mji wa Marhaj kutoka mikononi mwa kundi la Taliban.
Kampeni hiyo iliyo anza rasmi mapema leo alfajiri,inajulikana kama Operasheni Moshtarak ,amboyi nia ni kuukomboa mji hua na kukukabidhi chini ya serikali.
Hata hivyo mmoja wa viongozi wa kundi la Taliban, alisema ya kuwa wapiganaji wake watapigana hadi mtu wa mwisho ili kuilinda nchi yao iliyo vamiwa na jeshi la kigeni.
Picha hapo juu wanaonekana wanajeshi wakielekea mstari wa mbele na huku mbwa wa kunusa mabomu akiwa kazini tayari kupambana kundi la Taliban.

Monday, February 8, 2010

Kosta Rika yapata rais mwanmke kwa mara ya kwanza.

Kosta Rika yapata rais mwanamke kwa mara ya kwanza. Santa Jose, Kosta Rika - 08/02/2010. Matokea ya uchaguzi mkuu wa Kosta Rika yamempa ushindi mkuwa mgombea uchaguzi wa kiti cha urais Bi, Laura Chinchila kwa ushindi wa asilimia 47% dhidi ya wapinzani wake. Bi, Laura Chinchila, amekuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Kosta Rika, aligombea kiti hicho kupitia chama tawala. Picha hapo juu anaonekana, rais mtalajiwa wa Kosta Rika,Bi, Laura Chinchila, akiwaonyesha kidole gumba juu baada ya kutangazwa kuongoza matokeo ya uchaguzi.

Irani kuanza kurutubisha madini ya nyuklia.
Tehran, Iran - 08/02/2010. Serikali ya Iran imekabidhi waraka kwa shirika linalo shughulikia ukaguaji wa nguvu za nyuklia na kusema ya kuwa itaendelea kurutubisha madini ya nyuklia kufikia 20% kuanzia jumanne.
Barua hii imekabidhiwa, baada ya rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad kuagiza yakuwa kazi ya kurutubisha madini ya nyuklia kuanza mara moja.
Picha hapo juu anaonekana rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, katikati akikagua maendeleo ya moja ya mtambo wa kinyukli hivi karibuni.
Kiongozi wa upinzani nchini Sri Lanka akamatwa.
Kolombo, Sri Lanka - 08/02/2010. Aliyekuwa mgombea mpinzani wa kiti cha urais wa Sri La, General Fonseka ametiwa kizuizini na askari wa kijeshi.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, General Prasad Samarasinghe,alisema " General amekamatwa kutokana na makosa aliyo yafanya wakati alipo kuwa kazini kama mkuu wa jeshi.
Hata hivyo, kiongozi mmoja wa cha kisiasa, Sri Lanka Muslim Congress Rauff Hakeem, alisema "General Fonseka alikamatwa mbele yetu kwa kudhalilihswa."
Picha hapo juu ni ya General Fonseka, ambaye yupo kizuizini kwa sasa.